MOFOLOJIA YA KISWAHILI


Mofolojia-ni uwanja mdogo ndani ya isimu. Isimu-Ni taaluma inayochunguza lugha ya binadamu kisayansi. Mwanaisimu-ni mwanasayansi achunguzaye lugha ya binadamu katika nafasi zake zote yaani muundo, matumizi yake na nafasi yake katika jamii. Isimu ina nyanja na matawi yake. MATAWI YA ISIMU -Fonolojia -Sintaksia -Mofolojia -Isimu nadharia Nyanja za Isimu hushughulika na jinsi maneno yanavyoundwa. Mfano; mofolojia, fonolojia -Matawi ya Isimu huhusu mikabala ya kuchanganua taarifa mbalimbali za lugha. Mfano; Isimu nadharia huchunguza vipengele mbalimbali vya lugha. MATAWI YA ISIMU ISIMU NADHARIA -Taratibu zinazobuniwa kuwawezesha wachunguzaji fulani wa lugha kufuata taratibu fulani. ISIMU FAFANUZI -Hutoa uchunguzi wa sarufi za lugha na huhusu uchunguzi wa lugha na familia ya lugha fulani na historia ya lugha hiyo katika mazingira yaliyopo ISIMU HISTORIA -Huangalia jinsi lugha ilivyokua hapo awali. Hutumika kulinganisha lugha kulingana na jamii zake ukajua kama uhusiano ni wa umbali au wa ukaribu fulani. ISIMU JAAMII/ANTHROPOLOJIA -Inajielekeza kwenye lugha kama sehemu ya kijamii mbali na jinsia. Huhusisha matumizi ya lugha na watu kama walivyo. ISIMU KOMPYUTA -Huhusu lugha asilia katika matumizi ya kompyuta na kubadilisha kwenda katika lugha ya binadamu kama mfumo. ISIMU HISABATI ISIMU NUROLOJIA -Huhusu misingi ya ki……….. ISIMU NAFSIA -Huhusisha utendaji/kuona jinsi mtoto anavyojifunza lugha, anaanzaje na anaendeleaje. MOFOLOJIA -Ni nyanja ya Isimu inayochunguza maneno na muundo wake. Huchunguza vipashio vinavyohusika na taratibu zinazotumika katika uundaji wa maneno. -Neno huweza kuelezwa kifonolojia, kimofolojia nk. -Neno hutenganishwa na maumbo mbalimbali. Kwa mfano; A-me-ingi-a -Katika neno huweza kuwa herufi au sauti katika uundaji wa neno. Kwa mfano; „m“ -Baadhi ya herufi ambazo huweza kuunda maneno ni kama; ot-, ka-, ki-, pat-, kop-, tek-, chot-, tembe-, nk. -Hapa vipande vingi vinatumika kuunda maneno na haviwezi kutenganishwa zaidi. VIPANDE -Ni silabi ambazo huunganishwa kwa pamoja ili kuunda neno zima. MOFOLOJIA NA FONOLOJIA -Miundo na taratibu zake hizo ndizo huleta tofauti kati ya dhana mbili hizo hapo juu. Mfano; Umbo sauti na sauti- kuna sauti ambayo hutamkwa kwa pamoja ambayo hutoa silabi na kuna sauti ambayo hutamkwa kimoja kimoja au mojamoja. -Mfano; Sauti hutamkwa kwa pamoja –kifonolojia -Sauti kimofolojia- neno sauti ina kipande kimoja ambacho hakiwezi kugawanywa. Mfano;-jina Juma Juma-silabi 2 -Herufi 4 NB: Vipande huitwa hivyo kwa sababu huwezi kuvivunja zaidi katika uundaji wa neno. JINSI YA KUCHANGANUA MUUNDO KIMOFOLOJIA -Ili kuchanganua muundo katika lugha si lazima kujua lugha husika au lugha hiyo. -Jambo la msingi ni kupata orodha ya maneno na kujua muundo wa maneno hayo na namna yanavyoweza kubadilika. Mfano; kitabu- vitabu Hivyo msingi wa kuangalia umoja na uwingi ni msingi mojawapo katika kuchambua muundo wa maneno. 