KISWAHILI

SANIFU KWA SHULE
ZA SEKONDARI
KITABU CHA MWANAFUNZI
KIDATO CHA SITA
6

iii
KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA SITA
ISHAKIRO
UTANGULIZI iv
SURA YA KWANZA: FASIHI 1
SURA YA PILI: MNYAMBULIKO WA VITENZI 60
SURA YA TATU: UAMBISHAJI WA VITENZI 81
SURA YA NNE: UUNDAJI WA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI 101
SURA YA TANO: UTUNGAJI 117
SURA YA SITA: UTUNGAJI WA HOTUBA 118
MAREJEO 130
iv
KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI
UTANGULIZI
Vitabu ambavyo vilitangulia vilikuwa na lengo la kumsaidia mwanafunzi aweze
kuzungumza Kiswahili sanifu na kukiandika kwa urahisi. Kwa hiyo, kitabu hiki
kinakuja kuviunga mkono vitabu hivyo ili lugha ya Kiswahili iendelee kupiga hatua.
Kitabu hiki kitatumiwa katika kidato cha sita mkondo wa lugha ambapo lugha ya
Kiswahili ni mojawapo wa masomo makuu.
Madhumuni makubwa ya kitabu hiki ni kuwaongoza wanafunzi na walimu wa shule
za sekondari mkondo wa lugha kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili na kuimarisha
lugha hii.
Kitabu hiki kinaundwa na sura nne ambazo ni: FASIHI, MYAMBULIKO WA VITENZI,
UAMBISHAJI WA VITENZI NA MANENO YA KISWAHILI, UTUNGAJI (Risala na
hotuba). Mwishoni mwa kila sura kumeandaliwa mazoezi ambayo yatawasaidia
wanafunzi kufungua akili na kujaribu kuzama katika mada zilizojadiliwa kitabuni.
Katika kitabu hiki mkazo ni kueleza maana ya mnyambuliko na uambishaji wa vitenzi
kama sehemu moja ya sarufi ambayo haikujadiliwa zaidi katika vitabu vilivyotangulia.
Somo hili litamwongezea mwanafunzi ustadi wa lugha hii ya Kiswahili.
Uandishi wenyewe wa kitabu ulifanywa na NDAYAMBAJE Ladislas na NIYIRORA
Emmanuel kutoka Chuo Kikuu cha Elimu cha Kigali (KIE).
Mwishoni, hatuna budi kutoa shukrani zetu za dhati kwa mtu yeyote aliyehusika
katika kutoa maoni kuhusu uandishi wa kitabu hiki.
1
KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA SITA
SURA YA KWANZA: FASIHI
1.1. DHANA YA FASIHI
Fasihi ni kioo na mwonzi wa maisha ya mtu na ya jamii. Ni sehemu ya utamaduni
wa jamii: hushughulika na maisha ya jamii, huchota taarifa zake toka jamii, na kazi
hubaki mali na amali (maana yake mambo yanayothaminiwa na kuhifadhiwa na jamii,
dini, mila, ujuzi, siasa, jadi na lugha) ya jamii. Ni somo panuzi la ujuzi kuhusu lugha
iliyo fasaha. Kwa upande mwingine, Fasihi ni aina ya sanaa ambayo wasanii wake
huonyesha ustadi wao katika kutumia maneno kisanaa ili kuwasilisha ujumbe wao
kwa wasomaji/jamii iliyonuiwa. Fasihi hutumia lugha kutufafanulia tabia za watu na
athari zake huku ikituzindua ili tuone uzuri au ubaya wa jambo au tabia fulani kama
vile wizi, wivu, tamaa na kadhalika.
Fasihi hushughulikia ulimwengu halisi na mambo yale yale yanayotuzunguka.
Tunapoyachambua mambo hayo, tunaona kuwa yanatukia katika mazingira yetu pia
na yanatupa mafunzo muhimu maishani.
