Ajifungua pacha wa kike walioungana kifua, tumbo
Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Buhare, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Helena Paulo (20)
,Watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana eneo la kifua hadi tumboni mkoani Mara. Picha na Florence Focus
,Watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana eneo la kifua hadi tumboni mkoani Mara. Picha na Florence Focus
Musoma. Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya
Buhare, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Helena Paulo (20), amejifungua
watoto pacha wa kike walioungana eneo la kifuani hadi tumboni wakiwa na
uzito wa kilo 4.6 kwa pamoja.
Tukio hilo la ajabu
katika Mji wa Musoma na mkoa kwa jumla, liliwavutia hisia za wananchi
hali iliyosababisha msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa
madhumuni ya kutaka kushuhudia.
Akizungumza katika wodi
ya wazazi hospitalini hapo, muuguzi wa zamu, Naabu Geraruma alisema
mwanamke huyo alijifungua juzi saa saba usiku kwa njia ya upasuaji.
Geraruma
alisema tukio hilo ni la kwanza katika hospitali hiyo na hali ya afya
ya mzazi huyo na watoto inaendelea vizuri na muda wowote atahamishiwa
Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza.
Kwa upande wake,
Mganga wa Idara ya Magonjwa ya Wanawake, Dk Simon Kamuli alisema baada
ya jitihada za kuhakikisha mwanamke huyo anajifungua salama kukamilika,
kinachofuatia ni kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uangalizi
zaidi.
Alisema kuwa hospitali ya mkoa haina uwezo wa
kuwafanya chochote watoto hao, ikiwamo kuwatenganisha na taratibu
zingine kabla ya uchunguzi wa kina