FONOLOJIA NA FONETIKI YA KISWAHILI
FONOLOJIA YA KISWAHILI UTANGULIZI NA USULI WA
TAALUMA YA FONOLOJIA
Neno
fonolojia linatokana na maneno mawili ya Kigiriki phone-sauti za kusemwa na
logos- taaluma/mtalaa. Masimulizi yanadai kuwa taaluma hii ilianza zamani sana
kati ya mwaka 460 kabla ya Masia huko India ya kale, ambapo mtu aliyeitwa Panini, na ambaye huaminika kuwa ni baba
wa isimu aliandika kuhusu fonolojia ya Kisansikriti
katika matini aliyoiita Shiva Sutras.
Ni katika andiko hili ndipo alipobainisha kuwepo kwa dhanna ambazo leo hii
hujulikana kama fonimu, mofimu na mzizi. Baada ya andiko hilo, habari za taaluma ya fonolojia ni kama
zilipotea kabisa katika uwanja wa isimu hadi ilipofika karne ya 19 ambapo
wanaisimu wengine waliibuka na kuzungumzia upya masuala ya fonolojia. Miongoni
mwa wanaisimu wa mwanzo wanaotajwa kujihusisha na fonolojia ni Mpolandi "Jan Baudouin de Courtenay",(pamoja
na mwanafunzi wake wa zamani "Mikołaj
Kruszewski" alipobuni neno fonimu
mnamo mwaka 1876, na kazi yake, ijapokuwa hairejelewi sana, inachukuliwa kuwa
ni mwanzo wa fonolojia mamboleo. Mwanaisimu huyu si tu alishughulikia nadharia
ya fonimu, bali pia vighairi vya kifonetiki (ambavyo leo huitwa alofoni na mofofonolojia). Maandishi ya Panini
(Sarufi ya Kisanskriti) pamoja na Jan
Baudouin de Courtenay yalikuja kuwa na athari kubwa kwa anayeaminika kuwa
baba wa nadharia ya Umuundo Mamboleo, Ferdinand
de Saussure, ambaye pia alikuwa ni profesa wa Sansikriti. Wanaisimu wote hawa walikuwa wanajaribu kulinganisha
sauti za lugha za Asia Mashariki na za Ulaya, lengo lao likiwa ni kujua mizizi
ya lugha zilizoitwa India-Ulaya.
Kutokana na mkabala huo, katika kipindi hicho isimu ilikuwa Isimu-linganishi
tu. Kutokana na tafiti zao hizo waliweza kupata maneno yenye sauti na maana
zilizolingana, kufanana au kukaribiana. Utafiti huo uliweza kugundua jamii
mbili za lugha ambazo ni jamii ya lugha za Kirumi na jamii ya lugha za
Kijerumani. Baadhi ya wanaisimu mahususi kabisa wanaokumbukwa kuchangia katika
maendeleo ya fonolojia ni pamoja na:
(i)
Jan Baudouin
de Courtenay (1845-1929) Kama ilivyoelezwa hapo awali, huyu ni mwanaisimu
aliyebuni dhanna za foni na fonimu. Katika nadharia yake, alidai kuwa sauti za
mwanadamu ni za aina mbili—foni na fonimu. Alisema kuwa foni ni sauti za
kutamkwa tu lakini fonimu ni sauti za lugha. Hata hivyo, de Courtenay hakutumia
istilahi za foni na fonimu (kama zinavyotajwa sasa) bali alitumia istilahi za
anthrophonics—foni na psychophonics—fonimu. Yeye alidai kuwa foni zipo karibu
sana na taaluma ya kumuelewa binadamu pamoja na alasauti zake ambazo kwa hakika
hutofautiana sana na za wanyama wengine. Na kuhusu fonimu, alidai kuwa zinahusu
kumwelewa binadamu pamoja na akili zake na namna anavyofikiri katika akili
yake. Alidai kuwa, mara nyingi, binadamu hupokea kinachotamkwa na kufasiliwa.
(ii)
Ferdinand de
Saussure (1887-1913): Ni mwanaisimu wa Kiswisi anayejulikana kama baba wa isimu
kutokana na mchango wake alioutoa katika taaluma hii. Yeye anakumbukwa zaidi
kutokana na uwezo wake wa kutofautisha dhanna alizoziita langue-mfumo wa lugha mahsusi, parole-matamshi
ya mzungumzaji wa lugha husika na Langage
ambayo hufafanuliwa kuwa ni uwezo alionao mzungumzaji wa lugha mahususi wa
kuzungumza na kuelewa matamshi ya mzungumzaji mwingine wa lugha hiyohiyo. Ni
sehemu ya lugha inayowakilisha maarifa kati ya sauti na alama. Ni mfumo wa
alama kwa maana ya kiufundi tu. Dai lake la msingi ni kuwa alama inategemea
vitu viwili-kitaja na kitajwa-hivyo ili mawasiliano yafanyike, mfumo wa ishara
lazima ufahamike na ukubaliwe na wanajamii wote. Kwa upande wa parole, anadai kuwa ni matendo uneni.
Ni namna lugha inavyotamkwa katika hali halisi
na mtu mmoja mmoja. Dhanna ya parole
inalingana na dhanna ya performance
(utendi) ya Noam Chomsky. Katika
lugha, parole ni matamshi tofauti ya
sauti moja-alofoni. Wanaisimu wanaonekana kukubaliana na madai ya Saussure kwa kuwa inaelekea kuthibitika
kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kitaja na kitajwa [alama (lugha)
na kinachowakilishwa (masilugha)], bali makubaliano baina ya wazungumzaji wa
lugha moja husika ndiyo hutawala.
(iii)
Nikolai Trubetzkoy (1890-1939) Ni miongoni mwa waanzilishi wa
taaluma ya fonolojia akichota mizizi ya taaluma ya isimu kutoka katika Skuli ya
Prague. Mwanaisimu huyu aliandika
misingi ya fonolojia kwa kutumia maarifa yaliyoibuliwa na Ferdinand de Saussure. Ni mtaalamu wa kwanza kufasili dhanna ya
fonimu. Aliandika vitabu vingi kwa lugha ya Kijerumani, miongoni mwake ni
Grundzüge der Phonologie (Principles of Phonology, 1939), ambapo ni katika
kitabu hicho ndimo alimotoa fasili ya fonimu pamoja na kubainisha tofauti baina
ya fonetiki na fonolojia.
(iv)
Noam Chomsky (1928-) Huyu ni mwanaisimu wa Kimarekani anayevuma sana kwa mchango
wake katika taaluma ya isimu kwa ujumla. Dhanna za competence (umilisi/umahiri) na perfomance
(utendi) zimemfanya awe maarufu ulimwenguni. Dhanna hizi zinaelezea tofauti baina
ya maarifa na udhihirishaji wa maarifa hayo ya mtumiaji wa lugha. Katika
fonolojia, Chomsky anakumbukwa kwa
ufafanuzi wake wa dhana ya fonimu kwa mtazamo wa kisaikolojia. Anapochunguza
dhanna hii, hudai kuwa fonimu ni tukio la kisaikolojia, hivyo fonimu zimo
kichwani mwa mzungumzaji wa lugha.
Daniel Jones (1881-1967) Ni mwanafonetiki kinara na maarufu
kabisa katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini. Ni Mwingereza msomi ambaye
alikuwa na shahada ya kwanza ya hisabati na shahada ya umahiri wa sheria, shahada
ambazo hata hivyo, hakuwahi kuzitumia. Baadaye, alisomea lugha na kuhitimu
shahada ya uzamivu. Daniel Jones alifunzwa fonetiki na maprofesa mbalimbali,
japokuwa aliathiriwa zaidi na Paul Passy
na Henry Sweet. Hamu yake kuu ilikuwa
kwenye nadharia ya fonetiki. Anafahamika zaidi kwa ufafanuzi wa dhanna ya
fonimu kwa mtazamo wa kifonetiki (ufafanuzi wake tutauchunguza katika sehemu ya
mitazamo ya dhana ya fonimu).
FONETIKI
NA FONOLOJIA
Fasili ya taaluma
ya fonolojia haiwezi kukamilika, na pengine kueleweka, iwapo hakuna linalosemwa
kuhusiana na taaluma ya fonetiki. Hali hii inatokana na ukweli kuwa kuna
uhusiano wa kinasaba kati ya fonolojia na fonetiki. Massamba na wenzake
(2004:5) wanaeleza ukweli huu kwamba: .... fonetiki na fonolojia ni matawi
mawili tofauti ya isimu lakini yenye kuhusiana sana. Uhusiano wa matawi haya
unatokana na ukweli kwamba yote mawili yanajihusisha na uchunguzi na uchambuzi
unaohusu sauti za lugha za binadamu. Kutokana na ukweli huu, jitihada za
kufasili dhanna ya fonolojia inaelekea kuwa nyepesi, dhanna hizi mbili
zinapofasiliwa kwa mlinganyo. Tuanze na fonetiki:
FONETIKI NI NINI?
Fonetiki ni tawi la
isimu linalochunguza sauti za kutamkwa na binadamu ambazo huweza kutumika
katika lugha asilia. Massamba na wenzake (kama hapo juu) wanafasili fonetiki
kuwa ni tawi la isimu linalohusika na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu za
utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji, na ufasili wa sauti za lugha za
binadamu kwa ujumla. Wanasisitiza kwamba, kinachochunguzwa katika fonetiki ni [maumbo]
mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na alasauti za binadamu (yaani sauti za
binadamu zinazotamkwa tu). Kipashio cha msingi cha uchambuzi wa kifonetiki ni
foni. Foni ni sauti yoyote
inayotamkwa na binadamu na inayoweza kutumika katika lugha fulani. Hivyo basi,
foni ni nyingi sana na hazina maana yoyote. Wanafonetiki hudai kuwa foni zimo
katika bohari la sauti (dhanna dhahania) ambalo kila lugha huchota sauti chache
tu ambazo hutumika katika lugha mahususi. Sauti chache zinazoteuliwa na lugha
mahususi kutoka katika bohari la sauti huitwa fonimu.
