MASWALI NA MJIBU YA NECTA
Mwandishi ; Mwl GODLOVE J GWIVAHA
ENEO
LA KAZI; SHULE YA SEKONDARY TEGETA
MWAKA ;2015
1.Kwa kutumia mifano, thibitisha
ubantu wa Kiswahili kwa hoja madhubuti (nect 2010 swali la 10)
KISWAHILI NI KIBANTU
Nadharia hii hutumia
ushahidi wa kiisimu na kihistoria katika kuchunguza lugha ya Kiswahili katika
mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za kibantu.
Nadhalia hii huitimisha kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha katika jamii kubwa
ya lugha ya wabantu.
Wataalamu wa nadharia
hii ni kama vile makon Guthrie, meinhof c na rohlc.
Malcon Guthrie
amethibitisha kuwa Kiswahili kilikuwepo kabla ya wageni na kimeonyesha kuwa
Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za kibantu. Mwisho
amehitimisha kwa kusema Kiswahili kimeanza Pwani ya afrika mashariki.
Mein holf na Rolh wao wanaamini kuwa wakati wa utawala wa
washirazi katika upwa wa afrika mashariki kulikuwa na kabila la waswahili
ambalo ni dhulia la wazaramo wa leo. Wazalamo walizaliwa katika harakati za
biashara hivyo wakafuata nyayo za wazazi wao na lugha yao ilikuwa kibantu na
kwa kuwa wabantu ni wengi zaidi lugha yao ikaanza kutumika na kuenea katika
makabila mengine. Kutokana na waswahili kufanya biashara na waarabu, washirazi,
wamalaysia, wahindi na wareno vifaa na majina ya vitu vya biashara vya wageni
hao vikaenea na kuingizwa katika mfumo wa lugha hiyo ya kibantu.
Nadharsia hii
imekubalika kuwa ndio sahihi juu ya asili ya Kiswahili kwa kuzingatia ushahidi
wake wa kiisima na kihistoria.
USHAHIDI WA KIHISTORIA
Ushahidi wa
kihistoria unathibitisha kuwa lugha ya kiswahili ilizungumzwakatika upwa au
pwani ya afrika mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kama vile waarabu, na
wazungu.Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika hapa afrika
mashariki.wote wamehitimisha kwa kusema kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa
hapa afrika mashariki hata kabla ya ujio wa wageni.
A.UGUNDUZI WA AL-IDRIS
(1100-1166)
Ugunduzi
huu ulifanyika huko sicily mnamo mwaka 1100-1166kwenye mahakama ya mfalme Roger
, Al-idris alikuwa wa kwanza kugundua kuwa jina la kwanza la zamani la Zanzibar
kuwa ni unguja. katika maelezo yake aliandika baadhi ya majina kama kikombe,
mkono wa tembo,muriani na sukari ambayo ni majina ya ndizi mbalimbali
zilizokuwa zikipatikana Zanzibar.
B.USHAHIDI
WA MARCO POLO
Huyu
ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na maswala mbalimbali ya kijografia na
alisafi sehemu nyingi duniani Marco polo aliandika hivi:
“Zanzibar
ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa na mzunguko wa maili 200. Watu wote
wanaabudu (Mungu).Wana mfalme na wanatumia lugha yao, na hawalipi kodi (ushuru)
kwa mtu.
Safari ya Marco polo
Aliandika
kitabu cha kijografia ambacho kinasemekana kuwa hakikupata kuchapishwa lakini
sehemu zake zimepatwa kufanisiwa kwa kirusi na kifaransa. Katika lugha ya
Kiswahili ni kama ifuatavyo:
Katika
visiwa vya Djawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii ni kile cha Andjaba
ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao-zanzibar –ungudya na wakazi
wake.
Japokuwa
ni mchanganyiko kwa sasa wengi wao ni waislam chakula chao kikuu kikiwa ndizi,
kuna aina tano ambazo zilijulikana kama kundi, fili ambao uzito wake waweza
kuwa wakia 12, omani, mariyani, sukari.
Maelezo
haya ya Marco polo yalithibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa pwani ya
afrika mashariki na lugha yao.
C.USHAHIDI
WA AL- MASUDI (915, BK)
Katika
moja ya maandiko yake Al-masudi anazungumza juu ya wakazi wa mwambao ambao
wanajulikana kwa jina la “Wazanji” kwa dhana hii neno Zanzibar linalotokana na
neno “zanjibar” yaani pwani ya “Zenji” katika maelezo yake Al-masudi anaonyesha
kuwa wazenji walikuwa na watawala, wakilimi ambao waliaminiwa kuwa walitawala
kwa nguvu za Mungu.Kuna maelezo kuwa
huanda neno wakilima lina maana ya wafalme.Al-masudi alisisitiza katika
maelezo yake kuwa wazenji wasema lugha yao kwa ufasaha na walikuwa na viongozi
waliohutubia kwa lugha yao, kutokana na neno Zenji kuna uwezekano kuwa kabla ya
maajilio ya waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au Kizenji na wageni
waliofika pwani ya afrika mashariki.
D.
HISTORIA YA KILWA,Kimsingi habari zinaeleza historia ya
kilwa karne 10-16 B.K na zinahusisha na kutajwa majina ya utani kama mkoma
watu, nguo nyingi” nk ambao walipewa masltani wa kwanza wa kilwa Ali Ibnhussein
na mwanae Mohamed Ibn Ali.Kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahili
ilishaanzwa kusema mnamo karne ya 10 au ya 11 B.K. Maelezo juu ya sultani
aliyeitwa Talt Ibn Al Hasani ambaye alipewa jina la utani “Hasha Hazifiki” nayo
pia yalitolewa.
E.USHAIRI WA KISWAHILI
A. utenzi wa tambuka (karne ya 18
b.k)
Utenzi
huuuliandikwa mnamo karne ya 18 kuanzia mwaka 1700 na kuendelea (tarehe kamili
haijulikani). Utenzi huu umeandikwa kwa kutumia lugha (lahaja ya kimvita
)ambayo ni moja ya lahaja za lugha ya Kiswahili.
B.Utenzi
wa fumo liyongo
Shairi hili
linasemekana liliandikwa karne 13 B.K. kuwepo kwa shairi hili kunadhihirisha
uwepo wa lugha ya Kiswahili kabla ya hapo. Huenda kilianza kutumika kabla ya
karne ya 10 B.K. baadhi ya beti za utenzi wa fumo liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti
6 Liyongo kitamkali
Akabalighi
vijali
Akawa
mtu wa kweli
Na
hiba huongeya
Ubeti
7 Kilimo kama mtukufu
Mpana
sana mrefu
Majimboni
yu maarufu
Watu
huja kwangaliya
Ubeti 10 Sultani
pate Bwana
Papo
nne akanena
Wagala
mumemwona
Liyongo
kiwatokeya
Lgha
hii ni mfano wa lugha iliyokuwa ikitumika mnamo karne ya 13 BK.ni wazi kuwa
lugha hiyo ilianzwa kusemwa mapema kabla ya muda huo.
F.Vitabu
vya peryplus na yu-yang-tsa-tsu,Kitabu cha perplus
kinahusu mwongozo wa Bahari ya Hindi. Inasemekana kiliandikwa karne ya kwanza
huko Alexandria.kitabu hiki kinataja habari za Tanzania (afrika mashariki) na
habari za vyombo kama nyalawa, madema, mitepe. Kinaeleza kuwa watu wageni
hutozwa ushuru na wafanyabiashara wenyeji, wanaijua pia lugha ya wenyeji wao.
Kitabu cha Yu-yang Tsa Tsu kinaeleza
habari za upwa wa afrika mashariki na shughuli mbalimbali za wachina hapa
afrika mashariki
Kitabu kingine kiliitwa Chu fan chi
kilichochapishwa 1226 kinaelezea habari za Zanzibar na biashara, vyakula, dini,
na wanyama wa pwani ya afrika mashariki.
G.Ushahidi
wa ibn batuta karne ya 14 bk,Mohamed bin Abdallah
Ibn Batuta ana asili ya taifa la kiarabu. Alikika upwa wa afrika mashariki
mnamo mwaka 1331BK.katika maandishi yake
anaeleza juu ya maisha ya watu wan chi hii ya afrika mashariki ingawa yeye
aliita nchi ya waswahili. Anataja miji kama vile Mogadishu, na kilwa.anadai
kuwa;
“Basi nilianza safari baharini kutoka Mogadishu kwend nchi ya ya waswahili na nchi ya kilwa
ambao umo ndani ya nchi ya Zanji. Tulipofika Mombasa kisiwa kikubwa, mwendo wa
siku mbili kutoka nchi ya waswahili…………….watu hawajishughulishi na kilimo,
ingawa huagiza nafaka kutoka kwa waswahili”
Maelezo haya yanahusu eneo au mahali ambayo
waswahili walikuwa wakiishi na inaonyesha kuwa watu hawa walikuwa wakiishi katika
upwa au pwani wa afrika masharikikuanzia sehemu za bara upande wa kaskazini hadi
msumbiji na bukini kwa upande wa kusini.
H.Maandishi
ya Morice (karne ya 18 bk),Maandishi haya yalijitokeza
mwaka 1776.katika maandishi yake morice amewagawa
wakazi wa afrika mashariki katika makundi matatu yaani masuriyama,waarabu na
Waafrika.Anaendelea kusisitiza kuwa Masuriyama na wafrika walisha kaa na
kuungana kama jumuia moja wakaelewana na kusema lugha moja ya kisuriyama.Kuna
wazo kuwa huenda kisuriyama ndicho Kiswahili
cha leo.
USHAHIDI WA KIISIMU
Isimu ni nini?
Isimu ni sayansi au
taaluma inayoiangalia lugha kwa undani(kisayansi) kwa kuzungukia tanzu kama
vile;isimu jamii,isim historia,isimu linganishi,isimu matumizi,isimu nafsia na
isimu fafanuzi.Ushahidi wa kiisimu ni ushahidiunaothibitisha kwa kutumia
misingi inayohusu sayansi ya lugha.
Lugha ya Kiswahili
ilifanyiwa utafiti na wataalamu kadhaa kwa lengo la kuainisha kama ina misingi
ya kibantu.
Malcon Guthrie
kutoka chuo kikuu London Uingereza alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo
baina ya lugha za kibantu ziliko katika
eneo lote ambalo hukaliwa na
wabantu yaani kusini mwa jangwa la sahara.
Alifanya Uchanganuzi
wa mashina au mzizi(viini) ya maneno 22000 kutoka lugha 200 za kibantu .Kibantu
Uchunguzi wake alikuta mzizi (mashina)2300 imezagaa katika lugha mbalilmbali za
kibantu na kiswahli kikiwezo.Mashina au mizizi 500 yalilingana katika lugha
zote 200.Mashina haya yalipatikana
katika lugha zote za kibantu.Mashina haya yalikuwa ya asili moja.Baadhi
ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi,lugha ya Kiswahili ilionesha kuwa na
ulinganifu sawa na kikongo(44 asilimia)
Katika
kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina
hayo 500 yamo katika kila lugha ilionekana mgawa ufuatao;
Kiwemba
kizunguzwacho Zambia 54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga 51%
Kikongo kizungumzwacho 44%
Kiswahili
kizungumzwacho Afrika Mashariki 44%
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania 41%
Kiyao
kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji 35%
Sotho
kizungumzwacho Botwana 20%
Rundi
kizungumzwacho Burundi 43%
Kinyoro
kizungumzwacho Uganda 37%
Zulu
kizungumzwacho Afrika kusini 29%
Matokeo ya utafiti huu
yanathibitisha kuwa;
i.
Mashina mengi ya lugha za kibantu
yapo afrika ya kati hasa sehemu
zinazozungumkia mkoa wa Katanga huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
kupungua kadri unavyoelekea mbali nako. Hivyo ni dhahiri kuwa wabantu walienea
kutoka sehemu hizo na kuja sehemu mbalimbali zikiwemo zile za afrika mashariki.
ii.
Kufuatana na matokeo ya utafiti hua
ni wazi kuwa, lugha ya Kiswahili ni kibantu kama madai yake ya kusema Kiswahili
madai yake ni kiarabu yangekua sahihi basi lugha hiyo ingehusiana mno na
kiarabu.
1. MSAMIATI,Msamiati
ni msingi wa lugha ya Kiswahili na kibantu unafanana kabisa. Msamiati wa msingi
ni ule unaohusu ambayo hayabadiliki badiliki kutokana na mabadiliko ya
utamaduni tofauti zinaweza kujitokeza katika matamshi au mabadiliko kidogo ya
viambishi, kakini si katika mzizi.
Mfano;
Kiswahili
kindali kizigua kijita kikurya
Mtu umundu mritu omontu omonto
Maji amishi manzi amanji amanche
Moto umlilo moto omulilo omoro
2. Tungo (sentensi) za Kiswahili ,miundo
ya tungo (sentensi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana miundo ya tungo za
maneno ya kibantu. Sentensi za kiswahili na lugha za kibantu zina kiima na
kiarifu.
Mfano Kiswahili – Juma/ anakula ugali
K A
Kizigua – Juma/ adya ugali
K A
Kisukuma – Juma/ alelya bugali
K A
Kindali – Juma /akulya ubhugli
K A
Kijita –Juma/ kaiya ubusima.
K A
3.Ngeli
za majina,Hapo kuna makubaliano kufuatana na ngeli katika mambo ya nomino
(umoja na wingi wa majina) pamoja na kisarufi.
i.
Kigezo
cha maumbo ya majina
Kigezo
hiki hufuata mambo ya umoja na wingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo
mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufuata mkondo wa umoja na
wingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu yaliyomengi yana maumbo
dhahiri ya umoja na wingi.
Mfano Umoja wingi
Kiswahili Mtu
Watu
Mtoto
Watoto
Kikrya Omonto
Banto(abanto)
Omona Baria (abana)
Kizigua Mntu Bhantu
Mwana Bhana
Kindali Mundu
Bhandu
Mwana Bhana
ii.
Kigezo
cha upatanisho wa kisarufi
Katika
kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya nomino na kivumishi na
viambishi vya awali vya nafsi katika vitenzi vya Kiswahili na kibantu.vivumishi
majina pamoja na vitenzi hivyo hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na wingi.
Mfano
Umoja wingi
Kiswahili Baba analima Baba wanalima
Kindali Utata akulim Abhatata Bhakulima
Kikury Tata anarema Batata abalima
Kijita Tata kalmia Batata abalima
3. Vitenzi vya kiswahili na kibantu,Kuna
uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya kibantu.
Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu
ni viambishi, mnyambuliko pamoja na mwanzo/mwisho wa vitenzi.
a. Viambishi
Lugha
ya Kiswahili na lugha za kibantu vitenzi vyake hujengwa na mzizi (kiima) pamoja
na viambishi vyake (awali na tamati)
Mfano
Kiswahil
– analima – a-na-lim-a
1 2
3 4
Kikurya
– ararema – a-ra-rem-a
1 2
3 4
Kindali-
akulima – a – ku – li – ma
1 2 3 4
ü Kiambishi
awali kipatanishi cha nafsi.
ü Kiambishi
awali cha njeo.(wakati uliopo)
ü Mzizi
/kiima
ü Kiambishi
tamati
b. Mnyambuliko wa kitenzi
(uambishaji)
Mnyambuliko ni
kitendo cha kuunda neno jipya kwa kuunganisha viambishi kwenye mzizi wa shina
au neno mnyambuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya
lugha ya kibantu.
Mfano
Kiswahili – kucheka
– kuchekesha – kuchekelea
Kindali – kuseka –
kusekasha – kusekelela
Kibena – kuheka –
kuhekesha – kuhekelela
Kinyamwezi – kuseka
– kusekasha – kusekelela
Kikagulu – kuseka –
kusekesha – kusekelela
c. Mwanzo wa vitenzi
Vitenzi
vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za kibantu huanza na viambishi ambavyo ni
viwakilishi vya nafsi:
Mfano
Kiswahili
- Ninakwenda
Kihaya – Ningenda
Kiyao - Ngwenda
d. Mwisho wa kitenzi
Vitenzi vya lugha za
kibantu huishia na Irabu a
Mfano
Kiswahili – kukimbia
– kuwinda – kushuka.
Kindali - kukinda –
kubhinga – kukola
Kisukuma - kwihuka -
kuhiga – kisinga
2.Mofimu
–u- yaweza kuwa na dhima mbalimbali ukitunga
sentensi kwa kila dhima,Onesha dhima tano (5).Pigia mstari mofimu –U-
ili kubainidhima hiyo.(Mock 2014-Dar swali la 4)
(A) Inaweza
kuwa mzizi wa neno
Mfano: Amemu-u-a
(B)Inaweza kutaja
ngeli ya U-I,U-YA,U-ZI/Idadi
Mfano;Mti U-mekatwa
(c) Inaweza kutaja
nafsi ya pili umoja
Mfano; U-liondoka
(D) Inaweza kutaja
kauli ya kutenda
Mfano; Fung-u-a
(E) Inaweza kusimama
kama kitenzi shirikishi
Mfano;Wewe u-
mgonjwa
DHANA
NYINGINE
(A) “ NA”
i.
Hutumika kama kiunganishi
Mfano
Juma na Priska wanaimba
ii.
Hutumika kama kiambishi cha nafsi ya
kwanza
Mfano
Naomba aje mwenyewe
iii.
Hutumika kama kihusishi
Mfano
Amekaa mbali na maadui
iv.
Hutumika kama kiambishi cha njeo ya
wakati uliopo
Mfano
Elicia anaimba.
v.
Hutumika kama kauli
Mfano
Nani?
vi.
Hutumika kuunda mzizi wa kitenzi
Mfano
Yeye anataka
vii.
Hutumika kuonyesha mtazamo wa msingi
wa jambo
Mfano
Na aje sasa.
TUMIA
KIAMBISHI “KA” KUONYESHA MATUKIO KUMI (10)
(NECTA
2011 SWALI LA 3)
i.
Hutumika katika vitenzi vya kutoa
amri,ari,au ombi
Mfano
Nenda kamwite (amri)
Kafanye
kazi yake (ombi)
ii.
