Maji ya mvua kero kwa baadhi ya wakazi Mtwara
Maji ya mvua kero kwa baadhi ya wakazi Mtwara
Wakazi
wa manispaa ya mtwara mikindani wameiomba manispaa kuharakisha ujenzi
wa mtaro wa kukusanya maji ya mvua na kuyamwaga baharini wenye lengo la
kupunguza tatizo la mafuriko katika baadhi ya maeneo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa mtaa wa kiangu
kata ya shangani wamesema ujenzi huo kwa sasa umechangia njia za maji
kuzibwa na hivyo kuleta usumbufu kwa mvua zilizoanza sasa.
Akizungumzia hali hiyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kiangu
chadema -ALLY MAKANJILA amesema eneo lake linatatizo la kujaa maji
lakini mtaro huo umechangia nyumba nyingi kupata mafuriko kutokana na
mtaro huo kujaa maji na kuzagaa katika majumba ya watu.
Kufuatia hali hiyo ameiomba manispaa kuharakisha ujenzi huo ili
wakazi wake waondokane na adha hiyo vinginevyo hali itakuwa mbaya
kulingana na mvua za masika ndiyo kwanza zimeanza.