Matawi
ya Fonetiki:
Kuna mitazamo
miwili tofauti kuhusiana na matawi ya
fonetiki. Mtazamo wa kwanza ni unaodai kuwepo matawi matatu; na mtazamo wa pili
ni unaodai kuwepo matawi manne. Mtazamo wa kuwepo matawi matatu unataja fonetiki matamshi, fonetiki akustika (safirishi), na fonetiki masikizi. Mtazamo wa kuwepo matawi manne (kama Massamba na
wenzake (kama hapo juu), pamoja na matawi tuliyokwisha yataja, wanongezea tawi la
fonetiki tibamatamshi.
(a)
Fonetiki matamshi
huchunguza jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti. Hususani,
huchunguza namna na mahali pa kutamkia sauti husika mfano: [p] Ni kipasuo sighuna cha midomo.
(b)
Fonetiki
akustika huchunguza jinsi mawimbi ya sauti yanavyosafiri kutoka katika kinywa
cha mtamkaji hadi kufika katika sikio la msikilizaji.
(c)
Fonetiki
masikizi hujihusisha na mchakato wa ufasili wa sauti za lugha, hususani
uhusiano uliopo baina ya neva za sikio na za ubongo.
(d)
Fonetiki
tibamatamshi ni tawi jipya lililozuka mwanzoni mwa karne hii, ambalo huchunguza
matatizo ya utamkaji ambayo binadamu huweza kuzaliwa nayo au kuyapata baada ya
kuzaliwa. Ni tawi linalojaribu kutumia mbinu za kitabibu kuchunguza matatizo na
kutafuta namna ya kuyatatua mfano: Kuna
tatizo la mtu kuzaliwa na paa la kinywa au kaakaa lililogawanyika ambalo
huathiri matamshi katika usemaji.
FONOLOJIA NI NINI?
Fonolojia ni
taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya sauti za kutamkwa zinazotumika katika
lugha asilia mahususi za binadamu. Inapolinganishwa na fonetiki, inasisitizwa
kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza mifumo ya sauti za lugha
mahususi tu, kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kigogo, n.k. Hata hivyo,
wapo wanaisimu wanaoelekea kukubaliana kuwa kuna fonetiki ya lugha mahususi
pia, na kuna fonolojia ya jumla, na fonetiki ya lugha mahususi. Mathalani, Massamba (1996) licha ya kufasili
fonolojia kuwa ni taaluma ya isimu inayochunguza mfumo wa sauti za lugha
mahususi, anaenda mbele zaidi na kudai kuwa fonolojia inaweza kuchunguza sauti
kwa ujumla wake bila kuzihusisha na lugha mahususi. Akmajian na wenzake (2001), nao wanadokeza msimamo kama wa Massamba
wanapodai kwamba fonolojia inaweza kuchunguzwa kwa mitazamo miwili tofauti.
Kwanza, fonolojia kama tawi dogo la isimu linalochunguza mfumo na ruwaza za
sauti za lugha mahususi ya binadamu; na pili, fonolojia kama sehemu ya nadharia
ya jumla ya lugha ya binadamu inayohusika na tabia za jumla za mfumo wa sauti
za lugha asilia za binadamu. Katika mhadhara huu, hata hivyo, tutakuwa wafuasi
wa mtazamo unaoona kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mfumo wa
sauti za lugha mahususi tu, hivyo, tunapata fonolojia ya Kiswahili, fonolojia
ya Kiingereza, fonolojia ya Kiha, fonolojia ya Kihehe, na fonolojia ya Kibena,
n.k. Kipashio cha msingi cha fonolojia ni fonimu.
FONIMU:
Ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno.
Hivyo basi, fonimu ina maana, kwa kuwa inaweza kubadili maana ya neno
inapobadilishwa nafasi katika neno husika. Foni chache zilizoteuliwa kutoka
katika bohari la sauti ili zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahususi
ndiyo fonimu. Hivyo, fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya fonimu
za lugha hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Mathalani, Kiarabu kina
fonimu ishirini na nane (28), Kiswahili kina fonimu thelathini (30), Kifaransa
kina fonimu thelathini na tatu (33), na Kiingereza kina fonimu arobaini na nne
(44). Sauti ambayo huweza kubadilishwa nafasi yake katika neno lakini maana
ikabaki ileile huitwa alofoni.
Alofoni
ni kipashio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo fonimu moja hutamkwa na
kuandikwa tofautitofauti bila kubadili maana ya neno. Mfano: Fedha na feza Sasa
na thatha, Heri na kheri. Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti ya
fonimu (sauti) moja.
MITAZAMO YA DHANNA YA FONIMU
Juhudi za kufasili
dhana ya fonimu zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali zimezua mitazamo
mbalimbali ya namna ya kuchambua dhana hii. Hadi sasa, mitazamo mitatu ifuatayo
ndiyo hujulikana zaidi.
(i)
Fonimu kama tukio la Kisaikolojia; Huu ni mtazamo uliokuzwa na kutetewa na
wanasarufi geuzi-zalishi, mwanzilishi wake akiwa ni Noam Chomksy. Kwa mujibu wa
mtazamo huu, fonimu ni dhanna iliyo katika akili ya mzungumzaji wa lugha.
Mtazamo huu unadai kuwa kila mzungumzaji wa lugha ana maarifa bubu ya idadi na
jinsi ya kutamka fonimu za lugha yake. Chomsky anayaita maarifa haya kuwa ni umilisi (competence). Anadai kuwa
maarifa haya ya fonimu hufanana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wazungumzaji wa
lugha moja husika. Kinachotofautiana ni jinsi ya kudhihirisha (kutamka)
fonimu hizo, yaani utendi
(perfomance). Chomsky anabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuhitilafiana
baina ya umilisi na utendi kutokana na matatizo mbalimbali ambayo mzungumzaji
hukabiliana nayo. Matatizo hayo ni kama vile uchovu, ulemavu wa viungo vya
matamshi (alasauti za lugha), athari za mazingira, ulevi, na maradhi. Hivyo,
kutokana na hali hii, fonimu hubaki kuwa tukio la kiakili, yaani kisaikolojia
tu.
(ii)
Fonimu kama tukio la Kifonetiki; Wafuasi wa mtazamo huu wanaongozwa na Daniel
Jones. Daniel Jones anaiona fonimu kuwa ni [umbo] halisi.
(iii)
Fonimu kama tukio la kifonolojia; Huu ni mtazamo wa kidhanifu, ambapo huaminika
kuwa fonimu ni kipashio cha kimfumo, yaani fonimu huwa na maana pale tu
inapokuwa katika mfumo mahususi. Mwanzilishi wa mtazamo huu ni Nikolas Trubetzkoy. Yeye huamini kuwa
fonimu ni dhanna ya kiuamilifu na uamilifu huu hujitokeza tu fonimu husika
inapokuwa katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Kwa mujibu wa mtazamo huu,
fonimu ni kipashio kinachobainisha maana ya neno. Mtazamo huu hutumia jozi
sahihi kudhihirisha dai lake. Mathalani, maneno kama:
-
baba
na bata yana maana tofauti kwa sababu
ya tofauti ya fonimu /b/ na /t/. Mtazamo huu hujulikana kuwa ni wa kifonolojia.
Na kwa hakika, mawazo haya ndiyo yaliyoshika mzizi zaidi katika taaluma ya
fonolojia na ndiyo inayofunzwa hivi sasa katika sehemu nyingi ulimwenguni.
Tofauti kati ya Fonetiki na Fonolojia
FONETIKI
|
FONOLOJIA
|
Huchunguza sauti za lugha ya mwanadamu kwa
ujumla.
|
Huchunguza sauti za lugha mahususi.
|
Ni pana{huchunguza sauti nyingi}
|
Ni finyu {huchunguza sauti chache}
|
Huchunguza sauti zinavyozalishwa
|
Hushughulika na sauti zinavyotumika
|
Ni moja tu duniani
kote
|
Ni nyingi kwani kila lugha ina fonolojia yake
duniani.
|
Uwasilisho wa suti
hutumia mabano mraba mf. []
|
Sauti huwasilishwa na mabano mshazari. mfano //
|
Inahusisha sayansi
huru katika uchunguzi wake
|
Haitumii sayansi huru katika uchunguzi wake
|
DHANNA YA FONOLOJIA
VIPANDE NA FONOLOJIA ARUDHI
Fonolojia
imegawanywa katika aina kuu mbili ambazo ni Fonolojia arudhi na Fonolojia
vipande sauti.
(a)
Fonolojia vipande sauti; ni aina ya Fonolojia ambayo hushughulikia
uchunguzi wa vipande sauti vyenyewe. Wanaisimu katika aina hii hubainisha
vipande sauti bainifu katika lugha kama vile alofoni na fonimu pia hueleza
fonimu hizo jinsi zinavyoweza kuathiriana katika maeneo mbalimbali. (Mgullu,
2010).
(b)
Fonolojia arudhi; tawi hili hushughulikia masuala mengine ya sauti ambayo hayaathiri
vipashio vikubwa zaidi kuliko fonimu moja. Pia aina hii huchunguza mfumo wa
kuweka mkazo katika maneno na tungo katika lugha fulani kama vile kiimbo na
muundo wa silabi. (Mgullu, 2010). Fonolojia ya Kiswahili hujishughulisha na
vipengele mbalimbali ambavyo vinahusiana na sauti pamoja na mpangilio wake wa
uundaji maneno katika lugha mbalimbali. Vipengele hivi ni kama vile; matamshi, kiimbo,
mkazo, na mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu na maneno.
(i)
Matamshi;
ni utaratibu utumikao katika utoaji wa sauti za maneno ya lugha ya binadamu.
