FASIHI YA KISWAHILI, NADHARIA NA UHAKIKI (T.S.Y.M. Sengo

OSW 133 
FASIHI YA KISWAHILI, NADHARIA NA UHAKIKI (T.S.Y.M. Sengo) 
Utangulizi 
0.1 Kuna kusoma na kupata vyeti baada ya kufanikiwa katika mtihani. 
0.2 Kuna kuelimika, kwa kupitiya visomo, ujuzi na utunduwizi, tajriba za mawanda ya elimu na/au          dari za uwezo wa akili wa viwango mbalimbali. 
0.3 Ila za Msomi ni pamoja na magoda – mikogo, dharau na kedi, utovu wa adabu, ufisidi, ufisadi, hujuma, mbwembwe – ulimbwende, kushindwa au uvivu wa kutenda kazi; ugila-unyimi, inda, choyo, fitina n.n.k.h. Sifa za Mwenye elimu ni kutambuwa ujinga alionao, kwamba hajuwi kila kitu wala hajuwi anachokijuwa sana; anajitambua kuwa hayafahamu sana anayoyajuwa; tajriba – uzowefu wake ni ule wa kwao na mwahala alimopitiya – shuleni – kazini, maishani; nnje ya tajriba hizo, hana ujuzi wala fahamu. Na hata huko alikopitiya, hakumaliza yote. Mwenye elimu ana manufaa kwa nafsi yake na nafsi za viumbwa vyote vya Muumba wake. Ni katika manufaa hayo kwamba, akiajiriwa kuhudumiya watu au wanyama na ndege, hata mimeya na misitu, mtu huyo ataonekana akizitowa hizo huduma. Kinyume na Msomi, ambaye raha yake ni kuwanyanyasa hata kuwaoneya wale wanaopaswa, kwa haki zao za kimsingi kuhudumiwa nay eye awe daktari wa hospitali, Ndaki, Afisa wa shule, profesa wa Ndaki, Afisa wa jeshi n.w.k.h. Mwenye elimu ni yule aliye karibu sana na Muumba wake. Pale, Mwenyezi Mungu, Aliposema, “Kila mwenye kusubiri, yu pamoja Nami”, wenye kusubiri si wasomi – wasomi wa karatasi bali ni wasomi – alimu, wanaojifahamu na kumfahamu Mola wao. 
0.4 Mwanafunzi yeyote ni OMBWE linalohitaji ujuzi, fahamu, maarifa, kisomo au elimu, kisomo na elimu – vitu ambavyo mwalimu wake anaweza kumwongoza avipate. Mwalimu – Mwalimu ni mtu anayetarajiwa na kutakiwa (kwa mafunzo na mamlaka aliyokabidhiwa) kuwa mzazi / mlezi bora zaidi kuliko baba au mama wa kawaida wa nyumbani. Yeye ana sifa ambazo wazazi walezi wenziwe wasiokuwa walimu, hawana. Mwalimu mzuri ni sawa na mtu mzima anayekabidhiwa mtoto mdogo wa jirani ampeleke kwao ambako mtu mzima huyo amekiri anakujuwa. Mwalimu anayempokeya mtoto wa darasa la kwanza hadi la saba na kufeli mtihani huwo wa darasa la SABA au wa KIDATO CHA NNE, SITA au wa Mwaka wa Mwisho Ndakini, ni sawa na mtu mzima huyo aliyeshindwa kumfikisha mtoto aliyekabidhiwa kwenda naye kwao. Mwalimu – si lazima awe anajuwa na kufahamu mengi kuliko mwanafunzi wake. Kwa kawaida, mwanafunzi anatarajiya apate mapya mazuri mengi kutoka kwa Mwalimu wake. Njiya za mwalimu ni zile za kiutu, zinazokubalika na kupendwa na jamii. Shaaban Robert, katika Utenzi wa Mapenzi Bora , anahimiza upendo wa huruma za kufanikishiyana haja na mahitaji. Mwanafunzi aelekezwe, ahimizwe, aongozwe kwa upole na faraja hadi apate alimasi ya elimu ambayo mwalimu wake kaihifadhi katika OMBWE lake linaloaminika kwamba limejaa wakati wote. Uwalimu ni kazi ya wito. Asiyekuwa tayari, hajaitwa, asiingiye na aliyemo, ajitowe. Ni ulezi wa mapenzi makubwa ya kidaktari thieta au leba. Ni uundaji wa jamii mpya ya watu wenye uwezo mkubwa zaidi wa akili, hekima na busara.
Ni wito unaomfanya mtu afikiye kutamani kifo kama anashindwa kumrekebisha mtoto – mbaya kuwa mzuri, mvivu kuwa mchapakazi, fisidi – kuwacha wizi na hujuma, hasidi kuwacha hasada, inda na choyo, mchawi kuwacha kuroga, fatani kuwacha fitina, na fisadi kuwacha ulevi na umalaya. 1.0 Somo la Fasihi Hapa Tanzania, lilianza rasmi miyaka ya Sabini Chuwo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika Mulika na Kiswahili za mwanzo mwanzo, za Chuwo cha Uchunguzi wa Kiswahili – baadaye – Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (na leo hii, ni Taasisi ya Taaluma za Kiswahili), makala yaliandikwa yakijadili jina la somo hilo, liwe Adabu – kisawe cha Kiarabu, ama Fasihi – nacho piya Kiarabu kinachogusa Ufasaha (Ubora) wa Lugha. Kina Sengo na John Ramadhani, B. Matteru n.w. (1973) walishinda kwa hoja za kulikubali neno Fasihi kuwa kiashiriya cha dhanna ya Fasihi ambayo ni kongwe ndani ya kila jamii ya watu. Jamii zote za Tanzania, Afrika yote na Ulimwenguni kote, kila watu walikuwa na fasihi yao, ikielezwa kwa lugha zao. (Sengo : 2009) 1.1 Kwa miyaka kadhaa, neno hilo lililazimishwa kuashiriya neno/dhanna ya Literature ya Kizungu. Kitabu chetu cha Mwanzo cha Fasihi ya Kiswahili, Nadharia na Uhakiki (M. Mulokozi 1996) ni kielezeya kizuri cha kasumba ya kuiga ya “Bwana”. Hata hivyo, kila lenye mwando halikosi n’ta. Fikira mpya zikazuka na kuhimizwa (Sengo, 2009; Mwazembe, 2012), kwamba, wasomi wa Kiafrika, warudi makwao, kujifunza yote ambayo waliyakosa katika mbiyo zao za kukimbiza YES na NO na kuikosa MIZUNGU ya kikwao. Fikira za kujitambuwa na kujikiri kwamba na wao ni watu ni mafanikiyo makubwa sana. Sengo, alipoulizwa na mtu mwenziwe mmoja, akiwa nchini kumoja, Ulaya, “jee, ni kweli kwamba Afrika kuna manyani weusi wengi?” jawabu, “ni kweli, kama walivyo manyani weupe wengi huku 
Ulaya”. Mzungu alichukizwa na jibu hilo. Fasihi inatuimarisha kuwa na ujasiri wa kujiamini na uwezo wa kugunduwa dharau na kedi. Kama Ngulumbili anaonekana Nyani (mwenye miguu mine) basi iwe hivyo, kila alipo, Afrika, Marikani, Ulaya, Mashariki ya mbali, kote duniyani. Laa sivyo mtu ni mtu bila ya kujali rangi, urefu wa puwa yake, nywele n.k. Mtu anaukosa utu wake anapoanza kupoteza baadhi ya sifa zake za kimsingi ambazo zinajumuisha haya na aibu, upendo na huruma, mbeko na adabu njema, utenzi wa kazi, wema na takrima n.m. 1.2 Fasihi kwa Kiswahili Fasihi kwa (Literature in…) Wachina wameshachapisha riwaya mbili tatu kwa lugha ya Kiswahili. Riwaya hizo bado ni riwaya za Fasihi ya Kichina lakini zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahii. Wanafunzi msidanganywe wala kudanganyika kwamba Methali za Kikwere au za Kikerewe, za Kibena au za Kihehe, ati zikiandikwa kwa Kiswahili, ni za fasihi ya Kiswahili. Huwo ni uzushi na usomi wa elimu, hauruhusu urongo ama uhadazi. Utambulishi wa mtu kuzungumza lugha A, B, C… haupo. Kama hivyo ndivyo, hata chawa, kunguni, nyau, m-mbwa wanaofugwa na Wakwere, kwa kukielewa Kikwere, na wao waitwe Wakwere. Wajamaika walioko Uingereza kwa miyaka na karne, hawajakubalika kuwa ni Waingereza. Utambulishi ni jumla ya jiografiya, mapisi, biyolojiya, jadi, utamaduni, mila (hasa za chakula), desturi (hasa za mavazi na mbeko), lugha, fasihi n.m.) Elimu inahimiza kweli. Inalinda haki. Inaleya upendo na huruma. Itoshe, kwa wanafunzi wangu, kwamba Waswahili (Watu wa Sahel – Sahil – Pwani – Mwambao wa Afrika ya Mashariki) ni jumuiya kubwa zaidi kuliko watu wa makabila mengine ya Kenya na Tanzania. Uswahili ni mpana zaidi.
