HISTORIA NA MAENDELEO YA RIWAYA YA KISWAHILI
Kabla
ya kuelezea historia na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili ni vizuri kujua mambo
machache katika kuelezea historia ya riwaya ya Kiswahili kabla ya kujibu swali.
Mambo
ambayo yanafungamana na chimbuko la riwaya ya Kiswahili ni nini maana ya
riwaya, riwaya Kiswahili ni ipi, ukubwa wa riwaya, ugumu au wepesi wa riwaya.
Riwaya
ni utanzu mmojawapo tu kati ya tanzu za fasihi andishi ambazo hujumuisha
tamthiliya, hadithi na ushairi (mkacha na madumulla, 1991:1).
Rwaya ni hadithi zinazotokana na sisi wenyewe,
njozi za binadamu kuhusu maisha yake, pia ni mawazo anayo yaunganisha mwandishi
kutokana na ujuzi alionao (Mlacha na madumulla 1991:1).
Wamitila,
(2003), anasema riwaya ni kazi ya kinathari au kubinilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha.
Msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye
kuchukua nafasi / muda mwingi katika maandishi na kuhusisha mandhari maalumu.
Riwaya
ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya Kiswahili maana
watunzi wengi wamekuwa wakiandaa kazi zao wakirejelea utamaduni na mila
wanazozifuata au kuziamini.
Kuna
wataalamu mbalimbali wamejaribu kuelezea kwa kina juu ya riwaya ya Kiswahili,
ili kutupatia jibu au maana ya riwaya ya Kiswahili.
Mlacha
na madumulla, (1991:10), wanasema la muhimu hapa ni kuzingatia kuwa tunapozungumzia
riwaya ya Kiswahili tuna maanisha riwaya zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Riwaya
ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili……………
Senkoro (2011), anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi
ya kiutamaduni.
Mahundo
na Balosidya ( 1976:62), wanasema riwaya ni kazi ya kubuni, ni hadithi ambayo
hutungwa kufuatana na uwezo wa fanani. Kuibusha mambo kutokana na mazoea au
mazingira yake.
Ukubwa
wa riwaya, unaweza kuwa wa kurasa zozote zile kwani si idadi ya maneno au
kurasa tu ambavyo vitatufanya tuiite hadithi fulani kuwa ni riwaya na nyingine
kuwa hadithi fupi, zipo riwaya kana Nyota ya rehema (1981), yenye maneno zaidi
ya 54,000, kiza katika nuru, (1988), amnayo ina maneno kama 93,000, vilevile
kuna riwaya kama vile Bwana Myombokera na Bibi Bugonoka (1980), ambayo ndio
riwaya ndefu kuliko zote hivi sasa na inamaneno zaidi ya 195,000 (Mlacha na
Madumulla, 1991:1).
Riwaya
haitambuliki kutokana na ugumu au urahisi wa hadithi hiyo kwani Ngona (1988)
ambayo inaonekena ni tata kuliko Asali chungu (1977), bado ni riwaya. (Mlacha
na Madumula, 1991:2)
Riwaya
tupi kama vile Nagona inaweza kuonekena ngumu zaidi kuliko hata Bwana
Myombokera na Bibi Bugonoka, kwani urahisi au ugumu wa hadithi hutegemeana na
mambo mengi, ikiwa ni pamoja na msomaji mwenyewe, ujuzi wake kuhusu maisha na
lugha, uzoefu wake na mapenzi yake kuhusu hadithi. Vilevile inategemea ufudni
wa mwandishi katika kuelezea hadithi yake na uhusiano kimawazo baina yake na
wasomaji wanao tarajiwa n.k. (Mlacha na Madumulla, 1991:2).
Tukianza
kuzungumzia historia ya riwaya ya Kiswahili ni nuhimu kuhihusisha sana na
fasihi simulizi. Uhusiano huu sio wa kimuundo, ingawa muundo wa masimulizi
ulichangia kwa kiasi fulani katika riwarya nyingi za mwanzo, lakini zaidi ni
uhusiano uliotokana na uandikaji wa hadithi za Kiswahili. Edward Steere
alipokusanya na kuhariri hadithi alizozipata kutoka kwa wakazi hadithi alizozipata
tutoka kwa wakazi wa Zanzibar unaweza kuwa ndio wakati wa kwanza kuangalia
histori ya riwaya yetu ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:11).
