RIWAYA NA HADITHI FUPI
RIWAYA YA KISWAHILI
Maelezo ya msingi juu ya kozi hii
Kozi hii inalenga kutoa taaluma kunt‘u juu ya riwaya ya kiswahili kwa kuangazia chanzo na maendeleo ya riwaya sambamba na ufafanuzi wa vipera vyake. Vilevile inajadili athari zitokanazo na kuwepo kwa riwaya ndani ya jamii, mwisho, inaangazia vijenzi muhimu katika masimulizi ya kubuni.
Malengo ya kozi
Kozi hii itawawezesha wanafunzi kuuchunguza na kuutathmini muundo wa nje na wa ndani wa taaluma nzima ya riwaya ya kiswahili na riwaya zenyewe za kiswahili.
MUHTASARI WA KOZI
1. Nadharia ya riwaya:· Dhana ya riwaya· Historia ya chimbuko la riwayao Riwaya na matapo ya fasihio Dhana ya ubunilizi katika riwayao Muundo wa riwayao Mikondo (aina) kuu za riwaya2. Riwaya ya kiswahili· Maana ya riwaya ya Kiswahili· Historia ya riwaya ya Kiswahilio Kabla ya uhuruo Baada ya uhuruo Kipindi cha kuanzia miaka ya 1980o Baada ya kutamalaki kwa zama za sayansi ya teknolojia· Maendeleo ya riwaya ya Kiswahili (Sababu za kuibuka, kukua na keenea ama kudumaa kwa riwaya ya Kiswahili).· Wanariwaya maarufu wa riwaya ya Kiswahili
3. Mbinu za kifani zinazotumika katika ujenzi wa riwaya za Kiswahili
o Naratolojia (Usimulizi, mwendo)o Msuko wa vitushi na motifu zakeo Uhusika na wahusikao Mtagusano wa kifasihio Matumizi ya lughao Mianzo na miisho ya kifomula
4. Mitazamo na mielekeo inayojichomoza katika riwaya za Kiswahili
o Dhana ya usomaji wa riwaya za Kiswahili (maana, hadhi matatizo)o Uhai au ufu wa riwaya za Kiswahilio Mawazo yaliyotamalaki katika riwaya ya Kiswahili katika mapito yakeo Masuala mtambuka katika riwaya za Kiswahilio Tathmini ya mchango wa riwaya ya Kiswahili kwa ustawi wa waswahili
5. Uhakiki wa riwaya Teule za Kiswahili
o Dhana ya uhakiki na nadharia za kuhakikia kazi za fasihio Kuchambua riwaya teule za Kiswahilio Ulinganuzi na ulinganishi wa vipengele muhimu vya kiuhakiki vijitokezavyo katika riwaya za Kiswahili
Riwaya Teule zitakazoshughulikiwa:
o Nagonao Kusadikikao Kasiri ya Mwinyi Fuado Mfadhilio Barua Ndefu kama hiio Mirathi ya Hatario Bwana Myombekele na Bibi Bugonokao Hofuo Pesa zako zinanukao Mzimu wa watu wakale
Namna ya Ufundishaji: Mihadhara na Mijadala.
Saa za Ufundishaji: Jumla ya saa 45, saa 30 za Mihadhara na 15 za Mijadala.
Upimaji: Alama za Tamrini 40% na Mitihani ya mwisho 60%.
MATINI ILIYOTUMIKA
Nadharia ya Riwaya
Kumekuwa na misuguano kadhaa kutoka kwa wanazuoni waliothubutu kutoa fasili ya riwaya. Imeonekana wazi kuwa kunakukubaliana kwa baadhi ya masuala na kutofautiana pia katika kutoa fasili hii. Miongoni mwa masuala yaliyopelekea misuguano katika utoaji wa fasili hii ni pamoja na:o Dhima / maudhui ya riwayao Mipaka ya riwaya pindi inapohusishwa na hadithi fupi au novelao Ukubwa / urefu wa riwayao Aina za riwaya
Kuna wengine huchanganya utanzu wa riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari (yaani, vile vitumiavyo lugha ya mjazo) kama vile Hadithi fupi, Novela, Tawasifu na Wasifu.
Hadithi fupiTofauti yake na riwaya hujikita katika upeo na uchangamani. Hii inamaana kuwa hadithi fupi huwa sahili sana ilihali riwaya huwa imetanza zaidi.
NovelaHii huwa ni changamani zaidi kuliko hadithi fupi. Huweza kuwa na visa vingi kiasi kulinganisha na hadithi fupi.
TawasifuNi utungo utumiao lugha ya mjazo ukisimulia habari za mtunzi mwenyewe.
WasifuNi utungo utumiao lugha ya mjazo ambapo mtunzi husimulia habari za mtu mwingine.
Ukichunguza kwa makini vijitanzu hivyo utaona kuwa vinatofautiana na riwaya katika vigezo vya: urefu, uchangamani, idadi ya wahusika, lugha, vitushi, U―Kina, dhamira n.k.
Hivyo, mtu anayetaka kuifasili dhana ya riwaya hupaswa kumakinika katika vipengele hivyo.
Maswali ya msingi
1. Wanazuoni mbalimbali wametoa fasili ya riwaya. Eleza fasili hizo.2. Kwa nini fasili zao zimetofautiana?3. Je, wewe unadhani riwaya ni nini?4. Eleza tofauti ya riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari.5. Unadhani tofauti hizo kati ya riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari zinasababishwa na nini?
Sifa bainifu za riwayaIlinganishwapo na tanzu nyingine, riwaya huwa nasifa bainifu zifuatazo:o Kutokufungwa na sheria nyingi (kinyume na makumbo mengine ya tamthiliya na ushairi).o Matumizi ya lugha ya kinathari.o Kuwa na mawanda mapana katika urefu na kina.o Ni zao halisi la kibepari.o Kuwa na uhalisi kwa kiasi kikubwa.o Mahitaji ya kusoma na kuandika.o Kuwepo kwa maisha na makazi yenye utulivu.o Kuwa na uwezo wa kugusia hadi vitu vionekanavyo kama vidogo (kwa maelezo zaidi, tazama. Madumulla, 2009).
Miega ya Riwaya
Mwega ni nguzo au kiunzi kitumikacho kushikilia jambo / kitu. Kama ilivyo kwa kila kazi ya fasihi, riwaya yoyote lazima ijiegemeze katika miega au nguzo tatu muhimu za muktadha, fani na maudhui. Miega hiyo huishikilia vema riwaya katika uundwaji pamoja na utumiwaji (usomaji na uhakiki) wake. Miega yenyewe ni hii ifuatayo:
Muktadha Muktadha ni kitu cha lazima katika kila riwaya kwasababu ndiyo huipa uhai riwaya yoyote. Riwaya yoyote hutokana na muktadha fulani au mseto wa miktadha kadhaa. Aghalabu, miega mingi ya fani na maudhui hujengwa kutoka katika nguzo hii. Hivyo, ni lazima riwaya iiakisi miktadha hiyo. Aghalabu, ni nadra sana kukuta riwaya imejikita katika muktadha wa namna moja pekee. Kwa hiyo, riwaya nyingi ni zao la mseto wa miktadha ambayo mtunzi huipitia.Tanbihi: dhana hii ya muktadha ni vema ikachukuliwa kwa upana wake. Wengi huifinya kwa kuinasibisha na mazingira ya kijiografia (mandhari) pekee! Miktadha yaweza kuwa ya:o Taarifa za msingi zinazomuhusu mtunzi (kuzaliwa, kazi, elimu n.k)o Jografia (mandhari) ya maisha na mapitoo Historia ya mapito yake / jamii yake (matukio muhimu yaliyomgusa yeye au jamii yake)o Utamadunio Uchumi n.k.
MAUDHUINayo ni nguzo muhimu sana. Bila maudhui, hakuna riwaya. Hivyo, kila riwaya iliyosanwa vema lazima iwe na mwega huu. Ndani ya maudhui kuna mambo muhimu matatu ambayo ni: ujumbe, dhamira na vipopo vya fikra.
DhamiraBaadhi ya wataalamu hudai kuwa dhamira muhimu zipo 4: nazo ni: kuburudisha, kuhifadhi amali na historia, kuelimisha na kupambana na maovu / madhila yaikumbayo au yatakayoikumba jamii.
Vipopo vya FikraVipopo vya fikra au vitumba vya mawazo ni mawazo yajengekayo katika akili ya msomaji au mhakiki kutokana na vitushi vya riwaya, aghalabu, hutokana na utambuzi wake binafsi kuhusu mambo mbalimbali au tajiriba. Wengine huviita dhamira ndogo ndogo. Mara nyingine, vipopo vya fikra siyo lazima vijioneshe moja kwa moja riwayani. Bali, msomaji au mhakiki huweza kujiwa navyo tu kadri asomavyo riwaya huku akihusisha na utambuzi wake binafsi au tajiriba.
UjumbeHaya ni mavuno ayapatayo msomaji kutokana na dhamira au vipopo vya fikra. Pia, si lazima ujumbe aupatao msomaji au mhakiki ulandane na kile alichokikusudia msanii. Hii ni kwasababu, msomaji au mhakiki huweza kujenga maana ya akisomacho kutokana na kuhusisha na mazoea na utambuzi wake binafsi.
FANIHuhusisha vipengele vitengenezavyo umbo na sura ya riwaya (mjengeko na ladha ya riwaya). Vipengele hivyo viko katika makundi mawili ya: Muundo na Ubunilizi.
Dhana ya Muundo katika RiwayaHii hurejelea mjengo wa kazi yenyewe. Hujumuisha vipengele mbalimbali ambavyo huiweka kazi katika umbo na muundo husika. Muundo wa kazi ya mwandishi wategemea zaidi kanuni asilia za kazi husika pamoja na jamii aiandikiayo. Ili kupata mjengeko autakao katika kazi yake, msanii hutumia mbinu mbalimbali. Mbinu hizo huhusisha vipengele kama vile:
i. Mtindo vi. Lughaii. Vitushi vii. Migogoroiii. Udhamira viii. Muwalaiv. Wahusika ix. Mandhariv. Ushikamani Mitindo mbalimbali ya utunzi na uandishi hutokana na athari malimbali za jamii ambayo mtunzi amekulia au vionjo binafsi vya mtunzi.Kipengele kingine katika suala la mtindo ni matumizi ya nafsi. Dhana hii ya matumizi ya nafsi hurejelea matumizi ya midomo ya wahusika katika kufikisha mwazo yake. Waandishi wengi hupendelea nafsi I na ya III. Nafsi II haitumiki kwa sababu humrejelea msomaji. Hivyo, waandishi huepuka kumchoma na kumchusha msomaji. Nafsi I na III zina uhuru wa kuzitumia kwa sababu hujiweka mbali na athari zozote zimwelekeazo msomaji. Suala la nafsi ni muhimu sana katika uandishi. Kwa jumla, mbinu za kimuundo ni kipengele cha lazima cha mwega huu wa fani. Kamwe, hakiwezi kukosekana katika kazi husika na kazi hiyo ikabaki kuwa katika utanzu husika. Kipengele hiki ni tofauti na kipengele cha mbinu za kibunilizi.
Dhana ya Ubunilizi katika RiwayaRiwaya, pamoja na kazi za tanzu nyingine kama vile nudhumu na tamthiliya ni kazi za kibunilizi. Neno Ubunilizi au Ubunifu linatokana na kitenzi buni. Kubuni ni kuunda jambo. Aghalabu, jambo hilo huwa katika hali ya kidhahania kabla halijaonekana au halijadhihirika kwa hadhira kupitia ogani za fahamu. Hivyo, kwa jumla, twaweza kusema kuwa ubunilizi ni uwazaji na uundaji wa wazo katika hali inayohalisika. Dhana ya ubunilizi hutusaidia kutofautisha fasihi na matukio halisi maishani. Fasihi si maisha halisi bali ni tokeo la ubunifu wa mtunzi yaani, mtunzi ana uwezo wa kubuni visa na wahusika wake kwa njia ambayo haikanganyi hali halisi ya maisha. Mambo muhimu yamwezeshayo mtu kutunga kazi bunilizi ni:
o Silika / karama / kipawao Uwezo wa kiutafitio Uzoefuo Mawazo au fikra (taaluma)o Nia, lengo au azma
Misingi hii yatudokezea na kutusaidia kujibu swali la msingi tupaswalo kujiuliza tuifikiriapo kazi fulani ya kibunilizi na kuichukulia kuwa bora/nzuri ni: je, kazi hiyo ni tokeo/zao la msingi ya kitaaluma? Au silika (kipawa/karama)? Au tajiriba (uzoefu wa kimaisha)? Au ni tokeo la mseto wa vipengele hivyo vyote? Au ni tokeo la mseto wa baadhi ya vipengele hivyo?
Ubunifu wa riwaya na bunilizi za tanzu nyingine lazima uongozwe na kaida mbalimbali za hali halisi ya maisha. Mtunzi anapaswa kuufanya ulimwengu wake wa kubuni kuwa picha halisi ya maisha katika ukamilifu na ukweli wake. Uhalisia ni ukweli wa jambo kama lilivyo au linavyofahamika. Kuna ukweli wa aina 2 ambazo ni:
o Ukweli katika hali halisi (uhalisi na uasilia wa jambo/kitu).o Ukweli wa kisanaa (husawiri mambo yaliyobuniwa na mtunzi).Hivyo, ubunilizi ni utengenezaji wa ukweli wa jambo kadri afikiriavyo na akusudiavyo msanii. Kwa jumla, msanii hufanya ubunilizi kwa kuzingatia vigezo muhimu vinne. Hivi ni:
o Kaida za jamii (yake au anayoiandikia)o Uwezekano wa utokeaji wa jambo husikao Azma au lengo (hisia? ufunuo? kujibu?)o Hadhira
Yafaa ubunilizi usipitilize, kwani ni rahisi kwenda mbali na jamii halisi inayoandikiwa. Hata hivyo, ifahamike kuwa kumtaka mtunzi afuate kaida fulani si kumnyima uhuru wa ubunifu. Kama mtunzi atakanganya hali halisi ya maisha kama mbinu yake ya kutunga, basi na tumpe uhuru huo ilimradi kazi yake twaielewa kwa mtizamo huo. Kazi yoyote ya kisanaa lazima iwe na vipengele muhimu vya aina/makundi mawili. Haya ni: vipengele vya kimuundo na vipengele vya kibunilizi.
Vipengele vya kimuundoHivi ni vile vinavyoifanya kazi husika iwe katika utanzu au kumbo husika. Kila utanzu una aina na namna zake za vipengele vya kimuundo. Vipengele hivyo ndivyo huwa nguzo―msingi zishikiliazo tanzu husika. Kazi fulani hujulikana kuwa ni aina ama shairi, utenzi, utendi, hadithi, fupi, riwaya au tamthiliya kutokana na vipengele hivi. Vipengele vya kimuundo hutegemeana na utanzu husika. Hata hivyo, aghalabu, huhusisha vipengele kama vile: vitushi, uhusika na wahusika, ushikamani, lugha, muwala na mandhari.
Vipengele vya kibuniliziNi jumla ya mambo ambayo mtunzi huyabuni na kuyaingiza au kuyatumia katika kazi zake ili ilete mvuto na mnato kwa hadhira. Mbinu hizi huakisi kipawa cha utunzi alichonacho mtunzi na kumtofautisha na watunzi wengine. Hii ni kwa sababu, kupitia mbinu hizo, kazi hubeba vionjo tofauti (hata kama kazi hizo tofauti zinazungumzia jambo au mada inayofanana, lazima zitatofautiana kutokana na matumizi ya mbinu tofauti za kibunilizi). Vipengele vya kibunilizi vitumiwavyo sana na watunzi wa riwaya za Kiswahili ni:i. Taharuki vi. Kisengerenyumaii. Utomeleaji vii. Ufumbajiiii. Ritifaa viii. Usawiri wa wahusikaiv. Dayolojia ix. Utanziav. Ujadi x. Ufutuhi
Taharuki Ni hali ya kuwa na dukuduku la kutaka kujua juu ya nini kitafuatia katika usimulizi wa kazi ya fasihi. Mtunzi huijengea hamu hadhira yake ya kutaka kujua zaidi. Mbinu hii hutumiwa sana/hujitokeza sana katika kazi za fasihi pendwa. Hujitokeza pia katika fasihi nenwa. Taharuki, katika kazi za fasihi simulizi hujengwa kwa kutumia:
o Mabadiliko ya lugha―uso/surao Vipashio vya fonolojia arudhio MatendoNa, katika fasihi andishi, taharuki hujengwa kwa kutumia:o Mbinu nyingine za kibunilizi k.v. kisengerenyumao Utumizi wa wahusika wa ajabu―ajabuo Mandhari ya ajabuajabu
Kisengerenyuma Ni namna ya kupangilia vitushi au kusimulia kwa kuanza na tukio―tokeo kisha kufuatia tukio―chanzi. Watunzi huitumia kwa namna tofautitofauti. Mbinu hii pia husaidia sana kuboresha hamu ya hadhira kutaka kujua muundo wa vitushi vya kazi husika.
UtomeleajiHujulikana pia kama mwingiliano wa tanzu. Ni kitendo cha kuchopeka/kuingiza vipande vya utanzu mwingine (ulio tofauti na utanzu ushughulikiwao) na katika utanzu mkuu ambao mtunzi anautunga. Kwa mfano, mtunzi wa hadithi fupi huweza kuchopeka mashairi/tenzi au barua katika kazi yake kuu. Utanzu wa nathari huongoza kwa uhuru wa kufanya utomelezi ulinganishwapo na tanzu nyingine. Mbinu hii huwa na tija zifuatazo:o Kuonesha umbuji wa tanzu hizoo Kuimarisha maudhuio Kuondoa uchovu kwa wasomajio Kuweka msisitizoo Kujikaribisha na uhalisi (senkoro, 2011:70―71).
UfumbajiNi utumiaji wa kauli zenye maana fiche. Kauli hizo huwa na maana iliyo kinyume au tofauti na umbo la nje la kazi au matini husika. Ufumbaji huweza kujitokeza katika: Anuani/mada/kichwa cha habari, majina ya wahusika, Aya, Sura ya kazi, kazi nzima n.k. tija zake ni:
o Kuonesha umbuji wa kisanaao Kuishirikisha hadhira kwa karibuo Kujitanibu na ghasia za kufuatwa―fuatwa na mkono wa dola.
UjadiHuu ni utumiaji wa kauli, matendo au mazingira ya asili yanayofungamana sana na jamii inayoandikiwa. Aghalabu, ujadi hujumuisha:o Kauli kama vile methali, nahau, vipengele mbalimbali vya kimazungumzo ambavyo hutumiwa sana na jamii husika.o Matambikoo Vyakula asiliao Watunzi hufanya hivyo ili kujiweka karibu na hadhira yao.o Yaani, hadhira hujiona iko karibu sana na kazi husika waonapo baadhi ya vipengele vya usimulizi na kiutendaji vya kijadi wavitumiavyo kila siku vimetumiwa katika kazi fulani ya fasihi.o Pengine, husaidia kuongeza au kupanua hadhira.
DayalojiaHii ni mbinu ambayo mtunzi hutumia kauli za majibizano katika kuwasilisha mawazo yake. Hutumia vinywa vya wahusika wake kudokeza maudhui ayalengayo. Katika baadhi ya tanzu, dayalojia huwa ni kipengele cha kimuundo (kwa mfano, tamthiliya dayalojia ndiyo kijenzi cha msingi cha utanzu huu husika). Na kwa tanzu nyingine hujitokeza kama kipengele cha kibunilizi. Tija zake ni:o Huondoa uchovu kwa wasomajio Huonesha ufundi wa mtunzi katika matendo, maneno na hadhi ya wahusika.o Husaidia kuwasilisha mawazo kwa hali ya uasili (mtunzi huwa mbali na uwasilishaji, hadhira hupata ladha ya maudhui kutoka kinywa asilia).
Usawiri wa wahusikaNi kitendo cha kuwachora, kuwafafanua, kuwatambulisha na kuwajenga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana au unaowiana na uhusika wao. Wahusika hutumia mbinu nyingi sana katika kuwasawiri wahusika katika kazi zao. Mbinu hizo ni:o Majazi: utoaji wa majina kulingana na sifa, tabia au dhima. Kwa mfano, Rosa Mistika (katika Rosa Mistika) na Sulubu (katika Nyota ya Rehema).o Uzungumzaji nafsio Kuzungumza na hadhirao Kuwatumia wahusika wengine (Mhusika 1 kumfafanua mwingine).o Ulinganifu wa usambambao Maelezo (mtunzi kumwelezea mhusika)
RitifaaNi hali ambayo mtu mmoja hufanya mawasiliano na mtu aliye mbali naye (umbali huo huweza kuwa wa kijiografia au kufariki). Aghalabu, mawazo yasawiriwayo kupitia mbinu ya ritifaa huwa na vionjo vya kihisia sana. (kila mmoja kwa wakati wake achunguze ujitokeaji wa ritifaa katika riwaya zilizoteuliwa kama zilivyoainishwa kweye muktasari wa kozi hii).
UfutuhiNi mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali vizuavyo ucheshi, raha, kicheko au furaha kwa hadhira yake. Vipengele hivyo huweza kujengwa na kejeli, utani, dhihaka, ubeuzi na mizaha. Miongozi mwa tija zake ni:o Kufurahisha hadhirao Kuwaondolea uchovuo Kujikwepesha na nguvu za dolao Kulainisha uwasilishaji wa maudhui yanayochoma au yenye hisia kali (utasifida).