Hutumika katika kuonyesha wakati
katika mtindo wa kukubali
Mfano
Wakapanda
Mkapanda
iii.
Hutumika kama alama ya wakati na
kuonyesha masimulizi ya matukio yaliyopita
Mfano
Kati ya mwaka na mwaka
iv.
Hutumika kuonyesha matukio ya
mfululizo
Mfano
Nataka kusafiri niende mbali
nikatafute.
v.
Hutumika katika vitenzi kuonesha hali
au kusudis
Mfano
Naomba fedha nikanunue nguo
(B) MATUMIZI YA “KI”
i.
Hutumika kuonyesha masharti
Mfano.
Akija nitakupigia
ii.
Ngeli ya 4 (ki-vi)
Mfano.
Kisu kimepotea
Visu
vimepotea
iii.
Hutumika kuonyesha upungufu wa viungo
katika mwili
Mfano.
Kipofu,kiziwi, kibogoyo.
iv.
Hutumika kuonyesha uduni (kudunisha,
udogo)
Mfano.
Kizee kile kina mambo ya ujana
Kijana
Yule ana mambo ya kizee
v.
Hutumika kufananisha
Mfano.
Anaishi kikristo kweli kweli
vi.
Hutumika kuonyesha lugha mbalimbali
Mfano
Kiswahili, kingereza
UKITUMIA
MFANO WA SENTENSI KATIKA KILA TUMIZI ONYESHA MATUMIZI MATANO YA KIUNGANISHI
“KWA”
(NECTA 2006 SWALI LA 8)
AU
KWAKUTOA
MIFANO, TAJA MATUMIZI MATANO TOFAUTI YA KIUNGANISHI “KWA” (NECTA 2010 SWALI LA 5)
i.
Hutumika kama kiunganishi
Mfano. Walikusanyika
wazee kwa watoto.
ii.
Hutumika kama kielezi cha mahali
Mfano. Juma
alikwenda kwa rafiki yake
iii.
Hutumika kama kisababishi
Mfano. Watu wengi
hufa kwa ugonjwa wa Ukimwi
iv.
Hitumika kama kielezi cha jinsi (namna)
Mfano. Atatembea kwa maringo
v.
Hutumika kama kilingnishi
Mfano Simba
ilifungwa magoli sita kwa mbili.
vi.
Huonyesha hali ya kutakiana heri.
Mfano. Kwa heri
vii. Hutumika
kuuliza
Mfano. Kwa nini?
viii.
Hutumika kufananisha jambo
Mfano. Kwa tabia anafanana na mama yake
ix.
Hutumika katika nahau au misemo
Mfano. Sisi kwa sisi
Uso kwa uso
Jino kwa jino
KWA
KUTUMIA LUGHA ONYESHA KAZI TANO (5) ZA MOFIMU “KU”
(NECT 2007 SWALI LA 5)
i.
Kiambishi cha awali cha njeo ya
wakati uliopita
Mfano. Mwandishi hakuandika ubaoni
ii.
Kunominisha
Kufeli
kunachukiza
iii.
Kuonyesha mtendwa nafsi ya pili umoja
Nimekuona
iv.
Kuonyesha mahali
Kule
ni kuzuri
v. Kuunda mzizi wa kitenzi
Kumbuka,kuna
vi.Kuonyesha mtendwa
nafsi ya pili umoja
Nimekuona
vii.Kuonyesha
wakati/njeo
Kufika
kwetu
(C) MATUMIZI YA “N”
i.Hutumika
kuonyesha nafsi ya kwanza umoja
Mfano Ninaimba, nimeolewa
ii.Hutumika kama
urejeshi wa mtendwa
Mfano wameniuzi, wamenipiga
iii.Hutumika kama
mzizi wa neno kiulizi
Mfano Nani,nini, lini ?
iv.Hutumika
kushirikisha vitenzi katika sentensi
Mfano wewe ni mpole
(G)MATUMIZI YA “M”
(i)Hutumika
kuonyesha nafsi ya pili wingi
Mfano ninaimba, mnastaajabu, mmeiba
ii.Hutumika
kuonyesha idadi ya umoja
Mfano mti, mtu, mchezo
iii.Hutumika
kuonyesha urejeshi wa mtendwa
Mfano Anavyomchezea, wanamsifu.
(H)MATUMIZI YA “JI”
i.Hutumika kuonyesha
urejeshi wa mtenda jambo
Mfano anajiua
i.
Hutumika kuonyesha kijenzi cha nomino
Mfano mwimbaji, mchezaji
ii.
Hutumika kama mzizi wa neno
Mfano anakujia
3.Bainisha
aina ya vivumishi katika sentensi
(Mock 2014 mkoa wa
Dar, Swali 3 )
i.Mtoto wangu
amechaguliwa jeshini
Wangu
– Kivumishi kimilikishi
i.
Nani aliitisha mkutano huu?
Huu
– kavumishi kionyeshi
ii.
Mtu wa chama atakuja leo
Wa
chama – kivumishi
iii.
Yale matatu ya ache
Matatu
– kivumishi cha idadi
iv.
Mwanafunzi mwenyewe ametoroka
Mwenyewe
– kivumishi cha pekee
MOFIMU
Ni kipashio bkidogo
chenye maana ya kisarufi au ya kileksika.Kipashio hicho kinaweza kuwa sehemu ya
neno au neno zima.Mofimu zenye maana ya kileksika aghalabu huwa ni mofimu
ambazo haziambatanishwi na kipashio kingine chochote.
Mfano;
Baba,Mungu,Fikiri,Bora n.k
Mofimu zenye maana
ya kisarufi ni mofimu zinazoambatanishwa na mofimu nyingine katika uundaji wa
maneno.Mofimu hizo huwa n sehemu tu ya mmaneno yaambatanishwayo katika mzizi wa
neno.
Mfano; A-na-lim-a
AINA ZA MOFIMU
A.Mofimu huru
B.Mofimu tegemezi
A.Mofimu
huru,Ni neno/maneno yanayoweza kugawanyika katika vipande maana kisarufi.Ni
maneno ambayo hatuwezi kuyavunjavunja katika vipande vidogovidogo na vyenye
kuleta maana ya kisarufi. Agharabu ni maneno yasiyo na umoja kama vile Baba, Mama,
Jana, Leo,StareheHuitwa mofimo huru kwa sababu ya maneno haya hujitoshereza.
B.Mofimu tegemezi,Hivi
ni vipande vidogo kabisa vya neno vyenye maana kisarufi. Huitwa mofimu tegemezi
kwa sababu vipande hivi vinategemeana ili kutoa maana kisarufi kipande kimoja
cha neno hakiwezi kusimama peke yake na kutoa maana ya kisarufi mfano.
Sikukuona
a. Si-ku-kuon-a
Si
– mofimu awali kanushi nafsi ya kwanza.
Ku-mofim
awali ya nafsi ya pili
Kuon-mzizi
wa neno
a—
mofimu/kiambishi tamati
DHIMA ZA MOFIMU
Ni
matumizi au kazi za vipashio katika vitenzi. Dhima nyingi hutokea katika
vitenzi na dhima chache zinazoweza kujitokeza katika baadhi ya nomino kivumishi au kiwakilishi
i.
Hudokeza idadi
Mfano, umoja wingi
Ninasoma tunasoma
Limevunjika yamevunjika
Kiatu viatu
ii.Hudokeza
hali ya ukanushi na uyakinishi
Mfano;
Uyakinishi Ukanushi
Nitaondoka Sitaondoka
Utafaulu Hutafaulu
iii.Hudokeza hali ya Mazoea
Maana
yake jambo hufanyika mara kwa mara
Mfano;Hula,Hucheza,Huimba.
iv.Hudokeza nafsi zote tatu(3)
Nafsi
huoneshwa katika vitenzi kwa kutumia vipashio mbalimbali.Takribani kila
nafsi ina kipashio chake.
Mfano;
(a)
Nafsi ya kwanza
Umoja Wingi
Ninasoma Tunasoma
Ananipiga Wanatupiga
(b)
Nafsi ya pili
Umoja Wingi
Unacheza Mnacheza
Nilikufundisha Tuliwafundisha
(c)
Nafsi ya tatu
Umoja Wingi
Alimpiga Waliwapiga
v.
Hudokeza hali ya
Masharti
Hali ya masharti
katika Tungo huwaklishwa na vipashio kama vile;
Ngali,ngeli,nge-,ki.
Mfano;
Angesoma kwa bidii angefaulu mtihani.
Akija nitamchinjia mbuzi
vi.
Hudokeza njeo(wakati)
(A) Wakati uliopita
Huoneshwa
na vipashio “li” na “ku” kipashio ‘li’ hudokeza
wakati uliopita uyakinishi na ku- katika ukanushi.
Mfano. Uyakinishi ukanushi
Alisoma hakusoma
Alikunywa hakunywa
Nilikuja sikuja
Alilia hakulia
(B)Wakati
uliopita timilifu
Wakati
uliopita timilifu maana yake ni si muda mrefu tangu jambo lifanyike na matokeo
ya kufanyika kwa jambo hilo bado yapo
Wakati
uliopo timilifu huonyweshwa na vipashio me
katika uyakinishi na ja katika
ukanushi.
Mf. Uyakinishi ukanushi
Nimekunywa sijanywa
Nimekuja sijaja
Amekufa hajafa
C
Wakati uliopo unaoendelea
Huu ni wakati
unaonyesha tendo bado linaendelea na bado hatujui litakoma lini, wakati uliopo
unaendelea hudokez wa na vipashio Na, i, si
Kipashio
na hutumika katika uyalimishi na vipashio ‘i’ na ‘si’ hutumika kwenye ukanushi
‘i’ hujitokeza mwishoni mwa kitenzi.
Mfano Uyakinishi Ukanushi
Ninasoma sisomi
Ninacheza sichezi
D Wakati ujao maana
yake bado jambo halikufanyika
Wakati ujao
hudokezwa na kipashio
Mfano. Uyakinishi ukanushi
Atalima hatalima
Nitaondoka sitaondoka
NB
Iwapo kitenzi cha
wakati ujao kitakuwa na urejeshi (o-rejeshi) ndani kitapata kiambishi cha wakati ujao ka.
Mfano atakaye soma
Nitakapoondoka
vii.
Mofimu hudokeza hali ya urejeshi
Hivi
ni viambishi au mofimu ambavyo hurejerea kutaja au kudokeza kitu, mtu au jambo
ambalo linajulikana au lililokwaisha tajwa
Mfano Yaliyomwagika,
Waliotoroka
Aliyekamatwa
viii.
Mofimu hudokeza kauli mbalimbali
Kuna
kauli nyingi katika vitenzi na kauli hizi nyingi hujitokeza mwishoni mwa
kitenzi. Na kila kauli ina umbo yake linlosadifiana na kitenzi husika kilichomo
katika kauli
Mfano
a. Kauli
ya kutendwa
Mfano cheza, analima,anasali,
anatubu.
Kiambishi tamati cha kauli cha
kutenda huwa ni a,i,u hutegemea na
asili ya neno.
b.Kauli ya kutendea
Kiambishi cha e au i hii inategemea
asili ya mzizi
Mfano. Anasomea – A-na-som-e-a
Tulipigia Tu-li-pig-i-a
c. Kauli
ya kutendesha
Viambishi tamati vya kauli ya
kutendeshani esh, ish
Mfano. Chezesha chez-esh-a
Salisha Sal-ish-a
d.
Kauli ya kutendeshwa
Viambishi tamati vya kauli ya
kutendeshwa ni eshw, ishw
Chezeshwa
Someshwa
Safishwa
ix.
Kauli ya kutendana
Kiambishi
tamati cha kauli ya kutendeana ni an
Pigana
Chezeana
Imbana
x.
Kauli ya kutendwa Ni w
Mfano Pigwa
Chezwa
xi.
Kauli ya kutendewa ni iw, liw, lew
Mfano. Imbiwa
Somewa
Olewa
xii.
Kauli ya kutendeka
Viambishi
vya kauli ya kutendeka ni ek, k, lik, lek
Mfano. Pigika
Chezeka
Someka
6.Ni kipengele kipi
kinachotumika kuunda ngeli za kimapokeo? Dhihirisha utumiaji wa kigezo hicho
kwa kutunga sentensi (5) za ngeli tofauti.(nect 2010)
NGELI
ZA MAJINA
Ngeli
ni aina au namna ya kuweka majina katika makundi yanayofanana au yanayowiana
MIGAWANYO
YA NGELI
Katika
ngeli za nomino zimekuwa zikigawanywa kwa kuzingatia mitazamo mikuu miwili, mitazamo
hiyo ni
i. Mtazamo
wa kimapokeo/Ngeli za kimapokeo
ii.Mtazamo wa
kisasa/Ngeli za kisasa
MTAZAMO WA KIMAPOKEO
(NGELI ZA KIMAPOKEO)
Kiimofolojia)
Hapa
majina au nomino yalipangwa katika makundi yaliyofanana kwa kutegemea na maumbo
yake.Ni hali ya kupanga majina katika makundi yanayofanana kwa kuoanisha
viambishi awali vya majina hayo katika umoja na wingi.Mtazamo huu wa kimapokeo
unaungwa mkono na Mein holf na ashton
Ngeli ya 1: M/WA
Katika ngeli
hii majina yenye sifa zifuatazo yanaingia katika ngeli hii;
-Majina ya
Viumbe vyenye uhai isipokuwa mimea.
Mzee
–Wazee
Mtoto-Watoto
Mtu-Watu
Mwalimu-Waalimu
-Majina
yanayotokana na Vitenzi yanayotaja watu
Mfano
Mfungaji-Wafungaji
Mchezaji-Wachezaji
Ngeli ya 2: M/MI
-Yanaingia
majina ya mimea
Mti-miti
Mchungwa-Michungwa
Mpapai-Mipapai
- Yanaingia
ya vitu yanayoanza na M-
Mto - mito
Msumari – misumari
Msumeno – misumeno
Mwiko – miiko nk.
- Yanaingia
majina ya matendo yanayoanza na M-
Mchezo – michezo
Mkato – mikato
Mtego – mitego
Ngeli ya 3: KI/VI
- Hapa yanaingia majina yanayoanza na
Ki-(umoja) na Vi (uwingi)
Kiti – viti
Kisu – visu
Kikapu – vikapu
Kito – vito, nk.
- Yanaingia
majina ya vitu yanayoanza na ch- (umoja) na vy-(uwingi)
Chakula – vyakula
Chuma – vyuma
Chungu – vyungu
- Yanaingia
majina ya viumbe yaliyoambishwa Ki- ya kudumisha.
Kitoto – vitoto
Kizee – vizee
Kisichana – visichana
Kivulana – vivulana
Ngeli ya 4: N-
-Yanaingia majina ambayo huanza na
N-inayofuata na konsonanti ch-,d-,g-,j-,-z-, -y- katika umoja na wingi
Nguo njaa mvua
Nyama mboga mvinyo
Nchi ndizi
Mbuga nyota, nk.
Yanaingia majina ya mkopo
Barua taa meza
Kalamu redio, nk
Maumbo yote ya majina haya hayabadiliki
kwa umoja na uwingi.
Ngeli ya 5: JI/MA
Yanaingia majina yanayoanza na Ji-
(umoja) na Ma (uwingu)
Jiwe – mawe
Jicho – macho
Jina – majina n.k
Yanaingia majina ya sehemu za mwili
na sehemu za mti.
Goti – magoti
Sikio – masikio
Ini – maini
Ua – maua
- Yanaingia
majina ya mikopo.
Bwana – mabwana
Shati – mashati
- Majina
yenye kueleza dhana ya uwingi japokuw hayahesabiki.
Maji maisha manukato
Mate mafuta
mavi nk.
Ngeli ya 6: U/N
- Yanaingia
majina yanayoanza na U-(umoja)na N- au Mb- (uwingi).
Uso – nyuso
Uzi- nyuzi
Ubao – mbao
Ngeli ya 7: U/MA
Yanaingia majina yanayoanza na
U-(Umoja) na Ma- (uwingi).
Uasi – maasi
Ugonjwa – magonjwa
Uchweo – machweo
Ununuzi – manunuzi
Ngeli ya 8: KU-
- Yanaingia
maneno yale yanayohusu vitenzi (Vitenzi jina).
Cheka – kucheka
Cheza – kucheza
Imba – kuimba
Ngeli ya 9: PA/MU/KU
Mahali pale
Mahali kule
Mahali mule
Msingi wa kisintaksia/upatanisho
w kisarufi.
Huu ni mtazamo wa kisasa unaogawa
majina katika ngeli kwa kulingana na upashio wa kisarufi kati ya jina na
viambishi awali vilivyo kwenye viamgishi. Kwa mujibu wa mtazamo huu, ngeli za
majina ya Kiswahili ni tisa (9) kama ifuatavyo:-
Ngeli
|
Viambishi awalia vipatanishi.
|
Mifano
|
|
1.
|
A-WA
|
A-Umoja
WA-uwingi
|
Mtu anakuja – watu wanakuja
Mtoto analia – watoto wanalia
Mtoto anacheza – watoto wanacheza
|
2.
|
U-I
|
U-umoja
I-uwingi
|
Mti umeanguka - miti imeanguka
Mto umekauka – mito imekauka
Mguu unauma - miguu inauma
|
3.
|
LI- YA
|
Li – umoja
Ya - uwingi
|
Jicho linaona – macho yanaona
Panga linakata – mapanga yanakata
Jicho linauma – macho yanauma
|
4.
|
KI - VI
|
Ki – umoja
Vi – uwingi
|
Kisu kinakata – visu vinakata
Kizee kimelala – vizee vimelala
Chakula kimechacha – vyakula cmechacha
|
5.
|
I – ZI
|
I – umoja
Zi – uwingi
|
Nguo imechakaa –
nguo zimechakaa
Sahani imepasuka –
sahani zimepasuka
Nchi inaliwa nchi zinaliwa
|
4.
|
U -ZI
|
U – umoja
Zi – uwingi
|
Ukuta zimejengwa -
kuta zimejengwa
Uzi umekatika –
nyuzi zimekatika
Ubao umevunjika - mbao
zimevunjika
|
7.
|
U – YA
|
U- umoja
Ya- uwingi
|
Ugonjwa umeenea -
magonjwa yameeneo.
