SANAA YA MAIGIZO
Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio
wahusika. Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika
ndio huzungumza katika sehemu zao mbalimbali.
Mifano:
- Michezo ya Kuigiza (Jukwaani) - Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika mbele ya hadhira.
- Miviga - Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao
- Ngomezi - ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma hutumika kuwasilisha ujumbe mbalimbali.
- Malumbano ya Utani - Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani
- Ulumbi - Ulumbi ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi.
- Soga - Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum.
- Vichekesho - Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke.
- Maonyesho ya Sanaa - Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au