Fonetiki

d) i. Fonetiki
Fonetiki ni kiwango cha isimu kinachojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa
taratibu zote zin
azohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za
lugha za binadamu kwa jumla.
-
Husaidia kuimarisha matamsi bora ya sauti na kwa hivyo kuimarisha matumizi ya
lugha fasaha.
ii. Fonolojia
Fonolojia ni kiwango cha isimu ambacho huj
ishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na
uanishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za
lugha za binadamu.
-
Fonolojia huweka misingi ya jinsi lugha tofauti zinavyotumia sauti chache tu ili kuunda
maneno.
iii. Mofolojia
Mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika
uundaji wa maneno. Vipashio hivyo vya lugha huitwa mofimu.
-
Mofolojia huchunguza jinsi mofimu zinavyofuatana kwa utaratibu unaokubalika ili
kuunda maneno.
iv. Sintaksia
Ni taaluma ya isimu inayochunguza na kuchambua jinsi maneno hupangwa ili kuunda
sentensi za lugha kwa kufuata kanuni za sarufi katika lugha husika.
-
Sintaksia husaidia kuainisha miundo mbalimbali ya lugha na jinsi kanuni za sarufi
hufanya kazi katika miund
o mbalimbali ya lugha.
v. Semantiki
Ni taaluma inayojishughulisha na muundo wa maana katika lugha ya binadamu.
-
Dhima ya lugha ni mawasiliano, hivyo basi semantiki huchunguza jinsi maneno
hupata na kuwasilisha maana ili kuwezesha mawasiliano
Tuzo: Upambanu
zi wa hoja zozote 4 x alama 2 = Alama 8
2.
Zipo sifa nne kuu za uchambuzi wowote wa kisayansi. Sifa hizo ni pamoja na:
a)
Uwazi na Ukamilifu
Dhana hii ina maana kuwa masuala katika isimu huelezwa kwa udhahiri usio na utata. Hoja
huelezwa bila shaka yoyote kimaa
na. Ni sifa inayomtaka mwanaisimu kujiwekea lengo la
kupima kwa uangalifu kila analofanya na kuhakikisha kuwa hoja zake zote anazotoa ili
kutegemeza nadharia zake au mahitimisho yake ziko wazi na zinatokana na utafiti wake.
Wakati uchunguzi unapofanywa huw
a kuna machukulio. Machukulio haya hubainishwa wazi.
Kwa mfano, mwanaisimu anaweza kuchunguza jinsi watu hujifunza lugha za pili na matatizo
ambayo huwakumba. Machukulio ya utafiti kama huu ni kuwa hawa watu wana bongo imara na
razini. Hili inabidi mchungu
zi aweze kulibainisha.
b)
Utaratibu/Upangilifu
Utaratibu ni kufanya mambo kwa mpangilio mzuri wenye kubainika. Utaratibu unaweza
kuhusisha wakati, idadi, umuhimu na hata ukubwa. Kwa mujibu wa sifa hii, hoja za kisayansi
zinapaswa kupangwa vizuri. Taaluma yoyo
te ya kisayansi hufuata utaratibu maalumu na mambo
yake huendeshwa hatua kwa hatua. Wanaisimu huichunguza lugha kwa utaratibu maalumu, si
kiholela.Wanaisimu wamejaribu kuweka mpangilio wa kufuata katika uchunguzi wa lugha.
Mpangilio huu hurahisisha kazi in
ayowakabili. Mpangilio huu unajitokeza katika hatua
zifuatazo:
a)Kutambua tatizo linalohitaji uchunguzi
b)Kuunda nadharia tete
c)Kuchagua nadharia ya kuongoza utafiti
d)Kukusanya data
e)Kuchanganua data
Urazini/Uhoromo/Uhakikifu
Sifa hii pia inajulikana kama utonafs
i au kutopendelea. Huku ni kutazama mambo yalivyo bila
kushawishiwa na hisia. Katika kuzingatia sifa hii, mwanasayansi anapaswa kuhakikisha kuwa
yale anayoyasema, pamoja na mahitimisho anayoyafikia, yanatokana na data zilizo wazi na
ambazo zinaweza kuchung
uzika. Tamko lolote la kisayansi lazima liweze kuthibitishwa na hoja.
Umuhimu wa sifa hii ni kuhakikisha kwamba wanaisimu hawatoi matamko ya juujuu, ambayo hayawezi kuthibitishwa.

