Ukawa kuhamasisha wananchi wasipige kura ya maoni Katiba mpya
Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) vimetangaza rasmi kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni
ya katiba na kwamba kuanzia sasa vitahamasisha wananchi kuunga mkono.
Uamuzi
huo umetolewa leo na wenyeviti wa vyama wanaounda umoja huo wa ukawa
ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na
Mwenyekiti wa NLD, Makaidi.
Akizungumza wakati wa kutoa
msimamo huo Profesa Lipumba amesema wamefikia uamuzi wa kutoshiriki
katika zoezi hilo kwa sababu mchakato mzima haukuwa na maridhiano ya
kitaifa.
“Vyama vya siasa ikiwemo CCM vilikubaliana
mwaka jana kwamba zoezi la kura za maoni lifanyike mwaka 2016 baada ya
uchaguzi mkuu, tulisaini wote na Rais Jakaya Kikwete alikubali, kwa nini
mabadiliko yafanyike ghafla” amehoji Profesa Lipumba.
Amesema
jambo la kushangaza, Rais Kikwete aligeuka na kutangaza kwamba Aprili
30, mwaka huu kuwa siku ya kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba
Amesema pamoja na kutangaza siku ya kupiga kura, bado
uandikishaji katika daftari la wapiga kura haujaanza kwa sababu
wanasubiri vifaa.
“Hadi sasa vifaa vya Biometric
Voter Registration (BVR) vilivyopo ni seti 250 wakati vinavyohitajika ni
seti 7500, tume inasubiri hadi sasa, zoezi hili litafanyika kweli?,”
alihoji Lipumba.
“Mbinu hiyo inafanywa na Serikali kwa sababu Wazanzibari ndiyo wanaona kikwazo kwao,” alisema Makaidi.
Aprili
16 mwaka jana, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka vyama vya
Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD walitoka nje wakidai bunge hilo
lilikuwa halijadili maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.