MGOMO UDOM



wanafunzi katika mgomo


PICHA TOKA MAKTABA
Taarifa kutoka Dodoma zilizoifikia meza yetu ya habari jioni hii zinasema kuwa Chuo kikuu cha Dodoma UDOM kimepata sekeseke la mgomo uliohusisha College of Humanities and Social Sciences (COHSS) na DIPLOMA Special program kuanzia majira ya mchana.

Chanzo chetu cha habari  kilidai kuwa chanzo ya mgomo huo ambao ulidumu kwa muda mchache kufuatiwa na kuwasili kwa askari wa kutuliza ghasia,ni madai ya Diploma Special program kudai fedha za mkopo zilizocheleweshwa.

"Mwanafunzi mmoja wa kike (jina halikupatikana ) alikanyagwa na "difenda" sidhani kama amepona yule,ila kuna mwingine wa kiume yeye amevunjika mguu kutokana na kipigo cha askari Suma Jkt ambao ndiyo wahusika wa ulinzi chuoni". kilisema Chanzo chetu
PICHA TOKA MAKTABA
Aidha tulipotaka undani wa mgomo huo chanzo  kilidai kuwa leo majira ya saa saba mchana waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho aliyetajwa kwa jina moja la Bw.Mwakibinga aliitisha kikao muda mchache kabla ya mgomo huo kushika kasi na hadi taarifa hizi zinatufikia Bw.Mwakibinga alikuwa akihojiwa eneo la Block 19.
"Kwa sasa hali ni shwari ila kiukweli watu wana 'tensheni' maana wapo waliokuwa wakifanya test na baada ya kutoka wakakutana na hili jambo" aliongeza.


Powered by Blogger.