Walimu Mbeya waandamana
Mbeya. Zaidi ya walimu 150 wa shule
mbalimbali mjini hapa jana waliandamana kuelekea katika ofisi ya
mkurugenzi wa jiji kudai madeni ya fedha yaliyolimbikizwa kwa muda
mrefu.
Walimu hao walitokea katika Ofisi za Chama cha
Walimu (CWT), Wilaya ya Mbeya baada ya kutoridhishwa na maelezo ya
Katibu wa CWT, Felix Mnyanyi kuhusu fedha zao. Hata hivyo, jitihada zao
za kufika katika ofisi ya mkurugenzi ziligonga mwamba baada ya kujikuta
wakiishia mikononi mwa polisi.
Walimu hao walizuiwa na polisi wakiwa wamebakiza mita chache kufika katika ofisi hiyo.
Mmoja wa askari alisikika akisema:
“Jamani
kuandamana ni haki yenu, lakini leo hii ofisi ya jiji imezingirwa na
polisi ili kulinda usalama zaidi kwani wafanyabiashara nao wamejazana
mahakamani, hivyo hatujui hatima yao.
“Mkionekana pale mtadhaniwa ni wafanyabiashara, hivyo
mtazua jambo lingine ni vyema muondoke,” alisikika askari huyo
akiwaambia walimu hao.
Awali, wakiwa katika ofisi za
CWT, mmoja wa walimu hao, Isaack Mwalwajo alisema wanataka kufika kwa
mkurugenzi wa jiji ambaye ndiye mwajiri wao ili wakazungumze naye kwa
kuwa hawana imani na chama chao.
“Tumewachagua viongozi
ili mshughulikie matatizo yetu lakini hatuoni kitu chochote
mnachokifanya, watu tunadai malimbikizo mengi... tukienda kwa mwajiri
wetu tunajibiwa ovyo hata nyinyi viongozi wetu. Tunaomba mtueleze kama
mmeshindwa kazi,” alisema mmoja wa walimu hao.
Mnyanyi alikiri kuwa wanadai Sh1.3 bilioni zilizotokana na malimbikizo mbalimbali tangu mwaka 2007.
“Nimewasikia kilio chenu, ni kweli mnadai fedha hizo na haya ni madeni ambayo yamehakikiwa.