Historia ya Riwaya ya Kiswahili
Historia ya riwaya ulimwenguni haina muda mrefu sana hasa
inapolinganishwa na historia ya tanzu nyingine za fasihi kama vile ushairi,
tamthiliya, na fasihi simulizi. Riwaya ya Kiingereza kwa mfano, irnejitokeza
hasa mnamo karne ya 18 ingawa riwaya ya kwanza inasemekana kuwa ni ya Don
Quixote iliyoandikwa 1605-15. Riwaya za mwanzo kuandikwa ziliongozwa na
Fielding aliyeandika vitabu vya Joseph Andrews (1742) na Tom Jones
(1749); vile vile mwandishi kama Richardson alijitokeza na kuwa maarufu kwa
kitabu chake cha Pamela (1749). Riwaya ya Kirusi nayo ilijitokeza zaidi
wakati huo huo.
Historia ya riwaya ya Kiswahili nayo haikupishana sana na hali
hiyo ya kutanguliwa na tanzu nyingine za fasihi, ingawa kwa hakika imejitokeza
mapema zaidi kabla ya tamthiliya za Kiswahili. Tofauti kubwa kati ya riwaya ya
Kiswahili na riwaya za Ulaya ni kwamba yenyewe imeanza kujitokeza mwishoni mwa
karne ya kumi na tisa. Zaidi ya hilo, riwaya ya Kiswahili imekuwa na maendeleo
tofauti kabisa hasa kwa vile imeanza kukua kutokana na hadithi zilizotokana na
fasihi simulizi.
Pamoja na kutanguliwa na tanzu nyingine kama vile ushairi, ambao
historia yake ni ndefu sana, historia ya riwaya, kwa haraka mno imepitia hatua
tofauti nakukua kiasi ambacho hivi sasa umaarufu wake umezidi ule wa tanzu
nyingine kwa klwango kikubwa sana. Ikiangaliwa katika wakati wake wa sasa,
riwaya ya Kiswahili inaonckana kuwa imetajirika sana upandc wa dhamira, muundo,
ujenzi wa wahusika na hata kwa idadi. Ni utanzu ambao kwa upana na undani zaidi
umeweza kuzingatia nyanja tofauti za maisha kama vile uchumi, siasa, utawala na
maisha ya jamii kwa jumla. Riwaya ya Kiswahili imeweza kuvuka mipaka ya nchi na
hata kwenda nje ya Afrika Mashariki. Sababu za maendeleo kama hayo zitajitokeza
wakati wa kujadili vipindi tofauti vya historia ya riwaya ya Kiswahili. Mojawapo
ya sababu kubwa ambayo inaweza kutajwa hapa ni ongczeko la watu wanaoweza kusoma
na kuandika.
Historia ya riwaya ya Kiswahili imeangaliwa katika sura tofaati
na wataalamu na watafiti mbalimbali. Wapo wale ambao wameiangalia pamoja
na historia ya fasihi ya Kiswahili kama vile Rollins (1983), na wapo ambao
wamegusia uandishi wa hadithi za Kiswahili kama vile Balisidya N (1976), Rollins
(1985), Ohly (1981), Senkoro (1977), (1989) na wengine. Kuhusu historia ya
riwaya wapo wataalamu tofauti ambao wameiangalia historia hiyo katika sura
tofauti. Baadhi wanaiangalia historia hiyo kuanzia mwishoni mwa karne ya kumi na
tisa. Wataalamu hawa, ikiwa ni pamoja na Rajmund Ohly (1981) wanaiangalia
historia ya riwaya ya Kiswahili kuanzia wakati wa Edward Steere, ambaye mwaka
1870 alikusanya simulizi za wenyeji wa Zanzibar na kuzihariri. Hadithi hizi
zilikusanywa na kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Wataalamu kama hawa
wanaiangalia historia ya riwaya kuanzia kwenye chanzo chake na vilevile kuanzia
kwenye hatua za mwanzo katika maendeleo yake. Wapo wataalamu wengine ambao
wanaona kuwa historia ya riwaya ya Kiswahili ilianzia robo ya kwanza ya karne
hii ambapo vitabu kama vile Mwaka katika Minyororo (Mary Sehoza: 1921)
viliandikwa. Ni wakati huu ambapo wataalamu kama akina Senkoro (1976)
walichangia katika hoja hiyo wakiwa wametanguliza kitabu cha James Mbotela
(1934) cha Uhuru wa Watumwa kuwa ndicho kinachoweza kuchukuliwa kama
mwanzo wa historia ya riwaya ya Kiswahili. Senkoro (1976:75) anadai kuwa:
... riwaya ya Kiswahili ndipo hasa ilipoanza wakati James Mbotela alipoandika Uhuru wa Watumwa. Hii ndiyo iliyokuwa riwaya ya kwanza ya Kiswahili nayo ilikuwa na mandhari ya huku huku Afrika Mashariki, wahusika walikuwa Waswahili, na maudhui yake yaliwahusu Waswahili kwa jumla, na mwandishi mwenyewe alikuwa Mswahili.
