UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
Uhakiki ni kazi au kitendo cha kutafakari,
kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweka bayana maadili na
ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi. Hivyo mhakiki sharti asome kazi ya fasihi
andishi au kusikiliza masimulizi kwa makini ili aweze kuyahakiki
Mhakiki
ni mtu anayejishughulisha na kazi za kisanaa hususan za kifasihi za wasanii
asilia. Mhakiki ni mchambuzi na mfafanuzi wa kazi za kifasihi. Ni jicho la
jamii kwani ndiye agunduaye mazuri yaliyomo katika kazi hiyo, hali kadhali mabaya
(hatari) yaliyopo katika maandishi hayo kwa jamii husika .
Mhakiki
ni bingwa wa kusoma na kuchambua vipengele vya fani na maudhui katika maandishi
ya fashihi. Kwa mantiki hiyo mhakiki ni chombo madhubuti cha jamii inayohusika
cha kuleta maendeleo katika jamii. Kwa kuzingatia haya anawajibika kuwa
mwaminifu, mkweli, asiyeogopa kuweka wazi ubaya uliomo katika maandishi ya
mwandishi asilia, na asiyependelea waandishi Fulani Fulani kwa sababu zisizona
maslahi kwa jamii. Pamoja na hayo uhakiki wa kazi za fasihi unaambatana na mambo
yafuatayo:
(a)Kuisoma kazi ya fasihi kwa makini na kuielewa
(b)Kuchambua vipengele vya fani na maudhui katika
kazi hiyo
(c) Kueleza
ubora na udhaifu wa matumizi ya vipengele vya fani na maudhui katika kazi hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo hayo ni wazikuwa mhakiki
anabeba dhima zifuatazo:
1.Kuchambua na kuweka wazi funzolitolewalo na kazi
ya fasihi.
2. Kuchambua na kufafanua taswira (picha za
kisanii) zilizotumika katika kazi ya mwandishi.
3. Kumshauri
na kumtia moyo mwandishi ili afanye kazi bora zaidi (hivyo mhakiki pia ni mwalimu wa mwandishi)
4. Kumwelekeza
na kumchochea msomaji kusoma na kupata faida zaidi ya ambayo angeipata pasipo dira ya mhakiki
(mhakiki ni mwalimu na daraja kati ya
mwandishi na jamii)
5. Kuhimiza
na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
6. Kukuza
kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi za fasihi.
7. Kutafuta
na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
8. Kuthamini
na kuheshimu kazi za waandishi kwa kuzitendea haki
VIGEZO VYA UHAKIKI
Kwa
kuzingatia kwamba fasihi husawiri jamii katika mfumo mzima wa maisha ya jamiii
hiyo mathalani shughuli zinazofanywa katika jamii husika, basi si budi
kuzingatia yafuatayo katika kupima kazi ya fasihi:
(i) Ukweli
wa mambo yanayoelezwa – mhakiki kama hakimu na daraja atajiuliza, je, ni kweli yaliyoelezwa katika
kazi hiyo yanatendeka? Kama anahakiki habari
kuhusu ubakaji au rushwa – Anapaswa kujiuliza, Je ni kweli mambo hayo yapo katika jamii ya Tanzania?
(ii) Uhalisia
wa watu, mazingira na matukio katika jamii. Hapo mhakiki analinganisha wahusika wa
kazi husika na watu halisi ili kuona kama jamii zungumziwa ina watu
wanaotenda kama wahusika waliotumika. Mfano habari inaeleza kuwa mganga wa kienyeji aliwapaka dawa watoto wakawaona
wachawi, mhakiki anaweza
kujiuliza kama kweli hilo linaweza kutokea katika jamiii husika.
(iii) Umuhimu
wa kazi hiyo kwa jamii husika lazima uzingatiwe. Jambo linalozungumzwa linaweza
kuwa la kweli na linalihalisika lakini lisiwe na umuhimu mkubwa katika jamii
kiasi cha kuvuta utayari wa jamii hiyo.
vigezo
hivi ndivyo vitumikavyo kupimia vipengele vya maudhui,(dhamira, ujumbe,
migogoro, mafunzo na falsafa). Na vipengele vya fani, (muundo, mtindo, matumizi
ya lugha, wahusika, na mandhari)
Kwa mfano;
Hadithi inayosifu maisha ya vijijini na kuwashauri
vijana wasikimbilie mijini, lazima ipimwe kwa kuzingatia ukweli uliopo
vijijini. Mhakiki atajiuliza maswali ya dhamira, mafunzo, migogoro, ujumbe na
falsafa kama haya:- Je, ni kweli kuwa wanavijij wana maisha bora kuliko mjini?
Je, wanavijiji wanahuduma za lazima kama hospitali zenye waganga na dawa? Je,
wanavijiji wana maji salama kwa ajili yao, mifugo na mazao yao? Je, mazao ya
wanavijiji yananunuliwa kwa fedha taslimu na mapema? Je, wanavijiji hawa
bughudhiwi na wezi, waporaji n.k?
Hali
kadhalika mhakikia atajiuliza maswali
kadhaa kuhusu kukimbilia mijii, kwa mfano; Je kijana anapokimbilia mjinii ana
uhakika wa kupata kazi? Je, kazi kama kuuza machungwa au karanga mijini ni
shughuli inayoweza kumkimu huyo kijana? Na Je, vijana wasio na kazi mijini
hawalazimiki kuiba au kufanya uhalifu mwingine?
Hatimaye mhakiki atajiuliza maswali kuhusu
ufumbuzi unaopendekezwa na mwandishi katika kazi yake, mfano tunaozungumzia
mhakiki atajiuliza, je, mwandishi anashauri nini licha ya kusema vijana wabaki
vijijini? Je, ni mambo gani anayopendekeza mwandishi kuhusu kuinua shughuli za
kiuchumi vijijini? Je., suluhu la mwandishi (mapendekezo) linawezekana (ni
yakinifu) au ni la kinjozi tu (la kidhanifu). Msingi wa maswali yote haya ni
kujaribu kutambua ukweli, uhalisi na umuhimu wa kauli za mtunzi.
Katika uhakiki wa fani, vipengele vya fani
huangaliwa jinsi vilivyotumika na kupima usahihi wake kimatumizi, na hapa
maswali huweza kuwa hivi:
-Je, kazi husika ina muundo gani?
-Wahusika wamechorwaje?
-Je, wahusika wanahalisika katika jamii husika?
-Je,mpangilio wa maneno unavutia wahusika?
-Matumizi ya tamathali mbali mbali yanatosheleza
haja?
-Misemo na methali zilizotumika zinafaaa hapo
zilipotumika au zimepachikwa tu?
VIPENGELE VYA FANI NA MAUDHUI KATIKA KAZI ZA
FASIHI ANDISHI:
Riwaya na tamthiliya:
A. Maudhui.
Maudhui
katika kazi ya Fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumziwa pamoja na
mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumlisha mawazo, pamoja na
mafunzo mbali mbali yaliyomsukuma msanii hadi kutunga kazi Fulani ya Fasihi.
Vipengele vya maudhui:
1. Dhamira
Hili
ni wazo kuu au mawazo mbali mbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi ambayo
mwandishi huyajengea hoja. Dhamira hutokana na jamii na zipodhamira kuu na
dhamira ndogo ndogo. Dhamira kuu ni zile za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Dhamira kuu ndicho kiini cha kazi ya fasihi na dhamira ndogondogo ni zile
zinazoambatana na dhamira kuu.
2. Migogoro
Migogoro ni mivutano na misuguano mbali mbali ambayo
huibuliwa na mwandishi katika kazi ya fasihi. Mgogoro kati ya wahusika ama
vikundi vya wahusika, familia zao matabaka yao n.k. Migogoro hii mara nyingi
hujikita katika mahusiano ya kijamii na ndipo tunapata migogoro ya :
(a) kisiasa
(b) kiuchumi
(c) kiutamaduni
(d) kinafsia (kifikra)
3. Ujumbe
na maadili
Ujumbe
katika kazi ya fasihi ni mafunzo mbali mbali yapatikanayo baada ya kuisoma kazi
ya fasihi. Ujumbe huwa sanjari na maadili mbali mbali ambayo mwandishi
amekusudia jamii iyapate.
4. Mtazamo
Ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia
mazingira aliyonayo msanii
mwenyewe. Wasanii wana mitizamo ya aina mbili:
(a)Mtazamo wa kiyakinifu – mtazamo huu ni ule wa
kuyaangalia mambo waziwazi na
kuyaelezea kwa jamii kupitia kazi za kifasihi. Msanii anayeunga mkono mtazamo
huu huutazama ulimwengu au mazingira yanayomzunguka binadamu kisayansi na hivyo
huelezea mambo katika uhalisia wake.
(b) Mtazamo wa kidhanifu – msanii mwenye
mtazamo wa kidhanifu hujadili mambo na kuyatolea masuluhisho yaliyoegemea
katika kudhani tu pasipokuzingatia uhalisia wa mambo. Huchukulia ulimwengu kama
kitukinachobadilika kulingana na matakwa ya Mungu
5. Falsafa:
Huu ni mwelekeo wa imani ya msanii. Msanii anaweza
kuamini kuwa, mwanamke si kiumbe
duni kama wengine wanavyoamini au, kwa wale wapinga usawa, wanaweza kuwa na
falsafa ya kumwona mwanamke kuwa kiumbe duni au chombo cha starehe.
Hivyo
falsafa inatakiwa ichambuliwe kwa kuzingatia jinsi kazi hiyo ilivyoutazama
ulimwengu na kuueleza ukweli juu ya mambo mbali mbali na ukweli huo lazima
uhusishwe na binadamu.
6. Msimamo:
Hii ni hali ya mwandishi kuamua kushikilia na
kutetea jambo Fulani bila
kujali kuwa jambo analolishikilia linakubalika au la.
Misimamo
ya mwandishi huweza kuwekwa katika makundi (kategoria) matatu:
(a)Msimamo wa
kimapinduzi – mwandishi mwenye msimamo huu huyajadili masuala / matatizo
yanayoihusus jamii yake na kuonesha
bayana – mbinu (njia) za kuondokana na matatizo hayo
(b)Msimamo usio wa kimapinduzi, mwandishi mwenye msimamo huu huwa na asili ya
woga inayomfanya kuyajadili mambo kwa kufichaficha na hivyo kushindwa kuleta
athari chanya katika mapinduzi.kutokana na kutoonesha bayana masuluhisho ya
matatizo aliyoyajadili.
7. Mtazamo
Ni jinsi msanii anavyoyatazama mambo katika
ulimwengu wa kifasihi. Hapa tunapata mitazamo ya aina mbili.
(a)
Mtazamo
wa kiyanifu ambao unaegemea katika kuyajadili mambo kiuhalisia, msanii mwenye
mtazamo huu hujadili mambo kama yanavyojitokeza katika jamii. Kwa ujumla
mtazamo huu hushadadiwa sana na wanasayansi ambao huhitaji kuthibitisha kila
kitu kisayansi.
(b)
Mtazamo
wa kidhanifu, huu una misingi yake katika kudhani kuwa Mungu ndiye suluhisho la
kila kitu hivyo waandishi wenye mtazamo huu hujibainisha wazi kupitia kazi zao
hasa kwa kujadili mambo kiujumlajumla mathalani “kuon a kuwa mapenzi bora ndiyo
suluhisho la matatizo katika jamii” huu ni mtazamo wa kidhanifu.Wengi wa
wanadini hufuata mtazamo huu.
B: Fani
Fani katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa
anaoutumia msanii katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii inayohusika.
VIPENGELE VYA FANI
1. Muundo
Ni mgawanyo, mpangilio na mtiririko wa kazi hiyo
kwa upande wa visa na matukio. Ni
jinsi msanii wa kazi ya fasihi alivyoifuma, kuiunda na kuunganisha tukio moja
na lingine, sura moja na nyingine, ubeti na ubeti, na hata mstari wa ubeti na
mwingine.
AINA ZA MIUNDO:
(a) Muundo wa moja kwa moja/msago
Huu ni muundo wa moja kwa moja ambao matukio
huelezwa kwa kuanza la mwanzo hadi la
mwisho. Kwa mfano, mhusika huzaliwa, hukua, huchumbia au huchumbiwa, huoa au huolewa,
huzaa watoto, huzeeka, hufa. Riwaya ya “Kuli”imetumia
muundo huu. Katika riwaya tunamwona Rashidi, akizaliwa, akiwa, anaanza kazi, anaoa, anaanza harakati
za kudai haki za makuli namwisho anafungwa.
(b)
Muundo wa kioo/rejea
Huu ni muundo unaotumia mbinu rejeshi ambayo
huweza ama kumrudisha nyuma
msomaji wa kazi ya fasihi katika mpangilio wa matukio yake au kuipeleka mbele
hadhira ya kazi hiyo. Riwaya ya “Zaka la Damu” imeutmia muundo huu.
(c) Muundo wa rukia
Huu
ni muundo ambao visa na matukio hurukiana. Katika muundo huu kunakuwa na visa
viwili ambavyo hurukiana katika kusimuliwa kwake, na mwisho visa hivi huungana
na kujenga kisa kimoja. Mfano Njama.
2. Mtindo:
Mtindo
katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii huiwasilisha kazi yake kwa
jamii. Ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo
hudokeza upekee wa mwandishi.
Dhima
ya mtindo:
·
Humwezesha msomaji kujua hisia za mwandishi juu
ya aliloliandika.
·
Hudokeza kiasi cha hisia na mwamko wa wahusika
katika hadithi.
·
Kuonesha mtiririko (muwala) wa matukio.
·
Kuumba ulimwengu ambao utabeba maono ya msanii.
Lengo ni kuepusha mifarakano inayoweza kujitokeza. Kwa mfano, katika riwaya ya
“Kusadikika” ambayo imeumbiwa ulimwengu ulioko angani na nchi inayoelea.
Katika mtindo huangaliwa:
-Matumizi ya lugha
-Nafsi zilizotumiwa
-Matumizi ya monolojia (maelezo/ masimulizi) na
dialojia (majibizano).
-Mbinu ya kutumia tanzu nyingine za fasihi
simulizi
-Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi
-Matumizi ya barua n.k.
Jambo la
msingi katika mtindo ni lugha, na ndiyo inayotofautisha fasihi na sanaa
nyingine kama vile uchoraji, uchongaji, usukaji, ufinyazi n.k. Msanii wa fasihi
chombo chake (nyenzo) ni lugha.
3. Wahusika:
Wahusika
ni watu, vitu ama viumbe waliokusudiwa kubeba dhamira mbalimbali kwa lengo la
kuwakilisha tabia za watu katika kazi ya fasihi.
Aina za Wahusika:
(a) Wahusika
Wakuu:
Hawa
ni wale ambao wanajitokeza kila mara katika kazi za fasihi, hutokea tangu
mwanzo hadi mwisho. Wahusika hawa hubeba kiini cha dhamira kuu na maana ya
hadihti yote. Vituko, visa na matendo yote hujengwa kuwahusu au kutokana nao. Mara nyingi jambo hili limewafanya
wahusika wakuu wa kazi ya fasihi wawe “midomo” ya wasanii, na pia vipaza sauti
vya watunzi wa kazi za fasihi. Wahusika wakuu hasa wameelezwa kwa mapana na marefu juu ya maisha na tabia zao
ili kuukamilisha unafsi wao.
(b) Wahusika wadogo / wasaidizi
Hawa hujitokeza hapa na pale katika
kazi ya fasihi ili kuukamilisha ulimwengu wa kazi hiyo. Hawa husaidia kuijenga
dhamira fulani katika kazi ya fasihi na hasa hubeba dhamira ndogo na kwa
minajili hiyo huitwa wahusika wadogo ingawa wakati Fulani husaidia kujenga na
kuikamilisha dhamira kuu.
(c) Wahusika wajenzi:
Hawa ni wahusika ambao wamewekwa ili
kukamilisha dhamira na maudhui Fulani, kuwajenga na kuwakamilisha wahusika
wakuu na wasaidizi. Wahusika wakuu na wadogo huweza kuwekwa katika aina tatu:
(i) Wahusika
Bapa;
Hawa ni wahusika ambao hawwabadiliki kitabia wala kimawazo kulingana na mazingira au
matukio ya wakati wanayokutana nayo. Wahusika bapa huweza kugawanywa kwenye makundi mawili:
Wahusika Bapa – sugu-
Hawa huwa sugu katika hali zote, kiasi kwamba hata
tuwaonapo mahali pengine hali zao ni zile zile, wao ndio huhukumu hushauri na
kuongoza tu na si vinginevyo wanakuwa kama madikteta. Mfano” Bwana Msa” katika
riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale” ya M.s. Abdulla.
Wahusika bapa – vielelezo –
Hawa pamoja na kutobadilika kwao, hupewa majina
aghalabu ya kiishara ambayo – humfanya msomaji aelewe tabia na matendo yao.
Mfano: “Waziri Majivuno”, “Adili”, Utubora” na “Karama” katika kazi za “Shaaban
Robert” ni mfano wa wahusika bapa wala, kiasi ambacho anaondoa sehemu zote za
sifa za wahusika huyo.
(ii) Wahusika
duara / mviringo
Hawa ni wahusika ambao hubadilika kitabia,
kimawazo ama kisaikolojia. Maisha yao hutawaliwa na hali halisi yamaisha. Hivyo
wanavutia zaidi kisanii, kwani husogeza hadithi ielekee kwenye hali ya kutendeka
au kukubalika na jamii.Mfano, (Rose mistika) , Josina (pepo ya mabwege)
(iii) Wahusika
shida / foili
Hawa ni wahusika ambao huandamwa na shida,
misukosuko na taabu na wahusika hawa hutokea kati ya wahusika bapa na duara.
Wahusika shida huwategemea wahusika duara au bapa ili waweze kujengeka. Mfano:
“Najum” katika riwaya y’’ Mzimu wa Watu wa Kale’’ na m.s Abdulla.
4. Matumizi
ya lugha
Lugha ndiyo njia (nyenzo) aitumiayo msanii wa fasihi
kuyaelezea mambo mbali mbali yahusuyo jamii kwa njia ya ubunifu na usanii.
Hivyo lugha ndiyo mzizi wa
kazi ya fasihi na bila yenyewe kuwapo haiwezekani kuwa na fasihi.
Vipengele vya lugha
(i) Methali
Methali ni tungo fupi zenye hekima na
busara ndani yake ambazo hutumika kama kiungo cha lugha kwa lengo la kufunzia
na kupenyeza hekima kwa jamii kupitia
fashi.
Methali pia hutumika kujenga mandhari ya
kiutamaduni ya kuaminika kuhusu jamii itumiayo methali hizo. Hivyo huweza
kusemakuwa pale ambapo methali zimetumika katika kazi mbali mbali za fasihi, nyingi
zimejenga fani na maudhui ya kazi hizo.
(ii) Misemo
na nahau
Matumizi ya misemo na nahau katika kazi za fasihi
hushabihiana sana na yale ya methali.
Misemo na nahau hutumika kwa madhumuni anuai kama vile kutambulisha mazingira,
na wakati husika wa kazi hiyo, lakini pia kupamba kazi ya fasihi pamoja na
kuitajirisha lugha ya msanii katika Kazi yake.
(iii) Tamathali
za semi
Tamathali za usemi ni maneno ambayo hutumiwa na
wasanii wa fasihi ili kutia msisitizo, nguvu na maana katika kazi zao, hali
kadhalika kuboresha mtindo wa kazi zao. Wakati mwingine huwa na lengo la kupamba
kazi ya fasihi na kuongeza utamu wa lugha. Kuna aina nyingi zatamathali za
usemi kama ifuatavyo;
(a)Tamathali za mafumbo
Dhihaka (sarcasm)
Hii ni tamathali ya dharura na ina lengo la
kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi, lakini kwa mbinu ya mafumbo
Mfano:
“Adella alikuwa msichana msafi sana. Ndiyo maana
kila, mara alipata kupaka mafuta yaliyonukia na kukaribisha nzi
walioleta matatizo makubwa”.
Tafsida (Euphemism)
Hii hupunguza ukali wa maneno au utusi katika
usemi
Mfano:
-Kujisaidia au kwenda haja badala ya kunya au
kukojoa.
-Kuaga dunia badala ya kufa n.k
Kejeli / shitizai (Irony)
Hii imekusudiwa kuleta maana iliyo kinyume na ile
iliyokusudiwa ama kinyume na ukweli ulivyo. Lengo lake ni kutaka kuzuia
matatizo na migongano pindi itumikapo kwa lengo maalumu la kufundisha na kuasa.
Mfano:
-Mtu ni mchafu, lakini anaambiwa –sijamwona mtu
msafi kama wewe.
-Mtu ni adui, lakini anambiwa – wewe ni rafiki
mpenzi
-Mtu ni mweusi kama mkaa – anaitwa cheupe.
Kijembe / kiringo (Innuendo)
Huu ni usemi wa mzunguko, ni usemi wa kimafumbo wa
kumsema mtu kwa ubaya.
(b)Tamathali
za mliganisho
Sitiari (Metaphor)
Ni tamathali inayolinganisha matendo, vitu au
tabia ya vitu vyenye maumbile tofauti bila kutumia viunganishi linganishi
Mfano:
-Maisha ni moshi
-Pesa ni maua
-Penzi upepo
-Misitu ni uhai
Tashibiha (simile)
Tamathali inayolinganisha vitu kwa kutumia maneno
kama vile mfano wa, kama, mithili ya , sawa na , n.K
Mfano;
-Ana sauti tamu sawa na ya chiriku
-Ana maringo kama twiga
-Ananyata mithili ya kinyonga
-Ana ng’ang’ania kama kupe.
Tashihisi (personification)
Tamathali hii huvipa vitu sifa walizonazo binadamu
(hupewa uwezo walionao binadamu)
Mfano:
-Mvua iliponyesha misitu ilipiga makofi
-Mawimbi yalitabasamu kwa upepo wa kusi.
Lakabu
Katika tamathali hii uhusiano wa maneno mawili
kisarufi hugeuzwa na pengine huwekwa kinyume na taratibu za kisarufi zilivyo
Mfano:
-Baridi kali ilimkaribisha (lakini mtu ndiye
mwenye uwezo wa kukaribisha)
-Giza liliwapokea walipokuwa wakiingia pangoni
(c)Tamathali za msisitizo na
nyinginezo
Mubaalagha (Hyperbole)
Hii hutia chumvi kuhusu uwezo wa viumbe, tabia zao
na hata sifa zao kwa madhumuni ya kuchekesha au kusisitiza
Mfano:
-Loo! Hebu muangalie mrembo yule! Ana mlima wa
kiuno
-Tulimlilia Nyerere hadi kukawa na bahari ya
machozi
-Mrembo yule hubeba kila aina ya silaha na huwatia
wazimu wanaume wote anaokutana nao.
Taashira / metonumia
(metonymy)
Katika tamathali hii jina la sehemu ya kitu kimoja
au la kitu kidogo kinachohusiana na kingine kikubwa hutumiwa kuwakilisha kitu
kamili.
Mfano:
-Jembe huwakilisha mkulima
-Kutabasamu huwakilisha furaha
-Mvi huwakilisha uzee
-Kalamu huwakilisha mwanafunzi / msomi.
Majazi
Hii ni aina ya sitiari ambayo itajapo sehemu tu ya
kitu hapo hapo sehemu hiyo huashiria na kuwakilisha kitu hicho.
Mfano:
Roho – mtu
-Masikini, ajali ile ilipoteza roho tano hapo
hapo]
Taniaba (Antonomasia)
Hii ni tamathali ambayo kwayo jina la mtu binafsi
hutumiwa kwa watu wengine wenye tabia, mwenendo, hali au kazi sawa na ya mtu
huyo.
Mfano:
-Yesu – mkombozi
-Yesu wa kwanza wa Afrika alikuwa Kwame Nkrumah
-Nyerere alikuwa Yesu wa kwanza Tanzania
Tabaini (antithesis)
Hii ni usemi unaosisitiza jambo kwa kutumia maneno
ya ukinzani (unyume)
Mfano:
-Mwanadamu hupanga Mungu hupanga
-Amekuwa mrefu si mrefu, mfupi si mfupi ni wa
kadiri
-Usimwamini mtu, yu acheka machoni, rohoni ana
mabaya.
(d)Mbinu
nyingine za kisanaa
Takriri (Tautology)
Hapa yanakuwepo marudio kwenye sentensi au kwenye
usemi na lengo ni kusisitiza
Mfano:
-Dunia ni ngumu jamani, ni ngumu
-Haba na hapa hujaza kibaba
Mdokezo (Aposiopesis)
Hapa msemaji au mwandishi hukatiza maneno au
huacha maneno bila kutaja kitu au maneno ambayo kwa kawaida ni wazi na huweza kujazwa kwa ubunifu.
Mfano:
-Ally alipokuwa analia alisema………………
-Watu wengi huambukizwa ukimwi kwa kushiriki
………………
Tashtiti (Rhetorical
Questions)
Ni mbinu ya kuuliza maswali kwa jambo ambalo
majibu yake yanafahamika.
Mfano:
-Asha na uzuri wake amekufa?
-Loo! Asha ametutoka?
-Hatakuwa nasi tena?
Nidaa (!)
Huu ni msemo unaoonesha kushangazwa na jambo Fulani.
Msemo huu huambatana na alama ya kushangaa
Mfano:
-Baba ndiye amefariki!
-Ah! Havijawa nimekutoroka!
-Hakika nitakupenda!
Mjalizo (Asyndeton)
Hapa huwa ni mfuatano tu wa maneno yasiyo na
viunganishi vyovyote bali hutengwa kwa alama ya mkato(,)
Mfano:
-Nilikaa, nikasubiri, nikachoka
-Nilipanda, nikapalilia, nikavuna, nikauza,
nikajenga nyumba.
Tanakali sauti (onomatopeia)
Ni mbinu ya kuiga sauti za milio mbali mbali.
Milio hii ni ya wanyama, magari, vitu n.k
Mfano:
-Alitumbukia majini chubwi!
-Alidondoka chini pu!
(e) Taswira
Ni
picha zinazojitokeza ndani ya mawazo ya msomaji au msikilizaji wa kazi ya
fasihi. Matumizi mazuri ya taswira na ishara hutegemea ufundi wa yanayomzunguka
yeye na jamii yake pamoja na historia za maisha azijuazo.
Aina za Taswira
(i)Taswira za hisi
Taswira
hupenyeza hisia na kuzigandisha akilini mwa msomaji au msikilizaji na kunasisha
ujumbe wa mwandishi. Taswira hizi hushughulikia hisi za ndani, na kuweza
kumfanya msomaji au msikilizaji awe na wasi wasi aone woga, apandwe na hasira,
ahisi kinyaa, n.k
mfano:
Akadharau! Siwezi kula chakula kama hicho!
Rojorojo nyororo kama limbwata, mfano wa kohozi lenye pumu,liingie katika koo
langu lililozoea kuku wa mrija
-Maelezo hayo humfanya mtu akinahi na kutaka kutapika
mara akisoma rojorojo, kunyororoka mfano wa kohozi lenye pumu.
(ii)taswira za mawazo / kufikirika
Hizi zinatokana na mawazo yahusuyo mambo
yasiyoweza kuthibitika. Mambo kama
kifo, pendo, uchungu, fahamu, sahau, raha n.k
Mfano:
Kifo umefanya nini? Umeninyang’anya penzi langu
bila huruma? kumbuka, nilimpenda
nikapoteza fahamu, kifo ukazidi kunidunga sindano ya makiwa?
(iii) Taswira
zionekanazo
Hizi ni picha ambazo hujengwa kwa kutumia
vielelezo tunavyovijua vile vinavyofahamika katika maisha ya kila siku.
Mfano:
Dakika haikupita mijusi wawili wliokuwa
wamebebana walipita haraka. Midomo yao ilikuwa myekundu. Ghafla walikutana nanyoka
aliyeonekana mnene tumboni. Hapana shaka alikuwa amemeza mnyama.
5.Mandhari / mazingira
Ni sehemu ambamo kazi ya fasihi inafanyika.
Mandhari yaweza kuwa ya kubuni kama” Kusadikika” na “Kufikirika” au halisi (ya
kweli) mfano mandhari ya Dar es salaam, Arusha n.k. kwa Tanzania.
6 Jina lakitabu / Jalada la kitabu
Hapo
tunaoanisha jina la kitabu na yaliyoelezwa ndani ya kitabu hicho. Mfano”Kiu ya Haki”, jina hili linasadifu
vipi yaliyomo ndani ya riwaya hiyo. Je, kweli yaliyoelezewa yanadhihirisha kiu
ya haki? Pia tunaangalia picha mbali mbali
zilizochorwa juu ya jalada la kitabu na kutafsiri kifasihi jinsi picha hizo
zilivyotumika.
7.Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi kifani na
kimaudhui
Hapa tunaangalia ubora na udhaifu wa mwandishi
kifani na kimaudhui katika kazi husika. Hapa vipengele vya fani na maudhui
huzingatiwa kwa kina ili kuweza kupima umadhubuti wa kazi hiyo na hatimaye
kuamua kwa haki kama mwandishi amefaulu au la
NB: Rejea vipengele vya fani na maudhui
Soma hadithi ifuatayo kisha ikifuatiwa na uhakiki
wake
Sadiki Ukipenda
Kuna mengi – mengi yaliyonivutia kwa Mzee
Siwa hata niikaungana naye. Kwanza, ukweli wake. Kwake, neno ni deni kubwa
kuliko deni la fedha. Pili, ushujaa wake. Penye haki husimama kidete bila ya
kututetereka wala kuwa na hofu ya mtu yeyote; mkubwa au mdogo. Tatu, imani
yake, hasa kwangu – daima alikuwa tayari kugawa
mafungu chochote alichokuwa nacho, ijapokuwa ndicho hichohicho . Nne,
uhodari na ukakamavu wake wa kazi. Shamba lake ndilo lililokuwa kubwa kuliko
shamba la kijan ayeyote pale kijijini petu. Sikwambii wazee ambao daima
walistahabu kukaa kwenye mabao mikahawani kupiga domo.
“Katu,”
alikataa Mzee Siwa sirisiri, “sitokokonea uchochole wa sina sina ‘ni,
nikiulizwa siungami!”
Miongoni
mwa yote yale, nilihusudu kumsikia akisema. Ulimi wake daima ni nasaha. Kichwa
chake ni maarifa. Shauri lake ni busara na mwongozo wake ni mwangaza katika
maisha. Hasa kwa kijana kama mimi, ninayezikabili telezi za ulimwengu;
ninayepapasa kama kipofu kwenye njia mbaya ya hatari katika kutafuta yale
yanayoitwa maisha; njia ambayo vijana wengi huipita wakipambana na vikwazo vya
choyo, wivu, jitimai na msiba kwa jumla. Hakika ubongo wa Mzee Siwa ukifanya
kazi kwa njia ya ajabu. Hata wakati mwingine nilishindwa kuelewa aliwezaje
kutambua siri nyingi na jinsi gani aliweza kupambanua vitendawili vigumu ilhali
hata shule haijui
Kwa
kuwa binadamu asingalikosa ila, ila Mzee Siwa, kama ni ila, alijitenga makusudi
na wazee wengine wa kijijini na hakuficha kuwaambia kwa nini. Kama alivyo, mtu
wa nipe n’kupe, alikuwa akisema kinywa
kipana
“Mimi
na nyinyi tofauti. Mimi naishi leo na kesho, nyinyi mnaishi miaka mia moja
nyuma. Vipi tutangamana?” Tabia yake hiyo ya kutoweza kuzizuia akichokozwa
kweli chungu wenzake basi wamefarakana naye na kumpagaza jina la Mjuaji! Na
wengine Mchawi!
Lakini
si mimi. Mimi namjua kuwa ni mzee anayethamini ut kwa hivyo, asingaliweza
kuwa mchawa. Na baada ya kutokea kadhia
hiininayoieleza, ndiyo kabisa nimesadiki kuwa yeye si mchawi, na kwa kweli siku
zote hizi yeye amekuwa dhidi ya uchawi Adhuhuri. Jua linaatilisha kila kitu
kilichothubutu kupita kwenye uwazi wa dunia. Mbinu zimetakatika samawati, baada
ya mawingu kukimbia ukali wa jua. Ila, muda hata muda, kipepo mwanana
kilijitahidi kuzimua vuke la joto lililoning’inia angani. Ng’ombe walikuwa
wamejilalia malishoni kw auzito na machofu, wakichakua mabaki ya matafuno
vinywani mwao. Muda hata muda zilisikika ‘baa’ zao zikikata hewa. Kunguru tu
ndio walikuwa wameshughulika kwenye wakati hu wa dhiki. Kunguru hachoki mpaka
jua litue.
Na
mimi nilikuwa wa miongoni mwa kunguru. Mmbioni nilikuwa ingawa mbio zangu
hazikuambulia kitu cha maana, ila kumeza hewa. Ninapokuwa katika udhia na
kusaili mlolongo wa mambo na matukio yaliyotufumaniza sisi vijana na wazee bila
ya kup[ata fasili yoyote, huishia kwenda kwa mzee Siwa. Nilihisi kila siku
alikuwa na majibu ya masuala yangu ingawa wakati mwingine hayakuniridhisha
kumpa siri zangu. Hata kuliko baba’angu!
Leo
kwake alikuwa hayupo. Nilijua alikuwa wapi lakini, niliteremka bondeni, kondeni
kwake. Nikamkuta ameshamaliza kupalilia. Sasa akawaanakwangura jembe lililokuwa
limegandia tope. Baadaye akalisuuza kwa maji yaliyopita kwenye kijito
kilichotiririka mbele ya kibanda chake.
Baada
ya kwisha kumwamkia alinilaumu – “He, huonekani babu? Umeadimika kama wali wa
daku? Nilikuwa nikikuwaza moyoni sasa hivi, nikawa n’nasema, mbona Mussa
simwoni siku hizi? Nikajiambia, kama leo
hukuja nyumbani, basi nitajilazimisha kukufuata mimi. Nina jambo muhimu sana
nataka kukukwambia.” Sauti lake lilelile la kawaida kavu, zito!
“Salama
lakini?” nilimwuliza kwa wasiwasi.
“Salama
kama si salama,” alinijibu kwa mkato.
“He!
Kuna nini tena?” moyo ulianza kunipapa. Nilitabaruki.
Kilikuwa
kizungumkuti. Mara salama kama si salama, na kasha salama tu usiogope …. Lakini
ni kawaida yake mzee huyu. Mambo yake kinyumenyume! Yale yangu nilikwenda kwake
yalivia kwanza.
“N’ache
nisali kwanza …..je, wewe umeshasali adhuhuri? Au tutasali pamoja?”
ilinibidi
kutoa dharura ya uongo, maana Mzee Siwa kila siku alinihimiza kutekeleza
faradhi ya sala.”Nguo zangu hazina udhu. Nitasali nikifika nyumbani.”
Nikamwacha
akitawadha. Na mi’ nikavuta kumbi nikakaa kwa kuegemea nguzo ya kibanda.
Nikamwangalia alivyoliwa akijitayarisha kumkabili Mungu wake huku moyo wangu
ukinisimanga. Sijui kwa nini, lakini kutazama mzee huyu akijitia udhu
kujitayarisha kusali, kulinijaza amani moyoni. Katika hali ya kawaida sijapata
kuwa na amani yoyote moyoni mwangu! Kwa kweli wakati pekeemimi ninapopata nafuu
na pumziko namna hii ni wakati kama huu wa kutawadha na kumkabili muumba wa
vyote.
Mzee
Siwa alitia maji birikani, akanuilia kuvikosha viungo vya mwili wake
vilivyofuradhiwa na vilivyosumiwa. Kasha akapachua msala. Nao ulikuwa wa kuti
kumba lililosukwa mahsusi kwa kazi hiyo. Aaaa, alikuwa vyako mwenyewe,
kunyanyua kuti la kumba , kasha kurukuu na kusujudu. Ah, ukifikiri haya, utaona
vipi ilivyo vigumu kukutana na binadamu mwenzako. Ati uvae tai, suti, viatu vya
njuti, au kama mwanamke ujipure na kujipondoa, na kujirashia mafuta mazuri ……..
na papo mwanadamu atakupokea kwa jeuri!
Alipokwisha
kupiga rakaa zake nne na mbili za suna, alibaki palepale penye msala wake wa
kuti la kumba, akawa amenigeukia mimi badala ya kutazama kibla. Kwa muda
alinipuuza, akawa anamung’unya midomo akimaliza dua na myuradi.
Hapo
nikapata fursa ya kumwangalia kw akaribu. Ni mzee mwenye umri wa miaka sitini
na tano hivi; lakini amewapiku walioko kwenye arobaini na tano: kakacha,
kakamaa, mzima kama chuma! Damu ya siha bado inamwenda vizuri chini ya ngozi
yake nyeusi kama jongoo. Macho yake makubwa na makali; na mpaka sasa anajivunia
nayo kwmba anaweza kutunga uzi sindano anapotia viua kofia yake. Hakuhitajia
miwani au msaada wa mwana wa yeyote! Au pale alipotaka kujitoa kepu (ambao siku
hizi wamerejea tena katika janibu hii baada ya kupotea miaka thelathini
iliyopita). Alipotoa chepu kamwe hakumvalia miwani, alichukua mwiba tu na kama
mchezo, punje ya mtama ya chepu ilikuwa chini. Wazee wengi kama yeye ilibidi
watolewe chepu na cijana hata kama walivaa miwani.
Kichwani
mvi zilihesabika. Pua yake, midomo yake, masikio na kidevu, vyote bado
havijaporomoka; na mashavu hayajashobwekea ndani. Mikono yake bado ilimruhusu
kukamata jembe mchana kutwa, na wala mgongo wake haukukataa kuinama na
alipoinuka alikuwa kama hakuinama. Mwenyewe alipenda kujiboda,”Nyinyi vijana wa
siku hizi mmeubwa kwa mchanga. Sisi kwa udongo wa wa kinamu – ‘fa mchezo dongo
la kinamu!” Ukweli ni kwamba, kazi ya ubaharia aliyoifanya kwa muda mrefu wa
maisha yake iliufanya mwili wake ushibe upepo wa pwani ulioilinda siha yake. Na
zaidi, Mzee Siwa alipenda kujitunza tokea alipokuwa kijana. Ni hakika kwamba
mpaka leo hajan’goa hata jino moja!
Alinuka,
akachukua kijaluba chake cha uraibu – kipande cha jani la uambuu, chengachenga
za popoo, dole la chokaa akalirambisha juu yake, tumbaku kidogo, mvuato ukawa
tayari. Aliukunja vyema uraibu wake, kasha akautumbukiza kinywani.
Muda!
Halafu: “N’ambie…” maneno yake yalitoka ndani ya sshata la uraibu. Macho yake
yamenitunga sawasawa; “n’ambie,” aliemdelea, “kuwa m’talokwambia hapa leo,
litakuwa baina ya mimi,” alijielekeza kidogo cha sahada, “na wewe….” Akanielekeza
na mimi hichohicho kidole cha shahada.
“Ha…hakuna
si…si…siku n’liyotoa siri yako nje,” nilibabaika na kujibu. Mzee Siwa hajapata
kutoniamini hata siku moja, leo kimezidi nini?
Alitazama
huku na huku mule mwenye machaka ya Mungu, kasha akaweka panda ya kidole chake
cha shahada na kati kutema mate mekundu ya tambuu. Kasha alisogeza mwili wake
karibu yangu na kunong’ona, “Mussa, Mussa babu ……unatakiwa!” Kauli hiyo
sikuifahamu.
“Natakiwa?
……Natakiwa na nani?” nilimwuliza.
Mzee
Siwa hakujibu kitu kwa muda. Akawa anaimung’unya midomo wile alivyokuwa
akivuata uraibu. Kisaha akabatuka maneno bila ya kunitazama.
“Baba’ako”,
alionyesha wasiwasi kidogo; wasiwasi uliochanganyika na haya.
“Baba’angu!”
Nilishangaa “Ananitaka wapi? …..Na kama ananitaka mbona hajaniita kunieleza
alilonalo?”
Kwa
hakikaneno unatakiwa lilikuwa na utata Fulani. Sikujua ni maana ipi mzee huyu
aliyokuwa kakusudia. Mimio nilijibu nilivyolichukulia mwenyewe.
“Ati!”
alitema tena mate ya uraibu. “Sivyo kutakiwa hivyo unavyodhani wewe.”
“Vipi
basi?” niliuliza kwa mkato. Nimezidi kuemewa na moyo ukanijaa wahaka.
Nilihisisiifahamu lugha ya kiswahili kamwe, ama labda ulimwengu umejaa miujiza.
“Anataka
akutoe kikoa!” Mzee Siwa alisema hivyo huku akijaribu kutazama tena kule
machakani, haloafu kwa sauti ya chini aliendelea, “Baba ‘ako ni mchawi. Na sasa
anadaiwa mwana. Na ye’ kawaambia wachawi wenzie yu tayari yeyote kati ya ndugu
zako, ila si wewe. Lakini wenzake wamekataa. Wanataka sharti wewe, maana wewe
ni msomi; na wasomi wana hatari! Kila siku wanatafuna na kuuma!”
moyo
ulinibakuka Mussa. Baba’andu! Baba’angu mchawi! Kumbe kweli wasemayo
watu; ‘kikulacho kinguonimo.’ Lakini
a-a bado siamini. Baba’angu si mchawi kwa mara ya mwanzo, sitaamini analosema
Mzee Siwa.
“Mengi
umenambi Mzee Siwa na nimeyaamini, ila hili!”
“Haaa,”
alicheka kwa kicheko cha ghafla, “uchawi
upo, sadiki ukipenda,” aliendelea, “na tena usidharau hata jambo moja
katika yale niliyokwambia au utapoteza maisha yako. Na kama
unataka….”alinihakikishia,”mimi nitakuthibitishia ukweli wa maneno yangu …….”
alisita hapo, akawa anaramba dari na sakafu ya kinywa chake kugandua masalio ya
uraibu yaliyoganda. Muda ukapita. Kisha….
“Kesho
kutwwa,” aliendelea , “usiku wa manane, utakuja kutolewa. Mimi nitakupa kago la
kujikinga usipatikane. Kago pia litakupa macho ya kuwafedhehi wachawi. Na hata
kama utakuwa tayari kumdhuru baba’ako pia utaweza. Sema tu, unataka vipi? Naona
hawa wachawi watatumalizia watoto na vijana. Tutakuja kuuguzwa na kuzikwa na
nani?”
sikuwa
na la kusema ilikuwa uzito kuamini yote na kutenda pia. Lakini kudharau
sikuweza, kwa vile ninavyomjua Mzee Siwa, si mtu wa kusema uongo. Bila ya shaka
nilikuwa na masuala mengi ya kumwuliza, lakini nilihisi huo haukuwa wakati
wake.
“Ni
tayari,” nilijibu bila ya kufikiri huku nimetokwa na hisia yoyote kwa
baba’angu. Nilikuwa kama jiwe! Jambo moja lakini lilinitia moyo mpango wangu wa
kutoka nje ulielekkea kufanikiwa. Nilikuja kwa mzeeSiwa kumwambia hayo kwa
kweli, lakini yeye alinifumaniza na yake. Hata hivyo sasa nilimweleza na yeye
akakubakiana na mimi kwamba hilo lilikuwa jambo la busara, maana wachawi
hawatasita kujaribu tena na tena kuniondoa duniani.
“Baba
twen’zetu, niachie mimi nitayatengeneza yote,” alinihakikishia Mzeealitwaa
shepeo lake, akalivaa. Akaweka jembe lake begani, akatia chupa ya maji ya
kunywa kapuni mwake na kunikabidhi mimi. Tukatoka
Mzee Siwa alifanya wajibu wake. Dawa ya mizizi Fulani alinipa kuchemsha
na kunywa. Nyingine alinitaka niifukie kwenye kizingiti changu cha chumba. Pia
akanipa hirizi kubwa kuifunga mkono wa kulia. Akaniongezea kago nyingine kadha
ambazo nilizitekeleza. Sikupuuza agizo lake hata moja. Basi siku ilipofika,
nililala kitandani kungojea matokeo. Nusu nina imani, nusu naona haiwezi kuwa.
Kwa kweli nilijaa woga na sikuwa na roho. Saa ya msikitini ikagonga.
Nikaihesabu milio minane. Moyo wangu ukagutuka. Ukapiga mishindo zaidi kuliko
ile ya saa. Nikaanzaa kugwaya na kutetemeka. Damu ikaniruka. Baridi kali
ikanijia sijui kutoka wapi, ikanigandama ingawa chumbani mlikuwa na joto! Nilijua
leo ni leo, asemaye kesho mwongo. Kanibidi kupiga moyo konde na kusema, kufa au
kupona.
Mara nikaona ukuta
wangu wa chumba mkono wa kulia ukipasuka! Mbio, mbio, mbio nilitoka nje,
nikakimbia chini ya mbuyu. Kazi ya kwanza niliyoagizwa na mzee Siwa imekwisha.
Na’mi nikajihisi kama maiti niliyefufuka! Sikujiweza kwa jitimai na hofu. Naam,
alikuwa baba’angu! Niliyakumbuka maneno ya mzee Siwa; “Usipite ukuta wa kulia
utakaopasuliwa na baba’ko. Pasua ukuta wa kushoto kwa mundu. Na ‘mi nikafuata
hivyo hicyo.
Muda si mrefu
nilimwona baba’angu akitoka ndani ya chumba changu akimwongoza mtu aliyedhani
alikuwa ni mimi. Kumbe lilikuwa chege la mgomba ambalo kwa mazingaombwe ya Mzee
Siwa, limegeuzika mtu mwenye wasifu wangu. Wachawi wamekutana na mganguzi wa
uchawi! Basi nikamwandama baba’angu na lile zuzu lake. Mimi niliweza kuwaona,
lakini wao hawakuweza kuniona. Madawa yalikuwa yamenifunganimefungika. Hakukuwa
na uchawi ulioweza kuniingia. Walikwenda kitambo kirefu. Hatimaye wakafika
pahala penye uwanda ambapo watu wengi walikuwa wamekusanyika. Ilikuwa jumuia ya
wachawi. Wotewalikuwa uchi kama walivyozaliwa. Hawana haya. Nilimeza funda moto
na chungu la mate. Wale wachawi wenzake walipomwona baba’angu anaingilizana na
ng’ombe au zuzu lake walipayukwa kwa furaha na shangwe, na hapohapo ugoma
ukadudwa:
Chakatu chakatu, mahepe
Mtoto wa Kware, mlete!
Kware we Kware, mlete!
Kware
alikuwa baba’angu ambaye alionyesha kuchanua upeo wa furaha katika shamrashamra
hizo. Na ‘mi nikajongea karibu. Nikasadikisha umadhuburi wa kago la mzee Siwa.
Hakuna aliyeniona, ila mimi niliwaona wote waliokuwepo. Wengine niliowajua
hawakunishangaza , niliwahi kuwasikia watu wakiwataja kuwa wamo uchawini.
Lakini wengine walinishangaza. Walikuwa watu wa desturi niliodhani walikuwa
wapole, wacha Mungu na wasiopenda kumdhulumu mtu yeyote. Baba’angu akaingia
ngomani akimchezesha mwari wake kwa nguvu. Ngoma ilikuwa ya kukobeana na
kupeana uchawi – kike kwa kiume, mpata maptae. Nao ugoma uliendelea kwa muda
mrefu. Harafu ukasita ghafla! Sauti ya sheha wetu wa kijiji, mzee Mfaki kombo,
kinying’inya cha marehemu Bikirembwe, malkia wa wachawi, ilisikika ikpasua
ukimya wa usiku wa manane. Ilikuwa sauti ya hotuba fupi kimafumbofumbo,
iliyoeleza ya makusanyiko ule
“Bwana Kware ameleta changi yake.
Kupeana ni kikoa, toa na we’ upewe. Mla kuku w wenziwe, miguu humwelekea.
Ametoa mwanawe msomi anayemwonea uchungu zaidi. Na wasomi wanatuletea nini ila
balaa! Kware amethamini kilinge cha uchawini. Taireni wazee, musimwandame tena.
Na tokea sasa, Mussa mwanawe ni ng’ombe wetu; tumchezeni, tumpigeni,
tumchinjeni…”
ugoma ukadudwa tena. Nyimbo ya
safari hii ilikuwa:
Nasikia parakacha miembeni;
Kma
mshambiginya mleteni!
Huku
wakicheza ugoma, walilipiga lile Mussa zuzu. Lo! Hatari kumbe kupigwa uchawini!
Sijui ningekuwaje kama yule aliyekuwa akipigwa alikuwa mimi kweli. Nadhani
dhoruba mbili tu zingetosha kunitupa chini, maiti mkavu! Magongo, marungu,
mawe, mapanga, walilitwanga nalo zuzu. Furaha vicheko vifijo huku wakicheza kwa
hesabu. Walioona Wasahili. Hatimaye sheba, sheba wa kijiji chetu na uchawi,
alisitisha ugoma na hujuma
“Basi
tena, kesho ‘uyo. Kware, mrejeshe mwana. Kesho kutwa tutakuja mchukua kwa
shangwe kubwa zaidi, kesho kutwa tukapokuja kukuekea chege uzike na sisi utupe
mtoto tumle…”
Ole wao! Wameondokea patupu leo kwa
mara ya mwanzo. Hawana habari kuwa mara hii, udhalimu wao haukufua dafu. Mbinu
walizotaka kutumia wao, tumeshazitumia sisi. Mzee Siwa kawacheza!
Basi ikabaki kazi ya mwisho na ‘mi
sikusita, niliitekeleza. Ilinijia sauti ya Mzee Siwa tena …..Atakapokuwa
akilirejesha hilo
change la zuzu walilolipiga mfuate baba’ko mundu wako. Ukifika mlangoni pako tu
mpige dafran moja, moja tu usizidi…..ukizidisha! umekwisha ! nikamwandama.
Usiku ulikuwa na kimya cha ajabu- isipokuwa mara mojamoja, budi alibutia kama vile akiwazomea wachawi kwa uhasidi wao. Shaari
ilizuia hata miti kunong’ona na mazingira yote yalijaa kitisho. Ulikuwa usiku
wa kuogofya! Na sasa nikahisi ubaridi wa alfajiri ukinyotoa maungoni na ndani
ya nafsi yangu mkachimbuka hasira na chuki.sikuwaza kingine ila kisasi .hata kama yule niliye kuwa nikimfuata kumdhuru
alikuwa baba’angu.baba aliyetaka kuitoa roho ya mwanawe.
Alipofika mlangoni tu nilimrushia mundu wa kichwa. Mmoja tu!
Alipiga usiyahi mkali, lakini hakutoka
damu! Kasha alinijia kwa kilio cha
huzuni na kuniambia,’unaona sijatoka damu,nipige tena nife,mimi sistahiki
kuishi kwa nilivyokutendea….’
Niliyakumbuka
maneno ya mzee siwa..,ukizidisha umekwisha!;sikumsikiliza;la kwa haraka za
ajabu nilifunga mlango wa chumba changu na kupanda kitandani pangu.sikupata
usingizi kamwe jimbi la saa kumi za alfajiri
liliwika.niliinuka nikatawadha na kusali.nikaomba mungu anihifadhi na
kunizidishia maisha marefu. Kasha nilirudi kitandani na kujaribu kufumba macho.
Ng’o; usingizi haukuja. Nafsi yangu nzima ilizongwa na mawazo matupu! Huendaje
kufikia hivi dunia, mtu na mwanawe kuhujumiana? Ama kweli imani imekwisha. Hii
ni aheri dunia!
Asubuhi
nilipoangalia chumba changu, nilikuta kuta zote nzima. Nje, lile chege la
mgomba wachawi walilodhania ni Mussa, lilikuwa limelala mbele ya mlango – chege
la mgomba si mtu tena! Nilikuwa nina hakika sasa kwamba baba’angu atalala
hivyohivyo si muda mrefu. Na kweli, saa sita za mchana baba’angu aliiaga dunia,
akaniachia maisha yangu aliyotaka ni mwachie yeye. Kila mtu alishangazwa na
kifo chake, na kama kawaida kila mtu alisema vyake. Baaadhi walisema kapigwa na
wachawi wenzake kwa kushindwa kunitoa mimi. Wengine walisema karogwa na ndugu
zake waliomwekea kisasi kwa kuwaulia watoto wao. Hapana aliyejua sababu ya kifo
chake ila mimi na Mzee Siwa na labda wachawi wenzake waliotushuku sisi.
Na
jkwa hayo msinilaumu. Nakwambieni roho tamu; na penye ukatili wa kulana roho,
msiione ajabu mtu kutetea roho yake. Kisa mkasa! Zaidi ninafuraha kubwa. Hapo
nilipo nimo melini nikisafiri kuona ulimwengu mwingine. Wangu umenishinda kwa
muda. Ningependa kurudi pale nitakapokuwa mtu kamili nitakayekuwa huru mimi na
roho yangu. Nitakapoweza kusema hii ni nchi aliyoniachia baba’angu aliyejaribu
kuniua. Na si kuwa peke yangu niliyekuwa na mori huo – nilipoingia melini
niligundua vijana wengi kama mimi wamo humo. Wengine hata hawajui wanaelekea
wapi, lakini wanajua wanakotoka. Na wala hawajuti kwa nini wameondoka kwao,
ingawa hawana uhakika na wanakokwenda. Sijui kutatokezea nini katika dunia hii?
Na wengine walinihadithia kwamba wenzetu wengi wako nje wameshatangulia.
Wengine wameshaukata wengine wanahangaika naq kubuga na njia. Heri ya hayo
wanasema. Huzuni yangu kubwa ilikuwa tu kumwacha mtu kama Mzee Siwa – mtu adimu,
au unasemaje? Lakini Mzee Siwa anaweza
kuyamudu maisha ya pahala popote; hata motoni! Aliniambia hivyo, na akataka
n’ende na dunia yangu! Ati siku zake zimekwisha na zangu ndio kwanza zinaanza!
Katika kazi ya fasihi inafananishwa
na chombo cha chakula na maudhui kama chakula ndani ya chombo na msanii ndiye
mpishi, chombo kikiwa kibovu au kichafu chakula nacho chaweza kuwa kibovu hivyo
kushindwa kuliwa. Hivyo basi msanii analazimika kulia kikisha chombo na chakula
vinakuwa safi. Hata hivyo tunaweza kufananisha fani na maudhui kama pande mbili
za shilingi ambazo haziwezi kutenanishwa.
Katika hadithi hii
ya “Sadiki Ukipenda” iliyoandikwa na Said A. Mohamed tutaenda kuangalia
maudhui, fani na dhana zake pia tutaona nafsi ya hadithi hii katika fasihi ya
kiswahili ya majaribio.
Maudhui, haya ni jumla ya mawazo
yote au ujumbe uliomo ndani ya haduthi hii au ndani ya kazi yoyote ya kifasihi.
“Ni jumla ya mambo
yote yanayozungumziwa katika KAZI YA KIFASIHI”
Dhana hii inaundwa na dhamira, ujumbe falsafa,
migogoro na itikadi.
` Dhamira
kuu katika hadithi hii ni ujenzi wa jamii mpya, jamii ambayo itakuwa safi bila
kuwa na dhuluma, uvivu, na watenda maovu, bali iwe na viongozi waleta
maendeleo, wazalendo, wenye mapenzi ya dhati kwa jamii yao na wachapa kazi.
Dhamira hii inaundwa na dhamira ndogondogo kama
ifuatavyo
Umuhimu
na kufanya kazi, Msanii “Said A. Mohamed” ameweza kuonesha wanajamii hasa wazee
na vijana wanavyoshindwa kufanya kazi bali kukaa mikahawani kucheza bao tu
katika hadithi hii tunamuona mzee Siwa anavyowakilisha kundi la wachapakazi
kama sifa yake ya nne inavyosema “…. Kutoa sifa zake…..na ukakamavu wake wa
kazi. Shamba lake ndilo lililokuwa kubw akuliko shamba la kijana yeyote pale
kijijjini petu”
Pia
tunamuona Musa kama kijana anayejishughulisha na suala la utafutajji na kundi
lake na hata yeye mwenyewe alikuwa kijana msomi.
Dhumuni
na uonevu Mwandishi ameweza kuonesha kundi ambalo kazi yake ilikuwa ni kutenda
maovu yaani kudhulumu na kuonea na hili lilikuwa tabaka la juu. Msanii anasema
“………..lakini wengine walinishangza.Walikuwa watu wa desturi niliyodhani
walikuwa wapole,wacha Mungu na wasiopenda kudhulumu mtu yeyote….’[uk.7]hivyo
basi tunaona hata viongozi wa dini na wanaotegemewa katika jamii wanadhulumu
ndugu zae wa karibu. Mfano., mzee Kware.
Matabaka
katika jamii. Msanii ameonesha matabaka mbalimbali kama vile wasomi na ambao
hawakusoma, tabala tawala na walimu, wavuvi na wachapakazi, wema na watenda
maovu,
Tabaka la wasomi linawakilishwa na Mussa
na tabaka la ambao hawakusoma linawakilishwa na wachawi. Tabaka tawala
linawakilishwa na wachawi. Mfano, mzee Kware na kundi lake. Tabaka la
wachapakazi linawakilishwa na mzee Sira na wavivu wanawakilishwa na
watendamaovu ambapo mzee Siwa anawakilisha tabaka la wema na hasa wacha Mungu.
Ujasiri
na kujitoa mhanga, msanii ameweza kwa kiasi kikubwa kulifichua kundi la
wajasiri na umuhimu wakewake. Hii inadhihirishwa pale alipomuonesha mzee Sira
kama jasiri wa kusema lukweli na kujitoa mhanga ili kufichua maovu katika jamii
mfano, msanii anasema
“…mimi
ni mtu wa nipe nikupe…”(uk 1) akiwa na maana ya kwamba ukisema naye anasema/
atasema
Pia
mzee Siwa anaonekana jasiri pale ambapo alifichua siri ya watenda maovu kwa
Musa kw kumuambia wazi kuwa babaye ni mchawi. Kwa upande mwingine Musa
anaonesha ujasiri na kujitoa mhanga kwa kupambana na watenda maovu hadi
kuwashinda.
Usaliti,
Msanii anaonesha usaliti katika jamii usaliti huu uko katika makundi mawili,
usaliti mzuri na susaliti mbaya. Usaliti wa mzee Siwa kufichua siri ya wachawi
kwa Musa huu ni usaliti mzuri. Usaliti wa mzee Kware na wachawi wenzake kutaka
kuwazulu ndugu zao wa karibu ni usaliti mbaya katika jamii yoyote. Mfano , mzee
Mfaki Kombo kusaliti wananchi aliowaongoza pia ni usaliti mbaya.
Suala
la uzalendo, Mwandishi pia amefichua suala la uzalendo pale alipomuonesha mzee
Siwa akilitumika Taifa lake hata baada ya kuwa amestafu pia kitendo cha
kufichua siri ya uchawi bila uoga ni uzalendo wa pekee. Kwa upande mwingine
msanii amemuonesha Musa akipambana na Wachawi (watenda maovu)kitendo hiki ni
cha uzalendo wa pekee katika jamii.
Suala
la mapenzi, Msanii ameweza kuyonesha mapenzi ya aina mbili, mapenzi ya dhati na
mapenzi ya uongo. Mzee Siwa amechorwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa Musa pamoja
na jamii yake kwa ujumla, mfano kitendo cha kumpatia Musa kago ili aipukane na
maovu ni kitendo cha mapenzi ya kweli.
Pia Musa anaonesha mapenzi ya kweli kwa
mzeeSiwa kw akumtembelea mara kwa mara. Msanii anasema “….Na sasa hivi nilikuwa njiani kuelekea
kwake mtu pekee niliyeweza kumpa siri zangu…” (uk 2) mapenzi ya uongo
yameonekana yamejitokeza kwa mzee Kware na wachawi wenzake kutaka kuua Musa
ndugu yao wa karibu
Umuhimu
wa elimu, Mhusika Musa aliweza kuleta mapinduzi kwa kupkea ushauri toka kwa
mzee Siwa hii hi kwa sababu alikuwa na Msomi katika jamii. Lakini wale wazee
kijijini hawakueza maendeleo kwa sababu ya kukosa elimu.
UJUMBE;
“Hii ni DHANA inayotumiwa kuelezea taarifa ambazo MSANII au MTUNZI hutoa
kwa wasomaji ametoa ujumbe, kwamba, kikulacho kinguonmo, Mle kuku wa wenzio
miguu humuelekea.
MIGOGORO;
“Hii ni istilahi inayotumiwa kurejerea mvutano unaokuwako kati ya mhusika mmoja
na mwingine katika kazi ya kifasihi”, katika hadithi kundi na kundi katika
jamii.
Kwanza tunaona mgogoro kati …ya mzee Kware
na wenzake Msomi na si mwingine yeyote. Pili msanii ameonesha mgogoro kati ya
kundi la wasomi na wasio wasomi hii ni
pale hawa wanaoneshwa na Musa kama msomi na kundi la wachawi ambao sio wasomi
akiwemo babayake. Tatu mzee Siwa na mzee
wenzake kijijini pale ambapo mzee Siwa alipoweza kukataa mambo yao.
FALSAFA;
“Istilahi hii hutumiwa kuelezea wazo au mawazo anayoamini mtu au mwandishi kuwa
mwandishi9 anaamini kuwa, mapinduzi ndio njia pekee ya kujikombo toka kwenye
mikono ya wadhilumaji.vilevile msanii anaamini kuwa elimu ni siraha ya kuleta
mabadiliko maendeleo katika jamii
1.
Wamitila K.W(2003)KAMUSI YA FASIHI / ISTILAHI
NA NADHARIA, Nairobi Kenya uk 282
2.
T.H.J ………………ukk 121
3.
T.H.J ………………uk 41
Fani; Huu ni ufundi katika kazi ya fasihi
masnii hutumia katika kuomba kazi yake.
“Ni ule ufundi wa kisanaa anautumia msanii
katika kazi yake”1 Msanii ameweza kutumia sana fani katika vipengele
vifuatavyo.
MUUNDO; “Ni mpango na mtiririko wa kazi
kwa mpango wa visa na matukio”2 katika hadithi hii ya “Sadiki Ukipenda” msanii
ametumia muundo wa moja kwa moja au msago kwani tunaona mtiririko wa matukio
unafuatana kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hii ni pale Musa anapoanza kwa kusimulia
sifa za mzee Siwa, kifo cha baba yake na mwisho tunaona anahama nchi.
Mtindo; “Ni ile mnamna ambayo msanii
hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni
kawaida zilizofuatwa kama zilizopo (za kimapokeo) au ni za kipekee”3
Mwandishi katika hadithi hii ametumia
mtindo wa monolojia (masimulizi ya mtu mmoja) pia ametumia nafsi zote tatu mfano.
Mimi nafsi ya kwanza umoja uk 4, wewe nafsi ya kwanza wingi uk 5
LUGHA; “Lugha ndiyo nyenzo kuu katika kazi
ya fasihi. Dhamira na maudhui hayawezi kuwafikia au kuwasilishwa bila ya kuweko
kwa lugha “4 katika hadithi hii ya “Sadiki ukipenda” msanii ameweza kutu lugha
ya kisanii iliyosheheni methali misemo, nahau tamathali za usemi na hata mbinu
nyingine yote haya katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira
iliyokusudiwa.
1. SENKORO F.E.M.K(1980),
fasihi,FASIHI, PRESS AND PUBLICITY CENTRE, DAR ES SALAAM uk 8
2. T.H.J ……uk 26
3. T.H.J ……uk 26
4 Wamitila K.W(2002),KICHOCHEO CHA FASIHI
SIMULIZI NA ANDISHI
chuo cha Elimu na masomo ya mbali, Nairobi
uk 193.
