Kamati Kuu yayaweka njiapanda makundi CCM
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kulia) na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wakiimba nyimbo ya chama hicho kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati maalum ya chama hicho kilichifanyiaka jana katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. Picha na OMR
Dar es Salaam. Habari kuwa Kamati Kuu ya
CCM inayokutana Zanzibar kesho itajadili hatima ya vigogo sita wa chama
hicho waliopewa onyo kwa kuanza kampeni za urais mapema, zimezidi
kuyaweka makundi ya vigogo hao njiapanda.
Pamoja na
ajenda nyingine, jambo kubwa linalozisumbua kambi hizo ambalo
lilizifanya zipige simu jana chumba cha habari cha gazeti hili, ni
kutaka kujua ni suala gani litajadiliwa, wagombea gani watajadiliwa na
uwezekano wa ama kufutiwa onyo lililotolewa Februari mwaka jana au
kuongezewa adhabu.
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya
kikao cha Sekretarieti ya chama hicho iliyokutana juzi Dar es Salaam,
ilisema suala hilo halitakuwa moja ya ajenda za mkutano huo wa kesho,
licha ya Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana kueleza akiwa Tanga kuwa
moja ya ajenda itakuwa suala la maadili.
Miongoni mwa
ajenda zinazotajwa ni ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika
mwishoni mwa mwaka jana, kalenda ya chama kwa mwaka huu na sherehe za
miaka 38 ya CCM zinazotarajiwa kufanyika Songea mkoani Ruvuma.
Vyanzo
vingine vya habari vimeeleza kuwapo pia kwa ajenda ya hali ya siasa
inayohusishwa na harakati za urais, hususan kwa vigogo wanaopishana
kusaka nafasi hiyo na wale waliotajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta
Escrow.
Kamati Kuu inatarajia kutumia vikao hivyo
kuangalia namna ya kupata wagombea watakaokubalika kwa wananchi kuelekea
kwenye kinyang’anyiro cha urais, wabunge na madiwani.
Akiwa
katika ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kuipa CCM ushindi kwenye
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Tanga, Kinana alisema chama hicho
kitafanya kikao hicho kwa lengo pia la kupitia masuala mbalimbali
yanayokihusu.
Alisema salamu za CCM kwa Watanzania kwa
mwaka huu ni ahadi ya kuweka mkazo katika maadili kwa viongozi wake na
itafanya tathimini kwa lengo la kujipanga kwa Uchaguzi Mkuu.
Alipoulizwa
kuhusu ajenda katika vikao hivyo wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikuja juu na kusema hakuna kitu kama hicho.
“Hata mkiiandika vibaya CCM itashinda tu,” alisema hivi karibuni.
Vigogo
waliopewa onyo na CCM ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia, January Makamba na mawaziri wakuu wa zamani, Edward
Lowassa na Frederick Sumaye.
Wengine ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira na aliyewahi kuwa
Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William
Ngeleja na waziri waliokumbwa na kashfa ya escrow ni Profesa Anna
Tibaijuka na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhong-