ISTILAHI ZA FASIH

I
Adili (Moral): Funzo, elekevu, nyofu. Mambo yanayohusu malezi katika jamii. Kwa mfano: Vitabu vingi vilivyoandikwa wakati wa ukoloni ni vile vyenye maadili maovu.
Arudhi (Prosody): Elimu ya kanuni za ujenzi ama mawako ya ushairi. Ni jumla ya urari wa mizani, silabi, beti, vina, usuli na matumizi ya lugha kwa ujumla. mf. Arudhi ya ushairi wa kimapokeo, ni kule kuwa na misingi iliyotajwa.
Balaagha (Exaggeration): Chuku. Tia chumvi nyingi. mf. Alipiga shuti kali mpaka mguv wake ukachomoka. Hata hivyo alifanikiwa kufungd goli kwa mguu wake mmoja!
Bapa (Flat): Mhusika aliye kama picha anayeonyesha tabia fulani tu katika kazi ya sanaa, hususan hadithi. Mhusika bapa hawakilishi hali halisi ya maisha.
Bibliografia (Bibliography): Orodha ya vitabu na/au makala yaliyosomwa na pengine kunukuliwa na mwandishi katika kazi yake. Marejeo. Mf. Tazama Biliografia katika kitabu hiki
Chapwa (Obsolete): Kutokuwa na ladha nzuri, kutokuwa na ufundi wa kisanaa uliokuwa mwanzo. Mf. Hadithi za fasiht simulizi zikiandikwa zinakuwa chapwa kwa sababu ya kupoteza mambo mengi yanayokuwepo katika usimulizi.
Dialogia (Dialogue): Masimulizi yanayofanywa na wahusika zaidi ya mmoja katika kazi ya sanaa inayotumia lugha. Majibizano. Mf. Tamthiliya nyingi zinazingatia matumizi ya dialogia. Tazama pia mazungumzo yafuatayo:
"Unataka nini?"
"Kula"
"Chakula gani?"
"Ugali"
"Mboga?"
"Nyama"
"Nyama hakuna"
"Maharage?"
"Yapo"
"Basi nipe ugali na maharage."
Dialogia ina kazi mbalimbali katika kazi ya sanaa ya kifasihi mayotumia lugha.
Dhamini (Sponsor): Toa fedha ili jambo fulani lifanywe. Mf. Mtu kama ameshtakiwa anaweza kutolewa nje kwa dhamana. Au mtafiti kama anataka kufanya utafiti kuhusu jambo fulani, mashirika makubwa ya kibepari kama vile Ford Foundation yanaweza kumdhamini mtafiti huyo. Hasara ya udhamini ni kuwa mtafiti hawezi kwenda kinyume cha matakwa ya mdhamini wake.
Dhamira (Theme): Wazo kuu katika kazi ya fasihi. Pia mawazo mengme katika hiyo kazi ya sanaa itumiayo lugha. Mf. Dhamira kuu ya kitabu cha Kiu ni ya mapenzi.
Dhana (Concept): Wazo, picha au umbo la kitu fulani katika akili za mtu. Uonaji wa kimoyomoyo, fikra. Mf. Dhana muhimu inayojitokeza katika kitabu cha Mzalendo ni ukombozi wa miu kutoka ukoloni mkongwe.
Dhihaka (Sarcasm): Maelezo au masimulizi yaliyokusudiwa kubeuwa jambo kisirisiri. Ni maelezo yanayomdunisha mtu kifumbo. Mf. Tazama maelezo humo kitabuni.
Diwani (Anthology): Mkusanyo wa kazi za maandishi. Kazi hizo zinaweza kuwa za kifasihi kama vile hadithi fupi, mashairi n.k. Lakini pia diwani inaweza kuwa mkusanyo wa kazi za insha kama vile Kielezo cha Insha, ama insha mbalimbali kuhusu mada muhimu katikajamii. Kuna mifano mingi ya diwani, kama Parapanda (G. Ruhumbika) Diwani ya Massamba (Massamba). Mfano mwingine ni ule ulioko katika kitabu hiki.wa Diwani ya Hadithi fupi.
Drama (Drama): Aina ya utungo wa kazi ya sanaa unaotegemea utendaji. Utendaji unazingatia mbinu za uigizaji wa vitendo, tabia na mawazo ya binadamu. Mf. Lina Ubani (P. Muhando), Harakati za Ukombozi (Muhando, Lihamba na Matteru), Kapiula la Marx (E. Kezilahabi).
Falsafa (Philosophy): Wazo ambalo mtu anaamini lina ukweli fulani unaotawala maisha yake pamoja na maisha ya jamii.
Fani (Form): Umbo, ufundi, umbo au muundo wa kazi ya sanaa. Mambo kama lugha itumikayo, mtindo, muundo, mandhari n.k. Fani pia ina maana ya tawi. Mf. Fani ya ushairi, fani ya hadithi fupi, fani ya tamthiliya, fam ya nyimbo n.k. Ili kutofautisha dhana hizo mbili, maana ya kwanza ya fani itahusu umbo la kazi ya sanaa inayotumia lugha. Maana ya pili itahusu tawi la kazi ya sanaa na ambayo imepewa istilahi ya utanzu. Taz. Utanzu.
Fasihi (Literature): Taaluma maalumu inayoshughulikia kazi za sanaa zinazotumia lugha. Mf. Biwaya, hadithi fupi, ushairi, tamthiliya n.k. Fasihi ni moja, lakini kutokana na mbinu za uhifadhiaji wake tunasema kuna aina mbili za fasihi: Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi. (Taz. Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi).
Fasihi Andishi (Written, Literature): Kazi ya sanaa itumiayo lugha iliyo katika maandishi. Fasihi hii imekuwa ikihifadhiwa kimaandishi na kusomwa katika vitabu na magazetini. Fasihi hii imegawanyika katika matawi mengine ambayo ni ya ushairi, tamthiliya, riwaya, hadithi fupi, n.k. Kwa sasa ziko kazi za sanaa zinazoandikwa ambazo asili yake ni fasihi simulizi.
Fasihi Kale au Fasihi Kongwe (Old LHerature): Inaweza kuelezwa kwa dhana mbili.
(i) Fasihi ile ambayo imekuwa miongoni mwa'jamii toka zamani sana. Fasihi hiyo, japokuwa ni ya zamani, bado inahitajika na ni muhimu miongoni mwa jamii inayohusika. Mf. Fasihi Simulizi. Japokuwa fasihi hiyo m ya zamani sana ukilinganisha na Fasihi Andishi, umuhimu wake bado upo katika jamii ya sasa.
(ii) Fasihi ile ambayo ni ya zamani na kwamba kwa sasa imepitwa na wakati, haina thamani tena. Ni fasihi ile ambayo hailingani na hali halisi ya mfumo wa maisha yajamii inayohusika.
