Obama ajiandaa kutoa hotuba ya hali ya kitaifa

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama
Rais Barak Obama, amekwenda Phoenix Arizona kujadilia mapendekezo ambayo amepanga kuzindua wakati wa hotuba yake kuhusu hali ya kitaifa mbele ya bunge baadaye mwezi huu.
Hotuba italenga swala la kuwasaidia Wamarekani zaidi kuweza kujinunulia nyumba.
Baadae Rais Obama, atasafiri kuelekea katika jimbo la Tennessee, kwa majadiliano ya kufanya masomo ya chuo kikuu kuwa nafuu kwa kila mmoja.
Mazungumzao haya yanalenga kuinua hadhi yake hata zaidi.
Bw Obama ameinua hadhi yake katika siku za karibuni baada ya kutumia amri za kiutendaji kurudisha uhusiano mwema na Cuba.
Pia kuruhusu mamilioni ya wakazi wa marekani wasio na vibali vya kuishi kuendelea kuishi Marekani pamoja na uchumi ambao umekuwa ukiimarika.
Hotuba yake ya kwanza ilianza Jumatano kwenye kiwanda cha kutengenezea magari mjini Detroit, ambao ndio  kitovu cha  utengenezaji wa magari nchini Marekani.
Alitumia fursa hii kuhimiza uamuzi wa utawala wake wa mwaka wa 2009 wa kuvipa viwanda vya kutengeneza magari vya Chrysler na General Motors, mkopo wa mabilioni ya dola ili kujikwamua kutoka  hali ya kufilisika wakati  wa mporomoko wa uchumi duniani.
Powered by Blogger.