2. Kutazama njeo katika neno -Husaidia kuona miundo inayojitokeza katika neno. Kwa mfano; analala, alilala, atalala, lakini viambishi awali huweza kubadilika kulingana na mazingira yake. Uwepo wa aina ya neno ambalo linaweza kubadilika kuwa aina nyingine ya neno. Mfano; chafu-kivumishi Uchafu-Nomino Chafua-kitenzi -Katika msingi husika hapo juu, mabadiliko hayo huweza kuwa katika mazingira; a) Hali shuruti(condicional variation) Ubadilikaji wa umbo moja hadi jingine hutokana na ushurutishi. Mfano; Cup- Cups Tag- Tags b) Mabadiliko huru Mabadiliko katika lugha mbalimbali zenye mazingira huru haufuati mabadiliko mengine kama vile kuangalia njeo. Mfano; Zapote-Mexico Analala= (R-ahsyab)-lugha ya kawaida = (R-ahsy-ing)-lugha ya exima Pigisha – Pigiza Kwamisha – Kwamiza Katisha – Katiza Hivyo basi, mabadiliko ya hali shuruti ndio ya kawaida kuliko katika mabadiliko huru katika lugha mbalimbali ulimwenguni. -Katika lugha yoyote tunaanza kuona mabadiliko katika vipande -Kuchanganua umbo la neno ni kutaka kujua vipande vya neno, hili ndilo kusudi la kuchanganua muundo na maumbo ya maneno. -Wakati mwingine kugawanya maumbo kwenye vipande ni vigumu kupata/kutatua tatizo. Mfano; neno promise na promised, swear na sworeàNeno hili ni vigumu kulitenganisha kwenye vipande japo ni tofauti na la awali, zaidi hutusaidia kupata ojeo mbalimbali na kubadilika kutoka neno moja hadi jingine. -Kipande huweza kuchanganuliwa katika mazingira mengine. Kina umbo lake. Mfano; be, is , are , were, was, -Hapa “be” kuwa na “is” hutumika kuonyesha umoja, was- mtu mmoja wakati uliopita. -Hayo mazingira yamebadilishwa na njeo pamoja na idadi, pia I na Me ni mazingira yaleyale. -Baadhi ya maumbo yanayobadilika kivipande; Louse-lice, Mouse-mice, sing –sang i) Vipande vinadhihirika ii) Vipande vinabadilika iii) Mabadiliko ya maumbo lakini hakuna nyongeza ya maumbo yoyote. (Ablauti) Mfano; sing-sang-sung hii kitaalam huitwa ABLAUTI kunakuwa hakuna mabadiliko yoyote ya maneno. MFUMO MSONGE WA MUUNDO WA MANENO -Ni mfumo unaohusu uambatishaji wa vipande kuunda neno na inaweza kujitokeza kama ifuatavyo; N / \ Happy-ness | V Maelezo (ma-elez-o) N / | \ Ma elez o Uimbaji (U-imb-a-ji) U – Kiambishi cha hali kamili IMB – mzizi A – Kiambishi tamati maana JI – Kiambishi cha tendo linalojirudia. Mfano; Fasten- Un-fasten-ed Un – inatangulia na ed inafuata, hii ndiyo dhana ya mfumo msonge wa maumbo Uundaji wa maneno huhusu utaratibu zaidi ya viambishi awali na tamati, kuna taratibu nne (4); 1. Taratibu za viambishi kati. Una umbo ambalo kwa kawaida huwezi kuruhusu kipande cha neno kuingizwa katikati. Mfano; Bona- Boine (kihaya) Kiambishi kati kinapenyezwa katika mazingira ambayo haikuwa rahisi kuwepo kipande. 