Utaratibu wa matamshi ya sauti za lugha huzingatia mahali pa matamshi na jinsi
ya utamkaji. Mfumo huu ni maalumu kwa sababu binadamu hutumia ala za sauti na
upumuaji katika utamkaji.
(ii)
Lafudhi;
ni sifa ya kimasikizi inayomtambulisha msemaji anatoka eneo gani kijiografia.
Lafudhi hutokana na athari ya lugha ya kwanza au mazingira. Mfano:
·
Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa
(Wakuriya)
·
Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mafaranga
makumi mawili (Wakongo)
·
Ukikaa
nchale, ukichimama nchale (Wamakonde)
·
Wewe
unakamuaga mang’ombe tu moja
kwa
moja (Wasukuma)
·
Mbona
unakuwa kinganganizi,
nilishakwambia sikupendi
rakini
wewe bado unaningangania
tu!
(Wahaya)
(iii)
Silabi;
ni kipashio cha utamkaji ambacho kwa kawaida ni kikubwa kuliko fonimu na kidogo
kuliko neno. Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ya sauti
za lugha zinapotamkwa kwa pamoja kama fungu moja linalojitegemea kimatamshi.
Fungu hilo laweza kujumuisha sauti moja pekee au sauti mbili kutegemea muundo
wa lugha husika. (Massamba na wenzake, 2004). Mpaka wa silabi hutenganishwa na
alama ifuatayo; $ mfano: $ma$,$ma$, $a$,$na$,$ku$,$la$.
(iv)
Kiimbo;
ni utaratibu maalumu wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti katika usemaji
wa lugha au kiimbo ni kipengele cha kifonolojia chenye maana ya kupanda na
kushuka kwa mawimbi ya sauti za lugha. Vilvile kiimbo ndicho kinafanya sentensi
iwe ya swali, mshangao au maelezo. Mfano.
o
John
ameondoka?
o
John
ameondoka!
o
John
ameondoka.
(v)
Mkazo/shadda; Katika lugha ya Kiswahili kuna namna ya kutamka maneno ili kuleta
maana mbali mbali, kwa mfano neno “barabara” litaleta maana husika kulingana na
jinsi lilivyotamkwa. Hivyo, mkazo ni pale silabi inapotamkwa kwa kukazwa.
Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko
silabi nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa mkazo, sauti hupandishwa juu
kiasi.
Maneno mengi ya
Kiswahili, hasa yale yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika silabi ya pili
kutoka mwisho.
Kwa mfano: ba’bu,
maya’i, rama’ni (mimi nilikuwa nikitamka ra’mani), baraba'ra (njia).
Baadhi ya maneno
yenye asili ya kigeni, huwa na mkazo katika silabi nyingine. Kwa mfano:
bara'bara (sawa sawa), Alha’misi. Zipo baadhi ya lugha zenye uwezo wa kuhamisha
mkazo na maana ya neno ikabadilika.
Mfano: Kiingereza
A B
·
Produ’ce Pro’duce
(zalisha) (mazao)
·
Pro’ject Proje’ct
(mradi) (panga mradi)
·
Per’mit Permi’t
(ruhusu) (ruhusa)
Katika
lugha kama kiingereza mkazo unaweza kuhama na kubadili maana lakini katika
Kiswahili mkazo huwa hauwezi kuhama.
(vi)
Kidatu, Massamba,
Kihore, na Msajila (2004), wanakitazama kidatu kwa maana ya sauti isikikayo
wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati, au kuwa chini. Hii humaanisha
kwamba katika usemaji, mtu anaweza kupandisha kiwango cha sauti (yaani akaiweka
katika kidatu cha juu), kukishusha kidogo kiwango hicho na kuiweka sauti katika
kidatu cha kati, au kukishusha zaidi na kuiweka sauti katika kidatu cha chini.
Ni muhimu kuelewa kwamba kupanda au kushuka kwa mawimbisauti na kupanda au
kushuka kwa kiwango cha kidatu ni vitu viwili tofauti. Kupanda au kushuka kwa
mawimbisauti si lazima kuathiri kidatu; wala kidatu si lazima kuathiri kupanda
au kushuka kwa mawimbisauti. Hii ni kwa sababu mzungumzaji anaweza kusema kwa
kidatu cha juu (sauti ya juu), kidatu cha kati (sauti ya kati) au kidatu cha
chini (sauti ya chini) na bado akaweza kubadilisha mawimbisauti akiwa katika
kidatu hicho hicho kimoja. Lakini pia mzungumzaji anaweza kubadili kidatu. Kwa
mfano, anaweza kuanza kuzungumza kwa sauti ya juu (kidatu cha juu) akamalizia
kwa sauti ya kati (kidatu cha kati) au sauti
ya chini (kidatu cha chini).
Othografia; Kila lugha ina mfumo tofauti wa usemaji na
hutumia mfumo tofauti wa sauti. Kila lugha inakuwa haina budi kubuni mfumo wake
wa kuziwakilisha sauti zake katika maandishi. Mfumo huo wa maandishi ndio
ujulikanao kama othografia. Mfumo huu huwa unawasilisha herufi maalumu
zinazobuniwa ili kuwakilisha sauti za lugha inayohusika kimaandishi. Neno uthografia
lina asili ya kigiriki na maana yake ni utaratibu wa kutumia alama au michoro
ya maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika lugha.
(vii)
Toni; Kwa
mujibu wa Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha (2009:87). Toni ni sifa
inayowakilisha kiwango pambanuzi cha kidatu cha silabi katika neno au sentensi
na ambayo huweza kubadilisha maana ya neno katika sentensi kisemantiki au
kisarufi. Hivyo basi, Toni ni sifa katika lugha ambapo maana ya neno huathiriwa
na jinsi linavyotamkwa. Au. Toni ni kiwango cha kidatu pamoja na mabadiliko
yake ambayo hutokea wakati mtu anapotamka silabi au neno. Katika lugha
mabadiliko ya toni hubadili maana za yale yanayosemwa na sifa za toni hubainika
katika kiwango cha neno na silabi zake mbalimbali. Lugha nyingi za kibantu kama
vile kikuyu na kikamba zina sifa ya toni lakini lugha ya Kiswahili haina sifa hii.
Kuna aina tatu za toni ambazo ni, Kwanza, toni juu ni toni ambayo hudhihirishwa
na kidatu cha juu. Pili, toni kati ni toni ambayo hudhihirishwa na kidatu cha
kati. Tatu, toni chini ni toni ambayo hudhihirishwa na kidatu cha chini.
MUHADHARA WA II:
VITAMKWA VYA LUGHA KWA UJUMLA:
SAUTI ZA LUGHA ASILIA
Wanaisimu
wengi wanakubaliana kwamba lugha ya binadamu ni mfumo wa sauti nasibu zenye
kubeba maana na ambazo hutumiwa na jamii fulani ya watu kwa madhumuni ya
mawasiliano ya kimazoea tu ya watumiaji wa lugha inayosikika kati yao. Sauti
nasibu ni sauti ambazo uteuzi wake haukufanywa kwa kufuata mantiki au vigezo
fulani maalumu bali umetokana na makubaliano ya kimazoea tu ya watumiaji wa
lugha husika. Hii ndiyo maana sauti za lugha mbalimbali zinaweza kufanana sana au kwa kiasi fulani tu.
Na pia zinaweza kusigana sana au kiasi fulani tu.
Mhimili
muhimu wa lugha asilia ni sauti zitumikazo kuunda silabi au mofimu.
Uunganishaji wa mofimu huunda maneno, maneno huunda virai, virai huunda vishazi
na vishazi huunda sentensi. Utaratibu wa kuunganisha sauti kuunda maneno ni wa
nasibu kama ambavyo sauti zenyewe ni za nasibu.
ALASAUTI ZA LUGHA ASILIA
Alasauti
ni viungo vya mwili vinavyotumika katika utamkaji wa sauti mbalimbali za lugha.
Utamkaji wa sauti zitumiwazo katika lugha ya mwanadamu hufanyika kwa kutumia
sehemu au viungo mbalimbali maalumu vya mwili wa mwanadamu. Katika taaluma ya
Isimu sehemu ya maneno yatumikayo katika utamkaji wa sauti za lugha hujulikana
kama ala za sauti.
Ala
hizo za sauti za lugha ni:
-
Mapafu
-
Umio
-
Kaakaa gumu
na laini
-
Ulimi
-
Ufizi
-
Meno
-
Midomo
-
Pua, n.k
Kwa
kutumia ala hizo mwanadamu anaweza kuzalisha sauti mbalimbali.
FONOLOJIA NA MOFOLOJIA
Fonolojia
ni tawi la isimu linalojishughulisha na sauti za lugha mahususi jinsi
zinavyotamkwa na mahali zinapotamkiwa.
Mofolojia
ni taaluma ya kiisimu inayojishughulisha na maumbo ya lugha jinsi yanavyoundwa
na kazi za maumbo hayo katika lugha.
Fonolojia
na mofolojia hutegemeana kwa misingi kwamba mofolojia hutegemea sauti za
fonolojia katika kuunda maumbo mbalimbali. Sauti hizo huunda silabi,mofimu na
maneno. Bila fonolojia mofolojia haiwezi kufanya kazi wala uchambuzi wa
haukamiliki.
Mfano:
“baba” umbo hilo limeundwa na :
Fonimu -------4: b+a+b+a
Silabi------- 2: ba + ba
Katika
mfano huo utabaini kuwa umbo “baba” ni umbo tu la kimofolojia lakini
uchanganuzi wake hutegemea fonolojia.
MUHADHARA WA III:
VITAMKWA VYA MSINGI VYA KISWAHILI SANIFU
Kitamkwa
ni sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji wa maneno. Vitamkwa
huwakilishwa kimaandhishi kwa kutumia alama zijulikanazo kama herufi za
alfabeti. Mfano: p,the,dh, n.k
Kitamkwa
hujitokeza kama kipande sauti
kinachojibainisha kwa dhati yake kwa mfano: p,b, kila kimoja kina ubainifu
uliowazi kwa kuzingatia vitamkwa hivyo vinavyosikika masikioni, ni dhahiri
kwamba /p/ hutamkwa tofauti na /b/.