Uasi umeisha – maasi yameisha
|
8.
|
KU-
|
Ku – umoja
|
Kuimba kunachosha
Kucheza
kunaburudisha
Kusoma kunachekesha
|
9.
|
PA-MU-KU
|
Pa – umoja
|
Mahali hapa
pametuchosha
Mahali humu
panafaa
Mahali huku kunapendeza.
|
7.Dini zisingefika Tanzania Kiswahili
kisingekua na kuenea kwa haraka.Jadili kauli hii.(nectar 2004 swali la 1)
AU
Fafanua kwa hoja tano(5) madai
kuwa dini zisingefika Tanzania,Kiswahili kisingekua na kuenea kwa haraka(Mock
mkoa wa dar,2014 swali la 10)
Kuenea kwa lugha
ni kuongezeka la watu wanaotumia lugha yenyewendani ya nchi.Ongezeko linakomaa
kiasi cha kuvuka mipaka ya awali.
Wanaokubali
Ni
kweli kabisa dini zisingefika Tanzania Kiswahili kisingekua na kuenea haraka
kutokana na sababu za michango ifuatayo ya dini zote mbili yaani kiisilamu na
kikristo.
Wamishenari,walifika pwani ya Afrika mashariki kabla ya utawala wa
wakoloni ,baadhi ya mashirika ya dini kama vile”Roho mtakatifu” White father yote kutoka Ufaransa pia Church
Missionary Society(CMS) mambo waliofanya kukuza na kukieneza Kiswahili ni
kama ifuatavyo;
Waliandika
sarufi ya kwanza ya kiswahili ya kimvitakatika kitabu kilichoitwa “Outlines of
the elements of Kiswahili language with reference to the kinika dialects na walitafsiri injili ya luka na
yohana kutoka kwenye lugha ya kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili.
Walikiweka
kiunguja katika maandishi Edward Steere
alifanikiwa kuchapisha toleo la kwanza la sarufi ya Kiswahili cha kiunguja
kitabu hicho kiliitwa “A handbook of
Swahili Language as spoken at Zanzibar.
Walifanikiwa
Kutoa kamusi mbalimbali za Kiswahili kwenda kiingereza na kiingereza kwenda
kiswahili ambayo mwanzoni ilianzishwa na Edwrd steere na kumaliziwa na A.Madan.
Wamisheni
walitumia Kiswahili katika kaziya kueneza dini yao huku wakitumia Kiswahili
kama lugha ya mawasiliano hali hii ilipelekea Kiswahili kukua na kuenea kwa
haraka.
Waislamu
walifika pwani ya afrika mashariki wakakuta tayari wenyeji wana lugha zao za
kibantu na Kiswahili kutokana na malengo yao ya kutaka kueneza dini ya kiislamu
hivyo waliamua kutumia lugha ya Kiswahili katika mawaidha (mahubiri) hivyo
walifanya Kiswahili kukua na kuenea zaidi.
Wamisheni
walijenga vituo vyao vya dini katika maeneo mbalimbali ya Tanganyika kama vile
Mpwapwa,Zanzibar,Bagamoyo, masasi n.k katika vituo hivyo Kiswahili kilitumika
katika mawasiliano baina ya wamishenari na wenyeji hivyo kuchangia na kukua na
kuenea haraka.
Pia
Kiswahili kilitumika kufundishia elimu ya dini ya kiislamu (Madrasa) hivyo
kukua na kuenea kwa lugha ya kiswahili pia kulichangiwa na mafundisho hayo.
Waarabu
walijenga misikiti sehemu mbalimbali za Tanganyika kama vile Bagamoyo, Tabora,
nk. Katika maeneo hayo ya vituo lugha iliyotumika ni Kiswahili hivyo kukua na
kuenea haraka.
Wamisheni
walijenga shule za msingi na sekondari (middle school) katika maeneo mbalimbali
ya Tanganyika Kiswahili kilitumika kufundishia elimu ya shule ya msingi na
sekondari walisoma kama somo la Kiswahili hali hii ilipelekea kukua na kuenea
haraka
8.Fafanua matatizo
yaliyojitokeza katika kukisanifisha wakati wa ukoloni.(necta 2004 swali la 2)
Usafishaji
Ni
kulinganisha lugha na kuifanya ikubalike kwa watu wanaohusika kimatumizi.Mambo
muhimu katika usanifishajiwa lugha ni pamoja na kuangalia usahihi wake,kisarufi
na kimatamshi.Hapo awali hatukuwa na na aina moja ya Kiswahili ambacho kilikuwa
na maandishi ya aina na matamshi(lafudhi).Viswahili hivi vyote vilisambaa pwani
ya Afrika mashariki ndivyo tunavyoviita Lahaja.Uwepo wa lahajanyingi za
Kiswahili ndiyoiliyokuwa chanzo cha na haja
ya kuwa lugha moja ambayo ingetumiwa na kila msemaji.
Matatizo
yaliyojitokeza katika kusanifisha ni kama yafuatayo;
Uhaba wa fedha,kipindi
cha kusanifisha lugha ya Kiswahili wakoloni walikuwa na mitazamo tofauti kuhusu
kukisanifisha Kiswahili kwani walikuwa na lengo la kukifanya kiweze kutoa
huduma katika maeneo waliyokusudiwa,kwa vile hawakuwa na lengo la kukiendeleza
Kiswahili walihofia kuwa na hadhi sawa na kiingereza hivyo walitoa fedha kidogo mno kwaajili ya
kuendeshea kamati mbali mbali na shughuli za usanifishaji.
Kutowashirikisha wazawa wa lugha,Kipindi
cha kusanifisha lugha ya Kiswahili
shughuli zote za usanifishaji zilifanywa na wazungu matumizi ya baadhi
ya maneno yalipewa kibali yalikuwa na kasoro,Mfano nje(inje),nge(nje).
Kutokukubalika kwa uteuzi wa
Lahaja ya usanifishaji,Watu wengi hawakukubaliana na
uteuzi wa lahaja ya kiunguja,Baadhi walidai kimombasa kingeteuliwa katika
usanifishaji kutokana na historia yake ndefu kuliko kiunguja hivyo wataalamu
kutoka Kenya (Mombasa)walipinga kuteuliwa kwa kiunguja.
Tatizo la maneno(msamiati),Kipindi
cha usanifishaji kamati ilianzisha
maneno jinsi yanavyotamkwa na kuandikwa ni tofauti,wenyeji walilazimishwa
kukubaliana na kuyatumia maneno hayo yaliyoundwa katika kiswahili,Mfano
mba(maandishi),mbu(maandishi)-(umbu)matamshi.
Uhaba wa vitabu vya kusoma,Vitabu
vilivyotolewa na kamati ya usanifishaji vilikuwa vichache hivyo havikukidhi
mahitaji ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili.kutokana na uchache wa vitabu kazi
ya usanifishaji ikawa ngumu sana.
Watu hawakuthamini machapisho ya
Usananifishaji,watumiaji wengi wa Kiswahili hasa
wazalendo wa lugha hii hawakuthamni machapisho yaaaaliyotolewa na kamat ya
usanifishaji,kwasababu machapisho hayo yalikuwa na kasoro nyingi.Wazungu
waligeuza sarufi ya lugha ya Kiswahili ikawa sawa nay a lugha ya
kiingereza.Vile vile waliogopa Kiswahili kikisanifiwa zaidi kinaweza kuzaa
lugha nyingine tofauti kabisa.Kiswahili hiki kiliiitwa Kiswahili cha Serikali
(The standard Swahili) Hivyo wananchi waliona kama wameundiwa lugha ambayo
waliiona si sahihi.
Matumizi ya Kiswahili yalikuwa
duni ukilinganisha na kiingereza, Maneno ya lugha ya
kiingereza yalikuwa juu(yaani hali ya ubora na kiwango kizuri)lakini matumizi
ya Kiswahili yalikuwa duni,kilipangiwa maeneo ya chini mfano kufundishia shule
za msingi na vyuo vya ualimu wa shule za msingi,pia ilionekana kuwa Kiswahili
ni lugha ya watu wa hali ya chini (makabwela) na kingereza kilipangiwa maeneo
ya juu kama mahakama kuu,vyuo,sekondari
na n.k.
“Serikali
baada ya uhuru ilijitahidi sana katika kukuza Kiswahili nchini
Tanzania”Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa mfano dhahiri (Necta 2006 swali la 1)
Maana ya kukuza
Baada
ya uhuru mwaka 1961 serikali ya Tanzania ilichukua hatua tofauti tofauti za
kukuza Kiswahili hili mwaka 1962 iliunda kamati maalum ya kuangalia uwezekano
wa kiswahili katika shughuli rasmi za kiserikali na iliamuliwa Kiswahili
kitumike Bungeni na shughuli zote za kiserikali.
Baadhi
ya jitihada zilizochukuliwa ni:-
Kuteuliwa
kwa lugha ya Taifa Kiswahili mwaka kiliteuliwa kuwa lugha ya mwaka 1963, mwaka
1964 kilianza kutumika katika Bunge na shughuli zote za kiserikali wizara za
kiserikali zilihimizwa kutumia Kiswahili katika mawasiliano yote.
Kuundwa
kwa vyombo vya kukuza na kueneza Kiswahili vyombo hivi zilisaidia sana kukuza
na kueneza na kueneza Kiswahili mfano TUMI, UWAVITA, TUKI, BAKITA, TAKIKUKI NK.
Vyombo vya habari
Vyombo
hivi vilitumika sana na kukuza na na kueneza Kiswahili baada ya uhuru mpaka
sasa.Vyombo hivi vilijishughulisha na shuhuli zinazohusu kiswahili mfano,
Radio, Magazeti, Televisheni. Kulikuwa na vyombo vya habari vya serikali na
watu binafsi vyote vilitumia lugha ya Kiswahili kurusha matangazo yake na
vipindi mbalimbali mfano Redio na televisheni, kulikuwa na redio ya taifa
ambayo kwa sasa inaitwa TBC.
DINI
Dini
zote zilitumika za kiislamu na kikristo zilitumia lugha ya Kiswahili katika
mahubiri yake na kuchangia kukuza na kueneza.
BIASHARA
Misafara
ya biashara katika sehemu mbalimbali za nchi zilisaidia kukikuza na kukieneza
hadi nchi za nje ya Tanzania.
Kampeni za kisiasa
Kampeni
za kisiasa kama CCM, TANU zilisaidia sana ukuzaji na kueneza na vingine vyama
vingi tangu mwaka 1992 zilipoanzishwa kutokana na zilipoanzishwa kutokana na
kampeni za uchaguzi wa viongozi vyama cvya siasa na serikali zimechangia sana
kukuza na kueneza Kiswahili kutokana na matumizi ya Kiswahili.
Utawala
Shughuli
zote za utawala tangu mwaka 1963 kiswahili kilitumika katika shughuli zote za
utawalahivyo zilisaidia sana kukua na mfano, maofisini, bungeni, mikutano ya
serikali pia kilichaguliwa na serikali kuwa lugha rasmi.
Elimu ya watu wazima
Elimu
hii ilianzishwa nchi nzima ikiwa imelenga wasiojua kusoma na kuandika,afya,
ufundi,siasa na Kiswahili yalifunisha kwa Kiswahili kutokana program hii
Kiswahili kilikuwa na kuenea na watu wengi waliweza kuzungumza, kusoma na
kuandika.
Uchapishaji wa vitabu na
majarida mbalimbali vilevile uchapishaji wa vitabu. Na
majarija umechangia sana kukuza na kueneza Kiswahili kulikuwepo na vitabu
vilivyochambua sarufi ya Kiswahili pamoja na fasihi ya Kiswahilipia majarida
mbalimbali yalichapishwa mfano, mulika, zindiko jarida la Kiswahili nk. Vyote
hivi vilisaidia kukuza.
Shughuli mbalimbali za utamaduni
Shughuli
tofautofauti za kijamii zilisaidia kukuza hapa nchini hii ni kutokana na
shughuli ambazo ziliwakatisha watu kwa kutumia Kiswahili kama lugha ya
mawasiliano katika misibi, harusi, jando, nk. Shughuli hizi zilisaidia kukuza
Kiswahili.
Sherehe mbalimbali za vyama
Mara
nyingi zimeshangia kukua kwa Kiswahili kutokana na hotuba ambazo hutolewa kwa
lugha ya Kiswahili viongozi hutumia Kiswahili kuhutubia wananchi mfano, siku ya
muungano, sikukuu ya CCM, na siku ys uhuru wa Taifa nk.
a. Jadili sababu za Kiswahili kuwa
lugha ya taifa nchini Tanzania kuliko lugha nyingine za Tanzania (nect 2006)
swali la 2
Lugha
ya taifa
Ni
ile lugha iliyochaguliwa kutumika katika taifa zima na inayoweza kutekeleza
wajibu wa taifa.Lugha ya taifa inaweza kuwa kitambulisho cha taifa.
Lugha
ya kibantu ni lugha za asili (makabila) mfano kisukuma, kipare, kigogo, kikurya
nk.
Ili
lugha ichaguliwe kuwa lugha ya taifa inahitaji kuwa na sifa zinazohitajika ambazo Kiswahili kilikuwa
nazo na lugha za makabila hazikuwa na sifa zote hizi.
Kiswahili kilikuwa kimeandikwa
vya kutosha katika vitabu na magazeti mbalimbali
Mfano
vitabu vya fasihi, sarufi, magazeti kama vile habari za pwani, kiongozi,
ukulima wa siasa nk. Bali lugha za kibantu hazikuwa na magazeti
yaliyoandikwa/kuchapwa kwa kibantu.
Kiswahili kilitumika kwa namna
moja
Katika
makabila mbalimbali kilitumika kwa namna inayofanana na hii ni kutokana na
kufanyiwa usanifishaji kwa kutumia lahaja ya kiunguja.
Kiswahili kilikuwa na utamaduni
wake,
Lugha
hii ilikuwa na utamaduni wake asili haikutegemea kutokatamaduni nyingine.
Kiswahili kilikubaliwa kwa
watanzania wote,
Wananchi
au watumiaji walikubali Kiswahili kuwa lugha ya taifa lakini baadhi ya lugha za
kibantu hazikukubaliwa na watumiaji.
Kilitumiwa na watu wengi
Kiswahili
kilikuwa na watumiaji wengi kwa sababu watu walikuwa wanakijua kuongea na
kusoma na kilikuwa chepesi tofauti na lugha za kibantu ambazo zilikuwa na
watumiaji wachache.
Kilijitosheleza na mahitaji ya
watu
Hii
nayo sababu ilipelekea kuteuliwa kuwa lugha ya taifa kilitumika Nyanja zote
kiuchumi, kisiasa,kielimu na kiutamaduni.
b. Maneno ya lugha nyingine
yanapoingizwa katika lugha ya Kiswahili yanakidumaza Kiswahili. Jadili kauli
hii (nect 2007 swali la 1)
Wanaokataa
wana mitazamo ifuatayo
Lugha yoyote ina tabia ya kukopa
maneno kutoka katika lugha nyingine mfano Kiswahili
kimekopa maneno kama ifuatavyo stati- shirt (kiingereza) nyonge - dhaifu
(kiarabu) shule – schule (kijerumani) nk.
Zifuatazo ni hoja za
kuthibitisha;
Kukua kwa lugha, kutokana
na kukopa manenokutoka lugha nyingine lugha itajipatia msamiati ili lugha ikue
inahitaji kujionezea mmsamiati.
Kujitosheleza kwa lugha na
kukidhi mahitaji ya watumiaji, kwasbabu ya ongeko
la msamiati watumiaji wa lugha watakidhi mahitaji ya lugha.
Pia lugha itajipatia istilahi
mbalimbali mfano sayansi, kiuchumi, na kisiasa
Ambayo itakidhi mahitaji katika Nyanja hizo hasa istilah za kisayansi ambazo
dunia nzima inauratibu wa kutumia lugha moja ya kilatina lazima Kiswahili
kufuata utaratibu huo.
Vilevile
lugha itajipatia tafsiri mbalimbali kutoka katika lugha, maneno yaliyokopwa
katika lugha
Wanaokubali wana mitazamo
ifuatayo;
Kutotumia
badhi ya misamiati ya Kiswahili baadhi ya watumiaji wa lugha hupenda
kuchanganya maneno katika lugha mbili hasa wasomi mfano. Nina degree (badala ya
shahada) ninafatilia job(kazi) nimekumiss(nimekukosa)nk.
Lugha
inapokuwa na maneno mengi sana ya kukopa kiasi cha kupelekea kukopa kubadilika
kwa kugha husika na kuwa kama lugha nyingine hali hiyo itadumaza lughaa hiyo na
hatimaye kutumika kwa lugha ambayo maneno yake ni mengi mfano, waasisi wa dini
ya kiislamu nghini Tanzania walikizidishia msamiati ya kiarabu katika lugha ya
Kiswahili kuwa kama kiarabu.
12.“Tungo ni sentensi na
sentensi ni tungo” kubali au kataa kwa kutoa sababu za kiutalamu juu ya usemi
huo (NECTA 2005) swali la 5
Tungo ni matokeo ya kuweka na
kupanga pamoja vipashio sahihi kwa lengo la
kujenga vipashio vikubwa zaidi. Kuna ain nne (4) za tungo neno, kishazi, na
sentensi
Sentensi ni kifungu cha
maneno/neno chenye kiima na kiarifu ambacho hutoa
taarifa kamili si kweli kwamba sentensi ni tungo na tungo ni sentensi kutokana
na tofauti zifuatazo
Maana,tungo ni matokeo ya
kupanga na kuweka pamoja vipashio sahihi ili kujenga
vipashio vikubwa zaidi lakini sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja
na kuendelea chenye kiima na kiarifu na inatoa maana iliyokamili.
Aina, kuna aina nne za tungo
ambazo nni neno, kirai, kishazi, na sentensi lakini
sentensi ina aina nne ambazo ni sentensi shurutia, sahili, ambatano na
changamano.
