Tusubiri hii ya bangi kuuzwa madukani kama bidhaa nyingine ndani ya Jamaica…

marijuana_legal_gavel
Kwa huku kwetu T’zania Bangi ni moja ya dawa za kulevya ambazo zinapigwa marufuku, lakini kuna mahali hii kitu inaruhusiwa kabisa kutumika!
Kuna story nyingi mtaani kuhusu Bangi na Jamaica, mpya ninayokuletea kutoka huko ni kwamba Baraza la Mawaziri la Jamaica limeidhinisha muswada ambao unahalalisha watu kutumia marijuana au bangi kwa kiasi kidogo.
Kwa maamuzi haya ya Baraza za Mawaziri, kinachosubiriwa ni Baraza la Senate kupitisha muswada huo kuwa sheria japo haitaruhusiwa kuvutwa hadharani na kwenye maeneo ya mkusanyiko wa watu.
baaa
.
Kama hii ikipita itaruhusu kupandwa , kuuzwa na kusambazwa kwa bangi kama ilivyo bidhaa nyingine madukani kihalali.

Powered by Blogger.