“EPUKA KUFA KABLA YA WAKATI”




Je wataka kuishi miaka mingi?
Kifo
Kifo ni nini?
Ni kuharibu au mwisho wa kitu, Maisha ya mwanadamu au uhai wa mwanadamu hatima yake ni kifo au mauti. Hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuepuka au kukimbia kifo.
                   “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kusishi si nyingi, naye hujaa taabu (Ayubu 14:1-2)
       Kifo hakichagui wazuri, wabaya, warefu, wafupi n.k. Bali kila mmoja anakabiliwa na kifo na kila moja anasiku yake ya kufa.Katika maisha ya mwanadamu kuna aina mbili za vifo,ambazo ni;
i. Kifo cha kiroho
Ni hali ya mtu kuwa hai kimwili lakini kiroho ni mfu au amekufa. Mtu aliyekufa kiroho maisha yake huwa yamepungukiwa na nguvu ya kimungu na mtu huyu   hubakia  na imani isiyo na matendo yaani mtu anakuwa ni wa kumtaja Mungu kwa mdomo tu lakini matendo yake yanakuwa mabaya, ”Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo?........vivyo hivyo na imani isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake” (Yakobo 2:14-17)
Unaweza kujiuliza, ni kwa namna gani mtu anaweza kuwa hai kimwili na wakati huo huo asiwe hai kiroho?.
Kufa kiroho au kuto kufa kiroho hutegemea namna mtu binafsi anavyo ishi na Mungu wake kwani tukio hili la kufa kiroho huwa kwa katika nafsi au roho ya mtu binafsi anavyoishi kwani tukio hili la kufa kiroho huwa katika roho au natsi ya mtu mwenyewe “nayajua matendo yako yakuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa (ufunuo 3:1).
Ni dhahiri mtu anakuwa hai kimwili, anaweza kuwa mhudhuliaji wa Ibada na akafanya huduma zote kama kuimba, kusifu, kuhubiri, kuomba nk. Kakini yeye akawa mfu kiroho.
Hii ni kwasababu huanzia moyoni kabla ya kutokeza nje ya mtu mwenyewe.kila uharibifu wa kiroho wa mtu huanzia katika ulimwengu wa roho, huiondoa na kuiharibu ile nguvu ya kimungu au Roho mtakatifu hofu ya mungu iliyomo ndani ya mtu ili kumfanya mwanadamu afanye matendo au mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa kimungu bila kuhudumiwa na chochote moyoni yaani bila hata kufikiri, je ni dhambi au si dhambi?

i.                   Kifo cha kimwili
Ni hali ya uhai au pumzi kutoweka kabisa. Aina hii ya kifo mtu hawezi kuwa na uwezo wa kuongea chochote tena bali mwili huanza kuoza na mwili huu mfu huzikwa ardhini. Mwanzo wa kifo ya kimwili
Ni pale Adam na Eva walipokengeuka (walipotenda dhambi) Mungu alitoa adhabu ya kifo kwa wanadamu “………..kwa jasho la uso wako utakula, hata utakapo irudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” (mwanzo 3:19)
Mungu alitoa adhabu hii ya kifo baada ya wanadamu kutenda dhambi, tangu wakati huo hadi sasa kifo humkabili kila mwanadamu.
Je mtu akifa anaenda wapi?
Mtu akifa huingia peponi (kuzimu) Yesu alipokuwa msalabani alimwambia Yule mwizi aliyekuwa ametundikwa pamoja nae kuwa “amini nakwambia leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (luka 23:43). Peponi kuna sehemu mbili ambazo ni;
Ø Mahali pa mateso kwa watu wanaotenda mabaya.
Ø Mahali pa faraja kwa waliokuwa wanatenda mema.

“…… Basi kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso Akamwona Ibrahimu kwa mbali, na lazalo kifuani mwake, akalia akasema, Ee baba Ibrahimu niurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu…..”(luka 16:23-24)

Hivyo  ukifa kama ulikuwa unatenda dhambi hivyo utaelekea peponi kwenye mateso makali na kama ulikuwa unatenda mema utaelekea peponi yaani  mahali pa faraja.
Katika habari za tajiri na maskini Lazaro (luka 16:18-25) Biblia inaelezea kuwa Tajiri alikuwa peponi yaani ile sehemu ya mateso na Lazaro alikuwa peponi yaani mahali pa faraja.
Wanadamu wengi hujiuliza maswali mengi juu ya kifo cha kimwili, wapo wanaoamini kuwa mwili huu utaurithi uzima wa milele. Baadhi ya watu huosha mwili (maiti) kwa kuubinya ili kuondoa kila kilichopo tumboni kwani wanaamini mwili unaenda peponi (mbinguni) lakini si kweli, kwani mtu anapokata roho (mwili kutengana na roho) roho huondoka kwenda peponi na mwili hubaki ardhini, huzikwa kwani huoza na kunuka,“……Damu na nyama haviwezi kuurithi ufalme wa mungu; wala uhalibifu kurithi kuto kuharibika” (1Wakorintho 15:50) Hivyo mbinguni hatutakuwa na miili ya kibinadamu kwani mili hii tuliyonayo sasa ni miili ya kuharibika, Miili ya mbinguni ni ile isiyoharibika.
          
Hata siku ya ufufuo watakao fufuliwa watakuwa na miili mingine na sio hii tuliyonayo sasa. “…….Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?  36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa; 37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo; 38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.  40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. 41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. 42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika. (1wakorintho 15:36-50)
Je wafu wanaweza kutudhuru?
Baadhi ya watu baada ya kufiwa na baba, mama,bibi,babu nk. Hujisumbua sana wakiogopa kuwa wasipotambika au kujengea makaburi marehemu atawaletea madhara .
Kutambika, kuwajengea makaburi marehemu ni kazi bure kwani biblia inasema;
    kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
 6 Mapenzi yao na machuksio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.

Je wafu wanaweza kutusaidia?

Baadhi ya watu huomba kwa wafu pale wanapokuwa na hitaji wanadhani wafu wanaweza kuwasaidia jambo lolote. “Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua. Kupmba kwa wafu au kuhitaji msaada mbele za watu ni chukizo mbele za mungu wetu hivyo tunapaswa kumwomba mungu wetu na si wafu.
Pia nikaona waovu wamezikwa, nao wamefika kaburini; tena waliofanya mema wameondoka katika patakatifu, nao wamesahauliwa mjini. Hayo nayo ni ubatili. (mhubiri 8:10)

Pia (luka 16:19-30) Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.  22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.  23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.  25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.  27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,  28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.  29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

Biblia inawaeleza juu ya habari ya tajiri na maskini lazaro. Tajiri alitaka lazaro arudi duniani kuwasaidia ndugu zake tajiri, lakini ombi lake halikukubaliwa, hivyo weafu hawawezi kuwasaidia walio hai na kuwaomba wafu ni chukizo kwa Bwana Mungu wetu.
Pia baadhi ya watu huwatumia watakatifu wa kule kama Mariamu (mama yake Yesu) kama wapatanishi na Mungu wetu na Mungu.

Mfano
        Maria mtakatifu mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu ……………………
Mariamu alikuwa sawa na wanadamu wengine isipokuwa alibeba mimba kwa uwezo wa  Roho mtakatifu,Bado haijulikani kama mbinguni kuna watu wanaokesha na kuomba hivyo hatupaswi kumuomba Mariamu bali tumuombe Yesu Kristo kwani aliyempatanishi wetu na Mungu ni Yesu kristo peke yake.
 “Kwasababu Mungu ni mmoja na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja ambaye ni Yesu kristo” (1Timotheo 2:5)

Je tuwaombee Wafu?
   Tukumbuke  kuwa mtu akifa katika dhambi kinachobakia ni hukumu.
“Na  kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja  na baada ya kufa  hukumu”
(waebrania 9:27)

Hivyo hata ukiomba au kufanya ibada juu yao hawawezi kupata msamaha kabisa kwani Yesu alisema kuwa , tajiri mwovu alipokufa, aliingia mahara pa mteso wala hakupata msamaha au huruma hata ya kupewa tone la maji.
 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
 (Luka 16:23-25)

Pia katika “ matendo 5:1-11” Anania na Safira walipomkosea Mungu na kufa kwasababu ya uongo wao hawakuzikwa kisha wakaendelea kufanyiwa sala au ibada au Misa kwani ibada,misa au sala haviwezi  kumsaidia kitu chochote mtu aliyekufa.