UtanziaMbinu hii ni kinyume cha ufutuhi. Ni mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali vizuavyo huzuni, masikitiko, jitimai na mateso kwa hadhira yake. Vipengele hivyo huweza kujengwa na: mateso, ugumu wa maisha, vifungo, mabaa kama vile njaa, gharika, kimbunga, magonjwa na ulemavu (wa viungo au michakato ya mwili kama vile ugumba na utasa).
HISTORIA YA RIWAYA
Riwaya na Matapo ya Fasihi
Matapo ni vipindi mbalimbali vya kihistoria ambavyo fasihi au sanaa kwa jumla imevipitia. Matapo pia huweza kutafsiriwa kuwa ni mkondo au makundi makuu ya kinadharia ambayo yametawala katika fasihi/sanaa katika nyakati maalumu. sanaa/fasihi imepitia katika mikondo mingi sana. Bali ile mikuu ni minne. Nayo ni:o Tapo la Urasimi Mkongwe (850 ― 325 K. Y. M)o Tapo la Urasimi Mpya (1680 ― 1780 B. Y. M)o Tapo la Ulimbwende (1790 ― 1870 B. Y. M)o Tapo la Uhalisia (Baada ya utawala wa Malkia Viktoria na Mapinduzi ya viwanda hadi sasa).Matapo haya yaliingiliana na kukamilisha kwa kiwango kikubwa katika muda wa kuwapo kwake. Hivyo, yawezekana kuwa matapo mawili au zaidi yakatamalaki kwa wakati mmoja.TAPO LA URASIMI MKONGWEDhana ya Urasimi humaanisha mkusanyo wa mikondo ya kifikra au kimtazamo ambayo chanzo chake ni sanaa na utamaduni wa Wayunani na Warumi. Dhana hii ilijiegemeza sana katika usimikwaji wa sheria na taratibu mbalimbali za kuongoza utendekaji wa sanaa/fasihi. Sehemu kubwa ya mawazo yao katika sanaa ilimezwa na nadharia ya MWIGO. waasisi/wadau wakuu wa Urasimi mkongwe ni: Plato na AristotleMuhtasari wa Mawazo ya Plato Kuhusu Sanaao Uhusiano baina ya uwezo wa mshairi na nguvu za Mungu. Anaamini kuwa msanii ni kiumbe kitakatifu ambacho hupokea mawazo maalumu/ufunuo kutoka kwa Mungu ili afikishe ujumbe kwa hadhira.o Uwezo wa msanii hautokani na hekima zake, bali jazba na mpagao utokao kwa Mungu.o Muigo si chochote, kwani msanii huigiza uhalisia wa maisha ambao hata yeye mwenyewe haujui.o Alitoa sheria muhimu zilizopaswa kuimiliki sanaa ya utungaji mashairi (wasanii wote walipaswa kuzifuata). Sheria hizo ni:o Kazi yoyote ya ushairi lazima ipitiwe na kamati maalumu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50.o Watunga mashairi wote lazima watimize miaka 50.o Ushairi lazima ueleze mazuri tu (kama vile juu ya mashujaa na watawala wa nchi).o Washairi wasitunge chochote kilicho kinyume cha sheria za Jamhuri. (Rejea kitabu chake, The Laws)Muhtasari wa Mawazo ya Aristotle juu ya Sanaao Kuhusu Ushairi na Tamthiliya (sanaa): Mwigo/uwakilishi ni nadharia bora. Kulingana na Aristotle, mwigo ni kiwakilishi cha maisha (uhalisi), maisha yenyewe halisi. Mwigo hupunguza au kuondoa madhara yatokanayo na woga au hasira.o Kuhusu Hadhira: Sanaa iwe na hadhira mbili ambazo ni: Hadhira ya watu wa nasaba bora (Tanzia) na Hadhira ya watu wa nasaba duni (Futui). Tanzia: kwa mujibu wa Aristotle, ni masuala tata yenye kusikitisha na kufikirisha. Futuhi: ni masuala mepesi na yanayochekesha. Watu duni wapewe haya kwa vile akili yao haiwezi kuchambua mambo.o Kuhusu Muundo mahususi: Sehemu za kazi ya sanaa sharti zioane/ziwiane. Kazi ya sanaa iwe na sehemu 3 ambazo ni kichwa, kiwiliwili na miguu. Miundo hii itofautiane kulingana na aina ya kazi (kama ni tanzia au futuhi). Alisisitiza kuwapo kwa nguzo muhimu katika sanaa (tamthiliya). Nazo ni:ü Muundo/msukoü Wahusikaü Nyimboü Wazo kuu (maudhui)ü Hadhiraü Lugha bora kulingana na hadhirao Kuhusu Historian na ukweli katika sanaa: Sanaa ni mwigo au kiwakilisho cha ukweli na uhalisia wa maisha ya jamii. Hivyo, mwanasanaa huelezea historia kupitia sanaa. Huweza kuweka mipaka ya historia iliyopita na iliyopo. Pia huweza kuvuka mawanda ya uhalisia uliopita na uliopo. Hivyo akasema Sanaa ni halisi kuliko uhalisi wenyewe. Na ina ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe.Vigezo vya Jumla vya Tapo la Urasimio Kuwapo kwa fani mahsusio Kuoana kwa fani na lengo/maudhui ya kazi ya sanaa (ulinganifu)o Kueleweka kwa kazi ya sanaa (urahisi)o Kutiliwa maanani kwa muundo na mpango mahususio Mtindo mahsusio Kuheshimu jadio Kutotawaliwa na jazba (msanii aitawale jazba).
TAPO LA URASIMI MPYABaadhi ya wadau wake ni: Donne, Market, Herrick, Hrbvert, Cowley, Vongham, Crasha na wengine wengi.
Mambo ya Msingi Kuhusu Tapo hili ni:
o Lilizingatia kigezo cha Mantiki na Mjadala katika kazi za sanaa (mashairi)o Kazi za sanaa lazima ziwe na fumbo litakalomfikirisha msomaji (hadhira)o Sanaa lazima iwe kwa ajili ya watu. Wadau wa tapo hili walimchukulia binadamu kuwa ni kiumbe mwenye kasoro asotimia; ambaye alitakiwa arekebishwe na kazi za fasihi/sanaa. Hivyo, kufaulu au kushindwa kwa kazi ya fasihi/sanaa kupimwe kulingana na kufaulu au kushindwa kwake kumzingatia/kumtumikia mtu. Yaani, sanaa lazima imfurahishe, imsahihishe na imwelimishe mtu katika maisha yake.o Kuwapo kwa Mpango mahsusi katika kazi ya sanaa.o Kuzingatiwa kwa sheria za utungaji kulingana na aina ya utanzu.
Athari za Tapo la Urasimi Mpya katika Sanaa ya sasa
o Uteuzi mahsusi wa maneno na tungo/mishororoo Umuhimu wa taswira katika ushairio Matumizi ya akili kuliko jazba (hasa wakati wa utungaji wa kazi za fasihi)
TAPO LA ULIMBWENDELilishamiri barani Ulaya mnamo karne ya 18 hadi 19. Lilitokana na msisimko wa kifasihi, kifalsafa, kidini, kisiasa na kisanaa kutokana na Urasimi mpya. Wadau maarufu wa Tapo hili ni:o Uingereza, walikuwa: William Wordsmith na George Grabbeo Ujerumani, walikuwa: Goethe, Holderline na Schillero Ufaransa: Victor Hugoo Italia: Novalis
Mambo ya Msingi kuhusu Tapo hili:
o Sifa yake kuu ni uhuru wa msanii. Msanii alipata uhuru wa kuchagua mada, hadhira na lugha kwa matakwa yake. Mambo ya kufikirika kama vile mambo ya ndoto/ruya yalianza kuandikwa.o Pia wahusika wa ajabuajabu walianza kutumika kwa mfano, shetani na jangili.o Lilizingatia hisia za ndani pamoja na mazingira ya mzungukayo mtu huyo.o Tapo hili lilielezea maisha jinsi wao (watunzi) walivyotaka yawe.Kuzuka kwa tapo hili kulichangizwa na kuwapo kwa mambo kadhaa ambayo yalisababisha msisimko na athari za maisha ya wakati huo. Mambo hayo ni:o Safari za kuvumbua ulimwenguo Harakati za USA kudai uhuru wakati huoo Kuzuka kwa miji na viwanda kwa harakao Ulinganishi wa nguvu za kisilaha na kisiasa baina ya mataifa mbalimbalio Mivutano na harakati za kitabaka.
Vigezo vya Jumla vya wana―Ulimbwende ni:
o Kutilia mkazo mazingira na asilio Kuandika/kusana kazi mbalimbali zilizowazungumzia wahusika kuanzia utoto waoo Matumizi ya wahusika wa ajabuajabu kama vile shetani, jangili, wavunja sheria, Malaya n.k.o Kuruhusu matumizi ya ndoto zilizovuka mipaka ya uhalisi wa maisha. Hii iliruhusiwa ili kurekebisha matumizi ya fani na maudhui katika utunzi.o Kupinga sheria zilizowekwa na Wanaurasimi: kama vile: Kutenga hadhira, kutenga mitindo ya lugha kulingana na matabaka ya hadhira na kutenga baadhi ya wahusika kulingana na nasaba.
TAPO LA UHALISIA
Uhalisia ni sawa kabisa na udodosi―mambo ambapo huwa na uzingatiaji mkubwa wa uhalisi katika kuwasilisha uhalisi huo katika fasihi. Lilielezea maisha kwa jinsi yalivyo, yaani jambo lilielezwa kwa undani na kweli. Miongoni mwa waasisi wake ni Hegel. Mazingira na wahusika walisawiri kikwelikweli kuyaakisi maisha ya kila siku (kwa kuzingatia furaha, huzuni, matumaini, matazamio na matatizo)Lilishamiri katika karne ya 20. Tapo hili lilijihusisha sana na riwaya.
Mambo yaliyochochea kuzuka kwa Tapo hili
o Maendeleo ya sayansi na teknolojiao Kuwepo kwa silaha kali na mapiganoo Mivutano au migogoro kati ya matajiri na maskini duniani koteo Vuguvugu la nchi nyingine kudai uhuru
Vigezo vya Tapo la Uhalisia
o Demokrasia katika uumbaji wa fani na maudhui ya kazi ya fasihio Usawiri mwanana wa mambo yanayotokea kila siku katika maisha ya watu.o Kuijua kwa kina dhana ya MWIGO. Mwanauhalisia lazima ajue jinsi ya kuiga na akijue akiigacho. Kwa kufanya hivyo, itasaidia nafasi kati ya kiingwacho na mwigo kutokuwa kubwa.o Kutofungwa na ulazima wa kuwa na mpangilio wala muundo maalum katika kazi za sanaa. Hii ni kwa sababu maisha hayana muundo wala mpangilio maalum.o Msanii azingatie athari za kazi yake katika hadhira yake.o Athari hizo zaweza kuletwa na mambo kama vile urahisi (au usahili katika usanaji), umoja kwa moja katika kufafanua maudhui na usahihi wa mambo.o Kazi yoyote ya fasihi lazima iwe na jukumu la kuadilisha na kufunza.
Aina za uhalisia
1. Uhalisia wa Kibwanyenye2. Uhalisia wa Kihakiki3. Uhalisia wa Kijamaa4. Uhalisia Ajabu
Uhalisia wa Kibwanyenye
Waandishi wake huandika na kusawiri uozo wakati wa ubwanyenye. Hata hivyo, hawatoi masuluhisho ya kisayansi kuhusu migogoro iliyomo katika jamii.
Uhalisia wa Kihakiki
Mawanda yake hayaivuki jamii husika. Huihakiki jamii hiyo husika tu. Huchambua mambo ya jamii kwa namna moja, kwandani tu au kwa nje tu.
Uhalisia wa Kijamaa
Huchambua mambo ya jamii kutoka ndani na nje ya jamii. Humchambua mhusika kwa kumhusisha na nguvu mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.
Uhalisia Ajabu
Wengine huuita uhalisia mazingaombwe. Huchanganya uhalisia na mambo ya ajabuajabu. Uajabu―ajabu hapa unarejelea matumizi ya wahusika, mandhari na hata vitushi vilivyo nje ya hali ya kawaida. Mfano mmojawapo wa kazi iliyo katika kijitapo hiki ni Baba alipofufuka, utata wa 9/12, Nagona n.k.
HISTORIA YA KUIBUKA KWA RIWAYA Chimbuko la riwaya linapatikana katika fasihi simulizi, ambayo, kwa kiasi kikubwa, imebebwa na sanaa―jadi, miongoni mwa tanzu maarufu za fasihi simulizi zilizoibua riwaya ni ngano na hekaya.
Ngano, ni sanaa ya jadi ya kisimulizi itokanayo na matukio maalumu ya kihistoria katika jamii husika. Huwa fupi na wahusika wake ni wachache; huku ikitumia mifano mingi.
Hehaya, ni hadithi za kimapokeo zenye kusisimua na kustaajabisha huku ikijumuisha kitushi zaidi ya kimoja. Huwa fupi na wahusika wake ni wachache, huku ikitumia mifano mingi.
Kabla ya kuiangazia historia ya riwaya ya Kiswahili, ebu tutupie jicho katika kutazama historia ya riwaya kiulimwengu kwa kuangazia mabara mawili ya Ulaya na Asia.
Riwaya katika Bara la Ulaya
Riwaya ni utanzu mchanga zaidi ukilinganishwa na ushairi na tamthiliya. Tanzu za ushairi na tamthiliya zina umri karibu sawa na historia ya mwanadamu. Riwaya ilipata umbo ililonalo hivi sasa karne ya 18 huko Ulaya. Hata hivyo, mbali na umbo la hivi sasa, historia ya riwaya inaanzia karne ya 3 hadi ya 4 K.Y.M. Madumulla (2010) anadai kuwa katika miaka hiyo kuna mtaalamu aitwaye Voltaire ambaye alidai kuwa kulikuwa na kitabu kiitwacho Cyropaedeiakilichoandikwa na Myunani Xenopheno (430―355 KK). Kitabu hicho kilikuwa ni riwaya. Nchini Uingereza, uandishi wa riwaya ulizaliwa na kupata ukomavu katika kipindi kifupi.
Sababu zilizochochea utanzu wa riwaya kukomaa kwa haraka ni:
o Elimuo Ukomavu wa uchumio Maendeleo ya sayansi na teknolojiao Kutulia kwa jamii zao (utulivu wa kuishi pamoja).
Riwaya Asia
Habari za historia ya riwaya katika bara hilo ni chache sana. Hivyo, historia yao inatuangazia kuwapo kwa riwaya huko toka karne ya 7. Kwa mfano, katika karne hiyo, Dandin aliandika hadithi iitwayo Dasakumarakarita iliyohusu masaibu ya wana kumi wa Mfalme. Aidha, huko Japani kulikuwa tayari na maandiko kadhaa yenye mwelekeo wa kiriwaya. Mkabala wao wa kiuandishi ulijikita katika mtazamo wa Ki ― marx hasa baada ya kuzaliwa kwa Azimio la Kikomunisti (1848). Baadhi ya kazi hizo ni pamoja na: Taketori Monogatari (850 ― 920), Utsubo Monogatari (850 ― 900), diwani ya hadithi zilizoitwa Yamoto Monogatari, Ochikubo Monogatari (Mwishoni mwa karne ya 10), sumiyoshi Monogatari (1200), riwaya ya kimapenzi iliyoitwa Gempei Seisuku (1200 ― 1250) na riwaya ya kivita iliyoitwa Taibeki (1367 ― 75). (Kwa ziada, tazama. Madumulla, 2010).
Usuli wa Riwaya katika bara la Afrika
Historia ya riwaya katika bara la Afrika ni fupi sana. Inaanzia karne ya 20. Huko Afrika ya Kusini na Afrika ya Magharibi, maandiko ya kifasihi yalianza mwishono mwa karne ya 19. Yalichagizwa sana na kuwapo kwa shughuli za kimishenari au kikoloni kwa jumla. Fani na maudhui ya kazi hizo viliakisi mazingira ya kijadi ya maeneo hayo. Kwa maelezo zaidi, rejea Madumulla, (2010:23―35).
RIWAYA YA KISWAHILI
Kabla ya kuitupia jicho dhana ya riwaya ya Kiswahili, ni vema kuimulika dhana ya Fasihi ya Kiswahili. Dhana hii imekuwa inawachanganya wanataaluma wengi. Hii kwa sababu inachanganya kwa pamoja dhana kadhaa. Dhana hozo ni:
o Fasihi ya Kiswahilio Fasihi katika Kiswahilio Fasihi kwa Kiswahilio Fasihi ya Waswahili
Ili kuzielewa vema dhana za fasihi ya Kiswahili na riwaya ya Kiswahili, kwanza tunatakiwa ku mjua Mswahili.
Ponera (2010:69), Mswahili ni mtu mwenye kiwango kikubwa cha umilisi wa lugha ya Kiswahili. Vilevile, ni mtu ambaye amefungamana sana na mila na desturi za jamii ya watumiao lugha ya Kiswahili kiasi hata cha kumuathiri kifikra, kimtazamo na kiitikadi. Fasili hii inatumulikia ukweli kuhusu kuwapo kwa Fasihi ya Mswahili au Waswahili (watu). Fasihi hiyo ilisanwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili, hivyo kuwa na sifa ya kuitwa fasihi ya Kiswahili kama ilivyo kwa fasihi ya mjerumani isanwayo kwa kutumia lugha ya kijerumani; hivyo kuitwa fasihi ya kijerumani. Dhana ya fasihi katika Kiswahili au fasihi kwa Kiswahili imetokana na sababu kadhaa zikiwemo mwingiliano wa jamii mbalimbali za hapa duniani, pamoja na shabaha ya kupanua hadhira (hatimaye kupanua soko). Hii ni ile fasihi ambayo ina mahadhi ya lugha za kigeni lakini iko katika lugha ya Kiswahili (mfano. Alfu Lela U Lela, Mashimo ya Mfalme Suleimani, Safari za Guliva, Hekaya za Abunuwasi, Safari Saba za Sindbad Bharia).
Hivyo, kwa muktadha wa kozi hii, fasihi ya Kiswahili ni ile iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili na inazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mswahili. Nayo ni kama vile hali ya maisha yao, mila na desturi zao, chakula chao na kaida nyinginezo. Kuwapo kwa fasihi ya Kiswahili ni ithibati tosha ya kuwapo kwa riwaya ya Kiswahili. Chimbuko lake limo katika simulizi za asili (ngano, visa kale na visa sili).
HISTORIA YA RIWAYA YA KISWAHILI
Riwaya ya Kiswahili ina hazina ndefu. Misingi yake hupatikana katika fasihi simulizi. Riwaya za kisasa zinatokana na juhudi za wageni na wenyeji. Wageni walijihusisha na kuweka msingi katika karne ya 19.
Juhudi za kwanza zilihusu kukusanya nathari za wenjeji. Kisha, ikafuata hatua ya kutafsiri ngano za wenyeji katika lugha za kigeni. Kwa mfano, mwaka 1870 Edward Steere ilianza kutafsiri hadithi kutoka Zanzibar katika lugha ya Kiingereza. Mwaka 1889 alichapisha kitabu kiitwacho Swahili Tales as Told by the Native of Zaznzibar. Hiki ni kitabu cha muhimu kwa sababu kinatoa dira kuhusu historia ya mwanzo ya riwaya za Kiswahili. Mwaka 1907 Carl Vetten alichapisha kitabu kiitwacho Prosa and Poesie de Suaheli kwa lugha ya kijerumani.
Hatua iliyofuata ni kutafsiri fasihi za kigeni kuwa ya Kiswahili. Kwa mfano, mwaka 1928 Edwin Brenn alitafsiri kitabu kiitwacho Alaza. Mifano mingine ni: Alfu Lela Ulela, Mashimo ya Mfalme Suleimani, Hadithi za Esopo, Hadithi za Mjoma Remas na Hekaya za Abunuasi. Kazi hiyo ya kutafsiri ilipamba moto tangu mwaka 1930 wakati halmashauri ya Kiswahili ya Afrika mashariki ilipoanzishwa.
TANBIHI: Kila mmoja ajibidiishe kuchunguza mchango wa wageni katika kuchipuka kwa riwaya ya Kiswahili. Miongoni mwao ni:
o Edward Steereo Car Buttnero Carl Velteno Lyndon Harrieso Jann Knappero Edwin Brenno J.W.T. Allen
Baada ya hapo, waafrika wakaanza kutunga riwaya. Walitunga kutokana na kuhamasishwa na halmashauri hiyo ya Kiswahili. Mfano, mwaka 1934 James Mbotela alitunga riwaya ya Uhuru wa Watumwa. Riwaya hii ilisanifiwa na Halmashauri ya Kiswahili kwa sababu iliwaponda Waarabu na kuwakweza Waingereza ambao walikuwa katika Halmashauri ya Kiswahili.
Riwaya ya Uhuru wa Watumwa ni kielelezo kimojawapo cha riwaya za mwanzo za Kiswahili. Watunzi wengine wa kiafrika ni pamoja na Shaaban Robert na Abdallah S. Farsy (aliyetunga riwaya ya Kurwa na Doto: 1961).
