1. USIKU UTAKAPOKWISHA Na Mbunda Msokile M. Shekinyashi
2. Riwaya hii inahusu nini? •
Kwa ujumla riwaya hii inahusu hali ngumu ya maisha inayowakabili
watanzania wenye kipato kidogo. • Ujenzi wa wahusika, mandhari na
matukio kwa ujumla vinafafanua umasikini uliokithiri. • Motifu kuu ya
hadithi hii ni mahangaiko kila siku ya kutafuta kipato cha kujikimu,
kupitia motifu hiyo masuala mengi yanajadiliwa; masuala ya kisiasa,
kijamii, kiuchumi na hata ubinadamu.
3. Falsafa ya Mwandishi •
Mwandishi wa riwaya hii anaamini kuwa hali ngumu inayowakuta wengi
kwenye jamii ni zao la unyonyaji unaofanywa na wachache. Hili
linajidhihirisha kupitia mhusika Goza katika fikra na mawazo yake. • Pia
kwa upande mwingine mwandishi anaamini kuwa chanzo cha maovu katika
jamii na mfumo mbaya wa kiuchumi unaotengeneza matabaka. Maovu kama
wizi, rushwa, umalaya, utoaji wa mimba na ulevi uliokithiri. • Mwandishi
pia anatumaini la maisha mazuri kwa wengi. Katika ukurasa wa 89
anamtumia mhusika Chioko na kusema: “Ulitakiwa uwe na subira na utulivu
hadi pambazuko la umma ambalo lilikuwa likiingia kwa kasi kutokana na
kwisha kwa usiku”
4. Msimamo wa Mwandishi •
Msimamo wa mwandishi ni kwamba kuisha kwa matabaka kutajenga jamii
isiyo na maovu yaliyokithiri. • Anamsimamo kwamba umma pekee ndio
utakaoleta tumaini kwa watu wa kipato cha chini. • Hivyo msimamo wa
mwandishi ni wa kimapinduzi.
5. Migogoro iliyojitokeza •
Mgogoro wa kitabaka. Walionacho na wasionacho wameonekana kuwa katika
mgogoro wa kimaslahi. • Mgogoro kati ya mgambo na walalahoi. Mgambo
wametumika kama kiwakilishi cha tabaka tawala. Wamekuwa wakiwakandamiza
wanyonge na kuwanyima haki ya msingi ya kujitafutia. • Mgogoro kati ya
Chioko na mama yake alipokataa shule na kujichanganya katika jiji la Dar
es Salaam.
6. •
Mgogoro kati kondakta na abiria na miongoni mwa abilia pia: hii
inadhihirisha ni kwa namna gani huduma duni za kijamii zinaweza zikawa
chachu ya kukosekana kwa amani kwa watu wa tabaka la chini. • Mgogoro wa
kimawzo baina ya Goza na Chioko: wawili hawa walikuwa wanapishana
kimawazo juu ya namna ya kupambana na umasikini wao. Goza aliamini
katika njia ya mkato lakini Chioko aliamini katika subira na nguvu ya
umma. • Mgogoro wa kifikra: Chioko alikuwa na mgogoro wa kifikra. Alikwa
ameshindwa kuamua juu ya ushauri wa kukimbilia Zambia alipowa na rafiki
yake Goza. Alikuwa anawaza je, aende Zambia amuache Nelli au abaki na
Nelli na umasikini wao?
7. Ujumbe, Nimejifunza kwamba… •
Kujikwamua kiuchumi si lazima kupitia ajira. • Penzi ni kitovu cha
uvivu na uzembe; Chioko ni mvivu kuingia mitaani kutafuta pesa na mzito
kufanya maamuzi magumu kwa sababu ya mapenzi. • Kukosekana kwa mipango
binafsi ya kimaendeleo hupelekea watu kukata tamaa. • Ujira wa dhambi ni
mauti • Makundi ya marafiki wakati mwingine ni chachu ya uovu. • Kama
jamii haiwezi kutambua kiini cha matatizo yetu si rahisi kuweza kutatua
shida zetu. • Dhiki ikizidi sana mioyo ya binadamu huota kutu na huruma
hupotea. Wewe umejifunza nini?
9. Umasikini •
Ni hali ya kushindwa kujikimu katika mahitaji muhimu ya maisha ya kila
siku. • Mwandishi anatumia wahusika, mandhari, matukio na matumizi ya
lugha kali sana ya picha na kejeli kufafanua umasikini walionao wengi
kwenye jamii yetu. • Wahusika wakuu; Goza na Chioko wanaishi kwenye
mazingira magumu sana. Kupitia mahangaiko yao tunaona watu wengine wengi
wanaoishi kwenye maisha magumu kadharika. • Katika ukurasa wa 29
mwandishi anapendekeza njia za kuondoa umasikini. Ni kwa njia gani
unadhani umasikini unaweza ukapungua miongoni mwa watanzania wengi?
10. Kukosekana kwa makazi bora •
Mandhari iliyotumiwa na mwandishi inadhihirisha kukosekana kwa makazi
bora kwa wananchi. • Manzese kwa mujibu wa kitabu ni sehemu yenye makazi
ya watu wa hali ya chini. Mwandishi ameyatumia maeneo hayo huku
akifafanua kwa kina namna nyumba za maeneo hayo zilivyo duni. • Mhusika
Chioko na Goza wanaishi katika kibanda kibovu kinachofananishwa na mbavu
za mbwa. • Mhusika Nyundo naye kadhalika.