Je Mungu anaweza kumtaarifu mtu kuhusu kifo chake au siku ya kufa?
Ndiyo Mungu anaweza kumtaarifu mtu juu ya kifo chake au juu ya kifo cha mtu mwingine.Tuangalie ushuhuda wa Mwl Christopher Mwakasege juu ya kifo cha Mwimbaji sedekia wa Arusha Tanzania;
   Mwalimu Christopher mwakasege alitoa ushuhuda katika semina iliyofanyika katika viwanja vya Furahisha vya jijini mwanza semina hiyo yenye somo iliyoitwa “namna ambayo Roho mtakatifu awezavyo kukusaidia ili upokee kile unachokiomba ilianza tar 19-7-2011 na iliisha tar 23-7-2011.
Alisema “Roho mtakatifu akuambiayo omba hiyo haina MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate unachokiomba kwa kuwa gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa kukipata ni ndogo kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi hayo.
Roho matakatifu atakapokupa mzigo wa kuombea  jambo anakupa na muda ukizembea muda huo ukipita kinakuwa ni kipolo, na kipolo kinaweza kikalika na kipo ambacho hakiliki.
Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia kasha akaanza kuumwa, madaktari waliniambia ubongo wake kwa asilimia tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara nipo pale Hospitalini wakasema kwa nini usikae Hotelini kasha ukawa unapiga simu kuuliza hali ya mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa suala la kupiga simu tu sio tatizo ningeweza kurudi arusha nikawa napiga simu.
Suala hapa ni kuw nilikuwa naenda kila mara kwa ajili ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa kando kando ya Bahari ya Galilaya nafanya maombi juu ya Sedekia kwa masaa sita nikitoka hapo nasikia upako wa ajabu sana kasha napanda Taxi kuelekea Hospitali. Nikifika hospitali madaktari na watu wa ICU walikuwa washanifahamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye chumba cha nguo nabadili nguo kissha naingia ICU alikolazwa. Nikifika nambana Mungu kwa maswali mengi namuuliza Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu Muda wote huo si urudi? Na kisha namuuliza Yesu, hivi Yesu unafahamu kuwa Sedekia ana mke ukimchukua mkewe utamwachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mikono juu yake. Nilipokuwa naweka mikono juu yake ghafla upako wote unakuwa kama umenyonywa.
Baada ya hapo narudi hotelini naanza tena kumuuliza Mungu hivi Mungu kama husikii maombi yangu, sikia maombi ya watanzania kwa kuwa najua watanzania wengi walikuwa wanamuombea sedekia.
Inafika wakati nakata tamaa lakini ndani yangu najisemea Mwakasege haiwezekani jitie moyo kasha nabadili maombi aina ya maombi kwa kuwa nilikuwa nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake nikawa naiweka kati kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini usiku nazunguka nguo zake na passport yake huku nikifanya maombi.
Taraatibu Mungu akaanza kuniambia Sedekia harudi, Kipindi hicho mimi na familia yangu tulikuwa tumepanga kwenda kupumzika nchini uingereza wakati wa sikukuu ya krismass, na booking ya hotel tulikuwa tumeshafanya, na watoto wote wako nyumbani wakijiuliza tunaendaje kupunzika wakati Sedekia anaumwa? Chrismass ilipita na mwaka mpya pia kisha Sedekia akafariki.
Baada ya kifo chake sikuchoka nikarudi tena kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua Sedekia mikononi mwangu? Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi nikasema hapa.
Kila siku mimi nikiwa katika  maombi nahitaji ya ROHO anifundishe kwa upya kwa kuwa sijui vita gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu atabaki kuwa Mungu kwa kuwa hufanya atakavyo”.      
           
CHANZO CHA KIFO
Dhambi
Ni hali ya kufanya kinyume na maagizo ya mungu ambayo aliyaweka ili sisi kama binadamu tuyafuate lakini si kila dhambi mwanadamu akitenda anakufa kimwili.
“mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo na mauti, ataomba na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo na mauti (1 yohana 5:16).
Si kila dhambi ukiitenda unakufa kimwili bali dhambi nyingine mtu anakufa kiroho.Waumini wengi siku ya leo tunaabudu kama desturi, yaani tunaenda ibadani ili watuone na si kufikiri nafsi zetu kama tunapenda mapenzi ya baba au la! Wengine wanaenda kanisani ili kuwaheshimu viongozi  wa dini na kulinda hadhi zao walizonazo, serikalini, maofisini na makanisani.
Mungu alituumba kwa makusudi maalum, na hakutuumba kwa kubahatisha au kwa bahati nasibu. Kama yeye ndiye aliyeumba kuku, nyoka ng`ombe, mimi na wewe tuwe wanyama lakini kwa makundi maalumu aliweka tuwe wanadamu wenye akili na utashi.
“Hata walipokaribia yerusalemu na kufika Bethfage, katika mlima wa mlima wa mizeituni ndipo yesu alipotuma wanafunzi wawili akawaambia, Enendeni mpaka kijiji kile kinachawakabili na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; mfungueni na watu wakiwaambia neno semeni, Bwana anawahitaji, na mara huyo atawapeleka (mathayo 21:1-3)
Katika eneo hili la Beth fage ambalo Yesu alikaribia kilikuwa na punda wengi lakini punda huyu alifungiwa eneo hilo si kwa sababu mwenye punda bali kwa kusudi la Yesu, yamkini hata mwenye punda hakulitambua hili.
Hata kwangu mimi na wewe leo tuliumbwa kwa makusudi na tu wazima hadi leo si kwa maamuzi yetu kuwa wazima bali lipo kusudi maalumu la mungu ambalo amepanga juu yetu ndio maana wengi wamekufa kwa ajali na magonjwa lakini mimi na wewe tu wazima.
Mungu alituumba anategemea kupata matunda Fulani kwetu yaani tuzae matunda au matendo mema.
Mfano Ukipanda mche wa tunda lolote kama  Embe, Parachichi unategemea baada ya mti huo kuwa mkubwa utazaa matunda hivyo unapalilia na kuwekea samadi (mbolea). Ndivyo hivyo Mungu anategemea kupata matunda kutoka kwetu.
“hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia yasipatikane matunda kwako tangu leo na hata milele, mti ukanyauka mara. (mathayo 21:18) 
Hapa tunaona jinsi Yesu alipoamua kuulaani mti ambao Mungu aliuumba baada ya kuona hauzai matunda kabisa, tunaona mti huo ulinyauka na kukauka kabisa, hivyo hata kwetu tunaweza tusifanikiwe katika maisha yetu lakini pia kufa kabla ya wakati kwani hatuzai matunda.
Kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu.
Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano wake na kwa sura yake. Nia ya Mungu ni kwmba anataka tuwe na tabia kama yake. Tabia ya kuumba (creativity), kutawala, kuzalisha, kuponya na tabia nyingine zote nzuri. 
Wakati Mungu anapomwokoa mtu kutoka dhambini huwa ………. Kwa mtu maalumu alitemkusudia kwa wakati huo ili kutimiza mpango wake wa awali wa kuwafanya wanadamu wawe mfano wake.
Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu “(mwanzo 1:26)
Ili kulidhihirisha hili Mungu haoki watu wote kwa wakati mmoja, lakini anafanya kwa kila mtu na wakati wake yeye ndiye anayepanga majira na nyakati kwani ndiye anayejua mwanzo wa mwanadamu na maisha yake
Hivyo Yesu alivyokufa msalabani nia yake (Mungu) ni kuwarudisha wale walioondolewa kwenye mpango wa Mungu wa kuwa kama Mungu nakuwa kama mtumwa shetani.
“Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu vihalibikavyo, kwa fedha, dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mliopokea kwa baba zenu “(1petro 1:18).
Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vitu vyote kama vile milima, mito, mabonde, mbuzi, kuku nk. Angeweza kutuumba mimi na wewe tuwe wanyama lakini kwa kusudi lake akatuumba tuwe binadamu si kwa kubahatisha bali ni kwa makusudi maalumu.
SABABU ZA MUNGU KUTUUMBA WANADAMU:
Ø Alituumba tuwe wanadamu ili tumwabudu yeye katika ukamilifu.
ü Kuabudu ni kutoa heshima ya ya hali ya juu (ya mwisho) kwa kitu, mtu au kiumbe chochote.
ü Ni kuheshimu kwa nia yote kutoka ndani ya moyo bila kujali athali au hatari yoyote ambayo yaweza kujitokeza kama athari mbaya za kufanya hivyo.

Kuabudu haimaanishi tu kuimba nyimbo za taratibu bali ni maisha ya kumheshimu anayestairi kuheshimiwa kwa kila jambo.

Heshima hii anayestaili kupewa ni Mungu peke yake, na hii Mungu hajaruhu kuchangia (kushare) na yeyote au chochote.
“mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na miungu mingine ila mimi.