Baadhi ya waandishi wa kiafrika baada ya uhuru walipanua wigo na kuandika juu ya mambo mengi zaidi. Mfano, zikatungwa riwaya za upelelezi. Faraji katalambula alitunga riwaya ya Simu ya Kifo. mohammed Said Abdallah alitunga riwaya nyingi za upelelezi mhusika wake mkuu aliitwa MSA. Mifano ya kazi zake ni:
o Duniani Kuna watuo Kisima cha Giningio Mzimu wa watu wa kaleo Mwana wa yungi Hulewao Siri ya sifurio Kosa la Bwana MSA
Kisha, watunzi wakageukia kutunga juu ya siasa wakiongea juu ya masuala mbalimbali kama vile viongozi wanafiki, mikutano ya siasa. Mifano ya kazi hizi ni: Njozi iliyopotea na Gamba la Nyoka. Kwa ujumla, wanariwaya walikuwa wanaandika juu ya masuala ya jamii wakiwa na nia ya kukosoa, kuelimisha na kadhalika. Waandishi wamekuwa wakikomaa katika kuandika kwa kuzingatia maudhui na fani inayorandana na miktadha. Kabla ya uhuru waliandika kikasuku pasipo kuchambua. Kwa mfano, Mbotela alipowasifia waingereza katika Uhuru wa Watumwa. Pia uchoraji wa wahusika umekuwa ukikomaa kutoka kipindi kimoja hadi kingine.
Maendeleo ya riwaya ya Kiswahili
Toka ichimbuliwe ama ianzishwe, riwaya ya Kiswahili imepige hatua kubwa. Umekuwepo mwondoko mpya katika maeneo kama vile ya:
o Idadi ya kazi za riwayao Ubora wa riwaya zenyeweo Matumizi ya lughao Mwelekeo wa maudhuio Mabadiliko ya motifu n.k.
Maendeleo haya ya ubunilizi wa riwaya, pamoja na sababu nyingine, yamechochewa sana na ongezeko la hali ya usomi na wasomaji katika jamii ya waswahili. Mchango wa ongezeko hilo la hali ya usomi na wasomi katika jamii ya waswahili linaweza kutazamwa kupitia maeneo kama vile; Utungaji, Usomi na utafiti kuhusu masuala ya riwaya.
MAPOTE (MAKUNDI) YA RIWAYA
Riwaya kwa ujumla imegawanyika kwenye makundi makubwa mawili. Makundi hayo ni:
o Riwaya dhatio Riwaya pendwa
Riwaya dhati
Sifa zake ni pamoja na;
o Huzungumzia mambo nyeti, adhimu na yenye thamani katika jamii.o Watunzi wake huwa na nia ya dhati ya kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha.o Hukubalika na sehemu kubwa ya jamii.o Huwa na lugha fasaha, nyoofu, adilifu na zisizo na matusi.o Utolewaji wake huthibitishwa na ogani au mamlaka husika.Mifano ya riwaya dhati na watunzi wake:
Muhammed Said Abdulla (MSA)
o Kosa la Bwana MSAo Kisima cha Giningio Duniani kuna Watuo Siri ya Sifurio Mwana wa Yuni Hulewao Mzimu wa Watu wa Kaleo Mke Mmoja Wanaume Watatu
Said Ahmed Mohamed
o Asali Chunguo Tata za Asuminio Dunia Yaoo Kiza katika Nuruo Dunia Mti Mkavuo Utenganoo Babu Alipofufuka
Seti Chachage
o Makuadi wa Soko Huriao Almasi za Bandiao Sudi ya Yohanao Kivuli
Anicet Kitereza
o Bwana Muyombekere na Bibi Bugonoka
Shaffi Adamu Shaffi
o Kulio Hainio Vuta N‘kuvuteo Kasri ya Mwinyi Fuado Mbali na Nyumbani
J.K. Kiimbila
o Ubeberu Utashindwao Lila na Fila
Euphrase Kezilahabi
o Rosa Mistikao Kichwa Majio Gamba la Nyokao Dunia Uwanja wa Fujoo Nagonao Mzingile
Shaaban Robert
o Kusadikikao Kufikirikao Utubora Mkulimao Siku ya Watenzi Woteo Adili na Nduguzeo Wasifu wa Siti Binti Saad
Riwaya Pendwa
Hizi ni zile zinazovuta nadharaia na kupendwa sana na watu takriban wa marika yote. Zinahusu maeneo yafuatayo: Mapenzi, Ujambazi, Ujasusi na Upelelezi.Baadhi ya wataalamu hutilia mashaka ukubalifu na ufaafu wake katika jamii. Riwaya hizi aghalabu hujengwa na sifa zifuatazo:
o Kujichomoza zaidi kwa fani kuliko maudhuio Kujengwa zaidi kwa msingi wa taharukio Kuvuma ghafla na kuzima/kufifia ghaflao Huwa na u―mjini zaidi kuliko u―kijijinio Huwa na uharaka. Uharaka huo hujitokeza katika: Uhariri na Utunzi (mtiririko wa visa huwa na kasi)o Uzalishaji na usambazaji wake hufanywa bila udhibiti mkubwao Hutumia utusi na u ajabu ajabu kama nyenzo muhimu za kusisimua hadhira.
Mifano ya riwaya pendwa na watunzi wake:
John Simbamwene
o Mwisho wa Mapenzio Kwa sababu ya Pesao Mauaji Lojingi
Elvis Aristablus Musiba
o Kufa na Kuponao Njamao Kikosi cha Kisasio Hujumao Hofuo Kikomo
Eddie Ganzel
o Kitanzio Msako wa Hayawanio Zubaa Uzikweo Zawadi ya Bwege
A.Muhoza
o Pendo la Kifo
Mbunda Msokile
o Nitakuja kwa Sirio Usiku Utakapokwishao Mapambanoo Dhihaka ya Mumeo Amani ya Ukubwa
Ben R. Mtobwa
o Mikononi mwa Nundao Joram Lazima Ufeo Tutarudi na Roho Zetu?o Salamu Toka Kuzimuo Nyuma ya Paziao Roho ya Pakao Mtambo wa Mautio Dar es Salaam Usiku
Alex Banzi
o Titi la Mkweo Zika Mwenyewe
UAINISHAJI WA RIWAYA
Pamoja na riwaya zote kuangukia katika mojawapo ya makundi haya, bado zinaweza kuainishwa zaidi katika makundi mengine mbalimbali. Hata hivyo, uainishaji wa riwaya ni jambo linalosumbua sana mawazo ya wanazuoni. Pamoja na kukinzana huko, wanazuoni wanakubaliana kuwa uainishaji wa riwaya huweza kufanywa kwa kutumia vigezo anuai. Vigezo maarufu vitumikavyo ni vinne (4). Navyo ni: kwa kuzingatia fani, usimulizi, upeo wa kijiografia na maudhui.
Aina za Riwaya kwa Kuzingatia Fani
Kwa kigezo hiki, riwaya huwekwa katika makundi matatu. Nayo ni: Riwaya Sahili; Riwaya Changamani na Riwaya za Kimajaribio.
Riwaya Sahili
Sifa zake bainifu ni pamoja na;
o Maudhui yake ni mepesi kuelewekao Mandhari yake huwa halisi na rahisio Vitushi vyake viko wazio Hutumia lugha ya moja kwa mojao Kwa jumla, hazina utata katika vipengele vyake
Riwaya Changamani
Sifa zake bainifu (ni kinyume cha riwaya Sahili);o Maudhui yake huhitaji tafakuri ili kuyaelewao Vitushi vyake hutanzwao Hutumia lugha isiyo ya moja kwa moja (ya mafumbo).
Riwaya za Kimajaribio
Sifa zake bainifu ni pamoja na;
o Hutumia mbinu na utaratibu usiozoeleka katika kumbo hili la riwaya.
o Hii inamaanisha kuwa hutumia vipengele mbalimbali vya fani na maudhui ambavyo ni vigeni. Kwa mfano, matumizi ya nafsi ya MIMI kama mhusika katika riwaya.
o Mfano wa riwaya hizo ni Nagona na Mzingile.
Aina za Riwaya kwa Kuzingatia Upeo wa Kijiografia
Kwa kigezo hiki, riwaya huwekwa katika makundi manne (4). Nayo ni; Riwaya za Kiambo, Riwaya za Kitaifa, Riwaya za Kimataifa na Riwaya za Kidaistopia.
Riwaya za Kiambo
Huhusu masuala ya mila, desturi na mandhari maalum ya mahala fulani. Mifano ya riwaya hizi ni: Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka, Kurwa na Doto, Kisima cha Giningi na Mirathi ya Hatari n.k.
Riwaya za Kitaifa
Hujikita katika upeo wa kijiografia usiovuka mipaka ya taifa fulani. Hivyo, maudhui yake huzungukia yanayojiri, yaliyojiri au yatakayojiri katika taifa fulani.
Riwaya za Kimataifa
Hizi ni kinyume cha riwaya za kitaifa. Hujikita katika upeo wa kijiografia usiovuka mipaka ya taifa fulani. Hivyo, maudhui yake huzungukia yanayojiri, yaliyojiri au yatakayojiri katika taifa husika.
Riwaya za Kidaistopia
Hizi husawiri jografia ya jamii isiyokuwa ya kawaida, ya kidhahania. Kwa namna fulani, mandhari zake kuogofya. Baadhi ya riwaya za Shaaban Robert na Kezilahabi zinaweza kuingia katika kundi hili. Hizo ni pamoja na: Nagona,Mzingile, Kufikirika na Kusadikika.
Aina za Riwaya kwa Kuzingatia Usimulizi
Riwaya za Monolojia
Ni riwaya ambazo hutawaliwa na sauti ya mtunzi. Yaani mtunzi husimulia kwa sehemu kubwa kwenye kazi yake.
Riwaya za Barua
Usimulizi wake huwa wa kibarua. Kwa mfano, Barua Ndefu kama Hii.
Aina za Riwaya kwa Kuzingatia Maudhui
Riwaya za kihistoria
Riwaya za mwegamo huu huakisi matukio ya kihistoria. Wahusika wake husawiri kwa makini ili kutia kumbukizi ya wakati uliopita. Riwaya hizi si kitabu cha kihistoria, bali ni huakisi tu matukio ya kihistoria. Huwa na urazini wa historia ya jamii. Mifano ya riwaya za mtazamo huu ni: Miradi bubu ya Wazalendo (G. Ruhumbika), Kifo cha Ugenini (Olaf Msewe), Kasri ya Mwinyi Fuadi (Shaffi Adam Shaffi), Zawadi ya Ushindi, Kwa heri Islamagazi (Mapalala), Uhuru wa Watumwa na Moto wa Ngoma ya Mianzi (Mulokozi).
Riwaya za Kimaadili (Riwaya za kidini)
Maranyingi hudokeza mapito ya mhusika mkuu toka utoto wake. Hujaribu kueneza maadili kwa jamii. Wahusika huwekwa ili wawe chachu ya maadili kwa jamii na kupinga uovu. Kwa mfano, Adili na nduguze na Kusadikika vya Shaaban Robert. Aghalabu, hujikita katika masuala ya dini. Misingi yake hukitwa katika vitu au mambo matatu ambayo ni: Pathema (yaani makosa au kosa), Mathema (yaani mafunzo au funzo) na Catharsis (yaani utakaso).
Riwaya za Kiamapinduzi
Huwazindua wasomaji ili wapambane na udhalimu na kubomoa mifumo ya ukandamizaji iliyopo katika jamii. Hudodosa dhana za mapambano, mikinzano na matabaka, riwaya hizi maranyingi ni za kihalisia. Mifano ya kazi za kundi hili ni: Kabwela (Abdulhaman Jumbe Safari), Ubeberu Utashindwa (Kiimbika), Kuli na Haini (Shafi Adam Shafi),Kusadikika (Shaaban Robert), Utengano (S.A. Mohamed na Dunia Mti Mkavu (S.A. Mohamed).
Riwaya za Kisosholojia
Riwaya zake huchunguza na kuibua maswali ya kijamii na kupiga darubini kali katika jamii. Hukazia vipengele vihusuvyo maisha ya kila siku katika jamii (desturi, mila na mabadiliko ya jamii). Huwa na uhalisi katika vipengele vyake. Maranyingi huwa na maudhui yenye kuhuwisha. Hugusia migongano ya kijamii kama vile ukale na usasa, umji na uvijiji, familia na ndoa kwa ujumla. Kwa mfano: Kurwa na Doto (M. Farsi), Dunia Uwanja wa Fujo, Mzimu wa Babu ana Radhi (F. Nkwera), Bwana Mnyombekera na Bibi Bugonoka na Harusi (A.J. Safari).
Riwaya za Kisaikolojia
Hujaribu kufichua hali ya kisaikolojia katika jamii kwa kuwatumia baadhi ya wahusika. Maudhui yake huhusu vita vya mazoea dhima ya uhalisi. Hujadili mikinzano aipatayo mtu ki―nafsi, ki―jamii na ki―uana. Hukitwa katika kuwako kwa (Kosa/udhaifu/jambo hasi/ utata na misawajiko kwa mhusika kuu). Mfano: Tata za Asumini (S. Ahmed) Kichwamaji(Kezlahabi).
Riwaya za Kifalsafa
Hujadili mambo yenye urazini fiche. Mtunzi hudadisi mambo mbalimbali kwa jicho la kifalsafa (udodosi wa kina). Aghalabu, hutumia lugha tata na ngumu. Miongoni mwa mambo hayo yanayododoswa ni kuishi, ukweli, maisha, utu, kifo, kuwa na kutokuwapo kwa viumbe, kuwepo kwa Mungu n.k. baadhi ya maswali ya kifalsafa yaulizwayo ni kama vile:
o Maisha ni nini?o Kuwapo na kutokuwapo kwa dunia ni kwatokeaje?o Kuishi ni nini?o Utu ni nini?o Kwa nini watu au vitu vipo hivyo vilivyo?o Kwa nini mambo yapo hivyo yalivyo?Mifano ya riwaya za kifalsafa ni riwaya kadhaa za Kezilahabi. Nazo ni: Mzingile, Nagona, Rosa Mistika, Kichwamaji. Riwaya za kifalsafa zilizoandikwa na waandishi wengine ni pamoja na: Babu Alipofufuka, Umleavyo, Walenisi, Mafuta naBin―Adamu.
Riwaya Pendwa
Husisimua na huwa na mvuto wa pekee kwa wasomaji. Aghalabu, fani hujichomoza zaidi kuliko maudhui. Pia humfikirisha sana msomaji. Rejea sifa mbalimbali zilizojadiliwa katika tapo la riwaya pendwa pamoja na mifano yake.
Riwaya za kitawasifu (riwaya sira)
Hizi ni tofauti na tawasifu. Riwaya zenye mwegamo wa kitawasifu zimetungwa kama vile tawasifu. Tawasifu hueleza maisha ya mtunzi. Riwaya ya kitawasifu hueleza maisha ya mhusika aliyeteuliwa na mtunzi. Huweza kuegemea u―chanya tu na kuacha kudokeza mambo hasi. Hulenga kutoa kumbukizi ili kuwahimiza wengine kuwa kama mhusika wa tawasifu. Katika riwaya ya kitawasifu, sauti ya mtunzi husikika kupitia maisha ya mhusika. Mfano mzuri wa tawasifu ni: Maisha yangu na baada ya Miaka Hamsini na Tippu Tip.
Riwaya za kiwasifu
Hizi hutungwa kama wasifu. Mtunzi hueleza maisha ya wahusika fulani. Katika wasifu mwandishi hueleza juu ya mtu aliyewahi kuishi au anayeishi. Wakati katika riwaya ya kiwasifu mtunzu hueleza maisha ya kubuni ya mtu ambaye labda hajawahi kuishi. Mifano ya riwaya ya kiwasifu ni: Shida (Ndyanoa Balisdya), Wasifu wa Siti Binti Saad (S. Robert),Salum Addallah (J. Mkabarab), Maisha ya Seti Benjamini, Mtemi Mirambo na Mkwawa na Kabila Lake.
DHIMA ZA RIWAYA
Pamoja na dhima nyingine za fasihi, riwaya inayo dhima ya ziada. Hii ni kushawishi (Propaganda). Propaganda ni kani ilengayo kushawishi mtu au watu kuelekeza fikra zao kule ajiegemezako mtunzi, propaganda huweza kutokea katika uga wowote wa kimaisha (hata nje ya uga wa fasihi). Propaganda hulenga kuleta ushawishi kwa watu ili wapate mabadiliko ya aina tofauti; ambayo ni: Ya kimtenguo, ya kiuimarishaji na ya kiupya. Aina hizi za propaganda huweza kudhihirika katika riwaya mbalimbali.
Kazi ya mjadala:
Soma riwaya teule kwa makini, jenga mantiki kisha onyesha ujitokeaji wa dhima ya propaganda.
MBINU ZA KIFANI ZINAZOJICHOMOZA KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI
Kwa kiwango cha kozi yetu, tutavidodosa vipengele vifuatavyo:
o Naratolojia (usimulizi, mwendo wa riwaya)o Msuko wa vitushi na motifuo Uhusika na wahusikao Lughao Mianzo na miisho ya riwaya
Naratolojia
Ni taaluma inayohusu suala la usimuliaji katika kazi za kiuandishi. Hudokeza masuala muhimu yafuatayo:
o Usimulizi (aina, sehemu alipo msimuliaji n.k)o Kuhusiana kwa vitushi na matukio (kusababisha, kuathiriana na kuendelezana).o Suala la wakati/muda katika riwaya.o Mwendo wa kazi husika.
Aina za Usimulizi katika Riwaya
Kuna aina kuu mbili za usimulizi. Nazo ni: Usimulizi shahidi (huitwa pia usimulizi wa nafsi ya kwanza) na Usimulizi maizi (huitwa pia usimulizi wa nafsi ya tatu).
Usimulizi Shahidi
Huwa na sifa zifuatazo; o Hutumia nafsi ya kwanza.o Huwa na umakinifu zaidi katika usimuliaji.o Hudondoa yale yashuhudiwayo na mwandishi/msimuliaji tu.o Hufaa zaidi katika kazi za kitawasifu na kazi za fasihi pendwa.o Humrahisishia msomaji dhana ya masafa ya kiwakati na kijiografia katika kazi husika.o Ni rahisi zaidi kupenyeza matumizi ya nafsi ya pili.o Dhana ya wakati huenda taratibu.o Hujenga uhusiano wa karibu kati ya msomaji na kazi husika (msomaji huweza kujiona yu ahusika zaidi; hivyo, kuweza kwenda hatua kwa hatua samba na mapigo/mihemko ya kazi, hususan kama maudhui yenyewe ni chanya).o Mwandishi hana uwezo wa kuona mambo yote kwa wakati mmoja. Hivyo, husimulia jambo hili kisha lile.o Huibua kwa karibu kuwapo kwa dhana ya msimulizi ― mwandishi na/au mhusika msimulizi. Rejea usimulizi wa Willy Gamba katika NJAMA.o Aina hii ya usimulizi huwa na athari kubwa sana kwa wasomaji (kutokana na ufupi wa masafa ya kijiografia na kiwakati).
Usimulizi Maizi
dhana ya umaizi humaanisha uwezo wa mtu kufahamu mambo mbalimbali, ya wazi na ya siri; tena kwa wakati mmoja. Katika uga wa kifasihi, dhana ya umaizi hutumiwa kumrejelea mtunzi/mhusika mwenye uwezo wa kuona, kufuatilia ma kufafanua mambo mbalimbali kwa wakati mmoja. Hata hivyo, ni vema dhana hii ya umaizi ikatazamwa kwa jicho hili tu la kifasihi. Hii kutokana na ukweli kuwa kwa hakika, dhana yenyewe inafungamana sana na uwezo wa KI―UUNGU (uwezo alionao MUNGU). Kuna ukinzani mkubwa wa kimantiki kuhusu usahihi na uwezekano wa utokeaji wake. Hivyo, umaizi unakubalika tu katika muktadha wa kifasihi kutokana na ukweli kuwa mtunzi hujua yote ayatungayo, hujua kila kitu kuhusu wahusika, mandhari n.k. kikubwa akifanyacho ni kuamua tu ni wakati gani (katika tukio/sura gani) na kwa namna gani ayatongoe matukio yake. Kwa hali hiyo, mtunzi huweza kuonekana kuwa ni mmaizi.
Sifa chomozi za Usimulizi Maizi
o Hutumia nafsi ya tatu.o Huwa na uhuru zaidi katika usimuliaji (huweza kuteua la kusimuliwa na lakuachwa).o Humruhusu mtunzi kurukaruka katika usimulizi wake (huweza kusimulia hili mara lile).o Huruhusu usimulizi wa hata mambo yasiyoshuhudiwa na mwandishi/msimuliaji.o Hufaa zaidi katika kazi za kiwasifu.o Dhana ya masafa ya kiwakati katika kazi husika huweza kukimbizwa au kurushwa―rushwa, kwa mfano usimulizi katika Kusadikika (rejelea suala la safari na umri wa wajumbe).o Ni vigumu kupenyeza matumizi ya nafsi ya pili ikilinganishwa na usimulizi shahidi.o Uhusiano kati ya msomaji na kazi husika huwa wa kando 9msomaji hujiweka kando), hivyo hufuatilia mtiririko mtiririko wa vitushi kwa utulivu na mtuo.o Msimulizi huweza hata kuchupa hadi ndani ya fikra za watu na kutoa kifikiriwacho.
