Wanafunzi wapinga unyakuzi wa ardhi Kenya

Wanafunzi wakigonga uzio uliokuwa umewekwa katika ardhi hio iliyonyakuliwa na mtu asiyejulikana
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.
Polisi mmoja alijeruhiwa katika purukushani hizo
Baadhi ya wanafunzi walibeba vijiti na kuwafukuza polisi
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua rabsha.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.
Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.
Wanafunzi wakigonga uzio uliokuwa umewekwa katika ardhi hio iliyonyakuliwa na mtu asiyejulikana
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.
Polisi mmoja alijeruhiwa katika purukushani hizo
Baadhi ya wanafunzi walibeba vijiti na kuwafukuza polisi
Powered by Blogger.