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilichopo juu ya mbingu wala kilichopo duniani, wala kilicho majini na nchi kavu (Kutoka 20:1)

 Maelezo hapo juu mungu alizuia kuchonga sanamu yeyote na kuiabudu. (Hesabu 19:4) “Msigeuke kuwandama sanamu wala msijifanyizie Miungu ya kusujudu. Mimi ndimi Bwana Mungu wako”
Sanamu inayozungumziwa hapa si dhambi anayotenda mtu peke yake bali hata kuchonga kinyago na kukisujudia pia kuabudu sanamu.
Heshima ya mungu tumpe mungu na si kupuga magoti mbele ya sanamu ya bikira maria au mbele ya sanamu ya msalaba wenye sura ya Mungu, hili ni kosa.
Wanadamu wa leo wapo wanaoabudu mali, magari, simu, nk. Yaani wanaviona ni vitu vya msingi sana kuliko mungu, utamwona mtu yupo tayari asifike ibadani ila aende akashughulikie mali yake.
Vitu vyote vilivyopo ni vya kitambo tu.
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Mungu aliwaagiza wana wa Israel kumwabudu na kumpenda yeye tu nasi kitu kingine. Mungu yupo peke yake katika utatu wake hana mbadala wake wa kufananishwa naye.
Si kila mtu anaweza kumwabudu Mungu kama tunavyofikiria, ni watu wenye sifa hizi zifuatazo:-

·        Aliyetubu dhambi
Kutubu ni hali ya kuomba msamaha kwa kosa ulilofanya.

Toba ni kugeuka kutoka dhambini na kumwelekea Mungu.
“Tubuni basi mrejee ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwa Bwana (matendo 3:19).

Hivyo ili uweze kumwabudu mungu ni lazima utubu kwanza ili dhambi zako zifutwe ndipo umwabudu Mungu katika roho na kweli vinginevyo utamwabudu Mungu katika mwili tu hii ndio ibada iliyotawala kipindi hiki.
Mtu anaabudu Mungu au anaabudisha (ni muhumini) ndio huyo huyo mzinzi, mwizi,mchawi nk.

Je swali langu mimi na wewe Mtu mwenye tabia hii anamwabudu mungu katika roho na kweli?
“Mungu ni Roho, na wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli (Yohana 4:24).

Ili uweze kumwabudu mungu katika roho na kweli ni lazima utubu dhambi zako zote kwanza kwani mungu hawezi kushuka na kukaa mahali pachafu, endapo hutatubu basi huwezi kumwabudu mungu katika roho na kweli, utakuwa unajidanganya mwenyewe.                   
Ø Aliyemsamehe aliye/waliomkosea
Kusamehe ni hali ya kumhurumia au kumfutia makosa mtu aliyokukosea bila kujali umri, kabila wala jinsia, bila kujali kosa alilokukosea kwani bila kusamehe na Mungu hawezi kukusamehe wewe pia.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi makosa yenu. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu (mathayo 6:14).
Kutosamehe ni kipingamizi kikubwa cha kumwabudu mungu hivyo tunapaswa kuwasamehe wengine ili kufanya moyo uwe safi kwa ajili ya kumwabudu mungu.
Mungu hushuka wakati wa sifa hivyo usipowasamehe waliokukosea hutaweza kusifu na hutakutana na Mungu katika maisha yako.
“Lakini panapo usiku wa manane Paul na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza ............. (matendo 16:25).
Kwa mujibu wa maelezo hayo ya mistari ya biblia hapo juu mtu anapoishi maisha matakatifu hukutana na Mungu wakati wowote.

B.  KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII
Kumtumikia mungu ni kukubali kuungana na Mungu katika mpango wake wa wokovu duniani.
Ni kukubali kutumika na Mungu katika kila jambo analolitenda, yaani kuona ulimwengu kama Mungu anavyouona kuwa umeharibika.
Usimtumikie mwingine yeyote au chochote au vyovyote kuliko mimi usimtumikie Mungu kwa sababu unahitaji kitu Fulani toka kwake.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana mungu wako (torati 5:9)
Kumtumikia Mungu ni kufanya kazi ya Mungu, kuna namna nyingi za kumtumikia Mungu kama ifuatavyo;

Ø   Kutenda mema
Mungu ametuumba ili tutende mema na si mabaya wakati Fulani unaweza kujiuliza mema ni yapi na mabaya ni yapi?
“Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi kwake hayo ni dhambi (yakobo 4:17).
Yapo mambo mangapi ambayo ni mema Na yapo mambo mangapi ambayo tu kutenda lakini hatuyatendi?
Ni vema kutafakari na kujithamini, je ni kweli tunatenda mema? Au hatutendi? Mema tunamfurahisha Mungu au hatumfurahishi?
Na nini matokeo ya kutenda mema? Haya yote yapo mikononi mwako.Wapo wanaojipotosha wenyewe na kufanya matendo maovu kuwa mema huku wakimsingizia Mungu kuwa alimruhusu.
Mfano: Wapo watu wanaoamini kuwa ukinywa, usipolewa si dhambi na wana kunywa kileo au vileo
.( 22 Ole “wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;”Isaya 5:22).
Kweli halisi kuwa si kweli mungu hakuruhusu ulevi wa aina yoyote bali alikemea ulevi tena alikemea kwa ukali. Pia si kweli kuwa mlevi anaweza kunywa lakini asilewe hizi ni ndoto,sni  vigumu mlevi kuacha kunywa kama hajalewaacheni kujidanganya ulevi ni dhambi sawa na dhambi nyingine.
              11 “Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!”(Isaya 5:11)
Kama unajidanganya kutumia vileo ukidhani ulevi sio dhambi ni vyema ukatubu leo na dhambi yeyote ile hawezi kutubu kwa kusali sara Fulani mara kadhaa,wala viongozi wa dini hawana mamlaka ya kusamehe dhambi bali wanapaswa kutuombea ili Mungu atusamehe na sio wao watusamehe kwani Mungu husamehe pale mtu anapotubu toba ya kweli.Wapo viongozi wa kiroho wanaowaonea aibu kuwakemea waumini wao wanapotenda dhambi kwa kuhofia kuwapoteza au kukosa waumini,viongozi wa namna hii wanatenda dhambi kwani wanawapotosha waumini hivyo wanapaswa kuwaelekeza njia inayostahili.

Ø Kujitoa na kumtolea Mungu
Mungu alimuumba mwanadamu akampa vitu vingi avitawale wanyama, ndege wa angani nk. Nasi tunapaswa kumtolea kwa kumshukuru kwa uhai (afya njema) yeye ndiye mpaji wa vyote. Wanadamu katika suala ya kutoa huwa tunaona kama ni suala la ziada na halitiliwi maanani.
Mfano
Mungu anampa pumzi na uhai na ikumbukwe wengine wamekufa lakini mwanadamu hatoi sadaka au akitoa anatoa vilivyo vinyonge kabisa, kama ni fedha basi anatoa chenji kama shilingi mia ua mia mbili.
Swali la kujiuliza, Je Mungu kamgusa atoe kiasi hicho au kwa uchoyo wake ameamua?
Inakuwaje kama anakuwa na motto, anampa fedha au kitu halafu akimwomba tena anakunyima?
Mungu hapendezwi na uchoyo wetu hivyo tunapaswa kumtolea sadaka iliyo safi.
Unaweza ukawa mtafutaji lakini usifanikiwe kwa sababu ya kutomtolea Mungu sadaka, je atakupatiaje riziki yako ikiwa wewe ni mchoyo
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. (warumi 8:28)

Kumpenda mungu si kusali au kuimba kwa juhudi bali ni pamoja na kumtolea sadaka.
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. (malaki 3:10)
Hivyo Mungu akubariki unapaswa kuonyesha moyo wa utoaji na si vinginevyo.

Ø Kumtukuza Mungu na kutumia vipaji au karama ambayo Mungu ametupatia.
Mungu si mchoyo alimpa kila mwanadanmu kipawa chake au karama yake kama uimbaji, uombaji nk. Fanya kila jambo jema ambalo moyo wako au Roho mtakatifu atakavyokutuma kufanya.

 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa. (mithali 17:8).
Ø Kumtafuta Mungu kila iitwapo leo
Wanadamu hujisahau na kuona uzima na afya ni halali yao kuwa katika hali nzuri kumbe la hasha, ni rehema za Mungu hivyo tu na huacha kuomba, kutubu na kumtafuta Mungu bali hujikita katika kufanya mambo yasiyopendeza mungu, kumbukumbu ya kumtafuta au kumrudia mungu huja pale mmoja anapokuwa amekufa au kufariki na mara baada ya msiba kumalizika husahau kabisa uweza wa Mungu na nafasi yake kwa wanadamu.

6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;  7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. (isaya 55:6-7).