Vijitawi vya Usimulizi Maizi
Usimulizi maize huweza kufanywa kwa namna tatu ambazo ni: Usimulizi Penyezi, Usimulizi Tinde na Usimulizi Horomo.
(a) Usimulizi Penyezi: Ni Usimulizi ambao msimuliaji hujitokeza na hata wakati mwingine kuwashirikisha wasomaji. Huweza kusimulia kisha akajiingiza mwenyewe. Kwa mfano, "hata mimi niliona aibu, sijui wewe".
(b) Usimulizi Tinde. Huu ni usimulizi ambao hutumia kaida za ki―hisia/ki―dhana. Huweza pia kuitwa kwa jina la usimulizi nusu―nusu au usimulizi shinda. Hii ni kutokana na hiyo hali ya msimulizi kutokuwa na hakika ya akisimuliacho. Aghalabu, hutumika katika vitushi vinavyotakiwa kutafuta jawabu/ufumbuzi wa utata fulani. Kwa mfano, vitushi vya riwaya pendwa 9hususan riwaya za kipelelezi).
(c) Usimulizi Horomo. Usimulizi wa kurukia―rukia matukio na miktadha tofauti. Usimulizi huu ndiyo unaoruhusu uchanganyaji wa matukio yanayosimuliwa. Ni kama vile mtunzi/msimulizi huwa juu akimulika matukio yatokeayo kote duniani na ndani ya akili za watu kisha kuyasimulia. Ni vigumu sana kwa mtunzi kutumia aina noja tu katuka kazi yake. Mtunzi huweza kuchanganya aina zote za usimulizi katika kazi yake. Hii itategeneana na msuko wa kazi yenyewe pamoja na malengo ya mtunzi.
Mwendo wa Riwaya
Maana
Dhana hii hurejelea suala zima la kasi, mtiririko na mshindilio wa usimulizi wa vitushi vya riwaya kwa kuzingatia vigezo vya Msuko, Maudhui, Masafa ya Kiwakati na Masafa ya Kijiografia. Suala hili la mwendo huuathiri usomaji na msomaji mwenyewe katika ujenzi wa uelewa. Riwaya huwa na viwango tofauti vya mwendo kutokana na kuwepo kwa tofauti katika usanaji wa vigezo vilivyotajwa hapo juu. Kuna zenye mwendo wa kasi, nyingine zina mwendo wa kati/wastani na nyingine zina mwendo wa polepole.
Riwaya zenye mwendo wa kasi ni zile ambazo mtunzi huzisana kwa namna ya kurusha matukio. Aghalabu, riwaya zenye maudhui ya kusisimua au kufurahisha huwa na mwendo wa kasi. Kwa upande mwingine, riwaya zenye maudhui ya kitanzi (ya kuhuzunisha) huwa na mwendo wa polepole. Riwaya zenye maudhui yenye mseto wa kusisimua au kufurahisha pamoja na kuhuzunisha huwa na mwendo wa wastani.
Kwa mfano, riwaya yaweza kusimulia habari za mtu aliyeko Tunduru; kisha mtu huyo hupanga safari ya kwenda Tanga. Katika riwaya yenye mwendo kasi, twaweza kumuona mtu huyo Tunduru kisha ghafla twaambiwa yuko Tanga. Bali kama mwendo wa riwaya ni wa wastani au polepole, tutaweza kuchanganua jinsi atakavyosafiri safari yake yote pamoja na misukosuko mingine ya safari atakayokumbana nayo.
Mifano ya riwaya zenye mwendo wa polepole ni: riwaya nyingi za Shaaban Robert na Kezilahabi kama vileKusadikika, Adili na Nduguze, Mzingire, Nagona, Uhuru wa Watumwa. Mifano ya riwaya zenye mwendo wa wastani ni: Utata wa 9/12. Mifano ya riwaya zenye mwendo wa kasi ni: riwaya pendwa nyingi, mfano, Njama.
Hitimisho kuhusu mwendo wa riwaya
Kwa jumla, riwaya za Kiswahili zimekuwa zikibadilisha miendo yake kulingana na maudhui ya nyakati mbalimbali. Mwendo wa riwaya nyingi za wakati wa vuguvugu la kudai uhuru ni wa polepole. Hii ni kwasababu ya maudhui yaliyotamalaki kwa wakati huo yalijaa huzuni na jitimai kwa kiasi kikubwa. Baada ya uhuru, mwendo wa riwaya ulibadilika kidogo, ulikuwa wa wastani kwa kuakisi maudhui na msuko. Mwendo wa kasi katika riwaya ulishamiri katika miaka ya 80 ambapo kulikuwa na riwaya zilizoiga kazi pendwa za magharibi. Hizi zililenga kusisimua na kuburudisha zaidi.
Mtagusano
Ni mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi ya fasihi. Kwa namna fulani, huweza kuhusishwa na kaida za mwigo au uathiriano. Twaweza kusoma kazi fulani ya fasihi na kuona kuwa ina mwingiliano mkubwa na kazi nyingine. Mtagusano au mwingiliano huo waweza kuchagizwa na hali ya kuiga au kuathiriwa. Mtagusano huweza kujidhihirisha kupitia maudhui (mwingiliano wa kaida za maisha ya watu au jamii tofauti), lugha, mandhari n.k. dhana hii inajitokeza sana katika riwaya za Kiswahili kutokana na sababu zifuatazo: mosi, ni waswahili kuwa na mwingiliano mkubwa na watu wa jamii nyingine, hali ambayo husababisha pia wanariwaya kusawiri maisha hayo ya kimwangiliano katika kazi zao. Pili, ni utandawazi. Kupitia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, dunia imedogoshwa na hivyo, kukuza mwingiliano wa wanaulimwengu.
Msuko wa vitushi katika riwaya za Kiswahili
Riwaya za Kiswahili zimekuwa zikitumia motifu za namna mbalimbali katika kuvisuka vitushi vyake. Motifu ni msuko au mwegamo mkuu autumiao mtunzi kujenga fani na maudhui alengayo kuyawasilisha. Yaani; kupitia motifu husika, sehemu kubwa ya mambo mengine kama vile maudhui na fani. Aghalabu, motifu katika kazi za fasihi huwa na mrudio wa kiwango kikubwa katika ujitokezaji wake; kiasi cha hata kuweza kuathiri fikra za msomaji au mhakiki kwasababu huweza kumeza kiini cha dhamira halisi.
Baadhi ya motifu maarufu zitumiwazo na waandishi wa riwaya ya Kiswahili ni:
o Mapenzio Safario U ― jinio Mauajio Upelelezio Uhusika wa wanyamao Usihiri (umazingaombwe)o Ufutuhi (sherehe, raha na vichekesho)o Utanzia (mateso, vifungo, mabaa/majanga kama vile njaa na ukame).o Starehe (pombe, sigara, disko na kamari).
Riwaya za mwanzo zilitumia motifu ya safari katika kuvisuka vitushi vyake. Aghalabu, safari hizo zilihusisha bahari. Hivyo, motifu hizo ziliakisi pia misukosuko ya kibaharia. Mifano: riwaya za mwanzo za Shaaban Robert kama vile Adili na Nduhuze, Kusadikika. Pia Uhuru wa Watumwa. Riwaya nyingine zilitumia motifu ya u― jini au ki―jini. Hizi pia ziliakisi mazingira ya upwa wa bahari. Kama ilivyo kwa motifu ya safari, hii nayo ni miongoni mwa nduni za fasihi simulizi. Nduni nyingine maarufu ya fasihi simulizi ambayo inajitokeza katika vitushi vya riwaya za Kiswahili ni uhusika wa wanyama. Hali hiyo ya matumizi ya wahusika wanyama katika vitushi vya riwaya ni miongozi mwa ithibati ya kuwako kwa ufungamano wa karibu kati ya riwaya na fasihi simulizi; kwani hiyo ni kaida maarufu katika hekaya, visakale, visasili na ngano. Wanyama maarufu wajitokezao katika riwaya za Kiswahili hususani zile za mwanzo ni kama vile nyani (Adili na Nduguze), Paa (Nagona).
Mabadiliko makubwa ya msuko wa vitushi katika riwaya za Kiswahili yanadhihirika katika usahili na uchangamani wake. Dhana hii ya usahili na uchangamani wa vitushi yarejelea mpangilio wa vitushi vyenyewe katika kazi. Katika riwaya za mwanzo, kulikuwa na usahili. Kwa sasa, wasanii huviweka vitushi katika hali ya uchangamani. Riwaya pendwa, kwa upande wake, zilimezwa na motifu za mauaji, starehe, upelelezi na mapenzi.
Mianzo na miisho ya riwaya za Kiswahili
Mianzo
Namna mbalimbali za mianzo ya riwaya za Kiswahili:
o Ya kisirao Ya kifomyula au kijadi au kihafidhinao Ya kifalsafao Ya kifumboo Ya ki ― swalio Ya kiufafanuzio Ya kimajazi
Miisho
Kwa upande wa miisho, riwaya nyingi za Kiswahili huwa na miisho ya:
o Kifomyula au kijadio Ya kifalsafao Ya kiutatuzi
Maelezo ya jumla kuhusu mianzo na miisho ya riwaya za KiswahiliKuna tofauti kubwa ya riwaya za mwanzo na za sasa. Zile za mwanzo ziliakisi kwa kiasi kikubwa mianzo ya nathari simulizi. Mianzo na miisho hiyo twaweza kusema ilichukua matumizi ya vifungu vya kifomyula. Dhana ya vifungu vya kifomyula hapa yamaanisha utunzi wa neno, tungo au aya kwa namna ya kuirudia katika kazi moja au miongoni mwa waandishi tofauti. Mathalani, kulikuwa na matumizi ya vifungu kama vile:
o Hapo zamani za kale, palikuwa na....(mianzo)o Paukwa pakawa (mianzo)o Hadithi hadithi (mianzoo Na hadithi yangu yaishia hapo (miishoo Waliishi raha mustarehe (miisho)o Hatimaye alifanikiwa sana (miisho)Baadaye, mianzo na miisho ya hadithi ilibadilika. Mathalani, kukawa na mianzo ya ki ― taharuki, hususani katika riwaya ramsa. Hizi ni zile zinazotawaliwa na msisimko au burudani. Pia, riwaya za kifalsafa.Kuhusu miisho, ingawa wanariwaya waliowafuatia wale wa awali wamejikwepesha na miisho ya kifomyula; bado miisho yao inalandana kimaudhui. Hii ni kwa sababu, kwa jicho la jumla, riwaya nyingi bado zinaisha kwa namna ya kuonesha msfanikio. Mafanikio haya ni yale yatokanayo na mivutano baina ya ama ubaya na wema, ukale na usasa na kadhalika. Mathalani, katika Haini, twaona tutakosa, alifikiria, na kweli leo ametoka! Na hata hao waliobaki, pia watatoka tu! Alisema Hamza. (uk.267). Mwisho huu unamrejelea yuleyule mhusika mkee aliyedokezwa pia katika mwanzo wa kazi hiyo, Hamza.
MUELEKEO WA JUMLA JUU YA MAUDHUI YANAYOJICHOMOZA KATIKA RIWAYA YA KISWAHILI
Dondoo muhimu kuhusu mielekeo ya maudhui
Maudhui ya riwaya ya Kiswahili yalibeba mitazamo na mielekeo ya sera na mipango ya vipindi mbalimbali vilivyobeba mshindo wa fikra za Waswahili. Vipindi hivyo ni:o Kabla na wakati wa ukoloni (wakati wa vuguvugu la kudai uhuru)o Baada ya uhuru/wakati wa Azimio la Arushao Wakati wa vuguvugu la vijiji na vijiji vya ujamaao Wakati wa vita ya Kagerao Wakati wa didimio la uchumi wa duniao Wakati wa sera za mpango wa kuhuisha mfumo wa uchumi barani Afrika na Duniani.o Wakati wa vuguvugu la kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingio Wakati wa vuguvugu la utandawazi (ubinafsishaji)
Maudhui ya riwaya za Kiswahili kabla na wakati wa Ukoloni
Riwaya za Kiswahili kama mojawapo ya kazi za fasihi ya Afrika, zilikuwa na maudhui yaliyojaa manunguniko, jitimai na huzuni kutokana na hali halisi iliyokuwa inawakabili waafrika wengi. Katika wakati huu ndipo hasa yalipokuwa yanajidhihirisha maudhui yaliyolenga kuamsha urazini wa Waafrika kuhusu maovu waliyokwa wanatendewa. Aidha, maudhui yalikuwa yanawakumbusha kuhusu suala la ukombozi. Baadhi ya mifano ya riwaya zilizotungwa kabla ya uhuru ni: Uhuru wa Watumwa, Kusadikika, Kufikirika, Kasri ya Mwinyi Fuad n.k.
Maudhui ya riwaya za Kiswahili Baada ya Uhuru
Hapa, riwaya zilizotungwa zilibadili mkondo wa kimaudhui. Ziliwahimiza watu kuzijenga upya nchi zao na maisha yao kwa jumla. Aidha, kimaudhui zilichanganyika na zile zilizotungwa baada ya muongo mmoja kupita toka uhuru wan chi za Waswahili. Hizi ziliakisi hali halisi ya maendeleo yaliyofikiwa na jamii husika baada ya kupata uhuru. Zilimulika pengo la mafanikio baina ya malengo ya kupigania uhuru na kiwango cha kufanikiwa (matunda yaliyojitokeza). Kutokana na kuwako kwa kiwango kidogo cha maendeleo, maudhui haya yalijaa kejeli, malalamiko na manungu‘uniko. Malalamiko haya yalitoakana na mambo mengi kama vile tofauti ya kimaendeleo kati ya vijiji na mijini na umasikini wa kupitiliza. Mifano ya riwaya hizo ni: Shida, Njozi iliyopotea, Kichwamaji na Dunia Uwanja wa Fujo.
Baada ya hapo, kilifuata kipindi cha anguko kuu la uchumi wa Dunia. Anguko hilo lilifuatiwa na kipindi cha ufufuo wa uchumi wa dunia (sera za mpango wa kuhuisha mfumo wa uchumi wa dunia, hususani barani Afrika). Riwaya ya Kiswahili pia iliakisi hali hii.
Maudhui ya jumla yanayojichomoza
Maudhui yanayojichomoza sana katika riwaya ya Kiswahili ni pamoja na:o Historia au uhistoriao Mapambano dhidi ya ukoloni (vita vya uhuru/kujikomboa)o Ujumi wa kiafrikao Utabakao Sera za nchi na za kimataifao Utu na maadili (riwaya za sira)o Falsafa na itikadi ya kiafrikao Nafasi ya asasi za dinio Usihirio Epistemolojia ya Waswahili
Ujumi katika riwaya ya Kiswahili
Dhana ya ujumi
Ujumi ni tafsiri ya neno la kiingereza "Aesthetics" lililotokana na neno la Kigiriki "Aisthetikos". Dhana hii iliasisiwa na Alexander Baumgarten mwaka 1735. Ujumi ni taaluma inayoshughulikia falsafa ya uzuri, ubaya na ladha. Taaluma hii hujibu maswali kama vile:
o Uzuri/ubaya ni nini?o uzuri/ubaya hutokana na nini?o Nini hutuongoza kuamua uzuri/ubaya wa kitu?Maswali haya yakijibiwa, itakuwa rahisi kwetu kutoa maamuzi kuhusu ujumu unaojitokeza katika riwaya za Kiswahili na Fasihi ya Kiswahili kwa ujumla. Dhana ya uzuri au ubaya huweza kufafanuliwa vema kwa kuhusisha mambo makuu matau ambayo ni:
o Ufahamu/akili/hisio Idili za jamii husikao Malengo au matumizi
Idili ni jumla ya nguzo―msingi au vigezo ambavyo jamii hujiegemeza kwavyo kama vipimo vya kuhakikia au kulinganishia uzuri au ubaya wa jambo. Kila jamii na kila kipindi kina idili zake ambazo hutumika kupimia thamani ya vitu mbalimbali. Kigezo kingine (ambacho ni sehemu ya idili) kinachotuongoza kufanya maamuzi ya uzuri/ubaya wa kitu ni malengo au matumizi ya kitu husika. Kitu chochote huweza kuwa kizuri/kibaya kwa watu wa jamii tofauti kutokana na kuwa na malengo au matumizi tofauti.
Kwa mfano: Kalamu yaweza kuwa nzuri kwa mwanafunzi na ikawa mbaya kwa mkulima, mwanamke mnene aweza kuwa mzuri kwa Mwafrika na mbaya kwa mjapani. Katika muktadha wa kozi hii, maarifa haya ya ujumi ni kiunzi muhimu kwetu katika kufanya aamuzi ya kiulinganisho kuhusu falsafa za jamii mbalimbali.Hivyo, uzuri ni matokeo ya kuafikiana au kuwiana kwa uhalisi wa kitu (kadri kinavyoonekana) na idili za jamii husika. Ubaya (ambao ni kinyume cha uzuri), ni kutokuwapo kwa uwiano baina ya uhalisi wa kitu hicho na idili za jamii.Udhihirikaji wa ujumi katika riwaya za KiswahiliKatika kazi mbalimbali za fasihi, ujumi huweza kudhihirika kwa kuchunguza vipengele vifuatavyo:o Usawiri wa wahusikao Mtindo wa sanaa yenyewe kwa jumlao Uumbaji wa maumbile ya vitu (mandhari)o Ukweli na uthabiti wa maudhuio Katika riwaya za Kiswahili, ujumi wa kiafrika hujitokeza kupitia vipengele mbalimbali. Baadhi ya vipengele hivyo ni:o Dhana yenyewe ya U―Afrikao Utamadunio Vyakula na mfumo ― mloo Mgogoro wa mwingiliano wa ujumi wa Kiafrika na ujumi wan chi za kigeni.
Historia au uhistoria
Kwa jicho hili, riwaya huweza kutazamwa kama:o kama kazi ya historia ya waswahilio kama nyenzo ya kufundishia historiao kama sehemu ya historia yenyewe
Riwaya huweza kubeba vionjo vingi vya kihistoria. Kwa namna fulani, riwaya huweza hata kutumika kufundishia historia kwa jamii fulani. Hata hivyo, kwa yeyote aamuaye kuzitumia kwa lengo la kufundishia historia lazima awe na uelewa wa kutosha kuhusu dhana ya riwaya na historia.
Riwaya, kwa kawaida, zina vipengele vya ubunifu, hivyo uhistoria uweza kuwapo kwa malengo ya kiyakinifu (kuakisi uhalisia wa mambo) au kwa lengo la kisanaa. Hivyo, kupitia riwaya hizo, jamii hupata nafasi nzuri ya kujitambulisha na kujifunza mambo mengi yaliyotokea katika nyakati zilizopita. Baadhi ya mifano ambazo zaweza kutupatia maarifa ya kihistoria ni: Miradi Bubu ya Wazalendo, Gamba la Nyoka, Ndoto ya Ndaria, Uhuru wa Watumwa na Moto wa Mianzi.
Utabaka katika Riwaya za Kiswahili
Maudhui haya yalitokana na kuwako kwa wakoloni katika jamii za waswahili kwa muda mrefu. Hata baada ya uhuru bado jamii ilitawaliwa na matabaka. Riwaya ya Kiswahili haikuwa nyuma katika kuisawiri hali hiyo. Katika riwaya mbalimbali waandishi waliwajenga wahusika katika namna ya kujipambanua na kuyapambanua matabaka mbalimbali yaliyokuwapo katika jamii. Aidha, waandishi wenyewe walipaswa kuwa makini kwani walimulikwa na jamii. Hii ni kutokana na ukweli kuwa jamii ilikuwa inajiuliza:
o mwandishi au wahusika wa kazi husika ni nani?o Wako katika tabaka gani?o Wanamsemea nani?
Suala la mipango na sera za nchi na za kimataifa katika riwaya za KiswahiliSuala hili pia limezungumziwa sana na riwaya za Kiswahili. Suala la sera na mipango kadha huwenda sambamba na vipindi mbalimbali vinavyoshuhudia kuanzishwa kwa sera hizo. Kila kipindi kilikuwa na mipango na sera zake.
Epistemolojia ya waswahili katika riwaya za Kiswahili
Epistemolojia ni tawi la falsafa linalishughulikia maarifa. Kila jamii ina duara lake la maarifa na ujuzi. Riwaya za Kiswahili zinamchango mkubwa wakuwasilisha maarifa mbalimbali kwa wasomaji. Dhana ya maarifa hapa yafaa itazamwe kitofauti na dhamira za kawaida. Hii ni kwasababu, maarifa hayo si lazima yawe wazi kwa wakati mwingine huwa fiche. Jambo hili la kuwasili epistemolojia huweza kufanywa na mtunzi kwakukusudia au bila hata kukusudia. Vilevile, miongoni mwa wasomaji wa riwaya, lazima pawe na utofauti katika kuibua epistemolojia inayopatikana katika riwaya husika. Hii inatokana na ukweli kuwa suala la kubaini mafunzo, maarifa na ujuzi linauhusiana pia na utambuzi na tajiriba ya msomaji.
Falsafa na itikadi ya kiafrika katika riwaya za Kiswahili
Maana ya falsafa na itikadi
Falsafa: kweli ambayo mtu anaiamini, anaisimamia na anaiishi au anaishi nayo.