Mfano wao ni Wasomali, ambao Somalia ndiko kwao, lakini wamesambaa Kenya, Uganda na Tanzania, kwa idadi kubwa. Mfano mwingine ni Wachagga ambao wakifuwatwa Moshi (Kilimanjaro) hawapatikani ila Wakibosho, WaMarangu, Warombo, Wa-Machame au WaUru na kina Wa – Oldi Moshi. Waswahili ni Waafrika wenye damu nyingi zilizochanganyikana mno zaidi kuliko damu za Wazaramu na Wakwere (ambazo ndizo hizo hizo za Wahehe, Wabena, Waluguru, Wakami, Wanguu, Waziguwa, Wabondei (Waziguwa wa Bondeni – kwenye mboji), Wasambaa (Waziguwa waliohamahama kutafuta maisha). Wao (Waswahili), kama wengine, wana eneo lao, jadi zao, vyakula vyao (vya Bahari ya Hindi – tafauti ya nyama za Sokwe, Manyani, Ngedere za Misitu ya Kongo). Hivyo, wao ndiwo wenyewe wa lugha ya Kiswahili kama Sengo na Kikami, Kiluguru mama, Kinguu, Kiziguwa, Kizaramu na nyengine za Jimbo la Mashariki la Kikoloni. Siku hizi, kuna watu wanaoneya haya makwao. Wanajiita kwa majina ya Wilaya zao; WaKigoma, WaKasulu WaMbozi na wapo wanaojiita WaCCM, Wa Chadema, Wa CUF. Ubaya au uhasi wa kabila si kabila (na msidhani twamsema Kabila, Mheshimiwa Raisi wa Kongo, la hasha). Uhasi wa Kabila ni UKABILA, kwani ukabila ni ushenzi, ni umimi uliyokithiri. Ila hii ikiwemo mwa jamii yeyote – ya umimi wa mtu asiyemtambuwa mtu mwenziwe kuwa yu mtu kama yeye. Wasiotaka UKWERE waliukimbiya hadi alipopatikana Rais Mkwere – Tebe Jakaya Mrisho Khalfani (– Tati ya Tebe –) Mrisho - (Mmindu wa kudibuko –) Kikwete. Wanapoukimbiyua Uhaya (Kama alivyojaribu M. Mulokozi), Upogoro, Uluguru, Unyaturu n.w; tuwaulize; kwani huwo Unyaturu wasioutaka leo (ati kwa kuwa wana PhD) ni wao? Wao wamejikuta tu, wamezawa katika hizo koo na makabila ya watu. Jee, wataweza kuwa kenge hali wao ni machatu? Mnyaturu mjanja, mwenye PhD ya Uhandisi au Msung’hiza wa Magu mwenye PhD ya Bayo – Kemiya, bila ya kusoma Kiswahili, atake kuwa mwalimu wa Mwalimu wa walimu wa lugha hiyo! Jeuri, ya nini? Chuki, za nini? 
Kwa jeuri ipi? Chuki, inda, hasada, Uchawi, urogi, ubaya wa ;roho ubunye na uhenye! Waswahili waachiwe lugha yao wailee na wafundishe sisi wengine sote, tunaotaka tuijuwe kama yalivyo maarifa yetu ya good – better – best; badala ya good; doodier – goodiest; ama bad – worse – worst; badala ya bad - baddier – baddiest. Mbona kwenye lugha hii hatujitii vitanzi shingoni? Fasihi kwa Kiswahili ni yoyote, ya wowote, iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili; kama ilivyo ya African Writers Series (Literature in English). Kina Soyinka, wanaoandika kuwashinda Waingereza wenyewe, bado ni Waafrika wa Nigeria na fasihi wanayoiandikiya ni ya Kiafrika iliyoandikwa kwa Kiingereza. Msitu ni Msitu, miti inapomeya kwa wingi na pamoja lakini kila mti ni mti kwa kabila yake. Ajabu, hakuna mti unaojikana – Mpapai kutaka uwe Mpingo, au Mbuyu kuwa Mkwayu (Kilemela – N’hembo). Kamwe, miti haidharauliyani, hairogani lakini watu; Mvyele wa Kizigula, amroga kakiye, Mgosingwa wa Kizigula! Kirozo! 1.3 Chanzo cha fasihi ya jamii ya watu kisitafutwe nnje ya watu wa jamii hilyo. Katika kuifafanuwa dhanna ya Fasihi, mfafanuzi anapaswa kuanza na Mazingira – eneo la kijiografiya – ambamo ndimo mwao, watu wa jamii hiyo. Mazingira ni mengi; ya jangwa , ya theluji, ya pwani, ya bara, ya biyashara, ya dini , n.k. Kila watu na / au binadamu, wana yao. Jamii ni kielezeya au sifa nyingine. Jamii hiyo ya watu – mashine, watu watu (kwa maumbile ya kuonekana) au watu – binadamu (kwa adabu, heshima, huruma n.k.). Sifa hii ni ya msingi sana katika kuitendeya haki Fasihi ya watu hao. Mfano, maelezo ya Aristotle, kwa wakati wake, yalihusu fasihi aliyoijuwa yeye, ya huko kwao au ya majirani zake. Pamoja na ukweli kwamba kufanana kuko, inabaki pale pale kuwa hata mapacha wawili, Kurwa ni Kurwa na Doto ni Doto, Hassani na Hussein, Salim na Salima n.m.m.k.h. Hadi vikombe vya chai vinavyotumika pahala pa chai, kila mwenye nacho, anasema ni kikombe chake.
Mawazo yaliyopata kutajwa na kulalamikiwa, ni pamoja na kutajwa Chanzo cha cha vyote ambacho, kwa binadamu wanaokiri kuumbwa na Muumba Mmoja na Pekee, hawathubutu kukikanusha chanzo hicho. Ili kumtendeya haki Mwenyezi Mungu, yake yangeachwa Kwake, kwa vile ujuzi na mafuhumu ya hayo ni Yake Yeye Mwenyewe. Fasihi ni ya watu. Maumbile au Maumbizi ni ya Mwenyezi Mungu. Haya yasichanganywe. Katika Ujinga mzito wa mja ni kutokujijuwa na kutokumfahamu Mwenyezi Mungu Aliyemuumba na kuumba wote na vyote. Akishiba na kuvuta pumzi za Muumba wake, huthubutu kunena kuwa, kuwako kwa Mwenyezi Mungu, hakuna ithibati. Hajiulizi mja huyo, yeye katoka wapi kabla hajajiona alipo na alivyo. Msomi asiyeujuwa na kuufahamu uhai, tena uhai wake na wa watu wa kizazi chake, kifalsafa, si mtu wa kuhojiyana naye, kwa kuwa hana hoja na asiye na hoja si msomi. Akiwa, hana elimu. Ana karatasi tu. Waliopata kutaja sihiri (uchawi) kuwa ni Chanzo kimojawapo cha dhanna ya fasihi (Mulokozi :” 1996) tusiwabishiye kwa kuwa ubishi si kiwango chanya cha usomi. Uchawi ni sehemu ya mila na desturi za jamii nyingi duniyani. Katika maisha ya Mbale (Uganda) ya mzee Sengo, kwa miyaka mitano, neno uchawi lilikuwa na maana zaidi ya uganga, kuliko ya ukatili wa kudhuru, kuroga, kumwombeya mwema mabaya n.m.k.h. Maneno ya kiuchawi, k.v. nyimbo, methali, semi, maapizo n.k. yanaweza kusemwa ni ya kifasihi kama yana sifa au vielezeya vya uteuzi wa kusadifu ishara za kifasihi. Uchawi kama uchawi, tambiko kama tambiko, kazi kama kazi, muziki wa ala, ngoma kama ngoma na mifano ya sanaatendezi kama hizo, bila ya maneno mateule ya kifasihi, haziwi fani au tanzu za fasihi. Zishughulikiwe na wasomi wa utamaduni, mila na desturi, wasomi wa ujamii (sosholojiya), wanaushunuzi (wanasikolojiya, wachawi wenyewe kwa uchawi wao na muziki na ngoma ni kwa wanamuziki. Sona ambazo, aghalabu huwambatana na ngoma ni za wanasanaajadiiya waliokhitimu taalimu hiyo kwenye Idara za Sanaajadiiya na sanaa za Jadi, si mtu tu kujiita hivyo kwa kuwa kakhitimu shahada ya Fasihi – Simulizi.
Wigo ni chanzo au chimbuko jengine linalotajwa, hasa kwa baadhi ya nchi za Ulaya. Kuiga mazuri ni tabiya nzuri. Kila mwenye uwezo mzuri wa akili, huiga mema na mazuri. Si kila kiigwacho ni fasihi. Kufanana, piya si kuiga. Mfano, methali za “A friend in need is a friend indeed”; Rafiki katika dhiki ndiye rafiki wa kweli” zinafanana kutokana na umoja wa hisiya za kimaumbille; hakuna mmoja aliyemrudufu mwenziwe. Katika lugha nyingi, za jamii nyingi duniyani, methali zenye ujumbe huu zinakutikana. Ni suala la ubinadamu mmoja wa Muumba Mmoja Aliyemuumba mja kwa jumbo moja lakini kwa rangi, vimo, nywele, tabiya na hulka tafauti. Katika somo letu hili kuiga mazuri, kwaweza kusemwa ni moja ya dhima nzuri za fasihi na za ustaarabu au uungwana. Mzoweya kusota, akiiga kuchamba kwa maji, kisha akanawa kwa sabuni, atakuwa ameiga jema, linalomtowa ushenzini, likamtiya uungwanini. Juhudi za mja za kuyadhibiti mazingira yake ya kimaumbile ili aweze kuishi akijikimu kisitahiki. Wazo hili huonekana ni jipya, tena la Marx (Mulokozi; k.h.j) kwa usomi usiyo kina kama ambavyo ulimbe (sayansi) au utunduizi (tekinolojiya), yanavyoonekana vitu vipya sana na sharti vitoke kwa wenye lugha hiyo ya “Science and Technology”, hali huko huko, mabenki na viwanda vinavyofungwa, watu hawana ajira, na baya zaidi, hata ubinadamu wao unaelekeya kwenye umashineshine zaidi. mwanafunzi wangu wa fasihi asiishiye kusoma na kumrudufu, haya kasema fulani – sawa; lakini Nani? Lini? Wapi? Kawasemeya kina nani? Vipi? Kwa hoja na sababu zipi? Mawazo ya mtu au watu ni ya mtu au ni kwa hao watu. Yaliwafaa kidogo au sana kwa muda mfupi au mrefu. Yetu, hayo yaonwe kivyetu, huku kwetu. Yasiyotufaa, ni yao na sisi tushike yetu. 