Je kwanini mwanadamu anakufa?
Kifo kilitokea wapi?
Chanzo cha kifo ni dhambi baada ya Adamu na Eva kutenda dhambi pale bustanini ambapo
Mungu aliwaweka, Mungu alitoa adhabu ya mauti kwa mwanadamu .
  kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Ni dhairi kuwa kabla ya Adamu na Eva kutenda dhambi, Mungu hakuleta mauti kwa wanadamu hivyo kifo au mauti kinapoonekana pale wanapokengeuka na kutenda dhambi hapo ndipo wanadamu walipoanza kufa.

Lakini swali kubwa la kujiuliza ni hili kwa nini wanadamu wanatofautiana katika umri wa kufa?
Wengine wanakufa bado watoto wadogo wengine vijana na wazee.
Hata wakati wa agano la kale wanadamu walitofautiana katika kufa japo wao waliishi miaka mingi kama vile zaidi yetu.

Adamu (miaka 930 mwanzo 5:3-5)   
  Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
 4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
 5 Siku zote za Adamsu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
Sethi (miaka 912 mwanzo 5:6-8)
6 Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi. 7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake. 8 Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
Enoshi (miaka 905 mwanzo 5:9-11)
  9 Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10 Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. 11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
Kenani (miaka 910 mwanzo 5:12-14)
12 Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13 Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. 14 Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
Mahalaleli (miaka 895 mwanzo 5:15-17)
15 Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16 Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. 17 Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
Yaredi (miaka 962 miaka mwanzo 5:18-20)18 Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. 19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
Henoko (miaka 365 mwanzo 5:21-24)
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. 24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
Mathusela (miaka 960 mwanzo 5:25-27)
25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. 26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. 27 Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
Lameki (miaka 770 mwanzo 5:28-31)
28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. 29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana. 30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. 31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
Wanadamu hawa walioishi mwanzoni baada ya Mungu kuumba ulimwengu walitofautiana umri wao katika kufa japokuwa wao waliishi miaka mingi zaidi wingi wao waliishimiaka mia tatu (300) hadi miaka 960.

Swali kubwa ni kwanini hata wao walitofautiana hata kama waliishi miaka mingi?
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. 24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. (mwanzo 5:21-24).
Kwa mujibu wa maelezo haya Henoko hakufa bali Mungu alimtwaa hivyo ni dhahiri kamba dhambi ni kikwazo kikubwa cha kuishi maisha marefu.
Wakati wa Nuhu Mungu alileta adhabu ya kifo kutokana na ukengemfu uliokuwa unafanyika.
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. (mwanzo 6:1-3).
Kwa mujibu wa mistari hiyo hapa juu ya dhambi ilimfanya Mungu awape adhabu ya kifo kuuangamiza ulimwengu na vyote vilivyomo.
 
 1 Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. 2 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. 3 Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. 4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali. 5 Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. 6 Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi. 7 Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika.
 8 Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote vitambaavyo juu ya nchi,
 9 wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, mume na mke, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu. 10 Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. 11 Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka. 12 Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku. 13 Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye; 14 wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yo yote.
 15 Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. 16 Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; Bwana akamfungia. 17 Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi. 18 Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19 Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa. 20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. 21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;  22 kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. 23 Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina. 24 Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.  
Nuhu na watoto wake ndiyo watu pekee ambao hawakuathiriwa na gharika hiyo kwani Safina ilielea majini na kwenda kutua katika milima ya Ararah ipo katika bara la ulaya hata leo hivyo Dunia kuangamizaw kwa maji ni tukio halisi na la kweli.
Unapojiona wewe binafsi Mungu amekuumba, mahali na sehemu yoyote ile ulipotambua wewe si wa kwanza, kuishi hapa ulimwenguni, wapo walioishi hapa Duniani, walipokengeuka aliwahadhibu vikali na kufutilia mbali vitu vyote alivyokuwa ameviumba, usione kama amejiweka au amejikita yeye mwenyewe duniani tafakari kwa makini nini hatima ya maisha yako? Je unaenda vyema kama Henoko na Huhu? Kama sivyo basi tengeneza na mungu leo maana wakati huo Maana Mungu alitoa adhabu kwa ulimwengu mzima lakini je leo atatoa hivyo? Bali anaanza na habari ya mtu binafsi ikiwemo kufa kabla ya wakati.
 19 Nazishuhudiza si leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; (torati 30:19)
Pia wakati wa Ibrahimu, Mungu aliiangamiza miji ya Sodoma na Gomora kwa moto.
Sodoma na Gomora ni miji ambayo ilikuwa karibu na mwisho wa kusini ya bahari ya chumvi lakini kutokana na matetemeko ya nchi Bahari ilienea zaidi na kufunika mabaki ya magofu ya miji ile.
Eneo la kuzunguka sodoma lilifaa kwa kufuga wanyama na kwasababu hii Lutu alihamia huko (mwanzo 13: 10-13)
Wakati mmoja, Sodoma ilishambuliwa na maadui, Lutu alichuuliwa akawa mfungwa. Lakini Ibrahimu alichukua baadhi ya walinzi na wafanyakazi wake wakawashinda maadui na kumweka Lutu humu. Ibrahimu alitambua kuwa Mungu ndiye aliyempa ushindi na hivyoalikataa thawabu yoyote kutoka kwa mfalme wa sodoma na gomora. (mwanzo 14:1-24)
Watu wa Sodoma na Gomora walikuwa wenye dhambi nyingi, hasa zili dhambi za ufiraji.
 1 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
 2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.
 4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.
 5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
 6 Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.
 7 Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.
 8 Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.
 9 Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
 10 Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.
 11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.
 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; (mwanzo 19:1-12)
Mungu aliamua kuangamiza miji hiyo lakini Ibrahimu aliamua amwomba azuie hukumu yake kama mwenye haki  kumi wangepatikana mijini humo. Lakini wenye haki hawakuonekana huko na miji hiyo miwili iliangamizwa lakini Lutu na familia yake walitoroka kabla ya hukumu yake . (mwanzo 18:22-33)

Mafuta, aina ya lami, chumvi na kiberiti vilionekana kwa wingi katika eneo lile (mwanzo 14:10) na vitu hivyo vilitumika kuangamiza Miji. Maafa yale ya moto yalikuwa kazi ya Mungu kwa sababu wakati wake na ukubwa wake ulikuwa sawasawa kama Mungu alivyokuwa ametabiri kabla                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        
 24 Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. (19:24)
Bwana Yesu alipokuja duniani aliwaonya wayahudi waliosikia mafundisho yake na kuona matendo yake lakini walimkata, wangepata hukumu kali kuliko watu wa miji ya Sodoma na Gomora wasiosikia habari zake.
Hata wakati wa Yesu (kipindi cha agano jipya) Yesu alionya na kueleza uwepo wa kifo yaani kimwili na kiroho katika mafundisho yake.     
51 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. (yohana 8:51).
Mauti ya kifo ambacho Yesu anazungumzia hapo juu ni mauti au kifo cha kiroho, kifo ambacho mtu anakuwa bado kimwili ila moyoni mwake anakuwa amemkana kristo.
Pia Yesu alionyesha uwepo wa kifo cha mauti ya mwili pale alipomfufua Lazaro.
  4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
 5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro.
Hapa Yesu alidhihirisha uwepo wa mauti au kifo kwa wanadamu lakini bado alionyesha namna mungu alivyo na nguvu hata katika mauti au kifo kwani alimfufua hata Lazaro aliyekuwa na siku kadhaa kaburini. (yohana 11:4-5)

Je ni nani mwenye nguvu za kuzuia mauti au kifo kwa mwanadamu?
Kama ilivyonenwa kuwa chanzo kikubwa cha mauti au kifo cha kabla ya dhambi, tunapaswa kumcha Mungu na kuachana na uovu.    
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?   56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. (1 korintho 15:55-56)

Dhambi husababisha kifo katika namna mbali mfano, mtu akiwa mzinzi au muasherati atakufa kwa magonjwa au atafumaniwa na kupigwa na mwenye mume au mke hadi kifo, mtu akiwa mlevi basi anaweza kunywa vileo vikali mpaka vikaharibu mwili wake akafa kabla ya wakati, Mwizi anaweza kupigwa mpaka kufa.

