Raia wa Afrika Kusini akutwa amekufa makaburini Dar es Salaam

Dar es Salaam. Tukio la kuokotwa mwili wa raia wa Afrika Kusini makaburini jijini Dar es Salaam hivi karibuni kumeacha maswali mengi huku polisi wakilipiga danadana.
Mwanzoni mwa wiki iliyopita baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kuwa mtu huyo, Mark Wilson ambaye ni muhubiri,alipotea Tanzania wakati akiwa njiani kwenda Israel.
Taarifa hiyo ilisema kuwa Wilson aliondoka Cape Town kabla ya Krismasi na kwamba alikuwa na mpango wa kwenda Israel kwa njia ya barabara ili aweze kuhubiri njiani.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, SSP Advera Bulimba aliiambia Mwananchi jana kuwa tukio hilo lilitokea wilayani Temeke, hivyo kamanda wa polisi wa eneo hilo ndiye mwenye taarifa rasmi.
“Wasiliana naye anaweza kukupa taarifa zaidi,” alisema Advera.
Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoani Temeke, ACP Kihenya Kihenya alikiri kutokea kwa tukio hilo, lakini alikataa kulitolea maelezo kwa madai kuwa linafanyiwa uchunguzi na ofisi ya Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Alipoulizwa Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova alisema ni kweli tukio hilo limetokea lakini alimtaka mwandishi arudi tena kamanda wa Temeke.
Kwa mujibu wa jarida la Afrika Kusini la IOL, Januari 3, Wilson aliandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa alikuwa anajisikia malaria, lakini baada ya kuombewa, alipona.
Inaelezwa kuwa aliondoka Zambia Januari 5 kuja Tanzania na tangu wakati huo hakuonekana tena hadi alipopatikana makaburini Dar es Salaam siku 10 baadaye akiwa amefariki dunia.
Pia jarida hilo linaeleza kuwa mtu wa mwisho kuwasiliana na muhubiri huyo ni Frank Materu aliyewatumia ujumbe ndugu wa marehemu usemao:
“Vile vile, IOL lilimnukuu Benji Mumena anayeishi Zambia akisema ‘Mark alipitia kwetu akiwa njiani kwenda Jerusalem. Aliwaombea watu kadhaa akiwa hapa.’”
wakiwamo wazazi wangu. Jambo hili limepokewa kwa mshangao katika familia yetu.”
Powered by Blogger.