Siri nzito CCM 2015
Vikao vya Kamati Kuu ya CCM na Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar vinaonekana kuwa huenda vikaiweka hadharani siri nzito
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya CCM, Jakaya Kikwete akipiga makofi wakati alipowasili katika mkutano wa chama hicho Mjini Dodoma hivi karibuni. Picha ya Maktaba
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya CCM, Jakaya Kikwete akipiga makofi wakati alipowasili katika mkutano wa chama hicho Mjini Dodoma hivi karibuni. Picha ya Maktaba
Dar na Z’bar. Vikao vya Kamati Kuu ya CCM na Kamati Maalumu
ya NEC Zanzibar vinaonekana kuwa huenda vikaiweka hadharani siri nzito
za urais wa Jamhuri ya Muungano.
Mkutano wa
sekretarieti ndiyo utakaoanza leo ukifuatiwa na Kamati Maalumu ya NEC
Zanzibar huku Kamati Kuu ya CCM ikitarajiwa kukutana Jumanne wiki ijayo
katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kujadili na kutathmini hali ya kisasa
kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Kikao hicho kimekuja
huku wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia chama hicho wakipishana kwa usafiri wa ndege na boti kwenda
Zanzibar kutafutwa kuungwa mkono na wajumbe wa NEC na waliopo visiwani
humo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
alithibitisha kikao hicho kufanyika Zanzibar na kitaoongozwa na
Mwenyekiti wake Rais Dk Jakaya Kikwete ambaye amebakisha muda mfupi
kumaliza muhula wake wa uongozi tangu aingie madarakani mwaka 2005.
Vuai alisema Kamati Kuu ya CCM itakutana, itatanguliwa na Kikao cha Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar.
Alisema
suala kubwa ambalo watalijadili ni kuangalia mwenendo wa utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 tangu kumalizika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, Vuai alisema hayuko
tayari kuzungumzia ajenda ya kikao cha Kamati Kuu kwa vile majukumu hayo
yako kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye.
Pia,
alisema Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar itakuwa na ajenda ya mengineyo
itakayojadili hali ya kisiasa tangu kumalizika uchaguzi mkuu uliopita
ambapo kikao hicho tayari matayarisho yake yamekamilika kabla ya kuanza
kamati Kuu kukutana visiwani humu.
Nape
Hata
hivyo, Nape alisema jana kuwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM,
inakutana leo jijini Dar es Salaam kupanga ajenda zitakazojadiliwa
kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho
itakayokutana Zanzibar Jumanne ijayo.
Alisema kuwa kikao hicho ni cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
Kikao
cha Kamati Kuu kinakutana na kukiwa na patashika ya makada wa CCM
wanaotajwa kuwania nafasi ya urais wakipishana kwa safari za usafiri wa
majini na angani na wapambe wao kukutana na wajumbe wa NEC na mkutano
mkuu katika vikao vya faragha Pemba na Unguja kuomba ushawishi wa
kuungwa mkono.
Hali ya kisiasa Zanzibar, inadaiwa
kuchafuka na kuhatarisha uimara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)
baada ya vigogo wa Serikali hiyo kuanza kunyosheana vidole hadharani.
Inaelezwa
kuwa joto la uchaguzi wa urais ndilo ambalo limesabasisha hali hiyo
itokee. Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim, Seif Shariff Hamad na Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein huenda wakachuana katika uchaguzi wa
urais mwaka huu.
Sauala lingine zito ambalo linaweza
kujadiliwa katika vikao hivyo ni la kashfa ya escrow ambayo imewakumba
mawaziri na baadhi ya madaka wa chama hicho.
Mawaziri ambao wamekumbwa na kashfa hiyo ni pamoja na
aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospter Muhongo.
Profesa Tibaijuka tayari
ameondolewa kwenye nafasi yake ya uwaziri baada ya kupokea kiasi cha
Sh1.6 bilioni kutoka kwa Mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemarila
ambaye ni mbia wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.
Mwingine
anayetajwa kuhusika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew
Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, William
Ngeleja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Mbali
na wahusika wa Akaunti ya Escrow, vikao hivyo huenda vikajadili ripoti
ya maadili ya viongozi ikiwamo waliokumbwa zuio la kujihusisha na
kampeni za kuwania urais mapema kwa miezi 12, huku mienendo yao ya
kisiasa ikifuatiliwa.
Waliozuiwa kufanya kampeni ni
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi, Teknolojia January Makamba, Waziri
Mkuu Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na aliyewahi kuwa Waziri wa
Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Hata
hivyo, Nape alipoulizwa kuhusiana na wagombea wa urais kufanya kampeni
za nguvu na wengine kutumia mitandao ya simu kusambaza ujumbe, alikataa
kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo pamoja na sakata la escrow
iwapo litapewa nafasi katika vikao hivyo vya chama.
Mtikisiko Zanzibar
Maalim
Seif hivi karibuni alikaririwa akisema atapambana na Rais wa Zanzibar,
Dk Ali Mohamed Shein kwenye vikao vya Serikali na kulalamika kuna baadhi
ya masheha, wakuu wa wilaya na mikoa wakiwanyima wananchi haki ya
kupata vitambulisho vya Uzanzibari mkaazi na kutoandikisha kwenye
Daftari la Kudumu la Kupiga.
Akijibu dai hilo, Makamu
wa Pili wa Rais, Balozi Balozi Seif alisema hakuna wananchi wanaokatazwa
kupata Vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi na kueleza kuwa chini ya
Sheria Namba 7 ya mwaka 2005 hakuna mtu ambaye anaweza kupewa kama siyo
mkaazi wa Zanzibar kwa miaka mitatu.
Balozi Seif
alisema Serikali haitakubali kupata hasara ya kuzalisha vitambulisho
kutokana na idadi kubwa ya zaidi kuandikishwa watu ambao siyo wakazi ya
Pemba, wakati kuna vitambulisho vingi vimeshindwa kuchukuliwa na wenyewe
ambao alisema ni mamluki.
Mjumbe mmoja wa NEC ambaye
ameomba jina lake lihifadhiwe, alithibitisha vigogo wanaowania urais na
wapambe wao kumshawishi kuingia katika kundi lao.
Wagombea urais
Vigogo
wa urais waliofanya ziara kwa nyakati tofauti hivi karibuni visiwani
Zanzibar ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wasira, Mbunge wa Sengerema
William Ngeleja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye amealikwa kuhudhuria
Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) leo yaliyoandaliwa na Mbunge wa
Mpendae na Mafanyabiasha mashuhuri, Salum Turky.
Kadhalika Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye wakati wa Sikukuu ya Krismasi ya mwaka jana alikuwa Zanzibar