MAONO NA MALENGO YA MUNGU KWA MTU BINAFSI.
Mungu humuumba mtu kwa makusudi yake haumbi kwa kubahatisha, wala kwa bahati nasibu ila Mungu anakuwa na lengo maalumu, haijalishi kama mtu binafsi anatambua au hatambui,
Swali la kujiuliza; Je wanadamu wote wanafahamu kuhusu hilo?        
Wanadamu wengi hawafahamu chochote kuhusu kuhusiana na malengo ya Mungu kwa mtu binafsi, wapo walioumbwa kwa ajili ya kuongoza, kumsifu Mungu, kutangaza habari za Mungu (kuhubiri Injili) nk.
Mungu hujishughulisha na kumgeuza mtu asiyefahamu kabisa habari za Mungu ili aone umuhimu na nafasi ya Mungu katika maisha yake na kuanza kumtumikia Mungu popote pale Mungu atakapotaka.
Mungu hashughuliki na mtu aliyeisikia sauti yake na kuibeza au kuipuuza.
Baadhi ya wanadamu ambao hawakumjua Mungu lakini Mungu aliwageuza:-
Paulo au Sauli
Jina la asili la Paulo ni Sauli. Alikuwa myahudi safi aliyezaliwa mjini Tano huko Asia ndogo yamashariki-kusini.
11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;  (matendo 9:11)
Kwa kuzaliwa kwake alirithi upendeleo wa raia wa kirumi.
37 Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe. (matendo 16:37)

Paulo alikulia huko akisema, kusona na kuandika lugha ya kiyunani na kiebrania bila shida totote. Ushawishi wa kiyunani katika masomo yake ulimpa uwezo wa kufikiri wazi na akili timamu na ushawishi wa kiebrania ulisaidia kujenga ndani yake tabia ya ukweli na unyoofu na maadili safi. (wafilipi 3:6)

Akiwa kijana mwenye bidii ya dini, Paulo aliamiaYerusalemu alipopokea mafundisho kuhusu sheria ya kiyunani kufuatana na mapokeo yenye nidhamu ya mafarisayo. Mwalimu wake alikuwa Rabi (mwalimu wa kiyunani) mwenye sifa sana, yaani Gamalieli (matendo 22:3-6, 26:5)

Paulo alikuwa fundi wa kushona hema (matendo 18:3)
Bidii yake ya kiyunani ilimchemsha Paulo achukie wakristo kwa hasira kali, alifikiri kuwa Stephano alikuwa mwasi dhidi ya sheria hiyo na hivyo alistahili hukumu ya kifo. ( matendo 6:13)
Alipata mamlaka katika baraza kuu la wayahudi (yaani Sanhedrin) aliongoza adha kali dhidi ya wakristo, aliwafunga wanaume na wanawake na kuwapeleka magerezani (matendo 8:3, 9:1-3)
Paulo alifikiri kuwa wakristo walikuwa na hatia ya kufufua kwa sababu walimwamini masihi aliyekuwa msalabani kwa sababu mtu aliyekufa msalabani alikuwa chini ya laana ya Mungu.  (matendo 26:11)
Paulo alivyokuwa njiani kwenda Dameski ili akawakamate wakristo na kuwapeleka gerezani, alipatwa na tukio la ajabu sana lililombadilisha kabisa. Yesu mwenyewe alijidhihilisha kwake na jambo hili lilimhakikishia kuwa Yesu yu hai. (matendo 9:3-5).
Maana yake ilikuwa Yesu hakuwa chini ya laana ya Mungu. Alikufa si kwa sababu alikuwa amevunja sheria, bali kwa hiari yake mwenyewe alichukua laana kwa ajili ya watu waliokuwa wamevunja sheria hiyona ufafanuo wake ulikwa uthibitisho maalum kuwa Mungu aliridhika naye. (warumi 1:4) Galatia 3:13) (Galatia 6:14)
Wakati huo huo ambapo Paulo alibadilishwa mawazo yake kuhusu Yesu, ufufuo wa Yesu Ulitokea uliodhihirisha kuwa yeye Paulo angetumiwa awe mtume/mtumishi wa mungu wa kimataifa.   
15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi. (matendo 9:15)
 16 Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
 17 nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao;
 18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. (matendo 26:15-18)
Tangu wakati huo Paulo hakuacha kustajabia kazi ya Mungu ya kumwokoa mtu yeyote aliyekuwa adui makali wa ukristo na kumfanya mjumbe wa ukristo huo.
Kwa njia hii Paulo alitambua sehemu ya maisha yake. 
8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.
 9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.
 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.(1 korinth 15:8-10)
8 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; (efeso 3:8)
Paulo aliokoka (aliongoka) mwaka 32 baada ya kristo (B.K)
Baada ya kuokoka Paulo alihubili sehemu mbali mbali kama vile Dameski, Yerusalemu (matendo 9:22-26) Uarabuni wakristo wengi wa Yerusalemu walikuwa na mashaka kuwa endapo kuongoka kwake haikuwa jambo la kweli. Laini Barnaba hakuwa na mashaka. Baada ya kumpeleka na kumtambulisha kwa Petro na Yakobo ndugu yake Bwana wasiwasi ulikwisha. (matendo 9:26-28).

Paulo alipata upinzani toka kwa wayahudi, Alipanda meli kutoka kaisaria hadi sham (Syria) ya kaskazini na kutoka huko alisafiri kupitia kilikia hadi tarso. (matendo 9:29-30) Lakini Paulo hakuacha kuhubili habari njema bali aliendelea kufanya hivyo katika miji mbali mbali kama vile korinth, mileto, na troa. . (2 timotheo 4:13-20)
 Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso.
Alifungwa gerezani lakini hakuacha kumtumikia Mungu, alipokuwa gerezani aliandika barua kwa wajoli wake ambao ni kwanza Timotheo
Tito alipotoka gerezani aliandika waraka wa mwisho ambao ni waraka wa mwisho wa timotheo. Paulo aliuawa mjini Rumi mwaka 65 baada ya kristo (B.K)

Je unajifunza nini kutoka kwa Paulo.
i.                   Mungu hamuokoi mtu bila dhumuni/lengo maalum Paulo aliokolewa ili awe mtumishi au mtume. Mimi na wewe leo  “Mungu hajatuokoa ili tukae kanisani tu” bali tuwaeleze wengine habari za Yesu kama alivyofanya Paulo Je tumewashuhudia wangapi ili wamjue Mungu?
ii.                 Tunapaswa kumuuliza Mungu kuhusiana na kazi yake, kumuuliza Mungu ili akwambie kalama yako ni vyema, Je nikutumikie katika lipi katika uhai wangu? Mungu atakuambia nini ufanye.
iii.              Katika kufanya kazi ya Mungu usiogope kitu chochote hata kifo kwani mungu alikuwa na Paulo hata alipokuwa gerezani alifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu Mungu hawezi kukuacha, atakuokoa dhidi ya kifo hadi pale kazi na lengo la kukuokoa litakapotimia hivyo utaishi maisha marefu.
YUSUFU
Mungu alikuwa aaamemuhaidi Ibrahimu na uzao wake nchi ya kaanani, lakini wazao wake wangeweza kumiliki nchi ile kama idadi yao ingetosha kwa kazi hiyo, lakini kabla ya yote walipaswa wajengeke na kuwa taifa. (mwanzo 15:1)
Biblia inaeleza matukio yalivyosababisha wazao wale wahamie misri ili wapate kuongezeka.
22 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. 23 Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu.  24 Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine. Mwanzo 30:22-24)]
Ingawa walipoamia misri walipata mateso ya wakati wa utumwa baada ya kkufa kwaeke Yusufu, wakati ulipotimia walihama kutoka misri na kuhamia kaanani.
13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. 14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. 15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.  16 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado. (mwanzo 15:13-16)
KUPELEKWA  MISRI
Yusufu alikuwa mwana wa 11 wa Yakobo, lakini akiwa mwana wa kwanza wa Raheli, Alipendwa sana na baba yake. Yusufu alipopata umri wa miaka 17, kaka zake walimchukia kiasi kwamba waliamua kumwondoa. Walimwuza kama mtumwa kwa wafanyabiashara wa misri, ingawa walimwambia baba yao kwamba Yusufu ameliwa na mnyama mkali.
23 Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, 24 wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. 25 Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. 26 Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? 27 Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. 28 Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri. (mwanzo 37:23-28)
Ingawa Yusufu alikuwa na maisha safi kimaadili, alifungwa gerezani. Kwa sababu ya tabia yake nzuri alipewa kazi ya madaraka gerezani iliyonufaisha wafungwa wengine gerezani lakini alingojea watu wafikena kumsaidia.
   1 Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. 2 Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. 3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake. 4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. 5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba. 6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu. 7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. 8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
 9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? 10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. 11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; 12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje. 13 Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia nje, 14 akawaita watu wa nyumbani mwake, akasema nao, akinena, Angalieni, ametuletea mtu Mwebrania atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa sauti kuu. 15 Ikawa, aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake kwangu, akakimbia, akatoka nje. 16 Basi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani. 17 Naye akamwambia kama maneno hayo, akisema, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kwangu anidhihaki. 18 Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje. 19 Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka. 20 Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani. 21 Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. 22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya. 23 Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu; kwa kuwa Bwana alikuwa pamoja naye. Bwana akayafanikisha yote aliyoyafanya. (mwanzo 39:1-23)

Kutokana na Yusufu kukataa kulala na mke wa potifa, mke wa potifaalimshika nguo zake alimwambia lala name, lakini Yusufu aliacha nguo yake na alikimbilia nje.
Mke wa Potifa aliwaita wote watu wa nyumbani mwakena kuwaambia Yusufu ameingia chumbani ili alale na alipotaka kupiga yowe Yusufu alikimbia alikimbia na kuacha nguo. Taarifa hizi zilimfikia Potifa na aliamuru Yusufu awekwe gerezani. Lakini bado Mungu hakumwacha Yusufu bali alikuwa pamoja naye.
Mwishoni mtu mmoja alimwambia mfalme habari ya hekima ya Yusufu, yeye mfalme aliweza kumwonya mfalme kuhusu maafa ya njaa yaliyokabili nchi yake, akatoa ushauri juu ya kushinda maafa yale. Mfalme akastaajabu sana hata akamfanya Yusufu awe mtawala wa miradi ya kukabiliana na maafa ya njaa, kasha Yusufu akawa mtawala wan chi yote ya misri (mwanzo 41:1-45)   
  
YUSUFU KUTAWALA MISRI
Yusufu aliwekwa kuwa mtawala wa misri alikuwa na umri wa miaka 30.
46 Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya Misri. (mwanzo 41:46)
Alimwona mwanamke wa mmisri na akapata wana wawili yaani Manase na Efraimu. 