Si kila tungo inatoa maana
kamili mfano kirai, kishazi tegemezi vinaposimama peke
yake havileti maana lakini kila sentensi huleta maana kamili
Kuonesha hali mbalimbali
si kila tungo huonesha hali mbalimbali mfano neno, kirai lakini sentensi
huonesha hali mbalimbali mfano hali ya maulizo kushangaa, ombi, kuamuru
Muundo si kila tungo ina muundo
wa kiima na kiarifu bali sentensi ina muundo wa kiima na
kiarifu au muundo wa kirai nomino KN na kirai kitenzi (KT)
13. Kwa kutumia lugha onesha kazi tano (5) za
mofimu “ku” (Necta 2007) swali la 5
Jibu
Mofimu
ni kipashio kidgo kabisa cha kiisimu chenye maana ya kisarufi au ya kileksika,
mofimu hujidhihirisha maana yake kwa kisarufi amabapo uundaji wa maneno
unaambatanishwa na viambishi katika mzizi wa neno mfano lim- analim,
a-na-cheza, tulisafir nk. Na katika maana ya kileksia kipashio hicho huwa ni
sehemu ya neno ambalo haliambatanishwi na kiambishi linajitosheleza lenyewe
mfano kaka, babu, maji, mbuzi nk.
Vilevile
mofimu inasifa ya kutokugawanyika au kuvunja katika vipande bila kupoteza maana
pia mzizi wa neno nao ni mofimu zifuatazo ni kazi za mofimu “ku”
Huonesha
hali ya ukanushi katika njeo ya wakati uliopita ikiambatanishwa na pamoja
viambishi kanushi kama vile si, ha
Yakinishi Kanushi
Mfano Azizi alichelewa -
Azizi ha-kuchelewa
Prisca
alicheka - Prisca ha-kucheka
Inaonyesha kauli ya urejeshi
mtenda/mtendwa
Mfano
mazigo aliku – andika barua wewe
(mtendwa)
Felicia
ha-kumwona kujibu (mtenda)
Inaonyesha njeo ya wakati
uliopita
Mfano
Zainab ha-ku-imba siku ya idd
Inaonyesha ngeli ya mahali
(pa-mu-ku, ngeli 9)
Mfano
Kuhali kwenu kunapendeza
Mahali
kule kunavutia
Inanominisha vitenzi
Mfano
cheza – kucheza
Imba
– kuimba
Kuunda mzizi wa neno
Mfano
Fatuma anapenda kula maandazi
Kinasaidia ujenzi wa silabi
katika nomino
Mfano
kuta, Kulwa
14.“Hivi leo matumizi ya
Kiswahili ni makubwa ukilinganisha na yale yaliyomo kwenye kamusi ya Kiswahili
sanifu .Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano hai. (1983)”(Necta 2004 swali la 9)
Maana ya matumizi ya Kiswahili
na Kamusi
Kamusi
ni kitabu cha orodha ya maneno yaliyopangwa kwa mujibu wa alfabeti pamoja na
maana na maelezo yake. Kuna aina mbalimbali za kamusi; Lugha moja peke yake na
kuna kamusi inayohusisha lugha mbili mfano Kiswahili – kiingereza.
Hivi leo matumizi ya Kiswahili
ni makubwa tangu mwaka 1983 kamusi iliyoandikwa kipindi
hicho mpaka sasa kuna vipindi mbalimbali tumepitia vyenye matukio mbalimbali
hivyo kila tukio huwa lina msamiati mipya inayoibuka na kuongezeka kwa maneno
mapya ambapo awali hayakuwepo kwenye kamusi iliyokwisha tolewa/andikwa. Baadhi
ya maneno yanayoibuka husanifiwa na vyombo husika vya Kiswahili na kuwa lugha
sanifu.
Vile vile kuna istilahi za
maneno ambazo huhitajika kuundwa kutokana na ongezeko
la sayansi na teknologia na kupitia vipindi mbalimbali vyenye matukio tofauti
tofauti hivyo hulazimu hubadilika kutokana na historia huwa ni tofauti na
kipindi kingine.
Tangu
mwaka 1983 kuna matukio ambayo tumepitia kama vile wakati wa ulegezaji wa
masharti ya biashara nchini, wakati wa mfumo wa vyama vingi.
Kipindi cha ulegezaji wa
masharti ya biashara nchini baadhi ya maneno yalizuka na
kuanza kutumika katika jamii ambayo hawali hayakuwepo kwenye kamusi ya mwaka
1983. Mfano utandawazi, uwekezaji vitega uchumi, ubinafsishaji n.k
Kipindi cha mfumo wa vyama vingi
nchini mwaka 1992 hadi leo. Pia kuna maneno mapya
yaliyojitokeza ambayo awali hayakuandikwa kwenye kamusi ya 1983 mfano
mkereketwa, mfurukutwa, mpambe, ngangari na hivyo ongezeko la matumizi ya
Kiswahili sasa ni kubwa ukilinganisha na mwaka 1983.
15.Fafanua
dhana ya kiunganishi huru kwa kutumia mifano dhihirisha tofauti kati ya
kiunganishi huru na aina nyingine ya ya kiunganishi.
Viunganishi
ni maneno, kikundi cha amneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi,
au sentensi.
Dhima
ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa na kisarufi.
Viunganishi huru.
Ni
viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo katikati ya vipashio vinavyoungana
japokuwa baadhi ya kiunganishi huweza kutoka kabla ya vipashio vinavyoungwa.
Mfano. Nilitembea hata nikachoka
Hata
ukiniimbia sitakubali
Tofauti ya kiunganishi huru na
aina nyingine ya kiunganishi
i. kiunganishi
huru huonyesha nyongeza
mfano
Baba
na mama wamekwenda shambani.
ii.Viunganishi huru
huonyesha sababu
Mfano
Juma
alipigwa kwa sababu alitoroka
Kwa vile
nimerusiwa nitarejea nyumbani.
iii.
Viunganishi
huru huonyesha utenzi au chaguo.
Mfano Sitaki pilau wala ndizi
Utamwandikia
barua ama utampigia simu
iv.
Viunganishi
huru huonyesha ulinganishi au unyume
Mfano Juma alikuwa Maskini ingawa aliikuwa mchezaji
Pamoja
na elimu yake musa hakuwa na huruma.
v.Viunganishi
huru huonyesha wakati
Mfano Sara alitoroka kisha Haruna akamfuata
Tulisafiri
mpaka Tanga badaye tukaelekea
Mombasa.
vi.
Viunganishi
huru huonyesha mashrti.
Mfano
Kama unataka kufaulu soma kwa bidii.
Mahindi
yatastawi endapo utawekea mbolea.
16.Tofauti
kati yakiambishi awali na kiambishi tamati
a)
Viambishi awali ni viambishi ambavyo
huwekwa kabla ya mzizi wa neno. Na kwa kawaida hutokea upande wa kushoto wa
mzizi.
Mfano:
Anaimba
A-na
– viambishi awali
Imb
– mzizi wa neno
A
– kiambishi tamati
a)
Viambishi tamati ni viambishi ambavyo
hupachikwa ndani baada ya mzizi wa
neno.
Mfano.
Anacheza
A-na
– viambishi awali
Chez-mzizi
wa neno
a-
Kiambishi tamati
17.“Mofimu
huru zina hadhi ya neno” fafanua husemi huu kwa kutumia sentensi tano (5)
tofauti.
Mofimu
huru ni mofimu ambazo huundwa kwa umbo linalojitosheleza kimaana.
Mfano
i.
Lilian
ni mwanafunzi wa shule ya sekondari tegeta.
N
ii.
Mtoto mdogo analia
V
iii.
Isaya na pascal wanaimba
U
iv.
Mungu anasema samehe mara saba
sabini.
T
v.
Simu i mezani.
t
19.Wewe kama afisa manunuzi.
Andika barua kwa mfanya biashara mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la
bidhaa.
WILAYA YA KASULU
S.L.P 3456,
KIGOMA
13/8/2014
ELICIA
BOOK SHOP
S.L.P
4784
DAR
ES SALAAM
Ndugu;
YAH: AGIZO LA
BIDHAA
Mimi
ni Afisa mnunuzu wa bidhaa mbalimbali, tafadhari naomba uniletee bidhaa
zifuatazo.
i.
Vitabu vya Kiswahili kidato cha
5-6 20@15000
ii.
Vitabu vya phsics (oxford book 3) 30
@12000
iii.
Vitabu vya geography (oxford book
3-5) 50 @ 15000
iv.
Counter book (quire 3) 50 @ 3000
v.
Vitabu vya history (oxford book 5-6)
40 @ 2000
Ninaambatanisha
pamoja na hundi ya shilingi Milioni mbili 2,000,000/= ambayo ni gharama ya
ununuzi pamoja na usafirishaji, Ninaomba bidhaa hizo zitumwe kwenye basi la
“ulakozi trans”.
Wako katika kazi,
PRAXCEDA PROTAS
AFISA MNUNUZI.
20. Mofimu tegemezi zina kazi
nyingi katika neno.
Taja
kazi (tano) 5 na uzielezee kwa kutumia Mfano.
Mofimu
Tegemezi ni mofimu ambazo hufungamana na mofimu zingine na hazijitosherezi
katika maana hutegemeana ili kueleza dhamira iliyokusudiwa.
i.
Mofimu tegemezi huonyesha njeo/wakati
Mfano. Nitaimba
ii.
Mofimu tegemezi huonyesha urejeshi
Mfano.
Mtoto aliyeanguka
iii.
Mofimu tegemezi huonyesha ukanushi.
Nimesoma
– Sijasoma
iv.
Mofimu tagemezi huonyesha nafsi
Mfano.
Nimekuona – Nafsi ya pili umoja ‘mtendwa’
v.
Mofimu tegemezi huonyesha hali
mbalimbali
Mfano. Ukija utamkuta – masharti.
21. Eleza tofauti tano za barua
ya kindugu (kirafiki) na barua rasmi (kikazi)
Barua ya kindugu ni barua ya inayoandikwa kwa
ajili ya kusalimiana, kutoa shukrani nk.
Wakati barua ya kikazi ni barua inayoandikwa kwa
ajili ya kuomba kazi, kuagiza vifaa, kumwalika kiongozi, kuomba ruhusa na
mengineyo.
Barua
ya kirafiki huwa na anwani moja ya maandishi tu. Wakati barua rasmi (kikazi)
huwa na anwani mbili, anwani ya mwandishi na mwandikiwa.
Barua
ya kirafiki (kindugu) huwa haina kumbukumbu namba wakati barua rasmi (kikazi)
huwa na kumbukumbu namba ya mwandikiwa.
Barua
ya kirafiki (kindugu)huwa haina kichwa cha habari wakati barua rasmi (kikazi)
huwa n a kichwa cha habari kuhusu jambo Fulani. Mfano Kuomba kazi
Barua
ya kirafiki (kindugu) huanza na salaam wakati barua ya kikazi (rasmi) huwa aina
salamu.
Barua
ya kirafiki (kindugu) haina sahihi ya mwandishi wakati barua ya kikazi huwa na
sahihi ya mwandishi.
22. Fafanua misemo ifuatayo.
i.
Mungu si athumani
ii.
Kata mzizi wa fitina
iii.
Mtu kidole
iv.
Kondoo si mali
v.
Kuiba kauli
Mungu si athumani
Maana
yake Mungu ni Mungu si mwanadamu umuhimu wa msemo huu ni kwamba. Mungu hatendi
kama mwanadamu.
Kata mzizi wa fitina
Maana
yake ni kuondoa chanzo cha ubaya au fitina umuhimu wa msemo huu ni kuondoa
chanzo au mzizi.
Mtu kidole
Maana
yake mtu hatambuliki kwa kunyoshea kidole, umuhimu wa msemo huu ni kwamba
hutambulika kwa mazuri na mabaya.
Kondoo si mali.
Maana
yake ni kumdharau mtu au kumshusha thamani/hadhi, umuhimu wa msemo huu,
tusimdharau mtu wala kumshusha thamani.
Kuiba kauli
Maana
yake ni kuchangia jambo lisilokuhusu. Msemo huu unatufundisha kuwa tusifuatilie
mambo yasiyotuhusu.
23. . Kwa kutumia sentensi;
Onyesha maana ya kila neno kwa maneno yafuatayo.
AU
Maneno yafuatayo ni tata kwa
kila neno tunga sentensi zenye maana zaidi ya moja.(Necta 2004 swali 7 na Necta
2006 swali la 7)
a. Kata
Ø Ni
kitendo cha kugawa kitu katika vipande kadhaa.
Ø Ni
eneo Fulani la kijografia
b.Panda
Ø Kufukia
mbegu ardhini.
Ø Kukwea
mlima au mti.
c. Paa
Ø Sehemu
ya juu ya nyumba
Ø Mnyama
wa porini anaye fanana na mbuzi.
Ø Enda
juu.
d.
Kamba
Ø Aina
ya samaki
Ø Uzi
unaotokana na nailoni unaotumika kufungia kitu.
e. Mbuzi
Ø Ni
mnyama wa kufugwa
Ø Kifaa
cha kukunia nazi
f. Nyanya
Ø Ni
kiungo.
Ø Mzazi
wa kike wa baba au mama
g.Kima
Ø Ni
mnyama jamii ya nyani.
Ø Ni
kipimo
h.Kifaru
Ø Kifaa
cha vita
Ø Mnyama
wa porini
i. Juma
Ø Ni
jina (nomino)
Ø Jumla
ya siku saba
j. Shinda
Ø Faulu/fanikiwa
Ø Kaa
mahari kwa muda mrefu.
k.Tupa
Ø Kifaa
cha kunolea
Ø Rusha
kitu mbali
l. Meza
Ø Samani
Ø Kitendo
cha kutia kitu kinywani.
m.
Ua
Ø Kitendo
cha kutoa/kuondoa uhai kwa mtu au mnyama
Ø Pambo
n.Kaa
Ø Kipande
cha moto
Ø Kuweka
makalio chini
Ø Mdudu
wa majini/nchi kavu
o.
Jiko
Ø Mahali/kifaa
cha kupikia
Ø Mke
p.
Kanda
Ø Eneo
Fulani lenye misingi ya kisiasa na kijamii
Ø Kitendo
cha kuchanganya unga na maji ili kutengeneza bonge la maandazi, chapati nk.
q.
Mama
Ø Mzazi
wa kike
Ø Jinsia
ya kike.
r. Koo
Ø Sehemu
ya mwili wa binadamu
Ø Chimbuko
la udugu
s. Kibibi
Ø Kufanya
mambo kizee.
Ø ………………………………………………
t. shuka
…………………………………………
u.Wali
Ø Wasichana
waliowekwa ndani kwa ajili ya mafunzo.
Ø Chakula
cha wanga kinachotokana na mpunga.
24. Unganisha tungo zifuatazo
kwa kutumia o-rejeshi
(nectar 2013 swali la 4)
O-REJESHI
Ni
kiambishi kinachotumiwa kurejelea kwenye nomino ambayo huwa imetajwa kabla ya
kitenzi chenyewe kutajwa.viambishi hivi ndivyo vinavyosababisha utegemezi
katika sentensi.
Utegemezi
ni hali ya kipashio kimoja kutegemea kipashio kingine.
O-rejeshi
ni viambishi rejeshi vinavyotaja mtenda, mtendwa, mtendewa, wakati,hali au
sababu kama mazingira ya kutokea jambo Fulani au jingine.
MAZINGIRA YA UTOKEAJI WA
O-REJESHI
O-rejeshi
hutokea katika mazingira mbalimbali ya neno. Huweza kutokea katikati,mwishoni
au katika mzizi wa “AMBA”. mazingira hayo ni kama yafuatayo.
a. Kirejeshi
kinachopachikwa katikati
Hapa huwa ni O-rejeshi ambayo
huambikwa katikati ya viambishi awali kadhaa na mzizi wa kitenzi. Huwa na
muundo wa: Awali+Rejeshi+Mzizi.
Mfano. Mwalimu aliyesafiri jana
amerudi leo
Kisu kilichopotea jana
kimeonekana leo.
Nguo iliyochanika imetupwa
b.O-rejeshi inayopachikwa mwishoni
Hapa huwa na kilejeshi ambacho
hupachikwa mwishoni mwa kitenzi. Muundo wake huwa.
Kitenzi+Rejeshi. Viambishi hudokeza
mazoea
Mfano. Samba aungurumaye ni mkali
Jino liumalo hung’olewa.
c. O-rejeshi
hupachikwa kwenye mzizi wa AMBA
Umbo la AMBA hupachikwa kirejeshi mwishoni
na kuwa na muundo wa AMBA+Rejeshi.
Iwapo mzizi wa AMBA umetumika,
kirejeshi huweza kutokea mwishoni tu mwa mzizi huu na hakiwezi kurudiwa tena
katika kitenzi kingine.
Mfano, Kitabu ambacho umesoma kimechanika
Juma amepata adhabu ambayo haiwezi
Mtoto ambaye hatafaulu hatapewa zawadi
Unganisha
tungo zifuatazo kwa kutumia O-rejeshi.
a.
Mafisadi wamekamatwa. Mafisadi
wamefikishwa mahakamani.
Mfisadi
waliokamatwa wamefikishwa
mahakamani.
b.
Kitabu kimenunuliwa. Kitabu kipo
madukani.
Kitabu
kilichonunuliwa kipo kabatini.
c.
Mfadhili amepatikana. Mfadhili
mkarimu sana
Mfadhili
aliyepatikana ni mkarimu sana.
Eleza maana ya Istilahi
zifuatazo
i. Esperanto
ii.Pijini
iii.
Lahaja
Jibu
a. Esperanto
Ni
lugha sesere iliyoundwa na binadamu lugha hiyo ilikusudiwa kutumika kama lugha
ya pili ya kimataifa huko ulaya.
b. Pijini
Ni
lugha inatozuka baada ya makundi mawili au zaidi kukutana kila moja
likizungumza lugha yake. Ili waweze kuwasiliana, kila moja katika makundi hayo hujaribu
kurahisisha muundo wa lugha na sarufi yake, msamiati n.k. Ili kupata lugha
rahisi itakayowezesha kuwasiliana. Lugha ambayo huzuka huitwa pijini.
c. Lahaja
Ni
tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika lugha kuu yenye asili moja. Tofauti
hizo zipo katika matamshi (lafudhi),maumbo au matumizi ya maneno
AU
Ni
upashanaji wa habari kwa kutumia ishara au sauti za nasibu unaotumiwa na
kikundi Fulani cha watu.