1.2. TANZU ZA FASIHI
Fasihi ni moja lakini kutokana na jinsi taarifa inavyohifadhiwa na kurithiwa katika
jamii, Fasihi husemwa kuwa ni ya aina mbili: Fasihi simulizi (mapokeo ya mdomo)
na Fasihi andishi, yaani habari za kubuni zilizoandikwa. Baadhi ya habari hizo zikiwa
zinatokana na Fasihi simulizi. Vitabu vilivyotangulia tulijadili kwa undani Fasihi
simulizi na tanzu zake, ndiyo maana katika kitabu hiki tutajihusisha hasa hasa na
tanzu tofauti za fasihi kwa mapana na marefu.
Kama tunavyogusia hapo juu, ni lazima kwanza kuona tanzu hizo na kuzijadili moja
baada ya nyingine. Tanzu hizo ni: hadithi (hadithi fupi na riwaya), tamthilia, ushairi
(mashairi, tenzi, ngonjera, majigambo).
2
KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI
1.2.1. Hadithi
Hadithi fupi
Hizi huwa ni hadithi za kubuni kutoka katika mazingira ambazo huhusishwa na
matukio au mambo mbalimbali katika maisha ya watu ya kila siku.
Hadithi hizi hukusudiwa kuandikwa zaidi kuliko kusimiliwa.
Hadithi fupi, kwa umbo huwa fupi yaani angalau kuwa chini ya maneno 30, 000 hivi.
Fani katika hadithi
Katika kiwango hiki, tutazingatia mambo mbalimbali ya msingi katika kukabili kazi
ya fasihi andishi au kazi yoyote ya kifasihi. Japokuwa hapa tutaingia zaidi katika
kuitazama fani katika hadithi.
Kimsingi fani na maudhui hukamilishana, kwa sababu ujenzi wa fani huathiri moja
kwa moja jinsi maudhui yanavyotolewa. Itokeapo kwamba fani inalegalega, basi hata
maudhui itakuwa vigumu kuyafikisha yalivyokusudiwa. Hali kadhalika, upo umuhimu
mkubwa kwa maudhui kuwepo katika fani bora. Vile vile tutaangalia jinsi vipengele
mbalimbali vya fani vinavyoweza kuleta athari mbalimbali katika hadithi.
Katika utanzu wa hadithi, fani yake huzingatia mambo mbalimbali yakiwemo lugha,
mandhari, mtindo, mtiririko wa visa (muundo) na mengineyo ambayo tutayaangalia
kiundani zaidi hapa na hasa kuona vipengele hivyo jinsi vinavyotegemeana na
kuhusiana katika kuunda na kukamilisha fani ya hadithi za Kiswahili.
Wahusika
Katika kujadili kipengele hiki, ni muhimu kuangalia mambo yafuatayo:
- Jinsi wahusika hao wanavyojengwa na
- Jinsi wanavyojitokeza katika kazi ya sanaa inayohusika.
Wahusika huwa ni watu, wanyama, vitu au viumbe wa kufikirika. Mwandishi wa
hadithi, huwajenga wahusika wake kisanaa ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali
za uhalisi wa maisha katika jamii.
3
KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA SITA
Kwa hiyo, mwandishi wa hadithi au kazi yoyote ya fasihi hukabiliwa na kazi kubwa
ya kuwaonyesha wasomaji wake jinsi wahusika wake walivyo; iwapo ni watu kwa
kuwatambulisha na sifa zao; mambo wanayoyapendelea, na yale wasiyoyapenda,
jinsi walivyo, wanavyokabili maisha, n.k. Matumizi ya lugha ya wahusika hao pia
huwa muhimu. Jinsi wahusika wanavyotumia vipengele mbalimbali vya lugha kama
tamathali za usemi, misemo mbalimbali, nahau, methali, n.k.
Baadhi ya wasanii, wameamua kuwapa wahusika wao majina yanayoelezea au
kufafanua tabia zao. Msanii maarufu katika kutumia mbinu hii katika uandishi wa
Kiswahili ni Shaaban Robert, ambaye hutumia majina ya: Hisidi kwa mtu hasidi, Adili
kwa mtu adili, Mwivu kwa mtu mwenye tabia ya wivu, utubusara kwa mtu mwenye
busara. Hata mahali ambapo matukio ya hadithi yanatokea, kwa sababu ni pa kufikirika
tu, anapaita Ughaibu, kufikirika n.k.