2.0 Fasihi ya Kiswahili na Fasihi kwa Kiswahili Mfano wa “English Literature” na Literature in English”. Fasihi ni dhanna. Ina sifa au vielezeya vyake. Fasihi ya Kiswahili nayo ni dhanna. Kama zilivyo, Fasihi ya Kigogo, Fasihi ya Kikwere, Fasihi ya Kichina, Fasihi ya Kiarabu, Fasihi ya Kikerewe n.n.k.h. Utambulishi wa zote hizo ni kule kwao kwa kila Fasihi ya jamii ya watu. Ni kwenye eneo lao la kijiografiya – mazingira wanamoishi watu hao (Watu hawaishi uwandani – mwahala, mfano wa jangwa, msimomeya chochote n.k.) Jamii ipi? Jamii ya Waswahili / Wapwani – Wamwambao wa Afrika Mashariki – masafa mafupi (km. kadhaa) kutoka ufukweni mwa Bahari ya Hindi, kaskazini – Kisimayuu (cha juu), Kusini mwa Somalia na kusini ni Sofala ya Msumbiji ya siku hizo, kwa sasa tuseme, Pemba ya leo ya Msumbiji. Jamii hii ina jadi tatanishi – nyingi zilizochanganyika kwa karne nyingi. Si kila Wamwambao ni Waswahili. Saudia ina pwani. India, kadhalika, Libya, Iran, Nigeria hata Kongo, Msumbiji na Afrika ya Kusini. Pwani zao si za Waswahili na Kiswahili chao. Ni shani yake Muumba, Aliyezusha jamii na lugha. Kila watu wana nyumba, ndimi zao si vilugha. Kila jamii yatamba, kwa sarufi na balagha. Hili halina kufumba, neno sahihi ni lugha. Mazingira yana umuhimiu wake. Jamii nayo hupambika kwa ujumi wa mazingira hayo ambayo ni muunganiko wa ardhi, biyolojiya, kemiya, fizikiya, fiziyolojiya, akiyolojiya, ushunuzi na ujamii wa watu hao. Utambulishi, kwa uwezo wa mboni na macho, ndiyo unaowasafirisha watu kutoka makwao, kwenda kwengineko, kutafuta wake au waume. Hii ni mipango mikubwa zaidi ya kiumbizi kuliko ile ya juhudi za mtu. Yu wapi Marx? Yu wapi Nietsche? Yu wapi A? B? C? D na E? Wako wapi waliojiita miungu na kumkana Mungu Mmoja wa kweli? 
Kutokana na macho na mboni kuona na kuishi ndani ya tajriba ya ujumi wa jamii (mazingira) fulani, watu wa jadi hiyo, hujitokeza na uwezo wa kubuni na kusana sanaa za watu hao. Kwa hiyo, fasihi inaongezewa vielezeya (sifa) vya ubunifu na usanii au sanaa. Uweledi huu ukipanda daraja, huwa ni taaluma au taalimu maalumu ya maneno mateule ya hao watu maalumu wa hiyo jamii maalumu wa hayo mazingira maalumu. (Sengo : 2009). Taalimu ni ukweli. Hawi wala hakubaliki msomi mwenye PhD ya kilimo lakini hajuwi na hawezi kutafautisha njegere, mbaazi, kunde, fiwi, kikwila, choroko na dengu. Ama mhandisi asiyetambuwa uhandisi wa Maji Machafu (siyo maji-taka) au anayejiita mwanalughawiya anayemkanusha profesa wake aliyekhitimisha wanalughawiya kadhaa kwa kiwango cha PhD – akamsema si mwanalughawiya kwa msingi wa chuki binafsi na udini wa ujinga aliyodanganywa nao. Ukweli wa kitaalimu (kitaaluma) hupatikana kwa utafiti. Hapo zamani, tulisomeshwa ATOM kuwa, “the smallest particle”, kwenye somo la KIMIYA. Leo, baada ya utafiti wa kina, inasomeshwa PROTON kuwa ndiyo, “the smallest particle”. Utafiti unaendeleya. Kwenye Kiswahili, matamshi ya lugha za Kiafrika yameanza kuchukuwa nafasi yake. Waamerika wakiandika COLOR na Waingereza, wakaandika Kiingereza chao COLOUR kwa maana ya RANGI, Waswahili halisi, hawatamki KUSIKI – A bila ya Y kusikika. Paka, hajisemi Nyani, ati kwa kuwa na yeye anaweza kupanda na kudatiya miti. Nadhariya ya MAZOWEYA, tumeshaisemeya. Kusota ni kiwango hasi cha Ustaarabu. Kuchamba kwa maji masafi na kunawa kwa sabuni ni uchanya wa Uungwana wa watu. Wasomi (wenye elimu) wanadhaniwa ni waungwana. Wanapobakiya kwenye uroho, ugila unyimi, choyo – inda, fitina na majungu au wakiendeleya kusota, hao ndiwo waitwao “washomile” wakosa urombo. Wasiseme, wanatukanwa kwaNI fasihi ya methali inatukumbusha kuwa, “akutukanae hakuchagulii tusi” na hilo “tusi ni sawa na maji ya kuchemka juu ya nyasi”. Matusi ni kicheko na “Mchekwa uyo mwana – Mwenye kuchekwa – kutukanwa – kuonywa – ndiye awaye mrombo – mtu wa kisawasawa.

2.1 Fasili ya Dhima 

Neno dhima, linatumika Uswahilini kwa maana yafuwatayo; 2.1.1. Dhima ni Wajibu. Ni wajibu wa somo la fasihi kuieleza au kuifasili na kuifasiri dhanNa ya jadi – utamaduni – mila – desturi – sanaajadiIya – lugha na fasihi n.m.k.h. – kuielezeya kwa kina kirefu na mawanda mapana ili maarifa hayo yamwezeshE mwanakikowa hicho amudu kuyaishi maisha ya humo mwao, mifano ya humo mwao na kwengine kokote kwenye waja wenziwe. Wajibu wa fasihi ni huruma na upendo (nnje ya chuki au upendeleo) wa kweli, wa kuiliEya jamii. Kuleya ni kusema kweli, kuhimiza na kutenda mema na mazuri, kukemeya na kuwacha maasi, maovu na mabaya. 2.1.2. Dhima ni kazi. Kusema, fasihi ina kazi fulani kunasemwa tu lakini tafsiri yake ya kina ina utatanishi. Kazi hutowa matokeo. Matokeo ya fasihi hayajidhihirishi kama kupasuwa kuni au kuchemsha mayungu – mamung’unye. Kifalsafa, fasihi hueleza mambo kwa mifano na hoja za hija lakini haitowi majawabu juu ya uhakiki wa kuishi. 2.1.3. Dhima ni Jukumu. Hakuna neno la MAJUKUMU lwenye lugha fasaha ya asili ya Kiswahili. Jukuu nalo ni hali ya mbabaiko mkubwa ambao mja atakuwa nao siku atakayomkabili Mola wake akijiteteya dhidi ya dhambi alizozitenda uhaini mwake. Si kisawe cha dhima wala cha wajibu. Wanafunzi wanaojifunza Kiswahili na fasihi kwa mzee Sengo, Gwiji la Kiswahili nchini Tanzania na Gwiji nambari mbili, Uswahilini, hawatakiwi kulitumiya neno hilo popote na wakati wonwote.