Fasihi Leo (Contemporany Literature): Hii ni fasihi ya kipindi kilichoko chini ya mfumo wa kisiasa, kihistoria na kitamaduni ulioko. Fasihi Leo wakati mwingine huambatana na hujipambanua zaidi kwa migogoro ya jamii ya wakati huo, na. pengine huambatana na mabadiliko ya kifani. Mf. Katika Tanzania tungeweza kusema kuwa Fasihi Leo inaanzia na kutangazwa na kupokelewa kwa Azimio la Arusha. Azimio na Arusha limekuwa chombo kikubwa cha kiitikadi kwa wasanii wa Tanzania. Tazama pia Itikadi
Fasihi Simulizi (Oral Literature): Kazi ya sanaa itumiayo lugha iliyo katika masimulizi. Fasihi hii imetuwa ikihifadhiwa kwa kichwa na kusimuliwa kwa njia ya mdomo ikipokezwana katoka kizazi hadi kizazi. Aidha, imekuwa ikibadilika kutoka muda hadi muda Mf. Ngano, hekaya cf. Hekaya za Abunuwasi n.k., misemo, n.k. Fasihi hii imegawanyika katika matawi (tanzu) mbalimbali ya ushairi, nyimbo, hadithi, misemo n.k.
Foili (Foil character): Wahusika (mhusika) shinda. Wahusika wenye tabia na matendo ama msukumo wake wa nafsi ulio tofauti na tabia ya mhusika mwingine muhimu katika kazi ya fasihi. Tazama Wahusika.
Hadhira (Audience): Washiriki, watazamaji, wasikilizaji au wasomaji wa kazi za sanaa zinazotumia lugha. Mf. Tamthiliya inahitaji uwanja au mahala pa kutendea (jukwaa), hadhira (watazamaji) na watendaji (waigizaji). Mfumo huo hufuatwa pia na watambaji wa hadithi za fasihi simulizi.
Hadithi (Story): Masimulizi ya nathari (ujazo) ya kisanaa yanayotumia lugha. Hadithi lazima isimulie tukio fulani kwa wakati fulani, iwe na muundo, mtindo, ifanyike katika mandhari fulani, itumie lugha ya kisanaa, n.k.
Hadithi fupi (Short Story): Aina ya kazi ya sanaa ya utanzu wa hadithi inayotumia lugha iliyoandikwa katika nathari au iliyo katika masimulizi kama haijaandikwa. Hadithi ya aina hii inasimulia tukio moja au matukio mawili na inatumia mawanda yasiyo mapana sana, haina mchangamano mkubwa wa matukio. Hadithi fupi hutumia wahusika wachache sana ukilinganisha na wale wa liwaya, hutendeka kwa muda mfupi na ina mtiririko wa kiupeo. Mf. Tazama hadithi mbalimbali humo kitabuni na katika Mzalendo, Kiongozi, Mambo Leo, Nchi Yetu, Nyota ya Afrika Mashariki, Taifa, n.k.
Hadithi ya Kibarua (Barua) (Epistolary Story): Hadithi iliyo katika ujazo na ipo katika muundo wa barua.
Hadithi ya Kihistoria (Historical Story): Hadithi inayosimulia matukio kufuatana na kutokea kwake katika historia. Tarikh. Ni maandishi ya kifasihi yanaypsimuliwa na kusimulia mambo kufuatana na tarehe maalumu za kihistoria.
Hadithi Kikufu (Cumulative Story): Ni hadithi katika fasihi simulizi ambamo visa mbalimbali huzaliana kutokana na masharti mbalimbali kabla ya mhusika mkuu kufikiwa lengo linalotakiwa. Mf. Tazama Tiba katika Johari Ndogo F.V.Nkwera.
Hadithi la Maumbile (Environmental Story): Hadithi ambazo huelezea hali ya maumbile mbalimbali ya mazingira. Mf. Hadithi kuhusu majengo, maumbile ya watu na wanyama n.k.
Hadithi ndefu (Novel): Riwaya Ni kazi ya sanaa ya kubuniwa inayotumia lugha iliyoandikwa (au iliyo katika masimulizi-kama haikuandikwa) katika nathari (ujazo). Kuna mifano mingi katika Kiswahili, kama vile Dunia Uwanja wa Fujo (E. Kezilahabi), Njozi Iliyopotea (C. Mung'ong'o), Nyota ya Rehema (M.S.Mohamed) n.k. Upana wa mawanda ni jambo muBimu sana linaloifanya kazi ya hadithi ndefu kuwa tofauti na hadithi fupi.
Hadithi ya Propaganda (Propaganda Story). Hadithi iliyoandikwa kwa makusudi maalumu ya kutangaza na kutetea suala fulani kwa manufaa ya watu fulani. Mara nyingi huwa kwa manufaa ya tabaka tawala. Kimsingi kazi za namna hii kila zikiandikwa hutokea wakati mwingine zinakumbana na matatizo ya kupokelewa na jamii.
Hadithi za Vitendo (Action Story): Hadithi yenye vitendo vingi ndani yake.
Harafa (Fable): Hii ni simulizi ambayo ni ya kimasimulizi. Mara nyingi harafa hutoa mafunzo kwa kuwatumia wanyama na kuwafanya watende, wavalishwe kama binadamu. Mf. Hadithi nyingi za simulizi ni za aina hii. taz. hekaya, ngano.
Hasidi (Villain): Ni rohusika mkuu mwenye tabia mbovu katika kazi ya fasihi. Pengine huitwa Mui. Mhusika Kasim katika riwaya ya Duniani kuna Watu (M.S.Abdulla).
Hekaya (Parable): Hekaya ni hadithi ya mapokeo inayotoa ama inayotumia fumbo fulani ili kutoa funzo muhimu. Mf. Hekaya za Abunuwasi.
Insha (Essay): Mtungo wa nathari wa kitaalumajuu yajambo fulani. Maandishi yanayotoa habari juu ya jambo fulani. cf. Maandishi ya nathari yanayojadili jambo ama wazo moja kwa ufupi ama mapana juu ya mada ambayo huelezwa kwa ufasaha. Mf. Kielezo cha Insha (Shaaban Robert).
Innuendo (Kijembe): Ni usemi wa mzunguko, usemi wa kifumbo na humsema mtu kwa ubaya.
Ishara (Symbol): Konyezo ama kitendo cha kupungia mkono au kitendo chochote cha kuvutia macho ya mtu au kumdokezeajambo. Alama, dalili, Mf. Hakuna ishara ya mvua = hakuna dalili ya mvua. Jicho lake lakonyeza, linacheza kama tete. Kukonyeza = ishara. Lina cheza kama tete = tamathali ya usemi.
