Matokeo yako hapo Uchaguzi wa Rais Zambia…Matokeo yako hapo
Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG namba BA172288
na risasi 10 wakati wa mapambano makali ya ana kwa ana kati ya polisi na
majambazi.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Kanda
Maalumu Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alisema kwenye tukio hilo
majambazi wawili waliuawa kwa risasi walipojaribu kuwashambulia askari.
“Tukio
hilo lilitokea eneo la Kariakoo Mtaa wa Mkunguni na Livingstone, juzi
saa 3.00 usiku na kwamba wakati wa tukio hilo umeme ulikatika,” alisema
Kova.
Alisema baada ya kuanza tukio la uporaji,
wasamaria wema waliwajulisha polisi ndipo kikosi maalumu cha kupamba na
majambazi kilipofika na kupambana nao.
Majambazi hao,
walishtuka na kuanza kuwarushia risasi askari waliokuwa katika gari ya
polisi na ndipo kukawa na mapambano ya moja kwa moja kati ya pande hizo
mbili.
Aliwataja majambazi hao wawili waliuawa kuwa ni
pamoja na Allan Ocheng maarufu kama Onyango (24), raia wa Kenya na
Yussuph Hamis maarufu kama Twalib (46) mshiraz mkazi wa Kariakoo huku
majambazi wengine wakitoroka baada ya tukio hilo na polisi inaendelea na
msako wa kuwatafuta.
Pamoja na kuuawa kwa majambazi
hao na kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa pikipiki mbili moja ni
Sunlg yenye namba za usajili T 249 CMC rangi nyekundu na nyingine aina
ya Boxer namba za usajli MC 350 AM rangi nyeusi na kwamba zilitumiwa na
majambazi hao katika tukio.
Katika tukio jingine, Kova
alisema majambazi sugu tisa wamekamatwa katika msako mkali unaondelea
jijini Dar es Salaam, wakijihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi
wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.