Wawili wakamatwa na bunduki

Ngorongoro. Polisi wilayani Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, inawashikilia wafugaji wawili kwa kosa la kukutwa na bunduki aina ya Rifle wanayodaiwa kuitumia kufanya uhalifu wilayani hapa na Kenya.
Katika msako ulioongozwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo, Mrakibu (SP), Ally Mohamed Mkalipa alisema walifanikiwa kukamata silaha hiyo iliyokuwa imefichwa porini karibu na boma la ng’ombe la mfugaji mmoja.
Akizungumza jana na gazeti hili, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Liberatus Sabas aliwataja wafugaji hao kuwa ni wakazi wa Kijiji cha Soitisambu.
Kamanda Sabas alitaja silaha hiyo ni Rifle 370 na tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu saa 11 jioni katika Kitongoji cha Silalei, Kijiji cha Soitisambu, Loliondo.
Powered by Blogger.