2. Uambatano Maneno mawili huwekwa pamoja kuunda neno, mfano; Churchhyard, blackbird, mlalahoi, mwanajeshi. 3. Uradidi Umbo fulani hurudiarudia kuunda neno jipya. Mfano; barajara, sawasawa, kumbikumbi NB: Viini ni kipande kilicho na umuhimu wa kubeba maana. Viini katika mfomo msonge kwa mfano; -Mwanajeshi-kiini ni jeshi -Mwanaume-kiini ni Ume N / \ Mwana jeshi -Maumbo haya yana matatizo yake katika uchambuzi/uchanganuzi wake kivipande. (Matawi) mfano; vilevile- vile- vile, mbalimbali- mbali- mbali. -Katika maneno haya tunakosa viini vyake. -Kiini ni muhimu katika maumbo yote yanayohusishwa katika kuchanganuzi wa baadhi ya ya maumbo. Lazima kujua kiini cha neno. Mfano; ice cream- hapa lazima kujua aina ya neno kama ni moja au uhusiano wake katika neno. Pia kuna maneno kama churchyard, blackbird, Redwood, sittingroom nk Maneno ya muhimu kujua hapa ni bird, wood, room, yard. Neno- Un happy | | Kiambishi Nomino HADHI YA MANENO -Wakati mwingine kuna nyongeza ambazo hazina uhusiano katika kuunda maneno. KIANGAMI-Ni neno/kineno ambacho hakisimami peke yake ila huning’inizwa mwanzoni au mwishoni mwa neno. Mfano; Mamako -Kuongezwa kwa kipande hicho hakileti hadhi ya kuwa neno na ko haina maelezo yake zaidi ya kueleza maana zaidi. -Hivyo kiangami hakifanyi kazi ya kufanya umbo kuwa neno. -Kwa kawaida katika lugha, sentensi hazina kikomo lakini neno/manenoyana kikomo.i.e. inajikita zaidi katika kutofautiana. MATATIZO YA UCHANGANUZI WA KIMOFOLOJIA -Kuna taratibu ambazo hupelekea matatizo katika uchanganuzi kama ifuatavyo; i) Mofimu kapa -Ni umbo lisilo na alama Dairy huweza kujitokeza katika ngozi ya maneno au ngozi ya sentensi. Afamo; Godoro- Magodoro -Kuna kitu ambacho hakijadhihirika katika neno godoro kuonyesha umoja. -Katika muundo wa sentensi kwa mfano; neno ONDOKA (nafsi ya Pili umoja) inamaanisha mtu fulani aondoke hivyo kutokujidhihirisha lakini kuna kitu kinaonekana kuwa kinatajwa. ii) Mofimu tatizwa -Kuna mofimu ambayo inaanza kisha ikaingiliwa kati na mofimu nyingine kisha ikaendelea baadaye kukamilisha maana. Kwa mfano; absolutely – absobloodylutly MOFOLOJIA NA TAIPOLOJIA TAIPOLOJIA -Ni taaluma ya kiisimu ya kuainisha lugha kwa misingi mbalimbali. -Misingi mojawapo ni ule wa kuangalia mpangilio wa vipashio katika sentensi kuwa kuna kiima na kufuatia na kiarifu, kiarifu na kufuatia kiima, pia kuanza kutambua kiima na kiarifu Mfano; bad boys Wavulana wabaya -Msingi wa kimofolojia unaweza kuainisha lugha katika namna mbalimbali. Kwa mfumo wa kimofolojia hutupatia aina tatu (3); 1. Msingi wa lugha tenganishi (isolate language) -Maneno katika lugha hizi huundwa na kipande kimoja kimoja, kipande hakitenganishwiki. Mfano, lugha ya kichina, Vietnam 2. Lugha ambishi bainishi -Vipande vinawekwa pamoja na kila kipande kina kazi yake. Mfano katika lugha ya kiswahili. Unganishi-unga 3. Lugha