Nje ya matumizi ya kifasihi, kuna baadhi ya walimu wa Uwisilamu, wanalitumiya neno CHUMA badala ya neno JUKUMU, kama visawe. Usahihi wa mambo ni Jukumu ndilo accountability for failure to perform mbele ya Muumba Siku ya Siku – siku ya Watenzi Wote, Siku ya Hesabu – Siku ya Dini – Siku ya Qiyama. Anayesubiri kuona Ukweli siku hiuyo, atauwona. Atakiona, Atajuta majuto ya Firauni, hatasaidiwa, hatahurumiwa, hatasamehewa. Mkiulizwa, dhima ya fasihi, ya shairi, utenzi, wajiwaji, natiki ya Mashetani, riwaya ya Nyota ya Rehema au ya kitabu chote cha Diwani ya Mazigazi au ya Diwani ya Macho Mabovu au ya Diwani ya Macho Mapya (za mzee Sengo Muonelwa Muhonelwa); msikimbiliye nyimbo za fasihi inafundisha, inaadhibu, inaadilisha, inaonya, inahimiza, inahifadhi n,k. Hizi ni nyimbo za kitoto. Mtoto aliyenyimwa kitumbuwa na mamaake aliyembeba mgongoni, akiambiwa; bandagala ng’nyo, atatii, kwa kuwa hajuwi linaloendeleya. Akitii, mamaake ataipata faragha ya kukimung’unyuwa hicho kitumbuwa hadi akimalize. Mama, hula kwa mtindo huwo ili apate nyonyo ya mwanawe. Mtoto, mwenye kuleta kero, hukerezwa ili ajifiche anyamaze. Haki za watoto zisizo na mbeko si haki, ni deko na kero, uhenye na ubunye, hautoshi kuitwa ubozi au uhezi. Aristotole (1958), huko kwao, kwa wakati wake, wanafasihi wake waliandika kazi zilizojitokeza kuburudisha wasomaji, kujenga tabiya njema za jamii (Sengo: fc), kustarehesha, kusisimuwa hisiya za mwili na za kiakili. Waliomfuwata Aristotle, waliifasili dhima ya fasihi kuwa ni : (i) Kuelimisha (ii) Kuhifadhili amali za jamii (iii) Kudhihirisha kweli za jamii 
(iv) Kuimarisha lugha na (v) Kujenga Umoja wa kitaifa na ukomavu wa kisiyasa. (vi) Fasihi na Uchumi na Biashara. (vii) Fasihi, Falsafa na utamaduni wa jamii (viii) Fasihi na fasili yenyewe (ix) Dhima inasawiri uhalisiya wa kitu, jambo, hali , mtu au jamii. Dhamira ya Mapenzi (i) Kuna daraja kadhaa, mapenzi kwa mahaba yapo yasiyotufaa, yasiyojaza kibaba. Mwili na mwili balaa, hayo ni ya makahaba wengi wako kwenye Baa, hawajuwi la kushiba, mapenzi bora kifaa, huruma siri ya huba. (a) Inaarifu kuwa daraja za mapenzi ziko nyingi. (b) Kwamba mapenzi ya kweli ni yenye manufaa, na ya hadaa, ambayo hayajazi hata kibaba. (c) Mapenzi ya mwili na mwili ni ya balaa, yanawafaa makahaba, ambao huuziyana maradhi, dhambi na laana. (d) Huruma ndiyo siri ya mapenzi, wapendanao, huhurumiyana na kuondesheyana magumu, matatizo na mazito. (ii) Hadithi ya Mke Mjanja na Mume Bwege iliyoishiya kwa watoto kuhemewa na shida, dhiki na machungu mbalimbali, mke kukatwa matako, maziwa na masikiyo, na mume, kutiwa ndani kwa jaribiyo la kuuwa. Dhima ya hadithi fupi hii ya Sengo (2012) ni kutowa nadhari au hadhari (siyo angalizo, kuhusu wendani-wanandowa, mume na mkewe, wawe macho na maisha yao ya ndowa, ambayo yanahitaji mapenzi makubwa na mazito, ya kina na ya kweli. Ndowa yataka uwaminifu, kutosheka kwa nafsi na kukiri uzito wa maneno yasemwayo na methali ya Kiswahili (Makame : 2013), ukishakula 
Nanasi, si basi, tunda jengine la nini? Mzee Sengo, anashadidiya, kwa Nadhariya yake; “Mwili wa mja, usiposhibishwa kikamilifu, hausikii aya wala nasaha.” (2013) Chakula kisipowatosheleza wanandowa, si ajabu, wakakutwa wakila kwa babalishe, na kwa mamalishe. Vijana, siku hizi wanaowana kwenye mitandao. Mtoto wa mzee Ibrahimu Raha (Mzee Jongo maruhumu) alianguka siku ya ndowa, Bwana Harusi aliporukiwa na Bibi Harusi Shetani, naye alianguka na kuzimiya, kwa kukhofu na kuingiwa na woga mkubwa. Wazee walimuonya sana asiowe picha za kutoka kwenye “Face – book” lakini jibu ni kuwa, “Madingi”, hawana wajuwalo. Ndowa hiyo iliishiya kwenye khasara za kuwa mchumba kivuli, khasara za kuharibika ndowa na kuvunjika kwa harusi. Ndowa ni jambo zito sana. Maisha halisi na kamili hayapo ila ndani ya ndowa. Asiyeowa ama kuolewa, huwa amepungukiwa sana na uwezo wake wa kufikiri na kutenda. Profesa mzee, ambaye hajaowa maisha yake ingawa alijulikana kwa kubebesa wake za watu, alisikika akiropoka hadharani kuwa, mbuzi si mnyama, ni ndege. Kwa hiyo, ni wazi kwamba, DHIMA ni dhanna nzito. Kama ni kuelimisha, kuelimisha nini, nani, lini, wapi, vipi na sababu ni zipi. Fasihi inatenda kazi zake kutokana na tanzu zake. Sharti mwanafasihi azisome kazi kadhaa, nyingi sana za fasihi – tanzu mbalimbali. Wasomwe waandishi wa riwaya na riwaya zao. E. Kezilahabi na G. Ruhumbika ni mfano mzuri wa waandishi walioandika riwaya zao, nyingi za Kikerewe, kwa mtindo wa Kikerewe lakini kwa maneno ya Kiswahili. Sengo naye, katika baadhi ya kazi zake, huonekana akifikiri zaidi kwa Kikwere na Kiziguwa, kabla hajayapata maneno ya Kiswahili. Dhima hupatikana katika dhamira ya kazi ya fasihi fulani kutokana na hali halisi ya mazingira. Dhamiri si dhamira. 
Mwandishi au Mtunzi wa kazi ya fasihi hakusudii kutowa dhamira kadhaa ndani ya kazi yake. Yeye, hujikuta ana kero na halitoki ila kwa kuandika riwaya, natiki au kutunga tungo za kishairi. Ni mwanafasihi mkhitimu mzuri ndiye awezaye kuzipata hizo dhima za kila dhamira kwa upana na uzito wake. 3.0 Aina za Fasihi Hapa panakusudiwa kutajwa Fasihi Andishi ambayo isingepatikana thama na Fasihi - Simulizi. Hii ya pili nayo inagawanywa. Ipo Fasihi – Simulizi ya maneno matupu ya kusemw, kusimuliwa au kuimbwa. Mfano ni; Utambaji wa simo-hadithi, semi, mithali, nyimbo, vitendawili n.m.k.h. Aina ya tatu ni Fasihi – tendezi au Shirikishi. Mifano ni; Ngoma (chombo) inapigwa, ala za muziki zinapopigwa (siyo kuchezwa), kauli za kwenye tambiko au tiba – ugangani. Hii ni Fasihi Simulizi kwa vile inavyowashirikisha hadhira, kwa kuvutika kuyatamka kwa pamoja yanayosemwa; mf. Mizimu nailale, Nailale; Kama alalavyo Fungo; kama alalavyo Fungo. Wachawi nawafe, nawafe. Mulungu (Mungu Kauko; Kaukio. Yuko. Kwenye Sona (Sherehe ya Ngoma – Uluguruni – Ukamini – Ukwereni – Uzaramuni – Uziguwani – Ubondeini – Usambaani) nyimbo huimbwa kuiarifu jamii mambo yaliyotokeya ndani ya mwaka mzima – Mlao hadi Mlao – Mavuno hadi Mavuno; maovu hukemewa k.m. “Wewe, u shemeji yangu, mbona kunishika ziwa? Huimbwa ili kuonya, kitendo hicho kisifanywe tena. Wavivu huonywa, watovu wa adabu waache mabaya, wavivu waache uvivu, wafanye kazi kwa bidii kwani kazi ndiyo ibada kubwa ndani ya maisha ya mja. Fasihi Simulizi ya maneno, mfano wa paukwa pakawa, fanani na hadhira ni kitu kimoja. Mtambaji anapotamba hadithi yake huwa hafanyi kigeni ambacho hadhira hawakijuwi. Akikoseya au kusahau, mmoja wa hadhira, atamnyoosha kwa namna ambayo itaonekana ni sehemu ya kawaida ya mwendelozo wa utambaji hadithi. Penye kuimba, mwimbo au nyimbo huimbwa kwa pamoja.
Panaposemwa, hapo zamani za kale, hiyo “zamani”, yaweza kuwa ni kipindi chochote cha nyuma kidogo au cha nyuma sana, kabla ya kutambwa hiyo hadithi. Mapisi hutiya uzito wa tajriba, uzowefu wa mambo na majambo, umri, hadhi na taadhima. Fasihi Simulizi ya jadi za kina Bibi, Babu, Hadhira kwa nyakati za jiyoni, kwenye vioto vya moto n.k. ni zile zile, kwa siku za sasa, kwenye kumbi za umeme, madarasa ya shule na vyuwo, vituwo vya mwengoya (radio) na runinga (televisheni). Mashirika ya mitandao ya kisasa haina sababu ya kuingiza “programu za CD au filamu” za wenda-uchi na kuzionesha kwa watu wenye mwiko huwo. Uwalimu mzuri ni kufundisha lililo jema na zuri kwa jamii kwa namna ambayo jamii inaridhiya. Fasihi Simulizi hizi mbili; za maneno na za vitendo, hata zikiandikwa, hubakiya vivyo hivyo na sifa zake hizo. Uhariri usifanywe na mjinga asiyeijuwa lugha na undani wa hiyo hadithi. Mhariri, k.m., wa hadithi – tambwa, ni Mtambaji mwenyewe. Hata hadhira inayomsikiliza, mmoja akivunja mwiko na kujipa uhodari wa kuihariri, hiyo yake itakuw ncha mpya ya hadithi hiyo. Uwasili wa madhumuni na wa fani ndiyo utajiri wa sanaa ya hadithi na utambaji wake. 4.0 Falsafa ya Fasihi 4.1 Falsafa ni nini? Falsafa ni elimu kongwe, nzito, mama wa elimu zote, iliyojishughulisha na inayojitahidi kuuliza maswali mazito, kukereza mbong, hulimiza majadiliyano mazito, aghalabu ni majadiliyano yasiyo na mwisho wala majawabu. Kwa mfano, swali la, “Unajuwa nini?” Hicho NINI anachokijuwa mtu ni kipi? Cha wapi? Cha lini? Kipi – kwa vipi? Kipi – kwa nini? Mtu akisema, anamjuwa mama yake; kila mtu ana wake. 