Ishara (Allegory): Mtindo katika kazi ya sanaa ambao kwao vitu husimamia dhana ama wazo maalumu. Hadithi nyingi za kimapokeo ni za aina hii.
Istilahi (Literary term): Neno litumikalo kwa ufupi wa maneno mengi ya kiufundi kufuatana na ujuzi ama elimu maalumu. Mf. Istilahi za Fasihi, Istilahi za Kemia, Istilahi za Jiografia n.k.
Itikadi (Ideology):
(i) Mawazo fulani ambayo ni misingi ya nadharia za mfumo wa kisiasa au uchumi. Mf. Itikadi za Kijamaa, Itikadi za Kibepari...n.it.
(ii) Imani katika jambo fulani, kwa mfano dini: jinsi ya mapokezi yake, wanavyofuatajambo fulani, fikra za kuaminika n.k.
Jaribosi (Characters as opposed to main characters): Mhusika mpambe. Kutokana naye unaweza kupata sifa za wahusika wengine katika kazi za sanaa.
Jazanda (Imagery): Lugha ya kipicha, lugha ya kitaswira (imagery). Ni lugha ambayo huchora picha ya mahali kwa kutumia tamathali za usemi.
Kadhia (Incident): Tukio moja katika kazi ya sanaa. Mf. Tukio katika kazi ya tamthiliya, riwaya, hadithi fupi n.k.
Kaida (Convention): Mambo ambayo yamezoeleka na kukubalika katika jamii kwa wakati maalumu. Mf. Katika fasihi ya Kiswahili, kaida za ushairi wa kimapokeo ni pamoja na kuwa na urari wa vina na mizani n.k.
Kejeli (Irony): Hii ni tamathali ya usemi ambayo ina maana iliyo kinyume na kile kinachosemwa ama kuongelewa. Ni tamathali inayoleta maana iliyo kinyume na ukweli wa mambo ulivyo. Mf. Mtu ni nichafu lakini anaambtwa kuwa ni msafi sana.
Kichekesho (Farce): Aina ya sanaa ya utendaji ambayo madhumuni yake makubwa m kuchekesha hadhira. Mara nymgi hutumia wahusika ambao wanatilia chumvi sana. Kunakuwa na matukio ya ajabu sana.
Kidahizo (Anecdote): Masimulizi mafupi yanayoelezea tukio moja. Masimulizi hayo aghalabu hay.ajipambanui sana.
Kiini (Abstract): Kifupisho muhimu cha makala ama habari. Mf. Kifupisho cha tasnifu. Kiini ni kitu muhimu sana katika kazi ya fasihi. cf. Kiini cha habari.
Kikale (Archetype): Mtiririko, wahusika ama picha kongwe ambazo hujitokeza mara kwa mara katika kazi za sanaa Inawezekana inachukua picha tofauti mara kwa mara.
Kisuko (Sub-Plot): Huu ni mtiririko mdogo unaopatikana ndani ya mtiririko mkubwa katika kazi za sanaa, hususan riwaya na hadithi fupi.
Msuko (Plot): Huu ni mtiririko mkamilifu wa matukio katika kazi za sanaa. Katika riwaya kama ya Kichwamaji kisuko kimoja kilicho kamili ni kile cha kuigiza mchezo shuleni Nsurnba.
Kivuli-Mwanga (Light and Shade): Ni hali ya mwandishi ama msanii kuandika uzuri na ubaya kama unavyotokea katikajamii. Kwa kawaida Istilahi ya kivuli hutumika pamoja na ile ya nwanga.
Kubuni (Fiction): Masimulizi na/au maandishi ya kisanaa'yaliyobuniwa na kuonyesha ukweli fulani wa maisha katika jamii. Tukio la kubuniwa linaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja au kiishara. Mifano ya kazi za kubuniwa ni hadithi, ushairi, tamthiliya, n.k.
Lahaja (Dialect): Ni tofauti katika matamshi, mambo na matumizi ya maneno katika asili moja. Mf. Kimvita, Kiunguja, Kimakunduchi. zote ni lahaja za Kiswahili.
Lakabu (Synesthesia): Tamathaii ya usemi ambayo uhusiano wa kawaida wa maneno mawili kisarufi huwekwa kinyume.
Lugha (Language): Mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kabila moja kwa ajili ya kuwasiliana. Maneno na matumizi yake Mtindo anaotumia mtu kujieleza
Lugha Bayana (Dry Language): Lugha itoayo maana halisi. Lugha kavu.
Lugha Hisishii (Lugha mguso): (Emotive Language) Lugha inayogusia vionjo. Ni lugha inayogusa hisia za mtu na kujaribu kuathiri maoni yake kuhusu jambo fulani linalozungumziwa katika kazi ya sanaa. Mf. Maneno yake yalikuwa makali kiasi cha kuchoma maini yangu!
Lugha Sanifu (Standard Language): Lugha isiyo lahaja. Ni lugha ambayo inatumika rasmi katika shughuli mbalimbali za jamii.
Lugha Tarafa (Dialect): Lugha itumikayo kwa mawasiliano ya aina fulani. Ni watu wachache mno wanaweza kuwasiliana kwa kutumia lugha hiyo. Angalia mfano huu uliochukuliwa kutoka katika Gazeti la Mfanyakazi la Machi 16, 1985, ulioandikwa na Francis Mwakajongo.
'Check Bob mmoja. pamoja. na kikwapa chake (mke wake) waliamua kumwendea Mjumbe wa Nyumba kumi. Kufuatana. Ma agizo la kila mtu afanye kazi, walipofika kwa Mjumbe wa nyumba kumi mambo yakawa kama ifuatavyo:
Check Bob: Yee! Mjumbe, digree kama digree mimi oyee tu. Nadlani umeiget Fresh kuhusu nguvu - nguvu kazi au vipi. Mimi ndo nimecome ili unisave hiki kisanga. Maaaa mimi ndo longtime niko hapa town bila job nadunda na memsheni tu. Na vilevile ndo nina wiki bee tu (mbili)) tangu niopoe hiki kikwapa. Wewe mwenyewe ukicheki kikwapa, ckenyewe waa! gawa kwenda nacho bush nishai nishai au vipi Mjumbe? Serikali yenyewe inatutia mikwara sana. Sasa shika hivi visimbi (fedha) vya anda bee na kitembo (210) kusudi mimi nibane hapahapa iown. Hawa kinaa (askari) watilie mikwala mingi kwamba mimi ndo long-time nina job. Kwani memsheni hii ikijipa utaipata mwenyewe Mjumbe!
Mjumbe kabaki amepigwa na bumbuazi aaielewe kitu.