Dai hili linaweza kupambana na dai la Kezilahabi (1980) kuwa
waandishi wa Kiswahili sio lazima wawe Waswahili na pia suala la Mswahili ni
nani. Dai hilo kuhusu Mbotela limepingwa na Shariff (1988:18-19) ambaye haamini
kuwa kazi hiyo imeandikwa hasa na Mbotela na kuwa mawazo mengi hapo sio ya
Mswahili. Shariff anasema:
... lakini ukisoma kitabu hicho chenye jina lake, ni mara tu utagundua kuwa mara kwa mara maelezo yaliyokuwemo hayakuelezwa na mtu anayesema Kiswahili kuwa ni lugha yake. Utaona dhahiri kuwa mara nyingi mawazo ni ya Kiingereza ... ingawa wafasiri walichukua hadhari sana wasitambuliwe kuwa hadithi ni ya kubuni na fikira, kwanza zilipangwa kwa Kiingereza.
Wakati mawazo ya Senkoro yanaweza kuwa yamekitwa kwenye
ufafanuzi wake wa riwaya ya Kiswahili, uchunguzi wa Shariffunaonyesha kuwa
kufuatana na vigezo tunavyoviona kwa Senkoro riwaya ya Mbotela inaweza
isistahili sifa hiyo ya kuwa riwaya ya Kiswahili. Hata hivyo Shariff hakukiri
waziwazi kwamba hiyo si riwaya ya Kiswahili. Ufafanuzi wetu wa baadaye kuhusu
riwaya ya Kiswahili utaweza kutoa mwanga zaidi kuhusu suala hili. Ni muhimu
kufafanua riwaya ya Kiswahili ni ipi na ni nini.
Pamoja na wataalamu hao waliotajwa wa makundi hayo mawili, wapo
wataalamu wengine ambao wanadai kuwa histoha ya Kiswahili imefunguliwa mlango na
Shaaban Robert. Hawa ni akina Elena Bertoncini (1980:85) na Shegov (1976).
Pamoja nao wachunguzi kama akina Rollins (1983) wanachangia zaidi. Hawa
wameichukulia riwaya ya Kiswahili katika hatua yake ya juu kimaendeleo na kuacha
pengo kubwa ambalo ndilo hasa lililoweka msingi wa kukua kwa riwaya ya
Kiswahili. Na wapo wataalamu ambao wameiangalia riwaya ya Kiswahili na
kuilinganisha na liwaya zmgine za Ulaya kama vile Ohly (1981:16) anavyoona kuwa
riwaya ya Kiswahili ilianzia mwaka 1974 wakati Kezilahabi alipoandika
Kichwamaji.
Ili kuielewa historia ya riwaya ya Kiswahili kwa upana zaidi ni
muhimu kutoa ufafanuzi wa riwaya kama tutakavyoiangalia katika kazi hii na kama
ambavyo ufafanuzi huo unavyokubalika na wataalamu wengine. Tofauti yake na tanzu
nyingine za fasihi na uhusiano baina yake na tanzu kadhaa ni mambo muhimu ya
kuzingatia.