Historia
ya riwaya ulimwenguni haina muda mrefu sana hasa inapolinganishwa na historia
ya tanzu nyingine za fasihi kama vile ushairi, tamthiliya ya fasihi simulizi
(Mlacha na Madumulla, 1991:7).
Historia ya riwaya ya Kiswahili nayo
haikupishana sana na hali hiyo ya kutanguliwa na tanzu nyingine za fasihi (
Mlacha na Madumulla, 1991:7).
Historia
ya riwaya ya Kiswahili imeangaliwa katika sura tofauti na wataalamu na watafiti
mbalimbali (Mlacha na Madumulla, 1991:8).
TUKI,
(2004:48), inasema chimbuko maana yake ni mwanzo au asili, tanzu za asili zinaonesha
kuwa ndio zinachangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibia riwaya za Kiswahili.
Na
yafuatayo ni mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya historia ya riwaya ya
Kiswahili.
Wapo
wataalamu waliyoiangalia historia ya riwaya ya Kiswahili pamoja na historia ya
fasihi ya Kiswahili kama vile Rollins, 1993 (Mlacha na Madumulla, 1991:8).
Wapo
wataalamu ambao wameangalia/ wamegusia uandishi wa hadithi (riwaya) za
Kiswahili kama vile Balisidya (1976), senkora (1977), 1989), Ohly (1981), na
mengine wengi ( Mlacha na Madumulla, 1991:8).
Baadhi
wanaiangalia historia hiyo kuanzia mwishoni mwa karne ya kumi na tisa (19), ambao
ni pamoja na Rajmund Ohly (1981), na wenzake wanaangalia historia ya riwaya ya
Kiswahili wakati wa Edward Steere, ambaye mwaka 1870 alikusanya simulizi na
mwenyeji wa Zanzibar na kuzihariri. Hadithi hizi zilikusanywa na kuandikwa kwa
lugha ya kingereza. Wataalamu hawa wanaiangalia historia ya riwaya kuanzia
kwenye chanzo chake na vilevile kuanzia kwenye hatua za mwanzo katika maendeleo
yake (Mlacha na Madumulla, 1991:8).
Wapo
wataalamu wengine ambao wanaona kuwa historia ya riwaya ya Kiswahili ulianza
robo ya kwanza ya karne ya 20 ambapo vitabu kama vile, mwaka katika minyororo
(Mary Sehoza, 1921), viliandikwa. Mtaalamu mwingine aliyeungu mkono hoja hii ni
Senkroro (1976), walichangia hoja hiyo wakiwa wametanguliza kitabu cha James
Mbotela (1934), cha uhuru wa watumwa kuwa ndicho kilichoweza kuchukuliwa kama
mwanzo wa historia ya riwaya ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:8).
Senkoro,
(1976:75), anasema kuwa ……………………. Riwaya ya Kiswahili ndipo hasa ilipoanza wakati
James Mbotela alipoandika uhuru wa watumwa. Hii ndio ilikuwa riwaya ya kwanza
ya Kiswahili nayo ilikuwa na mandhari ya hukuhuku Afrika Mashariki, wahusika
walikuwa waswahili, na mandhari yake
yaliwahusu waswahili kwa jumla, waandishi mwenyewe alikuwa mswahili.
Wapo
wataalamu wengine ambao wanadai kuwa historia ya riwaya ya Kiswahili
imefunguliwa mlango na Shaaban Robert. Wataalamu hao ni akina Elena Bertoricini
(1983:85), Shegov (1976), na Rollins (1983) (Mlacha na Madumulla, 1991:9).
Hawa
Rollins, (1983), Shegov, (1976) na Elena Bertoncini (1983:85), wanaichukulia
historia ya riwaya ya Kiswahili katika hatua yake ya juu kimaendeleo na kuacha
pengo kubwa ambalo ndilo hasa lililoweka msingi wa kukua kwa riwaya ya
Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:9).
Kwa
mtazamo wangu historia riwaya ilianza tangu karne ya kumi na nane kipindi
ambacho Steer E. alipokuwa anakusanya hadithi fupifupi kwa wenyeji wa Zanzibar
kwani hapa ndio ilikuwa hatua ya awali ya kuijua na kuiandika riwaya ya
Kiswahili.