ambishi -Jinsi vipande mbalimbali vinavyoungana na kuunda neno. Lugha ya kilatini mfano, Domus-Nyumba yangu. UPAMBANUZI WA UAINISHAJI WA MOFIMU MOFIMU -Ni kipashio kidogo kabisa amilifu katika umbo la neno. Udogo si wa umbo bali hakuna ugawanywaji zaidi ukaendelea hapa na kupata vipande vingine amilifu. Yaani huwezi kupata maana. -Kuna mofimu inayoweza kuwa na herufi moja au zaidi, pia kuwa na urefu au kuwa na sauti zaidi. Mfano; jembe -Katika lugha mofimu hujitokeza katika namna tatu (3) 1. Kiini -Mofimu ni mofimu yenye kubeba maana ya neno husika. Mfano; mti -Hiki kiini huitwa mzizi. 2. Kiambishi -Ni kipande kinachoambikwa/pachikwa kwenye umbo muhimu/neno kuleta maana. 3. Maumbo yasiyogawanyika. -Kuna maumbo yasiyogawanyika, hayaambikwi wala kugawanyika. Mfano; jembe -Utokeaji wa namna hiyo hutupatia aina mbili za mofimu; a) MOFIMU FUNGE -Ni kipande ambacho hakiwezi kusimama peke yake kisarufi. Mfano; m-katika neno mti. M-Ni funge katika mazingira haya ya lugha(sarufi hii) pia umbo t-halina maana, hali kadhalika i, ili kufanya kuwa neno ni lazima yaungane pamoja. b) MOFIMU HURU -Ni maumbo yanayoweza kusimama peke yake kileksika na kisarufi. Hivyo basi ni vyema kujua kinachoitwa mofimu na neno ili kutoa dhana inayoeleweka na kutofautisha. Mfano neno OMBA OMBA -Lina silabi 2 -Lina herufi 4 -Lina sauti 3 -Lina mofimu 2 OA -Lina herufi 2 -Lina mofimu 2 -Lina sauti 2 -Lina sauti 2 Hivyo basi kila sauti inaumbiwa sauti yake katika neno. TOFAUTI KATI YA MOFIMU NA NENO -Kwa mujibu wa JOHN LION (1968) “An introduction to theoretical linguistics” Anaona kuwa neon linafafanuliwa au haliwezi kufafanuliwa kwa, i) Kiotografia-namna neno linavyoandikwa. ii) Kisarufi-kinachowakilishwa na umbo husika. iii) Sauti-maana inayohusika katika neno husika. -Kuna wakati maana na sauti hufanana na pia maandishi na sauti hutofautiana. Mfano; enough-inafu Liuntenant -Tafauti za maandishi na maana hufanya lugha kuwa ngumu kujifunza. -Pia katika kiswahili kuna maneno ambayo huwa tofauti na yanavyoandikwa katika utamkaji wake. Mfano; nje, mba, nge, mbu, ng’ungwe nk -Pia kuna uwezekano wa maandishi na matamshi kufanana. Mfano; kaa(hutamkwa kwa mpumuo) Ikiwa na maana mdudu, kuna dhana nyingi hutokea katika neno hili. Hivyo basi neno huweza kufanana na kutofautiana kimatamshi, kimaandishi na pia kisarufi. Hivyo si kila neno ni mofimu. -Zipo dhana mbili ambazo huhusishwa na mofimu ambazo ni; a) MOFU b) ALOMOFU MOFU -Ni kipashio cha kimaumbo kinachowakilisha mofimu. -Huweza kuwa sauti au herufi. Mfano huweza kuwakilishwa na herufi moja au zaidi, sauti, silabi moja au zaidi. Mfano;godoro-magodoro, kiti-viti ALOMOFU -Ni viwakilishi viwili au zaidi vya mofimu moja lakini hujitokeza katika mazingira fulani / tofauti ya kimtoano. Mfano neno mtu /m/ limejitokeza kutokana na mazingira yake lakini katika