Itikadi: ni njia mkondo au nyenzo ambayo mtu anaishikilia na kuitumia ili kuifikia kweli anayoiamini (falsafa). Dhana hizi mbili zinakanganya na zinachanganya wanazuoni wengi.
Falsafa na itikadi za kiafrika katika riwaya za Kiswahili
Kuna riwaya kadhaa zenye maudhui ya kifalsafa katika riwaya za Kiswahili. Baadhi ya wanazuoni wa kifalsafa wanadai kuwa hakuna mtu anayeishi bila falsafa. Hivyo, hata waandishi wa riwaya ni ngumu kusema huyu hana falsafa: kwamba, takribani kila riwaya kuna falsafa inayoshadidiwa na kupigiwa mbiu. Baadhi ya falsafa zinazojitokeza sana katika riwaya za Kiswahili ni:
o Uduara wa maishao Ujuala (kuwapo kwa Mungu na kani za Kiuungu)o Usihiri na ushirikinao Thamani ya mtu na utu:o Udugu na mbari/ukoo (thamani ya uzazi n.k.)Baadhi ya itikadi zinazojitokeza sana katika riwaya za Kiswahili ili kushadidia falsafa hizo ni:o Dhima ya dini na asasi zakeo Ujadio Sera mbalimbali kama vile ujamaa na kujitegemeao Dhana ya kijadi kama vile uganga, matambiko n.k.
Suala la nafasi na asasi za dini katika riwaya za Kiswahili
Maudhui yake yanamulika masuala yafuatayo: maana na asili ya dini: dini zinanafasi gani katika jamii? Umuhimu wa watu kumcha Mungu, unafiki wa wacha Mungu, udhaifu wa asasi za dini au viongozi wa asasi za dini n.k. mifano ya kazi au riwaya: Siku ya Watenzi Wote, Pete n.k.
Suala la Usihiri katika riwaya za Kiswahili
Ni miongoni mwa nduni maarufu zinazojitokeza katika baadhi ya riwaya za Kiswahili. Suala hili uhusisha dhana za ushirikina, uchawi, wanga na uganga.
Uchawi: ni ufundi au utaalamu wa kutumia dawa na mbinu nyingine za uganga kwaajili ya kuleta madhara kwa watu na viumbe. Pia uhusisha maudhui yanayoakisi uhalisia ajabu au uhalisia mazingaombwe. Kuna migongano kuhusu kuwa au kutokuwapo kwa dhana ya uchawi hapa duniani. Wapo wanaoafiki kuwapo kwake na wengine wanapinga na kudai kuwa hizo ni imani tu. Hata hivyo, kuwapo kwa jambo hili kunadhihirishwa na hata vitabu vitakatifu vya dini. Mifano ya riwaya zenye imelea vya usihiri ni: Babu alipofufuka, Utata wa 9/12, Dunia Yao, Miradhi ya Hatari, Walenisi, Bina —adamu n.k.
Riwaya ya Kiswahili na kumbo la maendeleo ya kiteknolojia
Sayansi na teknolojia kwapamoja zimesaidia kukuza utanzu huu wa riwaya. Sayansi na teknolojia zimeshadidia katika ukuaji wa mambo kadhaa katika maendeleo ya riwaya, baadhi ya mambo hayo ni pamoja na:
o Utunzio Uchapishajio Usambazajio Usomajio Urejeleaji n.k.
UHAKIKI WA RIWAYA TEULE ZA KISWAHILI
Dondoo muhimu katika uhakiki wa riwaya teule
o Vitabu vinavyopaswa kusomwao Vitabu vinavyopaswa kuzamiwao Mambo ya kuzingatia katika uhakiki
Mambo haya matatu yanaendana sanjari na:
o Kuijua nadharia ya uhakikio Nadharia za kuhakikiao Kufanya uhakiki (wajumla na ule mahususi, uzingatiao vipengele mahususi).o Ushahidi katika suala la uhakikio Kufanya uhakiki linganishi
Nadharia za kuhakikia fasihi
Ni jicho la kurunzi ya kufikia lengo fulani. Uhakiki mzuri ni ule utumiao nadharia. Zipo nyingi sana bali huweza kugawanywa kutokana na lengo la uhakiki. Hakuna nadharia bora wala dhaifu. Kati ya nadharia hizo nyingi hukamilishana, hutegemeana na kuathiriana. Makundi makuu au maaru ni:o Zilengazo masuala bia (Ya kiulimwengu)o Zilengazo masuala ya kijamii (za kisosholojia)o Zilengazo kazi husika (Umbo au muundo au maana)o Zilengazo msomaji wa kazi za fasihi.
Baadhi ya nadharia hizo ni:
o Uhemenitikio Usemezanoo Uhalisiao Uhalisia ajabuo Ualisiao Umatini au semiotikio Urasimio Urasimi mpyao Ulimbwendeo Undhanaishio Uana au Ufeministio Umaumboo Umuundoo Udenguzi au uumbajio Upokezio Udodosinafsi au saikolojia changanuzio Mwingiliano matinio Usimulizi au Naratolojiao Mwitikio wa Msomajio U — Bakhtini au Ukanivalio Ungitamaduni au Ubaada Ukolonio U — Foucaulto Umaksio Uyakinifu wa kitamadunio Uakisio Unegritudio Usasao Usasa leoo Uhistoriao Uhistoria mpyao Uhakiki mpya.
Vitabu vya riwaya vinavyopaswa kusomwaAngalau riwaya za kila kundi au kijikundi zisomwe na kupata picha ya jumla ya maudhui na fani yake (usomaji huu wa jumla pia uzingatie riwaya zilizotungwa na waandishi kutoka kanda kubwa za waswahili ambazo ni Tanzania bara, Tanzania visiwani na Kenya).Mwongozo kwa watakaowasilisha uhakikiMadondoo muhimu yapaswayo kuwemo katika uwasilishaji ni:o Ikisiri (taarifa za mtunzi na utunzi, aina ya riwaya)o Dhamira chomozio Mbinu chomozi za kibunilizio Hitimisho (kituo au mkolezo, riwaya zinazofanana nazo)
HALI NA HADHI YA RIWAYA YA KISWAHILI
Hali ya riwaya ya KiswahiliHizi ni zama za sayansi na teknolojia. Mwonekano wa jumla kuhusu hali ya riwaya nikwamba, kunaongezeko kubwa la riwaya kwa kigezo cha idadi. Mwamko wa riwaya katika zama hizi unaweza kushuhudiwa katika kona muhimu zifuatazo: uandaaji, usambazaji na usomaji.o Uandaaji, kwa sasa kuna mfumuko mkubwa wa utunzi na uchapishaji wa riwaya. Bali, tatizo ni kuhusu ubora wa viwanda vya uchapishaji vingi havina misingi bora ya wataalamu wa uhariri n.k. msukumo mkubwa pengine huwekwa katika soko zaidi (tija ya mtunzi na wachapishaji) kuliko tija ya msomaji. Hii, kwa upande mwingine, husababisha kupatikana kwa riwaya nyingi ambazo zinapwaya kimbinu na kimaudhui.o Usambazaji, kwa sasa, kuna nyenzo nyingi ambazo zinaharakisha kufikisha riwaya kwa hadhira, nyenzo hizo ni kama vile: mitandao pepe ambayo imesahilishwa sana siku hizi katika ufikiwaji wake, kwayo, mtu wa sehemu ya kwanza huweza kupata riwaya kutoka sehemu yeyote duniani na kuisoma. Kwa riwaya za maunzi ngumu, nyingi huuzwa na si kusambazwa kama ilivyokuwa miaka iliyopita.o Usomaji wa riwaya, pamoja na kupanuka kwa nyenzo za kupakulia, kuhifadhi na kusomea hapa bado kunatatizo kubwa. Ukubwa wa tatizo la usomaji linaanzia katika kuwapo kwa tofauti za usomaji wa kawaida na usomaji wa kifasihi. Namna hizi mbili za usomaji zinatofautiana sana. Usomaji wa kifasihi unahitaji misingi na usuli wa kifasihi. Usomaji wa kifasihi huathiriwa na mambo mengi kama vile:ü Misingi ya kidiniü Matatizo ya kiuchumiü Misingi ya kitamaduni (miiko)ü Mudaü Usuli wa kifasihi na uwezo binafsi wa uelewaü Malengo binafsi ya msomajiü Sera za nchi n.k.Kwa jumla, mambo yanayokwaza usomaji wa kifasihi kwa waswahili ni umaskini, sera duni za usomaji wa ziada, miiko ya kimila na kukosekana kwa nafasi.Hadhi ya riwaya ya KiswahiliUlimwengu umedogoshwa sana na Tehama. Kutokana na udogoishwaji huo, kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa kiutunzi katika riwaya kimbinu na kifani. Hali hii, ijulikanayo kama mtagusano wa kifasihi imesababisha kuwapo kwa riwaya zinazoendana sana kifani na kimaudhui kutoka katika sehemu mbalimbali za dunia. Mifano ya kazi hizo ni:o Take your money (chase) vs Pesa zako zinanuka (Mtobwa)o I will burry my Dead (Hardey Chase) vs Zika Mwenyewe (E. Ganzel)o Mzingile (Kezilahabi) vs Bin ― adamu (Wamitilia)o Dunia yao (SAM) na The Tin Drum (Gunter Grass)Baada ya fikra zote za hapo juu, vema sasa kujiuliza kuhusu hadhi ya riwaya ya Kiswahili. Maswali ni:o Je, fasihi ya Kiswahili kwa ujumla wake ina hadhi gani mbele ya sanaa nyinginezo za waswahili?o Je, riwaya ya Kiswahili ina hadhi gani mbele ya tanzu nyinginezo za fasihi ya kiswahili?o Je, riwaya ya Kiswahili ina hadhi gani mbele ya riwaya ya jamii nyinginezo?o Kwa hakika, majibu ya maswali haya si ya moja kwa moja: bali ni ya kimuktadha kwa sababu hushirikisha masuala au vigezo kadhaa vya kibinafsi kama vile:ü Upendeleo, jinsi mtu anavyopenda utanzu Fulaniü Mshindilio wa misingi ya utanzu husikaü Mitazamo binafi kuhusu utanzu husikaü Tujiulize msanii wa riwaya anahadhi gani mbele ya msanii wa sanaa nyinginezo kama vile muziki, uchoraji n.k. kuna baadhi ya sanaa zinachukuliwa kuwa ni za hadhi ya juu.ü Pia, tujiulize msanii wa riwaya anahadhi gani mbele ya msanii wa tamthiliya na ushairi? Msanii wa ushairi pengine huchukuliwa kwa u ― mbele zaidi ya Yule wa riwaya.ü Zaidi, suala la hadhi ya riwaya ya Kiswahili mbele ya riwaya ya jamii nyinginezo, ijapokuwa ni gumu kutathminiwa; ila mtu anaweza hata kuangalia kigezo cha kiasi cha riwaya za Kiswahili kutafsiriwa kwenda katika lugha nyinginezo au kiasi cha riwaya za lugha nyinginezo kutafsiriwa kwenda katika Kiswahili.
MASWALI YA MJADALA (VIKUNDI)
1. Vipengele vya kibunilizi vinajitokezaje katika riwaya ya kufikirika na Miradhi Hatari?
2. Shaffi adamu shafi katika vuta n‘ kuvute amefanikiwa kujenga vitumba vya kutosha. Jadili.
3. Huku ukirejelea mawazo na tafiti za wataalamu mbalimbali jadili asili ya riwaya.
4. Bainisha kwa mifano mchango wa MSA katika riwaya ya Kiswahili.
5. Jadili mchango wa Ben Mtobwa na Elvis Aristablus Musiba katika maendeleo ya riwaya pedwa za Kiswahili.
6. Riwaya za kimaadili ujengwa katika miega mitatu (3) jadili miega hiyo kama ilivyojitokeza katika riwaya ya Haini.
7. Bila Naratolojia hakuna riwaya. Jadili.
8. Kipengele cha utomeleaji katika riwaya kina faida na hasara. Tumia Barua ndefu kama hii kueleza ukweli wa kauli hii.
9. Jadili nafasi ya wahusika katika riwaya ya Kiswahili huku ukilinganisha na tanzu zingine za fasihi.
10. Mgogoro wa mswahili ni nani unaathiri vipi maendeleo ya riwaya ya Kiswahili?
11. Eleza mchango wa wataalamu wafuatao katika kuibuka na kuendelea kwa riwaya ya Kiswahili:
· Edward Steere· Carl Buttner· Carl Velten· Lyndon Harries· Jann Knappert· Edwin Brenn· J.w.T. Allen
12. Jadili faida na hasara ya vipengele vya kimajaribio katika riwaya ya Kiswahili.
13. Wanazuoni mbalimbali wametoa fasili ya riwaya. Eleza fasili hizo.· Kwa nini fasili zao zimetofautiana?· Je, wewe unadhani riwaya ni nini?
14. Eleza tofauti ya riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari.· Unadhani tofauti hizo kati ya riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari zinasababishwa na nini?
15. Wataalamu wa taaluma za fasihi usema bila muktadha hakuna maudhui wala fani. Unadhani kwanini wanasema hivyo. Tumieni riwaya kadhaa kushadadia hoja zenu.
16. Zote ni riwaya za Kiswahili, zote zinautamaduni wa waswahili, zote ni riwaya pendwa, zote zinahusu mapenzi, kwa nini riwaya moja iwe na mvuto kwa jamii na nyingine ikose mvuto. Tumia riwaya mbili kujadili hoja hii.
17. Plato na Aristotle waliweka msingi katika uundaji wa kazi za kisanaa na riwaya ikiwemo. Jadili ubora na udhaifu wa misingi yao.
18. Jadili kinagaubaga historia ya riwaya barani Asia.
19. Riwaya kwa Kiswahili zinahasara kubwa zaidi ukilinganisha na faida kwa jamii ya waswahili. Tumia mifano lukuki kueleza ukweli wa hoja hii.
20. Riwaya ya Bwana Muyombekere na Bibi Bugonoka ni miongoni mwa riwaya za Kiswahili za mwanzo kabisa. Jadili maudhui na ufundi unaojitokeza katika riwaya hii.
21. Maisha ni nini? Wanafalsafa katika riwaya ya Kiswahili wanatoa majibu gani juu ya swali hili. Uwanja ni wenu kutoa mifano kun‘tu.
22. Dhana ya Ujumi kwasasa inaonekana ndiyo nguzo ya muhimu katika kuhakiki kazi nyingi za kifasihi. Kufikirika na Kusadikika zinathibitishaje ukweli wa hoja hii?
23. Chunguzeni Epistemolojia katika riwaya teule tatu.
24. Chunguzeni falsafa za uduara maisha, ujaala na utu katika riwaya teule tatu.
25. Tumia nadharia ya unegritudi kuhakiki riwaya ya vuta n‘kuvute.
26. Tumia nadharia ya udodosi nafsi kuhakiki riwaya ya Nagona.
27. Riwaya ya Kiswahili na filamu za kiswahizi zinaumana kimaudhui. Tumia riwaya moja teule na filamu moja ya Kiswahili kueleza ukweli wa hoja hii.
28. Falsafa ya Shaaban Robert na ile ya Euphrase Kezilahabi zimeathiri waandishi wengine. Teua riwaya mbili kati ya riwaya teule (isiwe ya S. Robert na isiwe ya E. Kezilahabi) kushadadia kauli hiyo.
29. Shaaban Robert na MSA wanafanana na kutotautiana katika uwandishi wao wa riwaya. tumia riwaya moja kwa kila waandishi hawa kuelezea hoja hii.
30. Nadharia ya Semiotiki hutumiwa zaidi katika kuhakiki vipengele vilivyofumbwa. Tumia riwaya moja iliyofubwa vizuri kati ya riwaya teule kuhakiki kipendele cha ufundi kwa kutumia nadharia hii. MAWASILISHO YA WANAFUNZI KATIKA KUJIBU MASWALI YA MJADALA
KUNDI 1. ( KOLEJI YA ELIMU)
SWALI:
Jadili dhana ya ubunilizi kama inavyojitokeza katika riwaya ya Kufikirika na Mirathi ya Hatari.
Kazi yetu imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi, kiini cha kazi na hitimisho. Katika utangulizi kuna maana ya riwaya na maana ya ubunilizi, katika kiini cha kazi kuna vipengele vya ubunilizi kama vilivyojitokeza katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI na KUFIKIRIKA, na hitimisho ni mawazo kuhusu dhana na vipengele vya ubunilizi kama ilivyojikeza katika riwaya hizo.
Riwaya ni kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha, msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukua muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalumu (Wamitila, 2003).
Riwaya ni utungo wenye sifa ya ubunifu, usimulizi, mpangilio au msuko fulani wa matukio, ufungamano wa wakati, mawanda mapana na uchangamano (Mulokozi, 1996).
Kwa ujumla, riwaya ni masimulizi ya kinathari yenye ubunilizi na yenye kutumia lugha ya mjazo katika kuwasilisha mawazo yake.
Ubunilizi ni ubunifu aliyonao mtunzi kwa kubuni na kuingiza au kutumia kazi yake ili ilete mvuto na manato kwa hadhira. Mbinu hii huakisi kipawa cha utunzi alichonacho mtunzi na kumtofautisha na watu wengine.
Kwa kutumia vitabu viwili vya riwaya KUFIKIRIKA kilichoandikwa na SHAABANI ROBERT, na MIRATHI YA HATARI kilichoandikwa na C.G MUNG’ONG’O, vifuatavyo ni vipengele vya kibunilizi vilivyojitokeza katika riwaya hizi;
Dayalojia, ni kitendo cha mtunzi kutumia kauli za majibizano katika kuwasilisha mawazo yake au kazi yake katika jamii husika. Katika kipengele hiki mwandishi hutumia vinywa vya wahusika katika kuwasilisha maudhui aliyonayo katika jamii husika. Kwa mfano katika kitabu cha KUFIKIRIKA mwandishi ametumia dayalojia ndani ya masimulizi kama inavyojidhihirisha katika (uk… 27),
Mfalme anasema: “nimetumia fedha nyingi kwa mafunzo yako lakini mwalimu wako wa kwanza hakufanya kitu ila upotevu…” Mtoto wa mfalme anajibu “wajua baba kuwa mimi sichukii mtu ambae amekubaliwa na utukufu wako. Lakini mwalimu huyu ni bora?...”
Vilevile, katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI dayalojia imejitokeza katika (uk. 19), mazungumzo kati ya Gusto na Mzee Mavengi yanayohusu usihiri;
Mzee Mavengi: “unaziona shanga hizi? Gusto: ndio Mzee Mavengi: na manyoya haya? Gusto: ndio Mzee Mavengi: Basi hili baba yako alilitumia kama ndege ulaya akiwamo kazini”.
Ujadi, ni utumiaji wa kauli, matendo au mazingira ya asili yanayofungamana sana na jamii inayoandikiwa. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ametumia kipengele cha ujadi katika kazi yake kama vile methali, misemo na mazungumzo mbalimbali ya jamii husika; mfano katika (uk. 5), mwandishi ametumia methali isemayo “nyumba ya mgumba haina matanga”, vilevile mwandishi ametumia misemo mablimbali kwa mfano (uk. 37), “maisha ya mwongo ni mafupi”, pia mwandishi ametumia matendo mbalimbali ya kiganga katika kusawiri maisha halisi ya jamii husika kama ilivyoelezwa katika sura ya pili (uk. 8) na kuendelea ambapo mwandishi ameonesha makundi mabalimbali ya waganga pamoja na shughuli zao, makundi hayo ni:
“waganga wa mizizi, waganga wa makafara, Waganga wa mazinguo, waganga wa hirizi, waganga wa mashetani, waganga wa utabiri”
Waganga wote hao wanatumia dawa mbalimbali za asili kama mitishamba, dawa za wanyama, makombe, mashetani na ramri za kila aina.
Katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi ametumia methali, nahau, matambiko, na vyakula vya asili mfano, kiapo katika matambiko (uk. 16-17) anasema;
“nye misoha gya vakuhu Nye vasehe yemwalonguwe Nye vayangu yetulilumwi”
Pia mwanndishi ameonesha ujadi kwa kutumia vyakula vya asili kama vile maboga ya kuchemshwa na viazi vya kuchomwa, (uk. 3).
Utomeleaji, ni muingiliano wa tanzu, utanzu mmoja kuingilia au kuwekwa kwenye utanzu mwingine, mwandishi wa riwaya ya KUFIKIRIKA ametumia shairi katika (uk. 18) kama usemavyo;
“MFALME na MALKIA, Katika KUFIKIRIKA, Siku ya kuzaliwa, Mtoto tuliyetaka….”
Halikadhalika, katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi ametumia mbinu hii kwa kutumia barua, nyimbo, na simu ya maandishi mfano simu ya maandishi (uk. 9) anasema;
“GUSTO BABA MAHUTUTI NJOO HARAKA KITAMBI”
Pia picha inayoonekana juu ya kitabu pamoja na nyimbo (uk. 16,17, 32 na 33), mfano katika (uk. 33) Mavengi anaimba, “Gende ve dadna, gende Umvipwawo apigile uwivina Avedze lukule Gende, yane danda gende…”
Tanzia, ni mbinu ambayo mwandishi hutumia vipenegele mbalimbali ambavyo huibua huzuni, masononeko, masikitiko au mateso na majonzi kwa hadhira yake. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi anasema; “Mimi na malkia tumefadhaishwa mno na ugumba na utasa katika nyumba yetu wala hatujui tufanye jambo gani litawezaa kutufanya kuwa wazazi wa mtoto ambaye atarithi ufalme wa Kufikirika” (uk. 5). Pia katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi ametumia utanzia wa majonzi kwa Gusto kutokana na kufiwa na baba yake (uk. 13) ambapo anasema “tulimzika hayati baba…” mfano mwingine ni kutoka kwa mama Gusto ambapo anamwambia mwanae Gusto akisema “sipendi nimpoteze tena hata mmoja wenu kabla sijafa, alikaribia kulia nikamwonea huruma lakini wazo lilikua limekwisha kunivamia akilini..” (uk. 29).
