Riwaya

Riwaya (kutoka neno la Kiarabu) ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu kuliko hadithi fupi. Urefu wa riwaya, maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, unaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi.
Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni Nagona au Mzingile, riwaya za mwandishi Euphrase Kezilahabi.
Kamusi ya Fasihi iliyotolewa na K. W. Wamitila inataja aina nyingi tofauti za riwaya, k.m. riwaya changamano, riwaya sahili, riwaya kiambo, riwaya ya kibarua na nyingine nyingi.
Powered by Blogger.