Fasihi simulizi
Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo mdomo kwa mdomo—kwa mfano utenzi, ngano au nyimbo za jadi—hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.
Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Lakini mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake haiendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.
Hadithi | Ushairi | Semi | Maigizo |
---|---|---|---|
Ngano | Mashairi | Methali | Matambiko |
Vigano | Tenzi | Nahau | Majigambo |
Soga | Tendi | Misemo | Mivigha |
Visakale | Ngonjera | Mafumbo | Utani |
Visasili | Nyimbo | Vitendawili | Vichekesho |
Hekaya | Maghani | Mizungu | Ngoma |
Arafa | Michezo ya jukwaani | ||
Michezo ya watoto | |||
Ngonjera | |||
Semi
Semi ni tungo fupi za kisanaa zitumiazo picha na tamathali kuelezea maudhui yanayobeba mafunzo ya kijamii.Tanzu za semi
Semi ina vipera au tanzu sita ambazo ni:- Methali
- Vitendawili
- Nahau
- Misemo
- Mafumbo
- Mizungu
Methali
Methali ni semi fupi zenye mpangilio maalumu wa maneno ambazo huelezea kwa muhtasari mafumbo na mawazo mazito yanayotokana na uzoefu wa kijamii.Methali huundwa na vipande viwili vya maneno vyenye fikra yurani.Kipande cha kwanza huashilia tendo au sharti na kipannde cha pili huashilia matokeo ya tendo au sharti hilo.
Mifano ya methali
- Mcheka kilema,hali hakija mfika.
- Kupotea njia, ndiko kujua njia.
- Mchelea mwana kulia, utalia wewe.
Kazi za methali
Methali zina kazi nyingi katika jamii yoyote ile kama vile:- Kuionya jamii inayohusika au inayopewa methali hiyo.
- Kuishauri jamii inayopewa au kutamkiwa methali hiyo.
- Kuihiza jamii inayohusika.
- Kukejeli mambio mbalimbali yanayofanyika ndani ya jamii husika.