Ufutuhi, ni mbinu ambayo msanii hutumia ucheshi au furaha kwa hadhira yake mfano kejeli, utani, dhihaka, raha, ubeuzi na mizaha. Mfano Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ametumia ufutuhi kama vile dhihaka (uk. 27) anasema; “naona sura yake imechujuka kwa fikra”, pia katika (uk. 17) anasema “Nimefurahi sana kwa kujaliwa kupata mtoto na nimependezwa mno…….”. vilevile katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia ufutuhi kupitia utani kati ya John, Gusto na Rajabu (uk. 8), anasema “akamjibu kwa shere hunielewi nini yakhe? Una baridi ya bisi nini kaka?”.
Taharuki, ni hali ya kuwa na shauku ya kutaka kujua juu ya nini kitafuatia katika usimulizi wa kazi ya fasihi. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ameonesha taharuki kwa kutumia jina la kitabu “KUFIKIRIKA” ambapo humfanya msomaji kutaka kujua zaidi nini kilichomo ndani ya kitabu, na masuala ya usihiri (uk. 8), mwandishi ameonesha kwa kutumia mambo ya ushirikina ambapo msomaji hutaka kujua nini kinachofuata katika riwaya. Vilevile, katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia taharuki mbalimbali ikiwemo pale Gusto anapokua anaongea na baba yake kwa mara ya mwisho (uk.12) kuhusu kumrithisha mambo ya usihiri.
Mfano; Hapo nilishituka nikamaka “Baba…!” “Najua hukulitegemea hili,mwanangu lakini hakuna mwingine wa kunirithi” sauti yake ilikuwa ya kutetemeka yenye amri .Alisema “Jina lako nimekwishalipeleka mbele ya wenzangu watakapokuja usishangae”.
Usawiri wa wahusika, ni kitendo cha kuwachora, kuwafafanua, kuwatambulisha na kuwajemnga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana au unaouwiana na uhusika wao. wahusika hutumia mbinu kadha wa kadha ili kusawiri uhusika wao katika kazi ya fasihi ikiwemo majazi,uzungumzaji nafsi,kuzungumza na hadhira ,kuwatumia wahusika wengine ,ulinganifu na usambamba wa maelezo. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ametumia mbinu ya majazi, mfano, kiongozi amepewa jina la “mfalme”, pia “malkia” ambaye ni mke wa mfalme katika (uk. 1), na “utubusara” (uk. 48) ambaye ni mtu mwenye busara. Vilevile katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi amemtumia mhusika Gusto anaposhuhudia mambo ya usihiri (uk.80) anasema;
“Nilimwangalia mzee huyu akienda angani kama kimulimuli”
Ufumbaji, huu ni utumiaji wa kauli zenye maana fiche, Ufumbaji hujitokeza katika kichwa cha habari,majina ya wahusika,sura ya kazi,na hata aya. Mwandishi wa riwaya ya KUFIKIRIKA ametumia kauli zenye kuonesha maana fiche,kauli ambazo huwa na maana tofauti na umbo la nje la kazi au matini husika.Katika riwaya hii ufumbaji umejitokeza katika (uk.28)anasema;
“Kutu huaribu chombo kisichotumiwa.Lazima ubongo wake utengwe na uharibifu wa kutu”.Vilevile katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia kipengele hiki katika kazi yake, ametumia ufumbaji au fumbo katika(uk.8) ambapo anasema;
“ Gusto kapata simu!” alitamka rafiki yangu John. “Atavuta sigara leo”.
Ritifaa,ni hali ambayo mtu mmoja hufanya mawasiliano na mtu aliye mbali naye, umbali huo waweza kuwa wa kijografia au kufariki. Katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI Mwandishi ametumia ritifaa kupitia kiapo cha asili ambapo Gusto anaapa ili arithi mikoba ya uchawi wa baba yake (uk.17). Anaapa kwa mizimu akitumia lugha ya asili ambayo kwa Kiswahili ina maana ya ; “Enyi mahoka wa mababu, Enyi wazee mliotangulia, Enyi wenzangu, Sikilizeni kiapo change, Sitasema wala kuwaza lolote, La ndani ni la ndani, Nishindwe mara tatu, Pembe hili linichome moto…!”
Pia katika (uk. 71-72) ambapo Gusto yupo makaburini anaongea na mpenzi wake ambae alishafariki. Anasema; “pokea zawadi hizi za maua mfuto….”
Kisengerenyuma, hii ni namna ya kupangilia vitushi au kusimulia kwa kuanza na tukio-tokeo kisha kufuatia tukio-chanzi ili kuboresha hamu ya hadhira kujua muundo wa vitushi katika kazi husika. Katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia mbinu hii katika (uk. 1) ambapo ameonesha tayari Gusto emerudi kutoka chuo lakini katika (uk. 3) ameonesha historia ya Gusto tangu alipozaliwa.
Hivyo basi, watunzi wa riwaya zote mbili wametumia kwa kiasi kikubwa mbinu mbalimbali za ubunilizi ili kuleta mguso pamoja na kuzifanya kazi zao ziweze kuvutia. Lengo kuu la kutumia vipengele vya ubunilizi ni kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira yake ambapo kwa kiasi kikubwa waandishi wamefanikiwa kufikisha ujumbe kwa jamii husika.
MAREJELEO
Mulokozi,M.M.(1996), Fasihi ya Kiswahili,Dar es salaam:OUT.
Mung’ong’o C.G. (2016), Mirathi ya Hatari. Dar es salaam. Tanzania. Mkuki na Nyota Publishers Limited.
Shaaban R (2013), Kufikirika. Dar es salaam. Tanzania: Mkuki na Nyota Publishers limited.
Wamitila. K.W (2003), Kamusi ya fasihi; Istilahi na Nadharia. Nairobi. Focus publication Ltd.
KUNDI 1. ( KOLOJI YA HUMANITI)
SWALI:
Vipengele vya kibunilizi vimejitokezaje katika riwaya ya Kufikirika na Mirathi ya Hatari?
Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao umebeba fasili ya riwaya na dhana ya ubunilizi, sehemu ya pili ni kiini cha swali ambacho kinaonesha vipengele vya ubunilizi kama vile ufutuhi, utomeleaji,ritifaa,ufumbaji,tanzia,usawili wa wahusika na ujadi jinsi vilivyojitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” iliyoandikwa na C.G.Mung’ong’o na riwaya ya “Kufikirika”iliyoandikwa na Shaaban Robert na sehemu ya tatu ni hitimisho ya kazi hii ambayo imebeba umuhimu wa vipengele vya ubunilizi katika riwaya ya Kiswahili kwa ujumla wake.
Riwaya ni hadithi iliyotungwa ambayo ina urefu wa kutosha, visa vinavyooana na ambayo imezingatia suala la muda. (Mlacha na Madumlla 1991).
Riwaya ni utungo wa kinathari wenye maneno kati ya 35,000 hadi 75,000 ambapo riwaya fupi huwa na maneno kati ya 35,000 na 50,000 na ndefu huwa na maneno kama 75,000. (Mphahlele 1976).
Riwaya ni utanzu unaoweza kuanzia maneno 35,000 na kuendelea. (Muhando na Balisidya 1976).
Udhaifu wa fasili hizi ni kuwa kufasili dhana ya riwaya kwa kutumia kigezo cha maneno haitoshi kwani mtu anaweza kuweka habari yoyote ile katika idadi hiyo ya maneno lakini isiwe riwaya. Hapa jambo la muhimu ni kuwa inapaswa ksuwa na mchangamano wa matukio, ujenzi wa wahusika na dhamira, muundo wake na hata mtindo.
Kwa ujumla, riwaya ni utanzu wa fasihi andishi unaohusu kazi ndefu za kibunifu za kinathari ambazo zina mawanda mapana, (visa, matukio, dhamira, wahusika, muundo na mtindo) na mchangamano wa fani na maudhui yake na kuzungumzia tukio la wakati fulani mahususi.
Ubunilizi ni uwazaji na uundaji wa wazo katika hali inayohalisika. Aghalabu dhana hii imetokana na kitezi “buni” ambalo humaanisha kuunda jambo ambapo jambo hilo huwa katika hali ya kidhahania kabla halijaonekana au kudhihirika kwa hadhira kupitia ogani za fahamu. Kupitia ubunilizi msanii ama mtunzi ana uwezo wa kubuni visa na wahusika kwa njia ambayo haikanganyi katika maisha na kuleta uhalisia.
Vipengele vya kibunilizi vinajitokeza katika riwaya mbalimbali vikitumiwa na waandishi wenyewe kwa madhumuni mbalimbali, hivyo vifuatavyo ni vipengele vya kibunilizi kama vilivyojitokeza katika riwaya ya “Kufikirika” iliyoandikwa na Shaaban Robert na“Mirathi ya hatari”iliyoandikwa na C. G. Mung’ong’o;
Ritifaa, hii ni hali ambayo mtu mmoja hufanya mawasiliano na mtu aliye mbali naye kijiografia au kifikra. Mtu huyo anaweza akawa anazungumza na mtu aliyekufa zamani au mtu aliyesafiri na yuko mbali na hivyo anaongea naye kwa fikra tu. Kwa mfano katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”ritifaa imejitokeza wakati Gusto anaapishwa kule pangoni. Mzee Mavengi anasema katika ukurasa wa (17),“Enyi mahoka wa mababu, enyi wazee mliotutangulia”. Hapa mzee Mavengi anaongea na watu waliokufa zamani (wazee) na mahoka (vitu ambavyo havionekani) kifikra tu. Pia wakati Gusto anakwenda kwenye kaburi la mpenzi wake Dina anaongea peke yake juu ya kaburi kama vile anaonana na Dina akiwa hai, ukurasa wa (72) anasema, “Dina, sina budi kuondoka kesho jioni kurudi shuleni. Itakuwa ni muda mrefu baadaye nitakapokuja kukuona tena, lakini kurudi ni sharti nitaarudi. Hili naahidi. Nachukia sana kukuacha peke yako.” Anayaongea yote hayo akiwa juu ya kaburi la Dina kama anaongea na Dina aliye hai. Piakatika kitabu cha “kufikirika” kipengele hiki kimejjitokeza hasa katika matatizo ya mfalme. Katika Ukurasa wa (3) Mfalme anajisemea mwenyewe,“maskini mwenye mtoto namuona kuwa ni bora kuliko mimi na pengine moyo wangu huona wivu juu yake”. Pia Ukurasa wa (3) Mfalme anajisemea mwenyewe, “lakini ni sikitiko kubwa kwa kukosa mtoto”. Pia Ukurasa wa (25) Mfalme anajisemea,“Kijana safihi na mbumbumbu! Sijapata kuona mfano wake. Namna watu kama hawa wapatavyo ualimu na sifa mimi sielewi”. Hapa mfalme alikuwa akizungumza peke yake yaani anaongea na hadhira ambayo haiko karibu naye bali ni katika mawazo yake tu.
Utanzia, utanzia ni hali ya kuleta huzuni kwa kutumia vipengele mbalimbali kwa hadhira yake. Utanzia hujengwa kwa kutumia mambo mbalimbali kama vile; mateso, ugumu wa maisha, mabaa kama njaa na magonjwa. Katika riwaya ya “Mirathi ya hatari utanzia unajitokeza pale Gusto anapopelekwa kwenye moto na mzee Malipula ili akubali kuwa yeye ndiye aliyemuua Kapedzile. Mwandishi anasema katika ukurasa wa (48),“...Nilipotamka neno hapana tu Malipula alinishika kwapani akanisogeza karibu na moto huo. Miguu yangu ikawa nusu mita hivi kutoka motoni. Maumivu yalliyofuatia yalikuwa hayavumiliki, nikajaribu kujivuta lakini sikuweza.” Utanzia pia unajitokeza wakati Gusto akiwa kwenye njozi anapoona mama yake na dada yake Nandi wakiungua kwa moto na kugundua kweli walikuwa wamekufa kwa kuchomwa na moto. Mwandishi anasema ukurasa wa (78), “Moto uliendelea na uharibifu wake kwa kasi ya ajabu. Mama na Nandi wakateketezwa kwa moto! Dakika ile nilisikia uchungu usio kifani! Moyo ulinusuru kupasuka. Nikalia kilio cha huzuni isiyo tumaini…..uchungu wa mama ukanichoma moto!Pia kifo cha Dina mpenzi wake Gusto kinaleta huzuni ukurasa wa (72).Pia katika riwaya ya “Kufikirika” dhana hii imejitokeza kama ifuatavyo. Ukurasa wa (32), “wakati mtoto wa mfalme akiwa mgonjwa, mfalme alisema “lakini mtoto niliyepata sasa ni mgonjwa sana. Yaonekana kwamba matumaini yangu yote ya kurithiwa na mwanangu karibu yatapondwa chini”. Pia katika Ukurasa huohuo, mfalme anasema “Mwanangu akipatwa na faradhi msiba utanipeleka ahera mara moja”. Kukosa mtoto ni tatizo ambalo lilikuwa linamsumbua mfalme na kujiona kuwa hafai katika jamii yake.Matukio kama haya husababisha huzuni na jitimai kwa msomaji au msikilizaji kwa kumhurumia mhusika.
Kisengelenyuma, ni hali ya kusimulia kwa kuanza na tukio tokeo na kumalizia na tukio chanzi. Mwandishi huanza kuonesha kitu kilichopo tayari kabla kuelezea kilivyotokea. Kwa mfano riwaya ya “mirathi ya hatari” mwanzoni kabisa mwandishi ameanza kuonesha tayari Gusto akiwa chuo kikuu kabala ya kuelezea huku nyuma alisomea wapi shule ya msingi na sekondari. Pia ameanza kuonesha mkasa ambao ulimpata Gusto na familia yake kwa ujumla kabla ya kuonesha ulivyotokea au ulisababishwa na nini? Anasema ukurasa wa (1-2), “….kwa jumla ni hali inipayo ridhisho ambalo sijawahi kulipata mahali pengine tangu nyumba yetu ifarakane katika mkasa ule uliokitikisa kijiji chetu ukaashiria mfarakano mkubwa Zaidi, mkasa uliokiacha kijiji kizima katika mahame”. Pia mwandishi anaelezea mahusiano yaliyopo tayari kati ya Gusto na Lulu na mipango ya kuoana kabla ya kuelezea Lulu na Gusto walianzaje kuingia katika mahusiano ya kimapenzi. Anasema ukurasa wa (2), “kwa yakini ni ridhisho ninaloweza tu kulishabihisha na penzi la Lulu-Lulu yule aliyeniliwaza mawazo akanipa upendo dhahiri hata nikasahau kabisa uzito wa maisha ya ukiwa. Kwa hakika maisha yangu bila yeye sijui yangekuwaje. Mipango yangu sasa ni kumwoa punde tumalizapo masomo yetu hapo mwakani.”
Utomeleaji, huu ni mwingiliano wa tanzu zingine za fasihi katika riwaya. Kwa mfano, mtunzi kuchopeka ushairi kwenye riwaya na matumizi ya barua. Katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” mwandishi ametumia barua, kwa mfano ukurasa wa (24) Dina anamuandikia barua mpenzi wake Gusto kumpa pole ya kufiwa na baba yake, anasema:
“Gusto wangu, Nina uchungu wa moyo na masikitiko makubwa juu ya kifo cha mzee wako mpenzi. Habari hiyo ilinifikia kama pigo kubwa. …..Mara upatapo barua hii njoo haraka. Nina jambo muhimu la kukueleza. Na …..ah! Maneno yamenippotea! Dina.Pia kuna matumizi ya nyimbo katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” Mwandishi anaonesha ukurasa wa (33), “Mavengi aliyachoma yale mawe matatu niliyoyachukua. ….Alikuwa anaimba hivi, “Gende, ve dadna, gende; Umwipao apugile uwuvina; Avedze lukule; Gende, yane danda, gende…
Maana yake, “Damu tembea mpwao atambalie umwinya. Katika riwaya ya “Kufikirika” kumejitokeza tenzi mfano katika Ukurasa wa (18-19) kuna utenzi wenye beti 4 beti la tatu ni; “Jina lake Milele. Lazima likumbukwe.
Kama
watu
wateule. Na
yeye
anakiliwe.
Nchi
ijae
tele.
Watu
mfano wa
yeye.
Daima
kwendambele.
Mambo yatazaamiwe”.
Pia kuna utenzi mwingine Ukurasa wa 37, utenzi huu unabeti moja tu ambalo ni; “Kweli
kama lebasi.
Uongo nao
matusi. Tena Kitu
azizi halisi.
Uongo pia najisi.
Mtu mwema haaugusi”.
Hizi ni tanzu ambazo zimechopekwa katika riwaya hizo na waandishi hao kama mbinu ya kibunilizi.
Ufumbaji, ni utumiaji wa kauli zenye maana ya uficho. Kauli hizo huwa na maana iliyo tofauti na umbo la nje. Ufumbaji huweza kuwa majina ya wahusika, aya au sura nzima na jina la kitabu chenyewe. Ufumbaji umejitokeza katika sehemu mbalimbali katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”,kwa mfano jina la riwaya yenyewe“mirathi ya hatari” ni la kiufumbaji, kwa kawaida binadamu anaposikia urithi au mtu anaporithi inategemewa kuwa anarithi vitu vya thamani kama vile nyumba, magari au pesa, lakini mwandishi wa riawaya ya “mirathi ya hatari” anaonesha urithi anaorithi Gusto ni uchawi ambaoanaurithishwa na baba yake. Kwa mfano ukurasa wa (12) anasema, “mwanangu, nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukiutumia vema, bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo. Nakuachia dawa zote na milki yangu katika mizungu ya sihiri. …Hapo nilishituka.”
Pia katika katika riwaya ya,“kufikirika” jina lake ni la kimafumbo. Kwa mjibu wa mwadishi jina hili linatokana na jina la nchi ambayo nayo pia haipo katika ulimwengu halisi mwandishi amesema katika utangulizi kuwa,sehemu ya (vii) anasema,“Kufikirika ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia. Kazikazini imepakana na nchi ya Anasa. Kusini nchi ya Majaribu, mashariki bahari ya Kufaulu na magharibi safu ya milima ya Jitihadi”.Pia ukurasa huohuo anasema,“Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo”.Vilevile majina ya wahusika yasiyokuwa na umahususi mafano “mfalme, malkia, mtoto wa mfalme, waziri mkuu, makundi ya waganga, mwerevu, mjinga, wanachama, wanachuoni, wanashaeria, waongozi wa dini, mahatibu na mkulima”. Majina haya yametumika kwa lengo la kufanya kazi hii iwe na ufiche.
Taharuki, ni hali ya kuwa na dukuduku la kuendelea kusoma kazi ya fasihi. Taharuki hujengwa kwa kutumia mambo kadhaa kama vile matendo ya wahusika, kisengelenyuma na mabadiliko ya sura. Hii inajitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” ambapo mwandishi ameanza kuonesha mipango baada ya wanakijiji kuhama. Ukurasa wa (1) anasema, “ni juma la pili leo tangu nifike hapa kuwasaidia ndugu wanakijiji hawa katika operesheni sogeza; operesheni ya kuhamia katika vijiji vya maendeleo.” Pia kitendo cha Gusto kutoroka kutoka pangoni, ukurasa wa (34) anasema, “na mara ile Mavengi alianza kunisogelea nikaona wakati wangu umewadia. Nikakurupuka nikauandama mlango, mbio. ….yule mzee bawabu alinyanyuka kunizuia, lakini nilimpiga kumbo la bega akatetereka.”Katika riwaya ya “kufikirika” imejitokeza sehemu mbalimbali kama vileukurasa wa (38), “kwa sababu hii kila raia alihofu kuwa atakamatwa na kuchinjwa kama mnyama”, pia Ukurasa wa (39) mwandishi anasema “Mwerevu alipokuwa hawezi kuona hata njia ya nyembambaa ya kujiokoa, mjinga aliweza kuona barabara pana ya kujiokoa mwenyewe namwenziwe”. Pia taharuki imejitokeza ukurasa wa (8) wakati waganga walipo tengwa katika makundi katika kudadisi ni kundi gani litafanikiwa kuponya ugumba wa mfalme na utasa wa malkia. Haya matukio yote humfanya msomaji aendelee kusoma riwaya hii ili kujua kitakachotokea au kuendelea baadaye.
Dayalojia. Dayalojia ni mbinu ya majibizano katika kazi ya fasihi, katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” mwandishi ametumia dayalojia pale ambapo mzee Mavengi anamchukua Gusto na kumpeleka kwenye mapango. Majibizano yao yanaoneshwa ukurasa wa (19); “Baadaye mzee Mavengi alilichukua moja la yale mapembe matano akalionyesha kwangu akisema; “Unazionashangahizi?
