Kenge 140 wanaswa JNIA wakitoroshwa nje ya nchi
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere. Picha na Maktaba
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman
alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa
Kuwait ambaye alikamatwa uwanjani hapo jana majira ya saa 5 usiku
wakati akijiandaa na safari ya kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai
na Shirika la Ndege la Emirates .
Kamanda Selemani
alisema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao aliwahifadhi kwenye
mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.
“Kenge
waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja kuna kenge 15 na
mifuko mingine walikaa wawili,”alisema kamanda Selemani.
Alisema kati ya Kenge hao, 15 walikufa na walio hai walikuwa 134 ambao walikuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo.
Seleman
alisema wakati wanafanyiwa upekuzi ndipo walipogundua kuna vitu
ambavyo vinafanana na nyoka na kuamua kuwashirikisha wataalamu wa
maliasili ambao walibaini kuwa begi hilo lilikuwa na Kenge.
“Huyu mtuhumiwa alikuja nchini Januari 6,alitiliwa
mashaka na polisi wa JNIA na tulimuamuru akae pembeni kwa upekuzi
zaidi na kugundua anasafirisha kenge bila Kibali,”alisema Selemani.
Selemani
alisema walipoendelea kumuhoji mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuja
nchini kwa ajili ya kuchukua viumbe aina ya ndege lakini baada ya
kuwakosa aliamua kubeba Kenge hao.
Kamanda Selemani
aliwaomba wananchi kuwa na uzalendo wa nchi yao wanapoona mtu
anasafirisha rasilimali za nchi watoe taarifa katika jeshi la polisi.
Alisema
polisi wataendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mipakani na
viwanja vya ndege ili kudhibiti aina hiyo ya utoroshaji wa nyara.
Julai
31, mwaka jana raia wa Vietnam, Dong Van (47) naye alikamatwa
uwanjani hapo akiwa na meno 65 na kucha 447 za simba zenye thamani ya
Sh189.4 milioni.