Namna nyingine ni ile ya msanii kuwaelezea yeye mwenyewe jinsi walivyo.
“NYANGEZI alikuwa mtu mwenye roho iliyotakata, roho iliyompenda kila mmoja
kikijini pao. Maneno yaliyokuwa yanataka ulimini mwake yaliwapendeza wote,
licha ya kuwa na busara yeye hakuchagua hirimu ya watu…..”
Namna nyingine ni ile ya kuwaumba wahusika kutokana na matendo yao katika hadithi.
Jinsi wanavyotenda, wanavyosema, wanavyowaza, maumbile yao na kadhalika.
Kutokana na ujengaji wa wahusika wa namna hii, msomaji anaweza kumwona mhusika
akionyesha wasifu wake wa ndani na nje au anaweza kuonyesha mabadiliko yake.
Wakati mwingine ikibidi, mwandishi anaweza kumjenga mhusika mmoja kwa njia
ambayo ni tofauti na wahusika wengine katika kazi yake kwa makusudi ili aweze
kujenga dhamira aliyokusudia.
Msanii anaweza kuwawasilisha wahusika katika udhahiri. Katika mbinu hii sifa na
matendo ya mhusika yanaelezwa waziwazi. Msomaji akishasoma hadithi inayohusika
anaweza kumwelewa sana mhusika huyo.
Njia hii ya uumbaji wahusika husaidia kumfanya msomaji asipate taabu katika
kutambua kiini cha kisa, wazo au dhamira, msanii hapa anamjenga na kumtumia
mhusika huyo kutoka mwanzo hadi mwishoni mwa hadithi yake.
4
KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI
Uwasilishaji dhamira kwa upande mwingine huenda pamoja na mbinu nyingine za
usimuliaji wa hadithi.
Kwa kawaida uwasilishaji dhamira hutokea wakati hadithi inaposimuliwa na msimulizi
wa nafsi ya kwanza. Mfano wa hadithi hizo zinaweza kupatikana katika kitabu cha
Kichwamaji kilichotungwa na Euphrase Kezilahabi. Katika usimulizi wake, mhusika
mwenyewe hujieleza na kueleza kila jambo analolitenda.
Udhahiri pia unajitokeza wakati hadithi inaposimuliwa na mhusika mmaizi. Msimulizi
huyo ni wa nafsi ya tatu ambaye anazijua siri zote za wahusika wote. Ni msimulizi
anayeweza kuweko kila mahali kwa wakati mmoja na anayejua tangu mwanzo mambo
yote katika dunia yake ya hadithi. Uumbaji huu unaweza kutumia utangulizi ambao
mwandishi msanii anaweza kuuweka mwanzoni.
Msanii anaweza pia kuwaumba wahusika wake kwa kuwawasilisha kimatendo.
Katika aina hii ya uwasilishaji, msanii hutumia ufafanuzi na huambatisha maoni yake.
Sehemu kubwa aghalabu huachwa kwa msomaji anayetakiwa afasili maana na sifa za
mhusika kwa kutoa vitendo kidogo kidogo, nusu nusu, hatoi matendo yote mara moja.
Msanii hutumia mazungumzo ya wahusika kama vile kati ya mhusika na mhusika.
Hapa ndipo wazo la mhusika linapofafanuliwa. Kwa kuyaunganisha mazungumzo
yote ya wahusika kutoka mwanzo hadi mwisho tunaweza kuijua tabia na pengine
maumbile ya wahusika wa kazi ya sanaa inayohusika.
Makundi ya wahusika
Katika hadithi, tunaweza kuwagawa wahusika katika makundi matatu muhimu
ambayo kwayo hutumiwa na mwandishi kutolea dhamira zake. Makundi hayo ni ya
wahusika wakuu, wahusika wasaidizi na wahusika wajenzi.
a) Wahusika wakuu
Wahusika hao, ambao kwa kawaida ni mmoja au wawili hujitokeza kutoka mwanzo
hadi mwisho wa hadithi. Mara kwa mara wahusika hawa hubeba kiini cha dhamira
kuu na maana ya hadithi yote katika wahusika wa hadithi za tanzia, wahusika wengi
huonyesha mabadiliko mengi kama vile anguko pia mhusika hufikia kilele na mwisho
5
KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA SITA
akaanguka. Pengine mhusika anaweza kuonekana anapanda na kuwa mashuhuri, na
halafu akakuwa duni katika hadithi.