Vitamkwa vya kifonetiki
Tunapochunguza
vitamkwa vya kifonetiki tunazingatia sauti za lugha jumla. Kifonetiki kitamkwa
huzingatiwa jinsi kinavyotamkwa, kusafirishwa, usikikaji wake na ufasili wa
vitamkwa hivyo bila kuvihusisha na lugha fulani maalumu.
Uchambuzi
wa vitamkwa vya kifonetiki huzingatia sifa za jumla za vitamkwa kama vile
kipasuo kutamkiwa kwenye midomo, kuviringa midomo, n.k
Hizo
ni sifa za kitamkwa [p], sifa hizo huweza kujitokeza pia kwenye umbo [b].
katika kiwango hiki huwa haijalishi kama sauti zinazochunguzwa zinatumika
kuundaa maneno tofauti katika lugha au la.
Vitamkwa vya kifonolojia
Hapa
vitamkwa huchunguzwa katika lugha maalumu jinsi vinavyotamkwa, vinapotamkiwa na
jinsi vinavyohusiana na kuathiriana kimatumizi katika kuunda maneno. Mfano:
pumba,bumba,taka,daka
Katika
mifano hiyo vitamkwa [p,b,t,d] vinaleta utofauti wa kimaana vinapotumika katika
maneno.
Fonimu kwa ujumla
Fonimu
– ni kitamkwa cha msingi katika lugha kituwacho kuunda maneno ya lugha fulani
maalumu mfano: /p/,/b/,/u/,/m/,/t/,/d/,/a/,/k/,/n/ huweza kuunda maneno kama[
pumba,tunda,bumba,daka,] n.k. vilevile fonimu huweza kubadili maana ya neno.
Mfano:
-
Pumba – bumba
-
Funda – dunda
-
Damu – daku
-
Taka – daka
Fonimu
huweza kubatilisha maneno yaani kuyafanya maneno yawe batili kwa jinsi
yalivyoundwa.
Mfano:
-
Kaka – gaka
-
Sasa – thasa
-
Shoga –
shosha
Dhanna ya alofoni
Alofoni
ni nini?
Mgullu
(1999) akimnukuu Hartman (1972) anasema kuwa alofoni ni sauti mojawapo miongoni
mwa sauti kadhaa zinazowakilisha fonimu moja. Alofoni hutokea katika
mazingira mahsusi (mazingira ya kiutoano).
Aidha,
Mgullu (1999) akimnukuu Ladefoged (1962) anasema kuwa alofoni ni matamshi
tofauti tofauti ya fonimu moja. Pia anasema alofoni za fonimu moja
huunda kundi moja la sauti ambazo;
1. Hazibadili
maana ya neno,
2. Hutokea
katika mazingira tofauti ya kifonetiki, na
3. Alofoni
zote hufanana sana kifonetiki.
Kutokana
na fasili hizo, tunaweza kusema alofoni ni maumbo tofauti tofauti ya fonimu
moja, ingawa maumbo hayo huwa na tofauti ndogo ndogo za kifonetiki lakini
hayaleti tofauti yoyote katika maana za maneno.
Tuchukue
mifano ya maneno kutoka katika lugha ya Kiingereza;
tea; eat;
writer;
/thi:/ /i:t/ /raita/
Katika
maneno yetu hapo juu sauti [th] inayotokea mwanzoni mwa neno, na
sauti [t] inayotokea popote ni alofoni za fonimu /t/. Sauti hizi hazibadili
maana ya maneno, zinatokea katika mazingira tofauti na zinafanana sana
kifonetiki.
Katamba
(1996) anasema alofoni zinaweza kujitokeza pia katika maneno:
tea; two; eighth;
/ti:/ /twu/
/eitɵ/
[t]
katika /ti:/ hutamkwa wakati midomo ikiwa imesambaa, [tw] katika /twu/ hutamkwa
wakati midomo ikiwa mviringo na [t] katika /eitɵ/ ni sauti ya meno. Hivyo
[t], [tw] na [t] ni alofoni za fonimu /t/
Katamba,
anasema si kila sauti zenye kubadilishana mazingira basi zaweza kuwa alofoni
katika lugha ya Kiingereza. Kwa mfano sauti /h/ na /ŋ/ hubadilishana mazingira
ya utokeaji (sauti /h/ hutokea mwanzoni mwa silabi ikifuatiwa na
irabu mfano; hat, head, n.k wakati sauti /ŋ/ hutokea mwishoni
mwa silabi katika konsonanti zilizoungana, mfano; longer, long, bung
n.k), lakini hazifanani kifonetiki hivyo haziwezi kuwa alofoni
za sauti moja.
Aghalabu
alofoni hutumiwa katika muktadha au mazingira ya kifonetiki yaliyo tofauti,
ambapo alofoni moja ikitumika katika mazingira fulani basi nyingine haiwezi
kutumika katika mazingira hayo hayo.
Mbinu za kuzitambua fonimu na alofoni.
Kuna
mbinu mbalimbali za kuzibainisha fonimu na alofoni za lugha fulani. Mbinu au
njia hizo ni kama; kufanana kifonetiki, jozi za mlinganuo finyu, mgawanyo wa
kiutoano na mpishano huru.
(i)
Mbinu ya
kufanana kifonetiki.
Mbinu
hii huelezea kwamba sauti ambazo huwa na sifa za kifonetiki zinazofanana basi
huchukuliwa kuwa ni sauti za fonimu moja (alofoni). Kama sauti hazina sifa za
kifonetiki zinazofanana basi huchukuliwa kama ni fonimu mbili tofauti. Kwa
mfano tuchunguze sifa za kifonetiki za sauti /i/ na /u/ katika lugha ya
Kiswahili;
/i/ /u/
+irabu +irabu
+mbele +nyuma
+juu +juu
-mviringo +mviringo
Kwa
mujibu wa kigezo hiki, sauti /i/ na /u/ ni fonimu mbili tofauti katika lugha ya
Kiswahili kwa sababu zina sifa tofauti za kifonetiki.
(ii)
Mbinu ya Jozi
za Mlinganuo finyu.
Kama
anavyoeleza Fischer (1975), mlinganuo finyu ni tofauti ndogo kabisa ya
kifonolojia iliyopo baina ya maneno fulani: aghalabu maneno hayo huwa na;
·
Idadi sawa ya
fonimu
·
Fonimu
zinazofanana isipokuwa moja katika mazingira sawa ya kifonetiki
·
Mpangilio
wa fonimu uliosawa
·
Maana tofauti
Tuchunguze
seti ya maneno yafuatayo;
Pia - lia
Paka - taka
Wali - hali
Katika
seti ya maneno hapo juu tunaona kwamba maneno /pia/ na /lia/ yapo katika jozi
mlinganuo finyu kwa sababu yana idadi sawa ya fonimu, yaani fonimu tatu kila
neno, fonimu zinazofanana isipokuwa moja, na mpangilio wa fonimu ulio sawa na
maana zikiwa tofauti. Halikadhalika katika seti ya maneno /paka/ na /taka/ kwa
sababu nayo yana idadi sawa ya fonimu yaani, fonimu nne zinazofanana isipokuwa
moja na mpangilio wa fonimu ulio sawa. Pia katika seti ya maneno /wali/ na
/hali/ tunaona kuwa yapo katika jozi mlinganuo finyu kwa sababu yana idadi sawa
ya fonimu yaani fonimu nne zinazofanana isipokuwa moja na mpangilio wa fonimu
ulio sawa. Njia hii hutusaidia kuzitambua fonimu za lugha kwa sababu tofauti ya
fonimu moja yatosha kubadili maana za maneno hayo.
(iii)
Mbinu
ya mgawanyo wa kiutoano.
Hyman
(1975) anasema katika fonolojia, utoano ni dhanna ambayo hutumika kuelezea
uhusiano uliopo baina ya sauti mbili (au zaidi) za fonimu moja ambazo haziwezi
kutokea katika mazingira sawa katika neno. Hii ina maana kwamba sauti huwa ina
mahali/mazingira yake maalum ambayo hayawezi kukaliwa na sauti nyingine ya
kundi moja.
Tuchunguze
mifano kutoka katika lugha ya Kiingereza; kuhusu sauti /ph/ yenye
mpumuo na sauti /p/ isiyo na mpumuo. Sauti /ph/ yenye mpumuo hutokea
mwanzoni mwa maneno tu, kwa mfano katika maneno /phin/, /phen/,
/phut/ n.k . Kwa upande mwingine /p/ isiyo na mpumuo hutokea sehemu
yoyote ya neno isipokuwa mwanzoni; mfano katika maneno kama /top/, /cup/,
/span/, /spare/ n.k
Sauti
ambazo ziko katika mgawanyo wa kiutoano huwa hazitofautishi maana za maneno,
isipokuwa sauti hizo hugawana tu mahala pa kutokea au kutumika. Hivyo sauti
hizo huwa ni alofoni za fonimu moja.
Tuchunguze
sifa bainifu za sauti /ph/ yenye
mpumuo na sauti /p/ isiyo na mpumuo;
/ph/ /p/
+kons +kons
+mpumuo -mpumuo
-ghuna -ghuna
+midomo +midomo
+kipasuo +kipasuo
[ph]
yenye mpumuo na sauti [p] isiyo na mpumuo ni alofoni za
fonimu /p/. Sifa zote za sauti hizi zinafanana isipokuwa moja tu (sifa ya
mpumuo).
(iv)
Mbinu ya
Mpishano Huru.
