Habari / Dunia Uchunguzi wa tukio la Kigaidi unaendelea



 Vikosi vya Paris, Ufaransa wakiendelea na msako wa washukiwa wa ugaidi mjini Paris, Ufaransa.





Vikosi vya Paris, Ufaransa wakiendelea na msako wa washukiwa wa ugaidi mjini Paris, Ufaransa.


Maafisa wa usalama wa Ufaransa wamesema watu saba wamekamatwa kwenye juhudi za kuwasaka washukiwa wawili wakuu wa shambulizi lililosababisha vifo vya watu 12 kwenye ofisi za jarida la Charlie Hebdo, mjini Paris, Ufaransa.
Waziri mkuu Manuel Valls, amewambia wanahabari kwamba washukiwa hao wawili wanajulikana na idara za ujasusi ya Ufaransa.
Amesema washukiwa hao walitekekeleza shambulizi hilo kama wanajeshi.
Ameongeza jukumu kubwa kwa serikali sasa hivi ni kuzuia shambulizi la pili.
Askari mjini Paris wamesema polisi mmoja  mwanamke amepigwa risasai na kuuwawa Alhamisi na bado haijabainika iwapo tukio hili linahusiana na kuwasaka washukiwa wa shambulizi la hapo hilo la kigaidi.
Wakati huo huo mmoja wa washukiwa mwenye umri wa miaka18 Hamyd Mourad, alijisalimisha kwa mamlaka huku  askari wangali wanaendelea kuwasaka ndugu wawili.
Ndugu hao wametajwa kuwa ni Said na Cherif Kouachi wote wawili wakiwa ni wakazi wa Paris wenye umri wa miaka ya 30.
Cherif kwa wakati mmoja alifungwa gerezani kwa mashtaka ya ugaidi. Mamlaka ya ufaransa yamewataja kama waliojihami na hatari kwa usalama.

Powered by Blogger.