Matumizi ya methali; methali zifuatazo ndani ya
hadithi hii
(i) mla kuku wa wengi ,mguu humwelekea uk7
(ii)
Wakulacho wnguonimo
Misemo
(i) Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo ……uk6
(ii)Mtu wa nipe nikupe
……………………….uk 1
(iii)Kupiga
kupiga moyo konde ……. uk 6
Tamathali
za usemi; “Ni maneno, sentensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia
nguvu katika maana, mtindo hata sauti katika maandishi au kusema kuleta maana
au kubadili kulingana na kusudi la mtunzi”1
katika hadithi hii tamathaliza semi zilizotumika
ni kama ifuatavyo;
Takriri
neno
(i) Babangu
babangu …………..uk 5
(ii) Kuna
mengi mengi ………..uk 1
(iii)
Natakiwa nitakiwa na nani…..4
Takriri nusu mstari
(i) Mtoto
wa kware mlete! Kware we mlete …..6
Sitiari
(i) Kwake
neno ni deni …………1
(ii) Kichwa
chake ni maarifa ……...uk 1
(iii)
Mwanawe ni ng’ombe wetu …..uk 7
(iv) Ulimi
wake ni nasaha ……..1
1: Kahigi K.K na Mulokozi M.M. (1979) KUNGA ZA
USHAIRI NA DIWANI YETU, T.P.H. dar es salaamu uk
132.
Matumizi
ya Tabaini
(i) Mtu wa nipe nikupe ……….uk 1
(ii) Salama kama si salama …….uk 2
(iii)niliwaza
na kuazua ……..uk 5
Matumizi ya Tashibiha
(i)
Umeadimika kama wali wa daku ..uk2
(ii) Mzima kama chuma …….uk3.
(iii) Mweusi kama jongoo…
Matumizi ya Tashihisi
(i) Miti ilinong’ona………uk 9
(ii)
Mbingu zilitakatika baada ya mawingu kukimbia ukali wa jua …..uk2
Mjalizo
Ati
avae tai, suti, viatu vya njugu au kama mwanamke ajipare na kujipodoa na
kujishia mafuta mazuri. Uk
Mdokezo.
(i) Ha…. hakuna si ….si …siku niliyotoa siri nje
uk 4
(ii) Shahada na wewe ……….? Uk 4
Sitiari
(i)
Kwake naona ni deni ……….uk4
(ii)
Kichwa chake ni maarifa
(iii) Ulimi wake ni nasaha
(iv) Kupeana ni kuokoa
Nidaa
He! Kuna nini tena?
Matumizi
ya Tafaida
(i) Baba angu aliaga dunia …uk 9
Lugha ya
picha. Msanii ametumia lugha ya picha (taswira) “Hii ni dhana ambayo hutumiwa
kuelezea neon, kirai au maelezo ambayo yaaunda picha Fulani katika akili
msomaji”1 . Msanii ametumia tawsira zifuatazo.
Uchawi –
akimaanisha matatizo katika jamii
Ngoma
– Taratibu au sheria
Meli
– mzunguko wa maisha
Ng’ombe
– wanyonyaji / Tabuka taswila
Kunguru – watu wasio na maisha mazuri
Hirizi – mawazo ya kimapinduzi
Kago – mbinu / wazo zuri elimu
Mandhari, “Hutumika kuelezea sehemu Fulani ambako
lendo linatendeka au mazingira ya kisaikolojia ya tendo Fulani”2 Hadithi hii ya
“Sadiki Ukipenda” msanii ametumia mazingira ambayo yametenda kuanzia kijijini
wanakotumia jembe la mkono hadi mjini katika nchi za ulimwengu wa tatu hata
dunia kote.
Jina
la hadithi; “Sadiki Ukipenda” linasadifu kwa kiasi kikubwa yale yaliyomo ndani
ya hadithi hii kwani tunaona mzee Siwa anamtaarifu Mussa kuwa baba yake ni
mtendamaovu (mchawi) na Mussa anashindwa kuandiki na hivyo Mzee Siwa anamwambia
sadiki ukipenda.
Kufaulu
na kutofaulu kwa mwandishi amefaulu kwa kiasi kikubwa sana, na ndio maana
ameweza kuibua dhamira mbalimbali mfano dhuluma iliyotanda katika jamii na
suala la kutofanya kazi pamoja matabaka kwa ujumla. Na ametoa suluhisho ya
kwamba ili kuleta maendeleo katika jamii lazima matatizo yaondolewe
Kufaulu
kifani. Kifani msanii ameweza kufaulu sana kwani ametunia lugha nzuri
iliyosheheni usanii matumizi ya methali, misemo, nahau na tamathali za uemi na
nsuko mzima wa matukio.
Wahusika
katika hadithi hii msanii ametumia wahusika wa kutosha. Msanii amemtumia Mussa
kama mhusika mkuu na wengine.
Mussa mhusika mkuu
·
Kijana
·
Msomi
·
Anasikiliza ushauri
·
Alisimulia hadithi
·
Jasiri na mwanamapinduzi
Mzee Siwa, mzee wa miaka 65
·
Mchapakazi na mkakamavu
·
Mkweli
·
Shujaa
·
Mzalendo
·
Anaipenda nchi yake
·
Aliwahi kufanya kazi ya ubaharia
·
Mweusi kama jogoo
Mzee Kware, Baba yake Mussa.
·
Mchawi (mtendamaovu)
·
Alisaliti mwanae
·
Hana upendo kwa nchi yake
Mfaki Kombo, sheha, kiongozi
·
Tabaka la juu
·
Kiongozi wa watenda maovu
·
Kinying’inya cha Bi-kirembwe
Wachawi wengine (watenda maovu/ wadhulumaji)
·
Hawana upendo kwa nchi yao
·
Tabaka tawala
·
Hawana elimu
Nafasi ya hadithi hii ya
“Sadiki Ukipenda” katika fasihi ya majaribio. Fasihi ya majaribio ni fasihi
ambayo imeandikwa kwa mara ya kwanza na kukiuka faida au mazoea yaliyozoeleka
katika jamii. Mfano, matumizi ya taswira ndani ya taswira, vipengele vya fasihi
simulizi katika fasihi andishi, matumizi ya tashititi.
Hakika hadithi ya “Sadiki Ukipenda ni fasihi ya kiswahili
ya majaribio kwa sifa zake yenyewe. Kwanza
hadithi hii imejaa udhanishi kwa kiasi kikubwa kuelezea mambo ambayo hayawezi
kuonekana katika ulimwengu wa macho mfano ukuta kubomoka ili Mussa aweze kupita
yaani uhalisia mazingaombwe.
Pili matumizi ya majina ya wahusika ambao wameisha tumika
katika hadithi au kazi zingine za fasihi zilizopita mfano Bibi Kirembwe ni sifa
tosha ya kuifanya hadithi hii kuwa fasihi ya majaribio.
Tatu matumizi ya picha na nyimbo ndaini ya hadithi ni
kuifanya hadithi hii kuwa fasihi ya majaribio. Mwisho jicho la uhakiki
linaihakiki kazi hii kama fasihi ya majaribio
ya kiswahili.
UHAKIKI WA SADIKI
UKIPENDA
Sadiki ukipenda ni hadithi fupi
iliyoandikwa na said .A. Mohamed , kwa kutumia hadithi hii tutaangalia
vipengele vya Fani, maudhui
Pia tutaangalia kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi hii itatupa nafasi ya
kutoa maoni kuhusu vipengele hivyo vya fani na maudhui.
Kwanza tutaanza kuangalia maana ya Hadithi fupi, maana ya Fani na maudhui.
Hadithi fupi ni nini? Kwa mujibu wa Mbatiali swali hili huishia kujibiwa
kwa kueleza ni nini ambacho si hadithi fupi kwa ujumla hadithi fupi ni moja
tanzu za Riwaya.
Fani kwa mujibu wa kamusi ya Fasihi, istalahi na Nadharia ya k.w. wamitila
anasema:
“Dhana
hii hutumiwa kuelezea
muuundo au mpangilio wa kazi
ya kifasihi au hata sehemu zake”
senkoro f.e.m.k
anasema
“Fani katika fasihi ni ule
ufundi wa kisanii anaotumia
msanii katika kazi yake”
kwa ujumla Fani ni ujuzi atumiao msanii katika kufikisha ujumbe kwa hadhira
yake fani kuna vipengele vifuatavyo; muundo, mtindo, matumizi ya lugha mandhari
na wahusika.
Maudhui katika kamusi ya fasihi , istilahi na Nadharia iliyoandikwa na
wamitila anatoa maana ya maudhui ya kama ifuatayo:
“Ni jumla ya mambo yote
yanayozungumzia
katika kazi ya kifasihi”
maudhui hutumiwa kwa upana kujumlisha dhamira ujumbe, falsafa, msimamo na
migogoro.
Kwa kutumia hadithi fupi ya sadiki ukipenda tunaanza kuangalia vipengele
vya fani na maudhui
Tukianza na fani, tunaangalia muundo , mwandishi ametumia muundo wa moja
kwa moja, ambapo mwandishi anakisimulia kisa kwa kumuelezea mzee Siwa, kasha
uhusiano wake na Mussa. Pia anaelezea alivyomsaidia Mussa katika kuepukana na
kifo chake mwishoo anaonesha mafanikio waliyo yapata kwa kuua mzee Kware. Kisa
kimetungwa kwa mtiririko wa matukio kufuatana.
Mtindo; hapa tunaangalia upangaji wa fani na maudhui wa msanii ambapo
unapelekea kutofautiana na wasanii wengine mwandishi wa sadiki ukipenda
ametumia nafsi zote tatu katika kazi yake.
Mfano:- ameonesha
“mimi” nafsi ya kwanza umoja …nafsi ya kwanza wingi “sisi” nafsi ya pili umoja
“wewe” nafsi ya pili wingi “nyinyi”
Mtindo ambao ametumia katika lugha umemfanya mwandishi kuonesha upekee
katika kazi yake ametumia lahaja ambayo hajazoeleka kwa watumiaji wengi wa
lugha ya kiswahili hivyo kufanya lugha ionekane ngumu. Pia majibizano na
masimuzi yametumika katika hadithi hii vile vile mwandishi ametumia nyimbo
katika … mwandishi ametumia uchawi katika kazi yake hicyo kuonesha utofauti na
kazi nyingine kwani sikazi zote hutumia mbinu hii.
Matumizi ya lugha .mwandishi wa hadithi hii ametumia lugha ya kisanii
iliyosheni Taamathali za semi , methali, nahau, mafumbo, lugha ya picha yote
haya na katika kufikisha ujumbe kwa hadhira.
