Mwenyekiti auawa, viungo vyapikwa kama mboga
Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,
Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na
kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa viungo vya mikono na
miguu na sehemu za siri na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani
ya safuria kama mboga.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya
kikatili na kutisha yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa
marehemu.
Kidavashari alisema, siku
hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe
Meklina Mussa na ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na
kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema
watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga waliingia chumbani kwa marehemu
na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
Alisema
baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia
panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.
Kidavashari
alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria
na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya
marehemu.
Alisema kisha walirudi
ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye
safuria jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo
hivyo vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.
Kidavashari
alisema mke wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka
nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo
hilo na kukuta viongo hivyo vikiwa ninaendelea kuchemke kwenye
safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake
Amesema
uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji kimetokana na
visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora
ambae alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa amemnyanya mwanamke ambae
walikuwa na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua kuhama
nae kijijini hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele Wilaya Mlele
Kamanda
Kidavashari alieleza jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na
linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya
kikatili