mazingira ya m-wa neno /m/ litabadilika. MOFIMU NA UTARATIBU WA UUNDAJI WA MANENO KATIKA KISWAHILI -Utaratibu wa kawaida ni wa uambishaji wa viambishi katika mzizi. -Uambishaji aidha uanze kabla au baada ya mzizi. Ila kwa kawaida viambishi hutanguliwa na mzizi. Mfano; m-ti | |-mzizi Kiambishi -Katika kiswahili mara nyingi mzizi hutanguliwa na viambishi. Vivumishi Mfano; zuri, baya Vitenzi Mfano; pea, pevu Vielezi Mfano; vizuri -Vielezi vikiambishwa hutanguliwa na kiini. UAMBISHAJI -Mchakato wa ujumla wa uambishaji wa viambishi kwenye mzizi. Mfano; promise-promised Connect - connection – connectivity | | | T N V -Uambishaji unahusu dhana mbili; a) Unyambuzi b) Uambatizaji -Kila moja huhusika na utaratibu wa aina tatu; *Kuunda mzizi mpya Mfano; a-na-lala a-nafsi ya tatu umoja na-njeo (Huu ndio uambatizaji) -Neno lala-mzizi-lal Unaweza kupata neno jingine Mfano; lalia-lalika \ / Unyambatizaji -Hupata maumbo mengine ya maneno NADHARIA YA MOFIMU NA MOFOLOJIA YA KISWAHILI -Mofolojia ni kiwango cha kimuundo kati ya fonolojia na kisintaksia. -Inaeleza muundo wa ndani wa neno. -Sintaksia inafafanua jinsi maneno yanavyowekwa pamoja katika sentensi. NADHARIA YA MOFOLOJIA YA KISASA -Inatazamwa katika pande tatu (3); a) Inachunguza vipashio vya msingi vya muundo wa mofolojia. b) Je vipashio hivi vimejidhihirishaje katika muundo wa kimofolojia? (c) Ni kigezo kipi kinatumika kuamua muundo wa kimofolojia? -1940-1950 maswali yamepewa majibu mepesi. -Miaka ya hivi karibuni suala la vigezo limewekwa kando na haya maswali yamejibiwa. -Kati ya mwaka 1940-1950 Maswali mawili ya mwanzo yalipewa majibu. Katika miaka ya hivi karibuni suala la vigezo limewekwa kando na maswali mawili yamejadiliwa sana. -1950 ilikuwa kipindi maalum cha uchunguzi wa kifonolojia. -Hocheti (1954) alibainisha dhana tatu (3); i) Kipashio na mpangilio (item and remarks) ii) Kipashio na mchakato (item and process) iii) Neno na kielezo cha mfumo (Word and paradigms) -Dhana (1-2) ni dhana ambazo hueleza kipashio na mpangilio. -Hapa muundo wa maneno huweza kufanana na maumbo mengine. -Mfano; farmàfarm-er-s= farmers SingàSing-ing=singing -Hapa umbo huongezwa mofimu moja na kuwa nomino. -Vipashio ni vipande vya kisarufi vya kidhahania vyenye kufanana na vipande vinavyojitokeza katika kuunda maneno ambapo pengine maumbo yake ni tofauti kabisa. -Dhana ya kipashio na mpangilio hutoa majibu kwa maswali mawili ya kwanza. -Vipande vinavyojirudiarudia ndivyo huitwa MOFU. -Uchunguzi wa kimofolojia katika kipashio na mpangilio ulihusisha; i) Ubainishaji wa orodha ya vipashio ii) Kubainisha mifuatano ya mofimu iii) Kubainisha mofu inayojitokeza/inayodhihirisha mofimu (uhusiano mkati ya vipengele vya kisarufi vya muundo wa kimofolojia na kifonolojia) Dhana hii ilikosolewa kwa namna mbalimbali; -Kuwepo kwa maneno yasiyogawanyika katika