Wahusika wakuu wanaweza kuwakilisha vikundi, jamii au mtu binafsi.
b) Wahusika wajenzi
pamoja na kuwepo kwa wahusika wakuu, wapo pia wahusika wajenzi. Wahusika hao
ni muhimu sana kama walivyo wahusika wakuu katika kazi ya sanaa. Wakati mwingine
wahusika wa aina hii hujengwa sambamba na wahusika wakuu katika juhudi ya
kuwajenga na kuwafafanua vizuri zaidi wahusika wakuu. Kuweko kwa wahusika hao
kunasaidia sana kuipa hadithi ama kazi nyingine ya sanaa mwelekeo muhimu wa
kisanaa na maudhui. Wahusika hao wana tabia ya kujitokeza mara moja moja. Kwa
jumla wahusika wote hawa wana tabia ya kuhusiana na kutegemeana. Wanasaidia
kukuza, kudumaza ama kufanya maamuzi muhimu ya hadithini.
Tabia za wahusika
Katika makundi mawili ya wahusika tuliowaona hapa juu, tunaweza kupata tabia za
wahusika za aina tatu. Tabia hizo ni za ubapa, uduara na ufoili.
i) Ubapa: ubapa huwakilisha aina moja tu ya tabia kutoka mwanzo hadi mwisho wa
hadithi. Toka mwanzo hadi mwisho tabia hii inajidhihirisha katika mhusika anayeishi
katika wazo na sifa za aina moja bila kubadilishwa na wakati, mazingira, uhusiano
wao na wengine, n.k. Tabia hiyo haibadiliki kufuatana na hali za kawaida za maisha ya
binadamu zinazobadilika kihistoria. Tabia hii inaelezwa kwa kutumia wahusika bapasugu
na wahusika bapa vielelezo.
Wahusika bapa-sugu ni wale ambao wanaonyesha msimamo wao kutokana na
maelezo ya msanii. Wanakuwa sugu katika maana kwamba hawabadiliki, kila
wanapoonekana hali zao huwa ni zile zile, hawahukumiwi bali huhukumu tu,
hawashauriwi bali hushauri tu, hawaongozwi bali huongoza tu.
Wahusika bapa-vielelezo kwa upande mwingine ni wale ambao pamoja na
kutobadilika kwao, wanapewa majina ambayo humfanya msomaji aielewe tabia na
matendo ya mhusika huyo.
6
KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI
Katika hali hii ya wahusika, msanii anatilia mkazo wake katika aina moja ya tabia
inayotawala, na ambao iwafikie wasomaji kiasi ambacho sehemu zote za sifa za
mhusika huyo hazitokezi. Aidha, wahusika bapa hawawakilishi hali halisi ya tabia za
watu wanaoishi, kwa kawaida huonyesha kipengele kimoja tu cha tabia hata kama
wanakutana na mazingira mbalimbali.
ii) Uduara: uduara ni tabia ambayo mhusika mmoja hujenga akionyesha tabia tofauti.
Wahusika wa aina hii wanaonyesha aina mbalimbali za tabia katika hadithi ama
kazi nyingine japokuwa nazo haziwi zote zinazomhusu binadamu. Tabia ya uduara
humfanya mhusika kubadilikabadilika kihulka, kimawazo na kisaikolojia.
Wahusika wenye tabia hiyo huonyesha kubadilika ambako kunatokana na msukumo
wa nguvu zilizomo katika mazingira mapya. Sifa kuu ya wahusika wenye tabia hiyo,
hadithini huishi maisha kawaida yanayofanana sana na jamii kiasi ambacho msomaji
huwakubali kuwa ni wahusika hai.
iii) Ufoili: ufoili ni tabia inayojidhihirisha kati ya wahusika duara na wahusika bapa.
