IRABU

2.5. Irabu


Tumesema hapo mwanzo kuwa tofauti kati ya utamkaji wa irabu na ule wa konsonanti ni kuwa utamkaji wa irabu hauandamani na mzuio wowote wa mkondo-hewa, yaani hewa hupita kwa urahisi bila kuzuiliwa. Hivyo migawanyo ya irabu haitegemei mzuio wa.hewa, bali hutegemea sana rnkao wa ulimi katika kinywa wakati wa utamkaji, na pia mkao wa midomo wakati huo. Kwa sababu hizi, irabu hupangwa kufuatana na vigezo vitatu: Ulimi uko juu kiasi gani kinywani (ujuu); ni sehemu gani ya ulimi inainuliwa au kushushwa (umbele); na midomo ikoje wakati huo (uviringo).
i) Ujuu
Wakati wa kutamka irabu-juu ulimi unakuwa umeinuliwa juu katika kinywa, ambapo irabu-chini hutolewa wakati ulimi umeteremshwa chini. Irabu-juu ni kama [i, u], na irabu-chini ni kama [a]. Ulimi ukiwa katikati ya kinywa, irabu zinazotolewa huitwa irabu-kati, nazo ni kama [e, o].
ii) Umbele:
Wakati ulimi unainuliwa kinywani, unaweza kupelekwa mbele katika kinywa, na hivyo kutolewa irabu-mbele kama [i, e]. Ikiwa ulimi utarudishwa nyuma, basi irabu zitolewazo zitakuwa irabu-nyuma, kama [u, o]. Irabu [a] kama ya Kiswahili hutolewa ambapo ulimi hauko mbele au nyuma, bali uko katikati.
iii) uviringo
Wakati wa utamkaji wa irabu, midomo inaweza kuviringwa, na irabu zitakazotolewa zitakuwa viringo, kama [u, o]. Midomi inaweza kusambazwa au kupanuliwa na hivyo kutoa irabu siviringo, kama [i, e, a].
Irabu ziko nyingi sana zaidi ya hizi ambazo tumetolea mifano, na kila lugha inayo idadi tofauti. Lakini sifa za irabu hizo, kwa kiwango kikubwa, zinaafiki mgawanyo uliotolewa hapa. Kiswahili ni kati ya lugha ambazo zinatumia irabu chache sana katika mfumo-sauti wake, nazo ziko tano kama zinavyoonyeshwa hapa chini:
Kielelezo III: Irabu za Kiswahili
i
u
e
o
a
Irabu hizi huwa zinapewa sifa zifuatazo:
[i] irabu juu mbele siviringo
[u] irabu juu nyuma viringo
[e] irabu kati mbele siviringo
[o] irabu kati nyuma viringo
[a] irabu chini siviringo
Lugha zilizo nyingi zinazo irabu zaidi ya tano. Wanafonetiki wanaziwakilisha irabu hizi kwa namna tofauti kwa kila lugha ili kuonyesha tofauti na uhusiano uliopo baina yao. Hata hivyo kuna makubaliano ya kutosha kuwa irabu za msingi ziko nane, na kwa zile lugha zilizo na zaidi ya irabu nane, zile za ziada zinaweza kuwekwa katika nafasi zilizopo kati ya irabu msingi. Kifuatacho ni kielelezo cha irabu-msingi:
Kielelezo IV: Irabu Msingi
(1)
i
u
(8)
(2)
e
o
(7)
(3)
e
f
(6)
(4)
a
a
(5)

Katika kielelezo hiki irabu [e, o] zinajulikana kama nusu-juu, na [e, f] ni nusu-chini, ambapo [a, a] ni za chini. Kielelezo pia kinaonyesha kuwa irabu mbele zote ni siviringo, ambapo irabu nyuma zote ni viringo isipokuwa [a]. Lakini kuna lugba chache ambazo zinakuwa na irabu-mbele viringo, na irabu-nyuma siviringo, hizo nazo hupangwa mahali pake katika kielelezo. Kwa mfano:
[ü] ni irabu juu mbele viringo
[ö] ni irabu kati mbele viringo
[L] ni irabu kati nyuma siviringo, n.k.
Kama tulivyofanya katika kuchunguza konsonanti, sehemu hii ya irabu pia imefupishwa sana, na kuna mambo mengi ambayo yameacbwa, na mengine yemegusiwa tu. Kwa mfano, tulivyokuwa tunaangalia namna ya utamkaji kwa ujumla, tulisema kuwa kwa kawaida irabu ni ghuna na sing’ong’o. Lakini tukasema kuwa bata hivyo zipo lugba ambazo zina irabu sing’ong’o na ng’ong’o; na pia zipo ambazo zina irabu ghuna na sighuna. Katika sehemu hii, hatukuelezea jinsi irabu hizo zinavyotokea. Katika uchambuzi kamili wa kifonetiki ingekuwa muhimu kuelezea yote hayo. Sehemu hii imeweka tu misingi ya uchunguzi. Mambo mengine ambayo hayakugusiwa hapa ni pamoja na ‘urefu’ katika irabu. Kwa mfano, tunaweza kuuliza ikiwa ‘urefu’ wa neno <taa> katika Kiswahili ni sawa na wa neno <toa>. Yaani, katika utamkaji, je, <taa> linatamkwa [taa] au [ta:]? Matamshi ya kwanza yanaonyesha kuwa [aa] zote mbili zina hadhi sawa na hivyo kutamkwa kama mfuatano wa irabu mbili tofauti, na hivyo neno <taa> kupewa hadhi ya silabi mbili; ambapo [a:] ni mrefusho wa irabu moja, na hivyo <ta:> kupewa hadhi ya silabi moja. Wanafonolojia wanaochunguza lugha ambamo mambo haya ni muhimu wanatakiwa kuyashughulikia, na taaluma ya fonetiki inasaidia kutatatua matatizo kama haya ya ‘urefu’ na ‘ufupi’ wa sauti katika lugha zinazohusika.
to previous section
Powered by Blogger.