Ufundi nao kukopeshwa
Arusha. Serikali imeahidi kuangalia
utaratibu wa kuanzisha mfumo wa kugharimia elimu ya ufundi nchini ili
kuwawezesha wanafunzi kupata mikopo kama wa elimu ya juu. Lengo likiwa
ni kuwapata wataalamu wa kutosha katika viwanda na sekta nyingine.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama alitoa kauli hiyo
juzi wakati wa kuwatunuku vyeti wahitimu wa ngazi mbalimbali katika
mahafali ya Sita ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC). Alisema Serikali
inatambua jitihada zinazofanywa na chuo hicho za kupanua udahili ili
kuziba pengo la uhaba wa mafundi sanifu uliopo nchini.
Katika
mahafali hayo, wahitimu wa kwanza katika fani ya uhandisi wa umeme na
vifaatiba walitunukiwa stashahada zao. Naibu Waziri huyo alisema
wataalamu hao watasaidia kutengeneza vifaatiba katika hospitali jambo
litakaloongeza ubora wa huduma za afya na ajira.
Mkuu
wa Chuo hicho, Dk Richard Masika aliomba kuendelea kutolewa kwa Sh10
milioni kwa wanafunzi bora 10 katika masomo yao. ya mwisho ili kuongeza
ushindani katika masomo ya sayansi na ufundi hapa nchini.