Vitenzi vya Kiswahili vina tabia
yake. Kwa kutumia mifano ya sentensi tano (5). Onyesha tabia tano (5) za vitenzi.
Jibu
Vitenzi
ni aina ya neno linalotoa taarifa juu ya tendo linalofanyika au linalotendwa na
kiumbe au kitu.
AU
Ni
neno linaloeleza jambo lililotendwa au jambo lililotendeka. Kitenzi au vitenzi
huarifu tendo linalofanyika au linalofanywa na mnyama, mtu au kiumbe chochote
kinachoweza kutenda jambo kama vile.:
Soma,
imba, kimbia, andika, sikiliza, kula, kunywa, lala, uliza, amuru nk.
Vitendo
vya Kiswahili havisimami pekee vinapotumiwa katika tungo, bali huambatana na
viwakilishi vingine vyenye kuwakilisha mtenda wa tendo au mtenda.huambishwa pia
viambishi vyenye kuonyesha wakati tendo linapofanyika kama vile:
Dada a-na-soma
Watoto wa-na-ruka
AINA ZA VITENZI
i.
Kitenzi
kikuu (T)
Ni
kitenzi ambacho kinaweza kujitokezapekee katika sentensi.
AU
Ni
vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi. Kitenzi kikuu lazima
kiwepo katika sentensi, kwani ndicho hubeba maana ya kimsingi ya sentensi.
Huitwa kitenzi kikuu hasa kinapoandamana na kitenzi kisaidizi.
Mfano
Mchezaji
anacheza mpira
T
Mary
anaimba nyimbo
T
Anna
anaandika barua
T
ii.
Vitenzi
visaidizi (TS)
Ni
vitenzi ambavyo hutoa taarifa ya kusaidia kitenzi kikuu. Hutoa kama vile uwezekano, wakati hali n.k. Vitenzi
visaidizi daima hutumika pamoja na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi
vya wakati.
Mfano Mtoto alikuwa anacheza mpira
TS T
Juma
amewahi kunitembelea mara moja
TS T
Sisi
tutakuwa tumelala
TS
T
iii.
Vitenzi
vishirikishi
Ni
vitenzi ambavyo hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi
Hushirikisha
kitu kitabia, kihali na kimazingira. Sehemu ya kiarifu, yaani iliyo na kitenzi
si kamilifu
Mfano:
Juma
ni Daktari
Mtoto
si mgonjwa
Vitenzi vya Kiswahili vina tabia
zifuatazo.
i.
Kuonyesha
wakati tendo linapofanyika
Mfano
A-na-lima wakati uliopo
A-li-lima wakati uliopita
A-ta-lima wakati ujao
ii.
Kuonyesha
hali ya tendo
Mfano:
A-na-lima
- hali ya kuendelea kwa tendo
Hu-lima
- hali ya mazoea
A-me-lima
- hali timilifu
A-nge-lima
- hali ya mashart
iii.
Kuonyesha
nafsi
Mfano
Ni-na-lima.
Tu-na-lima. Nafsi ya kwanza
U-na-lima.
M-na-lima. Nafsi ya pili
A-na-li-ma.
Wa-na-lima. Nafsi ya tatu.
iv.
Kuonyesha
hali mbalimbali za tendo.
Mfano
Baba
analima shamba
Lima
- kutenda
Limwa
- kutendwa
Limiwa
- kutendewa
Limika
- kutendeka
v.
Kuonyesha
urejeshi wa mtenda/mtendwa/mtendewa.
Mfano
Mwanafunzi
anayesoma ni mwelevu (mtenda)
Mwalimu
amempiga mwanafunzi mtoro (mtendwa)
Kwa kutumia mifano dhihirisha,
fafanua dhana zifuatazo (nectar 2012 swali la 3)
A. KIIMA (K)
Ni
sehemu katika sentensi ambayo hujaza nafasi ya mtenda au mtendewa jambo
linaloelezwa. Katika sentensi kiima hutokea kushoto mwa kitenzi
Mfano
Baba/amempiga
mtoto
K
Mtoto
amepigwa na Baba
K
Vipashio vya kiima
Kiima
huundwa na vipashio vifuatazo:-
i.
Nomino peke yake (N)
Mfano
Mtoto
/anacheza
mpira.
N
Daktari/anamtibu
mgonjwa
K
ii.
Nomino, kiunganishi na nomino (N+U+N)
Baba
na mama /wanalima shamba.
K
Kaka
na dada wanacheza
K
iii.
Nomino
na kivumishi (N+V)
Mfano
Watoto
wote/
ni wagonjwa.
K
Wakulima
wote/
wameondoka.
K
iv.
Kivumishi
na nomino
(V+N)
Mfano
Yule
mtoto/ ni mlevi
K
Kile
kipini /ni cha dhahabu
K
v.
Kiwakilishi
peke yake
Mfano,
Wangapi/wamesafiri
leo
K
Wewe/huna
matatizo
K
vi.
Kiwakilishi
na kivumishi
Mfano.
Vile
vyao/vilivyookotwa kule
K
Zile
zingine/zilikuwa imara
K
B. CHANZO (CH)
Ni
neno au kikundi cha maneno kinachojaza nafasi ya kielezi katika tungo. Chagizo
huweza kutokea mara baada ya kitenzi kikuu au baada ya kishamirisho.
Mfano:-
Mama
ansoma kitabu polepole
Ch
Mtoto
anacheza vizuri sana
Ch
SIFA ZA CHAGIZO
i.
Chagizo kwa kawaidahuwa ni kielezi au
kirai kielezi au kirai kihusishi ambacho kinafanya kazi kama kielezi
Mfano
Mary
anaonekana mnyonge mno
Ch
ii.
Hutumika kufafanua
kitenzi/kivumishi/kielezi.
Mfano.
Mbwa
hukimbia haraka sana
Ch
C. SHAMIRISHO
Ni
jina au kikundi jina kinachojaza nafasi ya mtendwa katika sentensi.
Shamilisho
hutokea baada ya kitenzi kikuu au baada ya kitenzi kishirikishi
Mfano
Juma
analima shamba letu
D. UTOHOAJI
Ni
kulichukua neno kulifanyia marekebisho Fulani na kulitumia ili liendane na
kanuni na taratibu zilizoko katika lugha husika
Mfano.
Shirt
- shati
Skirt
– sketi
Cake
– keki
E. URUDUFISHAJI
Ni
hali ya kurudia rudia neno ili kuunda neno linguine
Mfano
Pole
– polepole
Kimya
– kimyakimya
Moja ya sifa za sentensi za
Kiswahili ni kuonyesha hali mbalimbali. Fafanua kwa hoja tano (5) ukitoa mifano
kwa kila moja (mock 2014-dar swali la 5)
i.
Hali ya kuendelea kwa tendo.
Mfano
Alifika
shuleni akilia.
ii.
Hali ya masharti
Mfano
Mwanafunzi
akisoma atafaulu mtihani.
iii. Hali timilifu
Mfano
Neema amekula chakula
iv.Hali ya kuamuru
Mfano
Nenda
Eleza
njia zilizotumika kuunda kila moja ya maneno haya.(mock 2014 dar swali la )
a. UDA
Ufipishaji
au kufupisha kikundi cha maneno. Silabi kutoka katika baadhi ya maneno ya
kikundi huchaguliwa ili kupata neno moja/jipya
Usafiri Dar es
salaam
b. UGILIGILI
Kuchukua
maneno. Maneno huchukuliwa kutoka makabila mbalimbali ya kibantu. Ugiligili
(kimiminika) kinyakyusa.
c. ASKARIKANZU
Miambatano
au kuambatisha maneno. Ni kuweka pamoja maneno mawili au zaidi ili kupata neno
jipya.
Askari
+ kanzu= askarikanzu.
d. MAREHEMU
Utoaji
au kutohoa maneno.
Ni
kulichukua neno kutoka lugha nyingine (ya kigeni ) na kufanyiwa marekebisho ya
kisarufi na kutumika katika lugha husika.
Marehemu
– Almarhum (kiarabu)
e. UMEME
Kutafsiri
neno.
Ni
kulipa maana neno kama linaloelezwa katika kamusi.
Electric
– umeme.
Kwa kutumia tungo kati ya
zifuatazo. Onyesha kivumishi kisha bainisha aina ya kivumishi husika (nectar
2011 swali la 4)
a.
Kikombe cha kaka kimevunjika
Cha
kaka – kivumishi cha
A
– unganifu
b.
Wachezaji wenu wanatafuta mpira.
Wenu
– kivumishi kishirikishi
c.
Msichana mrembo amejikwatua
Mrembo
– kivumishi cha sifa
d.
Viatu vyote vimechafuka
Vyote
kivumishi cha pekee
e.
Wanafunzi wachache wamenunua vitabu
Wachache
– kivumishi cha idadi
Bainisha kauli zinazowakilishwa
na vitenzi vilivyotumika katika katika sentensi zifuatazo.(nectar 2013 swali la
5).
a.
Refa alichezesha mechi vizuri
Kauli
ya kutendesha.
b.
Pili amevunjwa mguu
Kauli ya kutendwa
c.
Wanafunzi wanasomeana kitabu
Kauli ya kutendana
d.
Mafuta yamemwagika
Kauli ya kutendeka
Kwa
kutumia mifano taja miundo mitano ya kirai nomino (KN) (nectar 2012 swali la 7)
Ni aina ya kirai
ambacho hufanya kazi kama nomino. Neno kuu la kirai nomino ni nomino au
kiwakilishi cha nomino kinaundwa na:-
i.
Nomino peke yake
Mfano
Chakula kinapikwa
KN
ii.
Kiwakilishi peke yake
Mfano
Wao
wataondoka kesho mchana
KN
Chako
kimepotea kabisa
KN
iii.
Nomino, kiunganishi na nomino
Baba
na mama wanapika
KN
Neema
na Baraka wamesafiri
KN
iv.
Kiwakilishi na kivumishi
Mfano
Vile vyao viliokotwa kule
KN
Wengi
wao
hawapendi ngoma za asili.
KN
v.
Kivumishi na nomino
Kile
kiti
kinapendeza
KN
Maneno huweza kubadilika kutoka
aina moja na kuwa nyingine” Dhihirisha kauli hii kwa kubadili maneno yafuatayo
kwa kuzingatia maneno yalioko kwenye mabano (nectar 2012 swali la 4)
a.
Mkono (badili kuwa kielezi)
Mkononi
b.
Kwenda (badili kuwa nomino)
Mwendo
c.
Bora (badili kuwa kitenzi)
Ubora
d.
Ogopa (badili kuwa kivumishi)
Mwoga
e.
Mzazi (badili kuwa kitenzi)
Mlezi
f.
Bisha (badili kuwa kivumishi)
Mbishi
g.
Refu (badili kuwa kitenzi)
Ndefu/urefu
h.
Linda (badili kuwa nomino)
Lindo
i.
Kabati (badili kuwa kielezi)
Kabatini
j.
Uguza (badili kuwa nomino)
Muuguzi
Eleza maana ya dhana zifuatazo
kama zinavyotumika katika kamusi.
i.
Matini
Ni
sehemu ya vidakizo vyote vya kamusi husika kuanzia herufi za alfabeti a – z
ii.
Kidahizo
Ni
neno lolote linaloingizwa katika kamusi na kupewa fasihi yake.
iii.
Sherehe
Ni
taarifa ambazo huingizwa mwishoni mwa kitabu kama kiambatanisho.
iv.
Kitomeo
Ni
aya ndogo katika kamusi zenye vidakizo na maana yake.
Wakilisha
Fanya
kitu kwa niaba ya mtu mwingine.
Mfano
Yohana
alimwakilisha baba yake kwenye
harusi ya dada yake.
Wasilisha
Ni
kitendo cha kupeleka kitu/vitu.
Mfano
Mwalimu
wa zamu aliwasilisha Orodha ya mahudhulio
ya wanafunzi.
Kodi
Ni
kulipa ushuru au kitu ……………………
Mfano:-
Mamlaka
ya mapato imekusanya kodi katika maduka ya mtaa wa wazo.
Kodisha
Ni
kitendo cha kumpa mtu kitu atumie kwa malipo.
Mfano
Neema
amekodisha ukumbi wa home boys.
Kula
Ni
kitendo cha kuweka kitu mdomoni na kukimeza.
Mfano
Babu
anakula chakula.
Kura
Ni
kitendo cha kumchagua mtu ili ashike wadhifa Fulani (uongozi Fulani) kwa
kuandika karatasi ya siri au kunyoosha mkono.
Mfano
Wanakijiji
walipiga kura ili kumchagua mwenyekiti wao.
Baada
Ni
kitendo kinachotarajiwa kufanyika (matarajio)
Mfano
Nitakuja
baada ya kumaliza kula chakula cha mchana.
Badala
Niaba
ya kitu Fulani.
Mfano
Nilienda
arusini badala ya baba.
Onesha
Kueleza
uelekeo Fulani
Mfano
…………………
Onyesha ……………..
Kwa kutumia mifano. Fafanua
dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika fasihi (nectar 2013 swali la 11).
a. Tashibiha
Ni
tamathali inayounganisha vitu kwa kutumia viunganishi kama vile mfano wa,
mithili ya, kana kwamba, sawa na, nk.
Mfano
Juma
ni mweupe kama vyeta.
Saimon
alifoka kwa hasira mithili ya samba.
b. Takriri
Ni
kurudiarudia maneno kwenye sentensi au kwenye usemi ambayo nia yake ni
kusisitiza
Mfano
Neema
ni mwembambamwembamba sana.
c. Sitiari
Ni
tamathali inatolinganisha matendo, vitu au tabia ya vitu vyenye maumbile
tofauti bila viunganishi.
Mfano
Askari
Yule ni samba
Nywele
za mary ni chafu
d. Tashihisi
Ni
tamathali ambayo vitu visivyo na sifa walizonazo watu hupewa sifa hizo.
Mfano
Majani
yote porini yalishangilia kwa vigelegele.
Manyunyu
ya mvua hatimaye yaliimba wimbo kwa furaha.
e. Tanakari sauti
Ni
mbinu ya kuiga sauti ya milio mbalimbali. Milio hii ni ya wanyama, magari, vitu,
nk.
Mfano
Alianguka
chini pu!
Alitumbukia
majini chubwi!
f. Tafsida
Ni
tamathali/mbinu ya kupunguza ukali wa maneno au matusi katika usemi.
Mfano
Naenda
jikoni na wala si kupika.
Amejifungua
badala ya amezaa
Vishazi tegemezi hufanya kazi ya
vivumishi viwapo katika tungo. Onyesha ukweli wa kauli hito kwa kutumia mfano
mine (4) ya sentensi.
Vishazi Tegemezi (K/TG)
Ni
kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kisaidizi, ambacho muundo wake hukifanya
kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa kishazi
tegemezi peke yake hakitoi ujumbe unaojitosheleza.
Mfano
Kitabu
kilichopotea juzi
Mwanafunzi
anayesoma sana.
Kishazi tegemezi cha weza kutoa
maana kamili kinapoandamana na kishazi huru
Mfano
Kitabu
kilichopotea juzi kimepatikana leo.
K/TG/V
Mwanafunzi
anayesoma sana amefaulu.
K/TG/V
Hali
hii tegemezi inakinyima kishazi tegemezi hadhi ya kuwa sentensi.
Vishazi
tegemezi namana vinavyofanya kazi kama vivumishi.pale vinapotokea na nomino
inayovumishwa
Mfano
a. Kiti
kilichopotea jana kimeonekana
K/TG
b.Uzi ulionunuliwa
jana haufai kabisa
K/TG
Pale
visipotokea na nomino inayovumishwa
c. Uliyemwona
jana
anaondoka kesho asubuhi
K/TS
d.
Aliyekuwa katibu
kata wetu amehama
K/TS
Huku ukitumia mfano mmoja mmoja, taja
sifa nne za kishazi tegemezi.
Kishazi tegemezi, ni kishazi ambacho
muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa
ujumbe uliokusudiwa.
Sifa
za kishazi tegemezi.
i.
Kishazi tegemezi hakiwezi kutoa maana
kamili kama hakikuambatana na kishazi huru.
Mfano Mtoto aliyekuja jana.
ii.
Kishazi tegemezi kinaweza kikafutwa
katika sentensi bila kuharibu maana kamili ya sentensi.
Mfano.
Mwalimu aliyefundisha jana ni
mkarimu.
iii.
Kishazi tegemezi kinaweza kutanguliwa
na kufuatwa na kishazi huru.
Mfano Nilimwona Tina
nilipokuwa kanisani
Nilipokuwa kanisani
nilimwona Tina
iv.
Kishazi tegemezi kinaweza kutambulika
kwa kuwa na viambishi rejeshi vinavyoambatanishwa katika vitenzi.
Mfano Kitabu
kilichopotea jana kimeonekana
v.
Kishazi tegemezi kinaweza kutambulika
kwa kuwepo vivumishi tegemezi kama vile ingawa, kwamba.
Mfano.
Mwalimu amesema kwamba wanafunzi wengi hawana nidhamu.
Fafanua
dhima ya viambishi vilivyopigiwa mstari katika vitenzi vifuatavyo.
a.
Anacheza
Kuonyesha
njeo ya wakati uliopita.
b.
Tumelima
Kuonyesha
kauli ya kutenda
c.
Aliyekukumbuka
Kuonyesha
urejeshi
d.
Wangelisoma
Kuonyesha
masharti
Kama mtaalamu wa lugha ya Kiswahili.
Onyesha makosa ya kimantiki na ya kisarufi yanayosababishwa na wazungumzaji wa
lugha hiyo,
i.
Makosa
ya kisarufi
a. Matamshi
b.
Watu
wengi hushindwa kutamka baadhi ya sauti za Kiswahili.
Mfano.
Wakurya hutumia ‘r’ badala ya ‘l’
Naenda
kurara badala ya kulala
ii.
Makosa
ya msamiati
Baadhi
huchanganya msamiati wakati wa kuzungumza. Watu wengi huchanganya neno
mazingira na mazingira
Mfano.
