lungu


 Mgombea wa chama tawala cha Patriotic Front, Edgar Lungu ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zambia.
Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa Lungu ambaye alikuwa Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo amepata asilimia 48 ya kura zilizopigwa na alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema.
stt
Aliyekuwa rais wa muda wa Zambia Guy Scott akiwa na rais mpya Edgar Lungu
Uchaguzi huo uliandaliwa kufuatia kifo cha rais Michael Sata ambaye alifariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana na nafasi hiyo kushikiliwa na Guy Scott.
Powered by Blogger.