Huu
ni uhusiano wa fonimu mbili tofauti kubadilishana nafasi moja katika maneno
maalum bila kubadili maana za maneno hayo. Hapa mpishano unatumika kwa ile
maana ya “wewe ondoka, mimi niingie.” Kwa kuwa fonimu moja inatolewa katika
neno fulani na fonimu nyingine inakaa mahali pake bila kubadili maana ya neno
hilo. Mpishano huru unahusisha fonimu mbili kubadilishana nafasi moja
katika neno moja. Fonimu hizo huwa ni tofauti kabisa kifonetiki
hivyo hatuwezi kuziita alofoni.
Tuchunguze mifano ifuatayo;
·
/buibui/
na /baibui/ sauti /u/ na /a/ zimepishana nafasi bila kubadili maana ya
neno.
·
/Wasia/
na /wosia/ sauti /a/ na /o/ zimepishana bila kubadili maana ya maneno.
·
/kheri/ na
/heri/ sauti /kh/ na /h/ zimepishana bila kubadili maana ya maneno.
Tuchunguze
sifa bainifu za kifonetiki za sauti /a/ na /u/ katika maneno /baibui/ na
/buibui
/a/ /u/
+irabu +irabu
+mbele +nyuma
+chini +juu
-mviringo
+mviringo
Tuchunguze
pia sifa bainifu za kifonetiki za sauti /a/ na /o/ katika maneno /wasia/
na /wosia/
/a/ /o/
+irabu +irabu
+mbele
+nyuma
+chini +nusujuu
-mviringo +mviringo
Sauti
hizi haziwezi kuwa alofoni kwa sababu zinatofautiana sana kifonetiki. Pia sauti
hizi haziachiani mazingira ya utokeaji wake hivyo ni ngumu sana kuyaelezea
mazingira ya utokeaji wake.
Njia
hizi zitumikapo, aghalabu kwa pamoja, kwa kusaidiana huweza kutusaidia kutambua
fonimu na alofoni za lugha inayofanyiwa uchunguzi.
Alofoni katika lugha ya Kiswahili.
Sasa
tuchunguze dhana ya alofoni kama inavyojadiliwa na wataalamu mbalimbali wa
Isimu ya Kiswahili. Hapa tutaonesha fasili pamoja na mifano ya alofoni katika
lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa wataalamu hao.
Massamba
na wenzake (2013) wanasema alofoni ni sura au maumbo mbalimbali ya fonimu
moja. Fonimu za lugha huweza kupata sura tofauti tofauti kulingana
na mazingira katika neno ambamo hutokea. Hii ina maana kwamba fonimu inaweza
kubadilika ikachukua umbo moja kutokana na kutokea kwake katika mazingira
fulani na inaweza pia kubadilika ikachukua umbo jingine kutokana na kutokea
kwake katika mazingira mengine tofauti katika neno. Wanatoa mifano ya alofoni
kutoka katika lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:
Mofimu
za neno Matamshi
yake
(a) ki+ti ki+refu [kiti
kirɛfu]
(b) ki+ti ki+eusi [kiti ʧeusi]
(c)
u+limi
m+refu [ulimi
mrɛfu]
(d)
n+limi
n+refu [ndimi
ndɛfu]
(e)
n+buzi [mbuzi]
(f)
n+dama [ndama]
(g)
n+gombe [ŋɔmbɛ]
Katika
mifano ya Kiswahili hapo juu, tunaona mabadiliko ya kifonimu
yakijitokeza. Katika
mfano wa (b) fonimu /k/ inapofuatiwa na irabu /i/ halafu
kukawa na mpaka wa mofimu, kisha ikafuatiwa na irabu /e/ hubadilika
na kuwa /ch/ ki+eusi = [ʧeusi] na
katika (d) tunaona wazi kuwa fonimu
/l/ inapotanguliwa na nazali /n/ hubadilika na kuwa /d/ [n+limi =
ndimi]. Halikadhalika katika mifano ya (e) na (g) tunaona kwamba nazali
/n/
inapofuatiwa na kitamkwa /b/ hubadilika na kuwa /m/, inapofuatiwa na
kitamkwa /d/ hubakia /n/, na inapoafuatiwa na kitamkwa /g/
hubadilika na kuwa /ŋ/.
Hii ina maana kwamba katika mazingira haya sauti [ʧ] ni alofoni yafonimu /k/, [d] ni alofoni ya fonimu /l/ na [m], [n] na [ŋ] ni alofani za fonimu /n/(katika fonolijia herufi hii kubwa hutumika kuwakilisha
dhanna ya nazali) na alama /N/ ikiwa kama
kiwakilishi cha fonimu kuu.
Alofoni
hizo hapo juu zimetokana na michakato ya kimofofonolojia (taaluma ya isimu
inayoshughulikia uchunguzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri
maumbo ya mofimu au vipegele vya kisarufi vinavyoathiri maumbo ya fonimu).
Pamoja na kwamba mabadiliko haya yameitwa mabadiliko ya kifonimu lakini
tukichunguza vizuri tutaona kwamba kwa kiasi kikubwa ni maumbo yaliyobadilika
na kwa kiasi fulani ni fonimu.
Kwa
mfano, mofimu ya ngeli ya tisa {-n-} katika majina kama vile nyumba, mbuzi,
ng’ombe, n.k (inabadilika katika mazingira tabirifu) kuwa mofimu {m}, {ŋ} na
wakati mwingine hubaki vilevile {n}. Mchakato huu huitwa mchakato wa au kanuni
ya konsonanti kuathiri nazali. Hivi kwamba mofimu {n} hubadilika na kuwa mofimu
{m} pale inapokuwa imeitangulia sauti ya midomo. Halikadhalika fonimu {n}
hubadilika na kuwa mofimu {ŋ} pale inapokuwa imeitangulia sauti ya kaakaa
laini.
Kwa
mantiki hii basi maumbo haya yote yatakuwa yanaiwakilisha mofimu moja yaani
ngeli ya tisa {-n-}. Kama hivi ndivyo basi maumbo hayo yatakuwa ni alomofu na
si alofoni.
Alomofu
ni mojawapo ya viwakilishi viwili au zaidi vya mofimu moja ambavyo hujitokeza
katika mazingira tofauti ya mtoano. Massamba na wenzake (2012)
Katika
data ambayo imetolewa na Massamba na wenzake kuna baadhi ya sauti ambazo
zinatokana na michakato ya kifonolojia au badiliko la kifonolojia ambapo nazali
huiathiri konsonanti inayoambatana nayo ili kurahisisha matamshi. Sauti
zinazoathirika hapa ni sauti za likwidi (kimadende /r/ na kitambaza /l/).
(a) u+limi
m+refu [ulimi
mrɛfu]
(b) n+limi
n+refu [ndimi ndɛfu]
Sauti
/l/ hubadilika na kuwa kipasuo /d/ katika mazingira ya kutanguliwa na nazali
/n/, vilevile sauti /r/ hubadilika na kuwa kipasuo /d/ katika mazingira ya
kutanguliwa na nazali /n/.
Sauti
hizi zinatokea katika mazingira ya kiutoano na zinafanana sana kifonetiki hivyo
twaweza kuziita alofoni.
Tuchunguze
sifa za kifonetiki za sauti /r/ na /d/, na /l/ na /d/
/r/
/d/ /l/ /d/
+kons +kons +kons +kons
+ufizi +ufizi +ufizi +ufizi
+kimadende +kipasuo +ktambaza
+kipasuo
Mdee (1986), anadai kuwa
sauti [x] na [h] ni alofani za fonimu /h/ kama inavyodhihirika
katika maneno /kheri/ na /heri/.
Tukichunguza sauti hizi,
ni kweli kwamba hazileti tofauti za maana katika lugha ya Kiswahili isipokuwa sauti hizi ni tofauti mno kifonetiki.
Wakati sauti /x/ ni ya kaakaa laini, sauti /h/ ni ya
glota.
Je, sauti moja inaweza kutamkiwa
katika sehemu mbili tofauti?
Matinde
(2012) anasema alofoni ni maumbo mawili au zaidi ambayo huwakilisha fonimu
moja. Anaendelea kwa kusema kuwa alofoni ni matamshi tofauti tofauti ya fonimu
moja ambayo hujitokeza kutegemea mazingira ya utokeaji wa sauti hiyo.
Matinde,
yeye anatofautiana na wanaisimu kama Mdee ambao wanasema lugha ya Kiswahili ina
alofoni kwa kutumia jozi za maneno /kheri/ na /heri/ wakisema /x/ na /h/ ni
alofoni za fonimu /h/. Anasema tukizingatia vigezo vya kutambulisha alofoni,
hizi ni sauti ambazo ni tofauti kabisa kwa misingi ya sifa bainifu za
kifonetiki, hususan jinsi ya kutamkwa na mahali pa kutamkiwa.
Matinde,
anasema alofoni katika lugha ya Kiswahili sawa na lugha ya Kiingereza,
hudhihirika na vipasuo hafifu, hivi kwamba kipasuo hafifu kinapokuwa mwanzoni
mwa neno kutamkwa kikiwa na mpumuo, ilhali kipasuo hicho kinapotanguliwa na
fonimu tofauti hutamkwa bila mpumuo.
Kwa mfano neno /pale/ kipasuo (p)
hutamkwa kikiwa na mpumuo (ph) lakini kipasuo hicho kinapotanguliwa
na fonimu tofauti kwa mfano katika neno /alipo/ kipasuo /p/ hutamkwa bila
mpumuo. Anaendelea kueleza kuwa hali hii hudhihirishwa pia katika maneno;
Neno Utamkaji
Katika /khatika/
Palipo /phalipo/
Panda /phanda/
Kaa /khaa/
Kwa
hivyo, maumbo yote mawili yaani [p] na [ph] ni alofoni za
fonimu /p/. Aidha, maumbo [k] na [kh] ni alofoni za fonimu /k/.