mpangilio maalum. -Kutokana na kukosolewa huku ndiko kulitokea na dhana hizi nyingine mbili; Mfano; Penda-penzi (kuwepo kwa mabadiliko) Mfano; zote hutamkwa katika eneo moja. Gomba- gombi -Kuwepo kwa kipashio kimoja kunaweza kubadilisha umbo jipya. Mfano; ogopa-ogofya -Kipashio na mabadiliko minaanza kueleza mpangilio na kipashio. Mfano; gomvi-gomba Fuata –mfuasi i) Kubainisha umbo la msingi -Kuona kitu kinachoongezwa katika umbo la msingi ambalo linaweza kuleta mabadiliko. Mfano; sing – sang -Kilichochochea mabadiliko ni kuwepo kwa wakati. Mabadiliko ya kimofofonimu -Mabadiliko yanayohusu kimofolojia na kisauti. -Kitu kinapokuwa katika mazingira fulani huchochea mabadiliko. Mfano; mapenzi-mpendwa Penzi-pendo -Kwa nini kumetokea mabadiliko ya “Z” na “D” 3) Dhana ya kielelezo cha mfumo. -Dhana hii kimsingi inahoji kanuni ya alama tenganifu. -Vipashio ambavyo vinaweza kutenganishwa na nafasi yake ikachukuliwa na kipashio kingine. Mfano; Lugha ya kiitaliano UMOJA UWINGI -Donna-Mwanamke Donne-Wanawake -Monte-Mlima Monti-Milima -Raggazo-Kidole Dila-Vidole -Katika Donna-Donne unaweza kutenganisha a na e Je katika mazingira hayo ni nini unaweza kuhusisha na umoja na uwingi? Umoja (Mountenable) Uwingi (Mountenables) New horizons and linguistics Mfano 2; Kiitaliano -Kipashio kimoja kinaweza kuhusisha dhana kadhaa. Mfano; Cantarrebbene- Kama wangeimba(nafsi ya 3 uwingi) Hapa kunajitokeza sharti la nafsi ya 1 Rebberro (kubainisha sharti nafsi ya 3 uwingi kwa mazingira yapi?) Sharti limo katika sauti rre na bbe re bbe rro / | \ | / | \ Nafsi sharti wingi Nafsi wingi nafsi sharti -Dhana hii inakosolewa kwani imejikita zaidi katika kutazama neno na kuvuka mipaka ya kimofolojia. -Ni dhana ipi inaweza kutumika katika maelezo ya kimofolojia. -Dhana ya kipashio na imeonekana kuwa ni mwelekeo zaidi kwa ujumla wake inakwenda mbele ya kipashio na mpangilio. Dhana ya kipashio imekosolewa kwa viwango kadhaa. -Kuchukuliwa kuwa na umbo la msingi -Kuonekana kwa mabadiliko UNYAMBUZI/MICHAKATO YA KIMOFOLOJIA -Katika ligha maneno mapya huingia kwa njia kuu mbili (2); i) Kuingiza maneno kutoka katika lugha nyingine ii) Kujenga maneno kimofolojia hasa maneno yaliyo katika makundi ya wazi. -Kuongeza mofimu kwenye mofimu iliyopo (Unyambulizi) -Mofimu nyambulizi huhitajika kwa namna inayotofautiana na mofimu ambatishi. Mfano; Zuri (V) + M-Mzuri(V) Chek+aàCheka + esha àChekesha Chek + lea àchekelea Hivyo basi tumetumia mzizi “M” kupata maneno mapya U-chek-esh-a-ji àUchekeshaji -Mofimu nyambuzi huongeza msamiati na kuwasaidia watumiaji katika kuwapa uhuru wa kuzungumza. -Kuwepo kwa mofimu nyambuzi katika lugha hakuhusiani na muundo wa sentensi. Mfano; establish + ment àEstablishment. MAKUNDI YA MANENO i) MAKUNDI YA WAZI -Katika lugha kuna aina mbalimbali za maneno ambazo zina taratibu zake ambazo