Ili kufafanua riwaya ya Kiswahili ni nini itakuwa ni muhimu
kutambua hadithi au masimulizi ni vitu gani na kuweza kuonyesha uhusiano baina
ya tanzu hizi za fasihi ambazo hushabihiana sana. Tanzu hizi za fasihi zinaweza
kuwa na hali ya kuchanganywa sana. Ushairi na tamthiliya ni tanzu ambazo
zimetofautiana vya kutosha na hivyo hazitakuwa na umuhimu wa kujadiliwa hapa.
Riwaya ni hadithi ambayo imekitwa kwenye dhamira moja kuu.
Dhamira hiyo inaweza kuwa imejengwa na dhamira kadhaa ndogo pamoja na visa
tofauti. Dhamira hizo ndogo, kama vile visa, huwa vinahusiana katika kuijenga
riwaya nzima. Pamoja na hayo, riwaya huwa inakuwa na wahusika ambao aghalabu ni
watu wanaowakilisha matendo na maisha ya binadamu kwenye maandishi. Riwaya sio
maelezo halisi ya maisha ya binadamu bali ni maelezo ya mtunzi kuhusu
anavyoyaona maisha hayo, ambavyo angetaka yawe au hata ambavyo angependa yasiwe.
Kwa hivyo basi, riwaya ni mchanganyiko wa ukweli wa maisha na ubunifu wa
mwandishi uliojengwa kiasi cha kumfanya msomaji ahusishe hadithi hiyo na maisha
halisi ya binadamu.
Ingawa riwaya na hadithi zinazotokana na simulizi zote ni
hadithi, liwaya inazmgatia maisha yajamii wakati huo. Hadithi zingine zinakuwa
ni mapokezi ambayo huwa na nafasi ya msimuliaji kuongeza, kubadili au kupunguza
kile kilichokuwemo kwenye masimulizi ya awali. Ni hadithi ambazo zinazingatia
sifa za wahusika na maadili yaliyosimuliwa kuliko dhanura zilivyojengwa au
uhusiano wa visa, dhamira, lugha na wahusika wenyewe. Haya yatajitokeza kwa
upana zaidi katika kuielezea riwaya ya Kiswahili. Aidha ni muhimu kutambua kuwa
riwaya ni tokeo la maendeleo ya kiteknolojia ya uchapishaji, uchapaji na
uandishi. Hivyo basi, mwandishi wa riwaya hana ulazima wa kuweka kumbukumbu ya
hadithi yake kiwawani kama vile msimuliaji. Vile vile mwandishi anakuwa na uwezo
wa kupanga na kupangua hadithiyake. La muhimu hapa ni kuzingatia pia kuwa
tunapozungumzia riwaya ya Kiswahili tunamaanisha riwaya zilizoandikwa kwa lugha
ya Kiswahili. Hivyo riwaya zilizotafsiriwa kwa Kiswahili zitaangaliwa tofauti
katika mchango wake wa kuiendeleza riwaya ya Kiswahili na vile vile nafasi yake
katika historia ya riwaya ya Kiswahili.
Mawanda ya riwaya ni mapana zaidi kuliko yale ya tanzu nyingine
za fasihi. Ni utanzu ambao unaweza kujumuisha hadithi zaidi ya moja ambazo
zimeunganishwa kama visa. Vile vile unaweza kuingiza masimulizi ambayo yamekitwa
na kujengwa na dhamira moja kuu ndani yake zikiwemo dhamira ndogo ndogo. Riwaya
huundwa kwenye hali ya mkufu utokanao na visa. Riwaya, tofauti na tanzu
nyingine, inakuwa na wahusika ambao hujengwa kutokana na hali ya kimaisha ya
binadamu ili kumwakilisha binadamu katika kuufikisha ujumbe wa msanii. Hata
hivyo, haimaanishi kwamba hii ni aina nzuri zaidi ya kujieleza ingawa ni utanzu
unaowaelezea watu kwa undani zaidi na jinsi wanavyoishi. Ikiwa na mchanganyiko
wa matukio, hali, mazungumzo na majadiliano, maelezo na kauli za msanii, riwaya
imejizatiti kwenye kuelezea nyanja nyingi zaidi za maisha kuliko tanzu nyingine
za fasihi. Hii ni pamoja na kuonyesha hisia na maono yao, mawazo yao, nyendo na
tabia zao. Iwe imekitwa kwenye matukio halisi ya kudhaniwa au ya Kutungwa.