11. Tatizo la Ajira kwa Vijana •
Vijana wengi hawana ajira. Mwandishi anawaangazia vijana wa kitanzania
wenye nia ya kujikwamua kiuchumi lakini mfumo unawabana hata kushindwa
kupata ajira ndogondogo. • Mhusika Goza na Chioko ni mfano wa vijana
wengi wanaozurura mitaani kwa kukosa ajira. • Goza anazurura mitaani
akipita ofisi hadi ofisi kuomba ajira lakini anaishia kukutana na vibao
mlangoni vilivyoandikwa ‘HAKUNA KAZI’ • Mwandishi analijadili zaidi
suala hili na kuonesha linavyopelekea ukandamizwaji wa kijinsia.
Wasichana walihitajika kutoa rushwa ya ngono ili wapate ajira. Je,
katika jamii yetu kuna tatizo la ajira? Wewe Umejiandaa vipi kupambana
na tatizo la ajira?
12. Rushwa •
Rushwa ni kitendo cha kuuza au kununua stahiki isiyo yako kwa wakati
husika au isiyo yako kabisa. • Mwandishi anaijadili rushwa kupitia
wahusika Goza na Chioko. Vijana hawa wanaamini kuwa ukiwa na pesa ya
kuhonga hakuna kitu kitakachoshindika kwako. (uk 24) • Wanapokutana na
Mgambo mitaani rushwa huwaokoa na hata wamekosa kazi kwa sababu hawana
rushwa ya kuonga waajiri. Je, jamii yetu inaweza kupambana na rushwa?
13. Ukosefu wa huduma za Jamii •
Huduma za jamii ni pamoja na hospitali, shule, usafiri, na nyinginezo. •
Baada ya azimio la Arusha huduma za kijamii zilikuwa zikitolewa na
serikali pekee. • Kwa sasa huduma hizo hutolewa na serikali kwa
kusaidiana na watu au mashirika binafsi. • Katika riwaya hii mwandishi
anaonesha uduni wa huduma za usafiri akiangazia zaidi baada ya azimio la
Arusha. • Abiria wa UDA kutoka manzese wanakanyagana na kuumizaa kwa
kugombea daladala. • Kwa upande mwingine mwandishi anaikumbusha serikali
kuimarisha huduma za kijamii kwa walipakodi wao bila kubagua matabaka
yao.
14. Uongozi Mbaya •
Kiongozi katika jamii, taasisi, mashirika na serikali anapaswa kuwa
kioo cha matendo mema kwa wale anaowaongoza na jamii kwa ujumla. •
Tofauti na matarajio, viongozi wengi katika nchi yetu ni wabadhirifu,
waonevu, madikteta na wafujaji wa mali za umma. • Dhana hii inasadifiwa
na katibu mkuu wa kampuni ya mabomba. Kauli zake zinaashiria kiburi cha
ulevi wa madaraka. • Alimwamuru dereva wake aendeshe gari kwa kasi huku
akitumia mafuta ya umma.
15. Matabaka •
Ni mgawanyiko wa wanajamii katika makundi kwa misingi ya kielimu,
kipato na kiungozi. • Jamii yetu imegawanyika katika matabaka kadhaa. •
Mwandishi amelijadili suala hili kwa kina. Anaonesha nchi moja yenye
azimio moja lakini watu wake wanaishi katika dunia mbili tofauti. •
Wachache wanaishi katika dunia ya raha na wengi wakiishi katika dimbwi
la umasikini ,dhiki na karaha. • Katika ukurasa wa 43 mwandishi anaigawa
mitaa kwa majina yanayoashiria utabaka: kuna mtaa wa SALAMA, WENYEWE,
TUMAINI, MASHAKA na WASIWASI. Kwenu kuna matabaka?
16. Ulevi • Matumizi ya kileo huathiri vijana wengi. •
Pombe inapendwa lakini inaathari nyingi kwa mtumiaji. Athali zinaweza
kuwa za kijamii au kiafya. • Mwandishi analijadili swala hili kwa kina
huku akigusa vijana kwa ukaribu. • Anamtumia Goza na Chioko kuonesha
kuwa malengo mengi ya vijana hayafikiki kwa sababu ya ulevi uliokithiri.
• Pombe mara nyingine hupelekea kifo. Mhusika Liteketa anakufa baada ya
kunywa pombe ya Gongo. Nini athari za ulevi katika jamii yako?
17. Uhalifu • Uhalifu ni kitendo cha kuvunja sheria za nchi. •
Mwandishi anaonesha uhalifu katika matukio mbalimbali. • Tukio la mwizi
wa mifukoni aliyemchomolea abiria pesa yake katika UDA. • Pia tukio la
Goza kuwapora watu pesa zao. • Tukio la Goza na Nyundo kuvamia nyumba ya
meneja wa kampuni ya mabomba na kumuibia elfu sitini. Nafasi yako ni
ipi katika kuzuia vitendo vya uharifu katika jamii yako?
18. Nafasi ya mwanamke katika jamii •
Mtu anayedharaulika katika jamii. Mfano baada ya kifo cha baba yake
Chioko hakumsikiliza mama yake tena. • Chombo cha starehe: uwepo wa
wanawake wanaojiuza na pia vitendo vya rushwa za ngono. • Kama kitega
uchumi: Goza anapomshauri Chioko kumuuza Nelle ili wapate ajira au
wapate pesa za kujikimu. • kiumbe duni sana kwenye jamii; mama mwenye
watoto watatu alipokuwa akinyanyasika na kondakta wa UDA. • Mshauri
mzuri; alipowashauri Goza na Chioko kwenda kuanzisha miradi ya shamba.
Mwanamke ananafasi gani katika jamii yako?