SWALI: Je, kuna umuhimu wa kufanya uhakiki katika fasihi simulizi? Kama ndiyo, kwa nini?

Je, kuna umuhimu wa kufanya uhakiki katika fasihi simulizi? Kama ndiyo, kwa nini?
UTANGULIZI
Fasihi simulizi kama zilivyo kazi nyingine za fasihi andishi hufanyiwa uhakiki. Uhakiki huu huzingatia vipengele vya fani na maudhui ili kubainisha usanaa wa kazi husika pamoja na kile ilichokusudia kufikishwa kwa hadhira. Kwa hiyo ni kweli upo umuhimu wa kufanya uhakiki wa fasihi simulizi.
KIINI
Uhakiki wa fasihi iwayo yote ni jambo la muhimu sana hasa kwa msingi kuwa utunzi wa fasihi hutumia akili nyingi na maarifa makubwa katika kucheza na lugha, hali hii husababisha wakati mwingine kazi za fasihi kuonekana ngumu kiasi kwamba bila msaada wa mhakiki hadhira huweza kuambulia tupu.Umuhimu wa kuhakiki fasi simulizi unaelezeka kama ifuatavyo.
(i) Kuchambua na kuweka wazi funzo ambalo linatolewa na kazi ya fasihi simulizi.
(ii) Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi.
(iii) Kumshauri mtunzi ili afanye kazi bora zaidi.
(iv) Kumuelekeza msikilizaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila ya
        dira ya mhakiki.
(v) Kuhimiza na kushirikisha fikira za kihakiki katika kazi za fasihi.
(vi) Kuweka, kubakiza, na kukuza kiwango cha utunzi wa kazi za fasihi.
(vii) Kuonesha kuwa kwa kila kizuri kuna kizuri zaidi na hapana kizuri kisicho dosari.
(viii) Kusema kweli ipasayo kuhusu tamaduni na falsafa zinazotawala fasihi.
HITIMISHO

Fasihi ya Kiswahili, kwa maana ya fasihi ya Kigogo kwa lugha ya Kiswahili, au fasihi ya Kimbulu kwa lugha ya Kiswahili, ina nafasi kubwa katika malezi na elimu ya taifa hili. Hivyo, uhakiki ni jambo muhimu sana katika kuunganisha hadhira na mtunzi wa kazi husika ya fasihi.
Powered by Blogger.