Tamathali za semi
Sitiari?
-kwake neon ni
deni
-kichwa chake ni
maarifa
-ulimi wake daima
ni nasaha
-mwongozo wake ni
mwangaza wa maisha
-mwanawe ni
ngo’mbe wetu
takriri
Takriri
konsonanti
Hii imetokea
katika …………wimbo
“…..mtoto wa
kware, mlete!
Kware we kware, mlete!
Tashibiha
-ninayo papasa kama kipofu
-umeadimika kama wali wa
daku?
-…mzima kama chuma
-….ngozi yake nyeusi kama
jongoo
-…bundu alihutia
kama vile anawazomea wachawi
tabaini
-mtu wa nipe
n’kupe
-salama kama si
salama
-niliwaza na
kuwazua
Tashihisi
-baada ya mawingu
kukimbia
-maisha yake yaliufanya mwili wake ushibe upepo
-shuari ilizuia
hata miti kunong’ona
Tanakali sauti
-Muda baada ya
muda zilisikika “baa”zao
-“haa” alicheka
- parakacha
miembeni
Tafsida
- kuaga dunia
-unatakiwa
Mbinu nyingine za kisanii
Mdokezo
- Niambie……….
- na wewe………
- Ha.. hakuna ...
si … si
- Na kama unataka ….
Mjalizo
Magogo,
marungu,mawe,mapanga waliitwanga naku zuzu,furaha, vicheko, vifijo huku
wakicheza kwa wimbo mtamu.
Methali
- kikulacho
kinguonimo
Nahau
- kupiga moyoa
konde
Misemo
- sitakokonea
uchochole wa sina sina hi nikiulizwa siungami,
- nipe n’kupe
- mla kuku wa
mwenziwe miguu humwelekea
Lugha ya picha (Taswira)
- Mwandishi ameonesha
taswira kwa kuonesha jinsi zuzu likopigwa
- pia ameonesha
taweira katika , Jinsi ukuta
wa chumba cha Mussa ulivyo kuwa ukipasuka.
Sitiari
Mwandishi ametumia sitiari ya uchawi na
wachawi katika kufikisha ujumbe wake. Mwandishi ametumiwa wachawi katika
kuonesha tabaka tawala. Mfano wa wachawi ambao ndio tabaka tawala Mzee faki kombo na Mzee kware ambao
wanawakilisha tabaka tawala.
Ishara mbalimbali zimetumika katika
kufisha ujumbe.
Kunguru
mwandishi
ametumia kuguru ili kuonesha watu wenye maisha ya kubahatisha na wsiokuwa na mwelekeo.
Ng’ombe,
Pia mwandishi
ametumia ng’ombe ili ionesha tawala la watu wanyonyaji (winye nacho)
wamiridhika na maisha tofauti na kunguru.
Ngoma ya wachawi,
Mwandishi
ametumia mdundo wa ngoma ili kuonesha wachawi (tabaka tawala) kuwa lina
taratibu na sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na wao.
Zuzu/Ngoma,
Mwandishi
ameonesha jinsi ambavyo wachawi (tabaka tawala) linavyopewa mzugo kupumbazwa na mbinu za wanamapinduzi.(Mzee
siwa na Mussa).
Dawa na Hirizi.
Ambazo alipewa Mussa ni mawazo
aliyopewa na Mzee siwa. Ili aweze kuwashinda wachawi (tabaka tawala).
Meli.
Mwandishi
ametumia meli ili kuonesha kwamba maisha ni mzunguko na wote tupo safarini
wengi hatujui tuendako.
Mandhari.
Mwandishli
ametumia mandhari ya nchi za dunia ya tatu ambazo maendeleo yake ni duni na
zinakabiliwa na umaskini na watu kukosa elimu. Mwandishi ametumia madhari ya
kijiji ambapo wakulima hutumia jambe la mkono.
Wahusika.
Mwandishi amegawa
wahusika wake katika sehemu tatu mhusika mkuu, wahusika waasaudizi na wahusika
wajenzi.
Mussa
- msomi
aliyechukiwa na wachawi
- mwanamapinduzi
, alifanikewa kupambana na wachawi
- jasiri ,
aliweza kumuua baba yake (mchawi) mpiga maendeleo
- mdadisi,
aliweza kungundua mbinu za wachawi kw kusaidiwa na mzee siwa (alifuata nyendo
zao).
1. Wahusika
wasaidizi.
Mzee siwa
sirisiri
- mzee mwenye miaka 65
- mwanamapinduzi
- mchapa kazi
- anathamini utu kuliko pesa anapinga
mchawi na anapenda maendeleo
2. Mzee kware.
- baba yake mussa
- mchawi (
tabaka tawala)
- mtu
asiyependa kaendeleo ya jamii.
3. Mhusika mjenzi (FAKI KOMBO)
- mchawi (
mtawala)
-
kinyinginya cha marehemu Bi kirembwe
- anawapinga
wasomi.
Maudhui.
Dhamira.
Dhamira kuu – UJENZI WA JAMII MPYA.
Ujenzi wa jamii mpya ni dhamira ambayo mwandishi ameitumia kama dhamira kuu ili kuonesha jinsi mabadiliko
yanavyotokea katika jamii kwa kuyashinda maovu.
Dhamira ndogo ndogo
1. Ushirikina
na uchawi,
Mwandishi ameonesha imani za ushirikina
na uchawi kama ni moja ya vikwazo vya maendeleo katika jamii. Amewatumia
wahusika wawili Mzee siwa na Mzee faki kombo pia Mzee kware ambaye alikuwa
Tatari kumuua motto wake, ambayealikuwa ni msomi, kwani waliamini si kweli .
lakini mwandishi ameonesha jinsi wachawi walivyoshindwa na kufanya haraka za
ujenzi wa jamii zizidi kupata mafanikio.
2. Umuhimu wa Elimu
Mwandishi ameonesha kuna ukosefu wa
elimu wa aina mbili katika kadithi yake. Kwanza ukosefu wa elimu ya darasani
ambayo hata mzee siwa ameikosa na wapo watu wengi ambao wameikosa . Pili
mwandishiameonesha ukosefu wa elimu ya kujitambua, kama vile unyonyaji unaoendelea katika jamii wapo
watu wengi walikuwa hawaelewi hata Mussa mwenyewe alikuwa haelewi paka
alivyopewa Elimu ( Hilizi na Madawa) ndo akagundua. Hivyo elimu ni kitu muhimu
katika jamii ili kuleta maendeleo na kuondoa viongozi wasiofaa.
3. Umuhimu wa kufanya kazi
Mwndishi ameonesha tatizo lililopo
katika jamii yetu kwamba wapo watu wavivu ambao muda mwingi wanautumia katika
kufanya mambo yasiyo ya muhimu kama kucheza bao.
Vile vile mwandishi ameonesha
jinsi mzee siwa anayo jishughulisha na ukilima . yote ni katika kuleta mabadiliko katika
jamii.
Umuhimu wa kuthamini utu
Mwandishi ameonesha katika hadithi
yake kuwa katika jamii kuna umuhimu wa kuthamini utu wa mtu , kwani utu
ni bora kuliko pesa -mwandishi amemtumia mhusika Mzee siwa ,
jinsi anavyothamini utu, kitu ambacho kilinjengea maadui hasa kwa wale
wasiopenda maendeleo ya jamii . Tabia
hii yam zee siwa ndio iliyo fanya
mussa amukani hiyo kuwaza kushirikiana katika kufanya mabadiliko katka
jamii(kumuua moja ya wachawi)
Ujumbe
1. Uvivu ;ni adui
wa maendeleo
2. Kikulacho ki
nguoni mwako
3. Pesa si msingi
wa utu
4. Uchawi ni
kikwazo cha maendeleo
5. kuleta
maendeleo (mabadiliko ) katika jamii ni jambo (kitu) ambacho ni muhiumu ambapo mtu lazima ujitoe
mhanga .
Falsafa.
Msandishi anaamini uchawi ni kiwazo cha maendeleo katika jamii , Hivyo wachawi
lazima wauwawe.
Msimamo
Mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi , kwani
anataka mabadiliko katika jamii kwa kuwaondoa viongozi ( Tabaka tawala) wenye
kujali maslahi binafsi.
Migogoro
Mgogoro kati ya
wasomi na wasiosoma (Tabaka tawala)
Mwandishi
ameonesha kuwa katika jamii hiyo kuna watu ambao wamesoma na wapo wasiosoma .
Ambapo wasomi wanachukiwa na wale wasiosoma .
Mgogoro huu pia unahusisha wachawi
(tabaka tawala) na wasomi (walio tabaka tawala) wachawi wnahofia kwamba wasomi wataibusha
hisia kwa jamii na kuonesha maovu yafanywayo na tabaka tawala Mzee faki kombo anasema:
“ Na wasomi
wanatuletea nini ila balaa!
Mussa na nafsi yake
Mgogoro huu unaoneshwa na mwandishi anavyo muonesha Mussa asivyoamini
yale aliyoambiwa na Mzee Siwa kwamba baba yake ni mchawi .
Suluhisho la kisa hiki, mwandishi ameonesha suluhisho
kwa kuonesha ushindi uiopatikana kwa wanmapinduzi wakiongozwa na mzee siwa
pamoja Mussa .
Kwani kifo cha
Mzee kware badala kya Mussa kinaonesha ushindi mkubwa .Kwani mwisho
mwandishi Mussa akiingia melini, hiyo
inonesha Mussa anaendelea na maisha kwani maisha ni mzunguko .
Kwa kuhitimisha mwandishi amefaulu
kufika ujumbe kwa kutumia kipengele cha maudhui pia amefaulu kutumia njia (
Fani) yenye ubunifu na utofauti katika kufikisha ujumbe. Mafanikio makubwa
yameonekana zaidi kwa kutumia fasihi ya majaribio ya Kiswahili.
Pia mwandishi amefulu kw kufuata vigezo vya uandishi wa hadithi
fupi. Mambo ambayo mwandishi ameyafuata ni pamoja na uasili umoja , ubunifu na
mbano, ubora wa mtindo, tendo dhahiri pia umbo au kiini wazi.
CHATI (Chemsha Bongo)
Jaza Jedwali lifuatalo
2
|
3
|
4
|
|||||
1
|
|||||||
7
|
8
|
||||||
9
|
|||||||
10
|
|||||||
6
|
|||||||
13
|
5
|
||||||
11
|
|||||||
12
|
Kwenda Chini
1. Kufanikiwa kwa sherehe
2. Wazo au mawazo
yanayojadiliwa
Katika kazi ya fasihi
3. Mpangilio wa kazi ya
kifasihi
4. Eneo au mazingira ambamo kazi ya
Fasihi
inafanyika.
5. Kifaa cha kuonesha muda
6. Kubali kuwa jambo Fulani ni hakika.