Misri ilikuwa nchi pekee iliyokuwa imefanya maandalizi kwa ajili ya maafa ya njaa na hivyo watu walitoka kila sehemu ili wanunue chakula. Miongoni mwao walikuwa kaka zake Yusufu aliwatambua nduguze. Bali wao hawakumtambua yeye.    
8 Yusufu akawatambua nduguze, bali wao hawakumtambua yeye. (mwanzo 42:8)
     Yusufu aliishi kwa muda zaidi ya miaka tisini (90) na aliendelea kuamini kuwa Kaanani ilikuwa nchi ambayo watu wake siku moja wangeipokea kama nchi yao.kablaya kufa kwake aliionyesha imani yake katika ahadi za Mungu akitoa maaagizo kwamba kama watu wake siku moja wangeamia Kaanani wachukue maiti yake na kuizika Kaanani.

JE TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA YUSUFU
a)     Mungu hakumuumba kila binadamu kwa kusudi maalumu. Lakini si binadamu wote ambao hujitambua na kumuuliza Mungu nini anawaagiza wafanye bali huona kama wamezaliwa kwa bahati mbaya tu. Mungu alimwandaa Yusufu kuja kuwa mtawala wa misri na hakutaka apite mojakwa moja kuwa mtawala bali alimwandalia njia maalum ya kufikia kuwa mtawala.
b)    Mungu huyatimiza mambo yake kwa wakati na majira yake. Mungu alikuwa na uwezo wa kumwondoa Farao haraka na kumweka yusufu hatakama alikuwa na umri mdogo lakini wakati wake Mungu wa kumweka mtawala wake ulikuwa bado haujafika. Hata katika maisha ya kawaida unapokuwa namaisha ya shida, adha, dhiki unaweza ukaona kama Mungu hakuoni kutokana na kumuomba jambo Fulani kwa muda mrefu lakini Mungu anawakati wake wa kutenda ili ukuu wake uonekane.
c)     Mungu hamwachi mtu mwaminifu na anamwagiza tuwe waaminifu. Yusufu alishawishiwa na mke wa Potifa ili alale nae lakini Yusufu alikataa kwa kujua kuwa angelala naye angekuwa amemkosea Mungu. Hata sisi leo tunapaswa kuwa waaminifu hata kufa bila kujali mazingira wala kuogopa kitu chochote kile na tusishawishike na kitu chochote kile kumkosea Mungu.yusufu alifungwa gerezani lakini bado alikiri ukuu wa Mungu bila kukengeuka wala kumkosea Mungu.
d)    Mtu yeyote anayejitambua yeye ni nani mbele za Mungu humuepusha na mauti/kifo.ndugu zake Yusufu walitaka kumuuwa lakini MUNGU Salimtumia kaka yake Yusufu aitwae reubeni kuzuia wasimuue na mawazo yao yalibadilika na wakamweka kwenye birika na baadae wakaamua kumuuza.
Hata sasa Mungu huzungumza na wanadamu kuhusu kuacha njia zao mbaya na kumtumikia lakini binadamu wengi hupuuza kile ambacho Mungu anawaagiza wafanye, hali hii humfanya Mungu atuache na matokeo yake ni kufa kabla ya wakati. (luka 13: 6-9)

e)     Ikiwa Mungu yu pamoja nasi tusiogope wala tusiwe na hofu
  4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. (zaburi 23:4)
Mungu ndie aliyetuumba, anatuongoza na anajua hata siku ya kufa iliyo halali kwa kila mtu.
Si kila mauti/kifo Mungu anakuwa amemwita mtu huyo, bali kulingana na uasi wetu shetani hutusababishia kifo bila ya hata sisi wenyewe kujua.
Hivyo si kweli kuwa “BWANA AMELETA NA BWANA AMETWAA” kwani si kila anaye kufa Bwana amemwita.
Mfano
       Umekimbiza pikipiki au gari kupita kiasi ukapata ajali ukafa nayo utasema Bwana ameleta na Bwana ametwaa?
Mungu anaweza kuzuia mauti kwa mtu yeyote kwa kumpa taarifa mwenyewe au kutoa taarifa hapa kupitia kwa mtu mwingine, mara nyingi Mungu hufanya hivyo kwa mtu aliyekuwa amekengeuka ili amrudie kwa kumpa taarifa mtu ambaye ni mzee hivyo kwa wakati wake wa kufa umefika au mtu aliyetembea vyema na mungu. Tuone hahari za “Hezekia       
 1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana, 3 akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.  4 Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,  5 Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano. (isaya 38:1-5)

Hezekia alikuwa mfalme wa Yuda alitawala mwaka 716 hadi mwaka 657 B.K  yake ilikuwa katika hali ya kusikitisha. Siasa ya Ahadi aliiicha Yuda katika hali ya udhaifu ya kiuchumi na upnde wa dini isiharibike kwa kufuata dini za kinyume. Hezekia alijitwisha kazi ya kuimarisha hali ya nchi kuhusu uchumi, kupindua utawala wa washauri na kutengeneza dini ya Yuda. (2 wafalme 18:1-8)

Manabii wa wakati wa mfalme Hezekieli walikuwa Hosea, Isaya na Mika. Baada ya kuondoa uchafu wa dini za kinyume mjini Yerusalemu mfalme Hezekiel alisafisha nchi. (2 nyakati 31:1) 

Lengo lake lilikuwa taifa lote lifuate kanuni za dini zilizowekwa na Musa na zilizoendelezwa na Daudi.
Mashambulizi dhidi ya waashauri ya yerusalemu yalileta madhara makubwa kuliko Hezekia alivyokuwa ametazamia.
Siku moja Hezekia alikuwa mgonjwa sana hata ikaonekana kama angekufa. Kwa jibu la maombi yake, Mungu alimwongezea maisha yake miaka 15 hivyo alimwezesha kutawala Yuda katika matatizo yake. Kwa kumshukuru Mungu Hezekia alitunga wimbo wa sifa kwa kupona kwake. (isaya 38:9-22)
Hivyo ni dhahiri kuwa Mungu anaweza kuzuia Muti/kifo kwa mtu hasa anayeishi kwa kulifuata kusudi la Mungu, pale anapokosea Mungu hutoa maonyo na kuelezea matokeo yake ili mtu huyo abadili njia zake mbaya na amfuate yeye. Biblia inasema.
12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye. (mithali 3:12)

Mungu hutumia njia mbalimbali kuwaonya wanadamu, lakini binadamu hukaidi yale Mungu anayoagiza na matokeo yake Mungu  huacha wanaokaidi wakaenda kama vipofuna matokeo yake ni kufa kabla ya wakati.