Sauti
alizozionesha Matinde kama alofoni ni vibadala tu katika lugha
ambavyo hutokana na tofauti za kilahaja. Lakini pia mtindo wa uzungumzaji
waweza kusababisha vibadala hivi. Ndio maana si ajabu kukutana na binti wa
kimjini akitamka kwa madaa “palipo uzia penyeza mapenzi”.
Matamshi
yake ni kama; /phalipho uzia phenyeza
maphenzi/
Mpumuo
sio sifa bainifu ya sauti za Kiswahili sanifu. Sifa bainifu za sauti za
Kiswahili ni kama vile; sifa ya ukonsonanti, namna ya kutamka, mahali pa
kutamkia, mkao wa glota na unazali.
MUHADHARA WA IV:
SIFA PAMBANUZI (BAINIFU) ZA VITAMKWA VYA KISWAHILI
SIFA
KUU ZA KONSONANTI
Katika
taaluma ya fonolojia konsonanti zina sifa nyingi, hata hivyo sifa kuu za jumla
ndizo hushughulikiwa zaidi. Sifa hizo za jumla ni jinsi konsonanti
zinavyotamkwa,mahali zinapotamkiwa na kundi asilia la sauti husika.
Sifa
ya jinsi ya matamshi hutusaidia kupata makundi asilia ya konsonanti kama vile
vipasuo,vikwamizi,nazali,vilainisho,viyeyusho na irabu.
AINA ZA SAUTI KONSONANTI
1. Vipasuo ni sauti ambazo hutamkwa kwa mkondo hewa
toka mapafuni kuzuiwa na kisha kuachiwa ghafla.
Mfano:
Aina
|
Ghuna
|
sighuna
|
mifano
|
Vipasuo
vya midomo
|
b
|
p
|
Papai,baba
|
Vipasuo
vya ufizi
|
d
|
t
|
doa, toa
|
Vipasuo
vya vya kaakaa gumu
|
ɟ
|
c
|
Juma, chama
|
Vipasuo
vya vya kaakaa laini
|
g
|
k
|
gunia, kabati
|
2. Vikwamizi ni sauti ambazo hutamkwa kwa mkondo wa
hewa kuzuiliwa nusu hivyo kusababisha hewa kukwamakwama wakati wa utamkaji hewa
hupenya na kupitia katika nafasi iliyowazi.
Aina
|
ghuna
|
sighuna
|
mifano
|
Vikwamizi vya mdomo meno
|
v
|
f
|
Vema, fata
|
Vikwamizi vya meno
|
ð
|
θ
|
Dhanna, thumni
|
Vikwamizi vya ufizi
|
z
|
S
|
Zee, saa
|
Vikwamizi vya kaakaa gumu
|
-
|
ʃ
|
- shamba
|
Vikwamizi vya kaakaa laini
|
ɣ
|
x
|
ghala, kheri
|
3. Vizuio kwamizi ni sauti zenye kutamkwa kwa mkondo
wa hewa kuzuiwa na kuachiwa taratibu kwa kukwama kwama hivyo kuzalisha vizuio
kwamizi.
Mfano:
Aina
|
ghuna
|
sighuna
|
Mifano
|
Vizuio kwamizi vya ufizi
|
ɟ
|
c
|
Juma, chuma
|
Katika lugha ya Kiswahili vizuio
kwamizi ni vichache mno ila vipo katika ya Ibo, Yoruba, n.k
[PΦ],[bβ],[tθ],[dð],[gz]
4. Nazali/Ving’ong’o
Sauti hizi hutamkwa kwa hewa kupitia chemba ya
pua. Wakati wa kuzitamka sauti nazali kaakaa laini hushuka chini na kuzuia
mkondo hewa unaopitia kinywani na kupitia puani.
Sauti nazali pia zipo
ghuna na sighuna ingawa katika Kiswahili nazali zote ni ghuna kwa sababu
hutamkwa kwa msogeano mpana.
Mfano:
Aina
|
ghuna
|
sighuna
|
mifano
|
Nazali ya midomo
|
m
|
-
|
Mama,mtoto
|
Nazali ya mdomo meno
|
ɱ
|
-
|
Mvi
|
Nazali ya ufizi
|
n
|
-
|
Nani
|
Nazali ya kaakaa gumu
|
ᶮ
|
-
|
Nyau
|
Nazali ya kaakaa laini
|
ŋ
|
-
|
Ng’ambo
|
5. Vilainisho (Ligwidi)
Kundi hili linahusisha aina mbili za
sauti ambazo ni vimadende na vitambaza.
(i)
Vimadende- ni
sauti inayotamkwa wakati ala fulani inachezacheza kwenye mkondo wa hewa.
Mfano: /r/ kama katika ramani
(ii)
Vitambaza- ni
sauti zinazotamkwa kwa msogeano wa kubana katikati ya chemba ya kinywa. Hewa
hubanwa na kupita kwenye pembe ya ulimi. Mfano: /l/ kama katika lala
6. Viyeyusho
Ni sauti za kawaida katika lugha ya
Kiswahili na huitwa hivyo kwa sababu vinatokea baada ya maathiriano ya irabu
kuzalisha sauti mpya ambayo hushiriki sifa za irabu na wakati si irabu kwa
asili. Katika Kiswahili viyeyusho ni viwili tu navyo ni /w/ na /y/.
7. Irabu/Vokali/Vokoidi
Irabu ni sauti zinazotamkwa kwa
msogeano mpana n azote ni ghuna isipokuwa kwa baadhi ya lugha za nchi fulani
kama kichina na kijapani.
Uainishaji
wa irabu
Katika kuainisha irabu mambo
yanayozingatiwa ni:
(a)
Mwinuko wa
ulimi
Hapa tunazingatia kama ulimi umeinuka
juu kabisa,juu kiasi,chini kiasi au chini kabisa.
-
Irabu za juu
kabisa (i,u)
-
Irabu za juu
kiasi (e,o)
-
Irabu za
chini kiasi (ɛ, ɔ)
-
Irabu za
chini kabisa (a,ɑ)
(b)
Sehemu ya
ulimi iliyoinuka
Hapa tunaangalia ulimi kama umeinuka
sehemu ya mbele au ya nyuma,hii hutupatia irabu za mbele na irabu za nyuma.
-
Irabu za
mbele ni (i, e, ɛ, a)
-
Irabu za
nyuma ni (u, o, ɔ, ɑ)
(c)
Umbo la
midomo
Utamkaji wa sauti irabu huwa wa umbo
la mdomo mviringo au mtandazwa.
-
Irabu za umbo
mviringo ni (u, o, ɔ)
-
Irabu za umbo mtandazwa ni (i, e, ɛ,
a, ɑ)
Trapeza ya irabu za Kiswahili
i u (Juu kabisa)
irabu
irabu
e O (Juu kiasi) za za
mbele
ɛ ɔ
(Chini kiasi) nyuma
a
ɑ
(Chini kabisa)
NAMNA YA KUBAINISHA VITAMKWA
1. KONSONANTI
Uainishaji wa sauti konsonanti huzingatia vigezo
vifuatavyo.
(i)
Kuanza na
kundi asilia la sauti mf. Kipasuo,kikwamizo, n.k
(ii)
Kutaja endapo
ni ghuna au si ghuna mf. Kipasuo ghuna.....
(iii)
Kutaja mahali
pa matamshi mf. /p/ ni kipasuo sighuna cha midomo
NB: Vitamkwa
ambavyo viko katika makundi yanayojibainisha hayahitajiki kutajwa sifa zake za
kimatamshi (ghuna/sighuna) mf.
-
Irabu zote
-
Nazali zote
-
Vilainisho
-
Ving’ong’o
-
Viyeyusho
2. IRABU
Uinishaji wa irabu huzingatia mwinuko wa
ulimi,sehemu ya ulimi iliyoinuka na umbo la midomo (kama ilivyoelezwa hapo
juu).
UNUKUZI WA KIFONETIKI
Unukuzi wa kifonetiki ni namna ya kuziandika sauti
za lugha kwa kutumia misimbo ya kifonetiki kulingana na ALFABETI ZA KISWAHILI
ZA KIMATAIFA (AKIKI). Mambo ya kuzingatia unaponukuu sauti kifonetiki.
(i)
Zingatia
misimbo ya sauti mf. Ch-C
(ii)
Zingatia
ubora wa sauti inayonukuliwa mf. ɛ # e
IRABU
ZA KUREFUSHA
Irabu
za kurefusha huandikwa kwa kutumia nukta pacha ambazo huwekwa mbele ya irabu
ndefu. Mfano: dagaa huandikwa /dagɑ:/
KWA KUTUMIA SAUTI ZA KIFONETIKI HAPO JUU NUKUU
MANENO YAFUATAYO KIFONETIKI
(i)
Chagudoa = [Caŋgudɔa]
(ii)
King’ongo = [kiŋɔŋgɔ]
(iii)
Maembe = [maƐmbƐ]
(iv)
Malighafi = [maliɣafi]
(v)
Utambulisho = [utambuliʃɔ]
(vi)
Maandalizi = [mɑ:ndalizi]
(vii)
Unyonyaji = [uɲɔɲaɟi]
(viii)
Kinyang’anyiro
= [kiɲaŋaɲirɔ]
(ix)
Kichongeo = [kitʃɔŋgƐɔ]
(x)
Ubabaishaji = [ubabaiʃaɟi]
MATAMSHI NA MOFIMU
Ilivyo
ni kwamba katika baadhi ya mazingira mofimu zinapokubaliana hutokea mabadiliko
mbalimbali ya sauti. Utokeaji huo wa mabadiliko hufuata taratibu maalumu za
lugha inayohusika. Taratibu hizo hujulikana kiisimu kama kanuni au sheria. Kuna
kanuni nyingi za kifonolojia zinazohusu lugha, kila kanuni ni matokeo ya
mchakato fulani.
Michakato na kanuni za kifonolojia
Sauti
zote za lugha ziko katika mpangilio ambao ukikiukwa sauti huathiriana. Kila
kanuni hutokana na mchakato fulani.