“Mama” ni dhanna ya jamii, iko wazi, inaelezeka kwa sifa au vielezeya vyake. “Mama yake” ni dhanna binafsi, haiku wazi, si mama wala wa kila mtu. Mama akiitwa “Mother” kwa Kiingereza) au Ummi (kwa Kiarabu, utatanishi utaongezeka kwa sababu kina mama hao ni wamoja kwa umbile lakini si wamoja kwa mengi mengine. 4.2 Dhanna ya Dhanna Dhanna ni nini? Dhanna Q ni ile ambayo. Sifa za Q zikikamilika katika kuitambulisha, Q huwa Q katika mazingira ya lugha hiyo daima dumu. 4.2.1 Mfano; Dhanna ya Mungu; Chanzo kisicho chanzo. Chenyewe ni Chanzo, na ni Mwisho. Hakikuzawa. Hakizai. Ki Hai milele. Kipweke. Kinajitegemeya. Hakitegemei chochote. Hakina Umbo. Kina uwezo wote. Kinaona vyote na yote. Kinasikiya yote. Wenye kukiamini Chanzo hicho kikali na kinachojuwa na kuweza yote, wanakiita “Mwenyeza Mungu Mmoja” si yule mungu mwenye miungu yenziwe ya Monday thm Sunday au January the December na wengine kama wale; mungu wa vita, wa njaa (famine), wa mapenzi (ngono)n.w. Huyo Mwenyezi Mungu ana fakhari ya KUOMBWA na kuyajibu MAOMBI hayo kwa kuwapa waja wao wayatakayo. Mwenyezi Mungu Muumba huyo ni Mwanaume asiye na hadaa za kiume zinazojulikana na waja, Yeye si muowaji; HAOWI, HAZAI, hayo yote hayamuhusu. Ila na UJEURI NA KIBURI, Kwake ni Sifa, na ni Zake Yeye tu. Imani ya kweli, Ibada za kweli, khofu na woga wa kweli vyote vinamuhusu Mwenyezi Mungu Mmoja Muumba – Mfalme wa Ulimwengu na Mfalme wa Siku ya Qiyama na Ndiye Pekee Mfalme wa Pepo na Moto huko Akhera. Sifa zake hazimaliziki hata kama miti yote duniyani KALAMU na majimaji yote Ulimwenguni, yangekuwa WINO, zisingeandikika zikamaliza. 

4.2.2 Dhanna ya Fasihi 

Vielezeya vyake ni; Mazingira, Jamii ya watu, Jadi ya watu hao, Mapisi ya watu hao, Utamaduni – Mila – Dasturi - Ada – Kawaida – Tajriba – Lugha – Sanaajadiiya – Sanaa za Jadi Ujumi – Ubunifu – Usanii – fasihi – Sengo (2009) alipokataza maelezo ya A = B ni kwa sababu za kimsingi, kwa vile B#A.. Fasihi (kwa Kiswahili) na ni hiyo hiyo Literature (kwa Kiingereza) na ndiyo hiyo, hiyo Adab (kwa Kiarabu) LAKINI, tushasema, Fasihi ni fasihi kwa sifa za kwao, kama ya Kigogo, akiwa bingwa, atakuwa Mgogo E. Mgogo; kama ni ya Kikwere, akiwa bingwa, atakuwa Mkwere T. Sengo, ya Kizigula – bingwa ni Mzigula Mwekibindu T. Sengo wa Kibindu Kwa – Njeni nay a Kiswahili, bingwa wake sharti awe Mswahili – Mswahili Nabhany wa Pate – Matondooni – Lamu au Bi Moza, Bi Saida au Bi Kijakazi wa Utaani – Wete – Pemba. Sasa, suala hili limewekwa wazi. Ndege warukao angani ni pamoja na Mwewe, Kimanga, Tai, Kunguru, Yangeyange – wote ni ndege lakini kila mmoja, ndani ya jamii yake, ana fasihi yao. Kuwa Mnyaruwanda, Banyamulenge, Bakhutu, Mrundi au Mkongomani; akiwa kafika kuw Waziri katika Serikali ya Tanganyika, kusimpe jeuri ya kuzungumziya ya Watanganyika, ambao hana asili nao, hawajuwi na yao hayajuwi wala hayathamini. Fasihi ya Tanzania ndiyo kwanza twaijenga, iweje Fasihi ya Kiswahili kuifasiri iwe ya kila mtu na wenyewe wanyang’anywe. Kwani, mama zetu walotuzaa Ukwereni, Uziguwani, Unyaturuni, Ungonini, Ungwenoni, n.w. wamekosa nini? 

4.2.3 Nadhariya ya Nadhariya

Nadhariya ni Dhanna. Mswahili halitamki neno hili bila ya y-at Nadhari – a ila kwa ya. Jeuri ya kina Steere Krapf, Johnson hadi akina hawa wa leo, kina Knappart, Whiteley, Nurse, Geogre, David, Canute n.w. kwamba wao wana Ph.D; kwa hiyo lazima wajuwe zaidi Kiswahili na lughawiya ya Kiswahili kuliko Waswahili wenyewe, kwa kuwa hawana digrii za kupeyana; sasa haya yamefika mwishoni. Waswahili kina Maulid Haji Omar (PhD), Issa Rai (PhD; Prof.) na kina Mohamed Bakari (PhD. Profesa) wanakijuwa Kiswahili chao na lughawiya ya lugha yao vizuri zaidi kuliko ya hivyo wajuwavyo wageni. Nadhariya ya Nadhariya ni falsafa ya Nadhariya. Nadhariya ni nini? Ina sifa gani? Kama Nadhariya ni Mwongozo maalumu, Wazo Kuu (Sengo 2009), iwe ni njiya au mbinu ya kumsaidiya muhitaji namna ya kufanikisha linalotakiw kwa namna maalumu. Mfano wa Nadhariya ya nadhariya ni kitabu cha Propp (1984), ni Mwongozo wa kuwapa wanafunzi wa Sanaajadiiya uwezo wa kuifasili taalimu yao. Anayesikika kulilalamikiya swali ama suala la nadhariya ya nadhariya ni mgeni wa hayo. Angekuwa na akili kidogo tu, angejuwa kuwa hiyo si fani yake. Kwa mipaka hiyo , mtu hatakiwi kuchonga mdomo kusemeya jambo asilolijuwa. Criticism presupposes knowledge (tena ni thorough knowledge. Ujanja wa kuiba vya watu kutoka lugha ya Kirusi, Kijarumani, Kiarabu, Kigujurati na kukiandika kwa Kiswahili (na kujiita Prolific writer kunaisha pale ambapo kazi hizo zitakapomalizika ama kukamatwa na wenyewe). Nadhariya ya Nadhariya ni sawa na Dhanna ya Dhanna. Ni mzamiyambizi wa suala zito kama dhanna au nadhariya. Falsafa ya nadhariya ya Nadhariya inagusa misingi ya kuifasiri dhanna ya nadhariya kwa kina kirefu na mawanda mapana yenye hoja za hija. 
Kwa nini kuwe na dhanna? Kwa nini kuwe na nadhariya? Kwa nini kuwe na Fasili ya Waswahili ipo kujadili majambo, visa na mikasa inayotokeya katika jamii hiyo. Falsafa waliyonayo kwenye Methali ya Wa-Kibosho, Kiwade, Kiwade (Ulichonacho mkononi ndicho chenye thamani) wanayo piya Wakwere, kwenye methali yao – Gosolume Dilimmakonou. Hata, Chiudile icho unung’ha (“Ulichokula ndicho unukacho”, nayo inadekeza mawazo hay ohayo; ulichonacho, ulichokula, ulichokishika na ulichokula ndicho ulicho nacho. Uzito wa fikira na ukweli wa falsafa ya watu, dhanna na nadhariya za watu, waendewe watu wenyewe. Yasiwe mambo ya kurukiyarukiya na kushikiwa kipara sauti, mtu akatondoja au kuropoka ya kusema au kuchoweya. 5.0 TANZU ZA FASIHI Uswahili, Ushairi umetawala Sanaajadiya pamoja na fasihi yao. Utanzu unaoufuwata huu ni wa Tutumbi – Nathari – wa Hadithi na ndugui zake kina Semi, Methali mikasa, vijembe na visa. Utanzu wa tatu ni wa Sanaatendezi au Sanaa shirikishi. Nataki za kisasa zinazoitwa “Drama – Thiyeta” (za Kizungu), zimeingiya hivi karibuni. 5.1 Utanzu wa Ushairi Kufahamu Ushairi (Poetry) (Penn: 1960) kunatutaka tuelekeze Mbongo zetu kwenye chanzo cha umma wa watu kuanziya kwenye uvulivuli hadi hii leo. duniyani kote, kila umma una ushairi wake lakini si kila ushairi ni ushairi ule ule hata ndani ya jamii moja kwa wakati wote. Mabadiliko hutokeya ndani kwa ndani, kwa wenye lugha yao, kuutungiya ushairi wao miundo na mifindo, beti, mizani na vina kutokana na vionjo vya jamii hiyo. 