Riwaya kama kazi zote nzuri za fasihi, inaweza kusaidia Kufafanua na kutoa mambo
yaliyojificha au yasiyoonekana katika maisha ya kila siku. Tofauti nyingine kati
ya utanzu huu na tanzu nyingine za fasihi ni kuwa riwaya huyatoa matendo ya
binadamu kwa uwazi na ukamilifu wa kutosha kuweza kumfanya binadamu ajione,
ajifunze na kujikosoa. Ni utanzu ambao huweza kumsogeza zaidi msomaji kwenye
chanzo cha uhalisi au ukweli wa jambo na kumpa njia ya kuwazia au kujadili jambo
kwa upana zaidi. Kwa hali hiyo, utanzu huu hukidhi lengo la kumfunza binadamu
mambo mengi na kwa njia nyepesi, hasa kuliko ushairi.
Tofauti na simulizi, riwaya ni hadithi zenye matukio
yaliyopangwa kufuatana na muda wake kimantiki. Hadithi ambazo zinahusu maisha ya
watu wanaoishi katika wakati fulani. Tukio moja linafuatiwa na tukio jingine na
vilevile kuhusishwa nalo kwenye hali ambayo inakubalika kwa kuzingatia maisha na
tathmini ya maisha ya wakati huo. Ili kufanikisha hayo, muundo wa riwaya
unahitaji kutumia nyenzo maalum kama vile wahusika, lugha yao, visa vinavyooana
na msuko wa matukio yanayolingana na kuijenga dhamira. Vyote hivi, kwa pamoja na
kwa kuhusiana, vinatanda kwenye hadithi nzima ambayo inakuwa imejengwa na
dhamira ndogo ndogo. Hivyo, mwandishi wa riwaya hawezi kuukana wakati maalum
katika historia ya maisha anayoy- azungumzia katika msuko wake wa riwaya kama
vile ambavyo fasihi simulizi inavyoweza kuukana wakati maalum na hata kutoa
nafasi ya wahusika wa aina tofauti, wanyama, binadamu, miti n.k. Riwaya, pamoja
na kuweza kutumia wahusika wa aina zote, inazingatia historia ya jamii ya
wakati maalum.
Tukianza kuzungumzia historia ya riwaya ya Kiswahili ni muhimu
kuihusisha sana na fasihi simulizi. Vhusiano huu sio wa kimuundo, ingawa muundo
wa masimulizi ulichangia kwa kiasi fulani katika riwaya nyingi za mwanzo, lakini
zaidi ni uhusiano uliotokana na uandikaji wa hadithi za Kiswahili. Edward Steere
alipokusanya na kuhariri hadithi alizozipata kutoka kwa wakazi wa Zanzibar
unaweza kuwa ndio wakati wa kwanza kuiangalia historia ya riwaya yetu. Hadithi
hizi zilikuwa sio za kiriwaya bali hadithi fupi ambazo zilitokana na simulizi
tofauti za jamii hiyo. Katika mkusanyiko huo hadithi maarufu kama vile
“Sultan Majinuni” na 'Sultan Darai' zilikuwepo. hadithi hizi zilikuwa
maarufu sana na kuwa ni njia mojawapo ya kuwahamasisha watu wengine waliojua
kusoma na kuandika kuweza kupata picha ya uandishi wa hadithi. Baadaye hadithi
zingine zilikusanywa na kuhaririwa na Velten. Kati ya hadithi hizo zilikuwepo
hadithi ndefu kama zile za Mtoro bin Mwenyi Bakari ambazo zilijumuisha maelezo
marefu kuhusu watu ambao Mwenyi Bakari alikutana nao katika safari zake, mila na
desturi zao, vyakula na maisha yao. Nyingi ya hadithi hizi zilikuwa
hazikuzingatia au kuyahusisha maisha ya watu wa Afrika Mashariki. Hadithi nyingi
zilikuwa na ubunifu wa kinjozi usio wa dhati kwa maisha halisi ya wenyeji. Kwa
hali hiyo, maadili mengi ambayo yangewafaa wanajamii yalielekea kuwa
yangepokelewa kirahisi zaidi kwenye hali ya kisimulizi kuliko kimaandishi. Hivyo
lengo la kuielimisha jamii lilikuwa finyu zaidi. Ni hadithi ambazo ingawa
Mbughuni (1980:93) anadai kuwa serikali za kikoloni zilizichapisha kwa madhumuni
ya kielimu, tukichukulia kuwa waliokuwa na uwezo wa kusoma na kuandika wakati
huo hawakuwa wale wenye amali hiyo bali wageni, zilinuiwa kuwasaidia wageni hao
zaidi kujua maisha ya Mwafrika. Ndio maana hadithi nyingi kati ya hizo
zilipatiwa tafsiri za Kijerumani na ufafanuzi pamoja na maelezo ya ziada.