Lakini pia ni tabia inayoonyesha hali zaidi kuliko wahusika bapa. Ili waweze kujengeka
vyema, wahusika wenye tabia hii huwategemea sana wahusika duara na wahusika
bapa. Kwa hiyo, wahusika wenye tabia ya ufoili wana msukumo wa nafsi ulio tofauti
na wahusika wakuu ama wahusika wengine muhimu katika kazi ya sanaa.
MFANO WA HADITHI FUPI: MAMA WA KAMBO
Mama wa kambo:
Mzee Mnene alikuwa na wanawake watatu: Nyirabagenzi, Upendo, na Tunu.
Nyirabagenzi alikuwa na mototo aitwaye Kagabo na Gasunzu. Baada ya miaka Fulani
Nyirabagenzi akaachana na mzee Mnene Mnene. Mototo wake Kibaya akalewa na
mama yake wa kambo, Upendo. Kibaya alionekana kuwa mototo hodari kwa masomo
na kwa kazi. Walimu wake walikuwa walimpenda kwa sababu ya uelevu wake. Lakini
badala ya kutumia mda wake kwa kusoma mara nyingi aliutumia kwa kufanya kazi za
nyumbani kwa kupika chakula, kuchota maji, kuuza andazi, kufua nguo na kadhalika.
Vile vile siku nyingi hakuenda shuleni kwa sababu ya kukopa karo za shule iwapo
baba yake alikuwa mfanyabiashara huko Nyabugogo. Wakati ndugu zake walikuwa
7
KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA SITA
wanafishwa vizuri na kuwepo ruhusa ya kutembelea, Kibaya yeye alikuwa anaambulia
makombo, anavaa kufa Ulaya na kufanya kazi kama punda.
Mzee Mnene hakujali yaliyofanyiwa mtotowe kwa kuwa alikuwa anafanya zamu ya
siku tatu kwa kila mwanamke na kuzamia katika shughuli nyingine. Hivyo kibaya
hakuwahi kuendelea na masomo katika sekondari. Wakati mmoja, Kibaya aliugua
Malaria akakosa mtu wa kumpeleka hospitalini. Mpangaji wa hapo anampeleka
hospitalini kila asubuhi kwa kiutumia baiskeli yake alipopata nafuu alikataa kufanyia
Upendo kazi zile zote bila malipo. Wakati huo alikuwa na miaka 18. Upendo alimshitaki
kwa Mzee Mnene kuwa Kibaya anamtaka anamwambia kumtandikia. Kutoka siku ile,
Mnene akachukua uamuzi wa kumpiga marufuku. Kijana huyo alisaidiwa na mzee
Sembabazi kwa kumtafutia kazi katika Kumekucha Hoteli. Kwa uhodari wake wa
kupenda kazi alipendwa mwajiri wake hata na hoteli ikawa na wateja wengi. Lakini
siku moja KUMEKUCHA HOTELI ilipata ajali ya kuungua na moto na hoteli hiyo
ikateketezwa yote. Kibaya mwenyewe aliugua vibaya.
Kibaya alikaa hospitalini kwa muda wa miezi minane na baadaye akarudi kwa mzee
Sembabazi akiwa mlemavu. Alitafuta nyia ya kujifunza kwa kushona viatu. Kwa bahati
nzuri, kampuni ya Bima ilimbalikia faranga milioni nne kwa ulemavu wake. Fedha
hizo ndizo zilikuwa chanzo cha kazi yake ya ubiashara. Kibaya aligeuka mtu tajiri sana
na akapatiwa jina la Kizuri badala ya Kibaya.
Wakati alipokuwa katika shughuli za kufunga ndoa na msichana aitwaye Amina,
alivamiwa na majambazi. Majambazi hao walikuwa wanaongozwa na ndugu zake
(watoto wa Upendo, Gasunzu na Kagabo).Lakini hawakufanikiwa bali ujambazi huo
uliwageukia wakaaga dunia wote wawili. Upendo aliposikia habari hiyo naye aliamua
kujiuwa. Mazishi yao yakafanyika siku moja.
