DHANA YA MOFU NA ALOMOFU

 
 DHANA YA MOFU NA ALOMOFU
Mofu ni umbo kietimolojia
Mofimuni maana (kabla ya kuja kwa sarufi mamboleo neno mofimu lilitumika kwa maana ya umbo na maana, dhanna hii ilianzishwa na mtaalamu wa Isimu aitwaye Noam homsky lakini baadaye ikaamuliwa kuwa Mofimu itumike kuukilia maana kwa sababu kietimolojia mofimu humaanisha maana – elementi dhahania.
Alo = zaidi ya moja (mf. Alomofu = maumbo zaidi ya moja yanayowakilisha mofimu (maana) moja kisarufi).
NB: Maana ya kietimolojia ni fasili ya neno au kitu kutoka kwenye lugha yake ya asili.
MOFU
Ni kipashio cha kimofolojia kinachosetiri mofimu (maana). Mofu ni umbo ambalo huweza kuandikwa watu wanapoandika maneno na pia huweza kutamkwa watu wanapotamka maneno. Kwa hiyo neno lolote lenye maana sharti liwe na mofu angalau moja kwa msingi kwamba maana ni elementi dhahania ambayo hubebwa na umbo fulani.
AINA ZA MOFU
Mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili ambavyo ni:
-       Maana inayobebwa na mofu na
-       Mofolojia ya mofu
  (a) Aina za mofu kwa kigezo cha maana
Kigezo hiki kina aina tatu za mofu ambazo ni mofu huru, mofu funge na mofu tata
Ø Mofu huru
Hizi ni mofu ambazo husimama kama maneno kamili yanayojitosheleza kimuundo na kitaarifa.
mf. Baba, mama, safi, Sali, kaka, n.k
Ø Mofu funge/tegemezi
Ni vijisehemu vya neno vinavyojiegemeza kwenye mzizi wa neno ili kutoa taarifa fulani. Kila kipande cha neno ni mofu funge.
mf.
Anaimba = A-na-imb-a
Tuliochezeana = Tu-li-o-chez-ean-a
Ø Mofu Tata
Hizi ni mofu ambazo zikitumiwa katika maneno huleta utata, hufanya neno liwe na maana zaidi ya moja.
Mf:
Juma aliwachezea wanangu
Katika tungo hiyo kuna utata wa kimaana ambao unabebwa na neno aliwachezea. Kimsingi utata katika neno hilo unasababishwa na kauli ya kutendea ambayo imebebwa na mofu –e- ya utendea. Maana zinazoletwa na mofu hiyo ya utendea ni kuwa ukisema Juma aliwachezea wanangu  wanaokusikiliza wanaweza kuelewa kuwa:
(i)  Juma alicheza ili kuwafurahisha watoto
(ii)                   Juma alicheza kwa niaba ya watoto
(iii)                Juma aliwaroga watoto
(iv)                 Juma aliwafanyia watoto tendo la udhalilishaji
Maana zote hizo zinaletwa na mofu – e- na hiyo ndio tunaiita mofu tata.
   (b)       Aina za mofu kwa kigezo cha mofolojia
Hapa tunapata aina mbili za mofu za mofu ambazo ni mofu changamano na mofu kapa
Ø Mofu Changamano
Mofu changamano huundwa kwa kuweka pamoja mzizi au shina zaidi ya moja ili kuunda neno moja. Katika hali ya kawaida kila moja ya mizizi hiyo huweza kusimama peke yake na kuunda neno lake.
Mf.
Mwana + nchi
Mwana + chama
Askari + kanzu
Ø Mofu Kapa
Ni maumbo ambayo hayadhihiriki kimatamshi (kifonolojia) wala kimaandishi (kiothografia) lakini athari zake zipo akilini mwa wazungumzaji. Katika maandishi mofu hizi huwakilishwa na msimbo (alama) θ. Katika Kiswahili kuna mofu kapa za umoja na za wingi.
mf. 1
           Umoja                       Wingi
         θ+sanduku               ma+sanduku
         θ+debe                     ma+debe
         θ+chungwa              ma+chungwa
mf. 2
          Umoja                        wingi
        U+nywele                    θ+nywele
        U+kucha                      θ+kucha
        U+funguo                    θ+funguo
Katika mfano wa kwanza (1) hakuna mofu za umoja lakini za wingi zipo na katika mfano wa pili (2) mofu za umoja zipo na za wingi hazipo. Kwa hiyo mtu akisema “…niletee sanduku” inajulikana ni sanduku moja na akisema, “…niletee masanduku” inajulikana ni zaidi ya moja. Hali kadhalika ukiambiwa funguo ni tofauti na ukiambiwa ufunguo. Mofu kapa huwa akilini mwa wasemaji wa lugha.
DHANA YA ALOMOFU
Alomofu ni neno ambalo linatokana na maneno mawili ambayo ni Alo na mofu yenye maana ya zaidi ya moja na umbo mtawalia. Kwa hiyo tunapozungumzia alomofu tunamaanisha maumbo zaidi ya moja au mbalimbali yenye kuwakilisha mofimu (maana) moja kisarufi.
Mfano tunapoangalia viambishi vya wakati li,na,ta maumbo yote hayo ni tofauti lakini yanawakilisha wakati. Kwa hiyo tutayaita alomofu za wakati.
Mfano
ALOMOFU ZA
WAKATI
NAFSI
UREJESHI
UKANUSHI
UTENDESHI
LI
NA
TA
NI
TU
U
M
A
WA
YE
YO
O
CHO
VYO
LO, n.k
SI
HA
HA
ISH
ESH
LISH
LESH
Z
SH, n.k
 
