Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu akiutubia
Na Jovither Kaijage,Mwananchi
Kwa ufupi
Akizungumzia hatua hiyo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Nansio jana, Mwalimu ambaye ameanza ziara mkoani hapa
juzi kwa lengo la kuwashukuru wananchi baada ya kukichagua chama hicho
katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, alisema hakuridhishwa na
maandalizi yaliyofanywa na viongozi hao
Rungu hilo pia limemkuta katibu wa Chadema wilaya hiyo, Libelatus Mlebele ambaye amepewa onyo kali.
Akizungumzia hatua hiyo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Nansio jana, Mwalimu ambaye ameanza ziara mkoani hapa
juzi kwa lengo la kuwashukuru wananchi baada ya kukichagua chama hicho
katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, alisema hakuridhishwa na
maandalizi yaliyofanywa na viongozi hao.
Kutokana na hali hiyo, Mwalimu alimwagiza
Mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho, Jacobo Munyaga kwa gharama zake
amwandalie mkutano mwingine kabla ya mwisho wa mwezi ujao.
Mwalimu pia alitilia shaka matumizi ya fedha yaliyotajwa kutumika kutangaza uwepo wa mkutano wake.
Alisema Chadema hakipo tayari kulinda viongozi
wazembe na wasiowajibika na kuwaonya wajumbe wa kamati tendaji hasa
katibu ambaye bado yupo katika uangalizi wa miezi sita kwa maelezo kuwa
anaweza kuondolewa kazini.
Kabla ya kuchukua uamuzi huo, Mwalimu aliwaita
mbele wakazi wanne wa kata za Kakerege, Nansio, Nakatungulu na Kagera
ambao walikiri kutosikia matangazo ya ujio wake.
Hatua hiyo aliichukua baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Mongera wa mjini Nansio saa 9:30 alasiri huku kukiwa na idadi
ndogo ya watu ikilinganishwa na ziara zake za nyuma.
Mbali na hilo, pia Mwalimu ametumia mkutano huo
kukemea matumizi mabaya ya fedha za serikali yanayofanywa na viongozi
waandamizi wakati huduma za kijamii zikizidi kuwa mbaya.
Alisema ziara za mara kwa mara za nje ya nchi
zisizo za lazima zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi
wengine hazina tija kwa taifa.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo,
Joseph Mkundi akizungumza katika mkutano huo, alisema katika katika
kipindi cha miaka minne ya uongozi wao wamepata mafanikio makubwa.
Alisema mbali na kusimamia vyema matumizi ya fedha
za serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pia halmashauri
hiyo imekamilisha mipango ya kununua greda moja la kutengeneza barabara
lenye thamani ya Sh400 milioni hivi karibuni chama hiko kimeluwa
kikipigania kukishinikiza serikali kuwachukulia hatua watuhumiwa wa
ufisadi.