Maudhui ya hadithi hizi yalikuwa ya kigeni mno kiasi ambacho yangeweza
kuwaelimisha wenyeji mambo ya Uarabuni, kwani nyingi ya hadithi hizo zilikuwa na
misingi ya Kiarabu. Wasomaji wachache waliokuwepo walikuwa na elimu yenye
misingi ya Kiarabu au ile ya Kizungu. Kwa mfano tukiangalia hadithi ya 'Sultan
Majinuni', hadithi hii ilikuwa na habari zinazohusu uvunaji wa tende, uchezaji
karata n.k., vitu ambavyo havikuwa vinahusiana na maisha ya Waafrika.
Hadithi hizo fupi ziliendelea kuwepo chini ya misingi hiyo ya
simulizi hadi kitabu kikubwa cha Habari za Wakilindi kilipochapishwa
(1905-1907). Kitabu hiki kilikuwa na wahusika ambao walikuwa kwenye maisha na
mazingira yanayolingana na yale ya riwaya ya kisasa. Muundo wake na maelezo ya
hadithi hii yalizingatia watu wa mbari za Kisambaa, Kizigua na Kibondei na kama
alivyoeleza zaidi Ohly (1981), ni kitabu kilichoelezea mila na desturi za watu
hawa. Hatua iliyokuwa imepigwa kutoka kwenye mkusanyiko wa hadithi za Steere, na
Velten hadi kufikia kwenye kitabu cha Abdallah Hemed L'Ajjemiy ni kubwa mno kwa
kipindi kifupi hivyo kutoka kwenye mikusanyo ya hadithi fupi hadi kuandika
riwaya hiyo. Kama hatua za namna hiyo zingeendelezwa kwa kasi hiyohiyo huenda
historia ya riwaya ya Kiswahili ingekuwa na sura tofauti na vile
tunavyozungumzia hapa. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, wakoloni wa Kijerumani na
hata baadaye Waingereza, hawakuipa msukumo zaidi historia ya riwaya ya Kiswahili
kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi. Sababu mojawapo inayojitokeza ni ile ya
Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia ambavyo vilizihusisha nchi hizi mbili. Makoloni
yote yalizingatia kupigana na kutetea nchi zao. Sababu nyingine, ambayo pia
inahusiana na hiyo iliyotajwa ni kwamba baada ya vita, Afrika Mashariki
ilitawaliwa na Waingereza. Jitihada na malengo ya Wajerumani kuhusu lugha na
fasihi ya Kiswahili yalifika ukingoni baada ya kuondolewa Tanganyika. Waingereza
walianza kuangalia swala hili kwa upana zaidi, yaani nje ya Tanganyika. Kwa vile
waliitawala Kenya, nchi hizi mbili zilihusishwa zaidi katika uendelezaji wa
Kiswahili.
