CCM kuanza fagio la viongozi wiki ijayo
Tanga. Chama cha Mapinduzi (CCM) wiki ijayo
kitaanza rasmi vikao vyake kwa ngazi ya Taifa vitakavyo chunguza maadili
ya viongozi ikiwa ni maandalizi ya kuwapata wagombea wanaokubalika na
wananchi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana alitoa taarifa hiyo jana katika mkutano maalumu wa
kuwashukuru Watanzania kwa kukichagua chama hicho katika uchaguzi wa
Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka jana. Alisema chama
chake kinajipanga kuwa na viongozi wasio wamangimeza na wenye moyo wa
kuwatumikia wananchi.
Katibu huyo Mkuu aliwashukuru
Watanzania kwa kukipa ushindi chama chake na kubainisha kuwa kitaifa,
CCM imeshinda kwa asilimia 81.
Hata hivyo, alisema
katika maeneo ambayo imeshindwa kama Wilaya ya Pangani, itafanyika
tathmini na watajipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu ujao wanapa ushindi wa
kishindo.Alisema watahakikisha wanashinda katika maeneo yote
waliyofanya vibaya