Jeshi la polisi Morogoro linawashikilia watuhumiwa wa ujambazi akiwemo raia wa Kenya.


Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia watuwawili akiwemo raia wa Kenya kwa tuhuma za kutapeli laptop nne wanafunzi wa chuo kikuu mzumbe na mwingine mkazi wa ifakara kwa kupatikana na risari 100.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema mtu huyo amekamtwa akiwa ndani ya gari aina ya Noah yenye nambari za usajili T416 CJN iliyokuwa ikitokea mlimba kwenda ifakara januari mwaka huu majira ya saa tano asubuhi na askari wa usalama barabarani   baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
 
Katika hatua nyingine kamanda Paulo amesema jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia mtu mmoja raia wa Kenya aliyetambulika kwa jina la Alex Selenje kwa tuhuma za kufanya utapeli sehemu mbalimbali zikiwemo katika chuo kikuu cha  Mzumbe Morogoro.

Powered by Blogger.