    
                   Jedwali la hapo juu linaonesha baadhi ya alomofu za Kiswahili kwa uchache. Kumbuka kuwa alomofu ni maumbo mbalimbali yanayowakilisha mofimu moja kisarufi.
DHANNA YA FONI, FONIMU NA ALOFONI
FONI
Ni kipashio cha kifonetiki kinachodokeza sauti za lugha kwa ujumla, yaani foni ni sauti za lugha zote. Fonetiki ni taaluma inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa sauti za lugha zote kwa ujumla wake. Fonetiki ni kama bwawa la sauti ambalo hubeba sauti za lugha zote ulimwenguni. Sauti zote zinapokuwa katika kiwango hiki cha kifonetiki huitwa foni.Fonetiki huchunguza sauti za lugha pasipo kuzihusisha na jinsi zinavyotumika katika tungo.
FONIMU
Ni kipashio cha kifonolojia kinachowakilisha sauti katika lugha mahususi kwa maana nyingine fonimu ni kitamkwa cha msingi katika lugha.
Fonolojia ni taaluma inayoshughulikia fonimu katika lugha mahususi. Kwa hiyo foni ni fonimu ikitumika katika lugha mahususi na hapa huangaliwa kimatumizi zaidi na jinsi inavyoweza kuleta badiliko la kimaana. Hii ina maana kuwa fonimu zikibadili nafasi katika neno na maana hubadilika.
Mfano:
Sabuni ---- zabuni
Samani ---- thamani
Sindano ---- shindano
 Kwa kifupi ni kuwa iwapo sauti mbili tofauti zikibadilishana nafasi na maana ikabadilika basi hizo zitakuwa fonimu mbili tofauti na ikiwa zinabadilishana nafasi na maa isibadilike hizo zitakuwa ni alofoni mbili tofauti za fonimu moja.
Mfano:
Kibiriti – kiberiti
Kichuguu – kishuguu
Katika mfano huo sauti /i/ na /e/ pia /ch/ na /sh/ hazileti athari ya kimaana na hivyo hizo ni alofoni mbili za fonimu moja.
Lugha ya Kiswahili ina fonimu thelathini (30) ambapo irabu ni tano (5) na konsonanti ni ishirini na tano (25). Hata hivyo zipo fonimu ambazo zinatumiwa katika Kiswahili ingawa hazioneshwi katika chati ya alfabeti za kimataifa. Hii hufanya idadi ya fonimu za Kiswahili kuwa zaidi ya thelethini kama inavyooelezwa kwenye vitabu vingi.
            Zingatia orodha ya fonimu za Kiswahili
Alfabeti
Kifonetiki
kiswahili
ɑ
a, ɑ
a, ɑ
b
b
b
c
c, ɔ,
ch
d
d
d
e
e,ɛ
e
f
f
f
g
g
g
h
h
h
i
i
i
j
ɟ
j
k
k
k
l
l
l
m
m,ɱ
m
n
n
n
o
O, ɔ
o
p
p
p
q
q
-
r
r
r
s
s
s
t
t
t
u
u
u
v
v
v
w
w
w
x
x
-
y
j
y
z
z
z
sh
ʃ
sh
ny
ɲ
ny
ng
ŋg
ng
ng’
ŋ
ng’
th
θ
th
dh
ð
dh
gh
ɣ
gh
kh
x
kh
fy
fy
fy
nyw
nyw
nyw
ALOFONI
Alofoni ni sauti mbalimbali za fonimu moja, kwa maneno mengine alofoni ni sauti anuai zinazojitokeza wakati wa utamkaji wa maneno mawili tofauti yanayolingana bila kubadili maana asilia ya neno hilo.
Mfano:
Chakula ------- chakura
Mtoto ---------- ntoto

Kibiriti -------- kiberiti
Kichuguu ----- kishuguu
Kama ilivyoelewa hapo awali ni kuwa alofoni hazibadili maana asilia ya neno.
Powered by Blogger.