Utangulizi wa Lugha na Isimu (Fonetiki)

1.0.Fonetiki ni nini?
Habwe na Karanja (2004) wanasema fonetiki ni taaluma ya kisayansi inayochunguza sauti za lugha ya mwanadamu. Fonetiki hutimiza jukumu hili kwa kuchunguza sauti za lugha ya mwanadamu jinsi zinavyotamkwa, kusafirishra katika kinywa cha mnenaji na sikio la msikilizaji, na jinsi zinavyofasiliwa katika ubongo wa msikilizaji. Ni muhimu kukumbuka kuwa fonetiki hushughulikia sauti zile za lugha ya mwanadamu zinazowezesha mazungumzo kwa ujumla wake bila kujali sauti hizi ni za lugha gani

 
Powered by Blogger.