Mazingira ya hapa ni machafu hii sio sahihi.
Mazingira
ya hapa ni machafu hii ndio sahihi.
Jack
amenenepa sana hii sio sahihi.
Jack
amenenepa sana hii ndio sahihi.
iii.
Makosa
ya kimuundo
Kwa
kawaida sentensi za Kiswahili huanza na nomino ya mtenda au mtenda na kufuatiwa
na kitenzi.
Mfano.
Eva anaandika vizuri.
Mzungumzaji
asiyefuata kanuni ya mpangilio wa maneno anaweza kusema. Vizuri
anaandika Eva.
iv.
Makosa
ya kuongeza vitamkwa
Mfano.
Amekwendaga - Amekwenda
Hapendagi
– hapendi
Mtoto
msafi – mtoto safi
v.
Makosa
ya kimantiki
Mantiki
ni utaratibu mzuri wa kufikiri. Makosa ya kimantiki ni yale yanayoonyeshwa kukosekana
kwa utaratibu wa fikra. Makosa ya kimantiki yanatokana na upofu wa mawazo ya
mzungumzaji.
Usimwage
kuku kwenye mchele wengi
Usimwage
mchele kwenye kuku wengi.
Mfupa
hauna ulimi.
Ulimi hauna mfupa.
Kwa kutumia mifano ya lugha ya Kiswahili,taja sababu 5 za Utata katika
mawasiliano.(Necta 2012 swali 6)
AU
Maneno au tungo za Kiswahili
zisipotumiwa kwa umakini zinaweza kueleweka hivi au vile na hivyo zinaweza
kupotosha lengo la Mzungumzaji,Fafanua sababu tano(5) za kutoeleweka kwa maneno
au tungo kwa mifano dhahiri.
Utata
ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja.
Mfano
Neno
“Barabara” lina maana zifuatazo,
Ø Ni
njia ipitawayo na magari na binadamu.
Ø Sawasawa,au
hakuna dosari.
Neno “Paa”lina maana zifuatazo;
Ø Mnyama
anayefanana na mbuzi
Mfano;Paa ni mnyama mwenye pembe ndefu
Ø Enda
juu au kwea angani
Mfano;Mwewe ni ndege anayepaa juu
sana
Ø Ni
sehemu ya juu ya nyumba
Mfano;Paa la nyumba ya shule
limeezuliwa.
Utata wa Sentensi ni hali ya
sentensi kuwa na maana zaidi ya moja.
Mfano;
Ø Mtoto
anaendesha.
-Mtoto
anaongoja chombo cha moto.
-Mtoto
maradhi ya tumbo.
Chanzo cha utata katika
sentensi hii ni neno ‘’Anaendesha’’
Ø Musa
amenunua mbuzi.
-Juma amenunua kifaa cha kukunia nazi
-Juma
amenunua mnyama afugwaye
Chanzo
cha utata ni neno Mbuzi.
SABABU ZA UTATA KATIKA MANENO AU
SENTENSI
Ø Neno
kuwa na maana zaidi ya moja
Mfano;
ü Nileteeni
nyanya
-Nileteeni
kiungo/tunda
-Nileteeni
mzazi wa kike wa baba au mama
ü Sipendi
buibui
-Sipendi
mdudu anayejenga tandabui.
-Sipendi
vazi linalovaliwa na wanawake wa kiislamu.
Ø Utumiaji wa maneno yenye maana
ya picha au maana iliyofichika.
Mfano;
ü Nina
ua nyumbani kwangu.
-wigo
-kutoa
uhai wa mtu au kiumbe
-Binti
mzuri
-Mmea
unaopendezesha.
Ø Kutozingatia taratibu za uandishi.
Mfano;
Tulimkuta
Neema na rafiki yake,huruma.
Tulimkuta Neema na rafiki yake Huruma.
Sentensi
ya kwanza ina maana kuwa tuliwakuta
watu wawili yaani Neema na rafiki wa
Neema aitwaye Huruma.
-Alama
ya mkato baada ya neno “yake” huonyesha kuwa taarifa imekamilika na neno
“Huruma”ni Ufafanuzi tu wa “rafiki yake”
Sentensi
ya pili ina maana kuwa tulimkuta
Neema na mtumwingine ambaye ni rafiki wa Huruma.
ü Kutumia neno bila kuzingatia
mazingira au muktadha.
Mfano;Jeremia
ametumwa na Rehema.
Katika
sentensi hii ,msikilizaji na mzungumzaji wataelewana iwapo wote wanawajua
Jeremia na Rehema na hali ya uwezekano wa yupi kumtuma mwingine.
ü Kuwepo kwa mofimu za kauli ya
kutendea /li/le/i/ na e/
Mfano;
Amempig-i-a ngoma.Sentensi ina maana
zifuatazo;
I.
Amepiga ngoma ili amfurahishe.
II.
Amepiga ngoma kwa niaba yake.
III.
Amempiga kwa kutumia ngoma.
Nyambua mzizi “lima” ili upate
kauli zifuatazo za matendo (tahossa dar 2009)
a.
Kutenda
Lima
b.
Kutendeka
Limika
c.
Kutendwa
Limwa
d.
Kutendewa
Limiwa
e.
Kutendeka
Limika
f.
Kutendesha
Limisha
Eleza dhima za mofimu
zilizopigiwa mistari (tahossa Dar 2009)
i.
Kijana aliyewasili ni shupavu.
Inaonyesha
urejeshi.
ii.
Kiti kimevunjika
inaonyesha
umoja (ngeli ya 4, ki-vi)
iii.
Akija
nitafurahi
Inaonyesha
masharti
iv.
Kijana
hodari atoke mbele
Inaonyesha
umoja katika nomino.
Sentensi zifuatazo zina makosa.
Ziandike tena kwa kuepuka makosa hayo:-
a.
Ni budi kuoomba radhi kwa yaliyotokea
Sina budi kuomba radhi kwa
yaliyotokea
b.
Maziwa ya motto yameingia nzi.
Nzi ameingia kwenye maziwa ya mtoto.
c.
Naomba uninunulie maembe kumi na
mbili
Nakuomba uninunulie maembe kumi
na mawili.
d.
Dhumuni la barua hii ni kutaka hali
yako.
Dhumuni la kuandika barua hii ni
kukujulia hali.
Nominisha
vitenzi vifuatavyo kisha tunga sentensi moja kwa kila nomino.
a.
Hawili-Uhamisho
Baba
aliamishwa kutoka Dar kwenda Mombasa.
b.
Ghadhibika – Ghadhabu
Ghadhabu
yake haiwezi kuisha mpaka utubu.
c.
Afiki – Mafikiano
Mwalimu
na mwanafunzi walifikiana kufanya masahihisho ya mtihani.
d.
Laumu – Lawama
Musa
aliwalaumu sana watoto.
e.
Kumbuka – Kumbukumbu
Tarehe
14/10/ ni kumbukumbu ya Baba wa Taifa.
f.
Penya/Kipenyo/Mpenyo
Mwizi
alipata mpenyo wa kupita akavunja duka.
Andika nomino tano
(5) zinazoweza kuingia katika ngeli ya YU-A-WA, kasha tunga sentensi yenye
Umoja, Wingi kwa kila nomino huku ukizingatia upatanisho wa kisarufi (mock Dar
2012 swali la 5)
NOMINO
i.
Msichana
ii.
Panzi
iii.
Nzi
iv.
Kiwete
v.
Kiongozi
Umoja
Wingi
i.
Msichana anaimba Wasichana wanaimba
ii.
Panzi anaruka Panzi wanaruka
iii.
Nzi ananuka Nzi wananuka
iv.
Kiwete anatembea Viwete wanatembea
v.
Kiongozi yu aja Viongozi
wanakuja.
Fafanua
dhima ya “na” kama lilivyotumika katika
sentensi zifuatazo;
(Eastern
zone Education bord 2012)
(a)Ali
na Japhet ni marafiki.
Imetumika
Kuunganisha sentensi
(b)Tunafanya
mitihani
Inaonyesha
wakati uliopo
(c)Tangazo
lilitolewa na mkuu wa shule.
Imetumika
kama kihusishi
(d)
Nasi
tumefurahi.
Inaonesha
nafsi
(e)
Huyu anafanana na wewe.
Imetumika
kuwianisha/kufananisha
Nini maana ya upatanisho wa
kisarufi? kwa kutumia nomino zifuatazo taja ngeli zinazopatikana kutokana na
kanuni ya Upatanishi.(Eastern zone Education board-EZEB 2012)
a.
Kijana
b.
Uovu
c.
Kiti
d.
Ufa
Upatanisho wa kisarufi
Ni
uhusiano wa kisintaksia baina ya maneno ambapo neno moja hutawala umbo la
kimofolojia la neno au maneno katika tungo.
Mfano;Watoto wadogo wanasoma.
Nomino
(a)
Kijana
Ngeli
ya 4(ki-vi)
(b)Uovu
Ngeli ya 7(u-ya)
(c)
Kiti
Ngeli
ya 4(ki-vi)
(d)
Ufa
Ngeli
ya 6(u-zi)
“Kila Lugha ina tabia ya
kuchukua maneno kutoka lugha nyingine ili kukidhi mahitaji yake
kimsamiati”.fafanua kauli hii ukitumia maneno kumi (10) ya Kiswahili.(Necta
2011 swali la 4)
Msamiati
wa lugha Kiswahili uliongezeka na kukua kwa njia ya kuchukua maneno kama
yalivyo kutoka lugha nyingine kama ifuatavyo;
A.
Kiingereza
Kiswahili
i.
Tractor
Trekta
ii.
Number Namba
B. Kiarabu
Kiswahili
iii.
Saalam
salama
iv.
Mahabusu Mahabusu
C. Kireno
Kiswahili
v.
Bibo
Bibo
vi.
Mesa
Meza
D.
Kiajemi
Kiswahili
vii.Randah
Randa
vii.
Jamaadar
Jemedari
E.Kibantu kabila
ix.
Ngeli
kihaya
x.Kitivo
kipare
Yapange maneno yafuatayo kama
yanavyoonekana katika kamusi ,kisha eleza maana ya kila neno kwa kutoa mfano
mmoja(1) wa sentensi.
(a) Falsafa
(b) Barizi (c) Anuwai (d) Barubaru
(e)
Kinda
(f) Ajuza (g) Fanusi (h) Ghaibu
(i)
Goigoi (j) Kinanda.
Mpangilio wake;
(a)
Ajuza
-Mwanamke
mzee sana.
Mfano;
Ajuza
Yule anatembea polepole sana.
(b)
Anuwai
-Dhahiri
Mfano;
Wanafunzi
walijibu maswali yote kwa mifano anuwai
(c)
Barizi
-Punga
pepo
-Kusanyika
kwa watu kwaajili ya mazungumzo ya kawaida.
Mfano;
Baba
na Mama wamekwenda baharini kubarizi.
(d)
Barubaru.
-Kijana
wa kiume aliyekwisha kubalehe.
-Samaki
jamii ya papa.
Mfano;
Musa
ni barubaru wa mzee kisonga.
(e)
Falsafa
-Ni
elimu ya asili, maana na sababu ya za mambo au vitu.
-Busara,
hekima, mtazamo.
Mfano;
Falsafa
ya baba wa Taifa ilihimiza Umoja na Mshikamano.
(f)
Fanusi.
-Taa
ya mkono; kandili
Mfano;
Fanusi
ya Musa inachijiwa kwa siku moja.
(h)Ghaibu
-Mbali
Mbali na macho
Mfano;
Nyumba
ile ipo ghaibu yangu.
(i)
Goigoi
-Mtu
dhaifu
-Udhaifu
-Ngoma
ya kupunga shetani: ngoma ya pungwa
-Mtu
mvivu sana
Mfano;
Mtoto
wa Neema ni goigoi sana
(j)
Kinanda
-Chombo
kinachotoa sauti kwa kupulizwa au misumari yake.
Mfano;
Kinanda cha Musa ni kidogo kuliko cha Huruma.
Kwa kutumia mifano
taja kazi za alama zifuatazo; (pre-necta kanda ya Dar 2011 swali la 8)
a. Nukta
v Hutumika
kukamilisha sentensi.
Mfano; Baba yangu amefika
Hutumika
kuonyesha ufupisho wa maneno
Mfano; k.v- kama vile
K.m – kwa mfano
S.L.P - sanduku la posta.
v Hutumika
kuonyesha vipimo mbalimbali katika desimali.
Mfano:
Kilogramu 5.2
Mita 55:5
Saa 5:20
b. Nukta pacha
v Hutumika
kutaja maneno yaliyo katika orodha
Mfano;
Nililetee vitu hivi: wino,
karatasi, kalamu na kiti.
v Hutumika
kuashiria maneno ya msemaji
Mfano;
Alipomwona alimshambulia kwa
maneno.
Wewe ni jambazi na mwizi kweli
kweli.
v Hutumika
kutenganisha dakika na sekunde.
Mfano saa 5:56
Saa 4:15
v Hutumika
kuonyesha uwiano baina ya namba
Mfano 5:7 8:10
c. Mkato
v Hutumika
kuweka pumziko fupi katika sentensi
Mfano:
Tulipokuwa sokoni tulinunua
samaki, mchele na ndizi.
v Hutumika
kutenga maneno yaliyo katika orodha
Mfano:
Ukifika nyumbani pika Ugali,
Ndizi,samaki na wali.
v Hutukika
kabla ya alama za mitajo.
Mfano:
Musa alisema, “Nakupenda sana”
v Hutumika
kuonyesha vyeo, anuani au makazi baada ya jina la mtajwa
Mfano:
Hengapinge msambasa, Meya wa
jiji la njombe
d. Rutifaa (`)
v Hutumika
kutofautisha ng` na ng`
Mfano:
Ng`ambo, ng`ang`ania ng`arisha
nk.
e. Herufi kubwa
v Hutumika
kila mwanzo wa sentensi
v Hutumika
badala ya alama hizi (.), (?),(!) n.k
v Hutumika
kutaja majina ya pande za dira kama vile
Kusini, kaskazini, magharibi,
mashariki.
v Hutumika
kutaja majina ya pekee.
Mfano:
Kutaja majina ya watu, mji,
nchi, bara n.k.
Kama vile Nyaludzi, Gwivaha,
Arusha, Tanzania n.k
Eleza
dhima ya mofimu zilizopigiwa mstari katika maneno yafuatayo: (tahossa-zonal
kidato cha 4 2010 swali la 6)
i.
Ondokeni
Ni
– kuonyesha wingi
ii.
Ametoka
Me
– inaonyesha wakati (njeo ya wakati timilifu)
iii.
Mkulima
M
– inaonyesha umoja (mmoja katika nomino)
iv.
Cheza
Chez
– mzizi wa neno
v.
Amesomesha
Esh
– inaonyesha kauli ya kutendesha.
“Moja
ya hoja za kiisimu kuthibitisha ubantu wa lugha ya Kiswahili ni umbo la kitenzi”.
Kwa hoja nne zenye mifano na fafanua namna ambayo kitenzi cha lugha ya
Kiswahili kinavyofanana na lugha nyingine za kibantu (tahosa Dar zone 2013
swali la 10).
Vitenzi vya Kiswahili na
kibantu.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya
vitenzi vya Kiswahili na kibantu.uhusiano huu upo katika viambishi, mnyambuliko,
mwanzo na mwisho wa vitenzi.
a. Viambiashi
Vitenzi
vya lugha ya Kiswahili huundwa na viambishi awali mzizi na viambishi.
Mfano
Kiswahili-Analima-A-na-li-ma
Kikuyu-Ararema-A-ra-rem-a
Kindali-Akulim-A-ku-lim-a
1 2 3 4
b. Mnyumbuliko wa vitenzi
Mnyumbuliko wa maneno ya
Kiswahili na kibantu hufanana.
Mfano
Kiswahili – kucheka – kuchekesha
– kuchekelea
Kindali – kuseka – kusekasha –
kusekelela
Kibena – kuheka – kuhekesa –
kuhekelela
Kikagulu – kuseka – kusekesha –
kusekelela
c. Mwanzo wa vitenzi
Vitenzi
vya Kiswahili na kibantu huanza na kiambiashi awali cha nafsi.
Mfano
Kiswahili
– Ni – nakwenda
Kibena
– ndi – helela
Kindali
– Ingubhuka
Kiyao
– m - genda.
d. Mwisho wa vitenzi
Vitenzi
vya Kiswahili na kibantu huishia na Irabu a
Mfano
Kiswahili
– kukimbia, kuwinda, kushika
Kindali
– kukind-a kubhing-a, kukol-a
Hivyo
mfano
Wa
vitenzi vya Kiswahili na kibantu
a. Uandaaji wa simu ya maandishi
una utaratibu zake. Taja hatua zote unazopitia katika katika kuandaa simu ya
maandishi (nectar 2010 swali la 9a).
Hatua za kuzingatia katika
uandishi wa simu.
i.
Anuani ya mpelekewa taarifa.
Anuani
ya barua ya simu lazima iwe kamili na ya wazi wazi kuiwezesha barua hiyo
kupelekwa kwa haraka.
Anuani
ya mji ni lazima iwe na jina la mtu ikiwezekana na namba ya nyumba.
ii.
Ujumbe au taarifa
Hiki ni kiini cha
simu. Taarifa au ujumbe huelezwa kwa ufupi sana lakini hueleweke vizuri sana
iii.
Jina la mwandishi au mtuma simu
b.
Kwa kuzingatia hatua hizo andaa simu
ya maandishi isiyozidi maneno kumi (10)juu ya taarifa yoyote.
RIZIKI JACKSON SLP
432 NJOMBE.
NJOO HARAKA BIBI
ANAUMWA GODLOVE
|
Kwa kutumia mifano eleza maana
ya:
(nectar 2011 swali
la 7)
a.
Kamusi wahidiya
Ni
kamusi inayoandikwa katika lugha moja tu, na inalengwa kwa wazungumzaji wazawa
wa lugha hiyo mara nyingi huwafaa wanaojifunza lugha hiyo kama lugha ya pili au
ya kigeni.
Vidakizo
vya kamusi waliyo na maelezo ya maana huwa katika lugha moja.
b.