Kauli hii ya mwisho inaonyesba kuwa lugha hiyo iliyotumika haieleweki kwa watu wengi, na kwamba ni lugha ya kitarafa, m baadhi ya watu tu wanaoifahamu na kuitumia vyema!
Lugha Teule (Diction): Matunuzi ya lugha katika kazi ya fasihi. Uteuzi wa maneno unaozingatia matumizi mazuri ya tamathali za usemi, ridhimu, matumizi ya methali na kadhalika. Ni uteuzi wa maneno na matumizi ya tamathali za usemi, wizani, n.k. katika kazi za fasihi. Tazama mfano huu wa shairi liitwalo Rekebisha Yako Saa (Halijachapishwa) lililotungwa na Bi Christine Njombi.
Mwisho tulipoagana, kwa majonzi na imani
Nakumbuka ulinena, akadi tuithamini
Lipi lililokushona, likakufunga moyoni
Rekebisha yako saa, inapotexa majira
Ahadi yetu iwapi, tulopeana sahibu
Umeivuruga vipi, nani alokughilibu
Mtu huyo ni wa wapi, alojipa utabibu
Rekebisha yako saa, inapoteza majira
Tukisoma beti hizi mbili tu za shairi hili, tunaweza kutambua mbinu ambazo mwandishi ametumia katika kufanya uteuzi wa maneno na kuyapanga ili yaweze kuleta athari na hisia ambazo mwandishi ametaka ziwafikie wasomaji wake.
Mandhari (Mazingira): (Setting) Sura ya mahali aghalabu, ardhi inavyoonekana. Mf. Mandhari ya hadithi, mandhari ya tamthiliya n.k.
Maudhui (Content): Mawazo, fikra na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi.
Mbinu Rejeshi: (Flashback): Mbinu ambazo kwazo msanii hurudia mambo yaliyokwisha simuliwa awali. Muundo wa kioo. Tazama kielelezo kifaatacho:
Hadithi ya aina hii huanzia kusimuliwa katika A kupitia B hadi C. Lakini kila ikisimuliwa kuelekea C kuna kwenda mbele na nyuma kama mishale inavyoonyesha. Tazama pia kisengerenyuma.
Mchezo Bubu (Mime): Huu ni mchezo ambao mara nyingi, ama kwa kiasi kikubwa unategemea matendo kuliko maneno.
Methali (Riddle): Kifungu cha maneno yaliyosaniiwa kwa njia ya kufumba au kupigia mifano na ambacho kinachukua maana ndefu kuliko vile kinavyoonekana. Muhtasari wa maneno ya kisanaa yenye maana pana Mf. Bandu! Bandu! humala gogo. Bendera hufuata upe'po.
Metonumia (Metonymy): Hh m tamathali ya usemi inayotumia neno (userni) kuwakilisha neno, kitu, mtu au dhana nyingine yenye kuhusiana nalo. Tazama kwa mfano ubeti wa shairi hili la Rajabu M. Kianda (Selukindo) liitwalo Jembe.
Jembe wewe msifika
Utuonee huruma
Jembe shamba tukifyeka
Njoo ufanye kulima
Jembe njoo pasi shaka
Ukija lete mtama
Jembe ndiwe mtawala
Tangu enzi za wahenga!
Metonumia inafanana na tamathali za kitashihisi. Metonumia hutumika kwa dhana inayokaribiana au dhana ambayo ni sawa na ile mayozungumzwa. Kwa maelezo zaidi, tazama Kunga za Ushairi (1978:35) M.M. Mulokozi na K.K. Kahigi. (TPH, Dar es Salaam)
Mgogoro (Conflict): Hali ya kutoafikiana kwa pande mbili ama zaidi. Mgongano- katika kazi ya fasihi. Mgogoro unaweza kuzuka ama kukuzwa na uhusiano wa wazo na wazo, wahusika wawili ama zaidi, mtu na mazingira yake. Migogoro inaweza kuwa katika mifumo rnbalimbali: kisiasa, kitamaduni na kiuchumi.
Mpomoko (Anti-Climax): Hali iliyo kinyume na mategerneo ya hadhira inayokusudiwa katika kazi ya sanaa. Mf. Kuwashauri watu kwenda vitani. Wanapokuwa tayari na kukubali kwenda vitani, viongozi, badala ya kuongoza jahazi la vita, wanakimbia na kwenda kujificha ama wanawashauri watu kukimbia vita ambavyo hata hawajawahi kupigana.
Monologia (Monologue): Masimulizi katika kazi ya fasihi yanayofanywa na mtu mmoja tu. Mara nyingi hii hutokea katika tamthiliya, wakati mhusika mmoja anaonekana akizungumza peke yake mbele ya jukwaa juu ya masahibu yaliyokuwa yamemfika. Tazama pia Mjadala Nafsia.
Msanii (Artist): Huyu ni mtu anayeunda kazi za sanaa. Watu hawa ni kama vile wachoraji, wachongaji, waandishi wa tanzu mbalirnbali kama vile ushairi, tamthiliya, hadithi ndefu na fupi n.k.
Msanii Mtarazaki (Professional Artist): Msanii anayetoa sanaa yake ili kupata riziki yake ya maisha. Wasanii hawa ni kama wapiga muziki kama vile Intenational Orchestra Safari Sound, Orchestra DDC Mlimani Park, Orchestra Maquis Original, Muungano Ngoma Troupe n.k.
Msanii Mtarazaki Tinde (Part Time professional artist): Msanii anayepata malipo kutokana na kazi yake, lakini haitegemei sana kazi hii ya usami. Mfano ni waandishi wengi wa Tanzania ambao ni wafanyakazi na pia ni waandishi.
Mshabaha (Simile): Tashibiha. Hii ni tamathali ya usemi ambayo kwayo hulinganisha vitu viwili ama zaidi vyenye sifa tofauti kwa kutumia viunganishi kama vile mfano wa, kama, mithili ya, n.k.
Msimu (Cliche): Tamathali ya usemi iliyozoeleka sana katika matumizi yake.
Msimu (Cliche): Ni msemo wa kitarafa, msemo wa muda uzukao kulingana na mazingira fulani. Msimu huibuka na hudumu kwa muda mfupi halafu hufa. Wakati mwingine misimu hudumu, haifi Inapofikia hali hii, msimu hujitokeza kama nahau.
Msimulizi (Narrator): Mtu anayesimulia. Mf. Msimulizi wa hadithi fupi ama riwaya, lakini ni tofauti na mtambaji wa hadithi za fasihi simulizi Msimulizi anaweza kuandika hadithi yake Lakini mtambaji, lazima aiandae hadithi yake kichwani na kisha kuitamba kwa hadhira yake Kwa mtambaji lazima awe na mahali pa kutambia (kutendca), lazima awe na hadhira hai ambayo itamsikiliza, wakati rnsimulizi anaweza akawa na hadhira mahali popote na si lazima iwe inamsikiliza bali husoma kwa sauti ama kimyakimya. Mlambaji anayo nafasi ya kutia chumvi na kuongeza ama kupunguza kitu kila pale anaposimulia hadithi yake kwa kutamba. Msimulizi hana nafasi ya kuongeza ama kupunguza kitu kilichoandikwa. Tazama pia masimulizi.