d)
Iktisadi
Iktisadi ni sifa ya sayansi inayohitaji uchanganuzi ulenge katika
kutumia vipashio vichache zaidi
kadri iwezekanavyo. Inaeleza kwamba taarifa fupi ni bora kuliko sentensi ndefu ndefu. Imekuwa
kawaida kwa sayansi kutumia fomula na kanuni zilizoandikwa kwa ufupi ili kueleza mambo kwa
usahihi bila kutumia maneno mengi. Kwa
mfano katika somo la Kemia fomula hii inarejelea
‘maji’. Tutatoa mfano mmoja kutoka kwa fonolojia na sintaksia.
 
Isimu fafanuzi haitilii mkazo mabadiliko yaliyotokea katika lugha hata kama mabadiliko haya
yapo. Katika utanzu huu ndipo tunachambua muundo wa sauti za lugha, muundo wa maneno,
muundo wa sentensi, na hata maana za tungo za lugha.
b)
Isimu Histo
ria
Isimu historia ni miongoni mwa matawi makongwe zaidi. Tawi hili ndilo linashughulikia
uchunguzi wa maendeleo na mabadiliko ya lugha kiwakati kutoka kipindi kimoja cha kihistoria
hadi kingine, sababu na matokeo ya mabadiliko hayo. Isimu historia hudhihi
risha mabadiliko ya
sauti, maumbo ya maneno, sentensi, na maana za maneno kihistoria.
Isimu historia ni uchunguzi wa mabadiliko ya lugha katika mapito ya nyakati. Inaangaza jinsi
lugha inavyobadilika katika vipindi mbalimbali, sababu za mabadiliko hayo na
athari zake katika
lugha hiyohiyo na lugha nyinginezo. Tawi hili pia huangalia hatua mbalimbali ilizopitia lugha
katika kukua kwake.
c)
Isimu Linganishi
Hili ni tawi la isimu ambalo linafanya uchunguzi wa lugha mbalimbali ili kuzilinganisha na
kuzilinganua. W
anaisimu huchunguza lugha katika viwango vyote vya fonolojia, mofolojia,
sintaksia na semantiki ili kuonesha na kueleza jinsi lugha hizo zinavyofanana au kutofautiana.
Isimu Linganishi ndiyo imewezesha kubainisha makundi mbalimbali ya lugha. Kwa mfano,
fam
ilia za lugha kama vile lugha za ulaya na za kihindi na makundi mbalimbali ya lugha za
kiafrika. Wanaisimu wanapozilinganisha lugha mbalimbali, hufanikiwa kuunda lugha mame
ya
lugha hizo. Kutokana na hiyo lugha mame mwanaisimu hubainisha lugha hizo na uhus
iano wa
kinasaba na kuonesha jinsi lugha hizo zinavyotofautiana.
d)
Isimujamii
Hili ni tawi la isimu linalochunguza uhusiano uliopo baina ya lugha na watumiaji wake au jamii.
Baadhi ya mambo muhimu ambayo huchunguzwa ni pamoja na sera z
a lugha, lugha sanifu,
usanifishaji, lahaja, rejesta au sajili. Maswali muhimu yanayojibiwa katika utanzu huu ni pamoja
na: nani anasema nini, kwa nani au na nani, wakati gani, kuhusu nini. Wanaisimujamii huamini
kwamba umuhimu wa lugha upo katika matumizi
yake. Hii ndiyo sababu wanachunguza lugha


Powered by Blogger.