MIUNDO YA SILABI ZA KISWAHILI SANIFU.

MIUNDO YA SILABI ZA KISWAHILI SANIFU.
Katika maelezo yaliyopita maana ya silabi ilifafanuliwa  kama kipashio cha kifonolojia  kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti .Hii ina maana kuwa maneno ya lugha hutamkwa kwa kufuata utaratibu wa silabi.

Katika Kiswahili sanifu kuna miundo mbalimbali ya silabi kamainavyoelezwa hapa chini kwa mifano ya kutosha.
1.Muundo wa kwanza ni ule  unaojengwa na irabu peke yake.(I)
Hebu chunguza mifano ifuatayo:
  silabi “a” katika neno “angalia”   $a$ $nga$ $li$ $a$
  silabi “u” katika neno  “ugua”     $u$ $gu$ $a$
 silabi  “I” katika neno   “niite”      $ni$ $i$ $te$

2.Muundo wa silabi wa Konsonanti na Irabu. (KI)              
Mifano :
Zungumza     =$zu$ $ngu$ $m$ $za$
Tapatapa        =$ta$ $pa$ $ta$ $pa$
Maliza             = $ma$ $li$ $za$

3.Muundo wa silabi wa Konsonanti, kiyeyusho na irabu (KkI)
Mifano:
Bwana     =$bwa$
Fyata       =$fya$
Mpya        =$pya$
Upwa        =$pwa$
Ukwezi     =$kwe$

4.Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu (KKI)
Mifano:
Mwandani   =$nda$
Chongo       =$cho$  $ngo$
Nguru          =$ngu$
Daftari         =$fta$
Boksi           =$ksi$
Sekta           = $kta$

5.Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti, konsonanti, na irabu (KKKI)
Muundo huu wa silabi unajitokeza kutokana zaidi na mikopo ya maneno lkutoka lugha  ya kiingereza na lugha nyinginezo. Baadhi  ya mifano yake ni pamoja na:
Skrubu        =$skru$
Springi         =$spri$
Mbwambo    =$mbwa$
Nchi            =$nchi$

Katika lugha ya Kiswahili kuna miundo mingi ambayo huenda haijatajwa katika mifano yetu hapo juu; hii yote ni kutokana na ukweli kuwa kuna silabi ambazo zaweza kujengwa kutokana na maneno ya kibantu au maneno ya lugha nyinginezo za kigeni yaliyomo katika lugha yetu adhimu na sanifu ya Kiswahili.
Powered by Blogger.