MWONGOZO WA KUTAHINI


(a) Sifa za lugha:
Lugha ni mfumo
Lugha ni ishara
Lugha ni nasibu
Lugha ni sauti
Lugha ni mawasiliano
Lugha ni sifa ya binadamu
Ufafanuzi ufaao wa hoja zozote tatu: Alama 2 x Hoja 3 = Alama 6
(b) Malengo ya taaluma ya Isimu
Kuchambua na kueleza maarifa au umilisi wa mzawa wa lugha kuhusu lugha yake.
Kuunda nadharia, nadharia husaidia kuonesha
ruwaza zilizomo katika lugha na jinsi
inavyofanya kazi.
Kubainisha mbinu za kisayansi za kuchambua lugha ili matokeo yaweze kukubalika na
yawe yamejengwa kwa misingi thabiti.
Ufafanuzi toshelezi wa hoja : alama 2 x Hoja 3 = Aalama 6
(c)
Tofauti kati ya
lugha ya binadamu na mawasiliano ya wanyama:
Lugha ya binadamu ni ishara ya sauti ila wanyama hutumia milio tu
Binadamu ana uwezo wa kujifunza lugha iliyomo katika mazingira yake, wanyama
hawana uwezo wa kujifunza lugha
Binadamu ana uwezo wa kuelezea mambo
yaliyopo, layiyopita na yatakayokuja,
wanyama hawana uwezo huo, ila nyuki kwa kiwango kidogo sana
Binadamu akilelewa katika mazingira ombwe yasiyo na lugha, hatakuwa na lugha yoyote
ila mnyama akilelewa katika mazingira kama hayo atatoa milio ya aila yake
Binadamu harithi lugha bali hubwia
(d) i. Fonetiki
Fonetiki ni kiwango cha isimu kinachojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa
taratibu zote zin
azohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za
lugha za binadamu kwa jumla.
-
Husaidia kuimarisha matamsi bora ya sauti na kwa hivyo kuimarisha matumizi ya
lugha fasaha.
ii. Fonolojia
Fonolojia ni kiwango cha isimu ambacho huj
ishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na
uanishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimba
Powered by Blogger.