Uundaji wa kanuni
Kanuni
huanza kuelezea muundo ndani wa sauti inayohusika kisha huelezea muundo nje wa
sauti hiyo. Muundo ndani ni muundo halisi wa sauti fulani ikiwa katika lugha
yake ya asili na muundo nje ni ule unaojidhihirisha kama sauti hiyo ilivyo
katika lugha ingine mfano: kibantu – Kiswahili.
Ufafanuzi wa kanuni
/x/ [y]/N-
/x/ [y]/-N
/x/
= sauti fulani x
=
inajitokeza kama
[y]
= sauti fulani y
/
= katika mazingira ya
N-
= kutanguliwa na sauti fulani
-N
= kufuatiwa na sauti fulani
Michakato
Kuna
michakato anuwai inayotawala maathiriano ya sauti katika maneno,michakato hiyo
ni:
v Michakato asilia ya kiusilimisho
v Michakato asilia isiyo ya kiusilimisho
1. Michakato
asilia ya kiusilimisho
Michakato asilia ya kiusilimisho ni taratibu
zinazoonesha maathiriano ya sauti katika lugha nyingi duniani.
Usimilisho
wa nazali; ni aina ya
usilimisho ambao nazali huathiriwa na konsonanti inayofuatana nayo
hivyo nazali inasimilishwa yaani hutamkiwa mahali pale ambapo konsonanti
inatamkiwa.
Kwa hiyo, / n / [ m ]/ K-
Hivyo
basi, fonimu nazali / n / inapofuatwa na konsonanti ya midomo inaathiriwa na
kuwa nazali ya midomo ili iendane na konsonanti inayoiathiri.
Mfano
umbo ndani
umbo nje
/n+buzi/
[mbuzi]
/n+bwa/ [mbwa]
/n+papai/ [mpapai]
Usilimisho wa Konsonanti; ni aina ya usilimisho ambao konsonanti
huathiriwa na nazali inayofuatana nayo hivyo konsonanti inasimilishwa yaani
hutamkiwa mahali pale ambapo nazali inatamkiwa. kuna baadhi ya sauti ambazo
huathiriwa na nazali “n” inapokuwa inaandamia yaani kuna sauti ambazo
huathiriwa zinapokaribiana kiasi au moja kwa moja na nazali “n”. Mara nyingi
hutokea katika maumbo ya umoja na uwingi katika maumbo ya maneno
Mfano:-
Umbo
ndani Umbo nje
/n+limi/ [ndimi]
/n+refu/ [ndefu]
Hapa tunaona kwamba sauti [ l ] na [ r ]
zinapokaribiana na irabu na irabu haziathiriki lakini zinapokaribiana na nazali
“n” hubadilika na kuwa “d”
/l/ [d]/N-
/r/ [d]/N-
2. Michakato
asilia isiyo ya kiusilimisho
(a)
Udondoshaji; mchakato huu unahusu kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi wakati
mofimu mbili zinapokaribiana yaani katika mazingira hayo hayo ya sauti ambayo
ilikuwepo hapo awali hutoweka. Kwa mfano irabu /u/ ikifuatiwa na konsonanti
inayofanana nayo kwa sifa za matamshi kama nazali irabu hiyo hudondoshwa, kama
inavyooneshwa hapa chini.
Umbo ndani umbo
nje
/mutu/
[mtu]
/mwalimu/ [mwalim]
/muzito/ [mzito]
/u/ [θ]/M-
(b)
Uyeyushaji; wataalamu wengine huita irabu kuwa nusu irabu. Mgullu (1999),
anasema huu ni mchakato ambao irabu za juu /u/ na /i/ hubadlika na kuwa /w/ au
/y/ katika mazingira ya kufuatiwa na irabu zisizofana nazo. Kwa kifupi ni
kwamba /u/ inapofuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika kuwa [w] na
/i/ ikifuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika na kuwa [y].
Hivyo uyeyushaji ni
kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho kama [w] au
[y], hii ni kwa irabu zote za juu zinapofuatana na sauti zingine zisizofanana
nazo. Na sauti hizo hubadilika katika mazingira ya /u/ hubadilika kuwa [w]
inapofuatana na irabu nyingine isiyofanana nayo na /i/ inabadilika na kuwa [y]
pia inapofuatana na irabu isiyofanana nayo.
Mfano:
Umbo ndani Umbo
nje
/mu+ezi/ [mwezi]
/mu+alimu/ [mwalimu]
/mu+izi/ [mwizi]
/mi+aka/ [myaka]
/Vi+angu/ [vyangu]
/u/ [w]/-I; I
# u
/i/ [y]/-I; I # i
(c)
Muungano/mvutano wa irabu; kanuni hii hutokea pale ambapo irabu ya mofimu
moja inapokabiliana na irabu ya mofimu nyingine katika mpaka wa mofimu irabu
hizo huungana na kuzaa irabu moja, na irabu hizo sharti moja iwe ya chini na nyingine ya juu.
Mfano:
Umbo
ndani umbo nje
/Wa + enye/ [wenye]
/Wa + ingi/ [wengi]
/Ma + ino/ [meno]
/Wa + izi/ [wezi]
/a,i/ [e]/k-k
(d)
Tangamano la irabu; Huu ni mchakato ambao irabu fulani hukubali
kuandamana katika mazingira maalumu. Kwa mfano mofu [i] na [e] katika lugha ya
Kiswahili huonekana kama alomofu au maumbo mbalimbali ya mofu moja ya kutendea
na kutendesha, lakini utokeaji wake hutegemeana na mofu itakayojitokeza katika
mzizi. Kama irabu ya mzizi ni /a/, /i/ au /u/ basi irabu ya
kiambishi cha utendea lazima iwe ni [i] , wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e/ au
/o/ katika kauli ya utendea kiambishi chake kitakuwa ni [e].
Mfano.
Imba --------------imbia
Andika-------------andikia
Funga ------------ fungia
Daka --------------dakia
Oga----------------ogea
Sema --------------semea a
/Utendea/ [i]/-mz+ i
u
(e)
Ukaakaishaji; Mgullu (1999) akimnukuu Les (1984), anadai kuwa ukaakaishaji wa
fonimu hutokea ambapo fonimu zisizo za kaakaa gumu zinapobadilika na kuwa za kaakaa
gumu. Katika Kiswahili sauti za kaakaa gumu zipo mbili tu yaani /ɟ/ na /ʧ/ ambazo ni kwamizi.
Anamalizia kwa kusema kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu
zisizo vikwamizi hubadilika na kuwa vikwamizi. Hii katika ukokotozi wake unakuwa
kama ifuatavyo.
Mfano:
/ki+enu/ [chenu]
/ki+eusi/ [cheusi]
/ki+ombo/ [chombo]
/ki+umba/ [chumba]
Kanuni;
/k/
[ʧ]/-I
Hapa
tunaona kwamba kipasuo cha kaakaa laini /k/ hubadili mahali pa matamshi na kuwa
kikwamizi /ʧ/ cha kaakaa gumu katika mazingira ya kufuatiwa na sauti
irabu /I/
SIFA BAINIFU ZA VITAMKWA
Kila
kitamkwa huambatanishwa na seti ya sifa pambanuzi ambazo husaidia ubainishaji
wa sauti husika. Sifa hizo huwa ni za msingi na za ziada. Baadhi ya sifa kuu za
msingi ni:
1. Ukonsonanti ( + kons); sifa hii
hutofautisha konsonanti na irabu ambapo irabu zote ni (-kons) na konsonanti
zote ni (+kons)
2. Usilabi (+ sil); sifa hii huwekwa
katika vitamkwa vya msingi vilivyo katika muundo wa silabi zote. Usilabi huambatanishwa
kwenye irabu zote pamoja na baadhi ya sauti nazali ambazo huweza kusimama kama
silabi mfano [m] na [n].
3. Usonoranti (+
son); sifa hii huwekwa katika vitamkwa ambavyo vinatamkwa kwa hewa kupita bila
kubanwa katika chemba ya kinywa au pua. Kundi hili hubeba sauti zote ambazo ni:
-
Irabu
-
Viyeyusho
-
Vilainisho
-
Ving’ong’o
Sifa bainifu za ziada za vitamkwa
1. Ukorona (+ kor); hii ni sifa ya sauti
zinazotamwa kuanzia kwenye ufizi kuelekea ndani mf. /r/,/l/,/k/,/g/, n.k
2. Uanteria (+ ant); hii ni sifa inayohusu
sauti zinazotamkwa kwa kutumia ncha ya ulimi na vituta vya ufizi au bapa la
ufizi kuelekea nje mf. /r/ na /l/
3. Umeno (+ meno); hizi ni sauti zinazotamkiwa
kwenye meno mf. /th/,/dh/
4. Uglota (+ glota); sifa hii inahusu sauti za
glota tu mf. /h/, /kh/
5. Ukontinuanti (+ kont); sifa hii inahusu
sauti ambazo huambatana na muendelezo wa kutoka kwa sauti. Mf. /f/,/v/,/s/
Ustridenti
(+ strident); sifa hii huwekwa kwenye sauti zinazoambatana na umuluzi
wakati wa kuzitamka. Mf. /s/,/sh/.
MUHADHARA WA V:
MIUNDO YA SILABI ZA KISWAHILI SANIFU
Silabi
Silabi
ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha
hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Silabi ni kila fungu
la sauti linalotamkika mara moja na kwa pamoja. Kuna aina mbili za silabi,
yaani silabi funge na silabi huru. Silabi huru ni zile
ambazo huishia na irabu.
Kwa
mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.
Silabi funge ni
zile zinazoishia na konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra
kuzipata maana lugha hii inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno
ya Kiswahili yenye kutoka katika lugha nyingine za kigeni na baadhi ya maneno
yenye kuathiriwa kifonetiki kwa irabu zake.