Rejesta
Ni
mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli Fulani ambayo ni tofauti na
lugha ya kawaida
Mfano
Lugha
ya kivuvi ya kibiashara.
c.
Misemo
Ni
fungu la maneno linalotumiwa na jamii ya watu kwa namna maalum ilikutoa maana
Fulani
AU
Ni
kauli yenye ukweli wa jumla inayotumiwa kusemea mambo mbalimbali yanayoafiki
ukweli huo.
Mfano
·
Mtu kwao
·
Piga msasa
Misemo haina mana ya mafumbo bali
inaeleza maana ya kauli moja moja.
d.
Lahaja
Ni
tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza katika lugha kuu yenye asili moja. Tofauti
hozo zipo katika matamshi (lafudhi), maumbo au matumizi ya maneno.
e.
Lugha ya mazungumzo
Ni
lugha inayotolewa kwa njia ya mazungumzo yam domo. Ni mawasiliano yanayohusisha
msikilizaji na mzungumzaji.
Fafanua
dhima ya “ji” katika maneno yafuatayo:
(nectar
2011 swali la 6)
a.
Jitu
Inaonyesha
Ukubwaishaji
b.
Uzalishaji
Inaonyesha
Unominishaji
c.
Anajikwatua
Inaonyesha
urejeshi wa mtendwa
d.
Jicho
Inaonyesha
umoja wa nomino.
Kwa
kutumia mifano, eleza chanzo cha misimu na taja matumizi matatu 3 ya misimu.
Misimu
Ni
maneno yasiyosanifu yanayozushwa na kikundi cha watu wachache wenye utamaduni
moja ili kueleza mahusiano kama kikundi au kuhusu mahusiano ya kikundi au
kuhusu jamii kubwa ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi Fulani cha
wakati; maneno haya hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa
lugha inayohusika.
CHANZO
CHA MISIMU
i.
Huzuka kutokana na hali ya utani
miongoni mwa watu mbalimbali. Mara nyingi misimu ya aina hii hubeba kebehi,
dhihaka, kejeli, mabezo, dharau au kusifu kusiko kwa kawaida.
ii.
Huzuka kutokana na vipindi mbalimbali
vya kihistoria ambavyo huikumba jamii katika nyakati mbalimbali. Misingi ya
kuzua misimu inakuwa ileile ya kutaka kukueleza dhna Fulani ambayo imejitokeza
katika mfumo wa maisha ya mwana jamii.
MATUMIZI
YA MISIMU
i.
Hupamba lugha
Katika
mazungumzo misimu ina mvuto na hupamba lugha, kwani misimu mara nyingi huwa
imetiwa chumvi.
ii.
Huibua hisia mbalimbali kwa
wazungumzaji,misimu ina maneno yale yenye kubeba hisia, chuki, furaha, au
karaha nk.
iii.
Huchekesha na hufurahisha
Maneno
mengi ya misemo kuwa na mvuto na kutiwa chumvi nyingi,chuki, kejeli, mabezo,
dharau au kujisifia kusiko kwa kawaida.
Muktadha wa utumizi
wa lugha huwafanya wahusika kuibua maneno maalumu.
Jadili
usemi huu kwa kutumia mifano ya sentensi tano (5) zionyeshazo miktadha tofauti.
(nectar 2009 swali la 6)
MAJIBU
·
Mhudumu nipe chai mbili (hotelini)
·
Tusome somo ka kwanza (kanisani)
·
Kunywa mbili mara tatu kwa siku
(hospitalini)
·
Andika kumbukumbu zote za kikao
(ofisini)
·
Ambaye hakufanya mtihani apite mbele
(shuleni).
i.
Weka
nomino zifuatazo katika ngeli za upatanisho wa kisarufi.
JIBU
a.
Kipofu
v Kipofu
yu mgonjwa
v Vipofu
wa wagonjwa
Ngeli
ya 1 (yu-a-wa)
b.
Kiboko
v Kiboko
kimevunjika
v Viboko
vimevunjika
Ngeli
ya 4 (ki-vi)
c.
Mkono
v Mkono
umevunjika
v Mikono
imevunjika
Ngeli
ya 2 (u-i)
d.
Kalamu
v Kalamu
imevunjika
v Kalamu
zimevunjika
Ngeli
ya 6 (u-zi)
ii.
Kwa
kutumia nomino hizo tunga sentensi moja yenye kiambishi cha O-rejeshi kwa kila
nomino
a.
Kipofu aliyekuja jana ameondoka leo
b.
Viboko vilivyo vunjwa jana vimeisha
c.
Mkono uliovunjika juzi umepona
d.
Kalamu iliyopotea jana imeonekana
Kamusi ni muhimu kwa mtumiaji
yeyote wa lugha. Taja hoja tano (5) zinazothibitisha umuhimu huu. (nectar 2012
swali la 5)
Kamusi
ni kitabu cha marejesho chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa
jamii Fulani na kupangwa kwa utaratibu maalumu. Kasha kufafanuliwa kwa namna
ambayo msomaji aweze kuelewa.
Kuna aina mbalimbali za kamusi
kama vile kamusi wahidiya, thaniya na mahuruti.
UMUHIMU WA KAMUSI
i.
Kamusi huonyesha tahajia (spellings)
sahihi za maneno
ii.
Kamusi hueleza maana (fasihi)
mbalimbali za maneno
iii.
Kamusi hubainisha aina (kategoria) ya
neno
iv.
Kamusi huonyesha alama ya vifupisha
mbalimbali vinavyotumiwa katika lugha husika
v.
Kamusi huongeza maarifa zaidi kuhusu
lugha ya mzungumzaji.
vi.
Kamusi huonyesha Kamusi huonyesha
misemo, semi, misimu, methali, mbalimbali katika lugha inayohusika.
vii.
Kamusi huonyesha matamshi sahihi ya
maneno.
a.
Toa maana ya Hotuba
Hotuba
ni mazungumzo yanayofanywa na mtu
Eleza ubora na dhaifu wa
kuhifadhi fasihi simulizi kwa njia ya maandishi (pre form iv Dar 2011 swali la
11)
Maandishi
Uhifadhi kwa kutumia maandishi una matatizo
yafuatayo
· Fasihi
simulizi ikihifadhiwa katika maandishi kuna mambo ya msingi ambayo hayawezi
kuhifadhiwa katika maandishi. Mambo hayo ni yale yanayohusiana na utendaji,
sauti, vitendo, kuimba na vitabia. Matokeo ya kukosekana kwa vitu hivi ni
kwamba radha au athari ya kazi inayowasilishwa kupungua kabisa .
·
Katika maandishi, fasihi simulizi
haina sauti. Kwa hiyo, msomaji inambidi atie sauti na mahadhi yake mwenyewe.
Shuguli hii inaweza kuharibu au kufifisha ubora wa kazi hiyo.
·
Kuhifadhi fasihi simulizi katika
maandishi uhusiano wa ana kwa ana kati ya fanani na hadhira hupotea. Kwa hiyo,
hadhira inashiriki kwa kuona maandishi.
·
Fasihi simulizi ikihifadhiwa katika
maandishi haitabadilika kulingana na wakati na mazingira. Hivyo huweza kudumu
katika hali ileile kwa muda mrefu kama ilivyo fasihi andishi.
·
Fasihi simulizi ikihifadhiwa katika
maandishi itakuwa na watu wachache tu yaani wale wanaojua kusoma na kuandika.
Wale wasiojua kusoma na kuandika itawawia vigumu kuielewa fasihi hiyo iliyoko
kwenye maandishi.
·
Ni gharama kubwa kuhifadhi masimulizi
katika maandishi. Hii ni kwa sababu uandishi hutumia kalamu na karatasi. Hivyo,
hapa zinahitajika pesa za kununulia kalamu na karatasi na gharama za
uchapishaji.
Fafanua
aina ya tungo kwa kutoa mfano mmoja kw kila tungo.
Hii ni sentensi ya
kishazi huru. Kishazi hicho kinaweza kuwa na kifungu tenzi kimoja. Kifungu
tenzi hicho kinaweza kuwa kitenzi kikuu au kitenzi kuu na kitenzi kisaidizi au
kitenzi kisaidizi.
Mfano
Ali analima shamba
T
Musa ni mzembe
T
Mama alikuwa anapika chakula
Ts T
Mzee alikuwa anataka kwenda kuona mpira.
Ts Ts Ts T
Taja
aina nne za virai na kwa kila aina tolea mfano mmoja
Kirai nomino (KN)
Kirai
nomino ni kirai kinachotawaliwa na nomino au mahusiano ya nomino na neno au
mafungu ya maneno. Kirai nomino huundwa
na maneno yafuatayo:
-
Nomino peke yake. Mfano
Juma
anasoma
Baba
analima
KN
-
Nomino mbili au zaidi
zinazounganishwa. Mfano:
Baba
na mama wanalima
Juma
na ally wanacheza mpira
KN
-
Nomino na kivumishi (N+V). mfano
Watu
wawili wanalima
Mtoto
Yule
ni mpole
Mtu
mnene ameanguka
KN
-
Kivumishi na nomino (V+N). mfano
Yule
mtu
anapika
Kile
kiti
kimevunjika
Hawa
watoto ni watundu
KN
Kiwakilishi peke
yake (W). Mfano
Wewe
unaumwa kichwa.
Mimi
ninapika
chakula
Yeye
anacheza
mpira
KN
Eleza shughuli tano
za utawala wa waingereza kabla ya uhuru zilizokuza na kueneza Kiswahili nchini
Tanzania.
·
Elimu
Wakati
wa Waingeleza, Kiswahili kilitumika kufundishia shule za msingi darasa la
kwanza hadi la nne, na lilikuwa mojawapo hadi darasa la 12 katika shule za
waafrika.
·
Vyombo
vya habari
Vyombo
vya habari vilivyo jishughulisha sana na kukuza na kueneza Kiswahili ni
magazeti, redio nk.
Magazeti
yaliyo jishughulisha sana kukuza na kueneza ni Habari za leo (1954), sauti
ya pwani (1940), mwangaza (1923),
kiongozi (1950), mamboleo (1923) nk.
Chombo
kingine cha habari ni redio Tanganyika ilianza na matangazo kwa lugha ya
Kiswahili mwaka (1950). Kwanza kama sauti ya Dar es salaam halafu baadaye kama sauti ya Tanganyika.
·
Suala
la manamba
Utaratibu
wa serikali za kikoloni ulikuwa ni kuzitenga sehemu Fulani kwa ajili ya vibarua
wa kufanya kazi katika mashamba yao. Mawasiliano yote yalifanywa kwa Kiswahili.
Kwa njia hii, Kiswahili kilikua na kueneakwa urahisi zaidi hapa nchini.
·
Suala
la jeshi (KAR)
Wanajeshi
walipigana katika vita mbalimbali walikuwa na nafasi ya kusafiri sehemu mbali
mbali. Kwa kuwa lugha yao ya kiswahili ilikuwa ni Kiswahili, lugha hiyo iliweza
kuenea kwa urahisi nchini.
·
Suala
la utawala
Kama
ilivyokuwa kwa wajerumani, waingereza nao katika shughuli za utawala
walisisitiza matumizi ya Kiswahili. Waingereza walilazimisha kila chifu afahamu
Kiswahili ili atumike katika shughuli za utawala. Vilevile wafanyakazi wote wa
serikali wa ngazi za chini walilazimishwa kufahamu Kiswahili ili wapate ajira
za chini serikalini.
Kwa
kutumia hoja tano zenye mifano eleza kwa kifupi mchango wa wamisionar wa
kikristo katika kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanganyika kabla ya uhuru
(nectar 2013 PC swali la 10)
Wamisionari
Wamisionari walifika
Pwani ya afrika mashariki kabla ya utawala wa wakoloni mashirika mbali mbali ya
kidini liingia Afrika Mashariki katika nyakati tofauti.
Baadhi ya mashirika
ya kidini ni :-
ü Roho
matakatifu toka ufaransa mwaka 1868
ü White
father toka ufaransa mwaka 1878
ü Church
missionary society (C.M.S) iliyoongozwa na J.C krapf.
Mchango
wa missionary
a-
Waliandika sarufi ya kwanza ya
Kiswahili cha kimvita katika kitabu kilichoitwa “Ouline of the Elements of
Kiswahili language with specific reference to the kinika Dialect”.
b-
Walitafsiri Injili ya luka na yohana
ili kuwasaidia wamisionar wengine ambao walikuwa wakiletwa Afrika mashariki.
c-
Mwaka 1905 Misheni Magila (tanga)
walitoa kitabu cha historia ya wasambaa kilichoitwa “Habari za Wakilindi” na
makao makuu ya shirika hili yalikuwa Mombasa.
d-
Walichapisha kitabu cha kwanza cha
sarufi ya Kiswahili cha Unguja kilichoitwa “A Hand book of the Swahili language
as a spoken at Zanzibar” (1870- Askof Edwrd steere)
e-
Walichapisha vitatabu vya nyimbo na
kamusi za Kiswahili-kiingereza na kingereza – Kiswahili kazi ya mwanzo ya
kuandaa kamusi hizo zilifanywa na Askofu Edrard Steer na kurudiwa na A. Madam
na kurudiwa na F. Johnson
f-
Walichapisha magazeti, Magazeti hayo
ni masimulizi (1888). Habari za mwezi
(1976) Pwani na bara (1910).
g-
Walichapisha kamusi ya “A Standrd
English-swahili Dictionary na Swahili-English Dictionary ambazo zili tolewa
mwaka (1939).
Vishazi
tegemezi hufanya kazi ya vivumishi viwapo katika tungo. Ukweli wa kauli hiyo
kwa kutumia mifano mine ya sentensi. (nectar Pc 2013 swali la 6).
Jibu
i.
Kishazi tegemezi (K/Tg)
Ni kishazi
kinachotawaliwa na kitenzi kisaidizi
ambacho muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza
kutoa ujumbe ulio kusudiwa. Kishazi tegemezi peke yake hakitoi ujumbe
unaojitosheleza.
Mfano
Mwalimu
aliyefundisha darasani.
Kitabu kilichopotea
juzi.
SIFA
ZA KISHAZI TEGEMEZI.
a.
Kishazi tegemezi hakiwezi kutoa maana
kamili ikiwa haijafuatana na kishazi huru
Mfano
Kisichana anayecheza
uwanjani
Mbwa aliyekamata
paka.
b.
Kishazi tegemezi kinaweza kuondolewa
katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi
Mfano
Mbwa aliyekichaa
mwogope
Sentensi hii inaweza
kuondolewa kishazi tegemezi tegemezi “Aliyepata kichaa” ikawa mbwa mwogope”
c.
Vishazi tegemezi huweza kutambuliwa
kwa kuwepo vishazi kama vile “Ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, ambate, ambacho
nk.
Mfano
Kijana ambaye
anasoma atakuja
Dada huyu hapiki kwakuwa
ameshiba.
NAMNA VISHAZI TEGEMEZI
VINAVYOFANYA KAZI KAMA VIVUMISHI VIWAPO KATIKA TUNGO
i.
Soko lililoungua jana
limesafishwa.
K/Tg
(v)
ii.
Kisu kilichonunuliwa jana
kimepotea
K/Tg
(v)
iii.
Aliyekuwa mwalimu mkuu wetu
amesafiri.
K/Tg
(v)
iv.
Walioandamana barabarani
wamefukuzwa na mlinzi.
K/Tg
(v)
Kwa
kutumia mifano, Onyesha jinsi shughuli za dini, utawala, biashara na elimu
zinazokuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania (nectar 2012 swali la
10)
Utawala
Shughuli
zote za utawala hapa nchini Tanzania kama vile ofisini, bungeni, mahakamani,
shuleni nk. Hutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano. Hivyo
shughuli za utawala zinasaidia sana katika ukuaji na uenezaji wa Kiswahili hapa
nchini.
Dini
Dini
zote yaani ukristo na uislam zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza na kueneza
Kiswahili kwa kiasi kikubwa Tanzania tangu kipindi cha uhuru mpaka sasa.
Ukristo na uislam huendesha shughuli na mahubili yake kwa lugha ya Kiswahili hivyo
huchangia sana kuku na kueneza Kiswahili hapa nchini.
Biashara
Shughuli
na misafara mbalimbali ya kibiashara katika sehemu mbalimbali hapa nchini
husaidia sana kukuza na kueneza Kiswahili katika sehemu mbalimbali za ndani ya
Tanzania.
Elimu
Nchini
Tanzania Kiswahili hutumika kufundishia Elimu ya msingi yaani darasa la wanza
mpaka la saba na secondary Kiswahili wanasoma kama somo. Hali hii imesaidia
kukuza na kueneza Kiswahili nchini Tanzania.
Kwa
ujumla dini, utawala, biashara, elimu zimesaidia sana kukuza Kiswahili nchini
Tanzania.
Eleza
tofauti za msingi mbili zilizopo kati ya kirai na kishazi. Toa mifano miwili
kwa kila tofauti. (nectar 2010 swali la 10)
Tofauti
Maana,
kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi ambacho hakina muundo
wa kiima kiarifu. Lakini kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza
kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na
kitenzi kisichoweza kujitegemea mwenyewe.
Mfano
Mwanafunzi
anacheza mpira” (kishazi) hiki kinajitosheleza kwani kinakamisha ujumbe
uliokusudiwa na mzungumzaji.
“mwanafunzi
anayecheza mpira” (kishazi) hiki hakijitoshelezi kwani hakikamiliki ujumbe)
Aina,
Kirai
kimegawanyika katika aina nne ambazo ni kirai nomino, kirai kielezi, kirai
kivumishi, na kirai kitenzi. Lakini kishazi kimegawanyika katika aina mbili
ambazo ni kishazi huru (K/Hr) na kishazi tegemezi (K/Tg).
18.Eleza
tofauti kati ya hotuba na risara. Andika Risala huhusu maji ni uhai.
a.
Toa
hotuba ya maana
Hotuba
ni mazungumzo yanayofanywa na mtu au watu kuhusu. Hotuba inaweza kutolewa
kutolewa na waalimu kwa wanafunzi, wanasiasa kwa raia, ama wahuburi kwa
waumini.
b.
