Jela maisha kwa kumlawiti mtoto
Mpanda. Kijana mmoja aitwaye Michael Edward
(25) mkazi wa Mtaa wa Mji wa Zamani, Mkoa wa Katavi amehukumiwa kifungo
cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumlawiti
mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba.
Hukumu hiyo
iliyovuta hisia za watu wengi mjini Mpanda, ilitolewa juzi na Hakimu
mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada
ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa pande
zote mbili.
Awali, akisoma maelezo ya upande wa
mashtaka Mwendesha Mashtaka, Kulwa Sikwesa alidai mahakamani hapo kuwa,
mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 9, 2014, saa 12 jioni katika eneo la
Mji wa Zamani
Alisema siku hiyo ya tukio mshtakiwa
alikutana na mtoto huyo njiani akielekea nyumbani kwao ndipo alipomshika
mkono na kwenda naye kwenye pagala la nyumba katika mtaa huo.
Mwendesha
mashtaka huyo aliieleza Mahakama hiyo kuwa, baada ya kuingia naye ndani
mshtakiwa alitoa kisu na kuchoma kwenye ubao aliokuwa amemshikisha
mtoto huyo ikiwa ni ishara ya kumtishia kisha alimwambia endapo atakataa
kulawitiwa au akipiga kelele atamuua.
Sikwesa alidai
baada ya vitisho hivyo ndipo mshtakiwa alipomvua nguo mtoto huyo na yeye
suruali na kutoa sehemu zake za siri na kuupaka mate na kisha kuanza
kumlawiti mtoto huyo kwa nguvu. Alidai baada ya kumlawiti alimtishia
kutotoa siri hiyo lakini mtoto huyo baada ya kufika kwa wazazi wake
alilazimika kuwaambia kutokana na maumivu aliyokuwa nayo na ndipo
walipotoa taarifa Polisi kabla ya kukamatwa.