Baada
ya kuangalia kwa kina historia ya riwaya ya kiswahili tangu kwenye chanzo chake
ni vyema tukaingia kujadili maendeleo ya riwaya ya Kiswahili mpaka hapa
ilipofika na ikiwezekana kubashiri ni wapi inapoelekea au itafika baada ya
miongo mitatu au mine ijayo.
Kuna
wataalamu mbalimbali wamejaribu kuelezea maendelo ya riwaya ya Kiswahili na
katika mjadala huu nitajaribu kuelezea
wachache ili kuona maendeleo ya riwaya ya Kiswahili kwa Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla.
Katika
kuelezea riwaya ya Kiswahili, waingereza walitilia mkazo hadithi fupi na
masimulizi mengine (Mlacha na Madumulla,1991:12).
Maendeleo
ya riwaya ya Kiswahili yanameza kugawanyika katika vipindi tofauti tofauti kama
ambavyo wataalamu mbalimbali wanaelezea na kujaribu kugawa kama ifuatavyo:-
Kipindi
cha kwanza katika historia ya riwaya ya Kiswahili kinaishia mwaka 1910, kipindi
cha pili (1910 – 1920), kipindi chabtatu mwaka 1929. (Mlacha na Madumulla,
1991:12).
Mwaka
1920 Heller A. B na wenzake walianzisha vijigazeti ambavyo viliandika hadithi
tofauti. Hadithi hizi ziliweza kuwafikia wenyeji wachache ambao walikuwa na
ujuzi wa kusoma (Mlacha na Madumulla 1991:12),
Wahariri
wa magazeti walitoa hadithi katika magazeti kama vile mamboleo, walimwengu na
mengine machache hadithi zilizotolewa ni Kama vile “kibaraka”, sultan zuwera”,
Asha Binti Fulani, na nyingine nyingi. Hadithi hizi ziliwapa waandishi wenyeji
nafasi ya kujitokeza katika uandishi na kujifunza kujieleza kifasihi na
kifasaha. Mnamo mwaka 1921 hadithi kama vile mwaka katika minyororo, tuliyoyaona
na tuliyofaya uingereza, viliandikwa na waandishi wenyeji wa mwanzo kama vile
Sehoza na Kayamba (Mlacha na Madumulla 1991:12-13).
Kuundwa
kwa kamati ya lugha ya Afrika mashariki mnamo mwaka 1929, kazi ya Kamati hii
ilikuwa na nafasi kubwa sana katika kuendeleza lugha ya Kiswahili fasihi ya
Kiswahili. Mmoja wa wanakamati hii alikuwa ni hayati Shaaban Robert, ambaye
alikuwa ni mwanafasihi na mwandishi maarufu mno katika Afrika ya mashariki kwa
kazi zake mbalimbali kama kusadikika (1951) Adili na Nduguze (1952), utubora mkulima
(1968), maisha yangu (1966), siku ya watenzi wote (1968), (Mlacha na Madumulla, 1991:13).
Ripoti
ya magavana, tukirejea katika historia kipindi hiki nchi za Afrika mashariki
zilikuwa bado zinatawaliwa na mataifa ya kibepari, Tanganyika na Ujereumani
Uganda na Kenya Uingereza wakati Zanzibar ili kuwa chini ya utawala wa Sultani,
ambayo ilionesha umuhimu wa kuwa na Kiswahili katika shule na kuwa na Lugha
sanifu ambayo ingetunika katika
kujieleza kifasaha na kifasihi ilikuwa ni ripoti muhimu katika maendeleo na
hitoria ya riwaya ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla 1991:13).
Kuanzishwa
kama shirika la uchapishaji wa riwaya fupi za Kiswahili na kitabu cha mwanzo
kilikuwa mwaka 1950 , kitabu kilichoitwa Mwarabu na binti yake. Waandishi
maarufu kama vile Shaaban Robert walijitokeza na kuandika (Mlacha na Madumulla,
1991:13).
