Mlipuko wazua taharuki Tanga, mmoja ashikiiliwa
Tanga. Polisi Mkoani Tanga inamshikilia mmiliki wa banda la
wazi la kuonyesha video, eneo la Amboni Kata ya Chumbageni jijini Tanga
kwa mahojiano baada ya kutokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa ni bomu la
kutengeneza kienyeji katika eneo lake.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alisema kuwa tukio hilolilitokea
jana usiku na mara baada ya kitu hicho kurushwa kilisababisha hofu kubwa
kwa wakazi wa eneo hilo.
Alimtaja mmiliki wa banda
hilo kuwa ni Evarost Kiangazi (82) ambaye anashikiliwa kwa mahojiano
zaidi kwa lengo la kubaini chanzo cha tukio hilo.
Alisema
mlipuko huo ulisababisha wakazi wa eneo hilo kuanza kukimbia ovyo na
watu watano kati yao walijeruhiwa na kuwahishwa kwenye hospitali ya Mkoa
wa Tanga ya Bombo kwa matibabu.
Aliwataja majeruhi hao
Hassani Abdallah (72), Rashid Ally (45), Mrisho Abdi (29), Juma Mtoo
(15) na Abdul Ismail (19), ambao wote ni wakazi wa Amboni wakiwa
wamepata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.
Alisema kuwa baada ya majeruhi hao kupelekwa kwenye
hospitali hiyo walipatiwa matibabu na kisha kuruhusiwa, isipokuwa mmoja
aliyemtaja kwa jina la Hassani Abdallah (72) akiwa bado anaendelea na
matibabu kwenye hospitali hiyo.
Mwingine anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo ni Ally Rashid (25) mkazi wa Amboni Mafurikio
Hata
hivyo, alisema kuwa uchunguzi wa bomu hilo bado unaendelea ili kuweza
kubaini ni la aina gani pamoja na kuwa lilikuwa na malengo gani kwenye
eneohilo.
Polisi mkoani hapa Kijiji cha Maili Kumi wilayani Korogwe, iliwakamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika kuweka mabomu.
yaliyokuwa yameandaliwa tayari kulipuka kwenye nyumba mbili tofauti za ibada.