Ni vizuri kuzingatiya ukweli kwamba jamii yeyote ndiyo mamlaka ya fasihi na tanzu zake katika lugha na fasihi ya watu wake. Kunapokuja fikira ya upya, kusisemwe tu kwamba jambo fulani ni la kisasa;- linaweza kuwa jipya, linaonekana hapa kwetu leo kumbe juzi na jana, lilikuwapo katika kamii ya watu wengine kwahala kwengine. Ugeni si lazima uwe usasa. Kwa hivyo, wasemao, k.m. Nyimbo za Kizazi Kipya, ni lazima waulizwe na waweze kueleza kwa lugha hiyo yao mpya Nyimbo hizo ni zipi? Zimetokeya wapi? Zimezukazukaje? Ssifa au vielezeya vyao ni vipi? Dhanna zao zimeasisiwa kwa misingi ipi? Utungo wenye sifa za kishairi si lazima uitwe SHAIRI kwa kuwa SHAIRI, tayari ni dhanna au neno linalobeba dhanna ya watu maalumu kwa maelezo yao maalum, kwamba, ili shairi liitwe shairi, lazima liwe na beti, kiufundi 5 – 7 zinaweza kupunguwa, zinaweza kuzidi; kila ubeti uwe na mishororo au misitari mine, msitari wa mwisho ubebe uzito wa ubeti au wa shairi zima na uitwe kutuwo , kibwagizo au kiitikizii. Kisirudiwerudiwe matumizi ya neno zaidi ya mara moja kwenye ubeti au shairi zima. Vina vya kati na vina vya nje nip ambo zuri la ubeti au shairi. Tamathali za usemi zitumike vizuri, kuonesha ishara mbalimbai. Mfano; Mke mzuri tabiya, si unene si wembamba Hili ninalokwambiya, si wa mji si wa shamba Mwiko kumsingiziya, hasa mke wa mjomba Anziye tangu uchumba, sera kuitangaziya (Sengo: 02 – 10 – 2013) 
Neno mke ni picha ya mtu maalum. Si kila mwanamke anaitwa au anafaa kuitwa mke katika jamii ya Waswahili wa Mwambao wa Afrika ya Mashariki. Neno SHAIRI, katika Arudhi ya Kiswahili lina sifa maaum; ni bahari mojawapo kati ya 13 – 15 za Nabhany na Pera Ridhiwani. Aghalabu huwa na beti, kuanziya 1 – 7. Watunzi kufikisha hadi 25 – 35 lakini uhodari mkubwa umo katika kufikisha ujumbe mzito katika beti chache. Shairi lina mishororo mine – mitatu kwa wa nne wa kibwagizi au kituwo. Kila mshororo au msitari, una kina cha kati na cha nnje. Usizowee kunena, hili nitafanya kesho Ahadi kuhadiyana, hulijuwi lako fisho Bora kunyamaziyana, huku unavuja jasho Ogopa kuzuwa zusho, kesho ni yake Rabbana (TSYMS – 30-09-2013) Kina cha kati ni na ; cha nnje ni sho. Kwenye mshororo wa nne ambau ni kituwo au kibwagizo (kiitikizi) cha Ubeti, vinabadilishana naasi. Huwo ndiyo mfumo wa shairi la Arudhi ya Kiswahili. Wenye ushairi wao dniwo wenye mamlaka ya kuzileya taratibu hizo. Mwendesha gari, akifika kwenye taa zinazoelekeza kusimama na kupita, akiona ni udhiya, akachukuwa shoka au sururu kulivunja guzo lenye taa hizo ili yeye awe anapita atakavyo, ataonekana mwehu, karukwa na akili atakamatwa, ashitakiwe, aadhibiwe kwa kifungo, faini ya kulipiya gharama za guzo jipya na kunyang’anywa liseni ili asiendeshe tena gari. La msingi, kwa mwanafunzi wa ushairi ni kusoma vitabu vingi sana vya ushairi mbalimbali na kuzingatiya misingi mikuu ya ushairi na tafauti ambazo zimo katika ushairi wa watu fulani. Mwanafasihi wa RIWAYA asijilazimishe kuwa mtaalamu wa NATIKI (Drama – Tamthiriya – na Filamu) au awe bingwa wa tungo za kishairi. 
Lugha za nnje zisitupoteze. Neno poem ni la Kiingereza. Waitaliano wanalo lao. Kadhalika na wengine wote. Sasa neno SHAIRI lisilazimishwe kuwe sawa na hayo maneno ya lugha nyengine. La msingi, jengine kubwa ni, kusoma sana kazi zilizoandikwa vitabuni na mitandaoni. Waandishi wanaoandika juu ya Ushairi na Tungo za kishairi ni kundi moja, la pili ni la wahakiki, ambao ndiwo walimu wa walimu wa ushairi na la tatu, ni kundi la watunzi wenyewe wa mashairi, nyimbo, wajiwaji na bahari nyengine zilizomo ndani ya Arudhi ya Kiswahili au watungaji na waimbaji wa tungo za kishairi ambazo, majina ya hizo kazi ni lazima yawtafauti ili tungo hizo ziweze kusomwa, kufahamika na kutafitika. Panga la la Kiswahili limekosa kisawe kwenye Kiikngereza kwa vile Waingereza khawana asili ya kutengeneza na kutumiya panga. 5.2 Utanzu wa Tutumbi Semi fupi fupi k.v. siri, sirini, ujanja mali, jinga ni lako, duniya duniya, cheza shere, mwana wa nyoka n.n. ni kijitanzu cha nathari au tutumbi ambacho kinatumika sana katika fasihi ya mazungumzo, kwenye visa na mikasa, utani na ufundaji wa mizungu. Mithali, mafumbo, vitendawili, misimu, n.n. zina kazi kubwa ya kuitajirisha lugha ya Kiswahili na kufikisha ujumbe unaotakiwa kwa haraka na vizuri. Bakhili akiambiwa, “ashibae hamjuwi mwenye njaa” , atajuwa kapigwa kijembe ili akumbushike kutimiza wajibu wake wa kuwahudumiya wenye njaa “Kama si leo ni Kesho”, ni usemi mfupi lakini mzito sana, unakumbusha na kuapiza, unamtiya khofu na woga anayesemewa. Methali ni semi maarufu katika taalimu za uzamili na uzamivu. Ahmada (2008/9 ?) Moli (2012) na Makame (2013) wote wamemaliza masomo yao ya M.A. kwa kuzichambuwa methali, kila mmoja, kwa mada yake. 
Methali zimepambanishwa, za Kilibya na za Kitanzania, kuonesha mifanano na tafauti. Methali za Kiswahili zimechambuliwa na kuonekana uwezo wa methali hizo katika kufunza na kuleya watoto na watu wazima; (Moli) na Maalimu Makame (2013) kazichunguza methali, mapenzi na maisha ya ndowa. Methali zina hekima na busara, zina mantiki na falsafa nzito za maisha. Mkwere anapotaka kumfundisha mhemeyaji ambae humwendeya maneno laini; “mbeyu mditanda, kolonda mgelo, ahilima chose!” “unahitaji mbegu ya kwenda kupanda shambani mwako, umepewa tunga moja la hiyo mbegu, unasema kidogo, unataka tukutiliye kwenye kapu kubwa, kwani tumelima shamba moja!” Ndani ya kauli hii, mna ukweli, masuto, masimango na maonyo. Kwa mwenye akili, atashukuru kukumbushwa wajibu wa ndugu kupeyana na kutendeyana mema mengine. Kwa msununa, usemi huwo, utajibiwa kwa khasira, kuona kasemwa vibaya badala ya kuelekezw mazuri. Utafiti ufanywe zaidi wa zaida, methali zikusanywe, za Kiswahili, ziimarishe tamu ya Fasihi ya Kiswahili na za makabila engine, zionekane kuw zipo na kwamba nazo zina umuhimu wa kujenga na kuendeleza Fasihi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda hadi Kongo, kwa lugha ya Kiswahi. 5.3 Utanzu wa Natiki Katika Fasihi ya Kiswahili, natiki ilijificha kwenye ushairi wao. Sababu moja (ambayo Waingereza wanaiita “bitter pill”, mfano wa shubiri) ni Dini ya Kiisilamu, ambayo ndiyo utamaduni wa Waswahili, watu wapende wasipende, watake wasitake. Simba hawezi kumsaidiya swala anayeliwa na simba kila siku kwa kuukana uswala wake. Ni haki ya Simba kumla swala. Ni fakhari ya swala kuliwa na simba. Hayageuziki,k hayaadiliki wala hapana lawama ama uwonevu. 
Hizo ndizo haki za kinyama zilivyo. Kwa kuwa binadamu nao ni wanyamajamii, baadhi ya hulka za wanama wanyama, wanazo piya baadhi ya watu. Mapisi ya Nadhariya ya Tamthiliya (Wamitila 2002) Uswahili, natiki ni utanzu kongwe wa Fasihi – kongwe ya Simulizi nay a Ushirikishwaji wa hadhira tangu utangu wa tanguzi. Visa, Mikasa, Vichekesho na Maudhi ya kiutani yalitiwa katika tendezi ili kuipa jamii raha za maisha. Aristotle (Poetics) na maelezo yake amzuri ya Msuko – mythos , wahusika – ethos , nimbo – malopoeia, Utenzi na matumizi ya maneno – lexis , dhamira - theme na maonesho – opsis; yanafahamika vizuri zaidi kwenye mazingira ya dhanna hizo kwa lugha ya Kiyunani au ya tar-jama kwa wenye mafuhumu nayo. Uswahilini, natiki – shirikishi za asili zilihusu utendezi wa pamoja katika kujifurahisha na kujifariji aghalabu baada ya kazi ngumu za kulima na kuvuna, kusaka na kupata, kupigana zita na kushinda, kuingiya sonani – ukubwani, kuchezwa na kukhitimu na mifano ya mithili hiyo. Pa kucheka, watu walicheka kweli na pa kuliya watu waliliya kweli kwa kuwa suala la kufiwa si la masikhara la kuitaka “gwaya” ujiite iimbe nyimbo za msiba kwa niyaba ya mama mzazi aliyepoteza mwanawe au mtu na mzazi wake. Penye, kutambika, wazee maalumu waliongoza tambiko hizo, kuomba yaliyoombwa, kulingana na jadi za jamii. Uswahilini, tambiko hufanywa na visomo vya Dinii. Wakati Mrima, wana Mizimu (Mzimu – mlolongo wa kizazi kilichotanguiya kuzimu), Visiwani, kuna Panga. Kote huko, kuna walevi wa kasumba za wageni, wasiyoyajuwa yote hayo, wanaoropoka kuwa hayo ni mambo ya ushirikina. Mwingereza, mhuko kwao, lazima alikuwa na neno (dhanna) la STITION, ndipo alipozikuta STITIONS za kiafrika zkiwa chanya zaidi, akaziita superstitions. Mwafrika mwenyewe, ambaye kalewa saratani ya uhasi – utwana – utumwa, akaanza kujikana na kukana walomzaa kwa kuziitwa duwa au maombi ya wazee wake kwa Muomba wao, USHIRIKINA. 