Msimulizi Horomo (Narrator-Unintrusive): Huyu ni msimulizi wa nafsi ya tatu. Msimulizi huyu kwa kawaida hutoa habari tu na kuacha wahusika wa hadithi wazungume wenyewe kwa wenyewe bila ya kuwaingilia kati ama kutoa ushauri na maamuzi fulani ya msingi.
Msimulizi Mkengeushi (Narrator - Fallible): Huyu ni msimulizi anayetumia nafsi ya kwanza au ya tatu. Maadili yake kwa kawida hayalingani na mawazo ama falsafa ya mtunzi wa hadithi ama msomaji. Mf. Tazama sehemu ya kwanza ya kitabu cha Ndoto ya Ndaria, mfano huu pia umetolewa na Semina ya Fasihi (1978:TUKI).
Msimulizi Nafsi ya Tatu (Narrator - Third Person): Huyu ni msimulizi katika hadithi anayetumia nafsi ya tatu. Mf. Rosa Mistika, (E. Kezilahabi), Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani (E. Kezilahabi).
Msimulizi Tinde (Narrator-Limited): Ni msimulizi anayetumia nafsi ya tatu na ambaye anaelezea hisia na mawazo yanayojulikana na mhusika mmoja tu ama na wahusika wachache sana miongoni mwa wahusika wote wa kazi za sanaa, hususan hadithi. Tazama kwa mfano mawazo ya Msa katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale (1958) (EALB) kitabu kilichotungwa na Mohamed Saidi Abdulla.
Msimulizi Penyezi (Narrator-Intrusive): Msimulizi ambaye ni wa nafsi ya tatu ambaye mara nyingi hutoa mawazo yake kuhusu wahusika wa riwaya, vituko, mfumo wa matendo na masimulizi katika hadithi.
Mtamba Hadithi (Story teller): Msimulizi wa hadithi za fasihi simulizi. Mtamba hadithi kila mara anahitaji hadhira hai, mahali pamoja pa kutambia hadithi yake.
Msimulizi Maizi (Narrator - Omniscent): Msimulizi wa nafsi ya tatu anayezijua siri zote za wahusika wote, anayeweza kuwa kila mahali kwa wakati mmoja na anayejua mambo yote katika ulimwengu wake wa riwaya. Mtindo huu wa usimulizi unatumiwa sana na waandishi mbalimbali.
Mtindo (Style): Jinsi au namna ya kufanya kitu kwa kuzingatia misingi fulani. Katika kazi za sanaa, ni jinsi kitu kinavyoelezwa. 'Kitu kinachoelezwa.
Mtiririko (Structure) Mfuatano wa matukio katika kazi ya fasihi. Matuko lazima yajenge uhusiano na kisha kuleta mantiki ya hadithi.
Muktadha (Context) Mazingira ama hali inayoathiri maana ya neno, sentensi, ama sehemu ya kazi ya sanaa. Tazama pia Maana hali.
Msuko (Plot): Iluu ni mtiririko ama mfuatano wa matukio yanayosimuliwa kuanzia mwanzo hadi mwisho Hali hii huandamana na uchaguzi/mpangilio na ufundi wa kusimulia matukio yaliyoungwa vyema katika kazi ya sanaa ya kubuni itumiayo lugha. Muundo ndiyo huipa kazi ya sanaa ya fasihi kipengele kimojawapo cha fani na pia umoja wake. Penina Muhando na Ndyanao Balisidya wanataja miundo kadhaa ya adithi: Muundo Msago, Muundo wa Kioo, Mwanzo - Mwisho n.k.
Msuko Msago (Plot): Huu ni muundo wa moja kvva moja. Hadithi inaanza, inakua na kufikia upeo hadi mwisho. Angalia kielelezo.

Taswira
Katika kielelezo hiki, hadithi huanza kusimuliwa kwenye. A na kisha huendelezwa na kufikia kipeo B na hatimaye hufikia mwisho C.
Msuko-Kioo (Flashback) Tazama Mbinu Rejeshi hapa juu
Mtunzi (Author/Writer). Mwandishi. Ni yule anayetunga ama kuaudika makala, insha au kazi nyingme yoyote ya sanaa Mf Nguzo Mama (P. Muhando), Mashetani (E. Ilussein), Uwike Usiwikw Kutakucha (G. Ruhumbika) Gamba la Nyoka (E. Kezilahabi)
Mvutano (Conflict) Mgoro. Hali va kushindana ama kuvutana katika kazi ya sanaa baina ya wahusika. Pengine hutumika pia kueleza hali ya mvutano kati ya taswira mbalimbali.
Mwigo (Mime):
(i) Tendo la kufanya kufuatisha jambo lililofanywa na mtu mwingine kabla yake: Uigaji.
(ii) Aina ya njiwa mkubwa anayedhaniwa kuwa anao uwezo wa kuagua juu ya matokeo ya safari.
Nathari (Prose): Utungo katika maandishi ama katika matamshi ulio katika ujazo. Mf. Insha, hadithi, hotuba n.k.
Nadharia (Theory): Mawazo, mpango, mwongozo maelezo yaliyowekwa ili kusaidia kutatua au kutekeleza jambo fulani
Nguli (Protagonist): Mhusika mkuu katika kazi ya fasihi anayewakilisha kila mara mawazo yajamii. Mf. Kararna katika nwaya ya Kusadikika
Nidaa (Exclamation): Alama za kushangaa. Ni mbinu nyingine za kisanaa
Nahau (Idiom): Ni semi zenye kufumba na zmazonogesha na kuongeza habari uzuri wa kisanaa katika kazi ya sariaa itumiayo lugha.
Onomatopeia (Tanakali sauti): Tanakali sauti. Ni mwigo wa sauti katika kazi za sanaa. Matamshi yanayoiga sauti (pengme mwendo, wazo) n.k. ili kutoa dhana au picha fulani. Mf. Embe ilianguka pu! Mtoto alitumbukia majini chubwi! n.k.
Prosopeia (Personification): Tashihisi. Ni tamathali ya usemi ipayo kitu ama mnyama uwezo wa kutenda ama kuwaza kama binadamu Mf Kifo usinichokoze tafadhali Hapa kifo kinakemewa kuwa kiache uchokozi ambao labda umemwudhi msemaji wake Angalia tena Njiwa wangu, tafadhali vumilia, nitarudi nikimaliza masomo Njiwa hapa ina maana ya mpenzi wake anayetulizwa aache kulia amsubiri amalize masomo kwanza.