Ufumbaji, ni utumiaji wa kauli zenye maana ya uficho. Kauli hizo huwa na maana iliyo tofauti na umbo la nje. Ufumbaji huweza kuwa majina ya wahusika, aya au sura nzima na jina la kitabu chenyewe. Ufumbaji umejitokeza katika sehemu mbalimbali katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”,kwa mfano jina la riwaya yenyewe“mirathi ya hatari” ni la kiufumbaji, kwa kawaida binadamu anaposikia urithi au mtu anaporithi inategemewa kuwa anarithi vitu vya thamani kama vile nyumba, magari au pesa, lakini mwandishi wa riawaya ya “mirathi ya hatari” anaonesha urithi anaorithi Gusto ni uchawi ambaoanaurithishwa na baba yake. Kwa mfano ukurasa wa (12) anasema, “mwanangu, nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukiutumia vema, bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo. Nakuachia dawa zote na milki yangu katika mizungu ya sihiri. …Hapo nilishituka.”
Pia katika katika riwaya ya,“kufikirika” jina lake ni la kimafumbo. Kwa mjibu wa mwadishi jina hili linatokana na jina la nchi ambayo nayo pia haipo katika ulimwengu halisi mwandishi amesema katika utangulizi kuwa,sehemu ya (vii) anasema,“Kufikirika ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia. Kazikazini imepakana na nchi ya Anasa. Kusini nchi ya Majaribu, mashariki bahari ya Kufaulu na magharibi safu ya milima ya Jitihadi”.Pia ukurasa huohuo anasema,“Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo”.Vilevile majina ya wahusika yasiyokuwa na umahususi mafano “mfalme, malkia, mtoto wa mfalme, waziri mkuu, makundi ya waganga, mwerevu, mjinga, wanachama, wanachuoni, wanashaeria, waongozi wa dini, mahatibu na mkulima”. Majina haya yametumika kwa lengo la kufanya kazi hii iwe na ufiche.
Taharuki, ni hali ya kuwa na dukuduku la kuendelea kusoma kazi ya fasihi. Taharuki hujengwa kwa kutumia mambo kadhaa kama vile matendo ya wahusika, kisengelenyuma na mabadiliko ya sura. Hii inajitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” ambapo mwandishi ameanza kuonesha mipango baada ya wanakijiji kuhama. Ukurasa wa (1) anasema, “ni juma la pili leo tangu nifike hapa kuwasaidia ndugu wanakijiji hawa katika operesheni sogeza; operesheni ya kuhamia katika vijiji vya maendeleo.” Pia kitendo cha Gusto kutoroka kutoka pangoni, ukurasa wa (34) anasema, “na mara ile Mavengi alianza kunisogelea nikaona wakati wangu umewadia. Nikakurupuka nikauandama mlango, mbio. ….yule mzee bawabu alinyanyuka kunizuia, lakini nilimpiga kumbo la bega akatetereka.”Katika riwaya ya “kufikirika” imejitokeza sehemu mbalimbali kama vileukurasa wa (38), “kwa sababu hii kila raia alihofu kuwa atakamatwa na kuchinjwa kama mnyama”, pia Ukurasa wa (39) mwandishi anasema “Mwerevu alipokuwa hawezi kuona hata njia ya nyembambaa ya kujiokoa, mjinga aliweza kuona barabara pana ya kujiokoa mwenyewe namwenziwe”. Pia taharuki imejitokeza ukurasa wa (8) wakati waganga walipo tengwa katika makundi katika kudadisi ni kundi gani litafanikiwa kuponya ugumba wa mfalme na utasa wa malkia. Haya matukio yote humfanya msomaji aendelee kusoma riwaya hii ili kujua kitakachotokea au kuendelea baadaye.
Dayalojia. Dayalojia ni mbinu ya majibizano katika kazi ya fasihi, katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” mwandishi ametumia dayalojia pale ambapo mzee Mavengi anamchukua Gusto na kumpeleka kwenye mapango. Majibizano yao yanaoneshwa ukurasa wa (19); “Baadaye mzee Mavengi alilichukua moja la yale mapembe matano akalionyesha kwangu akisema; “Unazionashangahizi?
Ndiyo Na
manyoyahaya?
Ndiyo
Basi hili baba yako alilitumia kama ndege Ulaya akiwamokazini
Lakini mbona ni dogo sana kulinganisha na kimo cha mtu?”
Hayo ni majibizano kati ya Gusto na mzee Mavengi wanapokuwa kule pangoni mahsusi kabisa kumpa Gusto elimu kuhusu uchawi.
Katika riwaya ya“kufikirika” ukurasa wa (4) katika mazungumzo kati ya Mfalme na Waziri, Ukurasa wa (5-7) mazungmzo ya mfalme na waganga, Ukurasa wa (23-26) mazungumzo ya mwalimu na mfalme, Ukurasa wa (27-28) mazungumzo kati ya Mwalimu na mgeni. Kwa mfano katika ukurasa wa (24) Mfalme anasema, “Pia nilikataa kuwa mwanangu asicheze ila asome wakati wote lakini hukutii”na mwalimu anajibu kuwa “umefanya vyema, Mfalme mtukufu, kwa kutangulia kunitoa kazini”. Hapo wanazungumza kwa kupeana nafasi ili mwingine azungumze huku mwingine akisikiliza kabla ya kuzungumza.
Ujadi, hii ni hali ya kutumia vipengele vya fasihi simulizi katika kazi ya fasihi andishi. Hapa mwandishi huweza kutumia mambo kama vile nahau, methali na ama misemo. Hii inajitokeza katika riwaya ya “mirathi ya hatari” ukurasa wa (39), anasema, “majuto daima ni mjukuu”, ukurasa wa (73) anasema pia, “dawa ya moto ni moto.” Siyo hivyo tu lakini pia ukurasa wa (27) anasema, “mtegemea Mungu si mtovu.Pia katika kitabu cha riwaya cha“kufikirika” kuna matumizi ya methali mfano Ukurasa wa(6) mwandishi anasema“mwenye haya hazai”. Piaukurasa wa(26)“milima haikutani binadamu hukutana”. Vilevile Ukurasa wa(5) anasema,“nyumba ya mgumba haina matanga”.Pia matumizi ya majina ya waganga Ukurasa wa(8) ambao ni “waganga wa mizizi, waganga wa makafara, waganga wa mizinguo, waganga wa hirizi na waganga wa mashetani”. Pia Ukurasa wa (4) neno “ramli” na Ukurasa wa (9) neno “makafara”.Pia “makombe, Gilani, Kinani, ktimari, makusuri, shamhariri na ruhani. Huo ni ujadi ambao waandishi hao wamepachika kwenye riwaya hizo.
Usawili wa wahusika, ni kujenga wahusika kwa kuwapa maneno na matendo yanayofanana na uhusika wao. Katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”Gusto ni mhusika ambaye jina lake na anavyofanya vinasawili, kwa mfano ukursa wa (1) anashirikiana na wanakijiji kama ishara ya kuonesha kuwa elimu ya chuo kikuu imemsaidia kuwa na kushirikiana na jamii yake. Pia kitendo cha Gusto kutotaka kuwa mchawi ni usawili way eye kama mtu ambaye hataki ukale yaani uchawi. Katika riwaya ya“kufikirika”kuna usawiri wa wahusika, kwa mfano, mhusika “Mfalme” amepewa maneno yanayofanana na wadhifa wake kwa mfano katika sura ya kwanza ukurasa wa (1-3) mfalme anaelezea juu ya vitu vilivyopo katika nchi yake, maneno ambayo ni ya kawaida kwa watawala mfano Ukurasa wa (3) Mfalme anasema “nina majeshi ya askari walio shujaa, waongozi hodari na raia wema na watii”. Pia mhusika Utubusara ujinga hasara ametumiwa kutetea utu kwakuepushaumwagajidamunaalijitahidikuepukananaujinga mfano katika ukurasa wa (40) mjinga anasema “Hapana haja ya kumdharau mwanamke”. Hapa mtu mwerevu hawezi kumdharau mtu mwingine bali mjinga tu ndiye huweza kufanya hivyo.
Ufutuhi, hii ni mbinu ya ucheshi inayotumiwa na mwandishi kutokana na matendo na maneno ya wahusika. Katika riwaya ya “kufikirika”mbinu hii imejitokeza sehemu mbalimbali, kwa mfano; mwandishi ametumia ucheshi katika kutoa kauli za kejeli kama vile ukurasa wa (11) anasema, “mfalme na malkia walilemewa na uzito wa hirizi juu ya miili yao wakashukuru siku walipoamuriwa kuzivua…”, pia katika ukurasa huohuo mwandishi anasema “siku hiyo kuni, makaa na mafuta yote yalikwisha kwa kuchoma hirizi hizo”. Vilevile katika ukurasa wa (45) mwandishi anasema, “kama mkulima si mjinga na mchuuzi si mwerevu”, kauli hii imetumiwa kwa ajili ya kukejeli ambapo inaleta ucheshi. Vilevile majina ya wahusika mfano “Utubusara ujinga hasara” Ukurasa wa (47), ni jina la mhusika ambaye alipinga ujinga na umwagaji damu za watu na jina hilo linaleta hali ya ufutuhi kwa msomaji.
Kwa ujumla vipengele vya kibunilizi katika kazi ya fasihi huweza kusaidia kuonesha uumbaji wa tanzu hizo. Kuainisha maudhui, kuondoa uchovu wa kuendelea kusoma, kuweka msisitizo, kujikaribisha na uhalisia, Kushirikisha hadhira katika kutafakari kwa ukaribu, kujitanibu na ghasia za kufuatwafuatwa na mkono wa dola, kuonesha ufundi wa mtunzi katika kusawili maneno na hadhi ya wahusika. Vipengele vingine vinavyoweza kutumiwa na mwandishi katika kazi ya fasihi ni kama vile muundo, mtindo, ujumbe, vitushi, dhamira, wahusika na ushikamani
MAREJELEO
Mhando, P. & Balisidya, N (1976). Fasihi na Sanaa za Maonyesho, Dar es Salaam: Tanzania Publishig House.
Mlacha, S & Hurskainen, A., (1995). Lugha, Utamaduni na Fasihi Simulizi ya Kiswahili, TUKI na Chuo Kikuu cha Helsinki.
Mung’ong’o, C. G (1977). Mirathi ya hatari. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Robert, S (2013). Kufikirika. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers Ltd.
SWALI
Shaffi Adam Shaffi katika Vuta N’Kuvute amefanikiwa kujenga Vitumba vya kutosha.Jadili.
Swali letu linataka tuelezee ni jinsi gani Shafi Adam Shafi amefanikiwa kujenga vitumba katika riwaya ya Vuta N’kuvute. Katika kujadili swali hili tumeligawa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni utangulizi ambapo tutajadili historia fupi ya mwandishi pamoja na maana ya vitumba. Sehemu ya pili ni vitumba ambavyo vimejengwa na mwandishi na mwisho ni hitimisho.Shafi Adam Shafi alizaliwa mjini Zanzibar mwaka 1940. Baada ya kupata elimu yake ya msingi alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Seyyid Khalifa mwaka 1957 hadi 1960. Pia alibahatika kupata elimu yake ya diploma ya juu katika fani ya siasa ya uchumi katika chuo cha Fritza Heckert iliyokuwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani 1963. Alipata mafunzo ya uandishi wa habari nchini Parague, nchini Czechoslovakia mwaka 1964 hadi mwaka 1965, nchini Sweden mwaka 1982 na nchini Marekani mwaka1983. Mwaka 1978 aliandika riwaya yake iliyoitwa kasiri Ya Mwinyi Fuad, mwaka 1979 aliandika riwaya ya Kuli, mwaka 1999 aliweza kuandika riwaya ya Vuta N’kuvute na mwisho ni riwaya ya Haini mwaka 2003. Mwandishi huyu amejikita katika kuandika riwaya dhati au azizi.Katika kazi zake zilizo nyingi dhamira zinazojitokeza zaidi ni matabaka katika jamii, ndoa za kulazimishwa, mapenzi na ukarimu. Mbinu za kisanaa zinazotumiwa na mtunzi huyu katika uwasilishaji wake wa dhamira ni upambaji wa wahusika, usimulizi, kuingiliana kwa tanzu, tashibiha, misemo, takriri, taswira, motifu na matumizi ya barua.Ponera, A.S na Luhwago N. (2015), wanasema kuwa Vitumba au vipopo ni mawazo yajengekayo katika akili ya msomaji au muhakiki baadaa ya kuisoma kazi ya kifasihi kutokana na mjengo wa vitushi vya riwaya. Vitumba katika kazi ya fasihi siyo lazima vioneshwe wazi wazi kwakuwa huwa ni utambuzi wa msomaji mwenyewe kulingana na anavyoisoma kazi fulani ya kifasihi. Kuna baadhi huweza kuviita dhamira ndogondogo kwa sababu huwekwa pengine kwaajili ya kujenga dhamira kuu katika riwaya.Katika riwaya ya VUTA N’KUVUTE, iliyoandikwa na Shafi Adam Shafi amefanikiwa kujenga vitumba mbalimbali ambavyo ndiyo chachu ya ujenzi wa dhamira zake kuu kama mapenzi na ndoa, ukombozi wa kisiasa na kiutamaduni na hata kijamii. Kwa kutumia riwaya hii tumeweza kubaini vitumba au vipopo mbalimbali vilivyojengwa na mwandishi kama ifuatavyo;Kitumba cha ukasumba wa lugha zetu za asili; ukasumba ni hali ya mtu kudharau kitu Fulani kwa sababu ya kuwepo kwa kitu Fulani ambacho ni tofauti na kile kilichopo. Hii hali inatokea pale ambapo Denge baada ya kufika karimjee bar. Hili eneo lilikuwa ni kwaajili ya watu wa kipato cha juu. Inaonekana ni ukasumba kwa kuwa Denge alikuwa ni mwanaharakati wa kutaka kuikomboa jamii hivyo kutumia lugha ya kiingereza ni kusaliti lugha yake ya asili ambayo ni Kiswahili kama ishara ya ukombozi wa wazanzibar. Hii inajitokeza katika riwaya ya Vuta n’kuvute katika ukurasawa 134 anaposema, “Good evening young man,” Denge alimwamkia yule Bawabu “Good evening sir.” Alijibu akijipinda kuonyesha heshima.Kutumia lugha ya kiingereza ni dhahili kuwa Denge aliamua kuisaliti lugha yake ili apewe heshima kwa kuwa lugha ya kiingereza ilionekana kuwa ni lugha ya heshima pale Zanzibar kipindi cha ukoloni.Kitumba cha hali ya ugumu wa maisha gerezani; ugumu wa maisha ni vikwazo vyote vitokeavyo katika mchakato wa maisha ya mwanadamu. Hali hii tunaiona pale ambapo Denge alikamatwa na kupelekwa gerezani akiwa na nguo ya ndani tuu (chupi) akituhumiwa kubandika makaratasi ya kutaka uhuru. Katika hii riwaya ukurasa wa 192 anasema;-Chumbani mle mlijaa harufu ya uvundo. Mlikuwa na virago vilivyokunjwa upande mmoja vitano na mwingine vitano na pembeni kulikuwa na doo. Alifikiri ndani ya ndoo ile mtakuwa na maji angalau anawe mikono, lakini alipoikurubia harufu ya uvundo ilizidi nandoo ile ilikuwa tupu.Pia hata ukiangalia chakula alichopewa Denge kilikuwa kinatisha kuashiria kuwa yale maisha yalikuwa ni magumu. Ukurasawa 193 mwandishi anasema, Denge aliichukua ile sahani akaenda mpaka kiragoni, akakaa, ile sahani ameiweka mbele yake anaitazama. Halua si halua, mseto si mseto, ugali si ugali.Kutokana na haya maelezo ni dhahili kuwa wafungwa katika lile gereza walikuwa wanaishi maisha ya shida kwa sababu ya chakula kibovu pamoja na uchafu wa chumba.Mahangaiko ya kutaka kuikomboa jamii; hii ni hali ya kwenda huku na kule bila kutulia au shughulika. Au ni hali ya kusumbuliwa na jambo Fulani kichwani kiasi cha kukupa wasiwasi au gaya. Hii hali tunaiona pia kwa Denge aliyekuwa anahangaika kutafuta uhuru wa mzanzibar pale Yasimin alopoenda nyumbani kwa Denge na kukuta chumba kichafu kana kwamba siyo makazi ya mtu. Kitumba hiki tunakipata katika ukurasa wa 144, mwandishi anasema;-Hee utafikiri chumba kimefukizwa kwa moshi wa sigareti?” Yasmin alilalamika. Na hiki chumba haitatokea hata siku moja mtu akaja akakikuta Safi. “sina wakati wa kusafisha,” Denge alijibu. “huna wakati unafanya kazi gani? Hata ungekuwa na kazi ya kupaka mbingu rangi.” Pia hapa tunaona ni uhalisia kabisa kuwa Denge alikuwa anashindwa kusafisha chumba chake kwasabavu ya kuwa na majukumu mengi ya kutaka kuikomboa jamii yake.kitumba cha tamaa ya mapenzi; tamaa ni hali ya kutaka sana kitu au matamanio ya kuwa na hamu ya kupata kitu, au jambo fulani. Tamaa katika riwaya hii Shafi A Shafi amefanikiwa kuijenga vizuri kwa kutumia wahusika wake Denge na Yasmin nyumbani kwa Mwajuma. Hii inajitokeza pale Denge alipoenda kwa Mwajuma kumtaka hali na kumkuta Yasmin chumbani akiwa ndo anatoka kuoga akiwa na kanga. Baada ya kuingia chumbani Denge alianza kumwangalia Yasmin kwa matamanio ya kimapenzi. Hiki kitumba kimejengwa na mwandishi kwa lengo la kuijenga dhamira kuu ya mapenzi na ndoa. Katika ukurasawa 44 hadi 45 mwandish anasema,Alikuwa amejizonga kanga mwilini ncha moja ameitupia bega la kulia na nyingine la kushoto. Amejikumbatia mkono wa kulia ameshika bega la kushoto na mkono wa kushoto ameshika bega la kulia.Ile kanga ilikamatana sawasawa na mwili wake ikawa kama iliyopakwa gundi imeloa chepechepe.mkatiko wa mwili wake ulionekana waziwazi na Denge hakuweza kujizuia ila alimkodolea macho nayo yakathibitisha ile sifa ya kwamba hayana pazia.Pia hata katika ukurasa wa 45 mwandishi anaendelea kujenga kitumba hiki cha tamaa pale naposema,Kwa haraka macho ya Denge yakaangukia chini akaiona miguu ya Yasmin iliyo kama matendeguya kitanda cha simsim.Kutokana na haya maelezo yanadhihirisha kuwa Denge alikuwa anamtamani Yasmin kimapenzi kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa muda ule.Kitumba cha uasherati; uasherati kwa ujumla ni ile hali ambayo watu wawili wanaingia katika mahusiano ambayo yanabeba mambo mengi ikiwemo kufanya mapenzi kabla ya maisha ya ndoa, haya yamejitokeza katika riwaya hii pale ambapo Mambo aliweza kukutana kimwili na Mwajuma vilevile Denge na Yasmini, mwandish ameonesha suala hili katika ukurasa wa 117 na 118,“Mambo alimshika mkono Mwajuma. Aliondoka naye na kwenda chumbani kwake ambako walinong’ona kidogo tu na mara mlango ulisikika ukikomewa.”“Denge alianza kumvua Yasmini nguo mojamoja na hatimaye walijiona wamelala kitandani kila mmoja kama siku aliyozaliwa. Wote walisabiliana miili yao mpaka kila mmoja akatosheka.Huu ulikuwa ni uasherati kwa kuwa Mambo na Mwajuma walikuwa siyo wanandoa na wakafikia hatua ya kufanya mapenzi.Kitumba cha wivu; ni hali ya kuwa na kinyongo au kijicho wakati mtu aonapo mali, mafanikio au maendeleo ya mtu mwingine au ni tabia ya mtu kusononeka aonapo mpenzi wake ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwingine. Suala hili limejitokeza katika riwaya hii pale Mwajuma na Yasmini walikuwa wanamzungumzia Shihab kutokana na gubu alilokuwa nalo kwa mkewe kama mwandishi alivyoandika katika ukurasa wa 211.“Nisikonde! Mwanaume yule! Ana wivu, ana gubu, ana nongwakama mwanamke”, Yasmini alilalamika.“Nakwambia kaniweka kaniweka ndani kama mwari, hata huyo mwari ana afadhali, sina shoga sina jirani, sina jamaa, mimi na ndani na ndani na mimi, sendi sirudi.”Kutokana na maelezo yaliyotolewa na mwandishi ni dhahili kuwa Shihab alikuwa na wivu wa kumapenzi mpaka akafikia hatua ya kumfungia Yasmin ndani kama mwari.Kitumba cha ubaguzi wa rangi, ni hali, sera au mpango wa kuhudumia watu kwa kuegemea misingi ya hadhi, kabila, elimu, rangi. Hali hii imejitokeza katika kitabu hiki ambapo katika jamii hii kulikuwa na ubaguzi wa rangi kati ya Wazungu, Wahindi na Waafrika. Katika riwaya tunamuona Yasmin anavunja miiko waliyojiwekea Wahindi ya kutokuingiliana na Waafrika. Mwandishi ameonesha suala hili katika ukurasa wa 4 mwandishi anasema,“Ijapokuwa Yasmin alitumia muda wake mwingi dukani, lakini alipata muda wa kupanga ushoga na jirani yake Mwajuma. Mwajuma alikuwa ni mschana wa kiafrika na tabia yake ya ucheshi na masihara ilimfanya Yasmin avunje miiko ya kihindi ya kutokuingiliana na Waafrika.”Hapa ni dhahili kuwa kulikuwa na ubaguzi wa rangi katika hii jamii na ndiyo maana Wahindi wakaamua kuweka miiko ya kutokuingiliana na Waafrika.Kitumba cha ulevi; ulevi ni hali ya kukosa kuweza kutumia mwili na akili au kupoteza fahamu kwa sababu ya kutumia pombe. Mwandishi ameonesha dhana ya ulevi katika riwaya hiikwa kuwatumia wahusika Chande, Denge, Mambo na Huseni ambao walikuwa wanapanga wakutane baani yaani baa ya minazi miwii. Kwa kawaida mazingira ya baani huwa ni kwa lengo la ulevi au kunywa pombe na munywaji wa pombe kwa lugha ya kawaida ni mlevi. Katika riwaya hii ulevi umeoneshwa na mwandishi katika ukurasa wa 130- 131.“Mambo na Denge walimkuta Chande ndo kwanza anaamka na hawakuwa na mengi ya kumwambia ila,” tukutane baa ya minara miwili.”Chande aliwatazama na kuwauliza, “mbona na masuti na matai mnakwenda wapi?”.“Wewe tunakwambia tukutane minara miwili.”Kitendo cha Denge na Chande kuahidiana kwenda kukutana mazingira ya baani ni ushahidi tosha kuwa walikuwa ni walevi.Kitumba cha ushawishi; ushawishi ni tendo la kumubembeleza mtu akubali kufuata fikira au maelezo yako. Mwandishi amefanikiwa kuonesha kitumba hiki kwa kumtumia mhusika Mwajuma katika kumshawishi Yasmini hadi kashawishika kwenda kwenye dansi ambapo hajawahi kufika kabla kwa kuwa miiko ya Wahindi haikuruhusu kwenda maeneo kama yale kwa sababu yalikuwa ni maeneo ya Waafrika au ya tabaka la chini. Hii imejitokeza ukurasa wa 35 hadi 36 Mwandishi ameandika,“Yasimini unasemaje jumamosi ya leo?” Mwajuma aliuza. “Nafikiri hukupata kuuona usiku wa jumamosi,” aliongeza. Walikuwa wamekaa jikoni, Mwajuma anamenya ndizi na Yasmini anamsaidia kazi ndogondogo, kwani kazi ya kumenya ndizi hakuwahi kuifanya maishani mwake.“Kwani leo kuna nini?” Yasimini aliuliza. “Leo?” Mwajuma aliuliza kwa mushangao macho ameyatumbua.“Ama kweli shoga yangu ulikuwa hupo ulimwenguni. Leo mji mweupe, kuna dansa la kukata na shoka Raha Leo, kuna mbwa kachoka kiembe samaki na malindi kuna tarabu”. “Vipi sasa, Sista utaenda kutia macho nuru?”Huu ulikuwa ni ushawishi wa Mwajuma kumtaka Yasimini aende kucheza muziki
.Kitumba cha kupinga ukoloni;
kupinga ukoloni ni kitendo cha kuondoa uonevu, unyanyasaji na kuleta
ustawi katika jamii. Hiki kitumba kimejitokeza pale ambapo Mwandishi
ameandika katika ukurasa wa 76 hadi 77 kuhusu kitabu kinachohusu
harakati za kupinga ukoloni visiwa vya Zanzibar na Pemba ambapo hiki
kitabu kilikuwa kinaelezea mambo ya Waafrika kutaka uhuru wao kutoka kwa
wazungu. Hata neon lenyewe Pan-africanism linadhihirisha kuwa kulikuwa
na harakati za kadai uhuru Mwandishi anaposema,Inspekta Wright alipovuta mtoto wa meza na kutoa kitabu halafu akampa Kopolo Matata. “Soma,’’alimwamuru.“Pan-Africanism
or communism in Africa,by GeorgePadmore”. Kopolo Matata alisoma kwa
sauti ndogo halafu akamtazama Inspekta Wright.” “Wewe kwisha ona hii?” “Bado afendi.” “Nafikiri nini juu ya hii book?” “Hatari sana.” “Hatari sana,” Inspecta Wright aliyakariri maneno ya Kopolo Matata, “Wewe na nafikiri nani anaingiza material kama hii nchini?Kitumba cha vitisho;
ni mojawapo ya vitumba vilivyojitokeza katika riwaya hii ambapo
tunamuona Denge anaongea na Inspekta Wright akitoa vitisho vikali juu ya
kulipua club waliyokuwa wakitumia Wahindi kwa ajili ya starehe zao na
kuwabagua Waafrika. Kutokana na kitumba tunapata dhamira kuu ya ukombozi
wa kisiasa na matabaka. Kama mwandishi alivyoonesha katika ukurasawa
147 anaposema, “Mimi
nazungumza kwa niaba ya kikundi kinachoitwa Lipua, juzi tulilipua
Karimjee club na huo ulikua mwanzo tu, sasa tutalipua English club, siku
yoyote ile”.Maelezo
ya Denge kwa Inspekta Wright yanaonesha jinsi Denge alivyokuwa
anamtishia ili aweze kuogopa lakini apunguze kuwakandamiza Waafrika.Kitumba cha urafiki;ni
hali ya kuwepo na uhusiano mwema kati ya watu mbalimbali au jamii na
jamii.Ni mojawapo ya dhamira ndogondogo (kitumba) ambayo pia imejitokeza
katika riwaya hii, ambapo dhamira hii imepelekea ujenzi wa dhamira kuu
ambayo ni mapenzi ya dhati. Katika riwaya hii mapenzi ya dhati
yamejitokeza kati ya Yasmin na Mwajuma ambapo Mwajuma alikuwa anamsaidia
rafiki yake Yasmin alipokuwa akipatwa na matatizo. Suala hili
limejitokeza katika ukurasa wa 19-20 mwandishi anaposema, “Maskini
shoga yangu. Sasa una shauri gani?” Mwajuma aliuliza za kwa huruma za
dhati.”“Sina shauri lolote, nimekuja kwako kukusikiliza utanambia nini.
