Aguas aumia Cape Verde kutolewa


Kocha wa Cape Verde, Rui Aguas amesema anahisi kama  wamekatishwa uhai kwa kutolewa mapema katika fainali za Mataifa ya Afrika msimu.
Blue Sharks walilazimishwa suluhu na Zambia na kutolewa katika fainali za Afcon 2015 wakiwa hawajafungwa mchezo hata mmoja lakini walizidiwa kwa mabao na DR Congo katika msimamo wa Kundi B wakiangukia nafasi ya tatu.
“Nitasema nini tena unadhani? Kwa Congo hii ni furaha kwao, lakini kwetu ni tofauti,” alisema Aguas.
“Bao moja tulilolikosa limeweka tofauti kubwa na soka ndivyo lilivyo, wakati mwingine hakuna usawa na ni kama ukatili na kwa sasa ni zamu yetu.”
Cape Verde imefunga bao moja katika mashindano hayo baada ya kumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia  kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kundi B Januari 18 kabla ya kulazimishwa suluhu na DR Congo na Zambia.
Wakati huohuo, Tunisia imefuzu baada ya kumaliza ikiwa na pointi saba kwenye Kundi B, wakiwa na sare ya bao 1-1 dhidi ya DR Congo mjini Bata juzi.-
Powered by Blogger.