Eleza
kwa ufasaha sifa nne hotuba nzuri.
i.
Hotuba nzuri lazima iwe na sehemu kuu
tatu yaani Mwanzo, kati na mwisho.
ii.
Hotuba nzuri ni lazima izungumzie
ukweli wa jambo.
iii.
Hotuba nzuri ni lazima iendane na
Muktadha maalum.
iv.
Mzungumzaji wa hotuba nzuri ni lazima
azungumze kwa nidhamu.
Hotuba ni maelezo ambayo huolewa
mbele za watu. Hotuba hutolewa kama vile kutaka kuhimiza kazi, kufanya kampeni,
au kutoa taarifa kwa watu.
Risala
ni hotuba fupi inayosomwa mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi Fulani la watu
ili kutoa maelezo kuhusu kundi hilo kwa kiongozi. Mfano risala inaweza kusomwa
na wahitimu mbela ya mgeni rasmi.
RISALA
Ndugu
wananchi mabibii na mabwana. Ninayo furaha kubwa kuzungumza nanyi siku hii ya leo, kwa kifupi ni lengo la ujio
wangu na kuwaita hapa ni kutoa taarifa ya matumizi ya maji kwani “Maji ni uhai”
Ndugu
wananchi,nimepata taarifa kutoka kwa viongozi wenu na watu mbalimbali kuhusu
watu kutumia maji vibaya pasipo sababu maalum na kuharibu vyanzo vya
maji.Mfano, baadhi yetu wanalima kandokando yam to, wanakata miti ovyo hivyo
husababisha mvua kuwa kidogo katika kijiji chetu. Mvua ikikosekana je, Mazao
yetu yatastawi vipi mashambani? Na mazao yakikauka shambani tunaweza kukumbwa
na jangwa la njaa katika kijiji chetu.
Ndugu
wananchi katika mkutano huu napenda kuwakumbusha kuwa serikali yetu immekwishaonyesha
mfano kwa vitendo umuhimu wa maji.
Vijiji
vingi vimekwisha pewa fedha za kuendeshea miradi mbalimbali ya maji kama vile
kutengeneza mabomba, kuchimba visima vilivyojengewa na vinatoa maji safi kwa
ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani kama vile kupikia,kuoga,kufua na
mengine kadha wa kadha.
Hivyo
basi ili kutunza vyanzo vyetu vya maji hatuna budi kuacha kulima kandokando ya
mito na tunatakiwa kupanda miti kwa wingi hasa tukifuata sera ya ‘Panda mti
Kata mti’ ili tuweze kupata mvua za kutosha.
Nina
matumaini kuanzia sasa mtatekeleza haya niliyoyasema, kuanzisha miradi
mbalimbali ya maji na hakika tutatunza vyanzo vyetu vya maji. Mkifanya hivyo
kijiji chetu hakitakuwa na ukosefu wa maji tutakuwa na maji ya kutosha na mvua
nyingi za kutosha.
Nawatakia
utekelezaji mwema
Asanteni
sana kwa kunisikiliza
Eleza mchango wa
waarabu katika kukikuza,kukieneza na kukidumaza Kiswahili nchini Tanzania kabla
ya uhuru. (nectar 2005 swali la 1).
AU
Fafanua Athari ya
Waarabu katika Lugha ya Kiswahili kwa kutoa hoja nne(Necta 2011 swali 10)
Kukua kwa lugha
ni hali ya kuongezeka kwa msamiati katika lugha na Kuenea kwa lugha ni jinsi
lugha inavyoenea kwa watumiaji ndani na nje ya nchi au eneo husika na kufanya
lugha kuwa na eneo pana.Kudumaa kwa lugha ni hali au tendo la kuifanya lugha
isikue hivyo hupelekea kutokutumiwa mara kwa mara na kushuka kiwango kutoka
ilichokuwa nacho (juu) hadi chini.
Kukikuza Kiswahili; Waarabu
walipoingia nchini Tanzania maeneo ya Pwani ya Afrika mashariki karne ya 8,
walikuta tayari wenyeji wana lugha zao za ambazo walizitumia katika mawasiliano
zilijulikana kama lugha za kibantu ukijumuisha na Kiswahili.
Waarabu
walichangia baadhi ya maneno katika lugha ya Kiswahili, mfano maneno kama;
shikamoo, Laki, Abadi n.k hivyo kama ilivyo tabia ya lugha yeyote kukopa maneno
kutoka kwenye lugha nyingine ili iwe na msamiati yakujitosheleza, hivyo kukua
kwa lugha ya Kiswahili kumetokana na kukopa maneno kutoka katika lugha ya
kiarabu na lugha nyingine.
Neno
lenyewe Kiswahili limetokana na kiarabu ‘sahil’ (umoja) na ‘swahil’ (wingi) lenye maana ya Pwani au
Upwa.
Kukieneza Kiswahili;
waarabu walitumia njia tatu katika kukieneza Kiswahili kama ifutavyo;
Biashara, waarabu walipofika pwani ya afrika mashariki
walilazimika kutumia lugha ya Kiswahili katika biashara zao kama vile, Biashara
ya pembe za ndovu na biashara ya watumwa. Walitumia Kiswahili katika
mawasiliano katika biashara zao na biashara hiyo ilikuwa baina ya watu wa pwani
na bara, watu wa pwani walikipeleka Kiswahili bara kupitia misafara ya
kibiashara na katika misafara hiyo wenyeji waliwaongoza waarabu na kuwabebea
mizigo.
Dini, waarabu
walilazika kutumia Kiswahili kwa sababu kilikuwa tayari kinatumiwa na wenyeji
wa pwani, waarabu walijenga madrasa ambayo yalitoa mafundisho ya dini ya kiislamu
kwa kutumia lugha ya Kiswahili ili waweze kueneza mahubiri yao kwakiurahisi na
hivyo wakajikuta wanakisaidia kiswahili kuenea.
Kuoana, waarabu
walipoingia pwani ya afrika mashariki waliwakuta wenyeji wao wakitumia lugha ya
Kiswahili na kibantu kadri wavyozidi kuishi pamoja walioana na wenyeji wa pwani
na iliyotumika katika mazungumzo yao ya kila siku ilikuwa ni Kiswahili.
Athari au Namna
waarabu walivyodumaza lugha ya kiswahili
Waliingiza
msamiati na istilahi nyingi za kiarabu kuliko Kiswahili hivyo waliaribu lugha
Mfano;
abudu, samehe, fariji nk.
Katika
mafundisho ya kidini walitumia walitumia zaidi kiarabu kuliko
Kiswahili mfano; Madrasa na swala kwa ujumla walitumia walitumia kiarabu
Hawakutafsiri
vitabu vya kidini kwa lugha ya Kiswahili
Waarabu
walidharau lugha ya Kiswahili na kuiona kama lugha ya makabwela
Waarabu
walieneza Kiswahili sehemu chache tu ambazo walikuwa na malengo nazo. Walieneza
Kiswahili katika vituo vya biashara tu kama Tabora na ujiji tu.
Fafanua mambo matano (5)
yanayomtambulisha mtu kuwa ni mjuzi wa lugha.(Necta 2010 swali la 4)
Ujuzi
wa lugha unatazamwa katika stadi kuu nne yaani
kusoma,kuzungumza,kusikiliza na kuandika
Mtu anayeweza kuzungumza na kuielewa lugha na kukidhi vema mawasiliano
huitwa mjuzi wa lugha.
Mambo
yanayomtambulisha mtu kuwa mjuzi wa lugha
a. Kutambua kwa urahisi sentensi
amabazo ni tata na namna/jinsi ya
kuondoa utata huo
Sentensi zifuatazo ni ni
sentensi rahisi sana na za kawaida sana katika Kiswahili,
Ally anampenda dada yake
Mkewe anampenda Ally.
Ikiwa Sentensi hizi zitasikika
bila kuwekewa mazingira yanayopasa ,Mjuzi wa Kiswahili yeyote atatambua kuwa kila mojawapo ya sentensi hizi
inaweza kueleweka kwa namna zaidi ya moja.Katika sentensi ya kwanza kuna
wahusika wawili au watatu.
-Ally anampenda dada
yake(wahusika 2)
-Mtu fulani ana dada,Ally
anampenda dada wa mtu huyo (wahusika
3)
Sentensi ya pili
inaweza kuelewekahivi;
-Mtu Fulani ana
mke,mke huyo anampenda sana Ally.(wahusika 3)
-Mtu Fulani ana mke
na anampenda sana mke wake.
Utata wa sentensi
hizi hautokani na tofauti za kimuundo katika sentensi hizo,kwani miundo yake
inafanana na zote zina S K+A,yaani kiima na Kiarifu.
Hivyo mjuzi wa Lugha
lazima atambua Utata uliomo katika tungo na namna ya kuondoa utata huo.
b. Kutambua
ni sauti zipi zinatumika kuunda maneno ya lugha yake na mfuatano upi
unakubalika na upi haukubaliki.
Kwa mfano, ikiwa ni
mmahiri wa Kiswahili atapewa neno “baba” na akaambiwa aweke sauti nyingine
badala ya ile ya kwanza, haya ni baadhi ya maneno ya Kiswahili anayoweza
kuunda: kaba, saba na shaba. Ikiwa itabadili sauti ya pili anaweza
kupata beba na buba. Katika
kuunda maneno, kuna kanuni maalum ambazo ni mmahiri wa lugha anazifahamu na
anajua kuwa mifuatano Fulani inakubalika, na mengine haikubaliki kwa sababu
haiwezi kuunda maneno ya Kiswahili. Hivyo, kutokana na “baba” huweza kuunda, Abba,
bbaa, aabb au baab. Maarifa haya ya lugha
yanamwezesha mmahiri kutambua kuwa, ingawa anaweza kufananisha sauti katika
maneno tofauti ya lugha yake, si kila mahali anaweza kuzibadilisha kama
tulivyofanya hapo juu katika “baba”.
c.
Kwa kutambua mfuatano sahihi wa
vipashio katika maneno au sentensi za lugha yake.
Katika Kiswahili kwa
mfano, sentensi zake kwa kawaida huanza na nomino ya mtenda au mtendwa na huwa
na kitenzi.
Mfano
Ng’ombe anakula
majani porini.
Mmahiri wa Kiswahili
anayefuata kanuni ya mpangilio wa maneno anaweza kukataa sentensi hii: “mnene
ng’ombe anakula majani” kwa sababu haijapa mpangilio sahihi wa maneno wa maneno
katika sentensi hiyo.
d.
Kutambua tungo ambazo
zinavunja/hazivunji kanuni za sarufi ya (upatanisho wa kisarufi)
Mmahiri wa kiswahili
atakuwa na matatizo ya tungo zifuatazo,yaani atakuwa na wasiwasi kuwa kanuni
Fulani za lugha hii imevunjwa na pia atatambua zimrvunjwa kwa namna gani.
-
Ile motto imechana kitabu chake
-
Watoto yao na baba yao wamekuja
Katika
sentensi ya kwanza mmahiri wa lugha ya Kiswahili atatambua kuwa tungo hiyo
inaweza kutolewa na mtu anayejifunza Kiswahili kabla hajajizatiti sawasawa
katika upatamsho wa makundi tofauti ya maneno ya lugha hii.anaweza kuisahihisha
sentensi hiyo hivi.
“Yule mtoto amechana
kitabu chake”. Sentensi ya pili inaonekana imevujwa
kanuni za juu za za lugha na mmahiri wa Kiswahili itaikataa moja kwa moja tungo
hiyo, ingawaje anaweza kujaribu kuirekebisha isomeke kama:
Watoto wamekuja na
baba yao
e.
Kutambua kwa urahisi kusudio la
sentensi
Mmahiri
wa lugha yoyote anayo maarifa yanayomwezesha kutofautisha kati ya aina ya
sentensi katika lugha yake kutegemea kusudio la sentensi hiyo. Anajua, kwa
mfano,ni tungo zipi za kuuliza, aaina za
maswali yanayoweza kuulizwa,pamoja na majibu yanayotegemewa. Atajua zipi ni za
taarifa, za kebehi au utani. Kwa mfano, ikiwa mmahiri wa Kiswahili ataulizwa “mtoto
yuko wapi?” atatambua kwa urahisi kuwa jibu lake linaweza kuwa
“Amelala” ma sio “ndio”.
Lakini
akiulizwa “mtoto amekwisha kula?”. Atatambua kuwa “amelala” haliwezi kuwa
jibu ambapo “ndio” linaweza kuwa mojawapo ya majibu ya swali hilo.
Mmahiri
wa Kiswahili pia anayo maarifa yanayompa utambuzi kuwa tungo zifuatazo
hazihitaji kujibiwa kwa maneno, ila pengine kwa vitendo,kwa sababu ni tungo za
utendaji” yaani zinamtaka mzungumziwa kutekeleza kusudio la tamko.
-
Tafadhali nipatie maji ya kunywa
-
Samba huyu anaunguruma,
tukimbie.
Mambo
(5) yanayosababisha kutokea kwa lahaja (mock 2012 Dar swali la 10)
Chanzo
cha lahaja
i.
Utengano wa watu kijografia
Msukumo
wa kimazingira ndiyo chanzo cha jamii katika eneo pana zaidi. Kuna mambo
mbalimbali yanayotokea na kusababisha watu wanaosema lugha moja kutengana kimahali
na kimielekeo. Mambo haya ni kama vile kuongezeka kwa idadi ya watu, ukame na
vita mambo haya yanalazimisha watu walioishi pamoja kuachana ili kutafuta
makazi mapya yenye kuwapatia nafuu. Matokeo ya mwachano huu ni kwamba,
mawasiliano ya mara kwa mara yatapungua. Kwa kuwa mawasiliano ni haba, kuna
uwezekano mpano wa watu walioachana kukuza upekee wa namna Fulani katika
usemaji wao. Kwa hiyo, msingi wa pekee wa usemaji au kuzuka kwa lahaja ni
utengano, ama wa kijamii (kitamaduni) au wa kijografia (kimazingira).
ii.
Utengano wa watu kitabaka
Katika
jumuiya moja kunaweza kumea tabaka mbambali za watu.kila tabaka hujihisi na
kujitambulisha kwa namna ya pekee japokuwa matabaka hayo huishi katika eneo
moja la kijografia. Msingi wa mwachano wa kitabaka unaweza kuwa uchumi, dini,
elimu au siasa. Kwa sababu ya mwachano wa kitabaka, mawasiliano ya mara kwa
mara baina ya watu na tabaka mbalimbali hupungua. Mawasiliano ya mara kwa mara
yakipungua, nafasi ya kuchipuza upekee hata katika usemaji hupanuka. Hivi ndivyo
vianavyo vipengele vya upekee wa usemi vifungamanavyo na tabaka. Vipengele hivi
havionekani au havipatikani kwa urahisi hata kama ni jumuia zilizoendelea sana
kiuchumi. Ndio mana vigumu kusema kwamba, katika jumuia hasa za zamani za
wasema-kiswahili kilikuwa na lahaja za kitabaka. Miongoni mwa wasema-kiswahili
wasasa bila shaka inawezekana kuona vidokezo vya kuinukia vya lahaja ya
kitabaka.
iii.
Kupita kwa wakati
iv.
Utengano wa kiwakati ni
kipengele muhimu katika kusababisha kuzuka kwa lahaja. Umbali tu hautoshi-uwe
wa kijografia au kijamii au kijamii.hata baada ya wasemaji wa lugha moja
kutengana kwa sababu ya hiki au kile, upekee katika usemaji hauzuki mara moja.
Hutokea taratibu kadri wakati unavyopita. Kipengele cha wakati ni muhimu
vilevile katika ukuzaji wa lahaja za kijamii au za kitabaka.
v.
Kwa ujumla uzito mkubwa zaidi ya
kustawi kwa lahaja unabebwa na upitaji wa wakati hasa lahaja za kijografia. Kwa
mfano, tuseme kuna wana jamii lugha A. Kutoka jamii hii kikachipuka
kikundi-jamii B kwa kuhama. Wakati wa kuhama na hata miezi au miaka michache
baada ya kuhama wakazi wa B na A hawatakuwa tofauti. Wakazi wa B wataongea sawa
na wakazi wa A. Lakini kadri wakati unavyopita ndivyo wakazi wa B
watakavyochomoza na kusha tofauti za kilugha za kuwatofautisha na wa A. Kwa
hiyo umbali pekee hautoshi kuelezea umeaji wa tofauti za kudumu bali lazima
umbali huo upatiwe wakati. Kama wakazi wa B wasingekuwa mbali na wale wa A,
tofauti ambazo zingetokea ama zingesawazishwa na mvuto wa umoja wa umoja wao na
A, au zingefuata mkondo mwingine wa mabadiliko ya kiwakati. Ikumbukwe kuwa
wakati tofauti zinatokea kwa wakazi wa B, tofauti nyingine hutokea hata
miongoni mwa wakazi wa A. ingawa kijografia eneo la A halikugeuka, kiwakati na
kimahitaji wakazi wa eneo hilo hubadilika. Kwa hiyo, hata namna yao ya kusema
hubadilika.
Mpaka
wakazi wa eneo B waunde jamii pekee ya kilugha, mambo huku shinani walikotoka
huwa yamebadilika pia kutokana na mwachano wa wakati. Japokuwa A2
itahifadhi jina la A, na pia inawezekana, iwapo hakutatokeavurugu ya ghafla, A2
itakuwa jirani na A; hatuna budi kukiri kuwa, kuna lahaja mbili; A2
na B zilizotokana na A. ni muhimu kusisitiza jambo hili kwa sababu mara nyingi
tunapata kufikiri kuwa B ni lahaja ya A bila kufikiri ni A gani inayohusika.
Kipengele
cha wakati kinapaswa kushirikishwa pia katika umeaji wa lahaja za kitabaka.
Tabaka haziundwi ghafla bali kwa hatua za kiwakati. Hakuna jumuiya iliyozaliwa
ikiwa na wanajumuiya hujigawa vikundi vikundi kwa kadri ya kiwango cha ufanisi
wa kiuchumi au kitawala, kisiasa hata kielimu. Kwa hiyo, wakati pia ni
kipengele muhimu katika kueleza umeaji wa lahaja-tabaka.