Ukimwuliza mmoja miyongoni mwa hao waropokaji, maelezo ya USHIRIKINA, hana na hawana hawasa, fasihi wala tafsiri za hiyo dhanna. Mshiriki ni mtenzi mwenza wa mtenzi mkuu. Wakati Mwenyezi Mungu kajisema Yeye Mwenyewe kuwa kapwekeka, Anajitegemeya, Hategemei chochote wala yeyote, Hana Mtoto, Hana mzazi, Hana Chanzo, Hana Mwisho (Elimu ya Quraani Tukufu) Sura ya Ikhilas; Yake, hayahusishwi nay a watu. Uungu ni Wake Yueye Peke Yake. Kukitokeya mjinga akafananisha lolote la Ki – Mungu na la mtu au watu, huyo mtu atakuwa amekufuru na kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Lakini wanaotambika Mizimuni Sengo (akiwa kiongozi wa ukoo wa kwa mama yake), hajaona wala kusikiya, watambikaji wakimtaja mtu fulani kuwa ndiye Muumba Aombwaye (kama walivyoota Waintgereza, Ancestral Worship), Mizimu inathaminiwa na kuheshimiwa, haiabudiwi. Natiki – shirikishi k.v. Kikundi cha Kaswida cha Madrassa ni tafauti sana na natiki (drama, thiyeta au filamu za kutoka Uzunguni( za kigeni Wamitila (2008) anapozungumziya Drama ya Kiswahili, kumbe ni drama kwa lugha ya Kiswahili, anawakanganya watu kwa kuwa Drama si dhanna ya Waswahili na Kiswahili si lugha inayosawiri dhanna za kidrama, za kigeni, kwa vile, kila lugha hutumwa na wenye lugha kuwakilisha na kuwasilisha dhana za jamii ya lugha. Kila Muha anajulikana katokeya wapi – Kongo, Burundi au Rwanda. Kumwiita Muha, Mswahili, ni kuwiiba yeye na Waha wote na kuwafanya hawana makwao, na vile vile, kuwafanya Waswahili wajihisi, wanafanywa wakimbizi – kumbe wao ni watu na jamii yao kamili, yenye mashiko ya Kijiografiya (Pwani), Kimapisi (mchanganyiko maallumu wa damu na jadi) watu wake wameathiriwa na Umwambao kwa karne nyingi zisizo hesabu, kijadi – wana jadi, sanaajadiiya, sanaa za jadi, mila, desturi, ada n.k. zao wenyewe tafauti hata na za majirani zao Wakwere, Wazaramu, Wamrima wote wa Pwani ya Afrika Mashariki.
Kubwa linalosisitizwa kwenye sehemu hii ya somo ni kwamba sifa za Natiki za Kiswahili na zile zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili lakini si za Waswhili, lazima zifanyiwe utafiti na kuandikiwa vitrabu kwa jicho la kinyumbani. Waandishi wasianze na kina Aristotle wakati Tenzi za Kiswhili k.u.w. Mwanakupona na wa hivi karibuni Utendi wa Fumo Lyongo na nyengine za Mifano hiyo, zina misingi ya Uswahilini. Kuandika juu ya misingi bila ya kuthamini na kuzingatiya misingi ya jadi ya Kiswahii ni sawa na kuandika juu ya uzushi wa jambo lisilokuwako. Natiki za Kiswahili, kwa fani ya kinatiki, hazijatafitiwa na kuandikiwa sana, hasa na Waswahili wenyewe, kwani, kimitindo ya ki-Ulaya au Marikani, drama inavunja miko ya Dini ya Kiisilamu. Harukhusiki Mwisilamu, mwanaume, mwanamke kunenguwa, kwenda nusu – uchi na kufanya yote mengine, yaliyokatazwa kufanywa hadharani; kwenye faragha, chumbani, mtu peke yake, afanye atakalo. Akikutwa ataitwa, “hamnazo” au “punguwani”. Tenzi ama tendi za kinatiki ni tungo za kishairi zinazofuwata kanuni za Arudhi ya Kiswahili, zenye maneno na vitendo, Visa, Mikasa, Vituko na matendo. 5.4 Tanzu, Veitanzu na Vijitanzu vyengine Neno KISA lina maana mbili kubwa. Ki-lugha, yaani likitumika katika mtongoo wa kawaida, huwa na maelezo au fasili ya sababu. Nyinyi vijana mlikuw amarafiki, sote tumekuoneni hivyo kwa kitambo kirefu. Leo, mmetengana, hamko tena pamoja, kisa ni nini? Sababu ni ipi? Kisa chengine ni kama kijihadithi fulani kinachoelezeya sababu za kutokeya kwa kijambo fulani. Mfano, kisa cha Nabii Yusuf aliyetumbukizwa kisimani na kaka zake kutokana na uhadidi wa yeye kupendwa zaidi na babaake. Yusuf aliokotwa na wapiti njiya, akenda kuuzwa kwa Mfalme. Ilikuw auwawe kwa kanuni za nchi lakini alitetewa na Malkiya.
Mwisho wa kisa, Yusuf alipata kuwa Mku, kaka zake walipata kumtaka msaada. Wao, wala kunde, walimsahau. Yeye mtendwa maovu – mzowa maganda, aliwakumbuka. Akawahudumiya vema na kuwaomba wamchukuliye zawadi baba yao na wamwambiye anaitwa. Alipofika, babamtu alimkumbuka mwanawe. Aliliya sana na kuwasuta mno wale wanawe wakubwa. Nao, walipatwa na tahayuri kubwa. Wakamwomba msamaha ndugu yao. Naye akawajibu, damu nzito kuliko maji. Kisa cha pili kilisimuliwa Pemba na Tanga. Ncha ya Pemba ni kile cha mgeni mvaa kanzu lililoraruka, mbeba begi ya kidiplomasiya, aiyefika kwenye mji usio jina na kumtafuta Sheikh Mkuu wa mji. Begi ilipokelewa kwa furaha na tama kubwa zaidi kuliko mwenye begi. Mgeni alishinda akisali Msikitini tangu saa tatu asubuhi hadi wakati wa Isha. Baada ya Isha, alimfuwata Sheikh nyuma nyuma hadi nyumbani. Mgeni alipiga hodi mara tu baada ya Sheikh kufunguliwa mlango na mkuu mwenziwe. Sheikh alipomwona mgeni, moyoni, kaona kama ni mkosi au kisirani kikubwa kujiwa na Kisonoko mramba ukoko. “Kumradhini wenyeji wangu. Kilichonileta ni kukukabidhini kilichomo ndani ya begi, begin a funguwo.” Begi ikaletwa, ikafunguliwa, ilijaa pesa, noti mpya zenye thamani kubwa duniyani kutoka Benki. Begi ikafungwa. Begi na funguwo alikabidhiwa Sheikh Mkuu wa mji, sheikh, akampa mkewe, aitiye chumbani mwao. Naye, akafuwata nyuma. “Unasikiya mke wangu!” “Naam!” Siku zote ninakwambiya, nikiomba duwa, hairudi bure. Juzi na jana, nimekuwa naomba duwa ya kupata fedha. Leo, alhamdulillah, tumezipata mke wangu, si unazoziona!” “Laa, ila hilo. Mimi simo kabisa, juu ya hilo. Pesa za mgeni, tumtunziye mgeni amana yake.” “Wanawake, ndiyo maana mnasemwa, hamna akili.” Mara, Sheikh, akakwanguwakwanguwa pete yake, mkewe akapata usingizi fofofo. Akamtandikia mgeni chumba cha wageni. Naye, akafanyiwa yale yale ya Bi mkubwa. Sheikh, aliwamyonga mgeni.
Alifajiri, alipomwambiya mkewe, “mgeni katutoka,”, mke alijuwa zamani, kisa cha umauti huwo. Mara, baada ya Salla ya alfajiri, mgeni alikwenda kuzikwa. Mkasa uliyotokeya ni maiti kuzamishw ardhini na Sheikh Mkuu wa mji. Wazikaji wengine walirushwa nje ya kaburi na ardhi kujisawazisha kana kwamba hapakuchimbwa. Ncha ya Pemba ndiyo hii. watu wote walizirai. Walingojana wazinduke. Wote wakenda kwa Bi – mkubwa. Wakafafanuliwa kisa na mkasa wote, tangu awali hadi akheri. Nchi ya Tanga, pahala pasipojulikana, tukiyo ni hilo hilo. Maiti na Sheikh (aliyezongwazongwa na mnyororo mzito) walitupwa juu ya kaburi lililojifunika. Wazishi wengine na wasindikizaji jeneza wote walizirai kama kule Pemba. Nao, piya walikwenda kwa Bi – mkubwa kupata maelezo. Jee, Sheikh, alikuwa Sheikh kweli au Sheikh Kanzu, Shehena, Fisidi, Jambazi, Mnafiki mkubwa!? Jee, mgeni, alikuwa mtu au Malaika aliyetumwa? Baada ya kuwa na visa, mikasa, matukiyo na vituko piya vipo. Tumebahatika kuapta vituko viwili kutoka kwa Bi Felista – Samira wa Sumbawanga – Zambia – Kongo. Kijana aliitwa Sumbawanga, aende Ziwa Rukwa kwenda kuvuwa. Alijiandaa kwa vifaa na zana zake za kazi. Jiyoni ya kulaliya kazi, alilazimika kulala na vijana wenziwe, nymba moja maarufu kwa uvutaji bangi. Mgeni hakuwa na hili wala lile. Alifajiri, kabla hajatoka, maasikari waliingia ile nyumba, wakapiga risasi mbili tatu juu, wakatowa amri ya “CHINI YA ULINZI” na wote mliomo humu tokeni. Walipopelekwa Mahakamani asubuhi hiyo hiyo, Mshitakiwa wa kwanza alikuwa huyo mgeni wa kutoka Kijijini ambaye yote hayo hakuyaelewa. Hakusahau kubeba nyavu zake za kuvuliya samaki. Aiposemeshwa na Mheshimiwa wa kike kuwa alishitakiwa kwa tuhuma za kuvuta bangi. 
