Nadharia ya Kiswahili

Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayotumiwa na watu katika mawasiliano hasa Afrika Mashariki na ya Kati.
Lugha ni sauti za nasibu zenye mpangilio maalumu zilizokubaliwa na watu ili zitumike kwa mawasiliano

Asili ya Kiswahili

Kuna nadharia mbalimbali zinazohusu asili ya lugha ya Kiswahili. Nadharia hizo ni kama vile:

Kiswahili ni Kikongo

Nadharia hii inaeleza kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni huko nchini Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Inasemekana kwamba pwani ya Afrika ya Mashariki hapo mwanzo ilikuwa haikaliwi na watu, lakini kutokana na ugumu wa maisha hapo baadae watu kutoka maeneo ya Kongo walihamia pwani ya Afrika ya Mashariki. Watu hao bila shaka walihama na lugha zao ikiwemo Kiswahili.
Sababu hizo hazina mashiko kutokana na kuwa wanahistoria hawajaeleza ni lini hasa watu hao walihamia maeneo ya pwani ya Afrika ya Mashariki.

Kiswahili ni Pijini au Krioli

Nadharia hii inasema kwamba wakati Waarabu walipokuja pwani ya Afrika ya Mashariki walioa wanawake wa Afrika na hivyo kutokana na mwingiliano wa lugha zao tofauti ilizaliwa lugha mpya ambayo ni aina ya Pijini.
Baadae watoto walipozaliwa walikuta lugha hiyo mpya ambayo ni Pijini. Watoto hao waliiendeleza lugha waliyoikuta na baadae ikazaliwa Krioli. Krioli ni Pijini iliyokomaa.

Kiswahili ni Kibantu

Wanahistoria wanaeleza kuwa Kiswahili kimetokana na Kibantu kwa kutoa sababu mbalimbali. Miongoni mwa sababu hizo ni:
Powered by Blogger.