Picha (Imagery): Taswira. Tazama taswira. Ni kiwakilisho, maono ya kitu katika mawazo kwa kutumia lugha. Lugha mayotumika ni ya tamathali za usemi na ambayo imeambatana na ishara mbalimbali Mf Jicho lake lilikonyeza kama umeme umulikavyo na kuzima Neno kukonyeza hapa linaonyesha ishara fulani. Neno hilo linaleta dhana maalumu ya jambo linalotendwa. Kifungu cha maneno kama umeme ni cha kitamathali ya usemi. Kwa kuunganisha ishara na tamathali ya ya, picha inajitokeza akilini mwa msomaji
Ritifaa (Apostrophe): Namna ya usemi ambao mtu huongea mawazoni na kitu kisichokuwepo machoni bali mawazoni Tazama pia taabdili
Ridhmu (Rythm): Ni mapigo ya lugha ambayo ni ya asili. Kila lugha, ina mapigo yake ya asili. Katika lugha, ridhimu husaidia kujenga maana na mwendo wakati wa kusema. Ni mpangilio na urudiaji wa maneno, mapigo au mwendo katika tungo Mf. Siku tatu za mwanzo Chiku Ntale hakujua jiji la watu lilikuwa na tatizo gani . Alipewa vya kupewa... Alikula vilivyoliwa... Alitenda vinavyotendwa!
Riwaya (Novel): Ni kazi ya sanaa ya kubuni. Ni maandishi ya nathari (ujazo) yanayosimulia yanayosimulia hadithi ambayo kwa kawaida ina uzito, upana, urefu wa kutosha. kutosha. Ina wahusika mbalimbali wenye tabia za aina nyingi, ina migogoro mingi-mikubwa na midogo ndani yake. Kitu kingine cha muhimu kwa riwaya ni kuwa kina mawanda mapana ukilinganisha na hadithi fupi kwa mfano. Mf. Kuna riwaya mbalimbali za Kiswahili, kama vile Kichwamaji (E. Kezilahabi), Lwidiko (Martha Mlagala). Njozi Iliyopotea (C. Mung'ong'o), Shida (N. Balisidya).
Riwaya ya Kihistoria (Historical Novel): Riwaya iliyoandikwa kufuata matukio ya historia. Wahusika wengine huwa ni watu walioishi.
Riwaya Sahili (Novella): Ni riwaya fupi ambayo inachora kwa undani tukio na mtiririko mmoja, mhusika mmoja na uwanja wa kufanyia masimulizi ni mdogo kuliko ule wa riwaya kamili.
Riwaya Teti (Picaresque Novel): Ni riwaya ambayo inaathiriwa na kuchimbuka kutokana na jinsi mhusika mkuu anavyojengwa. Mhusika huyo kwa kawaida huonyesha hali ya kuukejeli mfumo wa kiutawala wajamii. Riwaya ya aina hii huonyesha vituko kadhaa vya kusisimua ambavyo ni vigumu kukubalika kama vinatokea katikajamii. Mhusika huyo kwa kawaida huonyesha hali ya kuukejeli mfumo wa kiutawala wajamii. Riwaya ya aina hii huonyesha vituko kadhaa vya kusisimua ambavyo ni vigumu kukubalika kama vinatokea katika jamii. Mhusika huyo hukutana na watu mbalimbali na kwa hiyo kuifanya hadithi kuwa ya dhihaka kwa jamii. Kwa kifupi, riwaya ya aina hiyo hufuata misingi ifuatayo: Kwanza inasimulia sehemu au maisha ya mhusika ambaye ni jambazi na kwa kawaida husimuliwa kwa kutumia nafsi ya kwanza, japokuwa hilo silo la msingi sana. Pili, mhusika mkuu kwa kawaida hutoka katika tabaka la chini na mara nyingi havumilii kazi za kuajiriwa. Tatu, hadithi ina mtiririko wa aina moja tu. Mhusika mkuu huanza na tabia ya ujambazi na hadithi humalizika mhusika huyo bado akiwa jambazi. Matendo yanayoonyesha na kuonyeshwa katika hadithi yanaonyesha uhalisi wa maisha ya jamii. Kuna dhihaka kubwa katika hadithi nzima.
Sanaa (Art): Kazi ya binadamu iliyojengwa kwa ufundi mkubwa. Kazi hiyo hujengwa kutokana na maumbile. Ni maumbile ambayo mtu hutumia kuelezea hisia zake. Kazi hiyo ya sanaa huelezea dhana mbalimbali. Sanaa hizo ni pamoja na uchoraji, uchongaji, ususi, hadithi, ushairi, tamthiliya, n.k.
Sanaa Tumizi (Applied Art): Sanaa ambazo huingizwa katika sura ya maumbo ya vifaa vya kutendea kazi. Mf. Fimbo ya kuchonga, mikeka" n.k.
Sanaa Ungamo (Confessional Art/Confessional Literature): Pia fasihi ungamo. Ni aina ya sanaa ambazo msanii hueleza madhambi yake ama makosa yake. Madhambi ama makosa hayo hatimaye huyajutia baada ya kuyakubali. Mf. Matambiko katika fasihi simulizi.
Sanaa la Utendaji (Performing Arts): Kazi zinazoambatana na nyimbo.
Shujaa (Hero):
(i) Mhusika mkuu mzuri
(ii) Mtujasiri... Amekuwa shujaa wa mashujaa!

Simulizi (Narrative): Maelezojuu ya tukio fulani. Mazungumzo
Fasihi Simulizi (Oral Literature): Fasihi inayotolewa kwa njia ya masimulizi ya mdomo na kupokezanwa kutoka kizazi hadi kizazi!
Sira (Sera): (Bildungsroman) Aina ya hadithi ambayo mtunzi husimulia maisha ya mhusika kutoka utoto hadi uzee/kifo. Mf. Rosa Mistika (E. Kezilahabi)
Sitiari (Metaphor): Tamathali ya usemi inayolinganisha kuhusisha vitu vilivyo tofauti kitabia na kimaumbile. Ni tamathali ambayo athari yake hutegemea kuhamishwa kwa maana na hisi kutoka katika kitu kimoja na kwenda katika kitu kingine. Kwa kawaida vitu ama viumbe viwili vilivyo tofauti kitabia ama kimaumbile vinahusishwa kwa msingi wa sifa fulani iliyopo katika vyote viwili ama zaidi bila ya kutaja dhahiri sifa yenyewe. Angalia kwa mfano semi zifuatazo: Juma ni kinyonga! Ujana ni moshi! Samwel ni mbogo.