SABABU ZA KUFA KABLA YA WAKATI
1.     Uzinzi au Uasherati.
Uzinzi ni ushiriki wa kimwili ni baina ya watu waliooa au kuolewa wakishirikiana na watu wasio wa ndoa yao yaani ushiriki wa kimwili nje ya ndoa au na mtu wa ndoa mwingine .
Uasherati ni ushirika wa kimwili baina ya watu wasiooana.Uchafu unaofanyika au unaotokana na uasherati na uzinzi kwa jumla tunaita zinaa.
2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. (1 korintho 7:2)
Maana ya kufanyika umoja au mwili mmoja wa mwanamke na mwanaume mmoja katika ndoa ni kwamba, hakuna nafasi kwa mtu mwingine awaye yote.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. (mwanzo 2:24)
Chanzo cha uzinzi au uasherati ni tamaa mbaya, uasherati au uzinzi hutokea kwa sababu watu baada ya kujaribu kuzuia majaribu ya tama ya kimwili, huichochea tu. Hawatawali mawazo na hisia zao na baada ya muda mfupi hujiona kuwa hawawezi kutawala tabia zao.
  24 Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni. 25 Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. (mithali 6:24-25)

28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. (mathayo 5:28)

Kufanya uzinzi au uasherati ni kuhatarisha maisha pia ni chukizo kwa mungu, kwani matokeo ya uasherati na uzinzi ni kuambukizwa magonjwa kama vile upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kaswende, kisonono nk.
Ni vema ikumbukwe kuwa miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu hivyo tuinapaswa kuepuka uzinzi na uasherati kwani roho mtakatifu huwa hakai mahali pachafu na Mungu atamwadhibu mtu yeyote anayechafua hekalu lake.
15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. (1 korintho 6:15-20)
Mungu anasisitiza kupitia mtume paulo kuzikataa tamaa za ujanani na kuziepuka kwani chanzo cha uzinzi na uasherati husababisha kuvunjika hali ya kupelekea watoto kutangatanga na kukosa mwelekeo. Wanandoa kuambukizana magonjwa kama vile ukimwi, kaswende, kisonono nk. Na hupelekea kifo au mauti.
Uasherati au uzinzi hupelekea uzinzi uliokithiri 
2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu. 3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?  4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.  5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. 6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. 7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. 10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo. 11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; 12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini. (marko 10:2-12)
Baadhi ya watu huacha wake zao na kutoa taraka kasha anaoa tena, hali hii inasababisha uzinzi uliokithiri kwani watakapoendelea kuishi na huyo mwanamke watakuwa wanazini.

Athari za kufanya tendo la ndoa kabla ya kuoana (ndoa)
       i.            Kufanya tendo la ndoa kabla ya kuoana ni dhambi kufanya ngono kabla ya kuoana ni dhambi kubwa kwani wanaofanya hivyo huhatarisha maisha yao kwa kuambukizana magonjwa na baadaye kufa.
 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (warumi 6:23)
       Hivyo kufanya tendo la ndoa kabla ya kuoana husababisha kifo cha kimwili na kasha kuhukumiwa na kutupwa jehanamu.

     ii.            Kuvamiwa na maroho machafu katika kufanya ngono, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji na huko wanapewa madawa ya ajabu ambayo yanapelekewa kuvamiwa na mapepo na kupenda au kuwa na hamu ya kufanya ngono kila wakati. Pia kutokana na kupenda ngono wengine wamefanya na majini bila ya wao kujua na majini hayo yanawamiliki na wao hawajui watatokaje katika vifungo hivyo .

  iii.            Husababisha majeraha na fedheha kubwa maishani katika kufanya ngono kuna majeraha ya maisha kama vile magonjwa hatari kama Ukimwi, kaswende, kisonono nk. Majeraha haya ya magonjwa yatapelekea mwili kupata maumivu makali na kumfanya mtu ashinwe kufikia malengo aliyopanga,mwisho hubakia kujuta na kuwajutia watu walio msababishia majeraha wakati huo upo kitandani. Mungu anaonya uzinzi kwa kukemea kuwa kuzini na mwanamke ni upumbavu kabisa.     
  32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
Hivyo kuzini ni chukizo kubwa kwa mungu wetu, epuka kabisa ili uishi vyema na mungu wetu.

   iv.            Kuwapa wengine miaka yako, uchunguzi unaonyesha mtu anayependelea kufanya ngono mara kwa mara kabla ya ndoa hawezi kuishi miaka mingi/muda mrefu na si hivyo tuvijana hujiua kwa kujinyonga, huuana na kufa kwa sababu ya mapenzi, wengine wanaugua hadi kufa angali wadogo na kupatwa na magonjwa mabaya na hivyo waliostaili waishi hapa duniani na hivyo wanakuwa wamewapa wengine  miaka yao.
              9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; (mithali 5:9)
      v.            Ni kuiangamiza nafsi yako. Nafsi kwa kiyunani Psuche, ndani yake kuna hisia, akili na maamuzi ya mtu.
             32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. (mithali 6:32)
              Hivyo kuiangamiza nafsi yako na kuangamiza malengo/matarajio (future) yako na mipango yako uliojiwekea                mwanzoni.
   vi.            Utavunjiwa heshima  
32      Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.   33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. (mithali 6:32-33)
Siku zote Yule unayefanya nae tendo la ndoa kwanza atakuona wewe ni mpumbavu kwa sababu atakujua jinsi ulivyo sirini na hivyo atakudharau zaidi na kukutangaza kwa wengine na wewe pindi utakapooa au kuolewa kwa kuwa nguvu zako uliwashibisha wengine basi utavunjiwa heshima na wengine.
 vii.            Kuwashibiasha wengine nguvu zako
 10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; (mithali 5:10)
Tendo la ndoa ni tendo ambalo linahitaji mtu atumie nguvu (hasa mwanaume) hivyo kadri mtu anapofanya mara kwa mara anajipotezea nguvu zake na kuwashibisha wengine na hivyo dhoruba itamkuta katika ndoa yake kwa sababu hatakuwa na nguvu tena kama awali.
Ni vyema kuacha kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati ili kuishi maisha marefu.
(http://sanga .wordpress.com/2007/02/06/ndoa-2/) (Partick sanga ministries)
2.     Kutowaheshimu wazazi (Baba na mama)     
16 Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. (torati 5;16)
Ni wazi kuwa uhusiano mzuri na wa uhakika kati ya kijana na mtu wa wazazi wake humfanya afanikiwena kinyume chake ni laana katika maisha na mtu huyo hawezi kuishi maisha marefu.
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. (efeso 6:1-3)
Kwa mujibu wa maneno ya Mungu hapo kweli kuwa usipowaheshimu wazazi ni vigumu kufanikiwa bali ni laana itakufatilia na mwishowe unakuwa na muda mfupi wa kuishi yaani unakufa mapema.
3.     Kutokumcha Mungu
Kumcha mungu ni hali ya kuishi maisha yanayoongozwa na Hofu ya Mungu yaani kuishi kwa woga dhidi ya Mungu bali kuishi maisha ambayo moyo, mwili, nafsi na roho ya mtu inakuwa imejazwa na kiu pamoja na njaa ya kumpendeza Mungu na kufanya mapenzi yake yote kwa furaha.
 27 Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa. (mithal 10:27)
Pia ili ufanikiwe katika mambo yako yote ni lazima umche Mungu kwani yeye ni kila chanzo cha kila kitu kitu iwe fedha, mali, kazi vyote vyatoka kwake.
7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. (mithali 1:7)
Hivyo ukimcha Mungu utaishi maisha marefu na hata katika mambo yako utafanikiwa kabisa yaani rohoni na mwilini pia.
4.     Kutomtumikia Mungu.
25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. (kutoka 23<25-26)
Watu wengi hukwepa kazi ya kumtumikia huona kazi ya kumtumikia Mungu ni ya watu Fulani tu. Mungu alituumba ili tuzae matunda kwake (tumtumikie)
Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. 19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. (mathayo 21: 18-19)
Kukwepa au kukimbia kufanya kazi ya Mungu ni laana. Biblia inasema kuwaYesu alipouona mti aliuendea asione matunda aliulaani kwani aliuumba kwa makusudi maalum. Swali langu mimi na wewe Je tangu tulipookoka/kumjua Mungu tunamtumikia?
Kama hatumtumikii basi anapoona atumtumikii anatulaani kamailivyokuwa kwa mti na matokeo yake tunakufa mapema. Hivyo tafakari mwenendo wako na nini umefanya kwa Mungu kama hakuna ulichofanya chukua hatua leo ili usife mapema.
5.     Kumwekea Mungu mipaka.
Ni hali ya kuamini kuwa Mungu anaweza mambo Fulani tu na mengine hawezi. Kitendo hiki ni kumdharau Mungu.  
41 Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu; Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli. s Hawakuukumbuka mkono wake, Wala siku ile alipowakomboa na mtesi. 43 Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika konde la Soani. (zaburi 78:41-43)
Maelezo hayo hapo juu yanaeleza namna wanaisrael walipokuwa safarini kwenda kanani walivyosahau mambo makubwa ambayo Mungu alikuwa amewafanyia na kuona kuwa baadhi ya mambo Mungu hawezi
Pia hesabu 13 na 14 Biblia inaeleza jinsi gani Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi (kaanani) waone kama kweli ni nchi ya ahadi na maziwa, wapelelezi hawa walileta walileta habari ya ile ni nchi ya ahadi na maziwa lakini inakaliwa na wafeli –wana wa Anaki, Ameleki (negebu), Mhiti,  Myabusi   na mwamori wapelelezi hao walisema waliwakuta huko ni majitu na wao (wanaisrael) ni kama panzi tu hivyo wawezi kwenda wakaimiliki. Lakini Musa, kalebu, Haruni na Joshua walizungumza mbele ya wana wa Israel wakiamini kuwa Mungu anaweza kuwapa ile nchi wamiliki kama walivyomwapia Ibrahimu. Na watu wote waliomwekea mungu mipaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi.
Pia Joshua 24:1-29 inaeleza kuwa Joshua alikufa akiwa na miaka 110 akiwa na nguvu zake kamili mpaka Bwana alipompumnzisha.
Kama unataka kuwa na maisha marefu unataka kuziongeza siku zako za kuishi kwa imani usimwekee Mungu mipaka.
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. (isaya 55:8)
Hivyo kila unachofanya Mungu anajua ni vema kumuomba ili akuongoze kwa kila jambo.
6.     Uongo na udanganyifu.
Uongo ni matendo na maneno ya udanganyifu nayo yanakataliwa na Mungu. Mtu anayehesabiwa kuwa na hatia hata kama amesema nusu ukweli pia mtu anapata hatia kwa kusema uongo kuwa ukweli.
  10 Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja. 11 Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, Bwana asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake 12 Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia, baada ya Hanania, nabii, kuivunja ile nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, kusema, 13 Enenda ukamwambie Hanania, ukisema, Bwana asema hivi, Umezivunja nira za mti; lakini badala yake utafanya nira za chuma. 14 Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo mataifa haya yote, ili wamtumikie Nebukadreza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami nimempa wanyama wa nchi pia. 15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo. 16 Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana. 17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba. (yeremia 28:10-17)
Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, nabii Hanania alitabili uongo hivyo alikufa ndani ya mwaka huo huo
Pia matendo  5:1-11 biblia inasema.  
1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, 2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. 3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. 6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. 7 Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. 8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. 10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. 11 Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.
 Hivyo Mungu hafurahishwi na udanganyifu unaofanywa na wanadamu hivyo anafikia uamuzi wa kukatisha uhai wa mtu kabla ya wakati wake
Ni vema kuacha tabia ya kinyonga yaani leo mkweli kesho mwongo, ndugu yangu hata kwa Hanania na Safira waliona kama Mungu hawaoni lakini aliamua kuwaadhibu mara moja. Acha tabia ya uongo tubu ili uishi miaka mingi.
7.     Kukosa bidii katika kumpenda Mungu    
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. (zaburi 91:14)
Ukizishika sheria na Amri alizotoa Bwana maishani mwako yeye atajidhihirisha kwako na upendo wako wake kwako na kadri unavyoongeza bidii ya kumtii na kumheshimu Mungu atakushibisha au atakuongezea siku za kuishi, wewe ndiye unayeweza kumwambia Bwana miaka 90 inatosha nataka kurudi nyumbani kupumnzika au 50 inatosha nataka kurudi kwa Bwana.
  1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. 2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.  ( mithali 3:1-2)
Hivyo ukitaka kuishi miaka mingi fanya juhudi za kumpenda Mungu.

