Uhusiano fonolojia vs mofolojia

  1. 1. Massamba na wenzake (2004). Wanasema,“fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu.” TUKI (2004) wanaifasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo linajishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha. Hivyo naweza kusema kuwa fonolojia ni utanzu wa Isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mahususi. Fonolojia hushughulikia jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Kipashio cha msingi katika fonolojia ni fonimu na katika fonimu kuna konsonanti na irabu. Massamba na wenzake (2009) wanafasili mofolojia kuwa ni kiwango cha sarufi kinachojishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa maneno katika lugha yaani jinsi maneno ya lugha yoyote iwayo inaundwa. Besha (2007) anasema mofolojia ni taaluma inayojishughulisha na kuchambua muundo wa maneno katika lugha. Misingi ya wataalamu hawa wawili wanaonekana kuingiliana katika kuonyesha namna ya taaluma ya mofolojia inavyojihusisha na muundo wa maneno katika lugha. Mofimu ndio kipashio cha msingi katika mofolojia. Hivyo mofolojia inaweza kuelezwa kwamba ni taaluma inayoshughulika na uchunguzi na uchambuzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugha. UHUSIANO WA FONOLOJIA NA MOFOLOJIA Ni kweli kimsingi taaluma ya mofolojia na fonolojia hufanana kwa kiasi kikubwa. Kwanza, taaluma zote huhusika na uchunguzi na uchambuzi wa lugha za binadamu sauti za lugha ni zile sauti zinazosaidia kujenga tungo zenye maana katika lugha. sauti za lugha zinavyofuata mihimili katika kujenga tungo zenye maana katika lugha. Kuna uunganishaji wa sauti kuunda silabi au mofimu, uunganisha wa mofimu kuunda maneno na maneno kuunda tungo kubwa zaidi (sentensi). sauti za lugha ni sauti zenye kubeba maana na ambazo hutumiwa na jamii fulani ya watu kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Hii ina maana kuwa sauti za lugha ya binadamu ama zinaweza kufanana sana au kwa kiasi fulani na pia zinaweza zikasigana sana au kwa kiasi fulani tu. Pili; vipashio vya kifonolojia ndivyo vinavyounda vipashio vya kimofolojia, kwa kutumia fonimu ambacho ndio kipashio cha msingi katika fonolojia huweza kuunda mofimu ambayo ndiyo kipashio cha msingi cha kimofolojia. Mfano: /h/,/p/,/t/,/k/,/g/,/m/,/n/,/o/,/u/,/e/,/s/,/a/. fonimu hizo zinaweza kuunda mfuatano wa maneno kama ifuatavyo. kat-a = kata hivyo mfuatano wa fonimu /k/+/ a/ + /t/+ /a/ tumepata mofimu kata pak-a = paka hivyo mfuatano wa fonimu /p/+/ a/ + /k/+ /a/ tumepata mofimu paka nus-a = nusa hivyo mfuatano wa fonimu /n/+/ u/ + /s/+ /a/ tumepata mofimu nusa
  2. 2. Kutokana na mifano hii tumeweza kupata maumbo mbalimbali ya maneno kama vile kata, paka na nusa ambayo ni maumbo ya kimofolojia.Hivyo ni dhahiri kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya fonolojia na mofolojia. Tatu; kanuni za kifonolojia zinaweza kutumika kuelezea maumbo ya kimofolojia . Kanuni hizi si kwa kuelezea maumbo tu pia huweza kubadili umbo la neno yaani umbo la ndani na umbo la nje. Kanuni hizo za kifonolojia ni udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuathiri konsonanti, konsonanti kuathiri nazali na tangamano la irabu. Udondoshaji, kanuni hii inahusu kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi wakati mofimu mbili zinapokaribiana yaani katika mazingira hayo hayo ya sauti ambayo ilikuwepo hapo awali hutoweka.hapa kuangalia umbo la ndani la neno na umbo la nje. Umbo la ndani ni jinsi neno lilivyoundwa na mofimu zake mbalimbali na umbo la nje ni jinsi neno lisikikavyo linapotamkwa. umbo la ndani umbo la nje Muguu mguu Mutu mtu Mara nyingi irabu [u] katika mofimu “mu” inapokabiliana na mofimu fulani hasa konsonati halisi katika mpaka wa mofimu, irabu [u] hudondoshwa lakini inapokabiliana na irabu inayofanana nayo hubaki kama ilivyo. Kama vile Muuguzi-muuguzi Muumba- muumba Uyeyushaji, hii ni kanuni inayohusu ubadilikaji wa irabu fulani kuwa nusu irabu au viyeyusho ”. Viyeyusho vinavyohusika ni /w/ na /y/. kanuni hii hutokea katika mazingira ambayo irabu [u] hukabiliana na irabu isiyo fanana nayo katika mpaka wa mofimu na kuwa /w/ lakini hubaki kama ilivyo mara ikabilianapo na irabu inayofanana nayo. Pia irabu [i] katika mofimu inapokabiliana na irabu isiyofanana nayo hubadilika na kuwa /y/ katika mpaka wa mofimu lakini hubaki kama ilivyo inapokabiliana na irabu inayofanana nayo.Mfano; Mu+ema-----mwema Mu+ana-------mwana Mu+eupe-------mweupe Vi+ao------vyao Muungano wa sauti, kanuni hii hutokea pale ambapo irabu ya mofimu moja inapokabiliana na irabu ya mofimu nyingine katika mpaka wa mofimu irabu hizo huungana na kuzaa irabu nyingine. Mfano; Wa + ingi wengi, Ma + ino meno, Wa + izi wezi Hivyo fonimu /a/ imeungana na fonimu /i/ na kubadilika na kuwa fonimu /e/ katika maneno wengi, meno na wezi. Lakini kanuni hii haifanyi kazi wakati wote kwani kuna mazingira mengine ambayo haifuati hasa katika mofimu mnyambuliko mfano; Wa +oko+a+ji - waokoaji Kwa kuhitimisha mofolojia na fonolojia zote ni nyanja za isimu zinazounda maarifa fulani ya lugha kwa kuchunguza sauti na maumbo ya maneno yatokanayo na sauti za lugha hiyo na mpangilio wake. Nyanja zingine za isimu ni kama fonetiki, sintaksia na semantiki. katika Uundaji wa maneno au tungo zenye kuleta maana, fonolojia hushughulikia jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Hivyo basi ili msemaji aweze kudhihirisha umilisi wake lazima aweze kupanga vizuri konsonanti na irabu ili kuunda silabi. hiyo mofolojia huchunguza masuala kama vile aina za mofimu, namna mofimu zinavyojenga maneno na namna mofimu zinavyohusiana ili kuunda neno na lenye maana.
  3. 3. MAREJELEO Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa lugha na Isimu. Macmillan Aidan Ltd. Dar es Salaam. Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Taaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es salaam. Massamba, D.P.B na wenzake. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn publishers. Ltd. Nairobi.
  4. 4. CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINO, TANZANIA KITUO CHA BUKOBA KITIVO CHA ELIMU IDARA : KISWAHILI. JINA LA KOZI: FONOLOJIA YA KISWAHILI. MSIMBO WA KOZI: SW 211 JINA LA MHADHIRI: LUPAPULA, ABEL. JINA LA MWANAFUNZI: MAPESA, NESTORY NAMBA YA USAJILI : BAEDII 41584 AINA YA KAZI: KAZI BINAFSI. TAREHE YA UWASILISHAJI: 16/12/2013 Swali; Eleza kwa mifano uhusiano uliopo baina ya fonolojia na mofolojia.
Powered by Blogger.