Sitiarifiche (Conceit): Tamathali ya usemi inayolinganisha vitu viwili kwa uhusiano wa mbali, wazo linalojitokeza huwa mbali kwa kawaida.
Sitiarififi (Dead Metaphor): Sitiari iliyozoeleka sana katika matumizi ya kawaida kiasi kwamba mtu hatambui kuwa ni tamathali ya kisitiari. Ni sitiari kale, sitiari chakavu!
Sitiari Shehenezi (Functional Metaphor): Sitiari inayoongoza maana na sifa ya neno linalolinganishwa.
Taabili (Eulogy): Ni maandishi yanayokusudiwa kumsifu mtu aliyekufa. Angalia shairi la Shaaban Robert lifuatalo:
AMINA
Amina umejitenga kufa umetangulia
Kama ua umefunga baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga Peponi kukubalika
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua
Nilitaka unyanyuke kwa kukuombea dua
Sikupenda ushindike maradhi kukuchukua
Mauti siyasadiki kuwa mwisho wa dunia
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua
Katika shairi hili tunaona kuwa Shaaban Robert anazungumza kwa masikitiko makubwa sana na mke wake marehemu Amina. Amina aliyepaswa kusikiliza kilio cha Shaaban Robert sasa ni marehemu, hana uwezo wa kumsikiliza. Hii ndiyo Taabili. Tazama pia Ritifaa.
Tabaini (Litotes): Tamathali ya uaemi inayosisitiza jambo kwa kutumia ukinzani Mf. (i) Amekuwa mrefu si mrefu (ii) mzima si mzima
Taashira (Metonymy): Ishara. Alama maalumu zitumikazo katika jami kuwakilisha tendo fulani katika jamii hiyo. Taashira hnsaidia sana katika kujenga taswira ama picha katika kazi za sanaa.
Taharuki (Suspense): Hali kubwa ya kusisimua na ambayo humfanya mtu apemle kujua mambo yanavyojiri katika kazi ya sanaa itumiayo lugha - fasihi. Hali hii hujengwa na msanii kwa makusudi kabisa. Mifano ya kazi zenye taharuki ni mingi, lakini tunaweza kutaja vitabu kama vile Kiu (M.S. Mohamed), Simu ya Kifo (F.H.H. Katalambula) n.k.
Tanzia (Tragedy): Aina ya kazi ya sanaa itumiayo lugha, aghalabu tamthiliya ambazo mhusika mkuu hupatwa na anguko kubwa na mwisho hufikwa na kifo. Mf. Kinjeketile, Rosa Mistika.
Tarazi (Decorum): Ulinganifu wa kaida za kisanaa katika kazi za sanaa, kama vile ushairi unaopaswa kujali vina na mizani n.k.
Tamathali (ya Usemi): (Figure of Speech) Fungu la maneno hlilogeuzwa maana yake kamili ili kuwakilisha maana nyingine. Mifano ya tamathali ni kama: sitiari, tashihiha, tashititi, n.k.
Tamthiliya (Play): Mchezo wa kuigiza. Ni kazi ya sanaa itumiayo lugha na ambayo ujenzi na muundo wake hutilia mkazo wa vitendo. Katika tamthiliya, lazima kuwe na eatendaji, mahala pa kutendea, hadi hadhira Sifa hizi aghalabu huwa pia katika hadithi simulizi kama zinasimuliwa.
Tamthiliya Tatizo (Problem Play): Ni aina ya tamthiliya inayochukua tatizo moja la jamii na kulijadili kwa mapana na kulichambua kwa undani. Katika aina hii ya tamthiliya, mwandishi si lazima kutatua tatizo hilo, lakini analionyesha kwa mapana. Mf. Matatizo yanayojadiliwa kwa mapana katika tamthiliya ya Lina Ubani (P Muhando) ambayo yametokana na kuikumba Tanzania baada ya vita vya kumwangusha Nduli Iddi Amin Dada wa Uganda.
Tanakali Sauti (Ideophone): Tazama pia Onomatopeia. Matamshi yanayosisitiza au kuiga mwendo, wazo, sauti n.k.
Tanakuzi (Antithesis): Usemi/uneni unaoonyesha kupingana kwa mawazo. Casmir Kuhenga anatoa mfano huu: Ilikuwa ajabu siku za uiumwa kuona wapagazi wadogo na wanyonge kubebeshwa mizigo mikubwa na miziio, na wale wenye nguvu wakichukua mizigo myepesi.
Tanakala (Naturalism): Mtindo wa/na falsafa ya sanaa ambayo hueleza maisha kwa kuyanakili kama yalivyo. Husisitiza pia jinsi mwanadamu anavyotawaliwa na mazingira yake. Mf. Emile Zola ameandika kitabu cha Therese Raquin kwa kuzingatia falsafa hiyo (Naturalism).
Takriri (Recurrence) Urudiaji wa herufi, silabi, maneno au sauti zinazolingana katika kazi ya sanaa.
Tapo (Movement): Kikundi cha wanasanaa ambao hukubaliana juu ya falsafa na mitindo maalumu wa fasihi. Mara nyingi hawa kimsingi hukuza na kueneza falsafa na msimamo wao kwa maandishi mbalimbali na tahakiki. Mfano: Kwa sasa kuna kundi la watu katika Kiswahili wanaokuza mtindo wa uandishi wa mashairi yasiyozingatia mizani na vina kama vile mashairi ya kimapokeo. Hawa wako chini ya E Kezilahabi na M.M.Mulokozi ambao huandika mashairi yaitwayo Mashain ya Kisasa.
Taaluma ya Drama (Dramaturgy): Taaluma mayofanana na kueleza vipengele mbalimbali vya drama kwa kuzingatia dhana, nadharia, falsafa, mtindo, utendaji n.k Theatre Development in East Africa (DUP) (L Hussein).
Tashbiha (Simile): Hii ni tamathali ya usemi. Mshabaha. Ni usemi unaolinganisha mambo, vitu au hali mbili n.k. kwa kutumia viunganishi kama mithili ya, mfano wa, kama, n.k
Tashihisi (Prosopoeia) (Personification) Hii ni tamathali ya nsemi ambayo hupa kitu au mnyama sifa za binadamu Viumbe hivyo visivyo mtu liufauya na kutenda, huwaza na kujazubika kama kuwa ni binadamu Mf Huufurahisha moyo, kazi yake Chiriku wangu! Hapa Chiriku amepewa uwezo wa kimtu ambaye anamfurahisha huyu fulani Hapana shaka ni mpenzi wake wa moyoni.
Tashtiti (Rhetoric Question) ama ya semi ama fasihi inayomfanya mtu ama jambo, jamii, kitu n.k. k. kuwa kidogo kwa kutumia dhihaka au bezo. Mf. Tamthiliya ya Tendehogo (L Semzaha).