8.     Maisha ya dhambi
Dhambi ni kuvunja sheria ya mungu ambayo ni sheria ile inayoeleza ukamilifu unaodaiwa na utakatifu wa Mungu. Dhambi ni mbaya kwani inkutenga mbali na Mungu.
  1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. (isaya 59:1-2)
Dhambi inakufanya ufe kabla ya muda wako. Usifurahie kuishi katika dhambi epuka uzinzi, oungo, uasherati, usengenyaji na kulipiza kisasi nk. Kwa kutenda dhambi unajipeleka jehanamu (kaburini) kabla ya wakati.    
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (warumi 6:23)
Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi, swali la kujiuliza ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kushindwa kuikwepa dhambi ya uzinzi na uasherati? Ni wezi wangapi wamekufa kwa kuchomwa moto? Epuka dhambi ili uishi maisha marefu.
Ninaamini baada ya kujifnza sababu za kufa kabla ya wakati utafanya mabadiliko makubwa katika maisha yako na utaishi maisha marefu. “Mungu akubariki”

MAMBO YA KUFANYA ILI USIFE KABLA YA WAKATI
             i.            Kufanya maamuzi ya kuokoka sasa kabla hujafa.
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (yohana 3:16)

Mungu hafurahii kifo cha mtu mwovu na hivyo kaukosa uzima wa milele hivyo kama hujaokoka nakushauri chukua hatua n a maamuzi ya kuokoka leo. Kama ujaokoka sema maneno haya kwa kumaanisha;

“mungu baba naomba unisamehe kwa yote niliyofanya kinyume na mapenzi yako kwa kuwaza, kunena, na kutenda. Naomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu, uniandike kwenye kitabu cha uzima, kuanzia leo unifanye kuwa mpya, uniongoze kwa kila jambo, Asante Yesu mana umeniokoa “Amen”
Baaada ya kusali sala hii ishi maisha matakatifu na usitende dhambi tena.
          ii.            Kulitumikia kusudi la Mungu  
Maana yake kulitambua wewe ni nani na unapaswa kufanya nini kwa ajili ya Mungu. Yaani ni kutekeleza au kukamilisha wajibu ambao ulimfanya Mungu. Mungu humuumba kila mtu kwa kusudi maalum. Ni muhimu kutambua lengo la Mungu kuumba kasha fanya jambo ambalo litalenga kutekeleza wajibu wako. Mungu haruhusu kifo kwa mtu anapokuwa amemaliza wajibu wake duniani. 
 36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. (matendo 13:36)
Hivyo katika maisha jiulize umefanya nini kwa ajili ya Bwana ambacho unaweza kujivunia.
        iii.            Kuishi maisha ya kumpendeza Mungu au kufanya mapenzi ya Mungu.
Katika maisha yako unapaswa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa kusali tu haitoshi
 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? (mathayo 7:22)
Hivyo ishi maisha yanayompa Mungu utukufu na ishi maisha matakatifu.

        iv.            Kuishi kwa imani  
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba thawabu wale watafuata”
Sote tunaamini kuwa Yesu kristo atarudi kulichukua kanisa lake au watakatifu.
Swala la kuaini kuwa Yesu atarudi ni la imani hivyo tunapaswa kuendelea kuamini hivyo hadi siku ya kufa, usije ukafika wakati ukasema huyu Yesu mbona harudi afadhali nianze kutenda dhambi, uwe na imani kwani siku akija utamwona. Usiruhusu kitu chochote kikuondolee imani kwa ‘Yesu’ kwa sababu huwezi kumwona Mungu bila kupitia kwa Yesu.
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. (yohana 14-6)
Hivyo tumwamini yesu ili alij au ukifa ufe katika Bwana.

          v.            Kufanyika msaada na sababu ya wokovu kwa walimwengu
Kuna orodha ya watu katikauflme wa Mungu ambao wanakusubili wewe uwaambie habari za Yesu.
Yesu anataka tuungane nae katika kuwarejesha mateka kwenye ufalmu wa Mungu, unapomwambia mtu habari za Yesu anaonyesha kuikubali (kuunga mkono) kazi aliyoifanya Yesu  pale msalabani.
Swala la kujiuliza “je kuna mtu/watu yeyote ambye amewahi hata kumshukuru Mungu na kuwashukuru wazazi kwa kukuleta hapa duniani baada ya kuona mambo mazuri ya kiungu uliyowafanyia?
15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. (marko 16:15)
Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuzitangaza habari za Yesu kunyamaza kimya ni kutozaa matunda hivyo ni kutafuta kufa kabla ya wakati ni muhimu watu watambue uwepo wako duniani.

        vi.            Kujithamini juu ya uhusiano wako na kristo
   25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti. (mithali 16:25)
Ni muhimu kufikiri kama maisha yako yanaleta utukufu kwa Mungu au hayaleti na kama hayaleti unafanya nini mpaka ili yalete?

Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, Mungu hutuvumilia ili tujitambue na tubadilike, tuishi maisha yenye utukufu. Unapokuwa umeshindwa kubadilika anaamua kukatisha maisha yako yaani KUFA KABLA YA WAKATI.
Hivyo kama kuishi maisha marefu chukua hatua
Ø Tubu toba ya kweli
Ø Jitathimini juu ya mwenendo wako
Ø Anza maisha mapya
Ø Mtumaini Mungu katika kila jambo
Baada ya kufikiri kwa makini Sali sala hii:-
Mungu baba naomba unisamehe mimi mwenye dhambi kwa kufanya mambo bila kutambua unisaidie nitambue kusudi la kuumbwa kwangu na nitekeleze agizo lako kasha niishi maisha marefu, unisaidie, unilinde, uniepushe na ajali pamoja na mauti/kifo cha aina yoyote kisicho cha halali hadi hapo Bwana utakaponiita
Powered by Blogger.