Katika jitihada za kuendeleza Kiswahili, na kuhusiana na mada
yetu hii, katika kuendeleza riwaya ya Kiswahili, Waingereza walitilia mkazo
hadithi fupi na simulizi nyingine. Hali hii, ambayo ilikuwepo kabla ya kuandikwa
Habari za Wakilindi iliendelea kwa muda mrefu hadi mwaka 1934 kama
tutakavyoona mbele. Jambo la muhimu hapa ni kuwa, pamoja na kipindi hicho cha
kusimama na kurudi nyuma, historia ya riwaya ya Kiswahili ilikuwa imekwishavuka
kiwango cha simulizi za kinjozi na uundaji wa riwaya ulikwisha kamilika mnamo
mwanzoni mwa karne ya ishirini. Hivyo, wakati kipindi cha kwanza katika historia
ya riwaya ya Kiswahili kinaishia mwaka 1910, kipindi cha pili (1910-1920) ni
kipindi ambacho kimeiweka historia hiyo katika hali ya kutosogea. Kipindi cha
tatu, ambacho tutakianzia mwaka 1929 ni kipindi cha kurudinyuma na kusonga
mbele.
Baada ya mwaka 1920 Hellier A.B. na wenzake walianzisha
vijigazeti ambavyo viliandika hadithi tofauti. Hadithi hizi ziliweza kuwafikia
wenyeji wachache ambao walikuwa na ujuzi wa kusoma. Wahariri wa magezeti kama
vile Mambo Leo, mwalimwengu, na mengine machache walitoa hadithi kama
vile 'Kibaraka', 'Sultan Zuwera', 'Asha Binfi Fulani' na nyingine nyingi.
Hadithi hizi ni muhimu sana katika historia ya riwaya ya Kiswahili. Ni hadithi
ambazo ziliwapa waandishi wenyeji nafasi ya kujitokeza katika uandishi wa
hadithi na kujifunza kujieleza kifasihi na kifasaha. Mnamo mwaka 1921 hadithi
kama vile Mwaka katika Minyororo na Tulivyoona na Tulivyofanya
Uingereza viliandikwa na waandishi wenyeji wa mwanzo kama vile Sehoza na
Kayamba. Mnamo mwaka 1934 ndipo James Mbotela alipojitokeza na riwaya yake
maarufu ya Uhuru wa Watumwa. Riwaya hii imekuwa ndio chanzo
kilichojitokeza zaidi cha kukua kwa riwaya ya Kiswahili. Hata hivyo, riwaya hii
haitofautiani sana na kazi za Sehoza na Kayamba kwa upande wa hadhi ya kiriwaya
na muundo wake, licha ya kwamba wahakiki wengine kama vile Shariff (1988)
wanaona kwamba msaada wa wamisionari ulijitokeza sana. Tofauti yake na kazi
nyingine za awali ni kwamba kitabu hiki kilikuzwa sana na wakoloni hasa kwa
sababu mbili. Sababu ya kwanza ambayo inajitokeza kwenye uchunguzi ni kwamba
kilikuwa kitabu ambacho kilionyesha kuwa Mwafrika alikuwa mtu duni na mtumwa
ambaye maisha yake na maendeleo yake yalimtegemea sana mtu mweupe. Ni kitabu
ambacho kimeonyesha jicho la Mwafrika kwa wakati huo kuhusu kutawaliwa na mawazo
yake kuhusu utumwa. Mawazo haya ya mtumwa aliyeachwa huru na kupelekwa
Uingereza, mawazo ambayo kwa kweli yalimdhalilisha Mwafrika na hayaridhishi
yakilinganishwa na historia ya utumwa, yalionyesha zaidi ujinga wa Mwafrika kwa
upande mmoja na kwa upande mwingine shukrani na kujipendekeza kwa mwandishi kwa
Wazungu. Sababu ya pili ni kuwa James Mbotela mwenyewe alikuwa mchungaji wa dini
aliyepata masomo yake chini ya chama cha kanisa la Kikristo. Sababu hizi
zinasaidia kuelewa kwa nini riwaya hii, pamoja na kuwa haikupevuka kisanii,
ilipigiwa parapanda kubwa.
Mnamo mwaka 1929 iliundwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki.