Tasifida (Euphemism). Tamathali ya usemi inayopunguza makali ya uneni. Ni tamathali iliyo katika kundi la "adabu" ama "ficho'' Mf Yako maneno fulani katika jamii hayapendezi kusikika yakitamkwa kuzingatia miiko ya utamaduni wa jamii. Kwa mfano rntu husema nakwenda haja, badala ya kusema nakwenda kunya. Ama husema fulani amejifungua badala ya kuserna amezaa. Ama fulani amesifiri njia ya wote badala ya amekufa. Kuna mifano mingi mingi ikiwa katika mfumo wa nahau.
Taswira (Imagery): Picha fulani inayojengwa akilini kutokana na matumizi ya tamathali za usemi pamoja na ishara mbalimbali katika kazi za sana zitumiazo lugha. Umbo ama maumbo ya vitu dhahiri yanayojitokeza kimawazoni baada ya kusoma au kusikia neno au maneno fulani.
Tata (Ambiguity): Neno linalotatanisha na lina maana isiyojitokeza waziwazi. Neno lenye maana zaidi ya moja ama mbili.
Tawasifu ((Autobiography): Ni maandishi ambayo mtu binafsi huandika kuhusu maisha yake mwenyewe. Mfano wa maandishi hayo ni kama kitabu cha Shaaban Robert kiitwacho Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini kilichochapishwa na Nelson & Sons, 1966.
Tauria (Word Play): Huu ni mchezo wa maneno yanayofanana. Mf. Papa alipapa kamba. Paka alipaka maji, Paa alipaa juu ya paa n.k.
Uadilifu wa Kifasihi (Poetic Justice): Ni hali ambayo hutokea katika kazi ya kifasihi ambapo mhusika wa) mwovu (wa) hupewa adhabu na wahusika wema hupata tuzo ama, zawadi ama tuzo la wema. Hii hutokea katika kazi zote za kisanaa zitumiazo lugha.
Uhakiki (Criticism): Ufafanuzi, uchambuzi ilioambatana na hukumu fulani wakati wa kuthaminisha kazi ya sanaa. Mifano ni vitabu viwili vya uchambuzi wa Ushairi wa Shaaban Robert uliofanywa na T.S.Y. Sengo na E. Kezilahabi.
Ufungamano (Allegiance): Ni dhana ya mwandishi au mwanasanaa yeyote katika kipindi fulani cha mfumo wa maisha na usanii wake kufungamana na matakwa ya umma. Msanii anaichambua kazi yake kwa makini na wakati huo huo kuipa welekeo ambao umma unauhitaji.
Umbuji (Aesthetics): Maarifa ya kupambanua yaliyo mazuri kwa kanuni za usanifu wa maandishi. Ni hali ya kupambanua uzuri na ubaya wa maandishi.
Ushairi (Poetry): Utanzu wa kifasihi unaozingatia misingi na kanuni zake katika usanii. Kuna ama nyingi za ushairi. (i) Ushairi wa Abjadi: Huu ni ushairi wa msanii ambao kila herufi ya kwanza ya ubeti hufuata mpango wa alfabeti hadi mwisho. (ii) Ushairi wa Sifa: Wawe Sifa: Ushairi unaosifia hali ya shambani. Mashairi mengi katika Gazeti la Uhuru ni ya namna hiyo. (iii) Ushairi Urari: (Nudhumu) Ni ushairi wa ushujaa: (Heroic poeirg). Ni utanzu wa ushairi ambao wakati mwingine unasimulia hadithi ndefu sana yenye maudhui mazito, mtindo na lugha ya hali yajuu, na ambao mhusika mkuu ni shujaa ambaye matendo na majaliwa yake huathiri jamii nzima ama taifa zima. Wakati mwingine unaweza kutaja tukio au kusifia shujaa fulani - kama vile sifo, majigambo, pembejezi (panegyrics) n.k. Ushairi wa ushujaa una matawi makuu matatu; kama hivi:
· utendi (epic)
· sifo (praise poem)
· nyimbo za vita (war poetry)
(v) Ushairi wa Msemele: Ni aina ya ushairi unaotumia misemo ya hekima kama vile methali, vitendawili, mafumbo n.k. ambayo wakati mwingine hayajulikani sana katika jamii. (vi) Ushairi wa Siasa: Huu ni ushairi ambao dhamira yake kuu ni ya kisiasa (vii) Ushairi wa Makiwa: Ni ushairi unaoonyesha huzuni na maombolezo mengi. (viii) Ushairi wa Mapenzi: Ni ushairi unaohusu mapenzi ama mahaba (ix) Ushairi wa Barua: Ni aina ya ushairi unaotungwa kibarua, lakini unazingatia kanuni zote za kishairi. (x) Ushairi kiambo pamoja na aina nyingine za ushairi.
Wahusika (Watendaji): (Characters) Hawani vitu, wanyama au watu katika kazi ya sanaa. Mf. Katika hadithi kuna wahusika wanyama, watu, mimea n.k. Kadhalika katika ushairi kuna wahusika kama hao, na hata katika tamthiliya. Kuna aina mbalimbali za wahusika. Kwa maelezo zaidi soma humu kitabuni.
Wasifu (Biography): Maandishi juu ya maisha ya mtu yanayoandikwa na mtu mwingine. Maisha ya Salum Abdala, Mwanamuziki wa Tanzania, kilichoandikwa na Jumaa R. Mkabarah na kuchapishwa Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, au Mohamed Ali Chuma, Mwanasoka wa Tanzania, kilichoandikwa na A.P.W. Mmallavi na kuchapishwa na East African Publishing House. Kingine ni Wasifu wa Siti Binti Saad kilichotungwa na Shaaban Robert na kuchapishwa na Nelson & Sons (1966).
Wigo (Imitation): Hali ya msanii na sanaa yake kuiga maisha.
Wigo-bezi (Travesty): Kazi ya sanaa ya kifasihi ambayo huiga kazi nyingine kwa kuibeza sana na kuidunisha nyingine. Mf. Washairi wanajadi hupendelea kudondoa mashairi ya mtiririko wakati wakiyaplnga kwa kuyabeza. Mf. Mazungumzo katika RTD kwenye kipindi cha Malenga Wetu, yaliyofanywa tarehe 8 Aprili, 1985, kati ya David Wakati (Mkurugenzi wa RTD) na John Joseph Komba (Mshairi) kuhusu masuala mbalimbali ya ushairi wa Kiswahili.
Wizani (Rythm): Tazama Ridhimu. Mapigo maalumu ambayo husaidia kujenga uzuri wa kisanaa katika kazi ya sanaa hususan ushairi.
to previous section
Powered by Blogger.