Shirika la uchapishaji vitbu la
Afrika Mashariki (EACB) lilianzishwa mwaka 1948 ili kushughulikia uchapishaji
wa vitabu shirika hilo lilipewa muhuri wa udhibiti wa maandishi, na kati ya 1948
na 1960 lilichapisha karibu vitabu 1000 kwa ajili ya shule na wasomaji wa
kawaida kulikuwa na vitabu vya hadithi , hasa za kingano, hekaya na visa hapa ndipo
Riwaya ya Kiswahili zilizopevuka zilianza kuchapisha miaka kumi baadaye. Riwaya zilizoanza kupevuka
kipindi hicho ni Farsy , kurwa na Doto (EACD 1960) na M.S Abdulla, Mzimu wa
watu wa kale (EACB 1960) (Mulokozi 1996: 164).
Kazi
za fasihi ya kizungu zilianza kutafsiriwa kwa Kiswahili kuanzia mwishoni mwa
Karne ya 19, mfano wa kazi hizo ni C.Kingslay, mashujaa Hadith za wayunani 1889
Wakati
wa ukoloni zilitafsiriwa kazi nyingi
zaidi za kigeni , mathalani, Banyan, J, Safaari za msafiri (Pilgrim’s progress)
S.P.C.K, London 1925), Hekaya za Abunuwas (Msafii S. chiponde, Macmillan 1928)
na kazi nyingine muhimu zilizofasiriwa ni baadhi ya tamthiriya za Willim shakespear
kama Mfanya Biashara wa Venisi katika mtindo wa kinathari (Mulokazi 1996:164).
Mwaka 1930, uandishi katika lugha ya Kiswahili
ulihimizwa kwa njia ya mashindano ili tokana na agizo la kamati ya lugha ya
Afrika mashariki kuanzisha mwaka 1929 na kutokana na mashindano hayo, riwaya ya
kwanza ya Kiswahili , Uhuru wa watumwa
(James Mbotela 1885 - 1976), ilichapishwa mwaka 1934. Baadaye baadhi ya riwaya
zilitoka kwa mfano M.S Abdulla, mzimu wa watu wa kale (EACB 1960), na faraji
Katambala, simu ya kifo (EACB 1965), zilitokana na mashindano ya utumwa
yaliyoendesha na kamati hiyo (Mulokazi 1996:164).
Miaka
thelathini iliyofuata baada a uhuru wa watumwa inayoaminika kuwa ndio riwaya ya
kwanza ya Kiswahili na James M, (1934). Ilitawaliwa na kazi za Shaaban Robert
(1909 – 1962), Riwaya yake ya kwanza utubora Mkulima (Nelson 1968) yasemekana ilitungwa mwaka
1946, lakini laikuchapisha hadi mwaka 1968. Riwaya iliyofuata ni kufikirika
(OUP 1968) iliyoandikwa mwaka 1947 na kuchapisha mwaka 1967. Riwaya ya tatu , kusadikika (Nerson
1951) ilichapisha mwaka 1951 na ya nne Adili na Nduguze (Macmillan, 1952) ilichapisha
mwaka 1952. Riwaya yake ya Mwisho , siku ya watenzi wote (Nelson 1968) iliandika kama 1960 – 62 na
kuchapisha mwaka 1968 karibu riwaya zote za Shaaban Robert
ziliathiriwa na ngano na hekaya, hasa katika muundo wake na uchoraji
wa wahusika (Karibu wahusika wote ni bapa) (Muokozi 1996:164).
Kipindi
cha miaka ya 1960 (1960’s) kwa afrika
swala kuu lilikuwa ukombozi wa bara la Afrika na ujuzi wa jamii mpya baada ya
uhuru . Hivyo palitokea riwaya za kisasa na kifalsafa zilizojadili maisha,
utawala, na ujenzi wa jamii mpya. Riwaya za wakati huo zilijaribu kuelezea
jamii katika mkondo wa ubinadamu usawa na ustawi mfano wa riwaya hizo
Shaaban Robert, Utubora Mkulima na siku
ya watenzi wote (Mulokozi , 1996: 164).
Kuibuka
kwa riwaya pendwa katika miaka 1960, hii ili changia maendeleo ya riwaya ya Kiswahili kwani watu wengi walijotokeza
kusoma kazi mbalimbali ambazo zilipendwa
na wasomaji miongoni mwa riwaya hizo ni Ms. Abdalla, mzimu wa watu wa Kale na
Kisima cha Giningi (Evans,1968), (Mulokozi, 1996:165).
Miaka ya 1970, riwaya Kiswahili imepevuka
kupanuka zaidi mambo makuu yanayoipambanua riwaya ya kiswahili katika kipindi
hiki ni: (mulokozi 1996:165).
