Mtalaa wa Isimu kinachambua kwa undani mada muhimu
katika nyanja za isimu kwa jumla, fonetiki, fonelojia, na mofolojia ya
Kiswahili. Dhana muhimu ambazo zimefafanuliwa ni pamoja na isimu, lugha,
umilisi,foni,fonimu, alofoni, alomofu, mofimu, miongoni mwa nyingine.
Dhana hizi zimefafanuliwa kwa kuzingatia kunga mahususi zilizopo katika
nadharia ya Sarufi Zalishi.Bila shaka kitabu hiki kitawaf aa sana walimu
na wanaf unzi wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari, vyuo vya
walimu na vyuo vikuu, ambao wamekuwa wakipata taabu sana kuyasoma masomo
haya katika vitabu ambavyo havikuandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Aidha
kitabu hiki kitawanufaisha pia wapenzi wengine wa lugha ya Kiswahili
ambao wanapenda kujifunza na kuielewa vizuri zaidi lugha ya
Kiswahili.Kwa mantiki hii, kitabu hiki kinashiriki kutoa mchango mkubwa
katika harakati za kuikuza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili hadi ipate
uwezo kamili wa kuweza kutumika si kama lugha ya mawasiliano tu bali pia
kama lugha ya kufundishia katika viwango mbalimbali hadi vyuo vikuu.