Kijana mgeni alionesha Nvyavu zake na kusema kuwa yeye, anangoja apewe rukhusa akanwe, hajuwi kwa nini haletwa hapo Mahakamani na hilo bangi, ndiyo kwanza analisikiya hapo, yeye halijuwi. Mheshimiwa Hakimu, alimwuliza kijana mgeni mshitakiwa, “Una hakika na unachokinena? Kijana, alivuwa bukta yake na kumwonesha Mheshimiwa Hakimu kinena na vifaa vyake yvote vya sirini; “Ndiyo, Mheshimiwa, kinena ninacho, hiki hapa”. Mheshimiwa Hakimu alilazimika kujificha Ofisini na kuwaamuru asikari wamtowe kijana pale Mahakamani kwa uwehu. Kijana alivaa, kawashangaa shangaa watu, akabeba nyavu zake kwenda kuvuwa samaki. Vijitanzu kama hivi viko vingi na bado havijafanyiwa utafiti wa kutosha ili (i) Vipatiwe majina ya huko vitokako (ii) dhanna zake zipewe vielezeya / sifa (iii) maudhuwi na dhamira zitongolewe (iv) Ujumbe na mafunzo makuu yaainishwe (v) Ufundi wa kiubunifu na kisanii uoneshwe (vi) wasanii wake wahifadhiwe kwa maandishi na kwa rekodi nyengine za kisasa. Mazungumzo kama Mazungumzo si fasihi. Mtu hasifiwi kwa uhodari wa kusema na wenziwe, kwa kutumiya vizuri maneno, akitunza adabu na mbeko za mazingira aliyomo. Mazungumzo yake yanaweza kupambwa na tamathali nyingi za usemi, visa, vituko, methali, semi namna kwa namna; lakini mazungumzo ya utaalamu na wataalamu wake. Ni hao waliopata kuonya kuwa, “Kutondoja au Kuropoka si Kuchoweya, si kuzungumza, si kusema.” Na sifa ya kuzungumza ni kusikilizana. Mpemba, akimkumbusha mwenyewe kwambiwa neno, “Mkwambiya neno kakupende” ana hayo mazungumzo ya manufaa kwa vile yasiyofaa ndiyo hayo ya waropokaji wenye kutowa maneno ya kutondojwa bila ya kufahamika. Mzungumzaji mzuri au mwandishi mzuri wa khotuba ama ripoti ni yule atumiyae tamathali za ishara na taswira wazi lakini mwanafasihi mpevu hatayachukuliya hayo kuwa ni fasihi. 
6.0 Mambo Muhimu
6.1 Usomi si uzushi.
Usomi ni Elimu inayotokana na kweli za jamii. Kila jamii ina elimu yake, jadi yake, falsafa yake, ujumi wake, ubunifu wake, usanii wake, fasihi kwa lugha yake, dhanna na maarifa yake n.k. haji mgeni wa lugha ya KINGONI akatowa fasili ya mgeni ya neno BAMBO (Baba) akasemwa Bambo ni Kwale. Mzushi huyo, hata awe na PhD zote za duniya, ni msomi – zushi, bombwe – kuu, bunye, henye, hezi, ombwe tupu na kama mna kitu kidogo, ni tope la kinyesi cha najisi kubwa isiyovumilika kwa watu wanaohisabika kuwa na fikira.

6.2 Fasihi si kila kitu. Mifano, Muziki wa ala ni taalimu ya Wanamuziki, wenye kuzisoma hizo noti zao na kuzisikiliza sauti zao (zisizo maneno) na kuzifahamu. Kamwe, taalimu hiyo si ya fasihi. Mchawi na uchawi wake, yake si fasihi. Bali, maneno teule yakitumika, k.m. Mchawi alitoka akiwa na vichwa saba, puwa kama mkuki n.m.k.h. hayo saa ndiyo yatakayotiwa katika vipimo vya fasihi. Jamii ya Dini, itakuwa na mazingira ya kidini, imani, itikadi za kidini, maisha ya kumthamini Mwenyezi Mungu. Fasihi ya watu hao ipimwe kwa vigezo vyao. Binti aliyezawa na Mwana Kupona hakuwa na mama mwengine ila amsikilize huyo, apate radhi yake na ya Muumba wake. Kusema Binti wa Mwana Kupona ati ananyanyasika ni utovu wa fahamu wa fasihi na hasa ffasihi za jamii za watu – washenzi wana yao, waungwana wana yao; wasungo – mfano wa migomba, wana yao na warombo – walokhitimu mafundo ya nyago na nyagizi – wana yao. Mwalimu wa fasihi anatarajiwa awe mpevu, mpana, mwenye kina na kimo cha kuyajuwa na kuyaenze ya watu. Hayawezi hayo, bora akawe asikari – buti na virungu, apigepige watu bila sababu, ajifiye kifo cha nyaudu.
6.3 Utaipataje Taalimu ya Fasihi Soma vitabu vingi. Soma makala mengi. Soma majarida, hata magazeti mengi. Wasome waandishi wengi, wa kila nchi, wa kila karne, wa kila rika na jinsiya. Vichaa piya huandika. Wasome. Waungwana na Washenzi nao, wasome. Mwalimu wangu, Profesa A.B. Wood, alinielimisha kuwa, kila mtu ni mkichaa, tafauti ni kiwango cha ukichaa. Mfano- Jaribu kuwa kichaa wa kushinda vituwoni – barabarani. Watapita watu, sampuli kwa sampuli; wachekao, waliyao, wanunao, waumwao, mafisidi, mahasidi, mafisadi, madhalimu, waonevu, waonelwa, wahonyoji, wahonyelwa, wasemaji, n.w.w. Barabarani wapo waindeshao magari kwa mwendo kasi mno, wapo wa kinyume cha hao. Wapo watu wanaojiita asikari, watozaji kodi ya matumbo yao, kila gari hutozwa faini ya shilingi ya alfu mbili hadi hamsini. Inasemekana watu hao hutumwa. Jiyoni, kwenda kupeleka hesabu Gimingi (siyo ya Pemba) na wahusika kufurahiya matunda wakati wenye magari hupata shinikizo la damu kwa maudhi. 
6.4 Vyanzo vya lazima vya Kusoma 
  • Sengo, (1985) PhD ya Sanaajadiiya ya Waswahili wa Pemba na Unguja (Maktaba: UDSM East            Africana; IAAS, KU, KU Graduate College) 
  • Dorson, R. M. (1963) “Current Folklore Theories” kwenye Current Antropology (jarida) 
  • Dundes, Alan. 1996 “The American Concept of Folklore” JFI – Indiana, 1976 “Structuralism and        Folklore” in Pentikainen (jarida) 
  • Mulokozi, M. Fasihi ya Kiswahili Nadharia na Uhakiki OSW 105. OUT 
  • Mulika zote CUK – TUKI – TATAKI – UDSM Makala za Uhakiki Kiswahili Na. zote k.h. 
  • Sengo na Kiango 1975/76 – 2012 Hisi Zetu 1 na 2 na Hisiya Zetu TUKI – TATAKI UDSM –               Uhakiki 
  • Sengo na Kiango 1975/76 Ndimi Zetu 1 na 2 (Maktaba UDSM, TATAKI,TAIFA) 
  • Sengo, T. 1975Shaaban Robert. Uhakiki wa maandishi Yuke 
  • Senkoro F.E. 1982 Fasihi , DSM Press and Publicity Centre 
  • Wamitila, K.W. Kanzi ya Fasihi Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi Vide – Muwa                    Publisher. 
  • Chimera, R. n.w.waf. 2011 Kiswahili Res.& Dev. In Eastern Africa. RISSEA MBS. 
  • Brooks, C et alia 1976 Understanding Poetry, Chicago. 
  • All English Publications. Helisinki SKS: Finish Folklore / Literature Society 
  • Math Kuusi et alia. Frans. 1977 Finishi Folk Poetry. Epic an Anthology. Helisinki. SKS 
  • Rice, P and Waugh P. 2001 Modern Literary Theory. Holder Headline Group 
  • Propp V. Martin & Martin 1984 Theory and History of Folklore. Minnesota. 
  • Literary Theories & Thesis of Literature – Nadhariya za Fasihi in all available journals, Internet         sources (libraries) 
  • Hawthorn, J. 2000 A Grossary of Contemporary Theory

6.5 Waandishi 
6.5.1 Riwaya 
  • Shaaban Robert 
  • M. S. Abdulla 
  • Mohamed Suleiman 
  • Said Ahmed Mohd Khamis 
  • Mbunda Msokile 
  • Adam Shafi 
  • E. Mbogo  
  • E. Kezirahabi 
  • T. Sengo (Insha Ndefu, Tembezi na Fumbizi) 
  • Nyengine zote – someni, someni, someni

  6.5.2 Ushairi (hasa, Arudhi ya Kiswahili 
  • Muyaka 
  • Mwanakupona 
  • Sayyid Abdalla A. Wasiri 
  • Kijumwa 
  • Nabhany 
  • Shaaban Robert 
  • Ahmed Nassir 
  • Abdilatif Abdallah 
  •  Haji Gora Haji 
  • Sengo, Tigiti 
  • Jumanne Mayoka 
  • Watunzi wa Tungo za Kishairi (k.v. wa UKUTA, Maryam Ponda, Siti Binti Saad, Bi Madina               Kibao, Bi Kidude n.w.) 6.5.3 Natiki (Tamthiliya, Drama, Thiyeta) 
  • E. Mbogo 
  • I. S. Ngozi 
  • Semzaba 
  • E. Hussein 
  • P. Mlama / Mhando 
  • Lihamba 
  • Vitabu kutoka Kenya, pote Afrika Mashariki. 

TAN – BIHI / NADHARI / HADHARI Soma sana, bila chuki wala upendeleo. Uwezo wako wa akili, hekima na busara yako ikuamuliye ya kukufaa wewe maishani na kuwafaa waja wote Ulimwenguni. Soma – Soma – Soma – tafuta ELIMU siyo Vyeti vya Kisomo bila ya Mbeko
Powered by Blogger.