Kutokea
kwa watunzi wapya, vijana ambao wameipa
uhai mpya riwaya baadhi yao ni E. kazilahabi (KZ 1944), Shafi Adam Shafi (kuz 1940 ), M.S Mohamed (Kuz 1943), AJ.
Safari kuz 1951), na B. Mpalal, (Kuz 1957).
Kuongezeka
kwa riwaya – pendwa ambako kuliambatana
na kutokeza kwa wachapishaji waandishi kama John Simbamwene na E. Musiba ambao
waliandika na kuchapisha riwaya zao wenyewe. Watunzi wa riwaya pendwa katika kipindi hiki ni E. Musiba, Ben
Mtobwa, J. Mkabarah, C. Merinyo, Mbunda
msokile (1950 – 1995), (Mulokozi, 1996:165).
Kujitokeza
kwa riwaya inayohakiki jamii kwa undani, wengine wameiita riwaya
ya uhakiki miongoni mwa waandishi hao ni shafi A. shafi, kasri ya mwinyi
fuad (TAH 1978), na kuli (TPH 1979), E.
kazilahabi, Dunia uwanja wa fujo (EACB
1975), G. Ruhumbika, Miradi Bubu ya wazalendo
(ERB 1992) . (Mulokozi, 1996:165).
Kuongezeka
kwa riwaya za vijana na watoto, P. Shija mashujaa wa kaza kamba. (TPH 1978) na
vijana Jasiri (TPH 1980) M.M Mulokozi ngoma
ya mianzi (MPB 1990), Ngoma ya
mianzi (TPH 1991) na moto wa mianzi (ECHOL 1995) (Mulokozi,
1996:165).
Kuzuka
kwa riwaya ya wana kisomo, hii ni riwaya inayoandika mahususi kwa ajili ya
wanakisomo wa madarasa ya elimu ya watu wazima na sifa za riwaya hiyo ni fupi,
sahihi kimuundo, huwa na lugha rahisi, maudhui yake ni sahihi lakini ya kiwango
cha watu wazima (Mulokozi 1996:166).
Kuanzisha
kwa taaluma ya uhakiki wa fasihi ya Kiswahili, taaluma hii ilianza kufundisha
baada ya kuanzisha kwa idara ya
Kiswahili katika chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 1968 mnamo mwaka 1970, taaluma ya uhakiki imeenezwa mashuleni
kote nchini , Taanzania na 1980 ilienezwa Kenya. Baadhi ya wahakiki mashariki
ni kezilahabi 1976, Topan 1971, 1977; Sengo na Kiango 1973, 1994, TUKI 1983,
Madumulla 1986; Mlacha 1990 , wamitila 1991 , msokile ni 1992 (Mulokozi 1996;
167).
Mwhisho
katika mjadala nimejaribu kuelezea kwa kina historia na maendeleo ya Kiswahili
katika vipindi totauti bila kusahau
chimbuko la riwaya kwa ujumla. Tunaweza
kuona kuwa riwaya ya Kiswahili imepita katika mikabala mingi mpaka katika karne
hii ya 21.
MAREJEO
Abdalla,
Ms. (1958), Mzimu wa watu wa kale . E.A.L.B Nairobi.
Mbunda
M. (1992) , Kunga za fasihi na lugha, EPD , Dar es salaam
Mhando
wa Balisidya (1976) Fasihi na sanaa ya
maonyesho .T.P.H Dar es salaam.
Mlacha
S.A.K na Madumula J.S (1991), Riwaya ya Kiswahili, University press Dar es
salaam
M.M
, Mulokozi (1996) , utangulizi wa fasihi ya Kiswahili, chuo kikuu huria Dar es
salaam
Ndungo
C. W na wangani M (1991),Misingi ya nadharia za Kiswahili, universityof
Nairobi,Nairobi, Kenya.
Robert,
S. (1952), Adili na nduguze, Macmillan
Co. Nairobi
Robert,S.
(1951) , Kusadikika, Nelson Nairobi
TUKI
(1983), Miaka ya semina ya Kimataifa ya waandishi wa Kiswahili 2: Uandishi wa
uchapishaji , TUKU, Dar es salaam.
Uganda,
P. (1959) ufunguo wenye Hazina, Evans
Brothers.