UCHAMBUZI WA HADITHI FUPI: MAMA WA KAMBO
1. MAUDHUI
a) Dhamira kuu
Dhamira kuu katika hadithi ya Mama wa kambo ni:
8
KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI
- Kutoswa kwa mama wa kambo: Kibaya alipata mateso yaliyotokana na
Upendo, mama yake wa kambo (kuachishwa shule, kufanya kazi kama punda,
kushambuliwa, kufukuzwa)
b) Dhamira ndogo
- Ushirika wa ndoa: Mnene alioa wanawake watatu
- Kuachika kwa ndoa: ndoa ya Mnene na Nyirabagenzi iliachika.
- Huduma mbaya za wazazi (malezi mabaya): mnene kwa kutokuwa mwangalifu
hakufuata malezi ya Kibaya na mwishoni alimfukuza.
- Kutakia wengine misaada: Mzee Sembabazi alimtakia Kibaya msaada kwa
kumtafutia kazi. Mpangaji wa nyumba naye alimsaidia Kibaya.
- Mapenzi: mapenzi yanadhihirishwa na Kibaya na Amina.
- Hudhuma za serikali ya kampuni ya bima: serikali na Kampuni ya bima
ilifanya kazi zao ipasavyo (bila rushwa au kuchelewesha kazi).
- Dini: dini ni taasisi muhimu katika kukuza utu na ubinadamu. Misaada ya
waamini wa Kiislamu wa Kibaya.
- Uwivu: Upendo alionea kijicho mafanikio yote ya Kibaya akaamua kumtesa na
kumkera kwa fitina na wengine.
- Ujambazi: ndugu zake Kibaya yaani Kagabo na Gasunzu walishambulia Kibaya
kwa ajili ya kumnyanganya mali yake na kumuondoa duniani.
- Kujuta: kujutia kosa baada ya kutofanikiwa katika maovu na kuangamizwa na
miradhi uliotengenezwa.
Maadili:
1. Mwavu huangamizwa na matendoye: Upendo, Gasunzu na Kagabo walipata shida
kwa sababu ya wivu na matendo mengine ya uovu.
2. Majuto ni mjukuu: Upendo alijutia na kosa lake.
9
KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA SITA
3. Mwenyezi Mungu ndiye mwongozi wa matendo yetu: Upendo alipanga mara
nyingi kumuangusha hata kumuondoa duniani Kibaya lakini hakufanikiwa.
4. Mtaka makaa ya migomba haoni kitu ila majivu tu.
5. Tamaa mbele mauti nyuma: Gasunzu na Kagabo walikuwa na nia ya kujitayarisha
kwa kumshambulia Kibaya lakini walijipatia mauti ya kifo.
6. Rafiki humuoni katika dhiki: Sembabazi aliyemsaidia Kibaya, Amina:
- Kujitegemea kwa kutumia ubima,
- Bora kuzaa watoto wa kutunza na kuletewa malezi mema.
- Mama wa kambo si mama
FANI
Wahusika
Aina za wahusika:
- Wahusika wakuu: wahusika wakuu ni wawili: Kibaya na Upendo. Kibaya ni
mhusika mkuu wa kweli na Upendo ni mhusika mpinzani wa Kibaya.
- Wahusika wasaidizi:
- Mzee Mnene, Gasunzu na Kagabo ni wahusika wasaidizi wa upendo.
- Nyirabagenzi, Sembabazi, Mpangaji wa nyumba, Amina ni wahusika wasaidizi
wa kibaya.
- Askari, afisa wa kampuni ya bima, ni wahusika wajenzi waliogeuka wasaidizi
kwa Kibaya.
Methali zilizotumiwa:
1. Siku njema huonekana asubuhi
2. Kuzaliwa mwanamke ni balaa.
3. Kazi ndiyo msingi wa uhai
10
KISWAHILI : SANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI
4. Ng’ombe wa maskini hazai
5. Alichokipoteza Mwenyezi Mungu hakuna binadamu wa kukiongoza na

Powered by Blogger.