Kwa
mfano: alhamisi – a-l-ha-mi-si; taksi - ta-k-si,mtu-m-tu,nta-n-ta
Miundo ya Silabi za Kiswahili
- Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo maneno katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu peke yake kama silabi. Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u = Au, n.k.
- Muundo wa konsonanti pekee (K) – Kiswahili hakina maneno mengi yanayoundwa na silabi ambazo ni konsonanti pekee isipokuwa maneno machache ambayo huwa ni ya nazali /m/ na /n/ na huwa zinatumika mwanzoni au katikati ya neno. Mfano; m+ke = Mke, m+bwa = Mbwa, n+chi = Nchi n.k.
- Muundo wa konsonanti na irabu (KI) – Katika muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a = Ka n.k.
- Muundo wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika muundo huu konsonanti mbili hutangulia irabu. Mara nyingi konsonanti ya pili huwa ni kiyeyusho. Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k.
- Muundo wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) – Muundo wa namna hii hujitokeza katika maneno machache. Mfano; Bambwa, Tingwa, Tindwa, Mbwa, n.k.
- Muundo wa silabi funge – Huu hujitokeza katika maneno machache ambayo huwa ya kigeni. Mfano; Il-ha-li = Ilhali, Lab-da = Labda,a-h-sa-n-te = ahsante
NB: Silabi hutengwa kwa
kutumia alama maalumu mfano: $ba$, $ma$, $m$, $n$
MUHADHARA WA VI:
MOFOFONOLOJIA
YA KISWAHILI SANIFU
Mofofonolojia/mofofonemiki ni taaluma ya kiisimu inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.
Mofofonolojia/mofofonemiki ni taaluma ya kiisimu inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.
Mfano:
(a)Funga – fungia
(b)Panga – pangia
(c)Piga – pigia
(d)Sema – semea
(e)Soma – somea
Mofofonolojia hubeba
kanuni mahususi zinazoelezea mazingira ya utokeaji wa alomofu. Tofauti ya
kanuni za kifonolojia na zile za kimofofonolojia.
(i)
Kanuni za
kifonolojia hazina vighairi, mf. Hakuna vighairi katika utokeaji wa mkazo
silabi ya pili toka mwishoni mwa neno.
(ii)
Kanuni za
kimofofonolojia huwa na vighairi vingi. Mf. Katika kauli ya kutendea.
- /i/ hubeba utendea iwapo mzizi wa neno unaundwa na
irabu (a,i,u)
- /e/ hubeba utendea iwapo mzizi wa neno unaundwa na
irabu (e,o)
(iii) Kanuni za kimofofonolojia mara nyingi hutegemea
mofimu inayohusika.
KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA
(a) Usilimisho wa nazali; ni aina ya usilimisho ambao nazali huathiriwa na konsonanti inayofuatana nayo hivyo nazali inasimilishwa yaani hutamkiwa mahali pale ambapo konsonanti inatamkiwa.
(a) Usilimisho wa nazali; ni aina ya usilimisho ambao nazali huathiriwa na konsonanti inayofuatana nayo hivyo nazali inasimilishwa yaani hutamkiwa mahali pale ambapo konsonanti inatamkiwa.
Kwa hiyo, n m / - K
Hivyo basi, fonimu nazali / n / inapofuatwa na
konsonanti ya midomo inaathiriwa na kuwa nazali ya midomo ili iendane na
konsonanti inayoiathiri.
Mfano
umbo
ndani umbo nje
n+buzi [mbuzi]
n+bwa [mbwa]
n+papai [mpapai]
(b) Usilimisho wa Konsonanti; ni aina ya usilimisho ambao konsonanti
huathiriwa na nazali inayofuatana nayo hivyo konsonanti inasimilishwa yaani
hutamkiwa mahali pale ambapo nazali inatamkiwa. kuna baadhi ya sauti ambazo
huathiriwa na nazali “n” inapokuwa inaandamia yaani kuna sauti ambazo huathiriwa
zinapokaribiana kiasi au moja kwa moja na nazali “n”. Mara nyingi hutokea
katika maumbo ya umoja na uwingi katika maumbo ya maneno.
Mfano:-
Umbo ndani Umbo
nje
n+limi [ndimi]
n+refu
[ndefu]
Hapa tunaona kwamba sauti [ l ] na [ r ]
zinapokaribiana na irabu haziathiriki lakini zinapokaribiana na nazali “n”
hubadilika na kuwa “d”
l d/N-
r d/N-
(c) Udondoshaji; mchakato huu unahusu
kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi wakati mofimu mbili zinapokaribiana
yaani katika mazingira hayo hayo ya sauti ambayo ilikuwepo hapo awali hutoweka.
Kwa mfano irabu /u/ ikifuatiwa na konsonanti inayofanana nayo kwa sifa za
matamshi kama nazali irabu hiyo hudondoshwa, kama inavyooneshwa hapa chini.
Umbo
ndani umbo nje
mutu
mtu
mwalimu
mwalim
muzito
mzito
/u/ [θ]/M-
(d) Uyeyushaji; wataalamu wengine huita
irabu kuwa nusu irabu. Mgullu (1999), anasema huu ni mchakato ambao irabu za
juu /u/ na /i/ hubadlika na kuwa /w/ au /y/ katika mazingira ya kufuatiwa na
irabu zisizofanana nazo. Kwa kifupi ni kwamba /u/ inapofuatiwa na irabu yoyote
isiyofanana nayo hubadilika kuwa [w] na /i/ ikifuatiwa na irabu yoyote
isiyofanana nayo hubadilika na kuwa [y].
Hivyo uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko
ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho kama [w] au [y], hii ni kwa irabu zote za
juu zinapofuatana na sauti zingine zisizofanana nazo. Na sauti hizo hubadilika
katika mazingira ya /u/ hubadilika kuwa [w] inapofuatana na irabu nyingine
isiyofanana nayo na /i/ inabadilika na kuwa [y] pia inapofuatana na irabu
isiyofanana nayo.
Mfano:
Umbo
ndani Umbo nje
mu+ezi mwezi
mu+alimu mwalimu
mu+izi mwizi
mi+aka
myaka
Vi+angu vyangu
u w/-I; I # u
i
y/-I;
I # i
(e) Muungano/mvutano wa irabu; kanuni hii
hutokea pale ambapo irabu ya mofimu moja inapokabiliana na irabu ya mofimu
nyingine katika mpaka wa mofimu irabu hizo huungana na kuzaa irabu moja, na
irabu hizo sharti moja iwe ya chini na
nyingine ya juu.
Mfano:
Umbo ndani umbo nje
Wa + enye wenye
Wa + ingi wengi
Ma + ino meno
Wa + izi wezi
/a,i/ e/k-k
(f) Tangamano la irabu;
Huu ni mchakato
ambao irabu fulani hukubali kuandamana katika mazingira maalumu. Kwa
mfano mofu
[i] na [e] katika lugha ya Kiswahili huonekana kama alomofu au maumbo
mbalimbali ya mofu moja ya kutendea na kutendesha, lakini utokeaji wake
hutegemeana na mofu itakayojitokeza katika mzizi. Kama irabu ya mzizi
ni /a/, /i/ au /u/ basi irabu ya kiambishi cha utendea lazima
iwe ni [i] , wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e/ au /o/ katika kauli ya
utendea kiambishi chake
kitakuwa ni [e].
Mfano.
Imba
--------------imbia
Andika-------------andikia
Funga
------------ fungia
Daka
--------------dakia
Oga----------------ogea
Sema --------------semea a
//Utendea// i/-mz+ i
U
e
//utendea// e/-mz+
o
(g) Ukaakaishaji; Mgullu (1999) akimnukuu
Les (1984), anadai kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea ambapo fonimu zisizo za
kaakaa gumu zinapobadilika na kuwa za kaakaa gumu. Katika Kiswahili sauti za
kaakaa gumu zipo mbili tu yaani /ɟ/ na /ʧ/
ambazo ni vikwamizi. Anamalizia kwa kusema kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea
wakati ambapo fonimu zisizo vikwamizi hubadilika na kuwa vikwamizi. Hii katika
ukokotozi wake inakuwa kama ifuatavyo.
Mfano:
ki+enu chenu
ki+eusi cheusi
ki+ombo
chombo
ki+umba
chumba
Kanuni; k ʧ/-I
Hapa tunaona kwamba kipasuo cha kaakaa laini /k/
hubadili mahali pa matamshi na kuwa kikwamizi /ʧ/ cha kaakaa gumu katika
mazingira ya kufuatiwa na sauti irabu /I/
(h) Udondoshaji;
wakati mwingine mofimu fulani
huweza kudondoka kutokana na mfuatano wa mofimu katika mazingira fulani.
Mfano:
-
Wanasoma ---------- hawasomi
-
Anasoma ----------- hasomi
-
Nilikunywa -------- sikunywa
//njeo iliyopo// θ/- [ukanushi]
// njeo iliyopita// θ/- [ukanushi]
Wakati uliopo unapokanushwa mofu ya wakati huo
hudondoka na taarifa yake hubebwa na kiambishi tamati kikanushi cha wakati huo.
(i) Uingizaji/uchopekaji; hii ni kanuni kinyume cha kanuni ya udondoshaji.
Hapa mofimu huingizwa mahali ambapo haikuwepo awali. Mara nyingi mofimu hizi ni
zile mofimu mahususi ambazo hufanya kazi ya kuimarisha mizizi ya silabi moja.
Mfano:
-
j---------
anakuja
-
nyw -------
anakunywa
-
f ---------
amekufa
-
l
--------- alikula
θ ku/- j,nyw,f,l
(j) Msinyao;
hii inahusu irabu ndefu ambapo
katika mazingira fulani irabu ya kurefuka inalazimishwa kutokea kama irabu
fupi.
Mfano:
-
Wa-ana
-------- wana
-
Wa –enyewe
---- wenyewe
-
Ma – ema
------ mema
-
Pa – ingi
------ pengi
(a+a) a
(a+e) e