Siku chache baada vyombo vya habari kukaririwa kuwa Ikulu inautambua mgogoro wa magereji Tegeta.
Siku chache baada vyombo vya habari kukaririwa kuwa Ikulu inautambua mgogoro wa magereji Tegeta.
Siku
chache baada vyombo vya habari kukaririwa kuwa ikulu inautambua mgogoro
wa magereji Tegeta ikieleza kushughulikiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam huku chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kuingilia kati
kupitia kurugenzi yake ya sheria mkuu wa mkoa ameeleza kujiingiza katika
masuala ambayo tayari yameamriwa na mahakama zaidi ya kusimamia
utekelezaji wake.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Saidi Meck Sadiki ambaye pamoja
na kueleza nia yake ya kutotaka kuongelea suala hilo katika vyombo vya
habari kwa njia ya simu amesema yeye kama kiongozi lazima asimamie
utekelezaji wa sheria huku viongozi wa magereji hayo wakieleza kuwa
hatua hiyo inalenga kupora haki yao ya uwekezaiji uliofikia zadi ya
shilingi billion 30.
Hata hivyo ITV ambayo imekuwa ikifuatilia sakata hilo kwa kipindi
chote imafanikiwa kupata nyaraka za manispaa kubariki zoezi hilo pamoja
na kuomba kubadilisha matumizi ya ardhi ya kiwanja tajwa no. 29971
kupitia mamlaka husika huku viongozi wa manispaa ya Kinondoni mara zote
wakionyesha kutetea uamuzi wao tangu ilipofanya opereshenmi ya kuondoa
gereji bubu mitaani kwa kuwabomolea mapema mwaka 2006 tofauti na msimamo
wa ofisi ya mkuu wa mkoa.
Hata hivyo katika uamuzi wa kuwakabidhi eneo hilo pia ITV
ilishuhudia uzinduzi rasmi wa magereji hayo uliofanywa mwaka 2010 chini
ya uratibu wa ofisi ya mkoa kupitia mkuu wa wilaya Jordan Rugimbana
akiwa mrithi wa ulezi wa mafundia hao zaidi elfu nne kutoka kwa muasisi
wa taifa na waziri mkuu mataafu mzee Rashd Mfaume Kawawa mara bada ya
afya yake kudhoofu kabla ya kupatwa na umauti.