Kamati hii, pamoja na umuhimu wake katika kuiendeleza lugha ya Kiswahili,
ilikuwa na nafasi kubwa mno katika kuendeleza fasihi ya Kiswahili. Katika kamati
hii aliwahi kuwemo mwanafasihi na mwandishi maarufu, hayati Shaaban Robert,
lakini pamoja na hayo, ripoti ya magavana ambayo ilionyesha umuhimu wa kuwa na
Kiswahili katika mashule na kuwa na lugha sanifu ambayo ingetumika katika
kujieleza kifasaha na kifasihi ilikuwa ni ripoti muhimu katika maendeleo na
historia ya riwaya ya Kiswahili. Mojawapo ya mafanikio ya Kamati hii ni
kuanzishwa Shirika la uchapishaji wa riwaya fupi za Kiswahili na kitabu chake
cha mwanzo kilikuwa mwaka 1950, kitabu kilichoitwa Mwarabu na Binti yake.
Waandishi maarufu kama vile Shaaban Robert walijitokeza na kupata msukumo zaidi
baada ya kuanzishwa kamati hii. Mchango wa wachapishaji kama vile Nelson na
Evans Brothers ulichangia sehemu kubwa sana katika kuikuza na kuikomaza riwaya
ya Kiswahili katika kipindi hiki.
Aina ya tatu ni ya Simbamwene. Aina hii ina waandishi wengi
zaidi. Vijitabu vyao ni vidogovidogo, vinavyoonyesha usanii ulioharakishwa,
unaoonyesha mianya ya upungufu wao, hususan wa kisanii hapa na pale na ambavyo
aghalabu maudhui yao yamezibwa kwa wingu la fani kwa kutumia uhodari wa mhusika
mkwezwa katika kutenda yasiyosadikika. Mifano rnizuri ya kuipitia ni
Mpango (1982), Je Kisasi? (1982), Kitanzi (1984),
Kivumbi Uwanjani (1978), n.k. Ni aina hii ya waandishi ambayo imeanzisha
vituo vya kwao (binafsi) vya uchapishaji ili kuchapisha kazi zao ambazo, kwa
kawaida, hazikuwa zikipokelewa na mashirika ya uchapishaji yenye mashiko
kutokana na masuala ya kimaadili na kupwaya kwa fani na maudhui.
Hitimisho
Katika sura hii tumejaribu kuiweka riwaya ya Kiswahili katika
aina kadhaa kadiri ilivyojibainisha katika maendeleo yake hadi kufikia miaka ya
themanini. Hatudai kwamba kujitokeza kwa aina hizo kumekuja kwa kuandamana,
yaani kwa mfuatano maalum. La hasha. Bali kujitokeza huko kumekuja kwa
mchangamano na mwingiliano; ndiyo maana aina moja ya riwaya inaweza kubainisha
baadhi ya sifa za aina nyingine. Hali kadhalika, aina zilizotajwa si Alfa
na Omega (A na Z) ya aina ya riwaya zinazojitokeza katika fasihi ya
Kiswahili, bali haya ni matokeo ya uchunguzi wa maktabani uliofanywa na mtu
mmoja. Jaribio jingine la namna hiyo lingeweza kuonyesha matokeo tofauti, kidogo
au sana, kutegemeana na mkabala wa mchunguzi. Hata hivyo, matokeo yaliyojitokeza
katika sura hii ni kichocheo cha kuweza kuyafikia matokeo mengine, kama vile
Kezilahabi anavyodokeza “....ukweli ukipambanuliwa mwanafalsafa huendelea
kudadisi hadi ule ukweli ukajitanua na kufunua ukweli mwingine”. Aidha
haina maana kuwa mwandishi aliyetokea kuandikia mkondo fulani atabaki kuutumikia
mkondo huo wakati wote. Inawezekana kabisa pakawa na tofauti kama ile
inayojibainisha kwa Abdulla alipouacha kidogo mkondo wa riwaya-pendwa yenye
mawanda ya uhalifu-upelelezi akaandika Mke Mmoja Waume Watatu. Aidha
katika baina ya mikondo iliyojadiliwa imejibainisha kuwa kuna 'kipindi cha
mpito' ambapo mabadiliko ya kifani, kimaudhui na zaidi ya yote, kisanaa,
hujitokeza wakati wote wa maendeleo ya
maisha.