Tafadhali nisitiri, nisitiri aibu yangu!”Kitumba cha ndoa za kulazimishwa, hizi
ni ndoa ambazo mara nyingi huwa za utotoni tena za kulazimishwa. Katika
riwaya ya Vuta n’Kuvute, mwandishi amesawiri ndoa ya utotoni ya
kulazimishwa kuolewa kwa Yasimin na Bwana Raza ambaye kwa umri wake ni
sawa na babu yake kupitia hiki kitumba tunapata ujenzi wa dhamira kuu
ambayo ya nafasi ya mwanamke katika jamii ambapo anaonekana kuwa ni mtu
duni na hawezi kujichagulia mume wa kuolewa naye. Watoto wa kike
wamekuwa wakiozwa kwa nguvu bila ridhaa yao. Shafi Adamu Shafi katika
ukurasa wa 1 anasema”“Mara
tu baada ya kuvunja Ungo, Yasimini aliozwa mume. Alikuwa mume wa jamii
yake ya Ithnaashiria ambaye alikuwa akiishi jirani naye hapo Mtendeni.
Alikuwa ni mume asiyelingana naye hata kidogo. Si kwa umri wala tabia,
kwani wakati Yasmini ni kigoli wa miaka kumi na tano tu, mumewe bwana
Raza alikuwa zee la miaka hamsini na mbili. Wakati bwana Raza
keshazeeka, Yasmini alikuwa mtoto mbichi asiyeelewa kitu chochote.
Kukubali kwake kuolewa ilikuwa ni kwa sababu ya kuwaridhi wazee wake tu.
Yeye mwenyewe hakuona fahari ya kuolewa na mzee anayeweza kumzaa.
Hakupenda kufuatana na mumewe pahala popote na hata ile siku inayotokea
wakeenda senema, basi yeye hapendi kukaa karibu naye”Yasimin
aliozeshwa kwa nguvu akiwa bado na ufahamu mdogo, hakuweza kujitetea
kukataa kuozwa na Bwana Raza, hali iliyompelekea Yasmini kutokuwa na
furaha na ndoa yake.
Kutumba cha Suala la ukarimu,ni
ile hali ya kuwasaidia watu wenye kuhitaji msaada au ni namna ya mtu
anavyowakaribisha watu vizuri nyumbani, kuwapatia chakula, kuwajali,
kuwathamini na kuwafariji pale wanapopatwa na maswahibu. Katika tamaduni
ya waswahili humchukulia mwanamke kama mtu mwenye ukarimu sana. Katika
riwaya hii ya Vuta n’Kuvute, Shafi Adamu Shafi amemtumia binti wa
Kiswahili Mwajuma kuwa ni mtu mkarimu sana hali iliyopelekea kupendwa na
watu. Mwandishi katika (ukurasa wa 22) anasema” “Mwajuma,
ijapokuwa ni mtoto wa kimasikini alikuwa na roho nzuri ya ajabu na roho
nzuri yake ilichanganyika na ukarimu usiokuwa na mfano. Alikuwa yuko
tayari kumkirimu mtu chochote kidogo alichokuwa nacho. Alikuwa mwingi wa
huruma na siku zote alikuwa tayari kumsaidia yeyote aliyemweleza shida
zake, pindi akiwa na uwezo wa kumsaidia mtu huyo”Mwajuma
alikuwa mwanamke mkarimu sana ambaye aliwakarimu watu bila kuwabagua
hasa walipokuwa na shida. Kwa mfano Yasmini alipomkimbia mumewe, na
kufukuzwa kwao alipokelewa na mwajuma licha ya kuwa mwajuma hakuwa na
chumba maalumu kwa wageni.
Kitumba cha kulipiza kisasi;ile
hali ambapo mtu aliyefanyiwa kitu au vitu vibaya kulipiza kwa mtu
aliyemfanyia tendo hilo. Polisi walienda kwa Denge na kuingia chumbani
kwake na kuvuruga vitu mule ndani na kusambalatisha kila kitu ovyo hivyo
Denge akapanga kulipiza kisasi kwa kile kitendo alichofanyiwa na wale
polisi kama mwandishi alivyoandika katika ukurasa wa 130,“Wao wamekuja kutufanyia fujo nyumbani mwetu na sisi lazima tulipize kisasi. Lazima tukawafanyie fujo Karimjee Club.” “Sikiliza
Mambo, tusfanye mambo ya kipumbavu, kwanza wewe unafanya kazi na
mshahara unaoupata unatusaidia sote, tena si kufukuzwa kazi kwasababu ya
maana lakini kufukuzwa kwasababu ya kufanya fujo, hiyo si…” Mambo
aliyakatiza maneno ya Denge akasema, “sikiliza brother, wewe siku zote
unasema haya ni mapambano ya vuta n’kuvute. Vuta n’kuvute maana yake
baada ya kisa nimkasa, kwahivyo wao leo wametufanyia kisa nasisi
tuwafanyie mkasa, au unasemaje?” Ni dhahili kwamba Denge na wenzie walikuwa wanapanga kulipiza kisasi wanaposema wamefanyiwa kisa kwahiyo na wao wanafanya mkasa.Kwa
ujumla, waandishi wa riwaya hujenga vitumba kwa lengo la kukamilisha
dhamira zao kuu ambazo huwa wamezilenga kupeleka kwa jamii husika. Hivyo
basi mwandishi huyu Shafi Adam Shafi amejenga hivi vitumba kwa lengo la
kukamilisha dhamira zake kuu za matabaka, mapenzi na ndoa pamoja na
ukombozi. Lakini pia ikumbukwe kuwa mwandishi anaweza kutumia kitumba
mawazo yake au malengo ya kile kitumba yakawa tofauti na mawazo ya
msomaji au muhakiki wa hiyo kazi.
MAREJELEO Kamusi ya Karne ya 21 (2013), Kamusi ya Kiswahili: Lnghorn Publishers, Nairob.Omari, A. A (2014), Kuchunguza Dhamira Za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: MifanoKutokaKulinaVuta N’kuvute: Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.Ponera, A.S na Luhwago N. (2015), Mwangozo wa Kozi ya Riwaya ya Kiswahili: Chuo Kikuu Cha Dodoma.Shafi, A.S (1999), Vuta N’kuvute, Mkuki na Nyota Publishers: Dar es salaam.
DHANA YA MOTIFU KATIKA RIWAYA INAVYOJADILIWA NA WATAALAMU WA KISWAHILI
Motifu ni kati ya vipengele muhimu katika uchambuzi wa kazi za kifasihi, hususani katika kuchambua vipengele vinavyojenga maudhui ya kazi hizo. Dhana ya motifu imefasiliwa na wataalamu mbalimbali. Kwa mfano: Dorson (1972) kama alivyomnukuu Thomson (1932:32) anasema motifu ni kizio kidogo thabiti kipatikanacho katika sanaa jadia, maelezo ambayo masimulizi yote yanajinasibisha nayo. Yanaweza kujikita kwa mhusika fulani ndani ya masimulizi, ndani ya matendo yaliyo katika masimulizi na mara nyingine katika hali inayojitokeza sana katika tendo lililo ndani ya usimulizi.
Thomson naye aliangalia motifu kwa kuihusisha kwa kiasi kikubwa na masimulizi ndani ya sanaa jadia. Hakuangalia motifu kwa mapana yake katika kazi zote za fasihi andishi na simulizi.
Wamitila (2003) kwa upande mwingine anasema dhana hii, motifu, hutumiwa kurejelea wazo kuu na sehemu ya dhamira katika kazi ya kifasihi. Huweza pia kutumiwa kuelezea elementi ya kimuundo au kimaudhui inayotawala kazi fulani. Anatoa mfano wa riwaya yake iitwayo Binaadamuambapo anasema safari ni motifu muhimu ya kimuundo na kimaudhui.
Umuhimu wa motifu anaouelezea Wamitila kwa kuzingatia maudhui na muundo unamaanisha kwamba, kuwapo kwa motifu ya safari katika hadithi hiyo ndiko kunakobeba muundo na maana ya hadithi. Motifu hiyo haiwezi ikaondolewa kwani itaathiri muundo na ujumbe au maana ya hadithi hiyo.
Encyclopedia the Free Dictionary (2011) inasema motifu ni kitu, jambo, wazo au muundo katika kazi ya fasihi linalojirudiarudia. Motifu ni muhimu kwa sababu inamwezesha mtu kuona mawazo makuu na dhamira anazojaribu kuzionyesha msanii ili aweze kuitafsiri kazi ya sanaa kwa ufasaha zaidi.
Mulokozi (2009) anayaendeleza mawazo ya Encyclopedia (imeshatajwa) na kusema motifu ni kipengele radidi cha kijadi/kikaida au kimaudhui kinachotumiwa na wasanii katika kazi zao ili kutoa ujumbe fulani. Mulokozi (keshatajwa) anatoa mifano ya motifu za kifasihi kuwa ni: motifu ya mama wa kambo, motifu ya safari, motifu ya msako, motifu ya mwanamke mshawishi, motifu ya bi kizee, motifu ya mzungu mweusi, motifu ya mtoto wa ajabu, motifu ya mtoto kigego, motifu ya mnyonge anayemshinda mwenye nguvu, motifu ya nunda/ zimwi mla watu, motifu ya mwali aliyekataa kuolewa pia motifu ya taksiri (Achilles’ heel).
Kwa kuzingatia umuhimu wa motifu katika kazi za fasihi, aidha kwa kukusudia au bila kukusudia, waandishi wengi wa kazi za fasihi wamekuwa wakijumuisha motifu katika uandishi wa kazi zao. Motifu nyingi zinajitokeza moja kwa moja au kisitiari katika kazi hizo.
Motifu za msako na safari ni kati ya motifu zinazojitokeza kwa kiasi kikubwa sana katika kazi za fasihi. Hii inaweza ikachangiwa na ukongwe wake kama fasihi yenyewe. Kama anavyosema (Senkoro 1997:11)
Kuna ukweli wa tangu kale wa kifasihi ambao unasisitiza kuwa roho ya kazi yoyote ya kifasihi iliyo bora ni safari. Na ni kweli motifu hii ni ya kale kama fasihi yenyewe.
Motifu za safari na msako kwa kiishara zinahusiana na hatua za makuzi za wahusika katika kazi za fasihi. Kama Senkoro (1997) anavyoiangalia motifu ya safari katika mitazamo mbalimbali na mmojawapo ukiwa “safari kama ishara ya mchakato wa makuzi.”
MAREJELEO Kamusi ya Karne ya 21 (2013), Kamusi ya Kiswahili: Lnghorn Publishers, Nairob.Omari, A. A (2014), Kuchunguza Dhamira Za Kijamii na Kiutamaduni katika Riwaya ya Kiswahili: MifanoKutokaKulinaVuta N’kuvute: Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.Ponera, A.S na Luhwago N. (2015), Mwangozo wa Kozi ya Riwaya ya Kiswahili: Chuo Kikuu Cha Dodoma.Shafi, A.S (1999), Vuta N’kuvute, Mkuki na Nyota Publishers: Dar es salaam.
DHANA YA MOTIFU KATIKA RIWAYA INAVYOJADILIWA NA WATAALAMU WA KISWAHILI
Motifu ni kati ya vipengele muhimu katika uchambuzi wa kazi za kifasihi, hususani katika kuchambua vipengele vinavyojenga maudhui ya kazi hizo. Dhana ya motifu imefasiliwa na wataalamu mbalimbali. Kwa mfano: Dorson (1972) kama alivyomnukuu Thomson (1932:32) anasema motifu ni kizio kidogo thabiti kipatikanacho katika sanaa jadia, maelezo ambayo masimulizi yote yanajinasibisha nayo. Yanaweza kujikita kwa mhusika fulani ndani ya masimulizi, ndani ya matendo yaliyo katika masimulizi na mara nyingine katika hali inayojitokeza sana katika tendo lililo ndani ya usimulizi.
Thomson naye aliangalia motifu kwa kuihusisha kwa kiasi kikubwa na masimulizi ndani ya sanaa jadia. Hakuangalia motifu kwa mapana yake katika kazi zote za fasihi andishi na simulizi.
Wamitila (2003) kwa upande mwingine anasema dhana hii, motifu, hutumiwa kurejelea wazo kuu na sehemu ya dhamira katika kazi ya kifasihi. Huweza pia kutumiwa kuelezea elementi ya kimuundo au kimaudhui inayotawala kazi fulani. Anatoa mfano wa riwaya yake iitwayo Binaadamuambapo anasema safari ni motifu muhimu ya kimuundo na kimaudhui.
Umuhimu wa motifu anaouelezea Wamitila kwa kuzingatia maudhui na muundo unamaanisha kwamba, kuwapo kwa motifu ya safari katika hadithi hiyo ndiko kunakobeba muundo na maana ya hadithi. Motifu hiyo haiwezi ikaondolewa kwani itaathiri muundo na ujumbe au maana ya hadithi hiyo.
Encyclopedia the Free Dictionary (2011) inasema motifu ni kitu, jambo, wazo au muundo katika kazi ya fasihi linalojirudiarudia. Motifu ni muhimu kwa sababu inamwezesha mtu kuona mawazo makuu na dhamira anazojaribu kuzionyesha msanii ili aweze kuitafsiri kazi ya sanaa kwa ufasaha zaidi.
Mulokozi (2009) anayaendeleza mawazo ya Encyclopedia (imeshatajwa) na kusema motifu ni kipengele radidi cha kijadi/kikaida au kimaudhui kinachotumiwa na wasanii katika kazi zao ili kutoa ujumbe fulani. Mulokozi (keshatajwa) anatoa mifano ya motifu za kifasihi kuwa ni: motifu ya mama wa kambo, motifu ya safari, motifu ya msako, motifu ya mwanamke mshawishi, motifu ya bi kizee, motifu ya mzungu mweusi, motifu ya mtoto wa ajabu, motifu ya mtoto kigego, motifu ya mnyonge anayemshinda mwenye nguvu, motifu ya nunda/ zimwi mla watu, motifu ya mwali aliyekataa kuolewa pia motifu ya taksiri (Achilles’ heel).
Kwa kuzingatia umuhimu wa motifu katika kazi za fasihi, aidha kwa kukusudia au bila kukusudia, waandishi wengi wa kazi za fasihi wamekuwa wakijumuisha motifu katika uandishi wa kazi zao. Motifu nyingi zinajitokeza moja kwa moja au kisitiari katika kazi hizo.
Motifu za msako na safari ni kati ya motifu zinazojitokeza kwa kiasi kikubwa sana katika kazi za fasihi. Hii inaweza ikachangiwa na ukongwe wake kama fasihi yenyewe. Kama anavyosema (Senkoro 1997:11)
Kuna ukweli wa tangu kale wa kifasihi ambao unasisitiza kuwa roho ya kazi yoyote ya kifasihi iliyo bora ni safari. Na ni kweli motifu hii ni ya kale kama fasihi yenyewe.
Motifu za safari na msako kwa kiishara zinahusiana na hatua za makuzi za wahusika katika kazi za fasihi. Kama Senkoro (1997) anavyoiangalia motifu ya safari katika mitazamo mbalimbali na mmojawapo ukiwa “safari kama ishara ya mchakato wa makuzi.”