zinafanya ziwe wazi au zimefungwa hivyo tunaweza kupata makundi mawili. ii) Makundi ya wazi na ii)Makundi yaliyofungwa -Aina ya maneno katika lugha ambazo unaweza nkuyaingiza maneno mapya bila kizuizi. Mfano; nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi nk. (iii) MAKUNDI YALIYOFUNGWA Mfano; viunganishi kama vile “na, lakini, walakini nk ni maneno ambayo hayaruhusu maneno mapya kuingia kwa namna mbalimbali. -Viingizi=Maneno yanayotangulia katika kuunda sentensi. Mfano; Yesu na Maria. -Uuundaji wa maneno mapya unahusu ubadilishaji wa maneno kuunda maneno mengine. Mfano; uchekeshaji-ucheshi-vichekesho- vyote ni nomino za aina moja. -Unaweza kupata vivumishi kutokana na kivumishi, nomino, kitenzi nk -Unaweza kunyumbua maneno ya aina mbalimbali, hapa tutaanza na unyambuzi wa vitenzi. -Kitenzi ni maneno yanayotoa taarifa juu ya tendo linalifanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu. -Imefafanuliwa kwa kutilia maanani kama/kwa namna linavyotumika katika sentensi. AINA ZA VITENZI i) Kitenzi kikuu mfano; Analala ii) Kitenzi kisaidizi mfano; Alikuwa analala iii) Kitenzi kishirikishi mfano; Huyu ni mtoto. -Msingi uliotumika katika kuunda aina za vitenzi ni wa kisintaksia sio kimofolojia. -Msingi wa kimofolojia wa uainishaji wa sentensi ni kutazama umbo la kitenzi ambalo linaweza kupatikana katika kamusi. Mfano; la-la Kul-a-la Kuj-a MAUMBO YA VITENZI -Mizizi yenye sauti au herufi mbili Mfano; Ol-a, On-a -Jumla ya maneno Mfano; Pon-a, lal-a -Sauti tatu na herufi nne Mfano; Teng-a, Pang-a -Maumbo ya vitenzi yenye sauti tatu na herufi sita Mfano; Shang-a, Chungu-a -Sauti sita na herufi saba Mfano; Tengam-a -Katika kiswahili kiuna maneno yamekopwa kutoka katika lugha nyingine mfano, rudi, adabu, hakiki nk -Maumbo hayo pia hubeba maana fulani ambapo yanaweza kuwa na sifa mojawapo kati ya hizi mbili; i) Sifa elekezi, huwa ndani ya mzizi. -Kwa kawaida kitenzi hicho huambatana na yambwa nyingine kwa lazima. Mfano; O na a, O- imeruhusu kuandamana na yambwa. iii) Si elekezi- Ni mizizi isiyolazimisha kitenzi kuambatana na kipashio kingine. VIAMBISHI NYAMBUZI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI i) Kiambishi kitendwa. Hiki huwakilishwa na kiambishi “wa” ii) Kiambishi kitendeka. Huwa mna umbo la “ik”, “ek” iii) Kiambishi kitendeshi. Huwa na maumbo ya ish, esh, iz, ez iv) Kiambishi kitendea. Huwa na umbo la i/e, il/el v) Kiambishi kibadilifu (reversive). Huwa na umbo la o/u vi) Kiambishi kifungamanishi (static). Huwa na umbo la am vii) Kiambishi kishikanishi (contactive). Huwa na umbo la al viii) Kiambishi kitenganishi (resprocal). Huwa na umbo la –an- NB: Hivi ni viambishi tofauti na viambishi vingine tulivyoviona. Mfano; Teng-a. a - ni kiambishi kuonyesha dhamira. e - ni kiambishi chenye dhamira ya kimatlaba (kuonesha nia ya jambo)
Powered by Blogger.